Kasheshe
JF-Expert Member
- Jun 29, 2007
- 4,694
- 787
Sie tunoona madhara yake tuwape njia m-badala, tusiwalaumu; nia yao ilikuwa njema, ila utekelezaji kama haufikii kile walichotegemea kupata warudi kujipanga upya nasi tuwasaidie mawazo mapya
Pinokyo,
Tunahitaji wazalendo kama wewe, hoja nzuri sana!
Lakini siku zote najiuliza swali hili!
Kwa kuwa mwananchi hawana raslimali za kufanya lile wanalotaka serikali ilifanye,,, na kwa kuwa mwananchi wanaweza kutoa mawazo tu kwa mambo ambayo yanahitaji rasilimali na sio kuyafanya wao!
Je kama mwananchi anatoa mawazo kama hivi tutoavyo hapa JF, si mwananchi atakuwa ametenda wajibu wake?
Huko nyuma kwenye thread hii hii, nilishasema nini kilitakiwa kifanyike kabla ya zoezi lenyewe!!! sasa kwa kuwa havijafanyika basi sasa vifanyike...
Hata hivyo sina imani kama waheshimiwa hao wanaona maoni yetu,,, maana idara kama ya polisi ambapo bado mfupi uliopita (sina hakika sasa) walikuwa wakiandikia mifuko ya sementi, je wataweza kuingia humu kwenye mitandao waone maoni yetu.
Ndio tunarudi kulekule kwamba tuwe wabunifu katika kupeleka ujumbe,,, mfano,,, maoni yanayotolewa yanaweza forwardiwa kwa waheshimiwa kamshina wa usalama barabarani... otherwise sisi kama raia tutakuwa hatujatekeleza wajibu wetu kisawasawa.