Mlolongo wa Ajali za Barabarani Tanzania 2007-2011

Mlolongo wa Ajali za Barabarani Tanzania 2007-2011

Wadau nimesikia tetesi kuwa, kuna ajali imetokea maeneo ya Segerea na imehusisha gari aina ya Hiace, watu wote waliokuwepo ndani ya gari hiyo wamefariki dunia....mwenye habari kamili atujulishe tafadhali
 
Naishi maeneo haya na sijaisikia ajali hiyo hata baada ya kuwapigia simu watu kadhaa;

Could it be Segera instead of segerea?
 
Ni SEGERA, Tanga. TBC wamesema ajali ya Hiace na lori imeua watu wote waliokuwa kwenye Hiace baada ya gari hilo kuungua moto. Wamesema watatuletea habari zaidi kadri wanavyozipata.
 
Ni SEGERA, Tanga. TBC wamesema ajali ya Hiace na lori imeua watu wote waliokuwa kwenye Hiace baada ya gari hilo kuungua moto. Wamesema watatuletea habari zaidi kadri wanavyozipata.

MUNGU WANGU ZIWEKE ROHO ZA MAREHEMU MAHALI PEMA............... WATZ na hizi ajali jamani,kila siku mpaka lini??
 
Ni SEGERA, Tanga. TBC wamesema ajali ya Hiace na lori imeua watu wote waliokuwa kwenye Hiace baada ya gari hilo kuungua moto. Wamesema watatuletea habari zaidi kadri wanavyozipata.

asante mkuu kwa habari hii...RIP kwa kila aliyekumbwa na mauti
 
Watu 20 wafariki katika ajali mbaya, 12 taabani




comment_bubble.png

Ni katikati ya Kiteto na Kondoa
headline_bullet.jpg
Hiace na lori uso kwa uso
headline_bullet.jpg
Ilibeba watu toka harusini
headline_bullet.jpg
Miili yote bado kutambuliwa

Watanzania wakiwa bado hawajasahau ajali mbaya ya mtumbwi uliozama katika ziwa Victoria na kuua wanafunzi 18, ajali nyingine mbaya jana imeua papo hapo watu 20 na wengine 12 kujeruhiwa baada ya magari mawili kugongana uso kwa uso katika kijiji cha Kelema kwa Simba wilayani Kondoa.
Ajali hiyo ilitokea majira ya saa 8:30 mchana, ambapo basi dogo aina ya Hiace (maarufu kipanya) yenye namba T929 AQA iliyokuwa imebeba watu waliokuwa wakitokea Kiteto kwenda Kondoa kwenye harusi, kugongana uso kwa uso na lori aina ya Scania lenye namba T899 AFP lilokuwa likitokea Kondoa.
Akizungumza kuhusu tukio hilo, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Kondoa John Luanda, alithibitisha kupokea maiti hizo na majeruhi na kueleza kuwa ajali hiyo ni mbaya tofauti na ajali zingine zilizowahi kutokea wilayani hapo.
Alisema kuwa kati ya majeruhi waliofikishwa, wawili hali zao ni mbaya na wanaendelea na matibabu hospitalini hapo.
Mganga huyo Mkuu alisema kuwa miili ya marehemu wote bado haijatambuliwa na kwamba imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Kondoa.
Aliongeza kusema kuwa kati ya watu waliokufa kumi ni wanaume na nane ni wanawake, ambapo kwa upande wa majeruhi wanawake ni wawili na wanaume ni saba.
Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Zelothe Stephen, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kuwa chanzo chake bado hakijajulikana na uchunguzi unaendelea.
Hata hivyo, Kamanda Zelothe, alisema utaratibu unafanywa katika hospitali ya wilaya ya Kondoa kwa ajili ya utambuzi wa maiti kwa kuwa mpaka jana jioni miili hiyo ilikuwa bado haijatambuliwa
Katika ajali hiyo inaelezwa kuwa Bwana Harusi ambaye jina lake halijatambuliwa aliyekuwa akienda kuoa naye ni mmoja wa watu waliofariki katika ajali hiyo.



CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
 
Mimi ni mkereketwa sana wa kufuatilia News Mbalimbali Nchini, Hasa za majanga na Za kusikitihsa,, Nikiwa Offisini, huwa ninaandika Report ya Ajali mbalimbali ambazo hutokea na kusababisha Vifo Vya watanznaia Wenzetu eti eiza kwa uzembe wa Madereva au Abilia Wenyewe kwa kuogopa kumwambia Dereva wao apunguze Mwendo kama mwendo ni mkali, au kutokubali kupanda Gali lililo jaa Abilia mpaka mlangoni..

Nasikitika mpaka sasa nilipokuta Takwimu za mkoa mmoja hapa nchini Tanzania kama nilivyo Quort kwenye DAILY NEWS Habari yenyewe unasema hivi..

"POLICE in Kilimanjaro region have confirmed that road accidents in Kilimanjaro Region claimed 273 lives between last year and this year. "

Hii ni idadi kubwa sana kama tukifanya sampling maana yake ni sawa na watu 7644, kwa Mikoa 28 ya Tanzania.. kwa mwaka wanapoteza maisha kwanini tusigeuke na kutaka, kutafuta Mabadiliko jamani?
 
Aisee aliekudanganya tutabaki wachache amekosea nenda muhimbili tu uone wanavyoshuka na hawaa watoto tena wengine wako na miaka 15 tutisha wapi sema nitaisha
 
usiogope silver muda bado ukifika aukimbii ....ila we jitahidi kuongeza ili tukave gep za hizi ajali
 
AJALI imetokea sasa h ivi hapa buguruni na kuhusisha magari matatu yaliyogongana kwa nyuma, kama kuna wadau wanaotumia njia hii wabadilishe kwani kwa muda huu kutakua na foleni kubwa! Siku njema kwenu
 
AJALI imetokea sasa h ivi hapa buguruni na kuhusisha magari matatu yaliyogongana kwa nyuma, kama kuna wadau wanaotumia njia hii wabadilishe kwani kwa muda huu kutakua na foleni kubwa! Siku njema kwenu
Thanks kwa taarifa. Majeruhi au vifo? Hope breakdown zinafanya faster kuclrear eneo la ajali.
 
Jamani ajali mbaya sana imetokea nje ya zhonghua garden mida hii.yaani gari 5 zimegongana kwa mpigo na karibu watu 3 wamepoteza maisha..ni habari ya kuhuzunisha sana..
 
Jamani ajali mbaya sana imetokea nje ya zhonghua garden mida hii.yaani gari 5 zimegongana kwa mpigo na karibu watu 3 wamepoteza maisha..ni habari ya kuhuzunisha sana..

Tooo sad. Nini chanzo mkuu ni watu wamelewa au?
 
Back
Top Bottom