Mlolongo wa Ajali za Barabarani Tanzania 2007-2011

Mlolongo wa Ajali za Barabarani Tanzania 2007-2011

Huu ni uzembe wa Taifa kutowathamini raia wake!!Kwanini waache waangamie tuu kwenye ajali za barabarani???
 
Du! Mungu awasaidie majeruhi......Nchi zetu hizi tatizo hatuna hata kikosi imara cha uokoaji, majeruhi wengine watapoteza maisha si kwa kuumia bali kwa sababu ya handling mbaya!
 
Ee Mungu uturehemu sawasawa na fadhili zako, kiasi cha wingi wa rehema zako uyafute makosa yetu, utuoshe kabisa uovu wetu ututakase dhambi zetu maana sisi twajua makosa yetu na dhambi zetu zipo mbele zetu daima. Tumekutenda dhambi wewe peke yako na kufanya maovu mbele za macho yako, wewe ujulikane kuwa una haki unenapo na kuwa safi utoapo hukumu. Tazama Wanadamu tumeumbwa katika hali ya uovu nasi tulichukuliwa mimba hatiani. Tazama wewe wapendezwa na kweli iliyo moyoni nawe utatujulisha hekima kwa siri. Tusafishe kwa Hisopo nasi tutakuwa safi, tuoshe nasi tutakuwa weupe kuliko theluji. Usitiri uso wako usizitazame dhambi zetu bali uzifute hatia zetu zote.
Ee Mungu utuumbie mioyo safi, uifanye upya roho uliyotulia ndani yetu usitutenge na uso wako wala roho wako mtakatifu usituondolee, uturudishie furaha ya wokovu wako ututegemeze kwa roho ya wepesi. Tutawafundisha wakosaji njia zako na wenye dhambi waterejea kwako. Amen.
 
kwa ajali za barabarani namba hii bila ufumbuzi ingekuwa nchi za ulaya, waziri wa usafiri ( au sijui miundo mbinu) angebidi ajieleze
 
Sidhani kama waziri ni wa kulaumiwa....madereva wa Tanzania wengi ni viburi na haya ndiyo matunda yake. Nimesafiri sana na mabasi yetu lakini madereva wengi hawajali sheria za barabarani....utakuta hapo kila mmoja alikuwa anataka kumwahi mwenzake.
 
Ee Yesu mwenye Huruma, Mpenda Roho za Watu, Tunakuomba kwa ajili ya Mateso uliyoona katika Moyo wako Mtakatifu, Tunakuomba kwa ajili ya mateso ya Mama yako mkingiwa dhambi ya asili, watakase kwa damu yako watu wote wenye dhambi wanaozimia sasa na watakao kufa leo. Moyo wa Yesu uliozimia wahurumie roho za watu wanao kufa. Kwa Jina la Baba nala Mwana nala Roho Mtakatifu. Amina.
 
Sidhani kama waziri ni wa kulaumiwa....madereva wa Tanzania wengi ni viburi na haya ndiyo matunda yake. Nimesafiri sana na mabasi yetu lakini madereva wengi hawajali sheria za barabarani....utakuta hapo kila mmoja alikuwa anataka kumwahi mwenzake.

Hapo penye nyekundi mbili! Unafikiri ni nani mwenye dhamani ya kisiasa kuhakikisha kuwa madereva wanaacha viburi na polisi wanaacha kupokea rushwa na kutekeleza kazi zao kwa mujibu wa sheria?

Zamani tulikwa na treni na hizi ni mara chache kukubwa na ajali mbaya kiasi hiki, labda viwe vitendo vya kigaidi. Lakini sisi na serikali yetu hatujui tunataka nini. Angalieni tusijekusingia kuwa haya yanaletwa na East Africa Community!
 
Poleni majeruhi...Hivi speed governors zimeishia wapi?
 
mmh! Jamani mbona tutamalizika kwa ajali. Poleni wote mlofikwa na mashwahibu hayo
 
Mi naona serikali ina mchango mkubwa katika ajali hizi zinazoendelea kutokea. Hasa katika miundo mbinu ya barabara, Utakuta sehemu hatarishi kama vile kwenye madaraja au kwenye kona kali barabara inakuwa finyu kabisa, hata kupishana kunakuwa kwa Timing, sasa kwa mtindo huu si kuwalaumu tu Drivers bali pia tuangalie hali halisi ya barabara zetu. Sidhani kuwa kuna Driver anayependa kufa au kupata ulemavu wa maisha
 
Mi naona serikali ina mchango mkubwa katika ajali hizi zinazoendelea kutokea. Hasa katika miundo mbinu ya barabara, Utakuta sehemu hatarishi kama vile kwenye madaraja au kwenye kona kali barabara inakuwa finyu kabisa, hata kupishana kunakuwa kwa Timing, sasa kwa mtindo huu si kuwalaumu tu Drivers bali pia tuangalie hali halisi ya barabara zetu. Sidhani kuwa kuna Driver anayependa kufa au kupata ulemavu wa maisha
Nakupongeza mambo mengi yanasababishwa na serikali mfano mkuu ni pale kibamba. Toka dar to moro unakutana na kona ghafla tena unakutana na tuta umalizdpo daraja tuta tena baada ya hapo mlima unapandisha.ona madhara yake endapo gari ghafla mno likakata breki driver atakomaa na usukani ndo mwokozi wake. Gari ikienda kwa kasi analala na kona na ghafla tena anakutana na tuta gari inapaa angani ujanja hakuna anasubiri lijiongoze.MUNGU IBARIKI TZ
 
Moja ya mambo yanayosikitisha lakini ambayo watanzania tumeyaona ya kawaida masikioni mwetu ni ajali za barabarani. Nafikiri sasa tufike mahali tujiulize kwanini kila baada ya siku 2 tunasikia kuna ajali imetokea mkoa fulani, watu kadhaa wamekufa, na kadhalika. Kwa mfano hii ajali iliyotokea Tanga leo na kukatiza yaisha ya wanachuo karibu 18 wakiwa kwenye fuso

Kwa uchunguzi mdogo nilioufanya nimebaini kuwa mbali na uzembe wa madereva na ubovu wa magari, sababu kubwa inaweza ikawa ni uzembe wa serikali katika kusimamia sheria

  1. TRA wanatoa leseni za madereva, lakini hawana kumbukumbu sahihi (database) ya madereva wenye leseni halali. Nasema hivi baada ya kushuhudia mtu akiwa anamiliki leseni mbili original zilizotolewa na TRA ndani ya siku 14 kwa mtu huyohuyo na jina lilelile. Hii ina maana madereva wanaposababisha ajali huwa hawaogopi kuhusu leseni yake kunyanganywa au kuchafuka, kwa kuwa ana uhakika wa kupata ingine bila tatizo ndani ya muda mfupi.
  2. Leseni nyingi za madereva hasa wa mjini zinanunuliwa, mtu akisema ni vigumu kupata leseni class C, maana yake utatakiwa kutoa pesa nyingi zaidi. Suala la udereva kama taaluma ya kusomea shule linaonekana halina maana yoyote kwa Trafiki wetu wanaotakiwa kuwafanyia usaili madereva
  3. Mtu akikamatwa kwa kosa la barabarani, ana uhakika wa kumaliza hilo tatizo na huyo askari aliyemkamata, kwa hiyo hakuna faini yoyote itakayolipwa serikalini.
Kwa mazingira haya yanayozunguka usalama wa barabarani sijui hizi ajali zitaisha au kupungua mwaka gani
 
Mdau, Hili kweli ni Tatizo kubwa kwa Taifa letu, kwanza nguvukazi kubwa inapotea,Pili resources zetu ni Haba hasa madawa na hospitals.

Ajali za magari zinaongezeka kutokana na sababu kubwa moja. Siku hizi chanzo kikubwa cha kusafirisha mizigo na abiria ni barabara, Miaka ya nyuma Reli za TRC na TAZARA zilitumika sana, pia Meli za Shirika la Reli. Kwa sasa barabara zetu zime jaa misururu ya magari makubwa yame beba Macontainer,na Mizigo mingine kama Carterpillar za migodi na ujenzi wa barabara. Mengi ya magari haya, yana mwendo mdogo kutokana na mizigo mizito au ubovu. hii inalazimisha magari mengine kuya overtake na hapo ndipo ajali nyingi hutokea.

Sasa nani alaumiwe?

Kama TRC isingehujumiwa,Macontainer mengi yange safirishwa kwa njia ya Reli hivyo ajali nyingi zinge epukika.
 
Wanajf bus la spider limepata ajali kilometa 10 toka morogoro mjini likienda dar asubuhi hii.taarifa kamili zitapatikana maana bado askari wako eneo la ajali ila kama kuna mwanajf ana ndugu ambaye anasafiri na spider au yuko safarini kwa njia hii ya moro dar basi amtafute ili ajue wapi alipo.
 
Nimepigiwa simu kuwa walitaka kugongana uso kwa uso na basi liendalo Mwanza Luck Star na kwamba dereva wa Spider ndio kajitahidi kukwepesha na kupinduka. Jamani hawa madereva watatumaliza, hivi ule utaratibu wa kuweka alama kwenye leseni za Madereva wanaofanya ajali bado tu? Polisi harakisheni jamani tutakwisha!!!!!
 
Thanxs kwa taarifa lakini taarifa ipo jukwaa lisilohusika!
 
Heshima mbele wakuu wa jamvi.Nimeonelea niwajuze kwa uchache na kipicha zaidi juu ya ajali iliyotokea mida ya saa moja ikihusisha RAV4 kugonga kibanda cha walinzi na kujeruhi walinzi pamoja na kufanya uhalibifu wa ATM room.

Samahani kwani mwanga wa picha ulikuwa mdogo na kwa hivyo zitaonekana kwa uhafifu ila nilifika kwa kuchelewa kidogo na kwa ufupi ndiyo hayo kama kutakuwa na mtu mwenye taarifa zaidi atujuze ila gari ilitokea mitaa ya baharini ikienda maktaba na ghafla ikaingia kwenye ATM ila nahisi dereva alikuwa amelewa.

Tafadhari Mode ikishasomwa waweza kuifuta/kuihamisha hapa

Walinzi wamepelekwa hospitali

Nawakilisha
 

Attachments

  • IMG00020-20100610-1901.jpg
    IMG00020-20100610-1901.jpg
    401.7 KB · Views: 125
  • IMG00019-20100610-1901.jpg
    IMG00019-20100610-1901.jpg
    342.5 KB · Views: 94
  • IMG00022-20100610-1902.jpg
    IMG00022-20100610-1902.jpg
    297.9 KB · Views: 82
  • IMG00012-20100610-1856.jpg
    IMG00012-20100610-1856.jpg
    372.8 KB · Views: 98
Back
Top Bottom