Hii imerudi tena, haya. Kwa kiasi kikubwa ni barabara na si ubovu tu bali na jinsi zilivyo ni tatizo. Kinafuata madereva kutokuwa waangalifu, kwa sababu wangekuwa waangalifu japo kidogo tu ingepunguza hizi ajali. Walioko Ujerumani wataungana nami, ukiwa unataka kuvuka barabara na ukaigeukia iwe ni kwenye zebra cross au sio magari yote yatasimama. Binafsi nilipata taabu sana wakati fulani kwani sikuwa nimelijua hili, na kila nilipokuwa nikiangalia upande wa barabara nikashangaa magari yanasimama ndio nikajua nawapa watu taabu kwa kunisubiri nivuke kumbe mimi nina shida yangu nyingine. Kwa hiyo utaona ustaarabu na uangalifu unahitajika.
Kuhusu barabara, hapa ndio kwenye muskel mkubwa. Barabara zetu karibu zote zipo chini ya kiwango na ndio maana barabara inajengwa leo kesho watu wanafikria kuweka matuta. Wakati kabla ya kujengwa ilikuwa yote yawe yamekwisha onekana na ufumbuzi umeshapatikana, ikiwa ni pamoja na kuzuia ajali na jinsi gani waendao kwa miguu watavuka. Karne ya 21 tunajenga barabara tunayoita high way na matuta tangu mwanzo hadi mwisho?, na tusipofanya hivi watu wanagongwa kwa kwenda mbele.