Mlipuko wa masalia ya mabomu Mbagal: Je, Dr. Mwinyi ajiuzulu?

nchi ya watu hii, yetu macho, kama kusema tumeshasema sana hakuna kinachoendelea
 
labda yangelipuka pale NGOME wangeweza kuwajibika ila kwa mbagala tutaongea mpaka tuchoke hawajibiki mtu
 
Mtu mwenye akili timamu atajua kuwa Bwana Mwinyi ana nafasi hiyo kutokana na baba yake kuwa Rais-Mzee Ruksa!!!
Anatayarishwa kuwa Rais wa Zanzibar baadee,japo ni mbara!
Ajabu ya Tanzania!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Angejiuzuru tuu kujenga jina na heshima yake mzee wake alijiuzuru alipokuwa waziri wa mambo ya ndani lakini badae akaja kuwa Rais wa ZNZ.

MJ
 
Tanzania hakuna utaratibu wa kujiuzulu bila kulazimishwa na nguvu ya umma, sitarajii mwinyi akajiuzulu kwa sasa ilhali anangojea kwa hamu urais wa zenji,kwani yeye hajipendi kwa kujipaka matope?
 
tanzania hatuna culture na kuachia ngazi tunapoaribu kazi! nashangaa hii issue ya mabomu inazimika taratiiibu siku zinaenda...kweli watanzania sisi hatuna hasira...wakazi wa mbagala mnatakiwa kuandamana...vyama vya upinzani chukueni hii nafasi kuanza kampeni mapema!
Kuna upinzani nchi hii au waganga njaa!
 
Huyu hawezi kujiuzulu akiwekee matope kitumbua chake cha ukuu za Zenj. Nasikia anapanga kuuza zile flats zake za kupangisha pale Mikocheni darajani $2.5 millioni ili asijeonekana fisadi wa aina flani vile.
 
Ndo hivyo watoto wawili wamesha poteza maisha na wengine wanne taabani.
Si walisema wataleta vifaa vya kusasa kuja kufukua na kusaka vipande vilivyo salia?
Ok nimegundua kwa vile kule wanaishi walalahoi haya mabomu yangelipuka kwa matajiri Mbezi beach huko najua serikali ingeleta wamerekani kuja kusaka vipande.
you are right mkuu
 
Nafikiria niuze plot yangu kule temeke (tuangoma) make nasikia makombora yameelekezwa huko.
 
Kwenye uchaguzi mdogo mwaka huu na ule mkuu mwakani, semeni SIDANGANYIKI kwa wagombea wa CCM.

Bila kuiondoa CCM madarakani, hakuna mabadiliko ya maana (+ve) yatakayopatikana. Uzembe kama huu wa Mbagala, utakuwa wimbo wa kila leo.
 
matangazo ya sidanganyiki ndio yamepigwa marufuku hivyo..

Hakuna kitu kinashinda nguvu ya umma. Wananchi wakigangamala, sidhani kama amri hiyo itakuwa na nguvu. Woga wa wananchi ndio inaweza kuwa tatizo kubwa hapa. La muhimu zaidi, wananchi tutekeleze hiyo mbiu ya sidanganyiki kwa vitendo; kwa kuikataa CCM.
 
Mtoto aliyejeruhiwa Mbagala afariki


na Datus Boniface

[source Tanzania Daima]


IDADI ya watoto waliokufa kwa ajali ya mlipuko wa mabomu ya Mbagala imezidi kuongezeka na kufikia watatu baada ya marejuhi mwingine kufariki usiku wa kuamkia jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Mtoto huyo , Stella Chalawa (2), alifariki baada ya kuhamishiwa kwenye wodi ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum, mahtuti ICU).

Taarifa ambazo Tanzania Daima Jumapili ilizipata jana na kuthibishwa na mfanyakazi mojawapo wa hospitali hiyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini zilisema kuwa hali ya mtoto huyo ilizidiwa kuwa mbaya kutokana na majereha aliyokuwa nayo.

"Yule mtoto (Stella), alifariki majira ya jioni jana (juzi) kwani alizidiwa sana, majeraha aliyoyapata yalikuwa ni makubwa…, lakini mimi sio msemaji wa hospitali jaribu kuwatafuta viongozi watakuambai zaidi, alisema mfanyakazi huyo.

Chanzo cha habari hicho kilisema kuwa, maiti ya mtoto huyo ilichukuliwa jana na ndugu zake kwa kufanya mipango ya mazishi, ambapo pia taarifa ambazo gazeti lilizipata kutoka kwa ndugu wa marehemu huyo ni kwamba walifanya taratibu za mazishi jana.

Mapema wiki hii, watoto wawili waliripotiwa kufariki baada ya kulipukiwa na bomu wakicheza kwenye eneo linalozunguka kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) iliyopo Manispaa ya Temeke, Dar es Salaam.

Serikali imeunda kikosi maalum ili kutafuta masalia ya mabomu mengine baada ya kuonekana yakiendelea kulipuka hovyo.

Alisema kuwa kikosi hicho kitatumia vifaa vya kitaalam zaidi kuhakikisha hakuna masalia ya vipande yatakayoleta matatizo tena.
 
Last edited:
Dk. Mwinyi alipata kunena kwamba kama kuna uzembe twenye hili tukio basi atajiuzulu. Huu ni wakati muafaka wa yeye kufuata nyayo za baba yake na kujijengea heshima kwa KUJIUZULU. Akumbuke Mzee Mwinyi alipata kujiuzulu kutokana na uzembe uliofanywa na watu walioko chini yake na bado baadaye akaja kuwa rais.

Kama Dk Mwinyi haoni hapa pana uzembe basi yeye ni mzembe wa kufikiri.

Halafu inasikitisha sana kuona Lukuvi akiongea kwenye luninga (huku Maofisa wengine wa jeshi wakicheka kwenye kikao) eti walitafuta mabomu yaliyokuwa juu ya ardhi tu. Dar es Salaam ardhi yake sehemu kubwa ni mchanga mtupu. Ina maana wanajeshi wetu hawana akili ya kufikiri kwamba haya mabomu yaliyotengenezwa kwa chuma ukiyarusha juu wakati yanatua hayawezi kujichimbia chini ya ardhi? Shame on you!

Hivi wale panya wa SAU wenye kunusa mabomu wako wapi? Au nao wananusa juu ya ardhi tu?
 
Tanzania hatuna desturi ya kujiuzulu, hivyo haiwezi kuanza leo.

Ile ya shinyanga ilkuwa an exception to our general rule ya kutojiuzulu.
 
Tunaambiwa Tanzania ni nchi yenye amani duniani pote!Huwezi ukawa Maputo Mozambique, au Luanda Angola mabomu yakalipuka down town!Ni kama tuna landmines Dar Es Salaam ,na vita haijawahi upiganwa!Kikwete anakula nchi Marekani!

It is sickening
 
Mnanichekesha wanasiasa! Kwanini JK awajibishwe, inamaana waliojenga karibu na kambi ya jeshi hawakufahamu madhara yake? Madhara ndo hayo yanaanza, mnawatupia rawama viongozi kwani ndo waliowapimia viwanja? Wizi mtupu

Redey wewe ndiye unayechekesha!!

Hawa waliojenga karibu na Jeshi walijipimia viwanja wenyewe? na hata kama walijipimia serikali haikuwaona na kuwazuia kama ni eneo la jeshi?


Sitaki kwenda mbali maana nadhani hutanielewa, fikiria uchungu walionao wafiwa na jiweke nafasini mwao
 
Back
Top Bottom