Kama hii habari niya kweli basi ninaanza kuhofia kama kuna uwezekano yale yaliyotokea Westgate shopping mall pale Kenya yakafanyika tena Tanzania.
Kadri wanavyofanikiwa katika 'mission' zao ndiyo pia wanazidi kupata ujasiri wa kufanya maangamizo zaidi kwa maana kuwa kama wanaweza kufanikiwa mara tatu Arusha, wanaweza kusema, 'let's move to anaother area/region' au wanaweza kuamua kufanya mission kubwa zaidi.
Usalama wa Taifa wako wapi kwa sasa pamoja na budget kwenye ofisi ya Rais kuongezeka kila mwaka wa fedha. Yaani kadri badget inaongezeka na utendaji wa watu wa Usalama wa Taifa unapungua.
Utashangaa viongozi wetu watakapo jipanga kutoa pole na kulaani walipua mabomu baada ya kufanya juu chini kuhakikisha wananchi wake safe kama katiba ya nchi inavyotaka.
Kwanza hata mipaka ya Tanzania iko wazi. Tumeona kule Kigoma watu wakivuka mto kutoka Tanzania kwenda Burundi kufanya biashara na kurudi bila bughudha yoyote. Kama kuna mtu wa nje anataka kutenda makosa nchini anaweza kuingia bila tatizo lolote.
Poleni sana wana Arusha na hasa wale mliofikwa na haya majanga.