Mlipuko mkubwa waitikisa Arusha!

Mlipuko mkubwa waitikisa Arusha!

Hizi hapa pic nyingine..
baa+yenyewe.jpg


uharibifu.jpg


Mlipuko wa bom uliotokea jana bar ya Night park Arusha
 
Wamepiga tena?

Watu kadhaa wamejeruhiwa kutokana na mlipuko unaodhaniwa kuwa ni wa bomu katika baa maarufu ya Arusha Night Park katika eneo la Mianzini katika jiji la Arusha.

Tukio hilo lilitokea jana saa mbili usiku wakati mamia ya watu wakiwa katika baa hiyo wakiangalia mechi ya soka ya Ligi Kuu ya England kati ya Chelsea na Swansea. Chelsea ilishinda 1-0.

Mmoja wa wamiliki wa baa hiyo, Angelo Mwoleka pia alithibitisha kutokea mlipuko huo na kueleza kujeruhiwa watu kadhaa.

"Ni kweli kuna mlipuko umetoka na watu kujeruhiwa, mimi sikuwepo ila nipo njiani nakwenda eneo la tukio, "alisema.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, John Lymo alisema watu saba waliumia vibaya kutokana na bomu hilo na walipelekwa katika Hospitali ya Mkoa Arusha ya Mount Meru.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus (pichani), alisema: "Hivi sasa tunaendelea na uokoaji na uchunguzi umeanza."

Tukio hilo limekuja wakati bado jiji la Arusha likiwa na kumbukumbu ya kushambuliwa kwa mabomu kwa Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi lililopo eneo la Olasiti na jingine Uwanja wa Soweto wakati Chadema walipokuwa wakifunga kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani. Katika matukio yote hayo, watu sita waliuawa na wengi kujeruhiwa.

 
Ninamashaka na watu wa uhamiaji wameingiza magaidi......... tumeingiliwa,
 
Wasomali kutoka Kenya wanahusika(Alshaabab). Rejea uchaguzi mdogo wa udiwani Makuyuni jinsi walivyomwumiza Mh Nasari kwa kipigo.Hili kundi la wasomali ndo wauaji wa tembo,wafanyabiashara madawa haramu kama miraa/mirungi,majambazi kwa kutumia silaha za kivita, na zaidi wafadhili wa CCM.
 
au jirani anataka kutuvurugia sekta ya utalii ili wote tupoteze kama yeye?siwaamini majirani zetu.
 
Damn you!! Who the hell are you to the extent of judging others??? If you dont have anything to say just shut your buccal cavity up!

Nahisi unatumia maziwa kama akil kufikir na u know nothng abt bible! shiit!
 
Tangu lema awembunge arusha haikaliki kabisa sujui ndiyo mbinu gani hizi
 
au jirani anataka kutuvurugia sekta ya utalii ili wote tupoteze kama yeye?siwaamini majirani zetu.

We ndio umeongea kitu cha akili sana. Hata mimi mawazo yananituma huko huko.
 
Hivi Ni Kweli Mlipuko Umetokea? Naogopa Kwenda Kuchukua Mshahara Wangu Benki,hivi Si Watapiga Bomu Benki?
 
Muda huu nipo hapa Mount Meru na Ambulance aina Iveco inaelekea uwanja wa ndege KIA kumpeleka rafiki wangu mkubwa Sudi mhanga wa bomu la jana tayari kupelekwa Muhimbili kwa matibabu zaidi.
 
Muda huu nipo hapa Mount Meru na Ambulance aina Iveco inaelekea uwanja wa ndege KIA kumpeleka rafiki wangu mkubwa Sudi mhanga wa bomu la jana tayari kupelekwa Muhimbili kwa matibabu zaidi.

Poleni sana kaka nawaombea kila la heri apate huduma inayostahili
 
Raia wa Arusha shirikianeni na serikali kudhabiti matukio haya yasije leta maafa makubwa zaidi,,maana ugaidi ni mwingi Kenya isije kuwa ni moja ya milolongo ya matukio ya kigaidi nchini kwetu.
 
Raia wa Arusha shirikianeni na serikali kudhabiti matukio haya yasije leta maafa makubwa zaidi,,maana ugaidi ni mwingi Kenya isije kuwa ni moja ya milolongo ya matukio ya kigaidi nchini kwetu.

mabomu warushe na polisi halafu unataka tushirikiane nao kwa lipi..
 
Back
Top Bottom