Mlioolewa mnawezaje kufanya haya?

Mlioolewa mnawezaje kufanya haya?

Ikumbukwe pia sio kila mwanamke anafaa kuolewa.
 
Napenda wanawake kama nyie maana mnatoa nafasi murua kwa house girl kua msaidizi mwenye umuhimu zaidi hakika mumeo atafaidi duh nimeikosa bahati maana nimeshaoa.
Tunasubiri ukifika miaka 30+ uje tena kuanzisha thread ya vilio kua umekosa ndoa na una mkosi na ukibahatika ndoa hakika utadondokea mikononi mwa bazazi mwenyewe utanyooka maana ukiingia ndio utaelewa ukiwa nje utaongea pumba kama hizi.
 
Hayo yote unafanya hata kama hujaolewa, mtoto wa kike mwenye maadili hayo ni ya kawaida sana, Sijui mwenzetu umefunzwa vipi.
 
Hivi inakuja naturally kumpikia mumeo, kufua nguo zake kutandika kitanda chenu?! Au huwa mnajilazimisha.... :-D:-D :-D

Mie nitafanya hivo vyote mume wangu akiwa disabled, kinyume na hapo sidhani kama nitaweza.

Na kwa tabia hiyo hutopata ndoa na ukipata haidumu
 
Hivi inakuja naturally kumpikia mumeo, kufua nguo zake kutandika kitanda chenu?! Au huwa mnajilazimisha.... :-D:-D :-D

Mie nitafanya hivo vyote mume wangu akiwa disabled, kinyume na hapo sidhani kama nitaweza.
We bado msichana.ukipevuka utajielewa.
 
ukiijua wajibu wako utafanya zaidi ya hayo na ukute mume naye anawajibika yani unaweza kaa ukawaza umfanyie jambo gani la ziada ili afurahi!ACHENI NDOA IITWE NDOA NA ACHENI MAPENZI YAITWE MAPENZI!
 
Utafanya vyote kama wajibu wako na kuna vitu vyadharura vitajitokeza utamfanyia tu ukishakuwa mke nitofauti na mpenz au mchumba hapo ndio uanamke wako unapoonekana.umesahau kumyooshea (kumuandaa) ili aende kazini sasa usiombe awe anakunywa chai kabla ya kwenda kazini ndio utajua kuwa wewe ni mwanamke
 
Hivi mke ukimuoa unajua kazi yake nn?!mke ni pambo hizo kazi kuzifanya au asizifanye ni uamuzi wake hatakiwi kushurutishwa.labda km ikiwa usafi wa mwili wake ndo unaweza kumlazmisha ila kisheria ht za kidini mkeo akikulelea watoto wako inatakiwa umlipe pesa!mkeo inatakiwa umwekee msaidizi ndani na sokoni mume ndo uende ila wengi wetu hatujielewi tu.me mke wangu ni malkia kila kitu namfanyia!yeye akifanya ni kwa mapenzi tu
 
Ndo maana ma housegirl wanalala na wanaume zenu then mnalalama kwa sababu ya tabia kama hizi.
 
Mwanaume nao hukatisha tamaa unafanya vyooote mwenzio anakuona wakuja tuu onyesheni ushirikiano ata ucipomsaidia kumpa pole kumshukuru. Anafarijika moyoni
 
Usjali Kila mwanamke Ni wife material inategemea na material mwanaume anayoyataka. Utampata wa material hayo. Kuna wanaojua kufanya yote hayo na wanapenda kuyafanya ila hawapati wa kuwaoa na Kuna ambao hawapendi kujituma na kumfanyia mume wake hayo bado wanaolewa. Kuolewa Ni bahati. Kazana mama na material yako.
 
Hivi kumbe hata wewe una ndoto za kuolewa? Kwa attitude hiyo?? Sijui kwanini watu wanayatazama mapenzi na kuyaishi kibabebabe!!! Hata hivyo, sidhani kama kuolewa let alone kudumu katika ndoa is your call. Wewe una nyota ya "mchepuko sugu". Ila unaweza umpate mwendokasi mwenzio...kila la kheri mkuu
 
Hivi inakuja naturally kumpikia mumeo, kufua nguo zake kutandika kitanda chenu?! Au huwa mnajilazimisha.... :-D:-D :-D

Mie nitafanya hivo vyote mume wangu akiwa disabled, kinyume na hapo sidhani kama nitaweza.
Kumbe ww unajua ndoa ni kupigwa mwendo kasi tu daaah unazidi kuchelewaa mdada ndoa ni zaidi ya kujitoa yaani hata nashindwa kikukuelezea endelea kudhani kupigwa mwendokasi tu
 
mimi afadhali gari langu liwe mkangafu lakini sio la mrs!!
afadhali nisivae vizuri lakini sio mrs.
afadhali nikose pocket money lakini sio pochi wa mrs.
afadhali nisipulizie a good perfume lakini sio mrs.
afadhali nave kiwembe lakini sio mrs.
So mke ndio kila kitu ni wajibu wangu, na yeye anajua wajibu wake kwangu. na sio kwamba sasa anafanya 24/7 hapana kama upendo upo mbona mnafanya wote tuu ila chief incharge ne yeye. alaskini kama ana kisirani huko jikoni atanisikia tu, tutakutana ndani ya shuka na lazima makamuzi yawepo!! maana ni masharti ya ndoa. hata akidunda mkifika 6x6 ngoma inapigwa sawia!! hehee , sasa nyie wa leo mkisemwa tu mwavaa jeans!! matokea jama huyooo ananoigesha nje , sasa ole huko nje kuwe kutamu na manjonjo kuliko wewe!!!!
Kwisha!!!
Mtumeee roho yangu!!!! Unatupa majaribu
 
Back
Top Bottom