Mliooa mtupe mrejesho sisi mabachela

1. Kikubwa upendo, kuwa kando na umpendaye, raha iliyoje.
2. Unakuwa na mtu wa kupanga na kupangua mipango mbalimbali ya maendeleo, waonaje hapo!! Rahaaa
3. Mnapojaaliwa kupata uzao, furaha ya kuwa na watoto na kuona wapo na furaha.
4. Kampani, unakuwa na mtu wa kushauriana nae mambo mbalimbali
5. Kupungua kwa baadhi ya majukumu ya kinyumbani, mfano kudeki, kufua, kupika japo hii kama upendo upo mnaweza kujikuta mnafanya wote hizo kazi
 
 
Wewe fahamu tu haya
1. Ndoa ni kama jambo la lazima kijamii, usipooa rasmi utaishia kuoa kienyeji, usipooa ukiwa kijana utaoa uzeeni, na kukwepa kuoa kunaweza kukutesa zaidi, hivyo jipange tu kuoa.

2. Kwenye ndoa hakuna kipya au cha maana sana, ni maisha haya haya.

3. Jipange kuumiza au kuumizwa, ndoa ni taasisi ya kuumizana.

Mambo mengine utakutana nayo mbele ya safari ukishaoa.
 
Imeandikwa "kijana atamuacha baba yake na mama yake, ataambatana na mke wake nao watakuwa mwili mmoja"......mwanamme atampenda mke wake na mke atamheshimu mume wake"
 
Umetokea familia ya aina Gani? Kama umekuzwa ktk familia yenye malezi ya baba na mama na yenye utulivu baadhi ya faida utakuwa unazijua tayari, kama umetokea kwenye familia ya single Maza basi endelea kusubiri comments za wadau
 
Huu uzi maalum kwa wale waliooa; tunataka kujua faida mnazozipata baada ya kuoa au tuseme ni kitu gani mnaweza tushawishi sisi ambao hatujaoa tuchukue hatua kama nyinyi, hebu mtupe faida mnazozipata baada ya kuoa ambazo sisi mabachela hatuzipati.
Ni basi tu, nimechelewa kuoa nikiwa 31's lakini amani ninayoipata, Ndugu zangu wenyewe wameshangaa kwanini nimeshindwa kabisa kupungua unene mbali na kufanya kote mazoezi na kuzingatia balanced diet

MUNGU apewe sifa na utukufu
 
Nimekosa uhuru kabisa,kutumia simu tu ni mtihani,mara aniongeleshe wakati niko nasoma nyuzi za watu humu mara anilalie nishindwe kutumia simu

Natamani kupata mwanya wa kula mbususu mpya zinazojileta nakosa

Suruali zangu za kadeti zinapauka sana kwasababu ya kufuliwa sana na mashuka pia yanafuliwa mpaka yanachakaa ndani ya muda mfupi

Kiukwel siifurahii ndoa,hata hivyo toka zamani nilikuwa sipendi ila niligandwa nikajikuta nimekamatwa kizembe
 
Back
Top Bottom