Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,034
- 144,387
Watu wenye akili, werevu na wazalendo walipokuwa wanalilia demokrasia wakati wa Mwendazake, walipingwa kwa hoja dhaifu kama vile demokrasi inachelewesha maendeleo na kwamba sasa tumepata kiongozi anaeweza kutuvusha na kuwa demokrasia ya kuchagua na kuchaguliwa haina maana na hata katiba bora nayo sio issue ya msingi tumuache Jembe apige kazi.
Leo hii tunashuhudia matunda ya kutokuwa na Bunge lilichaguliwa na wananchi wakipitisha na wakibarikia mkataba wa kuwakabidhi Waarabu waendeshe bandari yetu haya yakiwa na matunda ya Bunge la Chama kimoja linalofanya kazi yake chini ya hii katiba mbovu inayotoa madaraka makubwa kwa Raisi wa nchi hii.
Maswali:
1. Mliokuwa mnaona sahihi Mwendazake kuminya demokrasia, leo hii mna haki ya kulalamikia yaliyofanywa na hili Bunge?
2. Thamani ya kiuchumi ya miradi aliyoianzisha Mwendazake, inaweza kufidia hasara ya kiuchumi itayotokana na kuwapa wageni waendeshe Bandari yetu iwapo mkataba huo kweli utakuwa wa kimangungu?
3. Tungekuwa na uchaguzi huru, tungepata Bunge la kupitisha mikataba kama hii kirahisi kama ilivyotokea?
4. Je, bado mnaamini Mwendazake alikuwa sahihi katika misimamo yake?
5. Je, hamuoni kuwa Mwendazake alikuwa ni kiongozi asieona mbali?
6. Wafuasi wa Mwendazeke, bado hamuoni nchi hii inahitaji strong institutions na sio strong individuals?
7. Iwapo kweli Mkataba huu utakuwa mbovu kwa nchi yetu, baada ya Mama, mtu wa pili wa kulaumiwa katika hili la Bandari ni nani zaidi ya Mwendazake?
Endeleeni kupuuza madai ya katiba mpya mkifikiri mnawakomoa CHADEMA wakati huko majumbani mwenu mna watoto wadogo wataokuja kurithi hii nchi hapo baadae nyie mkiwa vikongwe au teyari marehemu.