Sababu ya wadau kupigania demokrasia ni kupigania maendeleo

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,609
8,753
Wadau wengi kama mimi tuna amini kwamba kupigania demokrasia ni kupigania maendeleo. Ni lazima tujue kwamba demokrasia nzuri inaendana na katiba nzuri, bunge la ushindani, Uraisi wa ushindani na serikali za mikoa na wilaya za ushindani. Haya ni mambo machache ambayo yanasababisha sisi wadau kupigania demokrasia na katiba mpya

1. Kukiwa na sheria nzuri na za wazi zitaongeza uwekezaji. Mfano tukiwa na sheria ambao mabadiliko ya Raisi yanaweza kuwepo bila kuhatarisha mitaji ya uwekezaji. Kitendo cha Raisi kuamua tu kuzuia pesa za wafanyabiashara bank ay kwenda kwenye maduka ya pesa kuchukua pesa si mazuri kwa wawekezaji. Hii dhana ya Raisi kuwa na uwezo wa kufanya chochote na lolote linahatarisha uwekezaji kwa kiasi kikubwa. Ni vizuri kuwe na sheria ambazo haziwezi kuingiliwa kisiasa.
2. Wananchi wanatakiwa wawe huru kuwachagua watu wa kuwawakilisha bila kuingiliwa na polisi, jeshi na wasimamizi wa kura wa vyama. Tume ya Uchaguzi inatakiwa iwe huru kwenye pesa, ichaguliwe na wadau huru, wasiripoti wa Raisi mgombea na wawe na kinga kisheria. Lakini kinga iwe pamoja na kutoingiliwa na Polisi.
3. Katiba ni muhimu kwenda na wakati ikiwa pamoja na sheria za Ardhi, diaspora, taasisi mbali mbali na urahisi wa kufungua biashara.

Demokrasia inaongeza usalama ukiangalia nchi zenye vita nyingi utakuwa hazikuwa zinatawaliwa kidemokrasia mifano ipo mingi sana.

Hivyo huwezi kutaka maendeleo ya Tanzania wakati huohuo hutaki katiba mpya. Unatakiwa kupenda nchi kuliko vyama.
 
Rwanda,Burundi,DRC na Uganda ni mfano mzuri.Kiongozi kuwa kama Mungu hudumaza fikra za wananchi wake.
 
Back
Top Bottom