Hili la Bandari, lawama hii iende kwa hayati Magufuli

Diwani

JF-Expert Member
Oct 25, 2014
2,672
2,697
Bado sehemu mbalimbali za nchi yetu zinaendelea kujadili kuhusu Uwekezaji wa DP-World. Mbaya zaidi, mitazamo inayotolewa sasa inajadiliwa kwa milengo ya kidini, jambo ambalo si la kawaida katika nchi yetu.

Ni nini mzizi wa haya yote?

Kisa kilianza Mwaka 2020, wakati wa Uchaguzi Mkuu. Ulikuwa ni moja kati ya chaguzi ambazo zilijawa na malalamiko mengi kutoka upinzani, uvunjifu wa sheria za uchaguzi na kupeleka Uchaguzi ule kugubikwa na ripoti chafu za Waangalizi wa ndani na nje.

Lakini kwa nini haya yote yalitokea?

Haya yote yalitokea ili kutimiza adhma ya aliyekuwa Rais wa wakati huo Hayati, Dkt. John Magufuli ya kutaka kutengeneza Bunge la Jamuhuri ya Muungano lenye wanachama wa chama chake tu (CCM). Hili linathibitishwa na kauli yake aliyoitoa Tarehe 22 Januari 2020, alisema;

“Haiwezekani Mkurugenzi nikuteue mimi, nikulipe mini mshahara na kukujazia mafuta kwenye gari halafu kwenye Uchaguzi utangaze kuwa Mpinzani ameshinda”

Kauli hii ndio leo hii imesababisha leo bunge letu kuwa ni Bunge la chama kimoja. Hivyo, maamuzi yote kufanywa kwa kuridhisha chama na viongozi wake wakuu, wakiwamo Rais wa Jamhuri ya Tanzania kama Mwenyekiti wa Chama hiko.

Je, hasara ya jambo hili ni nini?

Hapa kwenye hasara ndipo kwenye lawama, Magufuli alituachia Bunge lisilo na meno, Bunge ambalo lingekubali kila kitu kwa kuwa kimekubalika na Rais ambaye ndiye Mwenyekiti wa chama. Bunge linalopitisha hoja bila kuchunguza kwa kina.

SUALA LA BANDARI SI LA KUJADILIWA VIJIWENI NA KWENYE NYUMBA ZA IBADA.

Haya maoni ambayo watu wanayajadili, vipengele ambacho vinatia shaka kwenye Mkataba, vilipaswa kujadiliwa bungeni kwa sababu, Bunge ndicho chombo pekee chenye Mamlaka ya kuongoza mijadala hii ambayo imezua gumzo, si kuacha mambo haya kwenda mpaka kwenye nyumba za ibada.

Naamini ya kuwa; kuna kundi kubwa la Wabunge ambao wanaamka sasa hivi kutambua kumbe kuna baadhi ya vipengele katika Mkataba vinazua utata, ila walivyokuwa bungeni, kwa sababu ya “Mob Psychology” wakakubali tu bila kuvitathimini ili vinapofika mtaani wananchi waelewe kuwa Bunge lao limejadili kitu gani kupunguza uwezekano wa kuzuka kwa utata huku mitaani.

Matokeo yake, suala hili linajadiliwa kidini leo hii. Tupo kwenye hatari ya KUGAWANYIKA.

JE, CCM HUJALI MASLAHI YA CHAMA KULIKO NCHI WANAYOONGOZA?

Ni rahisi sana kwa mtu yeyote kujibu swali hili kwa jibu la NDIO. Kwa sababu kuu mbili;

  1. Hoja nilizojadili hapo juu, naamini Hayati Magufuli wakti wa uhai wake hakufikiria madhara ambayo nchi ingeweza kuyapata endapo Bunge litaundwa kwa chama chake tu kupitia kupora Uchaguzi mkuu. Lakini hapa ndipo tulipofikia.
  2. Leo, tarehe 27 Agosti, Rais amekasirishwa sana na amepoteza imani na Mkurugenzi na Mkuu wa wilaya ya Mtwara, kwa sababu ya kushindwa kusambaza kadi za CCM kwa wananchi ambao kwa madai yake wanasema ni Upinzani. Amesema“Siwezi kustahimili kadi za chama zinarudishwa, Mkuu wa wilaya yupo, DED yupo, namtimua leo, kadi za chama zinarudishwa na watu wanashida anaulizwa nini, ooh! Unajua kule wengi wapinzani, so what? Watanzania wale, sina imani na mkuu wa Wilaya aliyesababisha kadi zirudishwe
Inaonyesha dhahiri kuwa, Rais ameumizwa kuona chama kinakataliwa na baadhi ya watu, ila sikuona hatua kama hii ikichukuliwa kwenye ubadhilifu ulioandikwa kwenye ripoti ya CAG.

Makosa yale aliyofanya Hayati, ya kutanguliza chama kisha Taifa. Anayafanya aliyepo sasa. Muda utaongoea.



Mwl. Diwani.



 
Magufuli hakupanda ndege kwenda kujipendekeza kwa waarabu, wala Magufuli hakujigeuza bubu akiulizwa maswali kuhusu mkataba mbovu wa bandari, kuna watu hamna akili kabisa, mpo kama mbuzi tu.

Kumlaumu marehemu aliyeondoka bila kuacha tatizo, halafu unamuacha aliyetengeneza tatizo na bado analilinda, unatafuta laana.
 
Magufuli hakupanda ndege kwenda kujipendekeza kwa waarabu, wala Magufuli hakujigeuza bubu akiulizwa maswali kuhusu mkataba mbovu wa bandari, kuna watu hamna akili kabisa, mpo kama mbuzi tu.

Kumlaumu marehemu aliyeondoka bila kuacha tatizo, halafu unamuacha aliyetengeneza tatizo na bado analilinda, unatafuta laana.
Lakini amezungumzia hadi suala la kutumia mabavu kuhakikisha chama chake ndo kinakuwa na uwakilishi bungeni kitu ambacho kimepelekea kukosekana kwa wapinzani ambao wangepaza sauti bungeni kupinga mambo kama haya.

Ukiwa unatoa maoni yako ondoa hulka ya mahaba niue ndo utaiweka akili iwe huru ku argue mambo.
 
Bado sehemu mbalimbali za nchi yetu zinaendelea kujadili kuhusu Uwekezaji wa DP-World. Mbaya zaidi, mitazamo inayotolewa sasa inajadiliwa kwa milengo ya kidini, jambo ambalo si la kawaida katika nchi yetu.

Ni nini mzizi wa haya yote?

Kisa kilianza Mwaka 2020, wakati wa Uchaguzi Mkuu. Ulikuwa ni moja kati ya chaguzi ambazo zilijawa na malalamiko mengi kutoka upinzani, uvunjifu wa sheria za uchaguzi na kupeleka Uchaguzi ule kugubikwa na ripoti chafu za Waangalizi wa



Wewe utakuwa taahira siyo bure. Hebu mwache Rais wetu mpendwa Magufuli apumzike kwa amani na endelee kuwaongoza Malaika huko mbinguni kwa amani.
 
Kwani mama Abduli alivyo kua anasaini aliamrishwa na mjomba 🤔🤔 Kwani yeye hana akili timamu ya kujua lipi baya na lipi zuri 🤔🤔 Kwani hiyo 2020 mama abduli alikua wapi na alikua nani🤔🤔

Kwa lolote baya liliotokea kwenye utawala wa mjomba huwezi kumuweka pembeni bibi yenu kwa sababu alikua ni msaidizi wake na mengine alitumwa kuyafanya na akafanya,

haya uliyo andika ni mashudu pelekea ngurue bandani, kamuulizeni bibi yenu vizuri kama alipewa mzigo arudishe mapema kabla mambo hayaja haribika
 
Tusikae kimya sasa kusubiri miaka 10 ijayo Rais wetu aandike Kitabu cha kujutia kuingia mkataba huu mbovu wa Bandari, tumkosoe mapema ili akija kuandika kitabu hicho aseme nilishauriwa ila nilikataa Ushauri"-Baba Paroko wetu leo 27/08/2023
 
Back
Top Bottom