Mlinzi wa Obote arudi Uganda baada ya kuishi Tanzania kimyakimya kwa zaidi ya miaka 50

S V Surovikin

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
13,621
32,736
Mlinzi wa Obote arudi Uganda baada ya kuishi Tanzania kimyakimya kwa zaidi ya miaka 50.

Kijiji cha Agora wilayani Soroti nchini Uganda kililipuka kwa furaha baada ya wake wawili kuungana tena na mume wao, waliyedhani amekufa kwa miaka 51 iliyopita.

Bwana Vincent Obodo aliyekuwa mlinzi wa aliyekuwa Rais wa Uganda Milton Obote, alikimbia Uganda mwaka 1971 baada Idi Amin kumwondoa madarakani Obote.

Hiyo ilikuwa mara ya mwisho kwa kuonana wake Bibi Josephine Ariamo, 76, na Anna Loyce Ideta, 71. Bw. Obodo alijificha nchini Tanzania kwa muda wote huo, hadi ijumaa iliyopita aliporudishwa na wafanyakazi wa Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR.

Wake zake hao walisema walidhani amekufa kwani hawajawahi kuwasiliana naye tangu mwaka 1971.

 
Huyo hakua amejificha acha kutaka kumaanisha nchi yetu inehusika kuficha maspy huyo alikua hataki tu kurudi huko kwao unaposema alikuawa amejificha maana yake kwa miaka 50 amekua hajulikani alipo inawezekanelaje hii?
 
Mbona
Umeweka picha ya obote tuu,Yake wapi?!!!
 
Kwani Tz hapa hapa jilani na ug ukae miaka 51 bila kuenda kuona familia huyu alikua na yakwake mengine sio bure
 

 
Huyo hakua amejificha acha kutaka kumaanisha nchi yetu inehusika kuficha maspy huyo alikua hataki tu kurudi huko kwao unaposema alikuawa amejificha maana yake kwa miaka 50 amekua hajulikani alipo inawezekanelaje hii?
 
hiyo kwa kimakonde kile cha ndanindani tunasema "mission is successfully accomplished...job well done officer, now return to your base".
 
Kuna mmoja pia alikua anaitwa Tito alikua kwenye team ya obote aliajiriwaga kama afisa kilimo wakati wa nyerere huko mkoani rukwa akaoa akazaa na watoto sema badae alikuja kupata matatizo ya akili. Aliishi sana namanyere.

Aliwahi kufungwa kwa kosa la kumtoa bibi mmoja jicho jirani yake. Kiuhalisia hakua sawa kisaikolojia.

Huko uganda aliacha mke na watoto walimtafuta sana mpka wakafanikiwa kumpata hivi sasa yuko uganda mwaka wa 5 huu.

Najiuliza hawa walinzi wa obote walipata na nn kiasi cha kushindwa kabisa kurudi uganda licha ya kuacha wake+watoto.
 
Hatari na nusu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…