S V Surovikin
JF-Expert Member
- Aug 8, 2015
- 13,588
- 32,665
Mlinzi wa Obote arudi Uganda baada ya kuishi Tanzania kimyakimya kwa zaidi ya miaka 50.
Kijiji cha Agora wilayani Soroti nchini Uganda kililipuka kwa furaha baada ya wake wawili kuungana tena na mume wao, waliyedhani amekufa kwa miaka 51 iliyopita.
Bwana Vincent Obodo aliyekuwa mlinzi wa aliyekuwa Rais wa Uganda Milton Obote, alikimbia Uganda mwaka 1971 baada Idi Amin kumwondoa madarakani Obote.
Hiyo ilikuwa mara ya mwisho kwa kuonana wake Bibi Josephine Ariamo, 76, na Anna Loyce Ideta, 71. Bw. Obodo alijificha nchini Tanzania kwa muda wote huo, hadi ijumaa iliyopita aliporudishwa na wafanyakazi wa Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR.
Wake zake hao walisema walidhani amekufa kwani hawajawahi kuwasiliana naye tangu mwaka 1971.