Najuta kurudi Tanzania baada ya kuishi ughaibuni miaka 28

joseph2

Senior Member
May 31, 2015
126
251
Jamani wanajamiiForums, kwanza na wasalimia kwa heshima zote. Leo nakuja na story moja ya ukweli ya mzee mmoja aliye amua kurudi nyumbani baada ya kuishi nchini Marekani kwa zaidi ya miaka 28. nimekutana na huyu mzee akiwa kijijini kwake huko mkowani Shinnyanga, kwenye kimji kidogo kina itwa Bukombe. Mimi nilikwenda kwenye kimji hicho kumtembelea rafiki yangu wa siku nyingi kweli kweli. Nilivyo fika kwa rafiki yangu huyo msumbwa.

Wasumbwa ni kabila dogo ambalo mimi huwa nashindwa kulielewa kama ni subtribe ya wasukuma, Wanyamwezi au waha. Goja nisiwachoshe kwa sitori za waha na Wanyamwezi. Basi nimefika kwa rafiki yangu mida ya saa kumi na moja jioni. Rafiki yangu na huyo mzee walikuwa wamekaa kibarazani Wakiongea mambo Yao. Nilivyo fika wakawa kimya kidogo.

Wote wakaanza kunishangaa kidogo. Nikajuwa ni kwasababu mimi na rafiki yangu hatujaonana mda mrefu huwenda hawezi kunikumbuka vizuri. Tangu niondoke nchi kwenda nchi za wengine kutafuta maisha. Tumeisha wahi kukutana uso kwa uso kama mara tatu au nne. Mda mwingi huwa tunaongea tu kwenye simu. Wakati bado wananishangaa, mimi nikavuja kimya kwa kuwasalimia. Shikamo mzee! Akajibu marahaba. Nikamsalimia rafiki yangu, Mara tu baada ya kusikia sauti yangu akanikumbuka na kuanza kunikaribisha ndani kwa furaha kubwa. Wote tu kaingia ndani.

Akatuonyesha sehemu ya kukaa. Tulivyo kaa, rafiki yangu akaita mke wake aje kunisalimia. Imechukuwa kama dakika tatu mke wake kuja. Siunajuwa wanawake lazima kwanza wajiangarie kwenye kio kama maratatu kabla ya kusalimiana na wageni. Basi sisi sebureni tukawa tuendeleza story zetu, huku yule mzee akiwa anatusikiliza kwa maskini. Mara mke wake akaja kunisalimia. Yeye akanikumbuka kiurahisi maana yeye bado kijana kidogo kuliko mme wake.

Mme wake akamwambia mama ongea na wageni kidogo mimi ngoja ni kimbia hapo kwa mzee Shija nakuja Sasa hivi. Mke Akajibu nenda lakini usichelewa nataka niingie jikoni maana najuwa rafiki yako atakuwa na njaa Sana maana safari si mchezo. Itaendelea....
 
Jamani wanajami forum , kwanza na wasalimia kwa heshima zote. Leo nakuja na story moja ya ukweli ya mzee mmoja aliye amua kurudi nyumbani baada ya kuishi nchini marekani kwa zaidi ya miaka 28. nimekutana na huyu mzee akiwa
Rekebisha uandhishi wako mkuu.
 
Back
Top Bottom