Mlima Kitonga vs Mlima Sekenke, upi mkali?

Mlima Kitonga vs Mlima Sekenke, upi mkali?

Kagua tu Guard Rails zilizopo kwenye milima hiyo ndo utajua ni mlima upi mkali kwa maana ya Vertical na Horizontal curves. Lakini pia wakati mwingine angalia material iliyotumika kujenga kipande hicho cha mlima.

Huko ndio unazidi kumchanganya zaid maana hata kujua kama Sekenkr upo au haupo hajui.
 
Sekenke ndo ufananishe na Kitonga? Are you serious? Hata wakati huo uusemao bado Kitango ni hatarishi mara 100 kuliko Sekenke.Saranda ni kawaida sana pale!
sekenke ndio inaongoza kwa ajali kuliko miteremko yote tena hii mpya ndio balsa afadhali ile yazamani haikuua sana
 
kwa wale watu wa kusafiri safiri sana kati ya mlima sekenge uliopo singida mlima ulioua abiria kibao kwa ajari zake yaani mkifika na basi mnasali kwanza , enzi zile mkifika na basi abiria wanashuka na kutangulia kwa miguu than basi linakuja na mizigo na dereva, na mlinga kitonga wa iringa wenye kona kibao, upi unatisha sana kwa madereva?

Sekenke siku hizi limebaki jina tu kwani jamaa wamejitahidi sana kuumaliza na sasa ni kawaida sana,ila kitonga ile ni habari nyingine.juzi wakati natoka iringa mpaka nililihurumia gari langu kwani mguu hautoka kwenye breki hadi inatoka harufu.
 
tena yale maroli yalobeba nguzo hasa ndo huwa yanatisha, alafu madereva wengne wanapita kiboya wanaovatek kwa spidi kwenye vile vikonakonj

Washazoea na wanaona ni mlima wa kawaida sana,lkn pamoja na kutisha kwa kitonga bado hauna rekodi kubwa ya kuangamiza maisha ya watu kama milima ya sekenke na ile ya lukumbure njia ya njombe- songea
 
Kabisa mkuu,umenikumbusha Mashiku bus,pia kulikuwa na super najmunisa abiria wamebanana km daladala za Gongolamboto
Mkuu super najimunisa hadi leo wapo wanajikongoja
 
ungebadili ku compare mlima kitonga 1 na kitonga 2.
Kitonga one from mikumi to iringa via ruaha, mlima kitonga two from Dodoma to iringa via mtera
 
Back
Top Bottom