Hii kampeni, inarejea tukio la Kihistoria katika kupigania Uhuru wa Tanganyika, wakati huo Baba wa Taifa, Hayati Julius K. Nyerere, alikuwa kipiga kampeni ya watu wasinywe bia, zinazozalishwa na viwanda vya wakoloni, kwamba, "ukinywa bia unakunywa damu yako." Ilikuwa ni hujuma dhidi ya wakoloni.
Sasa kwa hili la Vodacom, hapa Mkoloni ni nani, na je yupo peke yake, na je huko kwenye mitandao mingine hakuna wenye sifa hizi za kikoloni - yaani kuwanyonya damu watanzania hadi wapauke zaidi ya sasa, ukimchunguza kuku hautamla.
Tukiacha hili mtakwenda kwenye mradi wa kutoa maji Ziwa Viktoria, kwenda Shinyanga ambako tender ya kusambaza mabomba ilikuwa ni huyu mwizi akilipwa shilingi milioni nne kwa kila moja lililokuwa likisafirishwa kutoka Dar es Salaam hadi eneo la Ihelele, Misungwi Mwanza kwenye chanzo cha maji cha mradi huu.
Hapa Bwana Mamvi alikuwemo ndani katika mradi (wiziii) huu, sijui kama muungwana kwa wakati huo kama alikuwemo kwenye njama hii. Lakini hapa ndipo uhasama wa Mamvi na mahasimu wake ulipoanza baada ya kuwazika kwenye deal hii, wakiwemo makada maarufu wa CCM.
mamvi akiwa waziri wa maji na Maendeleo ya Mifugo aliwahi hata kushtakiwa kwa Mkapa kutokana na kiu yake ya kushikiza mshiko na kupiga madili, huku kijana wa Kiiran, akiwa kamanda mpanga mipango. Halafu leo eti Siyo fisadi aliwajibika kisiasa.