Uchaguzi 2020 Mkutano wa Kampeni wa Dkt. Magufuli - Babati

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Mgombea urais kwa tiketi CCM, Dkt. Magufuli yuko mkoani Manyara akiendelea na mkutano wa kampeni

Alipokuwa Minjingu akielekea Babati amekataa kuingilia Uhuru wa mahakama baada ya mama mmoja aliyedai kudhurumiwa mali zake ambaye uamuzi ulitolewa mahakamani kuomba kusaidiwa, aidha amemshauri aende kukata rufaa ili kupta haki yake

Magufuli ameahidi kuifanya kata ya Magugu, Babati Vijijini kuwa Mamlaka ya Mji Mdogo

RAIS MAGUFULI AAMRISHA WANANCHI 4000 WALIOLIPIA UMEME WAUNGANISHIWE UMEME BABATI
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Manyara, Reheme Mashinji amesema wateja 4,000 wa Umeme Mkoa wa Manyara walishindwa kuunganishiwa Umeme kutokana na changamoto ya Fedha waliyonayo TANESCO mkoani hapo

Rais Magufuli akiwa kwenye mkutano wa kampeni kama Mgombea wa Urais kwa awamu ya pili amempigia simu Waziri wa Nishati na Madini kujua shida na amempa mwezi mmoja kwa wateja hao waliolipa kuunganishiwa umeme

Wateja hao waliolipia walishindwa kuunganishiwa umeme kwa kuwa pia wanaihitaji nguzo za kuweza kufikishiwa umeme katika maeneo yao wanayotaka nishati ya umeme
 
Uchaguzi huu CCM inakwenda kushinda kwa kishindo kwakua upinzani nidhaifu kuliko wakati wowote tangu kuanzishwa kwa vyama vingi.
 
Mgombea urais kwa tiketi CCM, Dkt. Magufuli yuko mkoani Manyara akiendelea na mkutano wa kampeni

Alipokuwa Minjingu akielekea Babati amekataa kuingilia Uhuru wa mahakama baada ya mama mmoja aliyedai kudhurumiwa mali zake ambaye uamuzi ulitolewa mahakamani kuomba kusaidiwa, aidha amemshauri aende kukata rufaa ili kupta haki yake
Huu ulikua mtego, Magu kaushtukia
 
SABABU 31 ZA KUMKATAA MAGUFULI 28 OKTOBA 2020:

1. Hajatoa ajira miaka 5
2. Hajaongeza mishahara kwa miaka 5
3. Ameongeza makato HESLB toka 8% to 15%
4. Amefukuza wafanyakazi na hajawapa hata senti tano kisa vyeti feki
5. Kaondoa fao la kujitoa NSSF
6. Kaondoa wanunuzi binafsi wa kahawa waliokuwa wanatoa bei nzuri
7. Karudisha gharama za matibabu kwa watoto na wajawazito
8. Anatoza maiti kodi kuzitoa mochwari
9. Kavunja katiba ya nchi kuzuia wapinzani kufanya mikutano halali ya siasa
10. Katunga sheria kandamizi kukomoa watu
11. Kabambikia kesi watu kwa visasi na chuki
12. Kafilisi wafanyabiashara kwa chuki binafsi
13. Kathibiti mashirika ya kutetea haki za binadamu
14. Kadhibiti na kutisha vyombo vya habari na kuviamrisha vimtangaze yeye tu na chama chake
15. Kavuruga sana mahusiano ya kimataifa
16. Kavuruga demokrasia na anataka wananchi waishi kama mifugo yake kufuata analotaka
17. Kazima bunge live na kulitumia bunge kama muhuri kufanya mambo yake
18. Mahakama imebinywa na imekuwa siyo huru tena
19. Kawadhibiti viongozi wa dini wanaomkosoa na kumwambia ukweli
20. Kanunua ndege bila kufuata sheria ya PPRA
21. Watu wengi wameuwawa na kupotea na kutekwa
22.Amelea na kulinda kikosi kazi cha "watu wasiojulikana"
23. Amepandikiza hofu,ukatili na dhuluma kama nyenzoza siasa mpya za Tanzania na utu umetoweka
24. Kakivuruga chama chake na kukimega vipande vipande
25. Kajenga uwanja wa ndege kwao bila ya approval ya bunge wala cabinet
26. Alisema tutaishi kama MASHETANI.. Kwa madai kuwa tulikuwa tunaishi kama Malaika. Hakika amelitimiza hilo.
27. Kuwa na kundi la watu wasiojulikana awamu hii ya tano na polisi hawajawai

28. Ni mwongo kupindukia – mwaka 2015 wakati anaomba kura aliongopa mengi km kumpa kila mwalimu kompyuta, kukipa kila Kijiji milioni 50 nk. Leo hii tunaingia uchaguzi mwingine, hajatimiza hayo na anaahidi mapya bila aibu.

29. Kudhalilisha akina mama kwenye majukwaa yake ya kisiasa

30. Kula rambirambi za wahanga wa majanga. Rais anayekula rambirambi zilizotolewa na watu mbalimbali ikiwemo nchi rafiki hatufai Watanzania.

31. Kuwakana Watanzania waliopata majanga km Wanakagera wakati wa tetemeko la ardhi.

Uchaguzi huu CCM inakwenda kushinda kwa kishindo kwakua upinzani nidhaifu kuliko wakati wowote tangu kuanzishwa kwa vyama vingi.
Kwa nilicho kishuhudia leo kwenye seminar ya wasimamizi wa vituo vya uchaguzi ni dhahiri CCM wanashirikiana na TISS kuiba kura
DSO/RSO wanasema
1.Marufuku mawakala kuingia na simu
2.Marufuku wasimamizi wasaidizi kuingia na simu
3.Marufuku kalani mwongozaji kuingia na simu
4.Marufuku wakala kuingia na kalam yake
5.Marufuku wakala kuondoka na karatasi ya matokeo

Wapinzani tumeshapigwa tayari!Yaani nimekuta kwanini niliumia kwenye hiyo seminar Ilikuwa kidogo tu nirushe ngumu!
 
Mgombea urais kwa tiketi CCM, Dkt. Magufuli yuko mkoani Manyara akiendelea na mkutano wa kampeni

Alipokuwa Minjingu akielekea Babati amekataa kuingilia Uhuru wa mahakama baada ya mama mmoja aliyedai kudhurumiwa mali zake ambaye uamuzi ulitolewa mahakamani kuomba kusaidiwa, aidha amemshauri aende kukata rufaa ili kupta haki yake
 
Attachments

  • 255756432130_status_efe3222840ad4ee4b3d6184eedea5e7e.mp4
    3.9 MB
Back
Top Bottom