Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,989
“Tunafahamu kuwa ukuaji wa uchumi ni mkubwa kwa watu wetu lakini vyanzo vyetu vya umeme bado ni vilevile, lazima tuongeze vyanzo vingine ili kuwa na umeme wa uhakika kwa ajili ya shughuli za kiuchumi.
“Kuna ripoti imetoka ikionesha Tanzania ni moja ya Nchi ambazo zinakua vizuri kiuchumi Afrika maana yake mahitaji ya umeme yataendelea kuwepo.
“Niwatoe wasiwasi Watanzania kuwa Rais na wasaidizi wake tunafanya kila tunaloweza upatikanaji wa umeme unakuwepo na hiki ni kipindi cha mpito wakati Bwawa la Mwalimu Nyerere linakamilika.”
=============
Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati, Dkt. Dotto Biteko amewaagiza Watendaji Wakuu wa Nishati akiwemo Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, Maharage Chande kutohudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Nishati unaoendelea Jijini Dar es salaam leo na badala yake waende kutatua tatizo la upatikanaji wa umeme ambao kwa sasa unasumbua Wananchi.
Akiongea mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Biteko amesema Wananchi wanachotaka kwa sasa ni upatikanaji wa umeme wa uhakika na kumaliza mgao ambao unaendelea hivyo amewataka waende kusimamia kuhakikisha umeme unarudi katika hali nzuri kama zamani.