Dr.slaa amefika hapa Kahama saa 11na nusu,na amepokelewa na bodaboda 5 ambazo walichangiwa sh.5000 kutoka kwa viongozi kadhaa walioambatana na Dr.slaa,hapo awali Vijana wa chadema walionekana wakizunguka maeneo ya kahama stendi kuomba madreva Bodaboda wahudhurie mapokezi ya Dr.slaa lakini hali haikuwa nzuri kwani asilimia 90 ya madreva waligoma kuifanya hivyo.Wakati akielekea eneo la Mkutano Dr.slaa alipokelewa na mabango yanayosema"CHADEMA BILA ZITTO HAIWEZEKANI,TUACHIENI CHAMA CHETU,ENDELEENI NA UBAGUZI WENU",Baada ya kupanda jukwaani Slaa alipokelewa na Mawe,na matusi ya kejeli sana kutoka kwa Wananchi wachache waliokuwepo eneo la Mkutano.
Dr.slaa aliomba Vijana wake wa usalama watulize ghasia za wananchi,kisha akazungumza maneno machache tu kwa kusema Naomba maswala ya Zitto mtuachie sisi tutayamaliza,Mkutano nauahirisha hadi Jumapili jioni hapahapa Kahama.Kwahiyo Mkutano Kahama hadi Jumapili.