Mkutano wa Dkt. Slaa mjini Kahama - Dec 4, 2013

Mkutano wa Dkt. Slaa mjini Kahama - Dec 4, 2013

CHADEMA

Political Party
Joined
Apr 13, 2013
Posts
495
Reaction score
2,540

Huu ndiyo mkutano wa Dkt. Slaa leo Kahama mjini ambao umeanza majira ya saa 12.15 jioni ambapo watu wamekuwepo uwanjani tangu saa 8 mchana kama walivyotangaziwa.


attachment.php



attachment.php

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilibrod Slaa akiwahutubia wanachi wa mji wa Kamaha na vitongoji vyake, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kukagua na kuimarisja uhai wa chama katika mikoa ya Shinyanga, Kigoma, Tabora na Singida, uliofanyika kwenye Uwanja wa CDT mjini Kahama jana. (Picha na Joseph Senga)

attachment.php

Katibu Kuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (chadema), Dk. Willibrod Slaa akiagana na wananchi wa mji wa Kahama baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa CDT mjini huo jana, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kuimarisha uhai wa chama katika mikoa ya Shinyanga, Tabora, Kigoma na Singida. (Picha na Joseph Senga)

Dkt. Slaa "Watanzania tulieni, tulieni, tulieni. Wingi wenu hapa na kunisubiri kwa muda mrefu namna hii tangu mchana kwenye jua kali ni ishara kubwa ya upendo wa dhati kwa chama chenu na viongozi wenu, asanteni sana sana sana Kahama.

"Chama hiki ni chenu, kipo kwa ajili ya kuwatumikia na kusimamia maslahi na matakwa yenu. Hakiwezi kuwa chama legelege. Ni lazima ili kiweze kuwasemea watu, kwanza muhimu kiweze kusimamia misingi yake, ikiwemo katiba, kanuni, maadili na itifaki, mambo ambao hata CCM hawana pamoja na ukongwe wao.'

"Wakati wa kampeni 2010 tuliwaambia tutasimama kidete kwa ajili yenu kuwavusha kutoka hapa kwenda nchi ya matumaini. Ni lazima mtuone hivyo bila chembe ya shaka kuwa chama chenu ni imara, kinaweza kusimamia misingi yake ambayo ni pamoja na katiba yake, kisha tutakuwa na ubavu wa kupigania maslahi yenu."

"Haya mambo tunayopitia sasa wapo wanofikiri yatatukwamisha, tunawaambia ndiyo kwanza yanatukomaza na kutuimarisha kuwa chama imara kwenda kushika dola," Dkt. Slaa leo mjini Kahama.
 

Attachments

  • Slaa kuhutubia Kahama 2..jpg
    Slaa kuhutubia Kahama 2..jpg
    383.7 KB · Views: 78,431
  • Slaa kuhutubia Kahama 1..jpg
    Slaa kuhutubia Kahama 1..jpg
    78.3 KB · Views: 65,616
  • Slaa kuagana na wananchi.jpg
    Slaa kuagana na wananchi.jpg
    56.2 KB · Views: 74,602
Nini kimechelewesha mkutano kuanza huoni ni kama kuwapotezea wananchi muda wa kuzalisha na kukuza uchumi
 
Naomba na hiyo picha uweke kwenye ule uzi wa mwanazito TUNTEMEKE
 
Last edited by a moderator:

Dkt. Slaa baada ya kuhutubia kwa takriban dakika 30, akiwaaga wananchi waliokuwa na shauku ya kumsikiliza wakiwa wamemsubiri zaidi ya masaa 4.

Pamoja na kuwa na kiu ya kuendelea kumsikiliza, wakipaza sauti 'endelea endeleea, endelea' wananchi walisikiliza kauli ya Dkt. Slaa pale alipowaambia kuwa anapaswa kuwahi kikao cha ndani hivyo akawaahidi kuwa atapanga mkutano mwingine ili kufidia masaa 'yaliyopotea' leo, ikiwa ni ishara ya heshima yake kwa wananchi hao kumsbiri uwanjani kwa muda mrefu kiasi hicho.




 

Attachments

  • Slaa kuagana na wananchi.jpg
    Slaa kuagana na wananchi.jpg
    290.3 KB · Views: 1,149
Back
Top Bottom