Mkutano Maalum wa Vyama vya Siasa, Septemba 13, 2023

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Hussein Mwinyi anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Siku ya Mwisho ya Mkutano Maalum wa wa Siku 3 wa Vyama vya Siasa na Wadau ambapo wamejadili Utekelezaji wa Mapendekezo ya Kikosi Kazi, Hali ya Demokrasia na Siasa kwa ujumla Nchini

Katika Siku hii Wajumbe watajadili umuhimu wa Maridhiano, Ustahilimilivu, Mageuzi na Ujenzi mpya wa Taifa katika Shughuli za Kisiasa Nchini

Fuatilia yanayojiri kwenye Siku ya tatu ya Mkutano Maalumu wa vyama vya Siasa, leo Septemba 13, 2023.


View: https://www.youtube.com/watch?v=vbzm-kNn4Ag

DEUS KIBAMBA, MHADHIRI – CHUO CHA DIPLOMASIA

Yupo msomi mmoja nguli wa masuala ya ujenzi wa Katib anasema hoja hii:

Masuala ya Siasa za Uchaguzi huongozwa na mashindano. Ushindani. Mnashindana. Maana mmoja aliye kwenye kiti anashindana na aliye nje ya kiti ili kama wapiga kura watataka, basi yule aliye nje ya kiti aingie na yule aliye kwenye kiti atoke. Hizo ni siasa za uchaguzi.

Msomi huyu nguli anasema, tofauti na siasa za uchaguzi. Siasa za katiba siyo siasa za mashindano. Sijui kama naeleweka tofauti yake hapa. Katiba ni siasa. Mchakato wa katiba pia ni siasa, lakini siyo za mashindano. Ni siasa za maridhiano. Toa hoja yako, jenga hoja mpaka tukuelewe. Lazima ushawishi wengine. Hizo ni siasa za katiba.

Kutokana na maneno ya msomi huyo nguli, kwa nilichokiona kwenye mkutano huu, kulikuwa na mchanganyiko wa vitu hivyo viwili. Muda mwingi tumejadili siasa zinazoenda kwenye mrengo wa uchaguzi.

Ili kupata katiba mpya tunahitaji kuridhiana…

Ukiweka siasa za katiba zikawa ni siasa za mashindano, ambacho ndicho nilichokiona kwa muda mrefu kwenye nchi yetu, hatutapata katiba mpya. Hatutapata kabisa katiba mpya. Maana Katiba Mpya ni suala la ujenzi wa Tanzania mpya.

Hatuwezi kusema tuende mbele bila kusema tulikwama vipi. Uchambuzi wangu unaonesha mchakato wa katiba uliposita 2014, ulisita kwa sababu tatu.

Sababu ya kwanza ilikuwa ni kushindwa kama Watanzania kufikiria kwamba mchakato wa katiba mpya unapoendelea, ungeweza kukumbwa na kashikashi. Hatukufikiria hivi mchakato wa katiba ukikumbwa na mawimbi, tutafanyaje? Mimi kwa maoni yangu hatukufikiria. Ndiyo maana katika sharia ya mabadiliko ya katiba tulisahau, katika hali isiyo ya kawaida kabisa, kuweka vifungu – angalau kimoja, viwili – vinavyoeleza utaratibu utakaotumika kutengeneza maridhiano au kutatua migogoro na mipishano itakayojitokeza wakati wa kuandika katiba mpya.

Ndiyo maana kwa kitendo kidogo tu ndani ya Bunge Maalum la Katiba, kusema “NduguMwenyekiti unayeongoza mjadala, unatuburuza kuhusu utaratibu, hautuendeshi vizuri” Jambo hili lilifanya kundi zima lenye mchango mkubwa kabisa kwenye Bunge Maalum likatoka nje; halikuitwa likarejea; hakuna aliyeliita wazungumze. Na katika sayansi ya siasa, mbinu ile inaweza kusaidia kutingisha kidogo ukitaraji uaitwa mukaongee. Ikitokea hujaitwa mkaongee, inakuwa balaa.

Napendekeza kuwa, hatua ya kwanza ni kupeleka Bngeni Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Katika Muswada huo, yatakuwemo mambo mengi lakini mawili tu yasikosekane. La kwanza, ni vifungu vinavyosema tukigombana kama Watanzania, kuanzia sasa mpaka tunakamilisha na kupata katiba mpya, tutafanyaje.

La pili ni hadidu za rejea za vyombo vyote vitakavyoundwa katika kukamilisha mchakato huu wa katiba.

DKT. BARUANI MSHALE, TWAWEZA
Maridhiano ni muhimu sana na maridhiano yanaleta uponyaji, lakini lazima tujiulize tunaponya nini, nan ani wanaohusika katika huo uponyaji. Nani alifanyiwa nini hadi kustahili huo uponyaji ili aweze kupata ahueni aweze kuchangia katika mustakabali wa taifa letu.

Historia yetu lazima tuiseme kwa ukamilifu wake. Na swali la kujiuliza hapa ni: Je, historia yetu jinsi ambavyo tumekuwa tukiifunza na kuambizana imekuwa ni style ya funika kombe mwanaharamu apite au imekuwa ni historia kwa maana kwama tunajifunza na ile methali inayosema “mficha maradhi kifo kitamuumbua”. Kwahiyo hilo ni suala ambalo lazima tujiulize.

Ustahimilivu ni muhimu sana kwa sasa na huko tuendako. Kuwa na ustahimilivu katika dunia ambayo ina mabadiliko mengi ni muhimu sana. Tumeona kwenye nchi kadhaa jinsi kumekuwa na mapinduzi hivi karibuni na wananchi wanashangilia na kuunga mkono yale mapinduzi. Yale ni wananchi wanaonesha hawana Imani na demokrasia. Kile kilichokuwa kinaitwa demokrasia hakikuwa kikiwaletea wao maendeleo na kuwafaidisha wao, kwahiyo yale yaliyotokea wanayaunga mkono.

Siasa ina jukumu muhimu sana katika kututengenezea utaratibu wa namna tutakaa na kujadiliana kutengeneza mustakabali wetu wa baadae. Lakini je, siasa zetu zikoje? Siasa zetu zinazingatia ustahimilivu?

Tafiti zinaonesha wananchi wengi duniani wanapoteza Imani na taasisi na mamlaka zilizopo… kama wanapoteza Imani na hizo taasisi, ni mbinu gani mbadala tunazoweza kutumia kuweza kuwashirikisha wananchi hasa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu, ambao Imani yao katika taasisi zetu inaenda ikipungua.

Kinachotuongoza sasa ni tunu yetu ya Utu, au ni tunu yetu ya Uchawa? Uchawa, kwa mtazamo wangu, sasa imekuwa kama ni tunu. Tujiulize, tumetoka kwenye utu kwenda kwenye Uchawa na itatupeleka wapi.

STELLA IKUPA, MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA DAR ES SALAAM
Kwakuwa masuala ya wenye ulemavu hayazungumzwi mara kwa mara, mimi nitajikita kujazia nyama kwenye eneo hili la watu wenye ulemavu.

Kwanza kabisa niombe kwenye Baraza la Vyama vya Siasa kuwe na uwakilishi wa mtu mwenye ulemavu… kama hakutakuwa na mtu wa kuyasimamia na kuongeza nyama kila inapoitwa leo, nadhani tunaweza kufika mahali pa kufeli.

Lakini pia ninaomba kwa upande wa watu wenye ulemavu, wasiishie tu kushirikishwa kwenye shughuli za chama husika, ila wapewe nafasi za maamuzi ndani ya chama husika…

Napendekeza pia wajengewe uwezo wa kugombea ubunge, uwakilishi pamoja na udiwani. Wajengewe uwezo wa kugombea nafasi ndani ya chama na wawekewe mazingira ya kueza kupata nafasi hizo.

Kuwe na mwongozo ndani ya vyama vya siasa. Kwa mfano kuna uchaguzi umefanyika ndani ya chama cha siasa, watu wenye ulemavu wawe ni asilimia ngapi. Labda kuna uchaguzi wa wenyeviti, uchaguzi wa makatibu. Lakini kunazile nafasi za wenyeviti na makatibu kwenye mikoa, kanda na maeneo mbalimbali. Watu wenye ulemavu wawe ni asilimia ngapi. Isiishie tu kuwa ni utashi wa chama kiamue kumpa au kutokumpa, iwe ni mwongozo kwamba ni asilimia ngapi iwe ni watu wenye ulemavu.

ISMAIL JUSSA, ACT-WAZALENDO
Serikali ifanye kazi ya ziada kurejesha Imani ya wahusika na washiriki mbalimbali wa shughuli hizi, hasa za kisiasa, kwasababu kilichotokea huko nyuma, kwa mfano katika uchaguzi wa 2020. Lakini kwa Z’bar turui nyuma 2015, kumeacha athari nyingi sana katika jamii.

Nadhani kuna haja ya kurudisha credibility na legitimacy. Nadhani hilo ni jukumu kubwa letu sote lakini zaidi, la serikali.

Njia ya kujenga legitimacy pale ambapo pana deficit ya legitimacy na kujenga credibility pale ambapo pana deficit ya credibility, ni mamo mawili yatatusaidia. La kwanza, ni ushirikishwaji wa wahusika mbalimbali katika michakato hii tunayoiendea. Yakifanyika mambo watu wakatafsiri kuna ujanja ujanja, kuna ulaghai na ubabaishaji, yanapunguza credibility.

La pili, kuna kazi ya kuweka ratiba. Tukishirikisha wat una tukaweka ratiba iliyo wazi, wale wenye wasiwasi tutawaondoshea wasiwasi wakijua lipi litafanywa lini na muhusika ni nani, na wanashirikishwa vipi wengine. Nadhani hiyo itaondosha kabisa yale ambayo yanazungumzwa.

MZEE JOHN CHEYO
Watanzania tuna tatizo moja kubwa; la kutoambiana ukweli na la kusifiana. This is a problem. Kikao hiki tusipokitengeneza vizuri, tunaondoka hapa tuna tofauti kati ya msimamo wa serikali na msimamo wa walio wengi humu…

Serikali imezungumza juu ya elimu, hakuna anayekataa elimu. Kitu kiachowatia watu wasiwasi ni darasa la watu milioni 61, la miaka mitatu. That is the problem! Inaonesha wazi ni kama vile serikali inatafuta njia ya kukwepa huu mchakato wa kikatiba kwa ujanja ujanja. Hii ni hatari.

Sisi wazee tusipolisema, tunadanganya! Mimi nashauri kikao hiki ni cha baraza la wadau. Kamati ya uongozi ya baraza ingekaa, ichukue kamati ndogo iende ikamuone Mh. Rais ili tupunguze ule muda. Elimu ni continuous; leo mimi hapa nimekaa siku tat una uzee wangu nimejifunza mambo mengi sana…

Watanzania tusiwa-underrate; Watanzania wamefundishwa. Mzee Warioba ametembea nchi nzima. Amefundisha. Jaji Kisanga ametembea nchi nzima. Amefundisha. Kikosi Kazi na chenyewe kimetuita, tumeandika. Tunaelewa tunachozungumza. Bunge la Katiba limekaa karibu miezi sita live, tunaeleweshana.

Kwa mambo madogo Hata Mwanasheria Mkuu hana kazi; ni kwenda tu kwenye katiba inayopendekezwa, unanyofoa ile page ya mambo yoteunayapeleka bungeni. Na jambo hili lilishaamuliwa tayari na Rais wa Awamu ya Nne.

Mimi nasema kazi iliyofanywa tayari kwenye issue ya katiba, tuitumie. Na haikuja bure. Tumetumia mapesa kibao. Mimi nilikuwa mbunge wa Bunge la Katiba; tumekula hela nyingi. Leo tunazitupa ndani ya dustbin! Na Rais aliyepo alikuwa Makamu Mwenyekiti na tulipiga kura pamoja.

Wengine tunasema sasa usianze mkutano wa Katiba nzima kwasababu utakwama. CCM hata ufanye nini huwezi kuwaondoa kwenye serikali mbili kwa sasa.

Tukubaliane, kamati ndogo iende ikazungumze na Rais tupunguze hiyo miaka mitatu ya kupata “degrii” ya Katiba, ili tuanze yale yanayowezekana yafanyike mara moja.

La mwisho, wanaotengeneza hizo sharia wazilete kisheria hapa kwenye kikao kama hiki kwasababu sisi ndiyo wenye ajenda. Ukipeleka kule yatakayotokea mtashangaa mwishoni mmepata kitu cha namna gani.

Wekeza katika amani kwasababu bila amani hakuna chochote.

MZEE STEPHEN WASSIRA
Kilichotokea ni kutoaminiana. Tulikuwa hatuaminiani sana. Tukitaka kwenda mbele lazima tujenge suala la kuaminiana. Sisi ni Watanzania; tofauti za vyama hazitufanyi tuwe Watanzania nusu au robo tatu. Kama ni maslahi ya taifa, tuzungumze maslahi ya taifa.

Tunapokwenda tuwe wastahimilivu kwasababu hakuna namna utafanya maamuzi bila kusikiliza maoni ya wengi na wachache kukubali wngi wanasemaje. Democracy ni ya wengi na wachache wanasikilizwa.

Kama taifa lazima tuwe na kitu tunaita Tunu za Taifa – tuziheshimu. Moja ya tunu zetu ni Umoja. Nyingine ni Uhuru, na tuliutafuta kwa tabu na ulipokosekana Z’bar wakapigana ili kuupata.

Mimi nina mashaka kidogo na siasa zetu za sasa kwasababu hata katika ethics, hatujaweka mambo yanayozuia watu kusema uongo. Hivi kusema uongo ni siasa au siasa ni kusema uongo? Mimi nadhani siasa ni mfumo wa Maisha. Sasa huwezi kuwa na mfumo wa Maisha ambao msingi wake ni uongo. Nchi itakuwa ya uongo tu.

Katika kutazama hizi siasa zetu na katika kutunza tunu za taifa, basi tuhakikishe ya kwamba kweli tunapingana kwa hoja.

PROF. IBRAHIM LIPUMBA
Katika mkutano wetu wa kujadili hali ya demokrasia nchini kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025, ambao ulishirikisha vyama vya TCD na vyama vyote vyenye usajili kamili na wadau wengine wa demokrasia. Katika mjadala huo, tulifikia makubaliano kuwa mchakato wa kupata Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi, ukwamuliwe na hatimaye tupate katiba yenye misingi imara ya demokrasia.

Zile ripoti za Tume ya Jaji Warioba, ambazo zilikuwa ni zaidi ya kumi nadhani, hivi sasa ni vigumu kweli kuzipata katika tovuti. Ni vyema tunavyoelekea katika masuala haya, taarifa hizi ziweze kupatikana kwa urahisi kwasababu zina mafunzo mengi na zinaeleza wazi kwamba baada ya kuifanya kazi Tume ya aji Warioba ikabaini kwamba kumbe Watanzania wanajua ni mambo gani wanataka yawemo ndani ya Katiba.

Lakini kwenye mkutano ule tukabaini kwamba kwakweli tutakuwa tunajidanganya tukidhani kwamba tunaweza kupata katiba mpya kabla yay a Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025. Na hili lilisisitizwa sana na Mzee Cheyo kwamba turejee kwenye mapendekezo yaliyotolewa na kukubaliwa na Rais Kikwete mwaka 2014 kwasababu chaguzi lazima zifanyike, basi tuweze kufanya mabadiliko madogo ya Katiba ili Uchaguzi unaokuja uweze kusimamiwa na Tume Huru ya Uchaguzi.

Lakini pia, paweze kuwa na ushiriki mpana. Kwamba mtu asiyekuwa na chama lakini anahitaji kuwa Mwenyekiti wa Kijiji ashughulikie matatizo ya Kijiji chake na haitaji kuingia kwenye taratibu za vyama vya siasa, huyu jamaa asizuiwe kuwa kiongozi katika Kijiji chake.

HEMED SULEIMAN ABDULLA, MAKAMU WA PILI WA RAIS Z’BAR
Nitoe pongezi nyingi sana kwa Baraza la Vyama vya Siasa kwa kazi kubwa sana ambayo wanaendelea kuifanya. Kwa hakika, jambo hili ni kubwa na linapaswa kupigiwa mfano. Juhudi hizi zinapaswa kulenga maendeleo ya Watanzania chini ya msingi wa amani na utulivu wa nchi yetu.

…ni Imani yangu sote tutaweka mbele maslahi ya Tanzania na tutaacha maslahi binafsi na tutaacha yale yote ambayo hayatalijenga taifa hili, na tutasimamia msingi wetu wa umoja, mshikamano na utulivu ambao msingi mkubwa ni usimamizi wa amani yetu tuliyonayo ndani ya Tanzania.
 
Kukosekana kwa wadau muhimu na makini katika mkutano huu, basi hauonekani tena kuwa wenye maana wala kuvutia tena.
 
Kuna mzalendo mmoja kanitonya kwamba na wale waliosusia nao wako chimbo wanaufuatilia mkutano ila chimbo hilo wanamulaumu sana ayatollah mbowe kwa kuwazuia wasihudhurie.
 
Askofu Dr Bagonza PhD amepongeza hatua ya Serikali kupeleka bungeni muswada wa mabadiliko ya sheria za Uchaguzi

" Tukisema tutafanya Chaguzi za Serikali za Mitaa na Uchaguzi mkuu kwa sheria zilizopo Tunajidanganya Bure sisi Wenyewe" amesisitiza baba askofu

Mungu ni mwema!
 
Mbali na sheria kuwa mbaya,lakini kwa sheria hizihizi akipatikana kiongozi mtenda haki,watu wanatoboa,isipokuwa sheria zinatakiwa zibadilishwe kwa ajili ya kuwadhibiti viongozi ambao kwao haki ni kama ardhi na mbingu.
 
Back
Top Bottom