Uchaguzi 2020 Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC: Watanzania hawataki mtu atakayeuza madini yao kwa wageni nje

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,016
9,885
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC, amesema watanzania wanataka Afya iliyoimarika, barabara nzuri, miradi ya umeme, elimu bora hawataki blah! Blah!

Amesema watanzania hawataki viongozi watakaochukua madini yao na kwenda kuyauza kwa wageni nje, watanzania wanataka viongozi watakaotetea madini yao

Ameyasema hayo alipokuwa anazungumza kumuandikia barua Tundu Lissu ili kutoa maelezo dhidi ya tuhuma za uongo anazotuhumiwa kuzitoa

Amesema Tundu Lissu amekuwa akitangaza matusi, tuhuma na kudanganya wafanyakazi badala ya kutangaza sera


==
YALIYOZUNGUMZWA KWENYE VIDEO YA MKURUGENZI WA UCHAGUZI NEC

Kwa mamlaka ya kisheria Tume iliyonayo, tayari imemuandikia Barua Mh. Tundu Lissu ya kumuita katika Kamati ya Maadili ya Kitaifa ili aje kutoa maelezo na ushahidi wa kile alichokisema katika mkutano wake huko Musoma.

Kwa mara nyengine tena Tume inawasihi Wagombea wa Vyama vyote kufuata sheria, kanuni na taratibu za nchi ili kulinda amani ya nchi yetu, katika kipindi cha kampeni kilichobaki kwa kujali muda wa kampeni, ratiba za kampeni na kuepuka matusi, sababu unatumia muda mwingi kutangaza matusi badala ya kutangaza sera, unatumia muda mwingi kutangaza tuhuma badala ya kutangaza sera, unatumia muda mwingi kuwadanganya Watanzania na wafanyakazi badala ya kutangaza sera.

Watanzania sasa hivi wanataka Afya iliyoimarika, Watanzania sasa hivi wanataka barabara nzuri, Watanzania sasa hivi wanataka miradi ya umeme, Watanzania sasa hivi wanataka elimu bora, Watanzania hawataki bra bra. Watanzania sasa hivi wanataka viongozi ambao watalinda madini yao, sio viongozi watakaokuja kuchukua madini yao na kupeleka kwa wageni nje.
 
Huyu mkurugenzi mkuu wa NEC anaitisha vyombo vya habari na kusema eti watanzania wanataka mtu atakayelinda madini yao, atakayewajengea vituo vya afya, atakayewajengea mabarabara, atakayewaletea umeme. Kwani haya yanaihusu NEC?

Mkurugenzi wa NEC anaposema kuwa watanzania hawataki mtu atakayetorosha madini nje, kwani inaihusu nini NEC?

Kweli nimeamini hawa NEC siyo wa kuwachekea hata kidogo. Hata hii engua ya wagombea wa upinzani inafanywa kimkakati na inaonekana wazi wazi.

Magufuli amevuruga mifumo mingi huru ya maamuzi. Hii nchi inakoelekea siko hata kidogo.

 
Hayo anayoyaongea ndiyo kazi ya Tume? Mbona anaiweka Tume kwenye nafasi ya hatari sana? Yaani Tume inawalazimisha wagombea kitu cha kuongea? Watanzania wanajua wanachotaka kusikia na kila Chama kina ya kwake ya kujinadi kwa wananchi na Wananchi ndiyo wataamua.

Kwani madini yetu huwa yanauzwa wapi? Tume inahusika vipi na utekelezwaji wa Ilani za vyama? Mbona haijaongea kitu kuhusu aliyejisifu kuwanyima wananchi maendeleo kwa kutomchagua na kuahidi kuendelea kuwanyima kama hawatomchagua?

Mpaka hapo Tume imeshapoteza uhalali wake wa kusimamia uchaguzi huu na naiona kwamba kuwa ndiyo chanzo cha vurugu nchini.
 
Huyu mkurugenzi mkuu wa NEC anaitisha vyombo vya habari na kusema eti watanzania wanataka mtu atakayelinda madini yao, atakayewajengea vituo vya afya, atakayewajengea mabarabara, atakayewaletea umeme. Kwani haya yanaihusu NEC?...
Mungu wangu sio kwa kujisahau huku ...hii evidence mambo yakienda vibaya itamuweka pabaya mno...
Bila kutaraji kajionesha rangi zake halisi
 
Yaani mkurugenzi mzima wa NEC haoni hata aibu kuonesha mahaba kwa CCM na hapo hapo kuonesha chuki zake dhidi ya Lissu.

Tume ya uchaguzi haina mamlaka wala wajibu wa kuwapangia wagombea watoa sera gani au kutusemea sisi watanzania tunataka nini kutokea kwa wagombea. Waache wagombea waseme yao na watuache sisi wananchi tuwasilikize, mwisho tutaamua. Pilipili iko shambani yawawashia nini?
 
Huyu mkurugenzi mkuu wa NEC anaitisha vyombo vya habari na kusema eti watanzania wanataka mtu atakayelinda madini yao, atakayewajengea vituo vya afya, atakayewajengea mabarabara, atakayewaletea umeme. Kwani haya yanaihusu NEC?...
Tume inaonesha upande iliyopo wazi wazi, haya ndio madhara ya Tume ya Uchaguzi KUWEKWA MFUKONI na Rais wa CCM. Inasikitisha sana kuwa na mfumo wa KIHUNI namna hii.
 
Tunaposema Lissu ni hatari ndio muelewe. Mkurugenzi wa uchaguzi kachanganyikiwa na kuanza kunadi sera kama kichaa. Sasa kama kibaraka hofu yake ni dhahiri namna hii ‘bosi’ wake ana hali gani?

Hii sio aibu, ni fedheha!
 
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC, amesema watanzania wanataka Afya iliyoimarika, barabara nzuri, miradi ya umeme, elimu bora hawataki blah! Blah!..
Kwani hayo madini hivi sasa yanachimbwa na kuchukuliwa na nani? kama sio haohao watu wa nje (makampuni ya kigeni).

Mwenyekiti wa NEC ameanza kampeni kuisaidia CCM na kumsaidia aliyemteua. Huyo mwenyekiti asipoangalia atakuwa chanzo cha kuvuruga amani nchini.
 
Back
Top Bottom