Mkuki Kwa Nguruwe (Kisa Cha Kweli)

Abdallahking

JF-Expert Member
Mar 19, 2018
1,989
2,000
SEHEMU YA 41


‘Docta ana mambo yake, ana shuku shuku zake..mimi sijamuelewa, najua ni kwanini,…muhimu kwangu, wewe uifanye hiyo kazi niliyokupa…sasa.., wewe ondoka ukaianze hiyo kazi mara moja, mengine niache mimi na docta tutayamaliza…’

Tuendelee na kisa chetu….

***************


Docta alikuwa anakuja, akiwa kashikilia simu yake mkononi, kama anaandika kitu kwenye simu yake, nahisi alikuwa akiongea na mtu fulani muhimu kwake…kuna muda alikuwa akiongea huku anageuka kidogo kutuangalia, ikanipa mashaka kuwa huyo anayeongea naye, anaweza akawa na jambo na sisi..lakini sikuwa na shaka na hilo.

Niliona kamaliza kuongea na sasa alikuwa akija pale tulipokaa mimi na rafiki yangu, lakini alikuwa hatuangalii, anaangalia simu yake,.. na alipotukaribia tu ,simu yake ikaita tena, ikabidi ageuka na kurudi pale alipokuwa awali, akaendelea kuongea na simu yake, na kwa muda huo rafiki yangu alikuwa kasimama hajui afanye nini,…

‘Sasa wewe unasubiria nini, nenda kaifanye hiyo kazi, ukimsubiria docta…akija hapa, ataanza kukudodosa, kwa maswali mengi ya ujanja ujanja…na lengo lake jingine anataka kumuona mtoto, nahisi kuna jambo analifahamu, anataka kulithibitisha,..au kuna jambo analifuatilia….’ nikasema hivyo.

‘Mhh,…ni kweli naondoka…ila mimi sijakuelewa hapo.., maana unachotaka ni kama mtu kuchunguza kivuli chako, ni mambo ambayo hata wewe mwenyewe unayafahamu,..’akasema

‘Nayafahamu kwa vipi, sijakuambia uchunguze mambo yetu, mimi ninachotaka ni wewe kuchunguza hili tukio la mume wangu, chanzo chake, na ni nini kipo nyuma ya haya yote, unajua…mimi sitaki mambo ya kusikia,..nataka ukweli, nataka uhakika,..sawa hisia hizo zipo, watu wanasema hili na lile, lakini mimi sio mtu wa kihivyo….nataka tuupate ukweli…’nikasema

‘Kwahiyo eeh, hili….’akasema na kabla hajamaliza, nikamkatiza kwa kusema;

‘Sitaki nikufundishe kazi…. siku zote nikikuelekeza kazi unasema nisikufundishe nimeshakupa kazi basi nikuachie wewe mwenyewe utajua jinsi gani ya kuifanya,…iweje leo, kulikoni, unajua naanza kukutilia mashaka,…’nikasema na yeye hapo akabakia kimia.

‘Katika jambo silitaki, ni kuwatilia mashaka watu wangu ninaowaamini…wewe nakuamini sana, nilikupeleka shule usomee ujasiri, ujua jinsi gani ya kujilinda, na uje kunisaidia na mimi, …unilinde kwa kila hali, unakumbuka, uliapa mbele yangu, ndio, urafiki upo pale pale, lakini mengine ni dhima, unanielewa hapo….’nikasema

‘Aaah,..ndio..naelewa…lakini kabla sijaifanya hii kazi, ni lazima tukubaliane…eeh, kuna utata hapa…’akasema

‘Kukubaliana husu malipo au, kama ni malipo hakuna shida, toka lini nikakupa kazi bila kukulipa, wewe angalia gharama zako nipatie ankara ya deni,…au unataka kusema nini…?’

‘Kwahiyo, mmh, unataka nimchunguze shemeji….mmmh….’akasema

‘Ndio…umchunguze, …kwa masilahi yake, na masilahi ya familia,….fanya ufanyalo, ila cha muhimu, nakuomba, na nasisitiza, mimi sitaki kashifa kwenye familia yangu, ..na hili tumeshaonywa na wazazi wangu mara nyingi, hata wewe uliwahi kusikia wakati baba akiongea, ..sasa kama kuna tatizo nataka tuliwahi mapema kabla halijafika kwa wazazi wangu,...’nikasema

‘Nikuulize tu, samahani bosi… kabla sijaondoka, sasa kama ni kweli mume wako kahusika na hicho unachokiita kashfa,..itakuwaje…?’ akauliza na mimi nikamuangalia kwa macho makali, nikasema

‘Ninacho-kiita mimi kashfa..una maana gani, lugha gani hiyo…..ok, sikiliza…mimi sitalivumilia kashfa yoyote kwenye familia yangu, hasa zile zenye kuharibu biashara, zenye kuharibu ndoa, zenye kuleta jina baya kwenye familia yangu, zote unazielewa..sitake nianza kuzitaja…’nikasema

‘Mhh…’akaguna hivyo.

‘Wazazi wangu unawafahamu walivyo, walinikataza nisioane na huyo mume wangu kisa ni kuhusu familia yao, kuwa eti imegubikwa na mambo hayo…mimi sikuamini hayo, najau tabia mtu anaijenga mwenyewe..mimi niliwahakikishia wazazi wangu kuwa kashfa mbaya hataiweza kutokea kwenye familia yangu…’nikasema

‘Lakini kashfa yaweza kutafsiriwa vingine,..kama jambo limefanyika kwa makubaliano linawezaje kuwa ni kashfa…muhimu tuliweke sawa,..kuna mambo labda yalifanyika hivyo, sasa labda imekuwa kinyume kutokana na kutokuelewana…sasa sizani ni kama ni kashfa, labda iwe ni kashafa kwa mtizamo wa watu wengine……’akasema

‘Kwa makubaliani!!! Weeeeh, makubaliano na nani..kuwa mimi nitendewe ubaya, kwa vipi sasa, kuwa mume wangu, mbona haiji akilini… kuwa yeye akazini nje ya ndoa au, tuchukulie kashfa hiyo ni ya ndoa, mimi sijui..yaani mimi, nikae na mume wangu kuwa akafanye hivyo,…au nimwambie mume wangu akaibe au..najua mume wangu hawezi kufanya hivyo, hata siku moja,..na mimi sio kichaa wa kukubaliana na ujinga kama huo, hata dunia itanicheka au unataka kusema nini…’nikasema.

‘Sawa…lakini nikuulize kitu kingine kutokana na hali ya shemeji, ukagundua kuwa kafanya hivyo, na hali kama hiyo, .. utachukua hatua gani, huoni unaweza kumuua mume wako bure....?’ akaniuliza na mimi nikageuka kumuangalia docta, alikuwa bado anaongea na simu, nikasema.

‘Kwanza tujue ukweli, unanielewa,, ....cha kufanya baada ya ukweli.. , nitajua mimi mwenyewe, hiyo sio kazi yako… ila kiukweli, kama ni kweli wanavyosema watu mimi bado siamini,…huyo aliyemghilibu mume wangu, huyo shetani mtu…kama kweli kaghilibiwa, maana mume wangu hakuwa na tabia hiyo,..huyo mtu, huyo shetani,,… nitahakikisha kuwa hanisahau maishani , na atajuta kuingilia ndoa za watu kupoje…’nikasema kwa ukali, na uso wangu ukiwa sasa umebadilika kabisa,….

Mdada aliniangalia usoni, akionyesha wasiwasi mkubwa, mpaka, akawa anarudi kinyume nyume..halafu akasimama ..rafiki yangu ni jasiri..alipitia mafunzo ya ujasiri, kwahiyo anajua aweje kwa wakati gani…, lakini kwa hali aliyoniona nayo usoni nahisi hakutarajia,…kabisa….

‘Ina maana utamuua au,…ha-ha- hata kama…?’ akaniuliza akionyesha wasiwasi, akasita kumalizia.

‘Wewe subiria tu…utaona nitakachokifanya, unajua nimevumilia sana, nimekuwa mtu wa watu, nawapenda sana watu wangu wa karibu, nawabeba kwa mbereko....sasa ina maana kwa hali hiyo watu wanipande hadi kichwani, hapana,..hata awe ni nani …’nikasema


‘Mhh, rafiki yangu siamini hili kabisa, lakini mume wako ni mtu mwema sana, na kama kafikia kulifanya lolote baya, atakuwa na sababu…sizani kama anaweza kufanya jambo ambalo analifahamu ni kinyume ..msamehe tu…’akasema

‘Nimsamehe nini sasa…kwanza, eeh, nisikilize, sio tukurupuke, kwanza, tujue kosa lake ni lipi,…ili tujue jinsii ya kumsaidia,…unajua yapo makosa ya kusamehe, mimi ni binadamu, nitayapima, …lakini sio kosa la kuingilia ndoa za watu…watu hao wanatakiwa kuuwawa…unasikia, ku-uwawa, sasa mimi niwachekee, ndoa sio kitu cha mchezo bibie…, ..’nikasema

‘Sikiliza…mimi naomba urejee yale mazungumzo yetu, mbona….’akasema

‘Mbona mbona nini…ile ni kitu kingine…najua unachotaka kukisema…ndio maana nilikusihi iwe siri…sasa kama na wewe umelikoroga huko, acha mwenye mali afanye kazi, yake utajua mwenyewe, na mimi natetea ndoa yangu…sasa nikuulize uUtaifanya hiyo kazi au huwezi nimpatie mtu mwingine..’nikasema kikazi zaidi.


‘Mimi naona sitaiweza hiyo kazi, ..na ukizingatia nina mtoto, si unajua tena….’akasema

‘Sikiliza, sitaki kusikia kauli hiyo…na nataka uifanye wewe….na nataka iwe siri kubwa, unanielewa, siri kubwa, sitaki watu wengine waje kuligundua hilo kabla yako, kuna watu wameshaanza kutaka kulifuatilia hilo tatizo la mume wangu, wanataka kujua kwanini mume wangu akawa hivyo,…hiyo ajali sio ya kawaida,…wameshaanza kutunga hadithi…najua wakitaka jambo watalipata tu…’nikasema

‘Akina nani hao…?’ akaniuliza akionyesha mashaka

‘Docta anataka na yeye kulichunguza kwa nia ya kumsaidia rafiki yake, najua sio hivyo tu,…najua kabisa… wazazi wangu watakuwa wamemtuma kufanya hivyo,…sasa sitaki aje kugundua kitu kabla ya yako, nataka wewe ukishagundua tunahakikisha hakijulikani kitu tena…unanisikia, umeona jinsi gani jambo hilo lilivyo nyeti,…umenielewa hapo…’nikasema

‘Mhh, mbona imekuwa ni tatizo, sikujua kuwa haya yote yanaweza kutokea,…sasa huyu docta anataka kutafuta nini,…ina maana ndio maana umeniita hapa, ili…na wazazi wako wanalifuatilia hili, mungu wangu …mimi sasa naanza kuogopa, naona nijiondokee tu kwenda kusoma haraka iwezekanavyo, ….’akasema sasa akirudi kinyume nyume

‘Sikiliza wewe ni rafiki yangu ninayekuamini, ndio maana kila kitu tunaambizana, na huwa tunashauriana kwa kila jambo, sawa si sawa....wewe ndio mimi, na wewe huwezi kufanya jambo la siri kinyume na makubaliano yetu, sizani kama wewe unaweza kunigeuka mimi…nimekuwa nikikulinda kwa kila hali, mpaka sasa.…’nikatulia

‘Ni kweli….’akasema sasa akiwa kainama chini kama mtoto mbele ya wazazi wake akiwa kakosa au kuona aibu. Ni lazima awe hivyo kwangu mimi licha ya urafiki lakini mimi nimekuwa kama mlezi, nilitumia gharama nyingi kumjenga huyu binti kutoka kwenye hali ya kukata tamaa hadi akafikia sehemu ya kujiamini..

***********

Rafiki yangu huyu, niliamua kumsaidia kutoka kwa wazazi wake, hii ni kutokana na ule ukaribu wetu, sikutaka nimsaidie kipesa tu, lakini pia kumjenga katika hali ambayo anaweza kufanya jambo lake kwa kujiamini.

Sisi kwenye familia yetu japokuwa tuna uwezo, lakini wazazi wetu walifanya juhudi kubwa ya kutujenga kihali ambayo mtu anaweza kufanya jambo bila kutegemea wazazi, walitujenga kujiajiri zaidi, pamoja na elimu yetu, na mimi nikaona nimsaidie rafiki yangu awe hivyo hivyo...

Wazazi wake kuna kipindi walitaka binti yao aolewe na mtu waliyeona kuwa atamfaa, na binti yao hakuwa tayari naye, kama alivyokuwa hayupo tayari kwa wanaume wengi waliomtaka kumuoa kabla ya huyo ambaye wazazi wake, waliamua kumshurutisha aolewe naye...ndio maana tatizo lake nikalichukulia sawa na la kwangu..kuwa hata mimi nilikataa kuolewa na chagua la wazazi wangu

‘Hawa wazazi wangu siwaelewi, kama wamenichoka, na huenda wanaona mimi ni mzigo kwao, waniambie, lakini sio kunitafutia mwanaume,....hivi wananionaje mimi, eti niolewe na yule mzee, ..eti kwa vile ni tajiri, ....hapana, siwezi kuishi na yule mzee, hata siku moja....’akaniambia.
 

Abdallahking

JF-Expert Member
Mar 19, 2018
1,989
2,000
SEHEMU YA 42


‘Lakini yule sio mzee,ukiangalai umri wako na yeye, huwezi kumuita yule mzee, yule ni saizi yako kabisa, au unataka kuolewa na dogodogo, usidanganyike, huko umeshakupita, sio kwako tena, huyo unayemuona ni mzee, ndiye saizi yako...’nikamshauri.

‘Simpendi, na simtaki....’akasema na mimi nikamuelewa, nikaona nimsaidie na nione vipi nitaweza kumfanya aishi maisha bila ya kutegemea wazazi wake, , kwani kwa muda huo alikuwa ameshakosana na wazazi wake kabisa..na wazazi wake, walisema kuwa binti yao huyo kazidi kwani kila mchumba anayemfuata yeye anamkataa,

‘Basi rafiki yangu mimi naona nikusaidie kwa hilo, unaonaje tukiwa washirika, ....?’ nikamuuliza.

‘Washirika kwa vipi, sisi ni marafiki tangia zamani, hilo la ushirika la kitu gani tena,…?’ akauliza.

Mimi namfahamu sana rafiki yangu huyo , hawezi kupata kazi ya kuajiriwa akatulia, sizani kama anaweza kuhimili sheria na taratibu za kazi, mara ngapi anaajiriwa na baada ya hata mwezi kuisha keshakosana na muajiri wake,...nikataka nimbadili kabisa aondokane na hulika hiyo, japokuwa hiyo ya kuchagua wanaume nilishindwa.

Nakumbuka wakati tunasoma rafiki yangu huyu alikuwa akipenda sana kazi za upelelezi, kutokana na kusoma vitabu mbali mbali vya hadithi za kipelelezi, na kuangalia sinema za namna hiyo,na hiyo ilikuwa ni ndoto yake kuwa akimaliza shule atajiunga na kazi za upelelezi.

Kwa bahati mbaya, ndoto yake hiyo haikuweza kufanikiwa, tulipomaliza shule, akajikuta akifanya kazi nyingine kutokana na matakwa ya wazazi wake, ambazo hakuweza kuzifanya itakiwavyo, akaanza kutafuta sehemu nyingine, na hata huko hakuweza kukaa muda mrefu,ikawa mtu wa kubadili kazi, mara leo yupo hapa , kesho yupo kule.

Basi siku hiyo alipokuja kwangu na malalamiko hayo juu ya wazazi wake, kutaka aolewe, mimi nikakumbuka ile ndoto yake hiyo, nikaona kwa vile tumekuwa watu wakusaidiana, kupendana, toka utotoni, ngoja na mimi nijaribu kumsaidia nionavyo mimi, na ndipo nikamapa wazo langu hilo nikamwambia;

‘Rafiki yangu mimi nataka kuifufua ile ndoyo yako ya shuleni, upo tayari....?’nikamwambia na yeye akawa kama hakunisikia,kwani wakati huo alikuwa anacheza na simu yake, nafikiri alikuwa akiandika ujumbe kwa watu wake, na baadaye akasema;

‘Ndoto ipi...?’ akaniuliza kwa dharau, na huku akiendelea kuangalia simu yake.

‘Kwanza rafiki yangu nakutaka unielewe, nikiongea na wewe uhakikishe kweli unaongea na mimi, ....kama bado una tabia za utoto, hutafika mbali, weka hiyo simu pembeni, nataka tuongee kikubwa....’nikasema kwa sauti ya ukali, na yeye aliponiangalia usoni akakutana na uso wa kazi, uso unaoashiria amri, akashangaa, kwanza, halafu akabetua mdomo, na kusema.

‘Ok. Bosi, maana kwa vile wewe ni bosi kwenye kampuni zako unafikiria kila mtu utamsimamia hivyo hivyo..lakini kwa vile nimekwama, nitakusikiliza bosi....’akasema huku akiiweka simu yake pembeni.

‘Nakumbuka wewe ulikuwa na ndoto ya kuwa askari mpelelezi...lakini haikuwezekana, sasa nataka hilo liwezekane, hujachelewa, utakwenda kusomea hilo, lakini sio askari mpelelezi wa kipolisi, nataka uwe mpelelezi wa watu binafsi,...mpelelezi muhutasi, hiyo si inawezekana...?’ nikamuuliza. Na yeye kwanza akawa kama haamini hilo kwani muda umeshapita, na huenda hakuwa na wazo hilo tena.

‘Mhh, hilo nilishalitoa akilini, hayo yalikuwa ya kishule, ...sijui kama inawezekana, sina uhakika na hilo.na hiyo kazi inapatika kweli, maana nahisi nitahitajika kwenda jeshini, na huu mwili sizani kama utakubali shuruba, na amri.....’akasema.

‘Inawekana,....kwanini isiwezekane, kila kitu ni nia, kila kitu ni utashi, na dhamira ya kweli, sasa hivi vipo vyuo vingi tu vya kutoa hayo mafunzo, na hata kwenye mitandao kuna elimu kama hiyo, tuifanyie kazi, ...na na kwa vile mimi nakuhitajia kwenye mambo yangu,...tushirikiane, tutaweza...upo tayari....?’nikamuuliza.

‘Sijui...tuone ,..’akasema na mimi nikafahamu kuwa yupo tayari, nikamwambia ili aonyeshe dhamira ya kweli, basi ahangaike mwenyewe kuvitafuta hivyo vyuo, na mimi nitamsaidia kwa hali na mali. Na kweli baada ya siku kadhaa akasema keshapata chuo cha namna hiyo, na yupo tayari kwa masomo, na mimi nikamwambia nitawasiliana na wahusika wa hicho chuo.

‘Kwani ni mpaka wewe uwasiliane nao, cha muhimu ni maombi, na maombi nimeshatuma na wao wameshanikubali, kilichobakia na malipo..hakuna zaidi....’akasema.

‘Usijali..malipo nitalipa, lakini kama nilivyokuambia, mafunzo hayo ni kwa ajili ya kazi zangu, kwahiyo nataka niongee nao, nione jinsi gani wanaweza kukupika nitakavyo mimi....’nikasema na kweli nikaenda kuonana na wahusika wa hicho chuo, na tutakakubaliana, kwani nilitaka kwanza wamjenge huyo binti kikakamavu, na kuondoa ulegelege wa kutegemea wazazi,..na wao wakasema hiyo kwao ni kazi ndogo tu.

Sikuamini, huenda ni kwa vile, alikuwa na ndoto hiyo, au ni dhamira tu, ilimtuma ajitume hivyo, kwani, aliweza, na akafuzu vizuri sana, na kuna muda aliombwa ajiunge na askari polisi, lakini yeye mwenyewe alikataa, na akaja kwangu na kusema yupo tayari kwa kazi zangu, na tukaingia naye mkataba, akawa ni mtu wangu nikimuhitajia, lakini hapo hapo akawa kaajiriwa kwenye kazi fulani.

Nikawa kila nikipata kazi inayohitajia mambo hayo, nimampa ananifanyia, namlipa vizuri tu, au wakati mwingine anapata kazi zake nyingine binafsi akikutana na mawakili binafsi kuchunguza kesi fulani, basi ikawa ndio kazi yake nje ya ajira yake.

Kwa hali kama hiyo tukawa ni kitu kimoja, na kikazi mimi ni bosi wake, na haikutokea siku nikampa kazi, akaikataa,...

Kwahiyo ni mtu nilishibana naye, na ananiheshimu mimi na familia yangu, na alishaapa kuwa hataweza kunifanyia jambo baya,…je kwa hali kama hiyo ninaweza kuamini mambo ya kusikia tu…hapana, ilihitajia mud asana kuyaamini maneno ya watu

****************
‘Kwahiyo umenielewa, nikamuuliza , wakato docta naye anaongea na simu

‘Nitafanyaje sasa..inabidi…’akasema

‘Unajua ni kwanini nataka hili, ni ili jamii isije kuniona mimi mjinga, kuwa nafuga nyoka,…hilo linawezekana kweli, kuwa nilifanya yote hayo kwa mtu ambaye atakuja kunizunguka, …’nikasema

‘Lakini…..’akataka kujitetea

‘Sikiliza…mimi sitakubaliana na mawazo yao hata mara moja kuwa wewe rafiki yangu unaweza kunisaliti mimi, nitauweka wapi uso wangu…sasa ni wewe kuilinda hiyo hali, sizani kama unaweza kufanya jambo kama hilo…sizani, …au ..niambie ukweli hapa hapa, je ni kweli…?’ nikamuuliza

‘Mim naondoka….’akasema sasa akitikisa kichwa cha kuchanganyikiwa.

‘Sawa, mimi nakuamini, na..unasikia, …mimi nimeosha mikono yangu, nimechukua dhamana yako mikononi mwangu.., na wewe usije kuniangusha kwa hilo,…umenielewa lakini, na nataka hata wazazi wangu ikiwezekana wasijue kuwa mume wangu kapatwa na ajali, nataka tufanye namna ambayo, sawa ni ajali, lakini kwa mazingira yasiyo kuwa na kashfa, sawa..umenielewa hapo..?’ nikamuuliza

Nilimuona kama anataka kutoa machozi, lakini mimi sikujali,..najua sio mtu wa kutoa machozi, labda kitu kimemuingia machoni,…na muda huo nilikuwa kikazi zaidi, sikutaka kupoteza muda, nilitaka yeye aifanye hiyo kazi, na nione ukweli wake kupitia kwake yeye mwenyewe…., nilikuwa na maana yangu kubwa tu.

‘Ninataka wewe….uifanye hiyo kazi, sitaki utani, nataka tumfahamu huyo mtu, ni nani anaweza kuingilia ndoa yangu, au kama kuna jingine, tulijue mapema…, kwanini mume wangu awe hivyo…hapo kuna mawili, kashfa ya ndoa, au…kuna tatizo kazini, mimi sijui, wewe ni mtaalamu wa mambo hayo, sasa mimi nahitaji msaada wako, hii ni kazi nimekupa…’nikasema kwa hasira

‘Mimi naondoka….’akasema sasa akitaka kuondoka

‘Ondoka bwana,… mimi naondoka, mimi naondoka…ila kumbuka mimi…sitaki utani, …unanielewa, sitaki utani kwenye ndoa yangu kwenye kazi yangu, kwenye maisha yangu…ole wake huyo mtu, sitajali ni nani…hili nakuambia wewe kama rafiki yangu, ukisikia mimi nimefanya jambo, hutaamini….’nikasema kwa jaziba.

‘Sawa bosi....naondoka…’akageuka na nikahisi kuna mtu nyuma yangu nikageuka kwa haraka, nikiwa sasa naangalina uso kwa uso na baba yangu mzazi.

‘Baba…….’nikasema kwa mshangao mkubwa, wenye wasiwasi,

‘Kuna nini kimetokea…?’ ilikuwa sauti ya baba ya kiaskari

WAO LA LEO: Mara nyingi tunapokuwa na shida, tunasahau kuwa wenzetu pia na wao wana shida kama hizo za kwetu au huenda shida zao ni zaidi ya shida zetu, wakati huo wa shida, hatujali shida za wenzetuo,cha muhimu kwa wakati huo ni shida zetu, tunachotamani ni jinsi gani ya kusaidiwa, ni jinsi gani, shida zetu zitachukuliwa kipaumbele, na hapo utaanza kuwachuja marafiki zako, na rafiki utakayemuona ni wa kweli kwako ni yule atakayesimama kwenye shida zako, na kutetea hoja zako.

Tukumbuke kuwa,sisi sote ni wanadamu, na shida zimeumbiwa kwetu, na kwahiyo sote ni wahitajia,kama ni hivyo basi, ili tuwe sawa, tujaribu kuona shida za wenzetu zina umhimu sawa sawa na shida zetu.
 

Abdallahking

JF-Expert Member
Mar 19, 2018
1,989
2,000
SEHEMU YA 43


‘Baba umerudi lini…?’ nikasema, nikiwa nimenywea, maana ili sura ya kutisha ilipotea ghafla, na uso ukawa wa aibu,…uso wa kujipendekeza.

Kwa muda huo, baba alikuwa kanikazia macho tu, akimaanisha anasubiria jibu la swali aliloniuliza. Nilipoligundua hilo, nikasema ;

‘Ni ajali tu baba,….mume wangu kapatwa na ajali….’nikasema

‘Nimeshaonana naye na nimeshapata taarifa zote kutoka kwa dakitari, na bado nasubiria taarifa nyingine, maana ajali hiyo sio ya kawaida,

…kuna kitu ndani yake. Ni lazima kujiuliza ni kwanini, akaendesha gari kwa mwendo kasi kiasi hicho, alikuwa kalewa..’ akawa kama

ananiuliza

‘Hapana….’nikasema

‘Una uhakika….?’ Sasa akaniuliza

‘Mhh…ndio baba, maana hata Docta wamesema hakuwa kalewa, na hakuwa amekunywa kabisa siku hiyo….’nikamtetea mume wangu.

‘Lakini kulewa sasa imekuwa kawaida yake au sio…? Ni kwanini anafanya hivyo…?’ akaniuliza

‘Ni starehe zake tu baba, lakini litamalizika hilo…’nikasema

‘Una uhakika…?’ akauliza akiniangalia kwa makini

‘Baba….’nikasema hivyo na kutulia.

‘Nauliza swali langu tena….kuna nini kati yako wewe na mume wako, nilishakuuliza hilo swali awali ukasema ni mambo ya kawaida tu…,

nilikuambia, nikusaidie ukasema hapana,..mtayamaliza wenyewe, sasa kwa hili, sitaweza kusubiria , nataka kujua kila kitu, au uniambie

mwenyewe kuna nini…?’ akauliza

‘Baba …ni mambo ya kawaida tu ya ndoa, sizani kama wewe na mama mpo na furaha wakati wote, ..kuna muda kunatokea hili na lile, na

sizani yote ya ndani ya ndoa nahitajika kuyasema kwako, tutayamaliza tu kwa amani baba, hii ni ajali tu…’nikasema

‘Bint, mimi sio mtoto mdogo wa kukuuliza haya, nimesoma, nina uzoefu wa maisha zaidi yako,…unanielewa,..sitaki nikukumbushe kila kitu…

kuwa tulikuambia, tulikuambia,.. hukutusikia…, na asiyesikia la mkuu hufanya nini…’akasema

‘Lakini baba, nilishawaambia, mimi nitaweza, na ninaweza…, haya ni maisha yangu na mume wangu, tuachieni wenyewe…, maana

tumeshaoana sasa…, sizani kama ni busara tukarudia yale yale malumbano ya zamani, sasa hivi tuna watoto, tuna familia..baba maji

nimeshayafulia nguo nitafanyaje sasa, hebu niambie baba…’nikasema

‘Nafahamu hilo..utasema hivyo, utajitetea tena na tena…., si umekuwa bwana, unajiweza au sio…..haina shida,… ila lile linalogusa familia

yangu…, lile linakuja kunigusa na mimi mwenyewe.., sitaliacha lipite hivi hivi, hebu nikuulize ikitokea tatizo, la kikashifa kwako, utaambiwa

wewe ni binti wa nani..?’ akaniuliza

‘Kuna kashfa gani baba imetokea, mbona baba mnataka kuyakuza mambo, a kuna nini umesikia kibaya,…baba hakuna kashafa yoyote,…

kama umesikia hivyo, ni ….watu tu, kama ujuavyo wanadamu hatuna wema, …mimi nakuhakikishia baba haya mambo nitayamaliza

mwenyewe,…niamini baba…’nikasema

‘Una uhakika …..?’ akaniuliza, baba akikuuliza hivyo ujue hilo jambo analifahamu , anakupima tu.

‘Baba…’nikasema na yeye akageuka kuangalia nyuma, ..nahisi alikuwa akimuangalia docta, nikaangalia kule anapoangalia, lakini docta

hakuwepo..sijui alikuwa kaenda wapi…lakini badala yake nilimuona jamaa mmoja kasimama, akiwa anatuangalia..alipoona baba

anamuangalia, kwa haraka akaja alikuwa kashikilia bahasha kubwa mkononi

‘Binti yangu..nilikuwa safarini, lakini hata nikiwa huko nimekuwa nikiiwazia familia yangu, na familia yangu ni pamoja na wewe…mimi nina

hisa kwenye kampuni zenu, nilifanya hivyo makusudi, maana siwezi kutoa pesa zangu ziwekezwe tu, bila ya mimi kujua

kinachoendelea,....hii hapa ni taarifa ya kibishara ya kampuni yako na mumeo ..umeshawahi kuipitia vyema…?’ akauliza

‘Ndi-ndio baba lakini….eeh, kuna matukio mengi yamepita hapa karibu, sijapata muda wa kuipitia vyema, ila naifanyia kazi, kwangu, kwa

mume wangu sijawahi kukaa naye, sijui kinachoendelea, nitakaa naye nione tatizo lipo wapi…’nikasema

‘Kwanini biashara imeshuka kiasi hiki, hasa ya mumeo…?’ akauliza

‘Baba ni hali halisi, sio sisi tu,…na ngoja nitakuja kuipitia, mimi nina nakala zangu, au hii ni nyingine zaidi..?’nikasema

‘Na hizo pesa nyingi alizochukua mumeo, ni za nini, ni kwa ajili ya nini, umeshawahi kumuulizia mumeo pesa hizo kazifanyia nini…?’ akauliza

‘Pesa gani baba…?’ nikauliza maana sijui kama mume wangu alichukua pesa nyingi kwenye kampuni yake, mimi siingilii kampuni ya mume

wangu.

‘Anyway..hilo sio tatizo kwa sasa…, lakini ndani ya bahasha hiyo kuna kitu kingine, kuna taarifa ya biashata ya mumeo pia, na mengine

utakuja kuyaangalia humo ndani, halafu tutaongea…utaniambia hayo yote yana maana gani..’akasema
‘Sawa baba, nita-ipitia..’nikasema

‘Na kingine je wewe unakubaliana na hali hiyo ya mumeo …au ni maisha gani mnaishi hivyo…, nataka majibu kutoka kwako, sio leo,

tukikutana unanielewa, maana hujalelewa hivyo, sitaki aibu kabisa....’akasema

Alinikabidhi ile bahasha, na kwa mashaka nikaipokea, na kabla sijataka kufanya chochote, akasema;

‘Ile hali ya mumeo itachukua muda kupona….na ina maana shughuli nyingi alizokuwa akizisimamia yeye, zitasimama, na..zaidi hatujui

mapesa yote aliyochota aliyachukua kufanyia nini…sasa, kazi ni kwako, kabla mumeo hajazindukana, ulifanyie hilo kazi, fuatilia

kinachoendelea , baada ya hapo, mimi mwenyewe, nitajua la kufanya, sikutoa mataji wangu upotee bure, umenielewa…’akaangalia saa yake.

‘Baba hapa sio mahali pa kuulizana maswala ya biashara baba…mume wangu yupo hali mbaya, nina mawazo kuhusu afya yake, nipe muda

kidogo kwa haya…, naomba hayo tuyaache kwanza…’nikasema

‘Haya, ninayokuuliza....ni moja ya sababu ya kuchanganyikiwa kwa mumeo, kuna mengine kati yako na yeye, usipoziba ufa utajenga ukuta,

akipona akirudia tena, itakuwaje,..ni bora ujua cha kufanya kuanzia sasa..’akasema

‘Sawa baba nimekuelewa…’nikasema

‘Kuna maelezo muhimu humo, ila mengine..eeh yanafanyiwa kazi, ikithibitishwa kuwa ni kweli…unajua ni nini kitafuta,…maana

tulishakubaliana hilo, na sitarudi nyuma tena, unanielewa…?’ akauliza nakabla sijamjibu akasema

‘Nilikuambia na narudia tena,…kunguru hafugiki, sasa yanaanza kujitokeza, usizarau maneno ya wazee wako, ukataka kushindana nao,

sasa ni lako hili, ila lisiharibu familia yangu kwa ujumla, sitarudia tena hili…’akasema

Hapo nikabakia kimia tu…nikiwa nimeishikilia ile bahasha kubwa mkononi.

‘Mume wako, ….kabla niliwahi kuongea naye, nikamwambia nikirudi nahitajia majibu na maelezo…. sasa sijui ni sababu hiyo au kuna jambo

jingine, nahisi pia kuna jambo jingine limejitokeza…ila ninachotaka isije ikawa ni kashfa kwenye familia…sitavumilia hilo kabisa…’akasema.

‘Sawa baba, nina imani hiyo, kuwa hakuna kashfa mbaya….’nikasema

‘Na iwe hivyo, na iwe-hivyo,….’akasema akiangalia saa

‘Sawa baba, niamini mimi…hakuna jambo baya …’nikasema

‘Na huyo rafiki yako, unamuamini sana eeh…’akaniuliza

‘Yupi baba…?’ nikauliza

‘Huyo mzazi….’akasema na mimi hapo moyo ukalipuka paah.

‘Baba huyo ana nini tena…’nikasema

‘Najua unamtetea sana,…, niliwahi kukuambia, unachokifanya wewe, ni kama kufuga nyoka mwenye sumu chumbani kwako, ipo siku

atakuuma wewe mwenyewe, sikiliza binti, huwezi kumbadili mtu aliyeshindikana na wazazi wake, hu-we-zi, umepanda mbegu juu ya

jiwe…’akasema

Hapo nikakaa kimia,… nilikawa nawaza mbali kuwa huenda docta ndiye anafanya kazi na baba, anachukua kwangu anayapeleka kwa baba,

na hili la rafiki yangu inaokena limekwenda mbali, litanisumbua sana, sasa nitafanya nini…lakini moyoni, nikajipa imani kuwa nitalimaliza

mimi na huyo rafiki yangu..sizani kama kuna jambo kubwa kiasi hicho.

‘Huyo rafiki yako, ndiye atakayekuangamiza,..unajua kuwa yeye anashirikiana na mume wako…?’akasema kama ananiuliza, na mimi hapo

nikamwangalia baba yangu kwa macho ya mshangao, ila sikuwa nimemuelewa ana maana gani hapo…

‘Anashirikiana na mume wangu, kwenye nini baba, hapana, ni kawaida tu….!!’nikasema kwa mshangao.

‘Una uhakika…’akauliza na mimi nikakaa kimia

‘Ndio maana nakuambia…kuna tatizo, na tatizo hilo linaweza kuleta taswira mbaya kwenye familia, na …narudia tena sitaki kashfa mbaya

kwenye familia yangu, muuguze mume wako apone,…na apone kweli, maana sitarudia tena. ….’akasema na kuondoka.


************

‘Huyo-huyo rafiki yako, ndiye atakayekuangamiza, akishirikiana na mume wako…’ ilikuwa sauti iliyokuwa imebakia akilini mwangu, na

kunifanya niduwae kwa muda, hadi pale nilipohisi mtu kunikaribia.

Nikainua kichwa kuangalia ni nani huyo, …alikuwa ni docta.

‘Vipi, mwenzako ndio keshaondoka….?’ Akaniuliza docta
 

Abdallahking

JF-Expert Member
Mar 19, 2018
1,989
2,000
SEHEMU YA 44

‘Wewe ulikuwa wapi..?’ nikamuuliza swali kabla sijajibu swali

‘Unajua nilimuona docta kwa mbali, akitoka, nikaamua kumkimbilia kumuwahi kabla hajaondoka, kwahiyo sikuweza kuwaambia,…na kweli

alikuwa akitoka, ,…na nimeweza kuongea naye na kwenda kumuangalia mume wako, bado amelala, ila yupo sawa, hana tatizo….’akasema

‘Kwahiyo mimi siwezi kwenda kumuona…?’ nikauliza

‘Kwa mujibu wa dakitari, ndio huwezi kwenda kumuona, kwa vile anatakiwa kulala ili dawa zifanye kazi....ila unaweza kwenda kumuona tu,

kwa mbali, kama unataka, muhimu usije kumghasi, mpaka hapo atakapozindukana kutoka usingizini yeye mwenyewe, …’akasema

‘Oh….hata hivyo, ni bora nikamuone tu…’nikasema

‘Sawa twende….’akaanza kutembea kuelekea huko alipolazwa mume wangu, na mimi nikawa namfuatilia kwa nyuma hadi chumba

alicholazwa mume wangu, alikuwa kweli kalala, ..nilimuangalia kwa muda, na kuhis machozi yakinilenga lenga, akilini sikuwa na wazo

jingine zaidi ya kumuombea apone haraka iwezekanavyo.

‘Haya umemuona, …twende maana tumejiiba tu, haitakiwi mtu kuja kumghasi, mpaka wakija kuhakikisha kuwa sasa hana maumivu

tena….’akasema, lakini nilikuwa kama simsikii, hadi pale aliponishika mkono na kunivuta tuondoke humo ndani.

‘Mume wangu jamani…’nikasema

‘Atapona ….’akasema docta

*********

Tulipokuwa nje, docta akaniuliza;

‘Kwanini rafiki yako kaondoka kwa haraka hivyo, tuiliongea nini na wewe umafanya nini, ..kuna kitu gani mnataka kukificha, mimi,

eeh...nilikuwa nataka kuongea naye maswala mengine….’akasema.

‘Ulitaka kumuona mtoto ili utake kuthibitisha uvumi na hisia zako, au…ndio keshaondoka hivyo, ..’nikasema.

‘Haya sawa, hamna shida, unaonaje sasa twende nyumbani,…maana kwa hivi sasa utakaa tu, na kwa mahesabu yao, mgonjwa ataamuka

baada ya kama masaa manne hivi,…chini au juu ya hapo… na akiamuka watamchunguza kwanza..ili kuhakikisha kama yupo sawa kabla

hawajawaruhusu watu kuongea naye, ….’akasema

‘Sawa…’nikasema hivyo tu, na tukatoka hadi tulipoweka magari yetu, kila mmoja akaingia kwenye gari lake na ikawa ni safari ya kurudi

nyumbani. Na sikutaka kabisa kusimama kwa docta, moja kwa moja nikaelekea nyumbani kwangu. Nilipofika kwangu, kwa haraka

nikampigia simu rafiki yangu.

Kwanza simu iliita kwa muda bila kupokelewa, …nikatulia dakika moja hivi nikapiga tena, ikawa hivyo hivyo,…lakini wakati inataka kukatika,

ndio ikapokelewa, na mimi nikamuuliza mdada, kwa haraka ni kwanini hapokei simu anajua namuitia nini.., yeye akajibu kwa haraka tu;

‘Nilikuwa naanika nguo za mtoto nje, sikuweza kusikia simu ikiita, na wakati naingia ndio nikasikia ikiita, nikaiwahi, habari za mgonjwa, kuna

lolote jipya tangia tuachane….?’akasema na kuniuliza.

‘Vipi umefikia wapi, au umeamuaje..?’ nikamuuliza , bila kujibu swali lake

‘Mhh…nimeongea na watu wa usalama barabarani kujua kinachoendelea kwanza, wamenipa picha halisi ya ajali yenyewe,…nilikuwa sijaipata

hiyo, zaidi ya kusikia kwa watu, sasa nimeweza kujua ajali ilivyotokea…zaidi ni mwendo kasi na wakati anakata kona kuingie ile bara bara

nyingine ndio wakakutana na lori, …kiukweli ni ajali mbaya…’akasema

‘Ndio hivyo, …kwahiyo umeshaianza hiyo kazi…au..?’nikamuuliza

‘Ndio nimeianza hivyo…bo-si’akasema na kumalizia neno la mwisho kwa kukata

‘Najua umetoka kujifungua na ulihitajia muda wa kupumzika, hilo nalifahamu sana, na sikuona kama kazi hii ina uzito wa kukufanya

ushindwe kuifanya kutokana na hiyo hali,…’nikasema, na nilisikia mlio wa simu kuingia, sijui ni ya kwake au ni yangu

‘Nitaangalia….’akasema, nahisi alitaka kukata simu.

‘Mimi nionavyo, ni kazi unayoweza kuifanya hata bila ya kutumia nguvu, kwani wewe una vyanzo vyako vingi vya kukusaidia bila ya hata ya

wewe kutoka hapo nyumbani kwako..'nikasema

'Sawa...'akasema

'Cha..., muhimu ni kuhakikisha kabla hawajafanikiwa watu wengine kujenga hoja za fitina, uwe umeshajua ni nini kinachoendelea, na je

umeshaweka mikakati yako tayari...?’ nikamuuliza, nikasikia mlio wa kuingia ujumbe nahisi ni simu yake.

‘Sawa nimekuelewa …’akatulia kwa muda, halafu akasema

‘Bosi…, nafahamu nipo kwenye mkataba na wewe, na niwajibu wangu kutimiza kila utakachoniambia, lakini nilitaka nikuweke wazi, kabla ya

kazi yenyewe ndio maana uliniona nasita sita...’akasema sasa kwa sauti ya kujiamini kidogo.

‘Kwahiyo umeshaelewa, au bado unasita sita, …’nikasema

‘Nitafanya kama utakavyo, hamna shida…na nilimuona baba yako, hapo hospitalini,....mliongea nini na yeye au…?’ akaniuliza.

‘Ni mambo ya baba na binti yake, ..ni yale yale…yeye hawezi kunizuia mimi nisifanye kazi yangu, ila kuna jambo..ndio maana nataka

ulifanyie kazi, kabla mambo hayajawa mabaya ....’nikasema

‘Sawa..nitaifanya tu, hamna shida… ila nami unielewe, ndio nimetoka kujifungua, kitoto changu bado kichanga, hali yangu bado haijawa safi,

nahitajia muda wa kutulia kwanza, nahitaji muda wa kukaa na mwanangu na pia nipo kwenye maandalizi ya ile safari ya kwenda nje

kusoma, kwahiyo huenda nisiifanye hiyo kazi kwa muda unaotaka wewe,.....’akasema rafiki yangu huyo.


‘Hamna shida, mimi naelewa hilo….ila fanya uwezevyo, kabla wengine hawajagundua lolote, kama kuna kashfa ya mume wangu nataka

niifahamu mapema ni kashafa gani, na …mengine nitayafanyia kazi mimi mwenyewe …’nikasema

‘Hamna shida, nitafanya hivyo…bosi…’akasema kwa kujiamini.

Ndio hapo nikakumbuka ile bahasha,..

‘Haya badae nitakupigia…’nikasema na kukata simu.

Nikakumbuka kuwa sikuichukua ile bahasha kwenye gari, haraka haraka hizi bwana, na mawazo mengi kichwani,….nikatoka hadi kwenye

gari, ..nakumbuka niliiweka kwenye kiti cha mbele, kwanza nikawasha kiwambo cha gari ile niweze kufungua mlango,..kwa haraka

nikafungua mlango,

Hakuna kitu…! Bahasha haipo….!

‘Haiwezekani…’nikasema nikikagua kila mahali, na kujaribu kuvuta hisia za kumbukumbu yangu kuwa labda niliondoka nayo, …hakuna kitu….

‘Nina uhakika sikuondoka nayo!..ilikuwa hapa..’nikasema mwenyewe.

Mara simu yangu ikaita,…nikaangalia, alikuwa ni docta

‘Unasemaje , una mzigo wangu…?’ nikajikuta namuuliza hivyo kwa haraka.

‘Mzigo gani…?! ‘akauliza kwa mshangao, halafu akaendelea kusema

‘Nataka kukuambia hivi, wakati tunakuja,…nikiwa nyumba yako, ..niliona kama kuna mtu alikuwa akikufuatilia kwa pikipiki,…hukumuona…?’

akauliza

‘Hapana…sikuwa makini kukagua nje. Mbona zilikuwa pikipiki nyingi tu, una uhakika ….ni nani…?’ nikasema na kuuliza

‘Lakini sizani kama alikuwa na nia mbaya, mimi nilipoona kapitiliza ulipokuwa unaingia kwako, nikajua labda ni hisia zangu tu, kuna lolote

limetokea…?’ akaniuliza

‘Huyo mtu aliishia wapi, hakuingia kwangu…?’ nikamuuliza

‘Alipitiliza, hakusimama, sikumuona akisimama,..kwani kuna tatizo…?’ akauliza

‘Hakuna tatizo,..ila…lakini sina uhakika, kuna kitu wamechukua kwenye gari langu…’nikasema

‘Haiwezekani, muda gani sasa huo..! Ina maana labda,… alirudi akaingia kwako, maana mimi nilipoona kapitiliza, niliingia kwangu, siwezi

kujua kama alirudi au laa..hakuna mtu hapo nje kwako unaweza kumuulizia…?’ akasema

‘Hamna shida, sio kitu muhimu sana…’nikasema

‘Kama wamehangaika kukichukua, kitakuwa muhimu kwao..jaribu kufanya uchunguzi…na kama unahitajia msaada wangu niambi..’akasema,

na mimi nikakata simu,

Nilipokata simu kuongea na docta,nikatoka nje na kukagua..sikuona dalili ya mtu, hata gari,…sikuona dalili kuwa mtu alilifungua, kwa vipi

lakini…nikataka kumpigia rafiki yangu simu, yeye ndiye msaada wangu wa vitu kama hivi, lakini kabla sijaanza kupiga simu, simu ikaanza

kuita, ….alikuwa ni baba!

NB: mambo ni mengi lakini tutafika tu


WAZO LA LEO: Wahenga walisema hata mbuyu ilianza kama mchicha au mche wa harage ukichipua..Na hata matatizo, yana chanzo

chake, kidogo kidogo huja kuwa tatizo kubwa, …nibora kuchukua tahadhari kabla tatizo halijawa kubwa, tusizarau matatizo, na kuyasubirisha

, kama lawezekana kushughulikiwa lifanyie kazi haraka iwezekanavyo, ya leo yaweza yasiwe ya kesho.
 

Abdallahking

JF-Expert Member
Mar 19, 2018
1,989
2,000
SEHEMU YA 45

Nilipomaliza kuongea na baba, nilihisi mwili mnzima ukinicheza cheza kwa hasira, lakini sikujua namkasirikia nani, au naogopa nini, lakini

anayoongea ni kama ana uhakika nayo,..awali nilijua ni ile chuki kuwa nimeolewa na mtu wasiyemtaka, lakini haya anayoongea sasa

yananifanya nianza kuingiwa na mashaka

Wakati anaongea akili yangu ilikuwa mbali, ikijaribu kuunganisha matukio yaliyofuatana, kujifungua kwa rafiki yangu mtoto anayefanana na

watoto wangu, ajali ya mume wangu, ambayo ina utata, na inaonekana alitokea upande anapoishi rafiki yangu.

Sasa kuna mtu kaiba bahasha , bahasha ambayo nahisi ilikuwa na ushahidi,…sikupata hata nafasi ya kuifungua,..kwa hali hiyo akili ikaanza

kunionya kuwa kuna kitu...kuna mtu, ananichezea, ..ni nani huyo

Mume wangu, ...hapana, mume wangu anaumwa, hajiwezi,

Rafiki yangu....…


‘Unasikiliza wewe bint...'baba akaongea kwa ukali kwenye simu

'Nakusikiliza baba...'nikasema

'Nimekupigia simu, kuwa kampuni ya mume wako, ipo karibu kufilisika, na kuna madeni mengi sana…una hiyo taarifa…?’ baba akauliza

‘Baba ndio nimerudi nyumbani, sijapata hata muda wa kuipitia ile taarifa uliyonipa, mimi sijui lolote kuhusu kampuni yake, alikuwa

akiendesha mambo yake na mimi yangu…’nikasema

‘Unaona sasa, hiyo ndio ndoa mnayoitaka nyie uhuru wa kufanya mtu apendavyo, hata kwa mke na mume, aah…kila mtu kivyake, ..nikuulize

hivyo ndivyo tulivyokufunza…’akasema baba na mimi nikabakia kimia.

‘Sasa sikiliza mimi sitaweza kutoa chochote tena kwenye kampuni ya mume wako, au hata yako, maana nyie sasa mnajiweza, au sio…na

hayo madeni ya mume wako mtajua jinsi gani ya kuyalipa, kama ni kufilisi mali za kampuni mtajua wenyewe, ila mjua kuwa mnahitajika

kurejesha mtaji wangu…’akasema

‘Baba, hatuwezi kufanya hivyo wakati mtu yupo mahututi hospitalini…’nikasema

‘Na huyo rafiki yako alizaa na nani…?’ akanishtukiza na swali ambalo lilikuwa kama mtu kazabwa kibao usoni.

‘Mi-mi…baba, sijui…’nikaweza kusema hivyo

‘Una uhakika…?’ akauliza

‘Mi-mi..sijui baba, kama mwenyewe hajawaweza kunieleza, nitajuaje, nahisi hataki watu walifahamu hilo…’nikasema

‘Mtoto wake anafanana na watoto wako au sio…’akasema kama kuuliza

‘Mhh, baba umeyajuaje hayo ina maana umeweza kumuona huyo mtoto…?’ nikauliza na mara kwenye simu yangu kukaingia ujumbe ,

sikutaka kukatiza simu ya baba, ila yeye akasema.

‘Tazama hiyo picha niliyokutumia kwenye simu yako…’akasema ikabidi niache kuongea naye nitazame hiyo picha.

‘Huyo ni nani…?’ akuliza

‘Hawa ni mapacha wangu, watoto wangu wakiwa wadogo…’nikasema

Baadae ukaingia ujumbe mwingine akionekana mtoto mchanga, .alikuwa mtoto wa rafiki yangu, na pembeni wamewekwa watoto wangu

kama kuwafananisha na huyo mtoto, kiukweli wanafanana sana, hana tofauti na watoto wangu kwa sura, isipokuwa yeye hana nyusi

nyingi…sura ya kiume ilionekana usoni mwake.

‘Hata usemeje,….mtoto wa rafiki yako anafanana sana na watoto wako…sasa niambie ukweli kuna nini hapo, je sio kweli kuwa mume wako

anashirikiana na rafiki yako au kuna nini kinachoendelea kati yenu, mimi nisichokifahamu…’akasema baba

‘Una maana gani baba…!!, kuwa rafiki yangu anaweza kutembea na mume wangu…?’ nikauliza

‘Nikuulize wewe sasa…’akasema

‘Haiwezekani baba, unataka kusema nini kuwa mimi nimeshirikiana na rafiki yangu kulifanikisha hilo, au…’nikasema

‘Sasa hilo utajua wewe mwenyewe na mume wako na huyo unayemuita rafiki yako kipenzi…ndugu yako…, lakini kama ikatokea kuwa ni

hivyo, sitaweza kuvumilia upuuzi huo, kwanini ukaruhusu hilo, au ulitaka rafiki yako awe mke mwenza wako…au?’akasema baba kwa ukali

‘Baba unanijua nilivyo, mimi siwezi kuruhusu kitu kama hicho, na sio kweli baba, kufanana kwa watoto sio ushahidi wa kulithibitisha hilo,

ndio hata mimi niliingiwa na mashaka hayo, lakini rafiki yangu hawezi kunifanyia hivyo baba, sio kweli…’nikasema

‘Sasa ilikuwaje…jiulize hilo kwa makini,…je ni mume wako kakuzunguka au unataka kusema nini, jitetee sasa….?’ Akauliza

‘Baba huyo anaweza akawa mdogo wake mume wangu, anaweza akawa ndiye baba wa huyo mtoto, niliongea na huyo rafiki yangu, na

kasema hivyo, hanificho kitu, kiukweli siwezi kuamini hayo, baba haiwezekani, …’nikasema hivyo japokuwa sina uhakika

‘Na iwe hivyo…..vinginevyo, utaniambia, mimi kama mzazi nimeshajua ukweli, lakini siwezi kwanza kuliingilia hilo, …isome hiyo taarifa

niliyokupa, halafu na hayo yaliyogundulikana , kila kitu kipo wazi, ukiunganisha hiyo taarifa, matukio na picha, utakuja kuniambia….umesikia,

…’akasema na kukata simu

‘Bahasha haipo, sasa itakuwaje..siwezi kumuambia baba ukweli kuwa imeibiwa, ataniona mimi ni mzembe..sasa nifanyeje…’nikawa naongea

peke yangu

Akilini nikajua kuwa baba atakuwa aliandaa taarifa inayohusiana na mume wangu, huenda na ….ingenisaidia sana, sasa nifanyeje, na ni

nani kaiba hiyo bahasha?

‘Sasa hiki ni kitendawili kwangu….’ Nikasema nikikaa kwenye sofa, nikashika kichwa nikiwaza…nifanyeje

Kwa haraka nikachukua simu yangu.

***********

‘Umefikia wapi…?’ nikamuuliza

‘Kuhusu hiyo kazi eeh… bado sijapata lolote la muhimu, ila kuna jambo nalifuatilia bado halijawa sawa, nikiwa na uhakika nalo

nitakuambia…’akasema

‘Wewe na mume wangu mumeanza lini mashirikiano ..?’ nikamuuliza na nilihsi hali ya kupumua kwa nguvu kutoka kwa rafiki yangu huyo

‘Una maana gani sijakuelewa hapo…?’ akauliza

‘Yoyote yale…najua unaelewa ninachokuuliza..?’ nikauliza

Kukapita ukimia fulani, halafu nikauliza tena

`Umenisikaa nilichokuuliza....?’ nikauliza .

‘Nimekusikia lakini sijakuelewa bosi, una maana ganu kuuliza hivyo, sijui unachokiongea bosi...’akasema

‘Kwanini unakuwa tofauti hivyo, sio kawaida yako unanipa mashaka , mara nyingi nikikuuliza swali unakuwa mwepesi kulitafsiri na majibu

yako yanakuwa ya haraka…na mara nyingi yanakuwa ya ukweli, tunageukana siku hizi…’nikasema kwa ukali

‘Rafiki yangu, mimi sijakuelewa,o-bosi, sina mashirikiano yoyote zaidi ya yale tuliyokubaliana, ukiniagiza nifenye ndivyo nafanya, na zaidi

subiria taarifa ya kazi uliyonipatia, kwani kuna nini bosi…’akauliza, kiukweli tukiwa kwenye maswala ya kikazi hupenda kutumia neno hilo

bosi.

‘Ukweli utadhiri,…endelea na kazi niliyokupatia, ila ujue mimi sio mjinga, kukuamini kiasi hicho sio kwamba nimefumba macho na kuziba

masikio, akili yangu inafanya kazi vizuri tu, …unanielewa…’nikasema

‘Nakuelewa bosi….’akasema

‘Watu wanasema , na sio mmoja sasa, na hili kama limefika kwa baba ni hatari sana, kama kaamua mwenyewe kulifuatilia, sijui itakuwaje,

mimi nilipomuona mtoto wako kufanana na watoto wangu niliingiwa na mashaka, hayo kama binadamu, lakini najua wewe kama rafiki yangu

huwezi kunisaliti…’nikasema

‘Ni kweli…siwezi kufanya hivyo….’akasema‘Je kuna kitu unanificha…?’ nikauliza

‘Bosi unakumbuka ni wewe uliyenishauri kuwa nikatembee nje ili nipate mimba, na ukanishauri nitafute hata mume wa mtu…’akasema

‘Ndio ukaamua kutembea na mume wangu…?’ nikamuuliza

‘Hapana bosi, mimi najiuliza ni kwanini wewe unapaniki kiasi hicho…’akasema

‘Kwasababu lisemwalo lipo…na wewe hutaki kuniambia ukweli, haya basi niambie baba wa huyo mtoto ni nani…kama hayo yanayosemwa sio

ukweli…?’ nikauliza

‘Yanasemwa mengi bosi na sio yote yana ukweli, …niamini bosi mimi sifanyi kitu kinyume na ulivyoniagiza….na..hebu kwanza subiria nimalize

kazi uliyonipa ili tukiongea tuwe na ushahidi….wewe si ndio unataka huo, sasa subiria….’akasema

‘Mume wangu ana kitu kinamsumbua, mdocta wananiuliza kuna jambo gani kalifanya ambalo halimpi amani, nataka kulifahamu, sasa kama

ni hilo, ..na wee unamjali shemeji yako, niambie, sema ukweli tuone jinsi gani ya kumsaidia…’nikasema

‘Sizani kama …’akatulia

‘Huzani nini, ..?’ nikauliza

‘Kuwa yeye kuna jambo linalohusiana na mimi au mtoto linamsumbua, sizani, nahisi ni mambo yenu wewe na yeye, au mambo ya kazini

kwake…’akasema

‘Aliwahi kukuambia hivyo…?’ nikauliza

‘Nasema tu..na yote utakuja kuyaona, si umenipa kazi, sasa subiria…’akasema

‘Kwahiyo katika ugunduzi wako, umeliona hilo..sawa…?’ nikauliza

‘Ndio nahakiki ukweli, siwezi kukujibu kwa sasa unajua nifanyavyo kazi yangu, niamini bosi…’akasema

‘Lakini baba anahitajia majibu nitamjibuje mfano akinipigi asimu sasa hivi…?’ nikauliza
‘Mwambia tunalifanyia kazi bosi…’akasema
 

Abdallahking

JF-Expert Member
Mar 19, 2018
1,989
2,000
SEHEMU YA 46


‘Sasa nisikilize sana, acha maneno hayo, ya kunizunguka, naona unapima hasira zangu, acha kauli za kufanya niondoe uaminifu wangu

kwako, nimeongea na baba, na nimemthibitishia kuwa huenda mtoto wako anafanana na watoto wangu kwa vile ulitembea labda na ndugu

za mume wangu, sasa tafuta ushahidi wa kulithibitisha hilo, kama ni kweli, vinginevyo, hutaamini nitakachokifanya…’nikasema

‘Kwani kamuonea wapi mtoto wangu, mbona hajawahi kuonana na mimi…?’ akauliza

‘Mimi sijui yeye kanitumia picha ya mtoto wako, na mimi nilipoichunguza kiukweli mtoto wako anafanana sana na watoto wangu, kwa mtu

yoyote atafikiria hivyo, kuwa wewe umetembea na mume wangu…’nikasema


‘Rafiki yangu, ...najua itafika muda ukweli utadhihiri, wa-ache watu wasema, lakini ukweli utabakia pale pale, na ukweli mwingine kama sitaki

ujulikane hakuna wa kunilizimisha, hata awe nani…’akasema

‘Kwahiyo unataka kusema nini…?’ nikauliza

‘Kuwa subiria taarifa ya kazi yako, halafu utakuja kuamua mwenyewe…’akasema

‘Kwahiyo ni kweli…?’ nikauliza

‘Kuhusu nini sasa…?’ akauliza

‘Usitake kunifanya mimi kama mtoto mdogo, unajua nimekuuliza nini…’nikasema kwa ukali

‘Hapana, sio kweli, kama ni hivyo unavyofikiria wewe, japokuwa sijui ina maana gani hapo, ukweli wote nitakuambia mimi ambao ni lazima

uujue, ngoja nimalize hii kazi uliyonipatia kwanza…’akasema

‘Narudie tena, mimi nimeongea na baba yangu nikamthibitishia hilo, kuwa mume wangu hawezi kufanya upuuzi huo, kwani kama ni kweli,

itakuwa kashfa kubwa sana kwenye familia yangu, unalifahamu hilo…’nikasema

‘Mhh…nakuomba kitu kimoja,kwanini usisubirie kwanza nimalize hii kazii uliyonipatia, kila kitu kitakuwa wazi, na hata baba yako, ataamini tu,

usiwe na wasiwasi kabisa, …’akasema

‘Nakuuliza tena, je kuna ukweli wowote wa hizi shutuma kuwa huenda wewe na mume wangu mna mashirikiano fulani, ambayo yamekwenda

zaidi hadi kuingilia ndoa yangu…?’ nikamuuliza

‘Sio kweli….’akasema

‘Nataka ushahidi…wa kumthibitishia baba yangu,,unanielewa, kesho niupate, nakupa muda huo hadi kesho, unanielewa…’nikasema na

kumuuliza

‘Sawa bosi….’akasema.

‘Kama ni kweli, umenithibitishia hilo, basi mimi nataka ukweli wote kuhusu mume wangu, nataka kujua ni kwanini hayo yakatokea, nataka

kufahamu huyo mwanamke mwingine aliye na mashirikiano naye, nilikuambia utafute huyo mzazi ni nani, nimeambiwa, hakuna mzazi

mwingine sasa ni nani zaidi yako…’nikasema

‘Utamfahamu bosi, kila kitu nimekifuatilia …’akasema.

‘Sawa, kwa ajili ya urafiki wetu, kwa ajili ya kupona kwa mume wangu nakusubiria wewe, natumai haitafikia muda tukawa

maadui,...’nikasema

‘Ni kweli, haitatokea hivyo, niamini, …’akasema

‘Una uhakika..?’ nikauliza kama anavyopenda kuuliza baba yangu.

‘Siwezi kukuangusha bosi, ndio maana nataka kila kitu kiwe wazi, ili nikikuletea hiyo taarifa, kusiwe na kigugumizi tena, unanielewa

nifanyavyo kazi zangu, najua baada ya taarifa hiyo hata baba yako, hatakuwa na tatizo tena, itabakia wewe kuchukua hatua

zako...’akasema.

‘Sawa ……na nitaichukua hatua ambayo hutaweza kuamini…’nikasema

‘Oh, hatua gani…?’ akauliza

‘Nimeliwazia sana hilo,…limeniumiza sana kichwa changu, huyo shetani nikimpata, kuna watu nimewapanga, kuna wale mabaunza, niliwahi

kukuambia walishaifanya hiyo kazi kwa rafiki yangu mmoja, unakumbuka yule binti aliyejiua, nataka iwe hivyo kwa huyo shetani, harabiwe

kiasi kwamba hatatamani kuishi tena....’nikasema.

‘Mungu wangu....’akasema.


‘Lakini kwanini kufanya unyama wa aina hiyo …?’ akauliza.

‘Wewe kafanye hiyo kazi…kuna jambo jingine nilitaka wewe ulifanyie kazi, lakini naona nitalifanya peke yangu, kuna watu wanataka

kunichezea…wameingia hadi kwenye anga zangu…sitaki baba anione mimi sijui kazi,…baadae nakwenda hospitalini kwanza...’nikasema na

kukata simu.

**********
Nilifika hospitalini, na kabla sijaenda wodini, akaja docta rafiki yangu, kumbe yeye alihawahi hapo hospitalini, …nilipotoka kwenye gari langu

tu, akajitokeza na kuniwahi, akanisalimia kwa haraka halafu akasema;

‘Niliongea na docta anayemshughulikia mume wako, hali yake ipo salama kuna mambo kidogo yapo kwenye uchunguzi, na docta

wamesema unaweza kwenda kuongea na yeye, japokuwa anaongea kwa shida, kumbukumbu zake bado hazijawa sawa, ni kawaida tu…

zitakuwa sawa taratibu, nab ado hajaweza kujiinua mwenyewe kitandani…’akasema

‘Mhh..kwahiyo unataka kusema nini… kuwa hakumbuki kilichotokea au hakumbuki watu….?’ akauliza.

‘Yah, kwa hivi sasa hata ukimuuliza atakuwa kama anatafakari, kujiuliza, sasa kwa hivi sasa haitakiwi kumuuliza uliza maswali kama hayo,

..ndio maana walizuia watu kuonana naye, kwa hivi sasa wanaruhsu watu wachache wanaomfahamu..lakini kwa tahadhari hizo…’akasema.

‘Sawa nimekuelewa, ..lakini huenda kukatokea athari gani nyingine, hata kama ni huenda, nataka kujua tu..’nikasema.

‘Mhh…athari nyingi ni za muda tu, Inawezekana ikatokea , asiwezi kuzaa tena, inawezekana sio lazima, athari nyingine ndio hizo kama hiyo

kushindwa kutembea kwa muda, kukosa kumbukumbu nk, lakini mengi ni ya muda tu,...’akasema.

‘Unaposema kuwa anaweza kushindwa kuzaa, ina maana gani, kuwa hataweza kabisa ku-ku....’nikasema kwa kigugumizi.

‘Kufanya kazi ya uanaume..sio hivyo…atafanyakazi kama kawaida, ila..kuzaa, hata hivyo, sio lazima kuwa hivyo…’akasema

Mara akaja, docta aliyekuwa akimshughulikia mume wangu, alikuwa anataka kuongea jambo, na huyo rafiki wa mume wangu akamuwahi

kabla hajasema lolote, na kitendo hiki sikukipenda, niliona kama anazuia nisisikie jambo fulani, nikawasogelea na yule docta akasema kwa

haraka;.

‘Mnaweza kwenda kumuona mgonjwa, yupo katika hali nzuri tu, ila kwa tahadhari, msimuongeleshe sana, au kumuuliza maswali ya

kumfanya afikirie sana, na mengine bado tunayafanyia kazi, bado yupo kwenye uchunguzi, ....kwa ujumla hali yake inaendelea

vyema...’akasema, na mimi nikataka kumuuliza swali, docta rafiki wa mume wangu akadakia na kusema,..

‘Hakuna shida docta, mimi nitahakikisha mgonjwa hapati shida, ...na tunashukuru sana, nitakuja tuongee vizuri....’akasema na yule docta

akaondoka, na mimi nikageuka kumwangalia docta na kumuuliza.

‘Hivi kwanini unakuwa hivyo, inakuwa kama kuna jambo hutaki mimi nilisikie kutoka kwa huyo docta, mimi ni mke wake, nina haki ya

kufahamu kila kitu...kwanini mnataka kuniweka roho juu...?’ nikauliza.

‘Sikiliza mimi ni docta, na pili mimi niliwahi kuwa mpenzi wako, nakufahamu ulivyo, ndio maana nataka habari zote kwako ziwe kwa maslahi

yako, zisije zikakufanya ukawa na mshituko, na pia usije ukafanya kitu kikaja kumuathiri mgonjwa..’akasema

‘Kwahiyo kuna kitu unanificha…?’ nikauliza

‘Hakuna…ni tahadhari tu,…niamini mimi, nayafanya haya kwa nia jema kabisa..nilikupenda na nitaendelea kukupenda…na namjali rafiki

yangu…sitaki aje kudhurika wakati nafahamu …’akasema na mimi nikamtupia jicho na kuangalia pembeni.

‘Wasiwasi wangu ni kuwa inavyoonekana kuna tatizo la kiafya kwa mume wangu, na nyie hamtaki kuniambia, ndio wasiwasi wangu

huo...’nikasema.

‘Ninachotaka hapa ni hekima, mara nyingi docta akisema mgonjwa wako anahisiwa kuwa tatizo, watu hulichukulia kama ndio tatizo, uvumi

husambaa, na hata kumfikia mgonjwa, kwa hivi sasa hatutaki mgonjwa apate kitu cha kumuumiza kichwa, ....inaonekena ana mfadhaiko

fulani unaomkera,, unampa shida sana, sasa hilo ndilo ninalotaka baadae tuongee....’akasema.

‘Mfadhaiko....?’ nikauiliza kwa mshangao.

‘Ndio kunaonekana kuna jambo lina mkera, linampa shida,na kwa minajili hiyo, anajikuta hana amani...au nafsini mwake, anaogopa kuwa

kuna kitu kitatokea kibaya, lakini yupo kwenye hali ambayo hawezi kufanya kitu..naweza kusema hivyo...’akasema.

‘Mhh, hapo mimi sijuii....’nikasema.

‘Ndio maana nataka utumie hekima kubwa katika kuliongelea hili , tumia hekima sana kuongea na mum e wako, na kwepa sana

kumshinikiza kwa maswali magumu na shutuma, ndio maana nilitaka wakati unaongea na yeye na mimi niwepo, kipindi kama hiki kwake ni

kigumu sana, ... na hebu nikuulize, je mwenzako hana tatizo jingine kubwa unalohisi kuwa kalifanya....’akaniuliza.

‘Kiukweli sijui, labda mambo ya kazini kwake, lakini nitajitahidi kutafuta kama kula lolote zaidi…kuna watu wanalifanyia kazi………’nikasema

‘Rafiki yako..au sio?’ akaniuliza

‘Yawezekana…’nikasema

‘Una uhakika hakuna kitu kingine kinamsumbua mume wako ambacho wewe unakifahamu na unaweza kukifanya kumsaidia ….ili awe na

amani…?’ akauliza na mimi sikutaka kumuambia hayo aliyoniambia baba, kuwa huenda ni madeni, …

‘Sina uhakika, ndio maana nasema , labda maswala ya kikazi, huko ofisini kwake, na mimi sina ushirika na yeye huko….’nikasema

‘Ya kikazi hayo mhh, ni ya kawaida, watu wanadaiwa wengi tu…nahisi kuna jingine kubwa ya hilo,…wewe ndiye mtu wake wa karibu wa

kulisaidia hili’akasema. Na kabla sijasema kitu simu ya docta ikawa inaita na yeye akaangalia mpigaji na kusema;

‘Tutaongea baadaye hii simu ni muhimu sana...wewe tangulia huko kwa mgonjwa, nakuja, ila kumbuka,....usimuulize maswali mengi ya

kumuumiza kichwa’akasema docta huku akianza kuongea na hiyo simu yake.

Nikawa natembea kuelekea huko kwa mgonjwa, nafsini nina wasiwasi, …nitaongea nini na yeye, na nashindwa kuvumilie mengina

yanayotokea, nimesikia mengi, nay eye ndio mwenye kauli ya kukubali au kukataaa..je nitaweza kujizuia..Nikashika kichwa nikiwaza,;

‘Lakini kwanini niteseke kwa mawazo wakati muhusika yupo...kwanini nisimuulize tu, hapana nitasubiria, lakini nikisubiria baba anahitajia

majibu, je kama ni kweli, kuwa mtoto wa rafiki yangu ni wake, nitajuaje, hapana sio wa kwake..mmh, sijui nifanyaje....’nikajisemea

mwenyewe kwa sauti ya chini chini.

‘Nitamuuliza tu, kinamna ambayo sitamuumiza…’nikasema, na nikageuka nyumba, kumuangalia docta, alikuwa bado anaongea na simu,

sasa akawa ananionyeshea ishara kuwa nisubirie kwanza...mimi sikumsubiri nikaingia ndani kukabiliana na mume wangu...

‘Nitamuuliza tu….’nikasema na nilipoingia nilishangaa, mume wangu alikuwa kakaa kwenye kitanda, miguu chini, nikashikwa na butwaa,

walisema hawezi kujiinua mwenyewe, mbona…na kwa mdua huo alikuwa …anaangalia mlangoni kama anasubiria mtu, akiwa na tabasamu

mdomoni, na aliponiona mimi, tabasamu lililokuwa mdomoni likatoweka, akakunja sura…

**********

WAZO LA LEO: Mwili wa binadamu ni mdhaifu sana, na kosa dogo linaweza likaharibu utaratibu mzima wa mwili wa binadamu, mfano

angalia wengi waliofikiwa na matatizo ya kupatwa na kiharusi, kupooza kwa viungo, ...ukichunguza sana utaona kuwa tatizo hilo lilitokea

baada ya jambo dogo tu, kwako wewe mzima, uliona ni jambo dogo tu, lakini kwa mwenzako mwenye tatizo, alishindwa kuhimili, hasira

kidogo, au mshituko kidogo tu, na vitu kama hivyo, vimeharibu utaratibu mzima wa mwili wake, na kupelekea kupooza sehemu za viungo

vyake.
 

Abdallahking

JF-Expert Member
Mar 19, 2018
1,989
2,000
SEHEMU YA 47

Ni muhimu, tunapokabiliana na watu wenye matatizo kama hayo iwe ni matatizo ya moyo, shinikizo la damu, sukari, au vidonda vya tumbo,

tuwe na hekima ya kuongea nao, tujaribu kufuata masharti ya dakitari, na tusipuuze, maana tunaweza kuja kujuta wakati tumeshaharibu.


‘Mnaweza kwenda kumuona mgonjwa, yupo katika hali nzuri tu, ila kwa tahadhari, msimuongeleshe sana, au kumuuliza maswali ya

kumfanya afikirie sana, na mengine bado tunayafanyia kazi, bado yupo kwenye uchunguzi, ....kwa ujumla hali yake inaendelea vyema...’

Tuendelee na kisa chetu…..

**************


Nilisimama nikiwa siamini,…au docta alikuwa ananidanganya,….nikatulia, nikawa namuangalia mume wangu, ambaye kwasasa uso niliouona

awali ukitabasamu sasa umekuwa hauna nuru tena, uso ukawa kwenye kukunjamana kwa maumivu au hasira.

Unajua wakati nafungua mlango nilikuwa nimepanga kumuuliza maswali yaliyokuwa yakiniumiza akilini, na nilipomkuta kakaa kitandani,

nikafurahia kuwa sasa nitaweza kupata majibu ya hayo maswali, ...

‘Swali la kwanza nilitaka nimuulize, je ni kweli kuwa ana mahusiano yoyote na mwanamke mwingine zaidi yangu mimi mke wake, jibu liwe

ndio au hapana, hakuna maelezo, sitaki nimchoshe..

‘Swali la pili je ana mtoto nje ya ndoa ...jibu ni ndio au hapana.....’ na kama majibu ya maswali hayo mawili yatakuwa ni ndio....basi hakuna

jinsi, akipona tu, ndoa imekwisha, kila mtu ashike mipango yake, mkataba wangu na yeye basi, ...niliwazia hilo nikiwa na dhamira ya dhati.

Lakini nilijipa moyo kuwa majibu yake yatakuwa hapana, kwani mume wangu hana tabia mbaya, hawezi kunisaliti,….

Lakini kabla ya maamuzi ya kuvunja ndoa, kwanza awe amepona kabisa, pili, ni lazima nimfahamu huyo mwanamke shetai ni nani,…ni

lazima nimfahamu huyo mwanamke ili abebe dhamana yake, ni lazima nimfunze adabu, mbele ya.....’

Na nilipofika hapo nikawa nimeshafungua mlango, na ndio hapo nikajijuta namuangalia mume wangu akiwa kakaa kitandani.

******************

‘Mume wangu umepona…’nikasema nikiwa bado nimesimama siamini. Mume wangu alikuwa kakaa, lakini mikono miwili huku na huku

imeshikilia kitanda, alikuwa kama anajilazimisha kukaa sawa…nilihisi mikono yake ikitetemeka.

Ghafla , nilipotoa kauli hiyo mume wangu akadondokea kitandani, na kilichofuata hapo ikawa heka heka, maana yule mtu aliyekuwa kakaa,

kwa shida, maana ilijionyesha kuwa alikaa vile kwa kujilazimisha, kwa jinsi nilivyomuona,.. sasa anatikiswa na bora alidondokea kitandani

miguu imening’inia , akawa sasa anatikisika, anatikiswa mwili mnzima.

Hapo sasa nikachanganyikiwa kwa haraka nikaanza kuita madocta, kuomba msaada, na haikupita muda, madocta wakaja, na nikaambiwa

nitoke humo ndani haraka…nikawa siwezi hata kuinua mguu, na kwa muda huo docta rafiki alishakuja, akanishika mkono, akawa sasa

ananikokota, kunitoa nje ya kile chumba.

‘Umefanya nini sasa…?’ akaniuliza docta kwa ukali

‘Mimi sijui, sijafanya kitu…’nikasema
‘Uliongea nini na yeye, si nilikuambia…usimsemeshe kitu cha kumpa mawazo..’akasema

‘Sikuwahi kuongea naye, nimeingia, akiwa kakaa kitandani, miguu chini..anatizama mlangoni akiwa na tabasamu, cha ajabu aliponiona tu,

akakunja uso…’nikasema

‘Unasema ulimkuta kakaa kitandan, haiwezeani,…?’ akaniuliza sasa akishangaa

‘Ndivyo nilivyomkuta hivyo…’nikasema

‘Mhh…matokeo mazuri hayo,…kama ulimkuta kakaa kitandani, basi tuna matumaini sasa….una uhakika…alikuwa kakaa kukaa..?’ akauliza

‘Ndio docta…..kwani wewe ulimuachaje..?’ nikauliza

‘Nilimuacha kalala, baada ya kumpatia mazoezi, kiukweli mwili wake ulikuwa bado haujawa tayari kukaa wenyewe bila msaada, basi

nilipomaliza kumfanyia usafi, nikamuacha akiwa amelala..’akasema

‘Sasaa, mhh…najiuliza ni kwanini …’nikasema

‘Unajiuliza nini…hiyo ni iashara nzuri, kama hukuongea naye, na ulimkuta amekaa peke yake bila ya msaada wa mtu, ujue ni kumbukumbu

zinarejea na pia mwili umeshaanza kukubaliana, …’akasema

‘Ninachojiuliza mimi ni kwanini alikuwa na furaha kama alitarajia kitu na nilipotokea mimi furaha hiyo ikatoweka…..na hali hiyo ikaja ?’

nikauliza.

‘Hapo ina maana kuwa kumbukumbu zinaanza kurejea, huenda katika kumbukumbu zake, alitarajia kuona kitu alichokuwa akikiwazia…lakini

ikatokea tofauti na matarajio yake…, inaweza ikawa hivyo, au alipokuona alikumbuka jambo, ..linalomsumbua, akashtuka…vyote au jingine

yaweza kuwa hivyo…’akasema

‘Sasa mbona naanza kuogopa….’nikasema

‘Usiogope, hiyo kwetu ni ishara nzuri..kama kaweza kuinua ule mgongo, na miguu peke yake, basi matajio ni mazuri sasa, ni swala la muda

tu…’akasema.

‘Sasa alitarajia nini, au kuna kitu gani ananiogopea mimi, au ndio keshajenga chuki na mimi kabisa, au nikuulize wewe ulisema uliwahi

kuongea na yeye,, si ulisema mliwahi kuongea naye..?’nikauliza.
‘Sikiliza, …usipende kujitwika mzigo kabla haujatua kichwani mwako, utachoka kabla huo mzigo haujatua kichwani, umenielewa, …mume

wako hapo alipo anapambana na mitihani mingi, hatujui kilichosababisha hayo yote ni nini..’akasema

‘Sasa tutamsaidiaje..?’ nikauliza

‘Cha kumsaidia ni kuhakikisha ukija una hali ya kumpa moyo,..usiongee lolote la kumuumiza kichwa, na nahisi kuna kitu anakitegemea au

mtu anapenda aje aonane naye, nahisi ndio maana ulipotokea wewe tabasamu likapotea…’akasema

‘Ni nani sasa huyo anayetaka kuonana naye…?’ nikauliza

‘Hapo mimi na wewe hatujui..tunawazia hivyo tu, lakin wewe ni mke wake, unahitajika kufika, kwasababu kutokufika kwako, kunaweza

kumfanya afikirie vibaya zaidi, cha muhimu nikugundua ni kitu gani anakihitajia kwa sasa…’akasema

‘Nani ataligundua hilo…?’ nikauliza

‘Mimi nitagundua anahitajia nini, usijali…’akasema

**********
Basi siku ile ilipita, nikawa nafika, namkuta kalala, haongei,..nikimsemesha ahasemi neno, ikawa sasa mimi sina raha…hata rafiki yake,
 

Abdallahking

JF-Expert Member
Mar 19, 2018
1,989
2,000
SEHEMU YA 48

yaani docta akaniambia hali ya mume wangu imekuwa tofauti na matarajiao yao.

Siku moja, nikafika hospitalini, nilimkuta mume wangu kalala tu, kaangalia juu, kama kawaida yake, nikamsaidia kumgeuza geuza japokuwa

alishafanyiwa mazoezi

Sasa nikamgeuza aniangalia, nilitaka kujua kama ananifahamu mimi, akawa ananiangalia tu, kama mtu mgeni kwake kabisa, moyoni

nikaanza kuingiwa na wasiwasi, nikihisi vibaya, mbona huyu mtu kawa hivi, ni kama mwili mtu....

Ghafla sasa nikaona hisia za uhai kwenye macho yake, nilimuona akigeuza mboni za macho yake, na mara machoni niliona machozi

yakimtoka...nikasogeza mono na kuyafuta machozi yake..nikawa najiuliza ni kwanini machozi hayo yanamtoka, anahisi maumivu au kuna

nini, .nikatulia, na hapo huruma, woga, wasiwasi na kukata tamaa, vikanitawala, ...

‘Mume wangu mbona upo hivyo, niambie kinakusumbua nini jamani..?’ nikauliza

Nilichoona ni machozi yakiendelea kumtoka kwenye macho yote mawili na mimi nikawa nakazana kumfuta hayo machozi;

‘Mume wangu unalia nini, niambie anagalau na mimi nijue, ..mimi ni mke wako, unavyokuwa hivyo mimi naumia sana, niambie kitu ili niwe na

amani moyoni, unalia nini, nimekukosea nini…?’ nikauliza

Mara mume wangu akawa anahangaika kupanua mdomo, unakuwa kama unatetemeka, kuashiria anataka kuongea jambo;

‘Kama huwezi basi usijilazimishe, ila ujue mimi mke wako nakupenda sana…’nikasema na hapo macho yakameta meta, kuashiria uhai, na

hali ya kutikisika tikisika kichwa, nikaogopa kuwa huenda ile hali iliyowahi kutokea inaweza kutokea tena, lakini haikuwa hivyo, mara

akasema;

‘Mke -wangu,…m-ke..w-w-wwngu..’akasema

‘Mimi hapa mume wangu, ..’nikasema

‘Ni-ni-samehe…na-na- na-kuomba ni-ni-s-s-samehe…’akasema

‘Mume wangu hujanitendea ubaya, hata hivyo usiwe na wasiwasi, sina tatizo na wewe…’nikasema

‘Ni-ni-ni…..me-me-ku-ku-kosea….’akasema

‘Nimekusamahe mume wangu japokuwa sijui …’nikasema

‘Yah---ohhhhh……’hapo akavuta pumzi halafu akatulia kwa muda, macho yapo wazi nayaona, na…machozi hayatoki tena…’halafu nikaona

kichwa inatikisika, ilichukua dakika chache kikatulia, ikaanza kwikwi….hapo ikabidi niwaite madocta…

Nikaambiwa nitoke, nikatoke pale na mimi machozi yakaanza kunitoka, nahisi huzuni, namuonea huruma mume wangu anavyopambana na

hiyo hali na siwezi kumsaidia ..

Nilikaa nje kwa muda, mara docta akaniita,…nikaingia, na docta akasema

‘Haya mwambie mke wako unachotaka kumuambia…’akasema docta

‘Mke wangu, so-so-sogea….’akasema na mimi nikasogea na kukaa kitandani karibu yake.

‘Ni-ni-sa-mehe..m-m-mke wangu…ha-ha-ya yo-yo-te ya-ya-na-na-natokea ku-ku-ku-toka-ka-kana na dh-dh-dhambi zangu, ni-n-nisamehe sa-

ss-sana...’akasema

‘Dhambi gani mume wangu...’nikasema na safari hii nikawa nimeshusha sauti na kuongea kiupole

‘Wewe kubali kuwa umeshamsamehe, na itoke moyoni…’akasema docta

‘Nimekusamehe mume wangu uwe na amani, upone, nakuhitajia sana nyumbani..’nikasema, na nilijikuta pale siwezi kujizuia, machozi

yakaanza kunitoka, na nilibakia vile mpaka nikahisi mtu akinishika begani sikutaka kugeuka kumwangala ni nani nikasema;

‘Mume wangu ana tatizo gani..mbona kawa hivi tena jamani...?’nikauliza huku nimeshika kichwa.

‘Ni tatizo la muda mfupi, litakwisha na ataweza kutembea cha muhimu ni kufuata masharti ya dakitari, dakitari bingwa wa mambo hayo

keshamwangalia , kasema hilo litakwisha, hali iankwenda vyema kabisa, kuna kitu anakihitajia, labda ilikuwa ni hiyo kukuomba

msamaha,lakini bado, kuna kitu anakihitajia....’akasema.

Niligeuka kumwangalia huyo aliyeongea haya, alikuwa docta rafiki wa mume wangu, na kwa muda huo nilitamani nimkumbatie, ili

nisianguke, maana miguu ilikuwa haina nguvu, nilihitajia mtu wa kunifariji na kusema mume wangu atapona tu, hakuna tatizo.....

Nikageuka kumwangalia mume wangu, na nilimuona akiwa sasa akiwa kaangalia juu, hatikisiki , alikuwa kama gogo tu, alikuwa kama mwili

wa marehemu, lakini unachojua kuwa yupo hai ni machoni, akiyapepesa na kuyageza huku na kule, na sasa machozi yanamtiririka.

Pale...moyoni nikaingiwa na huruma, woga ukachukua nafasi nikiwazia mbali zaidi, kuwa sasa mume sina tena, kauli hizi ni za kuniaga,

....na ile hali ya hasira chuki ..vikayeyuka...sasa namkabili mungu anisamehe, kama nina kinyongo na mume wangu mimi sina tena amponye

mume wangu tu.

‘Ndio maana nilikuwa nakuzuia sana, usiingie bila ya mimi….’akasema docta.

‘Hali kama hii hata ingelikuwa ni wewe…’nikasema na mara sauti ya mume wangu ikasema

‘Mke wa-wa-ngu, ...usiondoke kabla hujanisamehe, na-na-na taka nikifa niwe huru, na-jua ni-meku-kosea sana, nisa-mehe mke wangu...na

baba-ya-ko, ani-sa-sa-mehe..na-na deni…na..na..mto-ooooh..’hapo hakuweza kumalizia, akawa kimia

Milio ya mashine ya hatari ikaanza kulia, hapo ikawa heka heka kwa madocta na mimi nikatolewa nje kwa haraka…hapo ndio nikajua sina

mume tena,…..nililia, na kulia….

Sitaweza kuisahau siku hiyo…

NB: naishia hapa kwa leo


WAZO LA LEO: Katika maisha yetu, katika kuhangaika kwetu, maana yabidi tuhangaike, tutafute riziki za halali,..yabidi tupambane na

mitihani ya maisha magumu, kuna wenye maradhi ,madeni nk..yote ndiyo maisha yetu, vyovyote iwavyo, hata kama tupo kwenye raha,

hatuna shida, tunakula na kusaza…bado sisi ni waja wa mola, hatuna jinsi, tupo kwa rehema zake,…tuyakumbuke mauti, kuwa ipo siku

yatatukuta, hata tukiwa nani,…muhimu kwetu, ni kujiuliza je tumejiandaaje na siku hiyo, siku ambayo roho itauwacha mwili,…
 

Abdallahking

JF-Expert Member
Mar 19, 2018
1,989
2,000
SEHEMU YA 49


Sikutaka kuondoka kabisa siku hiyo hapo hospitalini, lakini baada ya ushawishi mkubwa wa madocta ilibidi niondoke, maana walisema hata

nikikaa hawataniruhusu nionane naye kwani hawajui ni kwanini ilitokea hivyo baada ya kuniona mimi.

Basi baada ya kurejea nyumbani, nikapiga simu kwa rafiki yangu, kabla hata sijamuuliza yeye akatangulia kusema kuwa ile kazi

hajaikamilika, kuna vitu bado hajaweza kuvipata kwahiyo nimpe muda zaidi, na mimi sikuwa na cha kumwambia maana mawazo yangu kwa

wakati huo yalikuwa mume wangu.

‘Mume wangu hali yake sio nzuri…kwahiyo sawa,…kama wahitaji muda, ..sijui wataka mpaka lini,… ila jitahidi, nakupa siku moja ya ziada,

ufanye haraka iwezekanavyo, maana huo uchunguzi ni moja ya mambo ya kumsaidia yeye mgonjwa..’nikasema

‘Kwani kazidiwa tena zaidi, si ndio hiyo hali ya kutafuta kumbukumbu au…?’ akauliza

‘Hivyo hivyo tu, unasema kumbukumbu, ulipata wapi taarifa hizo…?’nikasema na kuuliza

‘Atapona tu…ilimradi yupo na madakitari…’akasema bila kujibu swali langu, na sikutaka kumuuliza tena.

‘Ndio hivyo, ila kuna kitu kinamsumbua, mimi sijajua anasumbuliwa na nini hasa, hata madocta hawajui tatizo ni nini hasa…walitarajia mimi

nitaweza kusaidia..hata sijui nifanye nini,…, ndio maana nilitaka hiyo kazi uimalize kwa haraka iwezekanavyo, unielewe hapo rafiki yangu ni

muhimu sana kwangu na kwa mume wangu, nashindwa mimi nifanye nini sasa…’nikasema

‘Sawa nimekuelewa,…ila kiushauri wangu, hata ikikamilika hii taarifa ni bora ukasubiria apone kabisa, kuna mambo mengi, yatamsumbua

kichwa ukianza kumhoji ni kwanini, ni kwanini..unanielewa hapo lakini.., hasa ya kazini kwake, na mengine ni wewe na yeye, hakuna zaidi

ya hapo, mengine ndio haya sijapata uhakika nayo…’akasema

‘Mimi nikiipata hiyo taarifa nitajua kipi ni kipi cha kuongea naye..je huyo mzazi aliyekuwa akimfuatilia umeweza kumtambua ni nani, maana

siku hiyo ya ajali nasikia aliondoka kwenye kikao, akiaga kwenda kumuona mzazi, …sasa ni nani..?’ nikamuuliza

‘Mhh, nani kuambia hayo..ok,…hapo kuna utata, ndio kuna mzazi alijifungua siku hiyo, siku ambayo na mimi nilijifungua, lakini sio

mfanyakazi mwenzao, sasa hakuna uhakika wa moja kwa moja kuwa ndio yeye,..unaona hapo, na ni kweli, kuna kipindi cha nyumba mume

wako alikuwa karbu na huyo mama,…sasa huwezi kuchukulia hilo kama kigezo, ndio maaana nasema kuna mambo kidogo hayajakamilika

hapo

‘ Ni nani huyo…Je huyo mzazi anaweza kuwa mpenzi wa mume wangu , ndio huyo shetani ninayemtafuta mimi au, nataka majibu hayo

haraka iwezekanavyo, umenisikia, ..?’ nikauliza kwa ukali kidogo

‘Bado sijaweza kupata uhakika, maana kama nilivyosema sio mfanyakazi mwenzao…lakini sasa, huyo mwanamke ana mchumba wake,…

nilitaka...niende kwake,..lakini nimesikia kasafiri jana….ooh, hebu subiria kidogo,..’akasema na kutuli baadae akasema

‘Kuna kitu nafuatilia, ….ujumbe uliingia, lakini sio muhimu,…sasa ni hivi subiria kidogo,leo nahis nitafikia sehemu, nitakuambia …mambo

mengine naogopa kutumia watu, kwasababu za kiusalma na siri zetu, unanielewa hapo…’akasema

‘Ok….sawa, nimekuelewa,…mimi nakusubiria wewe…maana leo nilitakiwa kuonana na baba, kuna mambo ya kuongea naye, muhimu sana..na

nilipomueleza hayo mabadiliko ya afya ya mume wangu, akaona tuahirishe hicho kikao, ..na kasema kuna mambo zaidi kayagundua, sasa

sijui ni mambo gani…’akasema

‘Kagundua nini, hakusema ni mambo gani hayo, mmh…?’ akauliza

‘Mimi kwa hivi sasa akili haipo sawa, siwezi kujua, hakusema….labda yanaweza kuwa ya kazini kwa mume wangu au hata sijui, nahisi

anaona namficha jambo, kawa mkali sana..’nikasema.

‘Unajua baba yako nilionana naye, bahati nzuri sikuwa na mtoto, na kukutana kwetu ilikuwa ni bahati mbaya tu, sio kwa kupanga ilitokea tu,

nikiwa nafuatilia jambo fulani nikiwa na haraka kurudi nyumbani, na hakutaka hata kunisalimia, akakimbilia kuniuliza maswali ….’akasema

‘Maswali gani…?’ nikauliza

‘Kwanza alisema kwanini nimeamua kuzaa bila kuolewa,…nikamwambia ni bahati mbaya tu,…akaniuliza haya baba wa mtoto ni nani,

..nikamwambia hilo ni siri yangu,..akaniuliza mambo mengi-mengu tu mfululizo…, nahisi anajua kitu….sijui kajulia wapi mambo mengi ambayo

hata sikutagemea kuwa atayafahamu,…rafiki yangu…, tusipokuwa makini, baba yako anaweza kuchukua hatua ambayo hukutarajia, maana

keshafahamu kila kitu…’akasema

‘Ndio maana nilikuambia ufanye juhudu za haraka, ili uwahi kuziba sehemu zote nyeti, lakini wewe ukalichukulia taratibu, sijui ulijiamini nini,

ujue mimi nina mipaka yangu, na kama kuwajibika kama baya likitokea, sawa, nitawajibika kama mtendaji, lakini huyo ni baba yangu hawezi

kunitupa moja kwa moja lakini nyie je nitawasaidiaje, na ina maana juhudi yangu yote ndio ifike hivyo, inaniumiza sana, kama watu

niliowategemea, na lakini sawa....’nikasema

‘Nimejitahidi nilivyoweza, nikaziba sehemu nyingi tu…lakini baba yako kama umjuavyo anaweza kufika kokote bila vikwazo, hata

hivyo,..hawajafanikiwa kuupata uhakika wa baadhi ya mambo, ndio maana aliniuliza maswali mengi, kuashiria kuwa hana uhakika,…unajua

…mimi nimeshaamua, liwalo na liwe, sasa nitafanyaje .…’akasema

‘Una maana kusema hivyo, liwalo na liwe…?’ nikauliza

‘Sasa rafiki yangu yaliyotendeka, yameshatendeka, utafanyaje sasa hapo…eeh, hebu niambie, wakati mwingine tuangalie mbele, tukirudi

kinyume nyume kwa kujiuliza, tutajikuta tupo kwenye lawama sote …na lawama hizo zinaweza kutufikisha kubaya, kama tutajiangalai nafsi

zetu tu…na kumbe ilikuwa ni dhamira nzuri tu..lakini sawa, mimi nitakukamilishai huo uchunguzi na uamuzi utakuwa mikononi

mwako…’akasema

‘Nataka kufahamu tu, je wao wameshagundua lolote kuhusu baba wa mtoto, maana hilo linaweza kuleta picha mbaya

kwangu,..kama..lisemwalo lipo sijui nitauweka wapi uso wangu, lakini kama sio kweli..nataka kumkosha mume wangu..awe huru na shutuma

hizi..’nikasema

‘Kwani …mmh, mume wako si yupo, waache apone atasema mwenyewe, kwanini ulaumiwe wewe…’akasema

‘Baba anasema kagundua mambo mengi ambayo kama angelifuatlia awali yasingelitokea na hili limempa fundisho…sasa mimi sipendi hiyo

hali ya kuingilia mambo ya mume wangu, …ndio maana nilitaka ukweli kutoka kwako…na hilo la baba wa mtoto wako, lisiwe kama

wasemavyo, itakuwa heri sana kwangu, na kwa mume wangu, vinginevyo, sijui baba atachukua hatua gani…’nikasema

‘Unajua hizo shuku shuku zao kuhusu mtoto kama nimezaa na nani…nimemwambia baba yako wazi wazi hayo ni maisha yangu, hayawezi

kuingiliana na biashara zake, akifanya hivyo anakosea sana..kwani vyovyote iwavyo hakuna nitakayemwambia baba wa mtoto wangu, na

sina lawama na mtu, kuwa labda nitambebesha yoyote majukumu ya ulezi, kwahiyo sipendi watu kuniuliza-uliza hayo maswali …’akasema

‘Sawa , kwa baba unaweza kuongea hivyo, lakini kila kauli yako anaichukulia kwa uzito wake, maana naye sasa hivi keshasikia mengi, …

mimi nakupa angalizo tu, uwe makini sana ukiongea na baba, usimchukulie juu-juu, ana lengo lake, unaweza ukajikuta kubaya sana, na

anajua ni nini anachokifanya, hawezi kuingilia mambo ya watu bila sababu maalumu…’nikasema

‘Namafahamu sana…najua ni vipi niongee naye, na wapi ikibidi na mimi niwe mkali, maana na mimi nina haki zangu,kiukweli ndio baba yako

ni mkali, lakini mimi siwezi kumuogopa tu, ..ninachoogopa ni hatua zake, kuwa labda anaweza kuchukua hatua mbaya zikaumiza wengine

bila kujali, na visingizio vije kwangu, hapana kama ni langu aniumize mimi mwenyewe….’akasema

‘Baba anachoangalia ni heshima yake, pili bishara zake, maana heshima ndio inamletea wateja na biashara, na mambo ya kisiasa, hataki

kashfa mbaya …Na hilo litakuwa ndio ajenda kubwa kwenye hicho kikao, watakuwepo wakurugenzi wote wa vitega uchumi ambavyo ana

hisa navyo,…kwahiyo sio kikao kidogo, ni kikao cha maamuzi,..sasa haya mambo ni mengi na yanatokea kipindi hiki, na wewe ulikuwa

msaada wangu mkubwa, sijui, umekuwaje sasa…’nikasema

‘Niliponana na baba yako, alikuwa na mdogo wa mume wako…’akasema

‘Oh yupo yule aliyesafiri au huyu mwingine….kwahiyo wameshaongea, huenda kabanwa na kusema ukweli wote au…?’ nikauliza

‘Ndio, lakini huyo mtu nilishaongea naye kabla na kumuweka sawa, sizani kama anaweza kufungua bakuli lake, nina mambo mengi yake

mabaya ninayoyafahamu, anajua kabisa akinisaliti nitamuumbua kwa mkewe.., kaahidi hatasema loloye baya dhidi yangu, usiwe na

wasiwasi na huyo mtu….’akasema

‘Una uhakika hataweza kusema ukweli, maana nilipanga kuonana na mke wake…?’ nikauliza

‘Hawezi kusema chochote, …mambo yangu yatabakia kuwa yangu, nina uhakika, hilo litabakia sirini kwangu, hakuna nitayakemuambia

nimeshaamua hivyo, mpaka hapo muda muafaka ukifika, , kama ikibid kusema, nitasema…, lakini sizani kama kuna mtu atafahamu siri

hiyo,..na unasema unataka kuongea na mke wake unataka kuongea naye nini, …usije ukaharibu…’akasema

‘Hapana…kuna mambo yangu mengine na huyo mwanamke..mambo ya akina mama, unajua nimewekeza huko pia, kwa akina mama, sasa

yeye ni mmoja wa wahusika wakuu, na nilitaka nijue yeye anasemaje kuhusu haya yanayoendelea hasa kuhusu huyo mtoto wako,je

hamshuku mumewe …’nikasema
 

Abdallahking

JF-Expert Member
Mar 19, 2018
1,989
2,000
SEHEMU YA 50


‘Hata sijui….lakini kwangu nimehakikisha kila kitu kipo sawa, …mimi nakushauri wewe hangaika na mume wako, haya mengine yaache kama

yalivyo,..hiyo taarifa itakusaidia kidogo tu…sizani kama ina lolote jipya…’akasema

‘Unajua nilipokuwa naongea na docta, docta alisema mume wangu anaonekana kama anataka kuonana na wewe…?’ nikasema, nikahis

kama kashtuka na akahema kidogo na kusema

‘Kuonan na mimi, aliongea hivyo au…?’ akauliza

‘Docta, rafiki wa mume wangu ndiye anahisi hivyo…’nikasema

‘Mhh, kuna nini kilitokea mpaka ahisi hivyo, lakini eeh, hata hivyo ni wajibu wangu kumuona au sio , nyie ni kama ndugu zangu, tumeishi

nanyi, tumeleleana, shemeji namuona kama ndugu yangu pia, japo,…haya yanayotokea sasa yanaleta kigugumizi, ila …sijui nitafikaje na

mtoto,. Si unajua tena, …’akasema

‘Wewe fanya mpango uje uonane na yeye, kama itasaidia,..huyo mtoto isiwe kisingizio, huyo unaweza kuja naye…maana kutokana na docta

kuna muda akiwa anaweweseka, alitaja mtoto, kama ingelikuwa ni watoto wake, angelisema watoto, lakini katamka ‘mtoto’…hizi ni hisia

zinajengeka, na kumfanya docta ahisi kitu…’nikasema

‘Mtoto, katamka hivyo mtoto, mtoto wa nini, hapana, labda kamsikia vibaya, na hiyo sio sababu ya kuhisi mtoto wangu…sema kwa vile kuna

kitu kinatakiwa hapo, lakini hilo lisikusumbue kichwa, ni langu, najua jinsi gani ya kupambana nalo…’akasema

‘Docta analifuatilia hilo kwa karibu na anajaribu kuwa karibu na mume wangu, kusikia kama atapata chochote kutoka kwake…je hamjawahi

kuonana na docta ukiwa na mtoto wako…?’ nikamuuliza

‘Hajawahi, labda, ..sina uhakia maana huyu ndugu yangu anayekaa na mtoto angeliniambia…kama aliwahi kuja nikiwa sipo, na mimi

sijamuacha mtoto wangu kwa muda mrefu na huyo msaidizi wangu…’akasema.

‘Unajua kila hatua, naanza kuingiwa na mashaka..anyway, mimi nina imani hujanificha kitu,..sijui, maana, umeshasema huwezi kumuambia

mtu kuhusu baba wa huyo mtoto wako.., ikiwemo mimi, na kauli hiyo inanifanya nianza kuwaza mengi, ni kwanini hadi mimi unifiche,

najiuliza sana…’nikasema

‘Ndio maana naona bora iwe hivyo,…kama mwenyewe umeshaanza kubadili imani yako kwangu, unaanza kupinga hata kauli zako, basi hata

mimi naingiwa na mashaka, je mimi rafiki yako naweza kufanya jambo kinyume na kauli zako, aah, kwa hali hiyo, hata safari, sijui

itakuwaje….na huenda nikaondoka haraka iwezekanavyo…’akasema

‘Huwezi kuondoka kabla sijaufahamu ukweli. Ujue hiyo safari nimeidhamini mimi mwenyewe, sasa usije kuharibu kila kitu…Hilo la kuujua

ukweli, nitalijua tu, nimeahidi hivyo…, umesikia, kupitia kwako au kwa njia nyingine, nitamfahamu baba wa huyo mtoto, umesikia, na nina

maana yangu kufanya hivyo…’nikasema.

‘Haah , sawa…lakini ….hebu kidogo…’ na simu ikakatika, nilishtuka kwa kitendo hicho cha kukata simu kabla sijamalizana naye…, sio kawaida

yake kukata simu, kihivyo

Kwa vile nilikuwa na haraka, sikutaka kumpigia tena simu, …lakini kitendo icho kilinikwanza kweli kweli….

***********

Nilifika hospitalini, na nilihitajika kuonana na docta kwanza kama naruhusiwa kuonana na mume wangu.

‘Sawa unaweza kuonana naye, ila docta, jirani yako, yupo huko anaongea naye… NA kumpatia mazoezi kuna huduma nyingine tunataka

kumfanyia kidogo huenda ikasaidia..’akasema

‘Kwahiyo sasa anaongea vizuri…?’ nikauliza

‘Ndio ila, kumbukumbu hazijakaa vyema kabisa…kuna muda anajichanganya, na siku ya leo amekuwa akikuulizia wewe, ni mnyonge sana,

nahisi wewe utaweza kumsaidia, jaribu sana kuwa naye karibu…’akasema

‘Haya ngoja nikaonane naye, kwahiyo unahisi ana tatizo jingine kubwa…’nikauliza nikiwa na hamasa ya kwenda kuonana na mume wangu.

‘Hakuna zaidi ni hilo, …mengine hatuwezi kuyafahamu kwa sasa, maana hatua kwa hatua anaanza kuimarika, usiwe na wasiwasi

kabisa…’akasema

Basi nikaondoka na kuelelea huko alipolazwa mgonjwa, nilipoingia nilimkuta docta akimfanyia mume wangu mazoezi, nilishangaa kuona

hata ile kukaa kama kwanza hawezi, …sikutaka kuwashtua kwanza nikatulia kuwaangalia.

‘Sasa naona upo tayari,…unajua ni muhimu ukajitahidi mwenyewe ungelifanya kama ulivyojitahid kipindi kile ungelipona haraka tu…’akasema

docta

‘Hata sijui ilikuwaje, kwani nilijitahidi vipi…?’ akaliza suti yake ilikuwa ya kinyonge ya mgonjwa aliyekata tamaa.

‘Uliweza kukaa mwenyewe kitandani…’akasema

‘Mimi, nilikaa mwenyewe, ….sikumbuki. maana hata mwili siuhisi ni kama vile sina mwili kabisa….’akasema

‘Utakumbuka tu kidogo kidogo,…’akasema docta

‘Hivi unasema kweli ..kuwa Mke wangu aliwahi kuja kuniona, mbona mimi sikumbuki kumuona…’akasema

‘Mbona kila siku anakuja kukuona…’akasema docta

‘Mmhh, kweli nahisi hataki kuja kuniona kwa hayo niliyomtendea, nimemkosea sana, sijui kwanini, nahisi mimi ni mtu mbaya sana, na huyo

rafiki yake mhh…’akasema hapo akatulia hakuendeleza neno

‘Usijali,..kosa ni kosa, na ukikosa, ukatubu basi kosa linafutika, ila ukirudia kosa, ujue wewe ni mkosaji…’docta akasema

‘Nimerudia kosa mara nyingi sana..ndio maana nipo hivi…sijui atanisamehe kabla hajchelewa… unahisi atanisamehe, nataka nafsi yangu iwe

huru, nina imani akinisamehe, basi, nitapumzika kwa amani, atakuja leo…?’ akauliza

‘Atakusamehe, kwani hujafanya kosa kubwa la yeye kushindwa kukusamehe, makosa ni kawaida ya mwanadamu au sio…’akasema docta

‘Wewe hujui tu…nahisi moyo mwake ananichukia sana, tena sana, sijui kwanini ilitokea hivyo, lakini, hata sijui, nilifanya nini…’akasema

‘Kwani anafahamu kosa ulilomtendea, ni kosa gani kubwa hivyo..?’ akaulizwa

‘Ndio maana hataki kuja kuniona, nahisi keshafahamu, ni kosa kubwa sana, tena sana, lakini sikumbuki, tatizo, nahisi nimekosa, lakini haaa,

mbona sikumbuki kitu…’akasema

‘Kosa gani…lakini utakumbuka tu usijali…si hukumbuki, basi ni kosa dogo tu, au sio..au unalikumbuka, ni kosa gani…?’ akauliza na hapo

akageuka, wakaniona, na kimia kikatawala.

Mume wangu aliponiona akaonekana kutokuwa na raha, akawa katulia, nikamsalimia, akaitikia kwa unyonge sana, nikamuuliza

anaendeleaje akasema sasa hajambo.

‘Sasa ni kujitahidi kula na mazoezi, na nitajitahid kuja kukufanyisha mazoezi mwenyewe, maana walinikataza awali, sasa najua upo tayari,

au sio..?’ nikamuuliza

‘Sawa, lakini ..ulishanisamehe…’akasema hivyo

‘Kukusamehe, mume wangu usiwe na wasiwasi mimi ni mke wako, tunakoseana sana, au sio, kwani wewe si ulishasamehe au

sio..’nikasema

‘Lakini wewe hujanikosea kitu mke wangu, wewe ni mke mwema, nimeliona hilo, wewe ni mwema,…’akasema

‘Mh, mume wangu nimeshakusamehe kabisa…’nikasema, nikimtupia jicho docta na docta akaashiria kukubaliana na kauli yangu japokuwa

sikufahamu ni kosa gani analolisemea mume wangu.

‘Najua hujanisamehe, niona nafsi yako…unanichukia sana, nakuomba uondoke tu, kama hutaki kunisamehe…’akasema na kunifanya

nishtuke na kugeuka kumuangalia rafiki yake.

Docta..alipoona vile..kwanza alitulia, kama ananisubiria mimi niseme neno la kumsihi au kitu kama hicho, na aliponiona nipo kimiya yeye

akamsogelea mume wangu pale alipolala, akamwiinamia na akawa anamsemesha sauti ya chini-chini

‘Rafiki yangu nimeshakuambia, ukitaka usipone haraka, uendelee kujitesa na hayo mawazo yako, mke wako hana kinyongo na wewe

kabisa,…. anafahamu kuwa kila binadamu anakosea, na kutenda kosa sio kosa, bali kurejea kosa, wewe kama uliteleza, uliteleza tu kama

binadamu wengine,..na umeshafahamu kosa lako, umetubu, au sio ...hiyo inatosha kabisa..mimi nimeshaongea na mke wako, yeye kasema

ameshakusamehe.....’akasema.

‘Wewe huelewi tu, .....ninachotaka ni kauli ya mke wangu kuwa amekubali kunisamehe, kutoka moyoni mwake, nafsi yake bado

haijanisamehe, naiona kabisa, usimsemee…’akasema

‘Nafsi yake umeuonaje wewe…’akasema docta

‘Naiona,…naiona, naiona. Naiona…’akawa anaongea hivyo mfulululiza mpaka docta akamgusa begani ndio akanyamyaza

‘Mimi najua tu, mimi ni mtu wa kuangamia tu, maana hajanisamehe, ninajua mimi sio mtu kuishi tena, nimepewa muda wa toba, kabla sijafa,

niwe nimesamahewa, na mke wangu, lakini mke wangu, hajanisamehe, anaongea tu mdomoni, yeye na baba yake ni kitu kimoja, wanataka

niangamie tu,, ....’akasema na kauli hiyo ikanishitua, nikajikuta nikisema.

‘Wewe mume wangu unakazania nikusamehe, nikusamehe, kwa kosa gani,mume wangu mbona hujanikosea kitu, kama ni yale ya nyumba

nimeshakusamehe, lakini sijui kama una makosa mengine,labda uniambia makosa gani hayo,na hilo la baba yangu linatoka wapi,,,.?’

nikauliza na rafiki yake akasema.

‘Tulishaongea hilo na mke wako, kwake sio kosa kubwa sana, ni mambo yanatokea, hasa kwa wanadamu, baba yake alikuja hapa akasema

yeye yupo tayari kuangalia unapona haraka, na kama kuna lolote limekwama aambiwe, sasa unataka nini tena..’akasema docta

‘Baba yake au mwingine….hahaha, na akisikia hayo madhambi, si ndio, atanifukuza kabisa,…najua keshayafahamu ila anasubiria kuwa

nitapona ili aje kuniumbua, hatawahi kabisa, ila mke wangu, nisamahe jamani, naangamia mwenzako…’akasema kwa sauti ya uchungu kama

anataka kulia.

‘Kiukweli pale nilitaka kuongea kwa ghadhabu, maana sijui ni kosa gani, na nimetamka kuwa nimeshamsamehe bado ananisihi, …docta

akaingilia kati na kusema

‘Mkeo anakupenda sana, muda wote yupo na wewe, kaacha kila kitu kwa ajili yako, sasa unataka nini tena hapo, keshakuelewa, muhimi ni

wewe kupona hayo ya kufikiria kufa , kila mtu atakufa hata akiwa mnzima au sio....’akasema docta na kunigeuka akaniambia kwa sauti chini

chini

‘Toa kauli yenye udhabito kuwa umemsamehe, umeshafahamu kila kitu,..tusipoteze muda, kwani hali yake, itaboreka haraka akiwa na moyo

wa matumaini,..vinginevyo,…huyu mtu atachanganyikiwa… ‘akatulia kwani dakitari wawili na nesi waliingia wakiwa na vifaa, vikiwemo vyuma,

nikashangaa hivyo vyuma vya nini tena .

NB: Mambo ndio hayo, msichoke, maana hapo hospitali ndio tutagundua mengi.

WAZO LA LEO:Fadhila , baraka na rhema kutoka kwa mola wetu ni nyingi sana, je tunazikumbuka, je tunamshukuru, au tunasubiria mpaka

tuanza kuwa na hali mbaya ndio tuanze kusema ‘ooh mungu wangu…. tumkumbuke mola wetu tukiwa wazima, tukiwa na uwezo wetu, tukiwa

vijana, ..naye atatukumbuka tukiwa na shida.

Tumuombe mola wetu tuwe na imani hiyo, Aamin.
 

Abdallahking

JF-Expert Member
Mar 19, 2018
1,989
2,000
SEHEMU YA 51


‘Jamani tunaomba nafasi...tunataka kumweka mgonjwa vizuri,…kuna jambo tunatakiwa kumfanyia sasa hivi, na muda umekwisha,…na hata hivyo mgonjwa hakutakiwa kuongea na watu kwa muda mrefu hivyo, docta natumai unakumbuka masharti tuliyokupatia, naona hii inatosha, samahani docta,...’akasema huyo docta, akimgeukia docta mwenzake.

‘Tunataka tufanye kazi yetu samahani…’akasema docta bingwa wa mifupa, akianz kuweka vitu vyake sawa.

‘Hamna shida, tumeshamalizana, .....’akasema docta rafiki, sasa akiniangalia mimi machoni, na kunigusa begani akasema;

‘Toa kauli yako haraka, tuondoke....’akasema na mimi nikageuka kumuangalia mume wangu, na nilivyoona vile vyuma, wanavyotaka kumuwekea mume wangu, huruma, machungu yakanishika,…nilijiuliza moyoni, ni kosa gani alilolifanya mume wangu linalostahiki hayo yote, hapana mungu anisaidie, tu, mungu amsaidie tu mume wangu

Kiukweli pale moyo wangu ukawa mweupe, nikawa sina kinyongo na lolote kwa mume wangu, haraka nikamuinamia mume wangu, na yeye alikuwa akiniangalia kwa macho yaliyojaa huruma, ….kuonyesha kuwa anateseka moyoni na kiwili wili…tukawa tunaangaliana, niliona machoni kwake akianza kutoa machozi,…na mimi nikahisi machozi yangu yakinijia kwa kasi, kabla hayajaanza kutoka nikasema;

‘Mume wangu nimekusamehe, natamka haya kutoka moyoni mwangu, namomba mola mwenyezi akujalia upone, ili tuwe pamoja, sioni dhambi gani kubwa inayostahiki mateso hayo yote, nakupenda sana mume wangu, pambana na haya, uyashinde, ukijua mimi mke wako nipo kwa ajili yako,..na kama kuna mengine tutayamaliza nyumbani, sawa mpenzi mume wangu....nimeshakusamehe...’nikasema na nilipomaliza kusema maneno hayo;

Nikaona tabasamu likijitokeza usoni mwake, ..uso ukapambwa na nuru ya furaha,…akawa kama anataka kuongea kitu lakini hakuweza,mdomo ukawa unatikisika tikisika,,.. na mara akaanza kutikisika hivi,…madocta hawakuwa awali wameliona hilo.

Nikawa najaribu kuwaonyeseha ishara madocta, lakini walikuwa wakiongea na yule mwingine alikuwa akiweka vitu vyake sawa..ile hali ya kutikisika haikuchukua mdua mrefu, mara akafumba macho, ...na muda ule ule, nikasikia milio ile ya hatari ikilia chumba kizima, na wale madakitari wakamsogelea mgonjwa na kutuambia tutoke humo ndani haraka.....

‘Nini tena…’akasema docta wake, na haraka wakaanza kazi ya kumuhudumia, hata vile vyuma viliwekwa pembeni, wakawa sasa wanahangaika kumrejesha , azindukane, maana alishapoteza fahamu.

Mimi kuiona ile hali, kwanza nilibakia mdomo wazi, siamini,..nishikiwa na bumbuwazi, macho yamenitoka , nikawa sina nguvu kabisa miguu haiwezei hata kuinuka,…nikahisi maumivu makali kichwani ….maumiu makali kweli.., na pale pale nikahisi kizungu zungu, na kabla sijadondoka, giza likitanda usoni, na sikukumbuka kitu mpaka pale nilipozindukana nikajikuta nipo kitandani.

*********

Siku mbili nilikuwa kitandani sijiwezi, japokuwa siku nile kama walivyinielezea, nililazwa na kuwekewa maji, yalipoisha, nikawa nimshazindukana, nikauliza kuhusu mume wangu, wakaniambia anahudumiwa, siwezi kumuona.

Niligoma kuondoka nikitaka nimuone mume wangu kama yupo hai au la..sijui walifanya nini, usingizi ukanijia, na nilipoamuka tena nilijikuta nipo nyumbani kwangu, kitandani nimelala mwili ulikuwa hauna nguvu kabisa,

Ilikuwa sasa ni siku ya tatu ndio akaja docta rafiki wa mume wangu kuniangalia ninaendeleaje, nikajitutumua na kutoka, nje, kuonana naye, akasema;

‘Sasa unatia matumaini, naona leo upo safi, siku zote nakuja hata hunitambui vyema, sasa jitahidi hivyo hivyo, ujiimarishe mazoezi, na hali hiyo itakwisha,…’akasema

‘Sawa umekuja nataka kwenda kumuona mume wangu…kama….angalau niuone mwili wake..’nikasema

‘Unasema nini wewe…uuone mwili wake, kwani mume wako amefariki, nan kakudanganya…’akasema

‘Usitake kunificha…’nikasema

‘Unajua kwa hali kama hiyo, nahisi ni vyema tukaongozana ukaenda kumuona wewe mwenyewe....’akasema

‘Docta, usitake kunifanya mimi mtoto mdogo, niliona kwa macho yangu…’nikasema, nikijua wananificha tu.

‘Usijali, tutakwenda kumuona mgonjwa, hajambo mwenzako, leo ni muhimu twenxe ukamuone ili uwe na amani ....’akasema.

‘Ina maana kweli mume wangu yupo hai,..docta, usinifichei…oh, jamani, nimekua mgonjwa zaidi ya mgonjwa, vipi anaendeleaje lakini…, mimi nilijua siku ile ndio naagana naye…’nikasema sasa nikiwa na imani, na nguvu zikaongezeka mwilini kiaina yake

‘Unajua siku ile ilikuwa kizaa zaai, maana ulipotewa na fahamu, ikabidi uhudumiwe wewe kwanza..lakini baada ya kutolewa mle ndani maana kipindi kile ndicho mume wako naye alikuwa kapoteza fahamu, madota wake walikuwa na yeye , iakbdi mimi nipambane na wewe…’akasema.

‘Ahsante mungu wangu, kwahiyo mhh…, mungu mkubwa, mume wangu bado yupo hai…jamani hadi kwenye ndoto nikawa namuota tunaagana, hizi ndoto jamani…’nikasema

‘Hajambo kabisa, anaendelea na matibabu ya kuweka viungo vyake sawa, ile kauli yako ilitokea moyoni kuwa umemsamehe, aliihisi,…kwahiyo ila hali ya kuchanganyikiwa ikaondoka baada ya kuzindukana, akaja mtu mpya, mwenye afya yake, akawa
anaongea vizuri tu…’akasema

‘Hapo sasa umenipa nguvu …sasa naweza kwenda kumuona ila bado mimi naogopa…kwenda kuangaliana naye, unajua tangia mume wangu alazwe, anakuwa kama mgeni kwangu kabisa, sijui kwanini…’nikasema.

‘Usiogope ni lazima upambane na hiyo hali, na yeye pia, …hata hivyo baada ya kuzindukana, hali yake imeimarika sana, ..tuna imani mkikutana naye hakutakuwa na tatizo tena, na huenda akaanza kuongea tena, maana ghafla juzi alikataa kuongea kabisa na watu, hatutajua tatizo ni nini…lakini haya yatakwisha tu tu...’akasema.

‘Alikataa kuongea au ndio kule kuongea kwakwe kwa shida…?’ nikauliza

‘Ile hali ya kuongea kwa shida, ilishamalizika…na akawa anaongea vyema tu…hebu jiandae basi tuondoke, au unakwenda hivyo hivyo ulivyo…?’ akaniuliza

Baada ya kujiandaa, nikaingia kwenye gari la huyo rafiki wa mume wangu, na tukaanza kuongea maswala mengine, kwa muda ule nilitaka ninyamze tu, sikuataka kuongea kabisa, na mara nyingi nilikuwa mtu wa kuitikia tu, lakini aliponiuliza swali hili ikabidi nishtuke na kumjibu;.

‘Rafiki yako alikuaga?’ akaniuliza.

‘Rafiki yangu gani...?’ nikauliza huku nikionyesha mshangao.

‘Usipende kuuliza swali, wakati unafahamu nakuuliza nini, una marafiki wangapi, ..na unafahamu kabisa nikisema rafiki yako nina maana gani’akasema.

‘Kwani kaenda wapi?’ nikamuuliza kwa mshangao.

‘Haah, ina maana, hujui, si kaenda kusoma ulaya, nakumbuka kuna siku uliniambia kitu kama hicho, sasa kaondoka jana usiku ...’akasema.

‘Haiwezekani, hawezi kuondoka bila ya kuniaga, ina maana kaamua kuondoka bila ya kumuona mgonjwa, angalau angesubiria kuona mgonjwa anaendelea vipi, haiwezekani, ..hapana huyo sio rafiki yangu ninayemfahamu mimi ndio kafanya hivyo ili iweje, au unanitania..?’ nikauliza nikiwa siamini kabisa.

‘Ndiye huyo huyo rafiki yako, na kama ni swala la kumuona mgonjwa, mbona karibu siku mbili hizo, ulipokuwa unaumwa nyumbani yeye alikuwa akienda kumuona mgonjwa, alisema kwa vile unaumwa, ni wajibu wake kuchukua nafasi yako...’akasema.

‘Mimi sikuelewi, mliniambia nini mimi, kuwa mgonjwa haruhusiwi kuongea na mtu mwingine zaidi ya mimi na wewe, na hao madakitari wanaomshughulikia, ikawaje sasa mkamruhsu huyo mtu…?’ nikauliza kwa mshangao.

‘Hakuruhisiwa kumuona mgonjwa, yeye alikuwa akifika na kusimama kwenye kile kiyoo, unachoona ndani, basi, alikuwa akifanyaa hivyo kila siku ila jana, ndio akapata nafasi ya kuingia ndani, ...’akasema.

Nilitulia kwa muda, sikuweza kuongea, kwani moyo ulikuwa ukiniuma, nilihisi kuna jambo linaloendelea, na hawa watu, na wanachofanya wao ni kunichezea akili yangu,

‘Aliruhusiwa kumuona, sijui ilitokeaje, mume wako akaulizia kuhusu huyo rafiki yako, kuwa je aliwahi kuja kumuona, tukamwambia kwa vile analea mtoto mchanga inakuwa vigumu kwake, yeye akaomba aletwe , anataka kuonana nay eye, kama hajaondoka kwenye kusoma...’akasema na hapo nikageuka kumwangalia huyo rafiki yangu.

‘Ina maana …mbona sielewi hapo....!?’ nikauliza kwa mshangao,

‘Yaonekana mume wako akilini alikuwa anamkumbuka rafiki yako, na anafahamu kuwa atakwenda kusoma, ndio maana akaomba aje waongee naye kabla hajaondoka, na siku hiyo alikuwepo nje, sijui alijuaje kuwa yupo hapo nje, ikabidi aambiwe aingie…’ akasema.

‘Siwaelewi hapo kabisa, unazidi kunichanganya, halafu alipoingia alikuwepo nani mwingine aliyesikia wakiongea naye…’nikasema.

‘Mimi sikuwepo, nilifika wakati wameshamaliza kuongea nikaambiwa ilivyokuwa, sasa sijui waliongea nini, ..hata hivyo, kipindi wanaongea hakutaka mtu mwingine awepo , kwahiyo waliongea wao wawili tu…’akasema

‘Mhh…mimi sipendi hisia mbaya, nimejitahidi sana kulikwepa hilo, lakini kila hatua najikutwa nalazimishwa kuhisi vibaya, naanza kumshuku rafiki yangu mwenyewe ubaya, ni kwanini lakini, ni kwanini ….mimi nilimuamini sana, ..oh, hata sijui, …mungu anisamehe tu…’nikasema

‘Sio swala muhimu sana, kwa hivi sasa,…muhimu na la kuzingatia, ni ahadi kwa mume wako, kuwa umeshamsamehe au umesahau hilo?’ akaniuliza .

‘Mimi sijasahau, ila sikujua anataka nimsamehe nini, sasa , kosa gani nililomtendea, ndio maana nhitajia kumuuliza, sijui nifanyeje….’nikasema

‘Kwa hivi sasa hapana, inatakiwa wewe kuwa hivyo hivyo, kuwa umeshamsamehe, na sitaki kabisa kukulazimisha kuamini ubaya wowote dhdi ya rafiki yako na mumeo, kuwa labda kuna mahusiano ..labda…ila dalili zinajionyesha hivyo, ..’akasema

‘Hata mimi sasa naanza kuziona, lakini nafsini mwangu nashindwa kuliamini hilo, na kwanini iwe hivyo, rafiki yangu mwenyewe anifanyie hivyo, ..mume wangu mwenyewe anifanyie hivyo, hivi kweli wewe unaweza kulisamehe hilo…’nikawa nauliza

‘Kwa hivi sasa inabidi iwe hivyo, mpaka mumeo apone, mpaka, mumeo awe an nguvu za kukabiliana na wewe….naomba uwe hivyo, ujue lolote utakalolifanya kinyume na ulivyokiri kuwa umeshamsamehe, unaweza kuhatarisha maisha ya mumeo…’akasema

‘Ni vigumu sana, kama ni kweli hilo limefanyika, sizani kama msamaha huo utakuwepo, sizani,…hata kama kakimbia , nitafanya nifanyalo, akipate kile nilichoa hidi …sitamsamehe….siwezi kabisa…’nikasema

‘Kumbuka uliyatamka hayo mbele ya mume wako, akaamini kweli umeshamsamehe,..sasa usiwe kigeu geu wa kubadili kauli zako, unaongea vingine unakuja kutenda mengine, sio vizuri, nina imani kuwa siku ile uliyatamka hayo maneno ya kumsamehe kutoka moyoni mwako, au sio….’akasema docta

‘Ndio ilitoka moyoni, lakini sikujua kosa , sikujua nasamehe nini sasa, mlinitega tu, najua hata wewe unalifahamu hilo, na kama upo nyuma ya hili jambo sizani kama nitaweza kuwasamehe….’nikasema.

‘Mimi sijui lolote zaidi ya kufanya juhudu kuutafuta ukweli, mimi niliona hizo dalili, sikutaka kuamini hivyo, na ilichukua mud asana kuanza kuhis hivyo, japokuwa rafiki yangu alijitahidi kunificha..mimi sikupenda kabisa wewe wakufanyie hivyo, na rafiki yangu alilifahamu hilo, ndio maana hakuwahi kuniambia…’akasema

‘Rafiki yangu…siamini, bado sijaamin…’nikasema

‘Huenda ikawa sio kweli, kwasababu hata mimi pamoja na juhudi zote sijapata ushahidi wa moja kwa moja…nap engine huyo rafiki yako aliitwa kwa jambo hilo hilo....’akasema

‘Jambo gani…?’ nikauliza

‘Kuwa labda kamkosea,..kwahiyo alitaka asamehewe, au labda,…mimi naona labda zipo nyingi sana, na sio vyme kabisa kuwa na shaka shaka hizo tena, muhimu kwa sasa tuangalia afya ya mume wako,..hilo ndilo la muhimu mengine yasubiria kwanza…’akasema

‘Ni ngumu sana…’nikasema

‘Sasa tunakaribia kufika, leo foleni imezidi sana,…tukifika ukumbuke, ni vyema ukiingia pale uwe na uso wenye furaha, usionyeshe chuki yoyote, kuwa labda kuna jambo, maana toka jana alipofika huyo rafiki yako wakaongea naye, alipoondoka tu tulishangaa,…’akasema

‘Alikuwaje..?’ nikauliza

‘Amekataa kuongea tena na watu, tunahisi huko kukataa kuongea kwake, kuna mahusiano na huyo rafiki yako, hatujui waliongea nini, na mgonjwa mwenyewe akiulizwa kwanini anafanya hivyo hataki kusema, basi tukasema labda ni kwa vile na wewe hujafika, lakini hilo tulimuelezea awali kuwa unajisikia vibaya, akalipokea sasa jana ndio hali hiyo ikajitokeza...’akasema.

‘Kwahiyo …sasa kwanini hakuulizwa huyo mtu kabla hajaondoka, ni kwanini anamtesa mume wangu hivyo, kuna nini kati yao wawili, …hapana mimi sizani kama nitaweza kuvumilia tena, niambie nifanye nini sasa?’ nikauliza kwa hamaki.

‘Kama nilivyokuambia mengine yasubirie, labda kama hutaki mume wako apone, na hakuna aliyefahamu kuwa kutokuzungumza kwake huko kunaweza kuwa na mahusiano na huyo rafiki yako, tumekuja kulifikiria hilo baadae, asubuhi, wakati mtu aliondoka usiku…’akasema

‘Na kuondoka kwake, ni wachache walifahamu, mimi nimekuja kugundua nilipofika kwake asubuhi, na kuambiwa na jirani yake kuwa keshaondoka, nikauliza wapi, akasema amesafiri kwenda ulaya kusoma,....nikashangaa, mbona sikuwa makini na tarehe yake ya kuondoka, ina maana ulikuwa hujui anaondoka lini?’ akaniuliza.

‘Hapana kawahisha kuondoka, ilitakiwa akawie kidogo kwa ajili ya mtoto, sasa yeye akaamua kufuata tarehe ile ile ya awali,..tulikubaliana asubirie kidogo, na mimi nimekuwa kwenye wakati mgumu sikuwa makini kulifuatilia hilo…’nikasema

‘Basi yote hutokea ili iwe sababu, nahisi sasa utaweza kumuelewa rafiki yako ni mtu wa namna gani, kama aliyoyafanya kayafanya kwa makusudio yake mwenyewe…’akasema hivyo na kauli hiyo ikanifanya nisinyae kidogo.

‘Ok, labda,…ana sababu za kuwahi, basi angeliniambia.. ‘nikasema

‘Hapo moja kwa moja kila mtu atafahamu kuwa kuna sababu, na kuna jambo kati yake na mume wako, ..na sijui baba yako atasemaje kuhusu hilo…sasa ni wewe kupambana na hili jambo ili mumeo aweza kupona, huu ni mtihani kwako…akasema

‘Na wewe hujaongea naye, hata wewe hataki kuongea nawe…?’ nikamuuliza

‘Hata mimi ….hataki hata kuniangalia machoni…’akasema

‘Mimi siamini hilo, hata wewe rafiki yake, asiongee na wewe, akufiche mambo yake, usinitanie, nyie wawili, na sio wawili, nyie watatu, na huenda wa nne akawa mdogo wa mume wangu, nahisi nyie kuna jambo mumelifanya pamoja, na mnachokifanya ni kunizuga tu...mnanifanya mimi mtoto mdogo...’nikasema

‘Sijui kitu kwakweli, niamini hilo nakuambia zaidi ya shuku shuku tu ….’akasema

‘Mimi nawahakikishia kuwa nitaligundua hilo jambo mwenyewe, na ole wenu,...kama kuna jambo ambalo sio jema, sijui kama tutakuja kuongea, sitajali tena urafiki wetu, na huyo mume sijui,…’nikasema na kutulia.

‘Tatizo lako wewe unapenda kuchukulia mambo kihasira...na hilo ndilo litakufanya usijue mengi, na hata ukijua utakuwa hufaidiki nalo,utakuwa umeshachelewa....’akasema

‘Nimeshakuambia hivyo…’nikasema

‘Nikuambie ukweli, mimi nimejitahidi kadri ya uwezo wangu, nifahamu ni nini kinachoendelea kati ya mume wako na rafiki yako, sijaweza kukifahamu....nimejaribu kumhoji mdogo wa mume wako, .....lakini na yeye anaonekana hafahamu lolote...’akasema.

‘Mdogo wa mume wangu kasema hivyo, hafahamu kitu..?’ nikauliza kwa mshangao.

‘Ndio kama tulivyopanga, kuwa nitaongea naye, nimeongea naye, nimetumia kila mbinu, lakini inaonekana hilo jambo, ni kama tulivyo sisi anahisi hisi tu, hana uhakika, na yupo kama wewe, anamtetea sana kaka yake kuwa hawezi kufany ajambo kama hilo, …’akasema

‘Na hakukuambia kuwa zipo siku mume wangu alilewa sana wakampeleka kwa rafiki yangu wakalala huko…?’ nikajikuta nimeongea kitu ambacho sikutakiwa kukiongea.

‘Kwahiyo kumbe unafahamu ….’akasema

‘Ilitokea, …akalewa, lakini nafahamu bado wangelilinda ndoa..’nikasema

‘Watu wamelewa chakari, wakumbuke kulinda ndoa…hapo unanificha jambo….’akasema


‘Kuondoka kwa rafiki yangu huyo bila kuniaga, kunanitia wasiwasi,..tangu siku ile nilipoongea naye, mara ya mwisho, kauli yake imekuwa kama ya kunidharau,kuna kauli zenye kujiamini zaidi, ....sasa sielewi, kuna nini kimemfanya awe hivyo....’nikasema.

‘Je kwa mtizamo wako hadi hivi sasa huwezi kuhisi kuwa huenda rafiki yako alikuwa na mahusiano ya siri na mume wako?’ akaniuliza na mimi nikamjibu kw haraka.

‘Kwa mantiki hiyo naona kuna dalili hizo, lakini nafsi na akili yangu bado ipo gizani, sawa nahisi hivyo..lakini ushahidi upo wapi, maana sitaki kuja kukosana na mume wangu wakati kweli hana kosa,..nielewe hapo, maana kama ni kweli …’hapo nikatulia.

‘Ndio sasa uanze kufunguka masikio, nimekuwa nikijaribu kukueleza uelewe, ila sikutaka kukushinikiza kwa hilo..nimefanya hivyo , isije ikawa sio kweli ukanichukia kabisa, ukafikiria labda nina nia mbaya na ndoa yako au na urafiki wenu, natumai sasa upo na mimi,unaanza kuamini hilo, japokuwa hakuna uhakika wa moja kwa moja au sio, na usikimbilie kwenye kuvunja ndoa yako, hilo usiafanye kabisa, unasikia…?’ akaniuliza.

‘Mimi nilikuwa nasubiria hiyio taarifa ya rafiki yangu, ndio niweze kuwa na maamuzi yangu, maamuzi yangu yapo moyoni, hata rafiki yangu halifahamu hilo, lakini yeye akaondoka kabla hajanikabidhi hiyo taarifa, maana yake ni nini…kanidharau, kwa vile kafahamu kuwa kanikosea, si ndio maana yake hiyo…sasa hiyo kazi nitaifanya mimi mwenyewe ili nipate uhakika….’nikasema

‘Oh, nimekumbuka, kuna taarifa , alisema itakuwa ofisini kwako, mezani kwako, ukifika utaikuta, ila alimuambia katibu muhutasi wako asikusumbue, maana unaumwa, na ukijua kuwa taarifa hiyo ipo tayari haraka utakimbilia ofisini badala ya kusubiria upone vyema…’akasema

‘Unasema…!!! Ina maana hiyo taarifa ipo tayari, hiyo kwangu ina muhimu sana inabidi ugeuze gari nifike ofisini kwanza, tafadhali geuza gari…’nikasema

‘Tushakaribia hospitalini hatuwezi kugeuza gari tena hapa…na hata hivyo tukifanya hivyo, tutakuwa tumechelewa , tutakuta muda wa kuona wagonjwa umekwisha,..labda kama hutaki kumuona mume wako leo, …’akasema

‘Oh….’nikaguna nikiangalia saa kumbe muda ulikuwa umekwenda sana

‘Unasemaje maana tumeshafika, je unaiona hiyo taarifa ni muhimu kuliko mume wako….’akasema sasa akiingia eneo la hospitalini...

*************
Tulifika hospitalini, akili ikiwa imeshavurugwa,…hapa kwa upande mmoja natakiwa kuhakikisha mume wangu anapona, na ili hilo lifanikiwe, natakiwa nimeza machungu..nijifanye nipo sawa, lakini kwa upande mwingine baba ananishinikiza ili mume wangu aonekane mbaya, hafai hata kuongoza kampuni…na mpaka sasa nipo peke yangu, kwani mtu niliyekuwa nikimtegemea kwa kazi zangu nyingine ndio huyo kaondoka.

Nilitulia kimiya bila kusema neno, hadi tunakaribia kuingia chumba alicholazwa mume wangu, na hadi muda huo nilikuwa namuwazia huyo rafiki yangu, sikuwa bado nimemuwaza kwa mabaya, kwa chuki, badi nilikuwa nimempa nafasi..hapo nilikuwa nawazia tu huenda nimemtendea vibaya rafiki yangu huyo.., huenda nimemkosea ndio maana kafanya hivyo.

Hamuwezi kuamini jinsi gani nilikuwa nampenda huyo rafiki yangu, alikuwa ni kama ndugu yangu…na nilipofika hapo, nafsi ikaniuliza je ikiwa ni kweli katenda hayo yanayosemwa itakuwaje…oooh…kama ni kweli sijui kama nitaweza kuvumilia, sizani, na hata akimbie wapi…nitampata tu......atarudi, tutakutana au huko huko naweza kumtuma mtu..

‘Nilijitahidi sana nimuone mtoto wa rafiki yako, lakini mpaka anaondoka, sikubahatika kumuona sura yake....’akasema docta na kunisthua kutoka kwenye dimbwi la mawazo...

‘Sura ya mtoto wake ina umuhimu gani kwako…achana naye huyo bwana.., hana maana kabisa kwangu kaniuzi sana…’ nikasema.

‘Ingenisaidia kuwa na uhakika kuhusu baba wa huyo mtoto...yeye alijitahidi sana kufanya siri hiyo iwe siri…, dunia hii haina siri, wengi wameshaanza kuongea …sasa jiulize watu wamejuaje kuwa mtoto wake anafanana sana na watoto wako...’akasema.

‘Mhh, hata sijui …lakini hata hivyo hayo hayakuhusu au sio..labda uwe umetumwa na mtu fulani, na nafahamu kwanini unasema hivyo kuwa kama anafanana na watoto wangu basi mume wangu anahusika au sio..?’ nikamuuliza kimzaha.

‘Kwahiyo kumbe ni kweli, kuwa mtoto wake anafanana na watoto wako, nataka uhakika tu…?!’ akauliza kwaa mshangao.

‘Sijui mimi bwana, ....hata kama mtoto wake anafanana na watoto wangu, mbona watoto wakiwa wachanga wengi wanafafa tu, mimi hilo halinisumbui kichwa, na hata kama kanificha kumfahamu huyo bwana wake , mimi nitamfahamu kwa njia zangu nyingine...’nikasema

‘Ina maana wewe hujaamini hilo…’akasema

‘Nitaaminije hebu kaa kwenye nafasi yangu, jiulize ndugu yako anaweza kufanyakitu kama hicho, eeeh, sawa shuku kwenye nafsi zipo lakini nazishinda kwa kuweka hoja ya msingi, kuwa haiwezekani, yeye ni rafiki yangu, nimijitolea sana kwa ajili yake mpaka nimekosana na wazazi wake, hata huko kusoma ni juhudi zangu, je mtu kama huyo anaweza kunisaliti mimi…siamini..’nikasema

‘Mhh, hatujui lakini, hatujui, maana hata mume wako hajaliweka wazi hilo…’akasema

‘Mume wangu,…unajua mume wangu anamuheshimu sana huyo rafiki yangu, kuna kipindi aliniambia anavyomuheshimu anamuona kama mama mkwe…ndio uniambie mume wangu kafanya hivyo na rafiki yangu, hivi kweli inaingia akilini hapo, yaani siamini, siamini kabisa, hahaha, lakini lisemwalo lipo, na kama lipo, kutawaka moto, wewe subiria tu…..’nikasema.

‘Unajua ..kwanini nawashuku, sio tabia yangu kushuku watu ovyo vila vidhibiti…kama mtoto wake anafanana na watoto wako, ina maana mtoto wake anafanana na mume wako au sio, tunaangalia nadharia…’akasema

‘Mimi najua ipo siku tutathibitisha hili kivipimo, ila mimi nmefanya hivyo ili lituame kwenye nafsi yako mapema, ili usije kulipokea kwa mshtuko baadae…, na nasema hivyo sio kwamba nafahamu kitu, unielewe hapo, hata mimi bado sijawa na uhakika ila nilidhania kuwa labda ni mipango yenu wawili, upendo wenu umefikia hapo..’ akasema na kauli hiyo ilinichefua, nikamwangalia bila kusema kitu, nikajitahdi kulimeza tu…nikajikuta nimesema hivi;

‘Pia anafanana na mdogo wa mume wangu, mbona hilo hulisemi....’nikasema.

‘Yawezekana pia… lakini eeh, mdogo wa mume wako, angelianiambia, maana mengi yake ananiambia pia…alishaniambia jinsi gani alivyokuwa akimtaka huyo rafiki yako, na wakaishia kugombana, na tokea hapo wamekuwa hawaelewani , ni kusalimiana tu, sasa iweje leo,..lakini labda, kama alitaka mtoto na akaona haija jinsi amtumie yeey je..yawezekana pia…’ akasema.

‘Kama sio yeye, basi huyo ndugu yake mwingine…’nikasema

‘Kipindi kingi huyo ndugu yake mwingine amekuwa hakai sana hapa Dar, ni mtu wa kutoka toka…na hana ukaribu sana na rafiki yako,…sizani kama anahusika hapo…, mtu wa kumshuku alikuwa huyu ambaye mara kwa mara wamekuwa yupo hapa ambaye hata mumeo akizidiwa ndiye humchukua kwenye gari kumrejesha nyumbani….’akasema.

‘Mhh..labda hiyo ripoti ya rafiki yangu itasema kila kitu….natamani nipae ili nifike ofisini nione alichoandika,…niliitarajia sana, hata hivyo kwanini, asingeliniletea nyumbani, sawa hamna shida kama hiyo ipo tayari, hamna shida, kazi yangu kaimaliza kwahiyo namuombea kila la heri…’nikasema

‘Kwahiyo upo radhi naye, umemsamehe….’akasema

‘Nani …? Huyo rafiki yangu…? Kumsamehe kwa lipi, maana ni sawa na hilo la mume wangu kuwa nimsamehe tu, hata kosa hulijui…’nikasema

‘Kama ni kweli,..’akasema docta

‘Ohh.., kama ni kweli mnavyosema nyie, kama kweli anahusikana na ….na…ushetani huo, siwezi kumsamehe…katu…na..na.., hata mume wangu kwa hilo,…kama ni kweli, wote wawili kwangu watakuwa maadui… naomba, naombea sana isiwe ni kweli, maana, ohh…. nita-nita-ua mtu, wewe utaona tu…kwanini lakini, this is too much….’nikasema

Hapo docta akatulia, ..ukapita muda kidogo, halafu akasema;

‘Sasa tunaenda kukutana na mume wako, jaribu kukunjua sura yako, usije ukamuonyesha mumeo hiyo sura ya hasira, ukikunja uso wako hivyo, unakuwa kama unataka kuua mtu kweli.., mume wako akikuona hivyo anaweza kuhisi umefahamu ukweli wote...’akasema

‘Ukweli wote gani sasa, mpaka sasa sijafahamu kitu mimi, na nikifahamu,a kuthibitisha kuwa ni kweli,..hii sura itakuwa mara mbili, ok..ok..nahisi sipo vizuri....’ nikasema nikishika kichwa

‘Hebu tulia kidogo, vuta pumzi, eeeh, yes, fanya tena, haya tulia, unajisikiaje sasa…’akawa anafanyisha mazoezi ya kuvuta pumzi, nikajisikia sawa.

Alipoona nipo tayari, yeye akatoka kwa haraka kwenye gari na kuja kunifungulia mlango, nilisita kutoka , nikijipima kama kweli nipo tayari kukutana na mume wangu, na nikikutana naye, kweli nitaweza kujizuia.

‘Twende bwana, tumechelewa, hakikisha unaonyesha tabasamu,....usije ukamuonyesha mume wako chuki yoyote na uwe makini kumjibu maswali kwa yake akikuuliza eeh…’akasema

‘Maswali!!…hamna shida…’nikasema

‘Kumbuka kupona kwake haraka inategemeana na wewe utakavyomtendea....kama hutaki mume wako apone haraka endelea kujenga sura ya chuki......utakuja kujilaumu mwenyewe, usije ukasema sikukukanya ...ni muhimu sana hili, mengine yapumzishe kwanza....’akasema .

‘Sawa docta…’nikasema na mara simu yangu ikaita,..nilipoangalia nikaona ni baba ananipigia….

NB: Niendelee....


WAZO LA LEO: Wengi wetu tunafurahi kutendewa mema, kujali nafsi zetu kwanza na hasa tukiwa na shida, mara nyingi tunamuona mtenda wema huo ni mwema sana, hata kama kutenda kwake huko kunamgharimu. Lakini pindi ikatokea kuwa wema huo, au kutendewa huo hakupo tena, ni aghalabu kukubali ukweli kuwa na mwenzako anastahiki kutendewa hivyo-hivyo, huenda naye kakwama na yeye anastahiki kutendewa. Tujitahidi sana kulipa wema kwa jema, ili baraka ziongezeke, na maisha ya kupendana yazidi kuwepo.
 

Abdallahking

JF-Expert Member
Mar 19, 2018
1,989
2,000
SEHEMU YA 52

Alikuwa ni baba….baba ananipigia simu…nikawa najiuliza kuna nini tena...kwa pale ilikuwa sio vizuri kupokea simu, labda nitoke nje, nikamuangalia docta, docta akawa haniangalii,...na simu ikaita mpaka ikaacha yenyewe...

Haikuita tena...tulishaingia chumba alicholazwa mgonjwa na...nikawa nasita kidogo, na docta, akanigusa begani, nikageuka kumuangalia.. akaniashiria nisogee, nitembee kuelekea kule kwenye kitanda….alipolala mgonjwa.

Mapigo ya damu yalikuwa yanakwenda kwa kasi, ni kama nina wasiwasi, au kuna kitu kinakuja kutokea, ...sijui kwanini niliwaza hivyo...

Mume wangu alikuwa kalala kwenye kitanda huku akiwa kanyooka kabisa, na ilionekana kama kawekewa vyumba pembeni ili asitingishike,..lakini tofauti na ilivyokuwa mwanzo, safari hii kitanda kilikuwa kimeinuliwa kidogo, ili yeye kuweza kulala kama vile ameinuka sehemu ya begani na kichwani…

Nikasogea,…nilimchunguza, nikagundua kuwa, shingoni alikuwa kavalishwa, plastiki la kuzuia shingo isicheze cheze, na jinsi alivyowekwa ni kama mtu kakaa mwenyewe kimtindo. Na pale alipokuwa kalazwa, aliweza kuangalia mlangoni, kwahiyo tulipoingia tu, alituona.

Rafiki wa mume wangu yeye akawa kasimama, nilijua alifanya hivyo, ili kunifanya mimi nitangulie mbele yake, yeye akawa anakuja taratibu nyuma yangu, huku akinigusa kwenye mkono, kuniashiria kuwa nisogee pale alipokuwa mume wangu , na hata ilifikia hatua ya kuninong’oneza akisema;

‘Nenda pale kitandani kamsalimie mume wako,....mpaka nikifundishe,..., na kumbuka niliyokushauri .....’ nikaelewa ana maana gani, nilisogea huku macho yangu yakiwa yanamwangalia mume wangu.

Kwa pembeni karibu na ofisi ya docta, walisimama madakitari wawili wakihakikisha kila kitu kinakwenda salama, na mmoja wapo alikuwa dakitari wake bingwa wa maswala ya mifupa, alikuwa kashika makabrasha yake akimuelekeza msaidizi wake ni nini cha kufanya baada ya hapo....

Mimi sikuwa na haja na watu hawo kwa muda huo, mawazo na akili yangu ilikuwa kwa mume wangu, na macho yangu yalikuwa yamelekea pale alipo mume wangu, na nikawa namsogelea huku tumetizamana machoni.

Macho yangu na ya mume wangu yakawa yanaangaliana, kwanza niliona usoni kama anashituka,au kama ananishangaa kuniona, na baadaye mdomoni akaonekana kutabasamu, lakini niliona kama tabasamu la kulazimisha,..lakini kadri tulivyokuwa tukimsogelea ndivyo lile tabasamu lilivyozidi kuongezeka, na sasa likawa tabasamu halisi, na alikuwa wa kwanza kutamka neno.

‘Hatimaye mke wangu umefika...’akasema.

Na kauli hii ilinifanye nigeuke kumwangalia rafiki wa mume wangu , ambaye alikuwa nyumba yangu kama vile wafanyavyo walinzi, nahisi aliogopa nisije nikaongea jambo lisilotakiwa kwa wakati huo.

Kiukweli sikuwa nimependa jinsi anavyonifanya, nakuwa sina uhuru wa kuongea, lakini kwa namna nyingine niliona ni bora iwe hivyo, maana ananifahamu vyema, sina uvumilivu wa kumezea jambo, kama ni jambo la kuongewa, ni lazima litaongewa tu, sipendi kunyamaza nyamaza.

Nilimwangalia mume wangu huku nikitabasamu , lile tabasamu la kimodo, ili tu mume wangu aone kuwa nampenda, namjali, na sina kinyongi naye, kwakweli kwa hali ilivyo, tabasamu hilo lilikuwa kama la kubandikwa mdomoni, lakini nilijitahidi kuliigiza ipasavyo…

Nilipogeuka kumwangalia rafiki wa mume wangu, nilimuona naye akitabsamu, kama vile ananionyeshea kuwa na mimi nitabasamu hivyo hivyo,na akawa ananionyeshea ishara kuwa nisogee mbele karibu sana na mume wangu. Nami nikasogelea kile kitanda alicholala mume wangu , na kumuinamia..

Kwa ujumla mume wangu alikuwa amepungua sana, na hali hii ya kupungua, kukonda ilianza kujitokeza hata kabla ya hili tatizo, na baada ya hili tukio, nimeona kapungua kwa haraka sana, hali hii imezidi kumfanya akonde zaidi, hata mashavu, yalishaonyesha kubonyea, moyoni nikasema akipona tu nitahakikisha mashavu yanakuwa dodo...ni lazima nimrejeshe kwenye hali yake ya kawaida....

‘Nimefika mume wangu unaendeleaje?’ nikamuuliza nikiwa nimemkaribia, na kumuinamia nikambusu kwenye paji la uso, yeye akaguna kidogo na kusema;

‘Mhh, hata sijui niseme nini, kuwa sijambo au naumwa, mwenyewe unaiona hi hali niliyo nayo, maana hapa nilipo ni kama nusu mfu, mwili wote sio wangu tena, kama unavyoona, mwili wote chini hauna kazi,ni kama sio mwili wangu,....’akasema akionyeshea kwa ishara.

‘Utapona usijali..’nikaema

‘Unajua, eti wanasema ni swala la muda, lakini kwa hali kama hiii ....dakika,saa , siku ni kama mwaka, nateseka sana mke wangu,sijui hii ndio adhabu yenyewe, mungu wangu nisamehe sana.., nimekosa, sitarudia tena.....’akawa anaongea na mimi nikawa namwangalia tu.

Kiukweli macho yake yalionyesha huruma, na alivyokuwa akiongea, hata ingelikuwa nani angelimuonea huruma, …pale nilipo huruma ilinishika, na nilihis machozi yakianza kunijia, nikakumbuka maneno ya docta...

‘Hakikisha humuonyeshi mume wako kuwa anaumwa sana, zuia kulia, jenga tabasamu la kumuonyesha kuwa hajambo...muonyeshe kuwa hali aliyo nayo ni ya kawaida tu...’

‘Mume wangu mbona umeshapona tu, ..hatua uliyofikia ni kubwa sana, maana ukiona hilo gari lako lilivyoharibika, huwezi kuamini kuwa kuna mtu katoka hai, lakini mungu wako bado anakuhitajia uwepo dunia, sisi tunaokupenda tunakuhitajia sana..namshukuru mungu kuwa upo salama, na hali uliyo nayo ni ya kutia matumaini, cha muhimu ni kufuata masharti ya madakitari...’nikasema.

‘Eti masharti ya dakitari,..masharti gani hayo, hapa nilipo nitafanya nini cha kuvunja hayo masharti, maana kama unavyoona mwili wenyewe hausogei, nitavunja msharti gani, kinachofanya kazi hapa ni akili tu...kuwaza tu, ..haya na huko kuwaza nitawezaje kujizuia, wakati nafahamu fika , kuwa haya yote yametokana na dhambi ....nimewakosea watu.’akasema na hapo nikageuka kumwangalia rafiki wa mume wangu, akanionyesha ishara ya kuwa makini.

‘Mume wangu hakuna dhambi hapa duniani isiyoweza kusameheka,kama umetubu ..mimi nina imani kuwa kila binadamu anakosea, na wewe kama binadamu huwezi kujiaminisha moja kwa moja kuwa utaweza kutenda kila jambo sawasawa, ....kama ulitetereka, basi ..imetokea na huna jinsi nyingine, cha muhimu ni kujitahidi kutuliza kichwa chako na mawazo yako ukayaelekeza kwenye kupona, na wamesema kupona kwako itategemeana na wewe mwenyewe...’nikasema.

‘Mmh, kupona kwangu itategemea na mimi mwenyewe, sijui kwa vipi,...na wakati nimeshakuambia nimewakosea nyie watu wangu, ..nimewakosea watu muhimu sana, katika maisha yangu..nimekukosea wewe mke wangu …nisamahe sana...’hapo akatulia kidogo, na nilipomwangalia machoni, niliona kama analengwa legwa na machozi, akasema;

‘Mimi nimeshakusamahe mume wangu…’nikasema

‘Mke wangu umesema umenisamehe, kwanini ulikuwa huji kuniona mara kwa mara, maana hata kama nilikuwa sina kauli, siwezi kuongea, lakini nilikuwa naona kila kitu kinachotendeka…?’ akauliza na hapo ikabidi nigeuke kumuangalia docta.

Docta aliniashiria niwe makini hapo, na kabla sijasema kitu, akaendelea kusema

‘Unajua.., wote waliokuwa wakija nawaona, lakini wewe sikuweza kukuona, , nilikuona mara moja tu, siku ile...hali hii inanipa shida na kunifanya nisiamini kuwa kweli umenisamehe....hivi kweli umenisamehe mke wangu..?’akasema na alikuwa kama analalamika, na hali hiyo ikanifanya nigeuka kumwangalia tena rafiki wa mume wangu ambaye alijifanya kama haniangalii mimi, alikuwa akisoma kadi iliyokuwa imewekwa mezani.

‘Mume wangu, mimi nilikuwa nafuata masharti ya madakitari, kwani wao waliniambia kuwa huhitajiki kusumbuliwa, na ilitakiwa usikutane na watu wengine zaidi ya madakitari wako, hadi zipite siku saba, ili uweze kutuliza kichwa chako... ni masharti niliyopewa mimi, na ndivyo nilivyofanya, sikutaka litokee jambo la kukufanya usipone haraka...’nikasema.

‘Sio kweli, kama ni hivyo mbona rafiki yako wa karibu mara nyingi nilikuwa nikimuona akifika hapa...na aliniambia kuwa anaondoka na mtoto, kwenda kusoma, kwanini aondoke na mtoto bado mchanga, hivi nyie mna akili kweli...’akasema.

‘Alifika akakuambia hivyo..?’ nikauliza nikionyesha mshangao.

‘Ina maana wewe hujui kuwa keshaondoka, ...usinidanganye wakati wewe ndiye mfadhili wake, mimi sikuona umuhimu wa yeye kwenda kusoma kwa sasa, wakati ana mtoto mchanga,nilimshauri asubiria kwanza, lakini hakunisikiliza, nikajua mumepanga wote...’akasema.

‘Haina shida, huko Ulaya unaweza kusoma na mtoto, unaweza kusomea nyumbani,...hilo lisikutie mashaka, anajua ni nini anachokifanya yeye sio mtoto mdogo....’nikasema.

‘Kweli Ulaya ni ulaya, lakini mimi namuwazia sana mtoto, yule mtoto bado mchanga bwana, wewe hulioni hilo..yeye angelisubiria angalau miezi mitatu hivi, lakini haelezeki, htaaki kusikia, kaamua kaamua basi, rafiki yako mnajuana wenyewe,....’akasema.

‘Yule niachie mimi, namfahamu sana, ni rafiki yangu, usiwe na shaka na yeye, alishaambiwa huko mtoto hatakuwa na shida, kila kitu wamemuandalia....’nikasema.

‘Mimi sina shaka na yeye nina shaka na mtoto, mtoto yule bado mchanga, safari na hali ya hewa ya huko, mmh, mimi sijui....’akasema na kutulia, na baadaye akasema;

‘Yeye alikuwa anakuja, anasimama pale mbele kwenye kiyoo, ananiangalia kwa muda halafu anaondoka, mimi nilikuwa namuona…’akasema na mimi nikageuka kuangalia kwenye hilo dirisha.

‘Nikawa najiuliza kwanini haingii ndani na mara ya mwisho nikaona niongee na dakitari ili aruhusiwe aingie, inaonyesha alikuwa ana hamu sana ya kuniona, ..rafiki yako ni mtu mnzuri, ila akiamua jambo, hapo humuelezi kitu, hajali tena hisia za wengine..’akasema

‘Mhh, ndivyo alivyo…’nikasema maana naona imekuwa maongezi ni kuhusu huyo rafiki tu, sikutaka kumkatili.

‘Ila kiukweli kauvunja moyo wangu…kuondoka na mtoto, unajua yule tumeishi naye, tunamjali sana, kwanini hukumshauri wewe…lakini sawa mwache aondoke, si atarudi,....’akasema

Hapo nikawa nataka kuongea jambo, kuuliza maswali, lakini nikaogopa, nikaona nikae kimiya,maana nilipomwangalia rafiki wa mume wangu ambaye alikuwa kwa mbele, eneo la kichwani kwa mgonjwa, na alikuwa akiniangalai moja kwa moja ninavyoongea, akaniashiria nisiseme neno.

‘Mke wangu, mimi inanipa shida sana naona kama wewe hujanisamehe kiukweli, na nilikuambia ukinisamehe nahis hivyo,..siku ile kweli ulitamka na ilionekana hivyo, ila kila hatua nahisi kama hujanisamehe..’akasema

‘Kwanini unasema hivyo mume wangu..?’ nikauliza

‘Kama hujanisamehe sizani kama mimi nitakuwa na amani, na huenda nikarudi kuzimu , unajua nilikufa…ni maombezi tu, kuwa nirudi ili nimalizie toba, nihakikishe kuwa kila kitu kipo sawa…sasa kwa hali kama hiyo, sioni umuhimu wa haya yote...’akasema na mimi hapo nikashindwa kuvumilia nikajikuta nimetamka neno ambalo lilimfanya rafiki wa mume wangu kuniangalia kwa sura ya kunisuta;

‘Mume wangu mbona hujafanya kosa, kwani kuna kosa gani kubwa la kukufanya usononeke kiasi hicho...nimeshakuambia kuwa nimekusamehe, japokuwa sijui kosa gani ulilolifanya...’nikasema na nikaona akishtuka, na kunikazia macho, nikaona kama anabadilika.
Docta rafiki , akahisi kwa haraka akatoka kule alipokuwa kasimama na kunisogelea, sikuwa nimemuona, hadi pale aliponishika mkono, nilipogeuka nikamuona yeye akinionyesha ishara ya kuwa makini.

‘Mhh, mke wangu…unasema nini, ..ndio maana nilikuwa na wasiwasi sana, mungu wangu, ina maana kweli hujui kosa lako ni nini…mmmh,… hapana usinichekeshe,..ina maana kweli kosa lenyewe hulijui, halafu umekubali kunisamehe ..haah , kwahiyo ulikuwa wanichezea shere, unaigiza tu, nilijua tu…’akasema

‘Mume wangu mimi najua , kuwa umenikosea kwa yale mambo yetu ya nyumbani, unakwenda unakunywa, unakutana na wanawake huko..sasa sijui huko mnamalizana vipi, hiyo ni siri yako,..kama ni hivyo, basi mimi nimekusamehe ilimradi umefahamu kosa lako ni nini, ila sipendi kujua zaidi kama, ulipitiliza utajua wewe na mungu wako, ila mimi nimekusamahe, ni wapiti njia au sio..…’nikasema

‘Oh…kumbe hata kosa lenyewe unasema hulijui, hapana sio wapiti njia, mimi sikuwa na tabia hiyo…mimi nazungumzia kosa hilo jingine…kwahiyo sio kweli, niambie ukweli..., au unajifanya tu kuwa hulijui kosa langu, kwa vile kuna watu hapa, huyu ni rafiki yangu tu…’akasema akimuonyeshea docta.

‘Mume wangu haina haja, yamepita basi…’nikasema

‘Hayajapita, ni lazima unisamehe kiukweli, je hujaongea na mwenzako, mkakubaliana jambo..au kwa vile hayupo leo hapa,…najua angelikuwepo hapa ingelikuwa ni bora zaidi, ili alithibitishe hilo…lakini si atakuja tu, nitahakikisha anaongea kila kitu, hata hivyo mimi sina muda, sijui muda wangu..maisha haya hayana muamala..nataka niutue huu mzigo...’akasema na kutulia.

‘Mume wangu mimi nimekusamehe, na kwangu afya yako ni bora kuliko, hayo ya kupita tu, amini kuwa nimekusamehe, nisingelipenda kujua mengine zaidi, inatosha, unanisikia, wewe tuliza moyo wako ili upone haraka…’nikasema

‘Hapana mimi nataka kauli yako, nijue ukweli wako, je ni kweli kuwa hulifahamu hilo kosa,… aah..pumzi inakata kwanini docta…ni lazima niliongee hili leo hii,…niambie ni kwanini usilifahamu wakati wewe ndiye uliyemtuma kwangu ..?’ akauliza

‘Kumtuma nani…?’ nikauliza na docta akaniashiria nikubali tu.

‘Rafiki yako…’akasema

‘Rafiki yangu …ok, ndio, mara nyingi namtuma…alikuambiaje…’nikasema

Hapo mgonjwa, akatulia akionyesha kama anawaza jambo halafu nikaona kama anabadilika, anapata taabu ya hewa kitu kama hicho, mimi niligeuka kumuangalia docta, na docta wakati huo alikuwa anashughulika na kitu kingine.

Nikageuka tena kumuangalia mume wangu, akawa yupo sawa, …ila ni kama anajilazimisha,…akasema

‘Siamini kama hujui kosa langu,..nilijua tu , hukupenda, lakini unajua tena ulevi..na hapo imekuwa sababu ya madhambi mengi tu….ooh, kwanini hii hali haitulii, niongee na mke wangu…’akasema akijaribu kuinua kichwa kumuangalia docta, na docta akamsogelea na kusema;

‘Kama hujisikii vizuri usijilazimishe…’akasema docta

‘Usiniingilie haya docta,..hata kwangu ni mhimu kwangu kuliko chochote,..huenda nisipate muda tena…’akasema akimuangalia docta. Na docta akawa kama anataka kumzuia asiendeleee kuongea lakini hakuweza, akaniangalia mimi huku akionyesha wasiwasi, na kwa muda ule, mume wangu alikuwa akihangaika kama hewa inamuwia ndogo, lakini aliendelea kuongea.

‘Mke wangu, unafikiri mimi nilipenda kufanya hivyo, ilikuwa kazi kubwa sana kukubali hayo…, na nilikubali tu kilevi levi, lakini moyo haukutaka, na ni kwa vile ni rafiki yako, na ni kwa vile kasema mliongea naye ukakubaliana ila iwe siri,..hapo ukichanganya na ulevi, nikajikuta nimeingia kwenye mtego, ningelifanyaje hapo mke wangu nakiri kuwa ni kosa maana sikutaka kuhakiki kutoka kwako…’akatulia huku anaonekana anapata shida

‘Docta….’nikasema

‘Achana na …na huyo do-docta nisikilize mimi..unasikia , nisikilize mimi mumeo…’akasema, na mimi nikamuangalia, ndio akaendelea kuongea.

‘Ulevi, mawazo..na kauli yake, ikanihadaa…unasikia, nasema haya kiukweli…nisamahe tu, najua nimekosea sana, kwani sheria ya ndoa inanibana,…’akasema na nikaona akizidi kuhangaika.

‘Mhh…sikupenda mke wangu…ndio maana najuta sana, inaniuma sana, sijawahi na sikutarajia kufanya hilo, nimekuwa mwaminifu kwako mke wangu, wengi wakiniona nipo na mwanamke wanafikiri vibaya, lakini napoteza nao mawazo tu…’akasema na kukokhoa, halafu akatulia na nilitaka niongee lakini akaanza kuongea yeye.

‘Rafiki yako, ananiliwaza, tunaongea ananipa faraja, nikamzoea hivyo, lakini sikuwa na nia mbaya kwake…ila siku , oooh,…ikatokea , hata sijui ilikuwaje, nashindwa kuelezea, kauli yake ikaniponza,, yaani inaniuma sana, nilishindwa mke wangu, nikiri kuwa , ooh, nilitaka m-tttt.ooh wa-waaah, aaah..’akashindwa kuendelea na hapo rafiki wa mume wangu alifika na kumuinamia akamwambia;

‘Rafiki yangu acha kuongeza zaidi, mke wako ameshakuelewa, hukukusudia kabisa kujiingiza kwenye dhambi hizo, ulishawishika vibaya, kama ulivyosema, unakumbuka nilivyokuambia, acha kabisa kuongea hayo mambo....ni kosa na kama ni kosa limeshafanyika, ...basi’akasema…kukawa kimia, mimi nilikuwa mwili umekufa ganzi

Muda kidogo,akafunua mdomo na kusema;

‘Mke wangu hana kosa,…wewe huna kosa nisitoe kisingizio kuwa kwa vile..hapana, maana muda wote najizuia,…lakini rafiki yaka…alichosema, kilikuja kipindi kibaya nikiwa sijitambui…kwahiyo kwa hali kama ile, basi ikawa hivyo, kwahiyo, nisamehe tu mke wangu….’akasema

Docta akamwambia;-

‘Basi keshaelewa, tulia, sasa lala..au unataka ulazimishwe kulala kwa madawa…’akaambiwa, mimi kiukweli akili ilikuwa sio yangu, nilikuwa kama naota ..

‘Sogea pe-pembeni bwana,.. mimi nataka kuongea na mke wangu…nisipoongea leo, sitaongea tena, unanielewa, nilifunga kuongea, nikiwaza mengi, nikutubu, nikiwazia ya huyo rafiki yake, hataki kunisikiliza…sasa nipo peke yangu ni bora kufa tu, maana sitaeleweka, nakutegemea wewe mke wangu, basi…baba yako, hatanisikia, kampuni,…hata sielewi, ..’akasema.

Na hapo docta akageuka kule walipo madocta, nahisi alitaka kuwaashiria kitu , lakini wale madocta walikuwa wameinama wakiangalia kitu mezani.

‘Mke wangu unanifahamu sana, wakati wote nimekuwa nawajibika, nimekuwa mwaminifu kwa kazi, tukirudi nyumba wewe na laptop na mimi na laptop, hao ndio wapenzi wetu, haahaa…ni hivyo, basi mimi nikaongeza pombe, kumbe …ndio imenifikisha hapa…’akatulia

Pale nilipo najaribu kufunua mdomo lakini siwezi, nimebakia kimwili tu…na yeye akaendelea kuongea;

‘Mhh..sa-sa.., japokuwa wakati mwingine nateseka kama binadamu wa kawaida, unatamani kitu, unataka mtoto…..unajua tena…inabidi uvumilie, ndoa ni ndoa..mke yupo, lakini utafanyaje, nisingeliweza kumlazimisha mke wangu…’akasema na hap akawa kama anaongeza kitu kichwani mwangu, natamani nianza kuonega kwa jaziba, lakini siwezi.

‘Mke wangu ….kiukweli sikupenda, maana nakupenda sana mke wangu, na sikutaka kukuumiza mke wangu, japkuwa nilikuwa naumia, natamani, ndio nikaanza kulewa, kulewa ikawa ni shida, maana ndio imefanya akili ikaharibika…ila simlaumu mtu, aah, najilaumu mwenyewe dhambi ni zangu, usiponisamehe, basi acha nikaangamie, unasikia, nisimlaumu mtu, kabisa....’akasema

‘Mume wangu inatosha, sawa nimekuelewa, inatosha, mimi nimekosa, samahani kwa hilo sitarudia tena sikujua kuwa nakuumiza hivyo, nisamehe mume wangu, oh…ina maana haah, basi, ..hata, basi, hata..sielewi, inatosha mume wangu, basi …’hapo sikuweza kujizuia, nikaanza kulia.

‘M-mke -wangu, usilie….najua hujakosea, sikiliza…’akawa anahangaika kutaka kama kuinuka hawezi..

‘Ohoo, unafanya nini sasa wewe, utamuua mume wako, nilikuambia nini..’akasema docta akijaribu sasa kufanya lolote kuidhibiti ile hali

‘Mke wangu…mke wangu nisamahe tu…nimeongea hayo kukuonyesha kuwa sikutaka..ila nili..zidiwa, na kwa vile alisema mlikubaliana, upo radhi..basi, …’akatulia

‘Tulikubaliana nini..…’ hapo nikasema kwa ukali, mpaka docta akashtuka na kuniangalia kwa macho yasiyoaamini,..haraka akanishika mdomoni nisiendelee kuongea.

‘Ndio..alisema hivyo..ndio maana nikashindwa,...nikashindwa,....najuta sana kukubali kufanya hivyo , kwanini nilishindwa kujizuia,mbona wakati wote niliweza , kwanini safari ile nikashidwa ...nimeumia sana,…nisamehe sana mke …mke…tamka neno kuwa umenisamehe, niwe huru na mateso haya, aah, aah, aah,….. ’ madocta wakawa wameshafika;

‘Nini tena, hebu,..hebu….’nikasukumwa pembeni, maana pale nilipo sikuweza hata kuinua mguu.

‘Sogea, sogea, basi hatuwezi kumruhusu kuongea tena, ni vyema ukatoka nje, ...ngoja tumpe dawa, anahitajia kupumzika....’akasema

Hapo ndio nikagundua kuwa nimeharibu, nimeshindwa kuvumilia, kama alivyonitaka docta, badala ya kujenga nimebomoa, nikajua sasa nimeua…mume wangu akawa bado anajitahidi kuongea, nikasikia akilalamika,

‘Mbona sijamalizana na mke wangu, sijamwambia, nilichotaka kumwambia...nipeni dakika mbili niongee na mke wanguuu-uh...’akasema mume wangu, lakini maneno yake hayo ya mwisho yalikuwa kama ya mtu aliyelewa, na akatulia, kumbe kuna dawa waliipitishia kwenye mpira, ilikuwa dawa ya usingizi....

‘Mbona inachelewa….’akasema docta akiwa na maana ile dawa ya kumfanya alale imechelewa kufanya kazi

‘Mungu wangu nimefanya nini....’nikajikuta nimesema hivyo, nikijua kuwa nilishindwa aliyoniambia rafiki wa mume wangu nikageuka kumwangalia rafiki wa mume wangu, ambaye alikuwa akibenua mdomo, kuashiria kuwa hakuna tatizo.

Nikageuka kumwangalia mume wangu ambaye alikuwa keshafumba macho, na madaktari walikuwa wakiendelea kumkagua, na hapo kichwani nikaanza kukumbuka maneno yake, maana muda ule wakati anaongea kuna muda akili ilikuwa kama imeganda, sasa maneno yanaanza kujirejea kichwani;

‘Mke wangu, unafikiri mimi nilipenda kufanya hivyo, ilikuwa kazi kubwa sana kukubali,...kwa vile ni rafiki yako, na kwa vile kasema wewe ndiye uliyemtuma,

‘Oh, mungu wangu…’nikajikuta nimesema hivyo

Mimi ndiye niliyemtuma, ..aka-aka…sio hivyo, hatukukubaliana hivyo, kwa mume wangu hapana, hili halipo, kwa shameji yake, nimtume mimi, haiwezekani, sio kweli , sio kweli, labda kama …rafiki yangu aliamua kutumia kauli hiyo kutimiza malengo yake…lakini haiwezekani sio rafiki yangu…

‘Au mume wangu hana maana hiyo, labda ana maana ya jambo jingine labda sio hivyo, mungu wangu, mungu wangu sio kweli jamani…’maneno hayo nikayasema kwa sauti , na docta akayasikia, lakini wenzake walikuwa wakihangaika na mgonjwa..

Docta akaniashiria nitulie…hutaamini bado nilikuwa sijaweza kuinua mguu, nipo pale niliposukumiwa na wale madocta, …miguu haiana nguvu

Na muda huo nahisi kama kuna vitu vimeingia kichwani, maneno ya mume wangu yanajirudia rudia kichwani;

‘Mke wangu unanifahamu sana, wakati wote nimekuwa nawajibika, nimekuwa mwaminifu kwako na kazi yangu,nimekuwa nikijizuia kutenda dhambi yoyote, japokuwa wakati mwingine nateseka kama binadamu wa kawaida...


‘Oh…mbona sielewi, kuna nini hapa, ina maana ni kweli,…’nikasema kwa suti ndogo, kama namnong’oneza mtu..

‘Sio kweli, kachanganyikiwa tu mgonjwa sio kweli…’nikasema sasa kwa sauti, mpaka wote pale ndani wakageuka kuniangalia mimi.

Docta akanisogelea na aliponiangalia tu, akagundua kuwa nimeshabadilika na muda wowote naweza kudondoka, ..akanishikilia nikaona anamuashiria docta mwingine aje kusaidia..akawa anamuagiza kitu, sikuelewa ni kitu gani.

‘Ina maana ni kweli, aaah, hapana sio kweli jamani …docta niambie kuwa sio kweli..hana maana hiyo kabisa, eti docta ni kweli jamani...?’nikasema huku nashikilia kifuani, kiukweli pale nilihisi maumivu makali yalikuwa upande wa kushoto…nipo kama nimechanganyikiwa.

‘Mke -wangu,wakati mwingine kama binadamu wa kawaida natamani nitende dhambi, lakini najizuia, naogopa, ...lakini safari ile nikashindwa,...nikashindwa,....najuta sana kukubali kufanya hivyo , kwanini nilishindwa kujizuia,mbona wakati wote niliweza , kwanini safari ile nikashindwa....’

Maneno hayo yalijirudia rudia kichwani...yakanifanya niishiwe nguvu kabisa, kama isingelikuwa ni docta ningedondokea sakafuni, ..

‘Inatosha...haina haja, kumpiga sindano.’akasema docta akimwambia mwenzake sikujua ana maana gani, na mimi nikawa naongea tu..


‘Umefanya nini na mume wangu, ...mumefanya dhambi gani wewe na rafiki yangu, ina maana ni kweli ..ina maana ni kweli…hapana sio kweli jamani haiwezekani kabisa,…

Nikamwamgalia mume wangu ambaye wakati huo alikuwa katulia, kalala, na akili yangu pale ikanituma kuwa keshafariki…sijui kwanini niliwaza vile…;

‘Ina maana nimeongea vibaya, nimemuua mume wangu. Mume wangu usife nataka niusikie ukweli wote, jamani…sio kweli jamani, sio kweli, kwanini hivi jamani..mume wangu usife uje uniambie ni kwanini..’ sasa nikawa naongea kama mtu aliyechanganyikiwa..

‘Hajafa, tulia, …ukiendelea kuongea hivyo ndio utamuua…’akasema docta...na muda ule akawaashiria kitu, na mara nikahis sindani ikipigwa..haikuchukua muda, giza litanda usoni…lakini kabla sijafunga macho mlangoni nilimuona baba akiwa kasimama, kama anasubiria kuambiwa aiingie, sijui alifika muda gani ….


WAZO LA LEO: Mambo yakijirudia sana mwishowe watu huja huamini, hata kama ilikuwa sio kweli. Ndivyo akili zetu zilivyo., ni wachache sana wanaoweza kusubiria hadi ukweli uwe bayana hasa kwa mambo yanayokwanza mioyo yetu. Tunaweza kujiaminisha kuwa ni kweli, kwa vile tu linaongelewa sana, kwa vile tu mtu mashuhuri kalisema, nk..lakini hatujiuliza kwanza, je ni kweli, je kama sio kweli itakuwaje, na tujiulize hivyo huku tukifanya tafiti yakinifu…bora ya kuwa na subira kuamini jambo huku ukitafuta ukweli kuliko kukimbilia kuamini halafu ije kuwa sio kweli..
 

Abdallahking

JF-Expert Member
Mar 19, 2018
1,989
2,000
SEHEMU YA 53

Siku kadhaa zikapita na mume wangu akatakiwa kurejeshwa nyumbani, na kabla ya kurejeshwa nyumbani, docta aliyekuwa akimuhudumia, akaniita ofisini kwake, na kunishauri mambo mengi ili kuhakikisha mume wangu anaondoka kwenye hatari na kupona mapema.

'Unasikia wewe ni mke wake, na mtu muhimu kwake, wewe ndiye utamfanya apone haraka au....unasikia, muhimu tena sana,jitahidi kuwa karibu sana na mume wangu, na kukwepa kauli yoyote ya kumkwaza...unasikia...'akasema docta akinisisitiza hilo sana

'Nakusikia docta...'nikasema

'Mume wako, yupo kwenye hali ambayo akipata mshtuko tu inaweza kuzua tatizo kubwa ambalo litamfanya ashindwe kutembea kabisa....na ukijitahidi akawa hana mawazo, mazoezi...na kufuta masharti nilikuambia awali, ...atapona haraka tu...'akasema docta

‘Sawa docta mimi nitajitahidi kadri ya uwezo wangu, maana huyo ni mume wangu, sina jinsi…ila nimegundua kitu, hivi sasa ni mbishi sana, na ubishi huu hakuwa nao , nahisi umeanza baada ya hili tatizo, kila kitu anataka nimsikilize yeye tu, sasa sijui nikiwa naye huko nyumbani itakuwaje...’nikasema.

‘Ndio hivyo, jitahidi uwezevyo, kama kweli unamjali mume wako na unataka apone haraka, basi acha kila kitu kwa ajili ya mume wako …’akasema docta

'Sawa docta...'nikasema

Kabla ya kuondoka hapo hospitalini baba akanipigia simu, baba siku hizi amekuwa kila mara akinipigia simu , hasa baada ya kushuhudia nikipoteza fahamu hapo hospitalini, tukio hilo limemfanya awe karibu na mimi, kuliko alivyokuwa baada ya mimi kuolewa..;

‘Vipi hali yako na ya mume wako…?’ akaniuliza

‘Hajambo jambo, kama walivyokuwa wamesema leo tunaweza kuondoka naye…hapa tu, tupo nje tunataka kuondoka kurudi nyumbani..’nikasema

‘Ok, vizuri…sasa ok, naaah, umefikiriaje wazo langu..?’ akaniuliza kwa lugha ya upole, sio tabia ya baba akiongea na mimi, hasa nilipolazimisha kuolewa na mume ambaye hawamtaki.

‘Baba mengine yasubirie kwanza, ngoja nibebe hili jukumu la mume wangu maana nimejitakia mwenyewe, na sihitajii msaada kwenu baba, nitajimudu mwenyewe…’nikasema

‘Usiwe mkaidi kwa hilo, hilo ni tatizo kubwa sana, kama unafikia kupoteza fahamu, sio kitu kidogo hicho, sisi wazazi wako hatuwezi kukaa kimia, na mama yako atakuja akae nawewe, tuone jinsi gani ya kukusaidia, unasikia…’akasema

‘Baba hapana, mama mwenyewe mbovu, tutazidi kumchosha tu bure, nakuomba hilo liacheni kama lilivyo, ikibidi nitawaambia…’nikasema

Kila nikiombea na baba ni lazima akimbilie kwenye lawama, akasema;


‘Nilishakuambia huyo mwanaume hakufai, atakuhangaisha mwishowe atakuepeleka kubaya, utaumwa, unaweza hata kupooza mwili, mwishowe utaingia kaburini, wenzako wanastarehe..kitu ambacho kinatuuma sana sisi wazazi wako...'akasema

'Baba...'nikataka kujitetea lakini hakunipa nafasi akaendelea kuongea

'Nikuambie ukweli mume wako halijali hilo, la afya yako,... yeye anachojali ni masilahi yake tu, na anataka akukamue mpaka basi,..na sasa hivi utayaona hayo, hatukuombei mabaya, lakini yale tuliyowahi kuyasema sasa utaanza kuyaona kwa macho yako,..huyo mume wako atakusumbua sana...'akasema

'Baba lakini ni mume wangu...'nikasema

'Sawa..ni mume wako,....ngoja tuone itakavyokuwa,….ila ukikwama usiache kutuambia, mimi nitajitahidi kufika kwako mara kwa mara, kulifuatilia hili mimi mwenyewe…’akasema

‘Baba nashukuruni kwa kunijali, lakini nakuomba usisumbuke sana kwa ajili ya hili, sasa hivi mume wangu anaumwa, na naona akikuona wewe anakuwa hana amani, kwa hivi sasa, anahitajia, huruma, na baba sio kwamba sitaki ufike, ila ukifika naomba sana baba usije kuzungumza maneno ya kumweka kwenye wakati mgumu, ongea naye maneno ya kumfariji, asiogope, kama alivyotushauri docta...’nikajaribu kumtetea.

'Hilo sio la kunifundisha, nafahamu sana,...muda utafika nitapambana naye, sio sasa..usiwe na wasiwasi kwa hilo...'akasema

'Nashukuru sana baba...'nikasema

‘Ila kuna kitu nataka uniambie, siku ile nilipofika hospitalini nilisikia akiongea maneno, kama anakuomba msamaha, na akasema kitu kama wewe ulikuwa humjali kitu kama hicho, sikusikia vyema, alikuwa akiongea nini..?’ baba akauliza

‘Baba , ....mgonjwa alikuwa anaongea hivyo ni katika hali ya kuchanganyikiwa tu, kwasababu ya huko kuumwa, yeye alijiona kama ni mtu wa kufa tu, kwahiyo ndio akawa anajaribu kujitakasa, akihisi hili kakosea, basi anaomba msamaha, hata wewe ungelikuwepo angalikuomba msamaha ni katika kuhangaika tu baba…’ nilisema sikuelewa baba alisikia kiasi gani, na docta akawa anaongea baadae akasema

‘Vyovyote iwavyo mimi nataka maelezo,..najua kakuoa akiwa na malengo yake binafsi,..yeye kama hawezi kuishi na binti yangu labda ana mipango yake mingine au alikuwa na ndoto zake nyingine , basi awe muwazi tu, nimegundua mambo mengi ambayo hayafai kwa familia yangu…’akasema

‘Baba mengine ni ya kuharibu bora tuyapuuze tu..’nikasema

‘Sikiliza…anyway,a sitaki nikuumize kwa mawazo, hayo ni yake anatakiwa kuwajibika nayo, sasa.. ngoja apone, sawa poleni sana binti yangu, usijali mimi nitapambana na hili jambo mpaka nione mwisho wake, unasikia, usijali, nipo pamoja na wewe, …’akawa anaongea hivyona kipindi hicho ndio nimepata fahamu.

‘Baba, usiwazie hivyo…mengine yametokea tu, ile iwe sababu , mimi nina imani yatakwisha tu, ni sehemu ya changamoto za maisha, sasa nyie kama wazazi wangu sitaki mnitenge mimi tofauti na mume wangu, ….sipendi hivyo baba…’nikasema


‘Binti yangu usione nasema hivyo, sisi wazazi wako tunakupenda sana, lakini tunaumia, tunajitahidi kadri tuwezavyo ili uondokane na shida hizi, lakini wewe unakuwa mkaidi, sisi tunafahamu tatizo lipo wapi, hich ni kizalia , asili ya hulka ya mtu, hutaweza kumbadili mume wako, abadani…’akasema na mimi nikataka kuongea lakini hakunipa nafasi, akasema

‘Mengi tunayaona lakini hatusemi, lakini kwa hili, hapa lilipofikia, sisi kama wazazi tutalifuatilia mpaka tuone mwisho wake ni nini, ina maana gani ya ndoa eeh, niambie…, na kama nilivyosema awali, sitaki kashfa katika familia yangu…, na anyway, wewe angalia afya yako, unasikia, kama kuna lolote linahitajika niambie….’alisema .

Na leo ndio akanipigia simu akitaka kujua mimi nimefikia wapi, kwani anahitajika kutoa maamuzi kwenye kikao cha wakurugenzi, ..anasema hicho kikao ni muhimu , hata kama mimi sitakuwepo au mume wangu, maamuzi ya wengi yataheshimiwa.

‘Baba mimi naomba usifanye lolote kwenye kampuni ya mume wangu, utoe hija kuwa kwa upande wa hiyo kampuni tusubirie kwanza, …itakuwa sio vyema, hata kama inafirisika, …na madeni yabakie tu, kama wadaiwa wanataka kushitaki waache tu wafanye hivyo, tutapambana huko mahakamani…’nikasema

‘Sio rahis hivyo binti yangu…mimi kama mwenyekiti wa makampuni yote, siwezi kukubali hali hiyo ifikie huko, kuna wakurugenzi wa hisa kwenye hiyo kampuni, wananihoji,…wamewekeza pia huko, unataka niwaambieje…wewe sikiliza, wewe endelea na mume wako, mengine niachie mimi, ninajua ni nini cha kufanya, unasikia eeh,…tuliza kichwa chako, ila mume wako akipona nataka nipambane naye mimi mwenyewe, …hilo sitaki majadala…’akasema

‘Baba…’nikalalamika

‘Kwahiyo leo mimi sitakuja huko , nitakuwa na kikao, na nitakuwa napitia taarifa za uchunguzi, kuhusu mume wako, kuna mengi yamegundulikana, lakini mengine sitaki yawepo kwenye hiyo taarifa, ni aibu, uliweza kuisoma ile taarifa niliyowahi kukupatia ile kila kitu kipo, na mengi ambayo siamini...hebu nikuulize kwanza huyo rafiki yako kwanini kasafiri na mtoto mchanga..?’ akaniuliza

‘Ilibidi afanye hivyo kwa vile muhula wa masomo umeanzia hapo, na hakutaka kusubiria, tukaona ni bora tu aende….na huko kuna watu watamsaidia hatapata shida…’nikaongea kujifanya na mimi nimehusika kwenye maamuzi ya rafiki yangu kuondoka.

‘Una uhakika,…??... sio kuwa kakimbia,…?? anaogopa ukweli ukija kugundulikana awe keshajipanga vyema kimaisha, binti yangu hao watu wanakutumia vibaya, huyo rafiki yako, anataka ahakikishe hata likitokea jambo awe anajiweza mwenyewe..sawa sio mbaya, lakini kwanini aharibu nyumba iliyombeba..’akasema

‘Baba hayo mengine hata sitaki kuyafikiria kwanza,…’nikasema

‘Sawa sawa, usijali…nitapambana na hao watu mimi mwenyewe, ilimradi…’akasema na kukata simu.

**********

Mume wangu akawa hataki mimi niondoke karibu yake , ikawa ni kero, ina maana nisitoke au kwenda mbali na yeye, hata akija mgeni, anataka atoke awe pembeni nikiongea na mgeni,..kwa maagizo ya docta nikawa nafanya kila atakavyo, ila moyoni, pamoja na huruma kila nikiwazia hayo yanayosemwa nilimuona mume wangu kama sio yule ninayemfahamu.

Nilitaka niwe na nafasi ya kuipata ile taarifa aliyotayarisha rafiki yangu, lakini sikutakiwa nisome mbele ya mume wangu,..ikafika muda nikaagiza niletewe hiyo taarifa nyumbani,…lakini muda gani wa kuisoma nikawa sina,

Ikatokea siku moja mume wangu amelala kutokana na madawa nilikuja kugundua akinywa hizo dawa anaweza kulala hata saa nzima au zaidi..na siku hiyo ilipoletwa hiyoo taarifa ya rafiki yangu, nikaona nitumie huo mwanya..., ndio nikaanza kuipitia hiyo taarifa ni ndefu kidogo...;

Taarifa ya uchunguzi wa ajali ya mume wangu, aliandika jina la mume wangu, na akaelezea ilivyotokea, kuwa ni sababu ya mwendo kasi, katika kukata kona akakutana uso kwa uso na lori,..akajaribu kulikwepa, na gari likapinduka na kugeuka mara mbili…
Dereva aliwahi kutoka, hapo haijulikani aliwezaje kutoka katika hali hiyo, ni kwa uwezo wa mungu tu.

Je kipindi ajali hiyo inatokea mlengwa alikuwa katokea wapi, taarifa inasema alitokea kazini, akapitia sehemu za wateja wake, ndivyo alivyoaga kazini, lakini akiwa kwa wateja wake, akaamua kwenda sehemu nyingine …(yawezekana,) akaandika hivyo na kuzungushia hayo maneno,...

Kuna kauli za watu kuwa kwa muda huo ndio alimua kwenda kumuona mzazi, huyo mzazi ni nani, (bado sijamtambua)!.

Hili la mzazi halina uzito, ila limetokana na maelezo ya siku kadhaa nyuma kuwa aliondoka kazini akisema anakwenda kumuona mzazi, hospitalini, huyo mzazi hospitalini hakuweza kugundulikana ni nani..(kwahiyo ili kupata jibu kamili, aulizwe yeye mwenyewe)!

'Ssshti...'nikajikuta nikisema hivyo.

Kabla hajapatwa na ajali, gari lilisimamishwa kwenye geraji, sehemu ambayo pia panaoshwa magari kwa pembeni yake..., na wakati gari lake linafanyiwa usafi, yeye alikwenda mgahawani, kupata chochote,..lakini hakunywa kilevi…akiwa hapo, inaonekana alipokea simu , ya haraka, na kutoka hapo akaenda kulichukua gari kuwa muosha magari,

Muosha magari anasema ni kweli, aliwahi kuosha gari la mtu huyo, na ...hata la mdogo wake, na anachokumbuka, yeye, mlengwa, aliondoka hapo kwa mwendo wa kasi, lakini sio kasi kubwa, kama ilivyokuwa huko alipopatia ajali... ila alionekana ana haraka, hata chenji ya pesa yake hakuichukua.

Kwahiyo hapo akahitimisha kuwa,.simu aliyopigiwa inaonyesha ilikuwa na jambo, la kumfanya aharakishe kufika nyumbani na sivyo kama watu wanavyosema kuwa huenda alikuwa akikimbia jambo la hatari, hata hivyo bado haijafahamika simu hiyo ilitoka kwa nani, na kwanini aliharakisha hivyo (haijafahamika bado). Na huyo aliyefika kwake ni siri yake...akaandika hivyo!

‘Hii taarifa haina maana kabisa..’nikasema ni kuiweka pembeni.

Na wakati nawazia hiyo taarifa : huyo mzazi ni nani huyo au ni nani huyo alimpigia simu mume wangu na kumfanya awe na haraka kihivyo, ndio akaja docta rafiki, akanikuta nipo kwenye mawazo, akaniuliza kuna nini kimtokea…

‘Mambo ya kazi tu…na nilikuwa naipitia ile taarifa aliyoacha rafiki yangu, lakini hakuna alichokifanya, sio kawaida yake, ni taarifa ya mtu ambaye hajui kazi kabisa, sio yeye aliyeitayarisha…’nikasema

‘Hiyo taarifa ina muhimu gani kwako kwa hivi sasa…?’ akaniuliza

‘Bado nawajibika kuufahamu ukweli, najua baada ya hili, mume wangu akipata nafuu, nitahitajika kukaa kikao na baba, na wawekezaji wengine, kuna maswali mengi nitaulizwa, nitayajibu vipi kama siufahamu ukweli..’nikasema

‘Ukweli kuhusu mumeo au ukweli kuhusu maswala ya kikazi…ama kuhusu mume wako yeye alishakuambia kila kitu, sasa kama hayo yanaweza kuingiliana na kazi yake, ni jambo jingine linaelezeka... kwa hivi sasa mimi siioni kwanini unabeba mzigo kabla haujatua kichwani mwako…utachoka hata kabla hujahisi uzito wake, tulia kwanza..’akasema

‘Unajua siwezi nikaamini yale aliyoongea mume wangu moja kwa moja, na hakuwahi kusema ni kitu gani alikifanya, mpaka afikie kuniomba msamaha..tunahis tu..pale aliongea akiwa kachanganyikiwa, sawa yawezekana ni hilo kuwa kafanya madhambi…lakini mbona taarifa ya rafiki yangu haijabainisha hilo. Sawa naweza kuhitimisha hivyo kuwa ni kweli, labda ni kweli, je hilo latosha tu, hapana ni lazima niwe na ushahidi....’nikasema

‘Nikuambie kitu hiyo taarifa ya rafiki yale lengo lake ni kuvuta muda, kuhakikisha kuwa anakuchanganya ili yeye aweze kutimiza haja zake,..na huyo mzazi mume wako aliyewahi kuaga kuwa anakwenda kumuona, sio mwingine ni huyo huyo rafiki yako, amini usiamini huo ndio ukweli….’akasema docta

‘Sawa, tunaweza kusema ndivyo hivyo, haya nipeni ushahidi, hapa anasema mdogo wake siku hiyo alifika pia kuosha gari,...swali gari lipi, na muda gani, hajaelezea hapa…kama kweli ni yeye, maana kama ni kweli, basi, huyo sio rafiki yangu ninayemfahamu mimi...'nikatulia kidogo.

'Mimi sio mjinga wa kukataa kauli za watu...najua nahisi hata mimi hivyo hivyo, ….lakini siwezi kukubali hivi hivi tu, na kuchukua hatua hiyo kubwa niliyodhamiria moyoni, maana ni kweli nitafanya hivyo,...je nichukue haua hiyo bila ya kujirizisha, ushahidi, upo wapi, unanielewa hapo,…au wewe unao huo ushahidi.?’ nikauliza

‘Kwasababu rafiki yako anajua kafanya makosa, anajua yeye alishirikiana na mume wako kulifanikisha hilo, ...'akasema

'Ushahidi...'nikasema

'Ndio tunaweka nadharia hii sawa,...kuna kitu nataka unielewe, kuwa huenda rafiki yako, alipanga hivyo, au kuna kitu kilimsukuma kufanya hivyo, na kitu hicho akakitumia kama ngao yake, lakini yanayokuja kutokea sasa imekuwa kinyume na alivyotarajia, ndio maana kaamua kukimbia ili kuepusha shari, naanzia hapo…’akasema docta.

‘Mimi nataka ushahidi maana baada ya huo ushahidi, mimi nitachukua hatua kali, hutaamini, na sitaweza kurudi nyuma kwa hilo..bila kujali ni nani, sitak nadharia za kuhisi hisi, wewe ni docta, au... …’nikasema

‘Sasa hebu nikuulize utachukua hatua kwa nani, kwa mumeo au kwa huyo rafiki yako...maana kam ni kutenda kosa wametenda wote, ?’ akaniuliza

‘Ndio maana nataka ushahidi..na nikiupata huo ushahidi…, sitaojali kuwa ni mume au rafiki yangu, yoyote ataumia,…na kila mtu ataumia kutegemeana na kosa lake yeye mwenyewe, wewe ngoja utaona nitakachokifanya…’nikasema

‘Kwa maelezo ya mume wako, wewe ulishirikiana na rafiki yako kulifanikisha hilo, sasa sijui kwa vipi, yeye kadai kuwa wewe ulimtuma, afanye hivyo ni kweli si kweli, ulisikia mwenyewe akiongea pale hospitalini, …’akasema docta, kama ananiuliza

‘Mimi nina kichaa!!!…hahaha, hivi kweli inaingia akilini hiyo, mimi nimtume rafiki yangu akazini na mume wangu, hata wewe unaweza kuliamini hilo…?’ nikauliza

‘Ili kuweza kulijibu hilo, labda nikuulize wewe, je hamkuwahi kukaa na rafiki yako mkapanga kuwa labda rafiki yake ajitahidi kupata mimba, kwa...sio lazima useme kwa mume wako, kwa yoyote, labda yeye akaona kwa mume wako, au...hatuna uhakika bado hapo, nasema hivyo kukuuliza wewe...?’ akauliza

‘Wewe uliwahi kuongea na rafiki yangu akakuambia hivyo...?' nikauliza

'Hapana, baada ya kujifungue amekuwa makini sana, hata nikiongea naye ahataki nimuulize chochote,...'akasema

'Sasa umelitolea wapi hilo, kuwa mimi nimtume rafiki yangu akazini na mume wangu, au sio…ndio una maana hiyo, kuwa mimi nilimshauri hivyo, na ...yeye akaona kwa mume wangu ndio kwenye usiri ..huo ni ujinga haliji akilini kabisa, rafiki yangu mwenyewe, sawa na ndugu yangu aje kufanya hivyo...ingelikuwa wewe ungelifanya hivyo kweli hebnu jiulize kwanza kabla ya kutoa nadharia yako?’ nikauliza

‘Yawezekana mlikaa mkaongea kwa namna ambayo aliona akifanya hivyo haitaleta walakini, lakini sio kwa moja kwa moja kuwa akafanya hivyo kwa mume wako, yawezekana ushauri wako,..ndio uliomsukuma kufanya hivyo labda…’akasema

‘Hakuna kitu kama hicho,..kama kweli yeye ni rafiki yangu ananijali na kujali masilahi ya familia yangu, asingeliweza kufanya kitu kama hicho, yeye anafahamu mambo mengi ambayo kama mimi, au mume wangu akiyafanya hakutakuwa na huruma kwa baba, hilo analifahamu, na anamfahamu sana baba yangu, ..ndio maana mimi siamini kuwa kafanya hivyo, ndio maana nataka ushahidi, baba anauhitajia pia huo ushahidi.., …’nikasema

‘Baba yako keshajua hilo, kuwa huenda huyo mtoto wa rafiki yako kazaa na mumeo,a u mdogo wa mume wako, keshaniulizia hilo, akataka ushauri wangu kama docta , mdogo wa mume wako, hataki kusema ukweli, ukiongea naye, unaweza ukahisi ndio yeye, kwa jinsi anavyojiuma uma, lakini lengwa mkubwa ni mume wako, unahisi ni kwanini...?’ akauliza

‘Baba taarifa alizo nazo ni kama nijuavyo mimi..bado anafuatilia, kasema kama ni kweli, basi, na yeye atakuwa na maamuzii yake, mimi sitaki kusimamia mambo ya wazazi wangu maana nafahamu hukumu yao ni nini…mimi nina namna yangu ya kuhakikisha hao watu, kama ni kweli, wanapata kitu ambacho hawataweza kukisahau maishani mwao…’nikasema

‘Hebu niambiea ukweli wako..utachukuaje hukumu, wakati labda na wewe unahusika, ni kwanini hutaki kusema ukweli kuwa wewe na rafiki yako mlikaa mkakubaliana jambo fulani..?’ akauliza

‘Hata kama tulikaa tukaongea tukajadili mambo, lakini tunakaa sana, tunaongea sana, lakini sio kwa ….hapana, siwezi mimi na akili zangu nimwambie akatembee na mume wangu, na yeye...'mara kukawa kama kuna sauti, nikahisi huenda ni mume wangu, lakini kwa hizo dawa, bado atakuwa kwenye usingizi.

'Anaweza kufanya hayo kwa malengo fulani, au ...kutokana na jinsi mlivyoongea, mimi sijui....na kama anafahamu kuwa kitu kama hicho kikitendeka, yaweza kuharibu kabisa ndoa yako, au..mimi sijui, ...ni kwanini afanye...huoni kuwa kuna kitu ndani yake, na baba yako ndio anakitafuta...'akasema


‘Mimi sijui, ila nijuavyo, baba hataki kashfa, hatua ya kwanza ambayo nahisi ataanza nayo, akiugundua ukweli, ni yeye kutoa hisa zake, na kujitoa kwa baba kwenye kampuni ya mume wangu, ndio kuiua , maana baba ndiye mdau mkubwa wa hiyo kampuni...'nikasema

'Na kuna madeni,...'akasema

'Ni kweli hata ukiangalia hii taarifa kampuni hiyo ina madeni, ya nje, baba mwenye anamdai pesa nyingi…je hao wanaodai wengine watalipwa na nani…kiufupi kampuni ya mume wangu haipo…na hili ni moja ya mambo yanayomuumiza mume wangu..nimemuambia baba, na sio hayo anayofikiria yeye,…’nikasema

‘Je baba yako alisemaje, hawezi kusaidia vyovyote..?’ akauliza

‘Kasema anaweza kusaidia iwapo, hakuna kashfa, kama kuna baya, kuna kshfa mbaya, kaifanya mume wangu yenye kutia dosari, familia yake hataweza kusaidia kwa lolote lile, na atajitoa, na kudai pesa zake zote, na atachukua hatua nyingine kubwa zaidi…’nikasema

‘Na wewe huwezi kusaidia chochote..?’ akauliza docta

‘Mimi, hahaha...siwezi, maana hata mimi kampuni yangu haifanyi vizuri..na tatizo ni kuwa kampuni ya mume wangu, inataswira fulani kwa wateja wangu pia, sijui kwanini, kuna wateja wangu wameanza kukimbia kisa ni kutokana na mwenendo wa kampuni ya mume wangu,.. unajua siasa za biashara zilivyo, kuna vita ya chni kwa chini, katika ushindani wa biashara, wateja wengine, hutafuta visa tu,…’nikasema

‘Je unahisi kilichotokea kwa mume wako ni sababu hizo za kibiashara, au kuna jingine limajificha…?’ akauliza

Nikaichukua ile taarifa, nikamuonyesha naye akaipitia halafu akasema;

‘Unaona sehemu zote alizoweka mabano kuwa haijakamilika ni zile ambazo zinamgusa yeye…na simu ya mume wako mmh, haiwezi kusaidia kitu, ...lakini itasaidia nini hapa, kuna mambo kayafunika kiaina, ila haya kuwa mumeo anadaiwa, kampuni haiwendi vizuri, kaongea ukweli, na kayachukua kama sababu kubwa, huoni ni kitu kama kimelengwa kinamna fulani..?’ akaniuliza

‘Simu ya mume wangu haijulikani wapi ilipo hata yeye anasema hakumbuki, huenda iliungua kwenye gari, au iliibiwa..na nimejaribu kuulizia watu wa mitandao kama wanaweza kunisaidia wamesema hilo ni vigumu kwao…’nikasema

‘Ulishaongea na huyu muosha magari, kuhakikisha kuwa huyo aliyeondoka hapo kweli alikuwa mume wako au ni mdogo wa mume wako, maana hapa kwenye taarifa ni kama kulikuwa na watu wawili, huyo hapa alikwenda kupata kitu mgahawani, na huyo aliyekuja kwa rafiki yako ni nani.?’ akaniuliza

‘Huyo muosha magari, hayupo…kasafiri, na hata simu yake haipatikani…’nikasema

‘Je sio mbinu za kumuondoa hapo Dar….hana jamaa yoyote anayemfahamu, tukajaribu kumfuatilia, nahisi hapa tunaweza kugundua kitu..?’ akauliza

‘Sijaweza kufuatilia kiasi hicho, nitategemea hili angalifanya huyo rafiki yangu, lakini ndio hivyo…kama unavyoona, hii sio taarifa ya mtu aliyesomea kazi hiyo, ni kama kaandikiwa na mwanafunzi wake..’nikasema

‘Huku kwenye maelezo, ya uoni wake, katupia lawama ndoa yenu kuwa inaweza ikawa sababu nyingine, unahisi kuna ukweli wowote hapa…?’ akauliza

‘Sizani, kama kuna ukweli, kwanini hilo lisitokee nyuma, lije litokee siku hiyo..nakiri kuwa mimi nina madhaifu yangu, lakini haijafikia hadi yatendeke hayo,…na ndio maana bado sijaamini..’nikasema

‘Hujaamini nini sasa hapo..?’ akauliza

‘Kuwa kwanza ajali hiyo inatokana na matendo ya nyuma, pili, hapa kuna matatizo ya mume wangu na kampuni yake kwa upande mmoja, na huku kuna huyo mtoto wa rafiki yangu, lipi lenye uzito, tatu.... rafiki yangu anahusikanaje na mume wangu kwenye kusababisha kampuni ya mume wangu kufikia hapo ilipo, maana baba kalisema hilo. ukiangalia kuna mkanganyiko, na kwanini mdogo wa mume wangu ananipiga chenga, unajua ananikwepa sana, huoni anaweza kuhusika kama sio yeye…’nikasema

‘Baba yako anasemaje kwa ujumla wake..?’ akauliza

‘Baba yeye hataki kusema lolote mpaka sasa, anasema kuna taarifa anaisubiria, akiipata ndio itampa mwanya wa kusema jambo, ila kaahidi kulifuatilia hili tatizo la familia yangu na kampuni zote, hadi mwisho wake, na kasema sasa hatarudi nyuma, …’nikasema

‘Atasamehe tu, nyie ni watoto wake,…maana vyovyote iwavyo, itasaidia nini sasa eeh, atamfukuza, atavunja ndoa yenu, unaonaeeh, hawezi, na ukiangalia kwa makini,.. kampuni ya mumeo ikifa, mumeo atakuwa anategemea ajira yake tu…ambayo haiwezi kumkidhi haja zake,..na nimesikia huko kazini kwake kuna matatizo pia ni kweli…?’ akauliza

‘Nimesikia sasa hivi na kusoma kwenye taarifa ya huyo mdada, nilikuwa sijui, kiukweli kuna matatizo,…sijui alifanya nini huko…’nikasema

‘Mdada hakuelezea hilo…mmh, hapa…ngoja nisome, anasema, alikopa pesa, na kujikopesha bila idhini,…mmh, kwanini alifanya hivyo, …hapa anasema bado uchunguzi unaendelea…sasa mume akifukuzwa itakuwaje na kampuni ndio hiyonayo inayumba…huo sasa ni mzigo wako ambao sizani kama utaweza kuubeba…’ akasema

‘Hilo sio tatizo kwangu, yeye ni mume, na mengi kajitakia yeye mwenyewe, lakini je hayo ndio yamesababisha hayo yote, hiyo ajali sabau ni hayo, au ...na mmh, bado kichwa changu kina giza, ?’ nikauliza

‘Jibu hasa la haya yote tutalipata kutoka kwa mume wako,... je atakubali kusema ukweli…?’ akauliza

‘Akipona, ni lazima asema ukweli, nitahakikisha hilo analifanya na nitajua la kufanya, wewe subiria tu…’nikasema

‘Lakini usije kuongea chochote kwa hivi sasa, wala kumuuliza..’akasema docta

‘Nafahamu hilo sana, hapa nipo kama mtumwa, kila analotaka nalifanya, kila kitu kimesimama, nitafanyaje, lakini kuna ukweli huo nautaka, ..hata kabla hajapona, nautaka niufahamu, je ni kweli kuwa mume wangu kazaa na rafiki yangu, nikiwa na uhakika na hilo, basi mengine yote hayana maana kwangu, ….mimi na baba tutakiwa hivi, …’nikasema nikishikisha vidole viwili kwa pamoja.

Nikashtuka kusikia mtu anakohoa nyuma yangu,, …nikageuka na kumkuta mume wangu akiwa kwenye kigari chake anatuangalia …akiwa anatokea huko alipokuwa amelala…nikamuangalia mume wangu, alionekana kakasirika kakunja uso..

‘Kwanini umefanya hivyo mume wangu…unatakiwa ulale, hizo dawa zinahitajia wewe ulale, unakwenda wapi sasa…?’ nikamuuliza lakini hakunijibu, akawa anakiendesha kigari chake na kuelekea nje

‘Kasikia nini…?’ akauliza rafiki yangu

‘Sizani….’nikasema, nikiwa sina uhakika.

‘Basi ngoja nikaongee naye,..na wewe hakikisha hiyo taarifa unaificha asije kuiona, pili, nataka tuje tuongee mimi na wewe baadae…nataka.., nikusaidia kulimaliza hili jambo, nitahakikisha unaufahamu ukweli wote, na ushahidi unaoutaka, ila uniahidi jambo…’akasema

‘Jambo gani…?’ nikauliza na mara mume wangu akawa ananiita huko nje..WAZO LA SIKU: Maisha yalivyo, inafikia muda inabidi ukope, ili kukidhi haja fulani, ni muhimu tukikopa tujue jinsi gani ya kuja kulipa deni la watu, wengine hukopa tu, akisema tutajua huko mbele kwa mbele, na ukianza kudaiwa, unakimbia, unajificha au unajibu jeuri. Tukumbuke kuwa deni ni deni, na deni haliishi mpaka ulipe au mwenyewe kwa ridhaa yake akusamehe. Tusipende kudhulumu tukidaiwa, deni halitaondoka hata ukiondoka hapa duniani,..utaenda kulikuta huko kwa hakimu wa mahakimu.


Docta aliposikia mimi naitwa, akasema

‘Ngoja mimi nikaongee naye kwanza…’akasema na nilitaka kumpinga maana mume wangu kaniita mimi, ni wajibu wangu kuitika wito wake kwanza, lakini docta akaniwahi na kukimbilia huko nje alipo mume wangu, ikabidi nisubirie tu.

Nikiwa nimebakia pale peke yangu, niliweza kuipitia ile taarifa ya rafiki yangu kwa makini, na mpaka nafika mwisho nilianza kubadilika, kuwa huenda wanayoongea wenzangu yana ukweli fulani. Kwenye hii taarifa rafiki yangu alijaribu kama kuficha jambo, na kujihami kwa namna fulani, japokuwa haionyeshi wazi wazi kuwa kweli anahusika ..

Kwa maelezo ya taarifa hiyo, Muosha magari anasema aliosha gari la mume wangu, na pia la mdogo wa mume wangu kuonyesha kuwa wote wawili walifika hapo siku hiyo, lakini docta anasema mdogo wa mume wangu alikuwa kwake wakiangalia mpira,..je muda gani alitoka hapo na kwenda huko…. nikjiuliza.

Hapo nikaona kuna muhimu wa kuonana na mdogo wa mume wangu kwa haraka iwezekekanavyo, lakini nisingeliweza kuondoka hapo, nikachukua simu na kumpigia huyo shemeji yangu, lakini simu haikupokelewa.

‘Nitampata tu….’nikasema na muda huo docta akaingia akisukuma kile kigari cha mume wangu, na mume wangu alikuwa kakaa kinyonge, akitikisa kichwa kama kukubali jambo fulani kwenye maongezi yao..na walipofika ndani docta akasema;

‘Tumemalizana na rafiki yangu, …mimi nataka kuondoka…’akasema

‘Sawa mimi nipo na mume wangu, sikusindikizi…’nikasema

‘Ni wajibu wako, lazima mleane kwa shida na raha…’akasema

Mume wangu akawa anakiendesha kigari chake peke yake na kuelekea chumbani, nikamuangalia docta, na docta akaniashiria nimfuate mume wangu, basi ikabidi niagane na docta, yeye akaondoka, na mimi nikamfuata mume wangu ndani.

‘Mbona unakuja huku, mgeni anabakia na nani, msindikize mgeni au..?’ akaniuliza

‘Anaondoka, nimeshaagana naye, kaondoka…’nikasema

‘Mimi nipo safi mbona, sasa hivi nataka nilale tu, nasikia kulala tu, nahisi macho mazito…’akasema

‘Uliamuka kabla dawa haijaisha nguvu yake…’nikasema

‘Niliota ndoto mbaya…’akasema

‘Ndoto gani…?’ nikamuuliza

‘Docta, ananiibia mke wangu…’akasema sasa akiniangalia huku anatabasamu kama utani vile

‘Hahaha, kama nikukuibia basi angelikuibia zamani, sio sasa, keshachelewa, na uzee huu anatakia nini tena kwangu, hizo ni ndoto za shetani usiziamini…kwanza yeye ana mke wake mnzuri..’nikasema

‘Mhh,..ni kweli lakini wewe ni mnzuri zaidi yake…, na .. na una mengi ambayo mke wake hana…’akasema

‘Kama yapi, …?’ nilimuuliza lakini nikiwa na tahadhari.

‘Mali, familia yako ina julikana…na mengine mengi..’akasema

‘Na wewe umenioa kwa hayo pia, au sio…?’ nikauliza

‘Ofcourse yes, uzuri wako, na hayo mengine vilinifanya nijisikie nina mke wa maana sana,..ndio hivyo, mitihani hii inanifanya nijutie kwa niliyoyafanya, …lakini nakuahidi mke wangu hayo yaliyopita sitarudia tena…’Nilitaka kumuuliza yapi kayafanya, lakini nikaogopa, haitakiwi, nikabakia kimia.

‘Sikiliza mke wangu, ngoja nipone, nina uhakika nikipona, na nguvu zangu zikirejea vyema, kila kitu kitakuwa sawa, niamini, kila kitu kitarejea kama kilivyokuwa awali…,nimeligundua kosa langu....’akasema


‘Hilo neno mume wangu…, utapona tu, usijali…’nikasema

‘Niahidi mke wangu, kuwa hutaniacha…’akasema hivyo na kunifanya nishtuke kidogo, ni kauli yenye utata, sikufahamu ni kwa muda huo au ana lengo gani, lakini sikuruhusiwa kuanzisha mijadala, na pia, sikupenda kusema uwongo

‘Mume wangu dawa itakuwa haifanyi kazi, tukiendelea kuongea, wewe lala kwanza, umeshaharibu kwa kuamuka mapema, sasa inabidi ulale tu…ukiamuka tutaongea, unasikia, usipuuze maagizo ya docta, ukifanya makosa hutapona na ndoto yako haitatimia..’nikasema

‘Ndoto…!’akasema kwa mshangao

‘Ndio za kuendeleza miradi yako, au sio…’nikasema

‘Haya bosi, ngoja nilale..kweli nasikia kulala, lakini sitaki niote hiyo ndoto tena, lakini naomba usiondoke hapa kitandani kabisa, nataka ukae hapa karibu yangu, nikiamuka tuongee, nataka niongee na wewe mambo mengi mazuri, ma-zzzrrr..’akasema

‘Haya lala…’nikasema nikiwa nimekaa karibu yake, na baada ya muda nikasikia akitoa ile sauti ya kuonyesha kuwa kweli kalala.

***************

Siku nyingine, nilikuwa nimekaa nyumbani, sebuleni, na mume wangu alikuwa amelala chumbani baada ya kupata dawa. Na nilipohakikisha amelala, nikaona nitoke kidogo nje, kitahadhari, maana akiamuka akaona sipo karibu yake, ni mtihani,..nikasema leo nataka nifanye jambo, angalau nitoke hata kufika madukani,.

‘Nani huyo tena…nikasema, niliposikia mtu anagonga geti la nje

Muda huo nilikuwa varandani nakagua kuwa kila kitu kipo sawa, kwa vile najua kuwa mfanyakazi wetu wa ndani yupo, atafungua geti sikuhangaika kutok nje, lakini haikuwa hivyo, mfanyakazi alikuwa hayupo karibu na huyo mtu akawa anaendelea kugonga,..

‘Kaenda wapi huyu binti…’nikawa naongea peke yangu, nikachungulia kupitia dirishani, na muda huo, huyo mtu akawa anafungua geti mwenyewe, kabla sijajiuliza ni nani, mara akatokea mfanyakazi wetu, kumbe alikuwa anafanya usafi sehemu za ndani.

‘Nani kagonga geti na sasa anafungua geti mwenyewe…?’ nikamuuliza

‘Hata sijui ni nani ..ngoja nikaangalie…’akasema na kukimbilia nje.

Haikupita muda, nikasikia watu wanaongea huko nje na vicheko…nikaingiwa na hamasa ya kumtambua huyo mtu ni nani, maana ni sauti ya kime, nikachungulia dirishani, alikuwa ni mdogo wa mume wangu.

Mdogo wa mume wangu mhh, kajileta…!!

Kwa haraka nikatoka nje, nilitaka nimuwahi, kwani sikutaka mtu yoyote kumsumbua mume wangu, japokuwa nafahamu kuwa mdogo wake huyo, akijua kaka yake kalala hawezi kumsumbua, kwani anafahamu utaratibu ulivyo,japokuwa sijaonana naye muda sasa, lakini moyoni nilikuwa na hamu sana ya kuongea na huyu mtu!

‘Hii ndio nafasi pekee…’nikajisemea kimoyo moyo nikitokeza kwenye mlango.

Sasa hivi nakuwa na tahadhari, sio kama zamani, mume wangu anaweza kunywa hizo dawa ghafla akaamuka, na akiamuka huwa hapendi kukaa ndani, anapenda kuzungushwa nje na kigari chake cha kukokotwa. Ndio maana nikaona nimuwahi mapema huyu mtu kwa tahadhari.

Nilihakikisha nimeusindika mlango nyuma yangu, na sasa nikawa naangaliana uso kwa uso na shemeji yangu huyu, alikuwa mlangoni alitaka kufungua,.. inaonekana ni kama vile hakutarajia kuniona hapo nyumbani, akabakia mdomo wazi akishindwa hata kuongea, nikatabasamu ili kumuondoa wasiwasi, na yeye kwa aibu akatizama chini..

‘Habari yako shemeji, mbona unaonekana kama umeona kitu cha kukuogofya, hukutarajia kuniona mimi hapa nyumbani nini, au una wasiwasi gani, naona unajaribu kunikwepa kinamna?’ nikamuuliza

‘Ni kweli, nilijua labda haupo, labda umetoka kwenda kazini kidogo, sasa kazi inakuwaje shemeji, …mmh, huu ni mtihani, lakini yana mwisho au sio, si kukwepi shemeji ni shughuli tu....’akasema.

‘Kuna nini kinaendelea kati yako wewe na mfanyakazi wangu?’ nikamuuliza, nilimuuliza hivyo nikiwa na maana yangu, japokuwa ulikuwa ni utani.

‘Hakuna kitu shemeji, hahaha, shemeji naye bwana, na mfanyakazi wako hakuna kitu kama hicho kabisa ...mimi nimekuja kwa ajili ya kumwangalia kaka, na kwa muda sasa sijafika, nilikuwa nimesafiri kidogo, na unajua nikiwepo basi inabidi nije, na ikibidi nikae hapa, ili nisaidie saidie,..na kiukweli mnisamehe sana, sijafika muda kumuona mgonjwa,....’akasema,

Nilimwangalia alivyokuwa akipata taabu ya kutaka kujieleza , na baadaye nikasema

‘Usijali shemeji nakutania tu, karibu, lakini kaka yako kalala na dawa anazotumia hatakiwi kusumbuliwa, unasikia sana…’nikasema.

‘Kama kalala basi …niwasalimie kidogo niondoke zangu, …nilijua nitakuta keshaamuka,..jana alinipigia simu kuwa nijitahidi tuonane…’akasema

‘Alitaka muonane mbona hajaniambia..?’ nikauliza kwa mshangao, hata yeye akaonekana kushangaa, na akasema

‘Kwakweli mimi sijui, ila alinipigia, simu, tukawa hatuelewani, mawasiliano, maana nilikuwa kwenye gari, akasema nijitahidi nionane naye…’akasema

‘Ok, labda kapitiwa kuniambia, hamna shida, ngoja tuongee kwanza

‘Ndio shemeji niambie…’ akasema

‘Unajua shemeji, wewe ni sawa na mdogo wangu, ....nakuona hivyo licha ya kuwa wewe ni shemeji yangu, ndio maana wakati wote nimekuwa nikihakikisha kuwa maisha yako yanakuwa bora, ili uweze kusimama kwa miguu yako mwenyewe, na natumai hayo yameshakamilika...na hapa ni nyumbani kwako, wakati wowote unaruhusiwa kufika, nilishangaa tu, kukuona kama unani kwepa, hasa pale hospitalini, nikajiuliza kuna nini...’nikasema.

‘Hapana sijakukwepa shemeji hizi hisia zako tu, kwanini nikukwepe..’akasema.

‘Hakuna tatizo kaka yako ana maendeleo mazuri tu, ila kuna mambo muhimu sana tunahitajika kumsaidia, …ndio najua mengi ni majukumu yangu, maana huyo ni mume wangu, au sio, ....’nikasema.

‘Ni kweli shemeji, ila kama kuna lolote la kusaidia wewe niambie tu …’akasema.

‘Usiwe na wasiwasi, sio jambo kubwa sana,..’nikasema, nikimuelekeza huyo shemeji yangu twende bustanini, kuna sehemu maalumu tumetengeneza ya kuongelea, upepo wake ni mwanana, kama upo ufukweni mwa bahari, na mume wangu hupendelea kuja kukaa hapo.

‘Tuletee vinywaji, na hakikisha kuwa mume wangu akiamuka unaniita mara moja...unasikia.’nikasema.

‘Nitafanya hivyo dada.....’akasema.


*********

‘Shemeji, nataka tuyafupishe mazungumzo yetu iwezekanavyo, kwani kaka yako akiamuka natakiwa niwe naye karibu, kwahiyo nakuomba nikikuuliza mambo fulani fulani ujitahidi kunijibu kwa ufasaha, bila ya kuogopa....’nikamwambia.

‘Uliza tu shemeji.’akasema.

‘Ninachotaka kukuuliza ni mambo ya kawaida tu usiwe na shaka...’nikasema.

‘Sawa nakusikiliza,...lakini kama ni kuhusu kaka, mimi sijui lolote...’akaanza kwa kujitetea.

‘Usijali,....wewe utaongea tu kile unachokifahamu, sio swala la kesi au swala la kulazimishana, kitu ambacho hukijui hukijui,…ila haya yote nayafanya kwa manufaa ya kaka yako…’nikasema

‘Ni kweli….’akasema

‘Mimi,sizani kama wewe unafurahia hiyo hali aliyokuwa nayo kaka yako, na sizani utataka hilo litokee tena, ina maana ni lazima na sisi kama tunamjali tuone tunamsaidiaje, na kabla ya hilo tujaribu kuona kama kuna sababu iliyosababisha hilo kutokea, ili lisije kutokea tena, umenielewa hapo....’nikasema.

‘Kwakweli shemeji mimi sifurahi kabisa hiyo hali, kaka na wewe ni watu muhimu sana kwangu, wazazi wetu kama unavyowafahamu, hawana mbele wala nyuma, wewe ndiye umeisaidia familia yetu kupitia kwa kaka,sasa naogopa sana kaka asije akaondoka..sijui itakuwaje, japokuwa nimeanza maisha lakini bila ya nyie bado najiona sina uhakika wa maisha,...’akasema.

‘Basi kama unafahamu hivyo ni vyema, tukamsaidia kaka yako, kwani japokuwa kiafya anaendelea vyema, lakini mpaka sasa sijajua ni nini kilichomfanya hadi afikie hapo, je ni jambo la dharura tu, au kuna jambo jingine ambalo huenda bado lipo, na kama lipo ni nini, ,..’nikasema na hapo akakaa kimia tu.

‘Unaposema hivyo shemeji unahisi kaka kapatwa na hiyo ajali kutokana na jambo fulani au, mimi nilijua kuwa ni ajali ya kawaida tu, ambayo anaweza kupatwa mtu yoyote’ akasema.

‘Ajali ni ajali ndio, lakini kuna ajali inakupa maulizo mengi kutegemea ilivyotokea, ndio maana nataka nikuulize wewe ambaye muda mwingi akirudi kazini, au…ikitokea dharura mnakuwa naye,…’nikasema.

‘Shemeji mimi sio kwamba mchana kutwa nakuwa naye, unafahamu hilo, kwani hata mimi ninakuwa kwenye mishe mishe zangu,... na mimi najaribu kutafuta jinsi ya kusimama mwenyewe... wakati mwingine huwa nafanya kazi za kaka, lakini sipendi mimi nifanye kazi kwenye ofisi yake, kama tulivyowahi kuongea..’akasema.

‘Ni kweli, sasa turejee kwa kaka yako, tumsaidie, kuna onekana kuna tatizo, na hueda tatizo hilo lipo nje…kuna kitu kinamsumbua, na huenda kakuitia kwa hilo, kaka yako hatakiwi awaze sana, ndio maana najitahidi kuchuja kila jambo, unanielewa, sasa hebu uwe muwazi kwangu, hajakuambia anakuitia nini, au huna fununu ya jambo fulani…’nikasema

‘Nijuavyo mimi , biashara za kaka, huko kazini zilifikia kubaya, hakuna wateja, ..na ikawa watu hawalipo madeni, kwahiyo na yeye akawa hawezi kulipa madeni, hilo likawa linamsumbua sana, na mara nyingi ananituma kwa wateja wake kufuatilia madeni, labda ndio hivyo…’akasema

‘Unaona vitu kama hivyo mimi nilikuwa sijui, haniambii,..’nikasema

‘Kaka huwa ni msiri sana, hata akiwa na shida hapendi kusema huwa anapambana kivyake, hata mimi nilimshauri akuambie akasema hawezi, atapambana kivyake, kwahiyo sijui, zaidi…ila nilisikia siku moja akilalamika kuwa watu wanaomdai, wanataka kufungua mashitaka…’akasema

‘Unawafahamu kwa orodha…?’ nikauliza

‘Kwa kichwa hapana, ila ukitaka ninaweza kukutafutia huko ofisini…’akasema

‘Hilo liache kwanza, je hakuna kitu kingine umesikia, akilalamika au…ni kwanini akatokea kunywa pombe sana…?’ nikamuliza

‘Shemeji mimi nijuavyo, na aliwahi kuniambia ni sababu ya mawazo, amekuwa kwenye wakati mgumu na nahisi anaona kama hana mtu wa kumliwaza vile, ni yeye na kazi yake, na anaogopa kusema kashindwa, ,….nahisi ni hivyo shemeji..madeni, na…sijui, kama kuna tatizo jingine mimi siwezi kufahamu…’akasema

‘Unavyosema hivyo..kumliwaza.., ni kama vile aliwahi kulalamika, kama unavyosema anahisi hana mtu wa kumsaidia, mimi si nipo mkewe jamani,je hujawahi kusikia akilalamika mbele yako, kuwa kuna tatizo analipata dhidi yangu?’ nikamuuliza.

‘Shemeji hapana, lakini mimi nimeishi na nyie, kwahiyo mengine nayafahamu, wakati mwingine nilikuwa natamani kuwa kama nyie wachapakazi, mkirudi nyumbani hamna muda wa kuongea ni kazi tu….’akasema

‘Naomba uniambie waziwazi, nitafurahi sana ukianiambia ukweli, kuwa labda katika maisha yetu uligundua kasoro fulani, maana wewe tumeishi nawe, ukisoma mpaka ukapata kazi, niambie ukweli shemeji,kuna jambo gani tunakosea, au mimi nimekosea mpaka namkwaza kaka yako?’ nikamuuliza.

‘Mhh, shemeji mimi sioni walakini ndio maana nasema natamani niwe kama nyie, lakini kwangu ukifanya hivyo mke ataanza kulalamika, unanielewa hapo, wake zetu sisi, kisomo kidogo, ukiwa nyumbani wanataka usifanye kitu, uwe unawasikiliza wao, ukishika simu ugomvi, uki..ndio hivyo,…mimi hata laptop naogopa kwenda nayo nyumbani….’akasema

‘Ina maana kumbe labda hata kaka yako yupo hivyo, kuwa labda alikuwa hapendi hali hiyo ya mimi kuwa na kazi hata nyumbani, lakini hata yeye alikuwa akifanya hivyo au sio…’nikasema

‘Kiukweli, nyie mnaishi kama wazungu, ..sizani kama kaka anaweza kulilalamikia hilo, mimi sijui kabisa…’akasema

‘Kwahiyo kwa uoni wako, kaka yako …hiyo ajali haijasababishwa na jambo fulani,, unavyohisi wewe…?’ nikamuuliza

‘Yaweza ikawa na sababu kwa jinsi nilivyosikia kuwa aliendesha kwa mwendo kasi, na kaka hana tabia hiyo ya kuendesha gari kwa mwendo kasi, ndio maana wengi wanahisi kulikuwa na jambo zito.., hata mimi mwenyewe nimejiuliza sana hilo swali, lakini ajali ni ajali tu shemeji…’akasema.

‘Kwahiyo wewe unahisi tatizo la kaka yako ni madeni na sio labda kuna mataizo ya kifamilia, labda, kitu kama hicho...?’ nikamuuliza.

‘Inawezekana kuna tatizo nje, mimi na wewe hatulijui, lakini kwa uoni wangu mdogo, nahisi kama alikuwa na msongo wa mawazo, kwanza madeni, pili nahisi alihitajia mtu wa karibu sana wa kuyaondoa hayo mawazo ya kazini, lakini wewe upo, sijui kwanini hakutaka kukushirikisha, na sijui zaidi shemeji…’akasema

‘Hapo sasa unaanza kusema ukweli…kuwa pamoja na yote hayo, nahisi ananiona kama sipo karibu naye sana, anaogopa kuniambia, ataonekana mdhaifu…’nikasema

‘Sawa sawa shemeji…’akasema

‘Kwahiyo akaanza kunywa, kuondoa mawazo…’nikasema

‘Sawa sawa shemeji…’akasema

‘Na ulevi, nisikiavyo, raha yake uwe na wenza, marafiki, wa kike na wa kiume mnakunywa mnacheka, au sio…’nikasema

‘Ndio hivyo hivyo…’akasema

‘Na kaka yako ni binadamu au sio, na ni mwanaume au sio, ni lazima akiwa anakunywa alikuwa na marafiki, anakunywa nao ..au sio…?’ nikauliza hapo akasita halafu akasema

‘Yawezekana…ndio anakuwa nao, ni kawaida hiyo…’akasema

‘Na marafiki wanaweza kuwa wa kike na kiume na wewe unawaona , sema ukweli wako, kumbuka, tunaongea ili kupata namna ya kumsaida kaka yako…’nikasema

‘Ni sawa shemeji, kwnye kunywa hivyo vipo, na nijuavyo kaka pia alikuwa na marafiki zake, na wakati mwingine ndio, wanakuwepo wanawake…’akasema

‘Na wengi ni wale wa mara kwa mara ..au sio, maana ni lazima mzoeane, huwezi ukawa na marafiki wa siku moja moja, au sio,…?’ nikauliza

‘Ni kweli shemeji, ni wale wale marafiki zake….’akasema

‘Sasa nataka tu kuliweka sawa, hao marafiki zake, nimeshawafahamu, yupo docta,..yupo wale wafanyakazi wenzake, wapo wale majirani wake wa kazini, na wanawake ni nani na nani…?’ nikauliza

‘Mhh…mara nyingi,..wapo, lakini anayekuwa karibu naye ni…unamfahamu shemeji, ni yule…yule mdada rafiki yako, na wanawake wengine ni wapenzi wa marafiki zake,…’akasema

‘Kuna kipindi analewa kupitiliza…au sio…?’ nikauliza

‘Ndio, hilo siwezi kukukatalia, hata yeye hawezi kulipinga…’akasema

‘Na kuna muda aliwahi kulala nje, kwasababu ya kulewa sana…’nikasema

‘Mhh..shemeji…lakini mimi namchukua na kumleta nyumbani…’akasema

‘Haijatokea nyie mkalala nje na mkaja karibu na asubuhi..au yeye akaja karibu na asubuhi..?’ nikamuuliza

‘Mmmh labda kukiwa na sherehe…’akasema

‘Lakini ilishatokea au sio..?; nikauliza

‘Kiukweli….eeh, ndio ilishatokea…’akasema

‘Na muda mwingine huyo mdada rafiki yangu alikuwepo…?’ nikauliza

‘Sio muda wote..inatokea tu, na mara nyingi huyo mdada anaondoka mapema..’akasema

‘Na ile siku mlichelewa, mkawa mumelewa mkaenda kulala kwa huyo rafiki yangu je,ilikuwaje..?’ nikamuuliza hapo akashtuka na kusema;

‘Shemeji, …siku zile, hahaha, nani alikuambia,..ndio..lakini sio kulala, kaka yeye aliondoka, unajua ilikuwaje, tulipotoka kule tukampitisha shemeji kwake, mara kukazuka maongezi, akatukaribisha kwake,..ujuavyo pombe hatukuangalia muda, wengine wakajikuta wamelala kwenye sofa…’akasema

‘Yeye ndiye aliwakaribisha, au sio…?’ nikauliza

‘Ndio, …na muda huo kaka kalewa, akawa naye anakubali haraka, …basi tukaingia kwake, tukaendelea kunywa, kuongea, wengine usingizi tena,…lakini kaka aliondoka…’akasema

‘Kaka yako aliondoka, wew ukabakia na rafiki yangu, mkalala naye hadi asubuhi si ndio hivyo…?’ nikauliza

‘Ilibidi mimi nibakie, kwa maaagizo ya kaka, kuhakikisha, kuna usalama, ndio sababu hiyo, sio vinginevyo shemeji, na asubuhi aliponiona huyo mdada akanifukuza…’akasema

‘Huyo mdada alilewa hajitambui, na wewe ukachukua nafasi hiyo kufanya ulichodhamiria siku nyingi ni kweli si kweli, usinidanganye nimeshafahamu kila kitu..’nikasema

‘Hahaha, shemeji bwana, hakuna kitu kama hicho, kaka angeniua, hapana..’nikasema

‘Kwanini kaka yako akuue…?’ nikauliza

‘Unajua tena shemeji, yule ni sawa na wewe, hatafurahia kama nitafanya jambo baya dhidi yake…’akasema


‘Na hiyo hali ya kwenda kulala kwake, sio mara moja ni zaidi ya mara moja au sio..?’ nikauliza

‘Mhh, kama mara mbili, au tatu, sikumbuki vyema…’akasema

‘Kaka yako hakuwahi kuingia kulala na rafiki yangu..?’ nikauliza hapo akashtuka na kusema

‘Ha-hapana shemeji…mimi sijui , sikuwahi kuona, ..unajua anamuheshimu sana yule mdada, sizani, mimi hapo siwezi kuwa na uhakika…’akasema

‘Mdada ana mtoto, na nikuulize tangia ajifungue uliwahi kwenda kumtembelea huyo mdada..?’ nikamuliza

‘Hapana shemeji, mimi na yule mdada hatuivani sana, inatokea siku na siku akiwa na shida zake ndio ananiona wa maana, vinginevyo, sina habari na yeye kabisa…’akasema , mara nikahisi sauti kama ya watu wanaongea, nikatega sikio, kukawa kimia, nikaanza kuingiwa na wasiwasi, mume wangu asije akawa kaamuka

‘Hebu kidogo…’nikasema na kusimama kusikiliza, nilikuwa sijamalizana na huyo mtu, nikasema

‘Sasa sikiliza shemeji…, mimi ninakupa wewe muda wa kuyatafakari haya kwa makini, nataka uniambie ukweli, kuhusu mahusiano ya mume wako na rafiki yangu, je kaka yako hana mwanamke mwingine yupo naye karibu..?’ nikamuliza

‘Mhh..mimi simfahamu…’akasema

‘Sasa nitaongea na wewe tena kesho, lakini sio hapa nyumbani, nataka tuyaongelee haya na mengine tukiwa wawili, nataka uniambie ukweli, unasikia, kwa manufaa ya kaka yako, unanisikia,....’nikasema.

‘Shemeji hamna tatizo kabisa , lakini yote nimeshakuambia, ..sizani kama kuna jambo ninalolifahamu …’akasema

‘Nimefurahia sana maongezi yako ya leo, hatujawahi kukaa na kuongea hivi, ukaniambia ukweli kutoka moyoni mwako,,..nimefurahi sana, na wakati wote ninakuona kuwa ni mtu mwema, unayejali, wale wanaokujali, nimefurahi sana...sasa ili kulihakiki hilo, nataka tena tuongee, kuhusu rafiki yangu, unajua mtoto wake anafanana sana na wewe…’nikasema.

‘Eti nini, anafanana na mimi, hapana shemeji, sio kweli, haiwezekani sio kweli….’ Akasema na kushtuka, na muda huo simu yake ikawa inaita lakini hapokei ni kama kachanganyikiwa fulani.

Na muda huo nikasikia sauti ya wazi, kuwa mfanyakazi wangu anaongea na mtu ndani, nikajua mume wangu ameshaamuka kwahiyo mimi kwa haraka nikawa nakimbilia huko ndani, na nilimuona shemeji akisikiliza simu na huku anatoka nje....

**************

Nilifika ndani na kukuta kupo kimia, na wakati nataka kwenda chumbani ndio nikasikia watu wakiongea nje, nilipochungulia nje kwa kupitia dirishani nilimuona yule msaidizi wangu akiwa anasukuma kile kigari cha mume wangu, na mume wangu akiwa kakaa na alikuwa kaegemeza kichwa huku kashika shavu, a macho kayafumba kama lasinzia, hiyo ilikuwa ni dalili, kuwa alikuwa na mawazo.

Kumbe mfanyakazi alimchukua mume wangu na kutoka naye nje wakati tunaongea na shemeji yangu,inaonekana mume wangu aliamuka akanikuta sipo na wakati huo mfanyakazi wangu alikuwa anafanya usafi, au….mume wangu alisikia yupo akamuita, na akamuambia amtoe nje

Niliwaangalia, na mfanyakazi alikuwa akikisukuma kigari huku na kule ndivyo anavyopenda mume wangu, kufanyiwa hivyo, hataki kukaa sehemu moja kwa muda mrefu.

Kwanza nikaingiwa na wasiwasi, nikijiuliza huyu mtu alitoka muda gani, isije ikawa,walifika hadi kule bustanini, wakasikia maongezi yetu na shemeji yangu,kitu ambacho muda wote nilikuwa nikikikwepa, nikaona nithibitishe hilo, nikafungua mlango na kutoka nje,....

Mume wangu alipoisi kuna mtu anakuja akafungua macho na aliponiona akajitahidi kutabasamu, lakini lilikuwa tabasamu la kujilazimisha, kwanza aliniangalia machioni, mimi nikatabasamu, yeye akabenua mdomo, ila ya dharau au kujifanya anajua jambo

‘Mume wangu samahani, nilikuwa na mgeni nikakuacha chumbani peke yako..’nikasem

‘Mdogo wangu kashaondoka, mbona hajanisalimia, nilitaka kuongea naye.....’ akasema

‘Ndio kapigiwa simu ya haraka, labda atarudi baadae lakini kwanini hukusema , kuwa umeamuka, nije, huyu mfanyakazi sio kazi yake hii, hii ni kazi yangu,..’ nikasema

‘Unajua upepo, na hali ya bustanini ni kama dawa kwangu nilipoamuka tu, nikaona haupo nikajua umetingwa na jambo, nikamuambia mfanyakaz anisaidie nitoke nje,..na wakati natoka ndio nikawaona mnaongea, nikaona nisiwasumbue, ….’akasema

‘Hutusumbui bwana…yule ni ndugu yako na mimi ni mke wako, wote tunawajibika kwako...’nikasema

‘Aaah, ni kweli, lakini na mimi ni binadamu, nakuonea huruma, na…..yawezekana na wewe ulikuwa unatafuta njia za kunisaidia nipone haraka, na mimi nataka kupona haraka, au sio…’akasema na kunifanya nihisi kuwa huenda alisikia jambo.

‘Mume wangu na wewe siku hizi una maneno, …’nikasema

‘Mke wangu hata mimi sijui yametoka wapi,..ila mengine uwe unaniuliza mimi mwenyewe nitakuambia kila kitu, usiogope kuniuliza mke wangu…nakupenda sana mke wangu usije kuniacha, ukiniacha na mimi nitaicha hii dunia ya mateso,..naumia mke wangu, kweli hujafa hujaumbika…’akasema kwa unyonge

‘Mume wangu kwanini unaongea hivyo…?’ nikauliza

‘Najua na wewe unajua, kuwa nimekosea sana, na kiukweli mke wangu, mengine tuyasahu tu, tusonge mbele, ukiwasikiliza sana wazazi wako tutaharibu kila kitu, kiukweli mimi najua nimekosea wapi, na mimi kwa hali kama hii, nimepata fundishi kuba sana, na kwahiyo naahidi sitarudia tena, najua kazini kupoje lakini najua jinsi gani ya kupainua tena, hata bila ya msaada wa baba yako…’akasema

‘Hayo usiyawazie sana mume wangu…muhimu ni wewe kupona, muhimu ni afya yako, ukiyawazia hayo hutapona, na kazi zipo tu, muhimu ni afya yako…’nikasema

‘Kupona kwangu ni pamoja na kufahamu kuwa wewe upo na mimi na kamwe hutaweza kuniacha…hata iweje ..lakini najua nipo kwenye kuti kavu, kwa hali kama hiyo nitawezaje kupona…, mawazo yataishaje, wakati najua kupona kwangu ni kuingia kwenye jela nyingine ya sintofahamu, najua yote hayo, baba yako, anasubiria tu, nipone, au sio…’akasema.

‘Sikiliza mume wangu…’nikasema

‘Nisikilize nini bwana,..hata ujifanye vipi najua, wewe na baba yako mpo kitu kimoja, najua..rafiki yako kaharibu kila kitu najua…lakini itasaidia nini kwa sasa, ila nikuambie ukweli, mimi nikiwa hivi miaka nenda rudi, na kama nitaendelea kuteseka hivi, aah, kwanini bwana niwasumbue watu…’akasema

‘Mume wangu hayo yametokea wapi, tulishaongea ukasema utajitahidi ili upone haraka…’’nikasema

‘Yaaah…nitapona haraka, …ili niingie kwenye kizima cha kesi, …unajua baba yako anatamani sana, ukaishi na watu kama docta, sio watu kama mimi, kwahiyo anatafuta kila namna, ndio maana alinitega, nimeliona hilo kwenye ndoto, na..mke wangu nasema hili kwako, kama ni hivyo, sawa, lakini utanikumbuka, labda, nikiwa huko kuzimu…’akasema na kuanza kusukuma kigari kuondoka.

‘Mume wangu…unaongea nini sasa..’nikasema lakini huyoo akasukuma kigari kuelekea ndani. Na muda huo nikahisi kichwa kinaniuma ni hiyo ni dalili mbaya kwangu…

NB: Kwa leo inatosha ....WAZO LA LEO:Katika maisha yetu ya ndoa, na katika maisha yetu ya kila siku, tujifunze kuwa wakweli, kila mmoja amwamini mwenzake , awe mkweli kwa mwenzake....kwani, ukweli wakati wote, ni kinga ya uhasama,...japokuwa kuna wakati mwingine inatulazima kukwepa kusema ukweli kwa maana fulani, ili kukwepa madhara..tukihisi tunafanya hivyo kwa nia njema….lakini kama tukianza hivyo kusema uwongo, kidogo kidogo hujenga mazoea, na tutajikuta tunahasimiania, unafiki unatawala nafsi zetu..kwa vyovyote iwavyo, tujifunze kuwa wakweli kwa wenza wetu, ili kujenga uaminifu, upendo na furaha na kujenga familia zilizo bora
 

Abdallahking

JF-Expert Member
Mar 19, 2018
1,989
2,000
SEHEMU YA 54

Nilipomaliza kuongea na mdogo wa mume wangu, akili yangu ilikuwa kama imefunguka, japokuwa kwa jinsi nilivyomuona huyu shemeji yangu, nahisi kama anahusika kwa amna moja au fulani, anaweza akawa ndiye baba wa mtoto wa rafiki yangu au anajua lolote kuhusu hilo..na kwa hali hiyo, nikajikuta naanza kutawaliwa na hasira, hasira kwa watu wangu niliowapenda sana…

Kuna muda nikawa natamani niongee kwa hasira… , nifoke, kama vile nipo ofisini na wafanyakazi wangu, lakini haikuwa rahisi , kwani nilikuwa kwenye kifungo maalumu,..kifungo cha kuwajibika kwa mume.

Tuendelee na kisa chetu…

*****************

Mume wangu siku hiyo hakutaka kuongea kabisa, na nikaona nisimsumbue zaidi, nikajitahidi kutimiza kila kinachostahki, na akaja kulala…


Yakapita masiku kadhaa, na siku hiyo nilikuwa nimetoka nje kidogo, nikiangalia taratibu za usafi, ni baada ya kuhakikisha kuwa mume wangu bado amelala, Nilikaa nje kama nusu saa au karibu saa nzima, baadae nikarudi ndani kuona kama mume wangu amesha-amuka ili nimpatie kifungua kinywa...

Wakati naingia ndani nikamkuta kashikilia simu,...simu kuashiria kuwa anaongea na mtu, na aliponiona naingia kwa haraka akakata hiyo simu , na kujifanya kama ndio anataka kupiga...

‘Ulikuwa unaongea na nani, …mume wangu, kwanini unaharibu, ulishaambiwa usijisumbue na simu, au huyo mtu kakupigia wewe ndio maana sitaki ubakai na simu…?’ nikauliza, na alitulia kidogo , baadae akaniangalia na kusema

‘Mdogo wangu kakukosea nini..?’ aliuliza hivyo na kunifanya nishtuke, swala la mdogo wake nilishamalizana naye, iweje tena aulizie hivyo.

‘Mdogo wako…!?’ nikauliza kwa mshangao

‘Ndio…’akasema hivyo na kutulia


‘Kama ni ile siku tuliongea naye mambo ya kawaida tu, kwani ndiye umempigia simu au yeye ndio kakupigia simu kwani.. kasema nini…?’ nikauliza.

‘Nimekuuliza swali na unakwepa kunijibu, hufahamu jinsi gani ninavyojisikia vibaya familia yangu kuonekana tegemezi, kuwa kama omba mba, au huko kumsaidia imekuwa ni tatizo...’akasema

‘Mume wangu kwani shemeji kasemaje, niambie ukweli, ..unajua mume wangu hutakiwi kuwa na mawazo mengine ya kifamilia, utashindwa kupona haraka…’nikasema.

‘Inaonekana unamshuku vibaya, na kama ni mambo yangu mimi, kwanini umuulize yeyem niulize mimi mwenyewe…’akasema

‘Nilimuuliza kwa nia ya kutaka kukusaidia wewe, sikuwa na nia mbaya mume wangu…’nikasema

‘Ok…sasa unahitajia nini, nikuambie mimi mwenyewe..?’ akauliza

‘Hakuna kitu nahitajia kutoka kwako…’nikasema

‘Kama ni kuhusu kazini, ndio nina madeni mengi tu..na inatokana na biashara kuwa mbaya…ilibidi nikope nikitafuta masoko, ilibid nikope kuweka vifaa vya kisasa, lakini bishara haikutikia, ni hali ilivyo, nikajikuta naongeza madeni juu ya madeni, na hilo litakuja kulimaliza mimi mwenyewe…’akasema

‘Nimekuelewa mume wangu, lakini hukuwahi kuniambia hayo au sio, lakini sio shida, na wala lisikuumize kichwa… nashukuru sasa nimekuelewa, tutaangalia jinsi gani ya kufanya, kama itabidi tutakopa pesa kwa baba ili tulipe hayo madeni..’nikasema

‘Hahaha, ukope pesa kwa baba yako…labda awes io yeye,…kwa kauli yako hiyo naona wewe na baba yako kitu kimoja, ndio maana aliniwekea mitego, hataki mimi niwe mume wako, hili lipo wazi, lakini mimi sitakubali, hataweza nakuhakikishia,…’akasema

‘Mume wangu haya yote hayana maana kwa sasa, hebu achana nayo uangalie kwanza afya yako, kwanini unanipa wakati mgumu, ...?’ nikamuuliza na kabla hajajibu nikasema;

‘Jitahidi kusahau kila kitu ili upone haraka , tuendelee na maisha mengine..’nikasema

‘Pole sana mke wangu, najua nakupa wakati mgumu, lakini mimi sijapenda hilo, hivi kuna mtu anajitakia ajali…?’ akauliza

‘Ni ajali haina kinga nafahamu..’nikasema

‘Muhimu kwangu,..ni msamaha wako…na kiukweli sasa naanza kufahamu kuwa nakuumiza, nakuweka kwenye wakati mgumu sana, utanisamehe tu mke wangu, lakini haya yanahusuje mdogo wangu,…’akasema

‘Mdogo wako hana tatizo, nilikuwa naongea naye tu….mambo ya kawaida, kumuulizia maendeleo yake , kama kuna sehemu kakwama niweze kuona kama tutaweza kumsaidia…’nikasema

‘Mhh…ndio hapo sitaki,…yeye anajiweza, kwanini asaidiwe, kwanini azidi kuongeza mzigo kwako, baba yako akisikia hivyo atakuja juu, na kutusimanga, mimi sipendi hilo kabisa, na kama kuna adhabu ya madhambi yangu, basi nipeni mimi....’akasema.

‘Mume wangu, ukumbuke shemeji kwangu namuona kama mdogo wangu, kama ulivyooona tumekuwa tukijitahidi kwa pamoja kumjenga katika njia njema,ya kumbadili kutoka kwenye tabia ya utegemezi kwenda kwenye tabia ya kuweza kuishi mwenyewe, na hilo tumefanikiwa, kwahiyo kila hatua pia tunahitajika kumuuliza, wewe sasa unaumwa, ni lazima mimi niwajibike naye...’nikasema.

‘Ni kweli mke wangu, na inabidi nikushukuru sana kwa wema wako huo, kama ingelikuwa ni mimi mwenyewe ningelishakata tamaa, maana bwana mdogo alikuwa keshadekezwa na mama,maana yeye ni kipenzi cha mama, na wao walifikiria kwa kmfanyia hivyo ndio wanampenda,wakawa wanamdekeza, kumbe wanamharibu tusingelimwahi mapema, angeshajiunga na hayo makundi ya kuuza madawa ya kulevya....’akasema.

‘Ni kweli mume wangu, hilo ni kosa wanalofanya wazazi wengi, ambao kwa kuwadekeza watoto wao ndio wanafikiria kuwa ndio mapenzi kwa mtoto, kumbe ni kinyume chake…’nikasema nikibadili mada.

‘Nashukuru sana mke wangu najua sasa naingiwa na moyo kuwa umenisamehe kabisa, kama una lolote unataa kufahamu niulize mimi mwenyewe, najuta sana kwa hayo yaliyotokea...na kama hutanisamehe, ukaamua kumsikiliza baba yako hewala, lakini mimi sizani kama nitaishi ikitokea hivyo,ni..heri ya kufa tu...’akasema

‘Mume wangu usijali,..nimeshakusamehe, cha muhimu ni wewe kupona, hilo ndilo unatakiwa uliwazie jinsi gani unatakiwa kufanya mazoezi na kuondoa mawazo....’nikamwambia

‘Nikipona mke wangu, nitakuwa mimi na wewe bega kwa bega, ...unajua mke wangu, wakati mwingine kama binadamu, tunajisahau…mimi nimeliona hilo kivitendo..na eeh,..na wakati mwingine inatokea kwa vile tunakuwa mbali mbali kimawazo, nawaza hivi mwenzangu vile, lakini hayo yamepita au sio mke wangu…?’ akauliza

‘Ni kweli…hayo yasahau…’nikasema

‘Sasa mke wangu, nakuahisi kuwa mimi mume wako, ...nitajitahidi sana tuwe pamoja tuiondoe hiyo hali, au unasemaje mke wangu..?’akasema, nikakumbuka kuwa mtu huyu hatakiwi kuongea kwa muda mrefu, kwahiyo natakiwa kukubali tu, japokuwa nilikuwa sijamuelewa bado , hapo nikasema.

‘Usijali mume wangu, cha muhimu kwa sasa, ni kuhakikisha yale tuliyo anza nayo yanafankiwa,…kampuni eeh, hiyo nitapambana nayo, na hili la huyo mdogo wetu achana naye, lisikuumize kichwa, au kuna nini zaidi,..hakuna achana naye, jingine ni kuhusu watoto wetu , najua familia inakua, sasa, hapa kuna kitu nataka tukiongee....’akasema

‘Tutakuja kuongea tu mume wangu usijali…’nikasema lakini hapo nahis kuna jambo anatakak kulisema, naogopa anaweza kusema jambo, nikaingiwa na hasira, na haitakiwi,..hapo nikasema.

‘Lakini mume wangu…’akanikatiza na kusema;

‘Huyu mdogo wangu kwa sasa hana tatizo, keshajiweka mahali ambapo hatuna haja ya kuhangaika naye tena,....na kwa watoto wetu bado wadogo, hatuna shaka nao, tutawajenga kimaadili, na umeshafanikiwa kwa hilo, kama wanaweza kuamuka asubuhi na kuwajibika hata bila kuelekezwa, tunataka nini tena mke wangu..au sio….’akasema.

‘Ni kweli…’nikasema

‘Sasa mke wangu kuna kitu kingine nilitaka tuongee…’akasema

‘Mume wangu unakumbuka docta alisemaje…’nikasema

‘Ndio nakumbuka alisema nisiwaze sana, na nisiongee sana…’akasema

‘Sasa hapa umeongea vya kutosha, unahitajika kumpumzika..’nikasema

‘Lakini niliyo nayo kichwani yananifanya niwaze sana , ndio maana nataka tuyaongee, tuyaweke sawa, yananifanya niwaze sana, na baba yako, yupo nyuma ya hili, akiona nimepona tu, atanivaa, sitaki, nataka tuyaweke sawa sisi wawili kwanza…’akasema

‘Tutaongea tu mume wangu usijali, sasa hivi wewe unahitajika kupumzika kwanza…unajua mume wangu nimekukosa sana, nataka upone haraka, au wewe hulioni hili, …’nikasema

‘Kweli mke wangu nafahamu..hata mimi naona nakutesa sana, nawazia sana hilo pia, utaishi hivi mpka lini, ndio maana naingiwa na wivu, nahisi kama naibiwa…’akasema

‘Hahaha mume wangu….wivu gani huo, kwa umri huu usiwe na wasiwasi kabisa, si unanifahamu mimi sina mwili wa tamaa tamaa za ajabu ajabu, mimi najimudu mwenyewe kabisa…’nikasema

‘Mhh, ..ni kweli, hata hivyo wivu hauachi kuwepo,…ila kiukweli mungu alikujalia , lakini tatizo ni mimi mume wako, tamaa ni nyingi sana, ndio maana mungu kaona aniadhibu….’akasema

‘Oh,…. pole sana, sasa mume wangu tulia , dawa zifanye kazi, ulale sasa…’nikasema

‘Ngoja nikuambie ukweli kwanza kabla sijalala,…mke wangu, nataka tufurahi pamoja, tuongee pamoja,… nilishaanza kuwazia vibaya sana, hii ajali ndio imeniokoa, sasa nataka kusiwepo na uadui, kati yangu mimi na wewe na …marafiki zako pia..kama ni langu liwe langu…’akasema

‘Usijali mume wangu nimekuelewa tu…’nikasema

‘Hapana, wewe hujui tu…nilishaanza kufikia kubaya, na….isingelikuwa hayo mambo ya baba yako, ningelishajiandaa kufanya mabaya tu, tamaa zilishaanza kuitawala nafasi yangu,…wakati mwingine mungu anajua tu nilikuwa naelekea wapi…’akasema

‘Mume wangu sasa lala…’nikasema

‘Nakupenda sana mke wangu, niache nikuambie ukweli, nimekukosea sana, na kosa langu linakwenda kuathiri wengine ndio maana naogopa, sasa mdogo wangu kesho atakuwa mwingine, unaona eehe, ni vyema tukayamaliza haya sisi wenyewe achana na mipango ya baba yako, hebu sogea hapa mke wangu, nahisi sauti inakwisha, dawa hizo…’akasema hapo nilitaka kuanza kukasirika, maana ni kama unaongea na mtoto ambaye unamkanya kitu hasikii, lakini sikuwa na jinsi, nikasogea na kukaa karibu yake

‘Kaa hapa kwenye miguu yangu…’akasema

‘Mume wangu lala basi…’nikasema

‘Ni amri ya mume wako…’akasema na mimi nikaenda na kujiegesha kwenye miguu yake, na akawa ananishika ili kunifanya nikae, huku namuonea huruma, ..kitendo hicho kikamfanya acheke..na mimi nikajikuta nacheka tu

‘mke wangu kweli unanipenda, wanionea huruma sana, lakini huruma hiyo isiishie hapa,..unihurumie kabisa kabisa..usimsikilize baba yako, kila kitu alichpanga tukisahau, unanielewa, hayo niachie mimi, au sio…akanishika kama ananitekenya,......’

‘Aah, mumu wangu, nini tena lala, utajiuliza…’nikasema na kucheka na yeye akacheka, na mara nikasikia sauti ya mtu akipiga hodi, na kabla sijasema karibu mlango ukafunguliwa, ..., alikuwa ni docta.

‘Kumbe ni wewe jirani…’nikasema na kujiinua haraka miguuni mwa mume wangu.

‘Oh, naona leo mpo na raha, maana nimesikia kicheko, ..kicheko cha raha, ...’akasema na mimi nikashukuru kuwa hatmaye mgonjwa atakubali kulala.

‘Kwanini nisiwe na raha na mimi nipo na mume wangu..’nikasema.

‘Ni kweli hayo ndio maisha,...inatakiwa mfanye hivyo kila siku,, au mara kwa mara, au sio rafiki yangu?’ akamuuliza mume wangu huku akimsogelea na kushikilia kile kigari,..na mume akasema;

‘Na wewe bwana, unakuwa dakitari wa kila kitu....’akasema

‘Ni kweli natamani iwe hivyo, na nimekuja na mtu wa mazoezi, leo tunataka kumfanyisha mume wako mazoezi maalumu, na kama hutajali naomba nimchukue mume wako’akasema

‘Unataka kumpeleka wapi?’ nikauliza nikimwangalia kwa uso uliotahayari.

‘Ndani ofcourse, tunahitajia tuyafanyie ndani, sehemu yenye nafasi, hasa kule maktaba au sio…docta kaja na vifaa maalumu, yupo nje,…docta ingia...’akasema, na mara akaingia docta akiwa kavalia kikazi zaidi.

Mimi hapo sikuwa na jinsi…nikawaacha wao wakielekea kwenye chumba cha maktaba, na wakati wanaondoka kuingia mume wangu akageuza kichwa na kuniangalia kwa nyuma, akasema;

‘Mke wangu nakupenda sana....’akaniambia mimi sikujibu kitu, muda huo akili ilikuwa imezama kwenye mawazo, nawaza hayo mume wangu aliyoongea, inaonekana kiukweli mume wangu kakosea, na huenda, ..kuna ukweli wa hayo yanayosemwa, na …na huenda baba yangu ameshaligundua hilo…sasa itakuwaje…

*************

Baadae docta akarudi, naona alimuacha mwenzake akiendelea na mazoezi na mume wangu.

‘Nimekuona ukimuhoji sana mume wako, ...huu sio wakati muafaka, wa hayo maongezi yako...’akasema

‘Mbona sijamuhoji kitu chochote cha kumfanya awaze sana, yeye ndio anaongea mambo mengi tu…’nikasema

‘Kwanini una haraka na hayo mambo, uwe na subira na hicho unachotaka kukijua, utakifahamu na…utakuja kuniamini niliyokuwa nikikuambia.., lakini kwa hivi sasa yasubirishe hayo..wasiwasi wangu ni kuwa, unaweza ukafanya jambo ambalo utakuja kujijutia. Ukiwa umeshachelewa….unanielewa hapo…’ Akasema na mimi nikawa namsikiliza tu..

‘Japokuwa namuona mume wao leo ana furaha sijui kwanini…lakini ndivyo itakwavyo, awali alikuwa akionyesha kuwa ana jambo linamkera, hata hivyo hayo ysikupe mawazo kuwazia kuna nini, hayo yaweke pembeni kwanza, mengine nakusaidia, niamini mimi…’akasema

‘Kwani wewe unafikiri mimi nimemuuliza nini mume wangu kibaya,..tulikuwa tunaongea tu, ila mimi najiuliza kwanini wewe unayejua ukweli hutaki kuniambia,..’nikasema

‘Kukuambia nini sasa, wakati mimi nimeshakuambia kila kitu au…?’ akauliza

‘Hapana,..hujaniambia…’nikasema

‘Tatizo ..wewe unataka nikutafunie kila kitu, mimi siwezi kuvunja ndoa ya mtu, na sitaki hilo litokee, …unasikia, snitajuta sana ndoa yenu ikivunjika…’akasema

‘Unajua mimi sikuelewi, wewe unajifanya kuwa unanijali, kumbe kuna mengi makubwa unanificha, hukutaka kuniambia mapema, na huenda yote yasingelitokea kama ungelikuja kuniambia mapema..’nikasema.

‘Ina maana unanilaumu mimi kwa hilo, ...unanichekesha kweli, wa kujilaumu ni wewe mwenyewe, wewe umeshindwa kuihudumia ndoa yako halafu na hatimaye hayo yakatokea,mengine yameanzia huko…, umesahau eeh, ni mara ngapi ninakuja kuongea na wewe na kujaribu kukuelekeza…’akasema.

‘Usijitetee bwana…, wewe ulikuwa na mume wangu wakati anafanya yasiyofaa, kama alishaanza kujihusisha na umalaya, kama alivyosema leo hii , ina maana wewe ulikuwa unafahamu,, je hukuwahi kumuona na wanawake wewe huniambii, ni nini maana ya kunijali...’nikasema.

‘Na wanawake, kakumbia hivyo…hapana ….’akasema

‘Kasema tamaa zilimzidi, akaanza na kutamani kufanya mabaya, hayo yana maana gani…?’ nikauliza

‘Sizani kama alikuwa na maana hiyo…’akasema

‘Lakini kuna kipindi nilikuambia hilo, unakumbuka kuna siku nilikuja nikakuambia kuwa mume wako naona kama ana…kuwa kuwa karibu na wanawake, kitu ambacho sio kawaida yake, lakini sio kwa ubaya, sikuona huo ubaya wa ndani …’akasema

‘Anakwua nao kwa vipi,…?’ nikauliza

‘Lakini nilikuambia, ukasema mimi naleta fitina, umeshasahau eeh, usinione kuwa mimi ni mjinga, nafanya haya mambo kihekima, nisingelikuja na kukuambia moja kwa moja, nilikuambia kwa namna ya wewe kulielewa, ukaniona mimi ni mbaya...’akasema.

‘Swali je kuwa nao karibu ni kwa nia mbaya, kuvunja ahdi ya ndoa , au kwa vipi, nataka unijibu hapo…’nikasema

‘Hilo kwa utashi wangu sijaliona, wanakunywa pamoja, kuongea inaishia hapo ila mimi niliona hilo lina muelekeo mbaya…’akasema

‘Kwahiyo wewe umesahau ile ahadi yako,?’ nikamuuliza

‘Ahadi gani?’ akaniuliza

‘Kuwa kamwe hutakubali mtu aniumize...’nikasema.

‘Na ndicho ninachokifanya...wewe mwenyewe utaona, si unajifanya mpelelezi, endelea,...lakini mimi nitajitahidi kuhakikisha kuwa hakuna mtu atakayekuumiza,ahadi yangu ipo pale pale, hata kama hunitaki niwe karibu na wewe....ila nakukanya uwe mwangalifu, usichukulie mambo kwa pupa..’akasema huku akitabasamu na kushika kidevu

‘Halafu kuna ujumbe, nimeupata, kutoka eeh, kwa rafiki yako, anasema kuna mambo yameshindikana anahitajika arudi kwanza huku, ...sijui ni mambo gani, kwani hamjawasiliana naye ?’akaniuliza


‘Rafiki yangu yupi tena, ooh, kwahiyo mnawasiliana naye wewe, mimi ananiona sina maana tena kwake…’ nikasema.

‘Una marafiki mangapi bwana, huyo huyo,..unayemwamini kupidukia,...nahisi akija sasa mtamalizana naye na ukweli utagundulikana, ila bado nakukanya, uwe makini, hasa akija huyo rafiki yako,...’akasema

‘Mimi hajaniambia, kwanza kaondoka bila kuniaga kwahiyo hata akija sizani kama nitakwua na muda wa kuongea naye…’nikasema

‘Hutataka kuujua ukweli…?’ akaniuliza

‘Ukweli upi…?’ nikauliza

‘Kuhusu mtoto…?’ akaniuliza na ikawa kama kanitonyesha jeraha, nikakunja uso, nikabakia nimeduwaa, halafu nikasema;

‘Nimeongea na mdogo wa mume wangu, anavyojikanyaga inawezekana akawa ndio yeye, au anaufahamu ukweli wote, nataka nije kuongea naye kabla huyo shetani hajarudi…’nikasema

‘Leo hii inamuita shetani…’akasema

‘Kutokana na wewe..ila mimi sijaamini, kama nimekosea mungu atanisamehe, ila kama ni kweli…sizani kama tutaelewana…’nikasama

‘Utamzuia asirudi kusoma, wewe si ndio umemfadhili…?’ akauliza

‘Hilo ni jambo jingine halihusiani kabisa na hili, siwezi kukosa fadhila za utu wema kwa ajili ya ubaya wa mtu…kama ataniambia ukweli, na ikawa hivyo ni kweli, kila kitu kipo wazi,…’nikasema

‘Kwa vipi…?’ akauliza

‘Mume wangu anafahamu…’nikasema

Mara tukasikia docta akija na alipotufikia akasema;

‘Oh mume wako kajitahidi sana leo, naona anafuraha fulani, mpaka kaweza kuinua miguu ni hatua nzuri sana, sasa jitahidini, awe na furaha kama hivyo, atapona haraka, ila mwishowe kaonekana mnyonge, …’akasema

‘Kwanini docta…?’ akauliza docta rafiki

‘Nahisi kuna kitu akikikumbuka kina mtesa, kuna kitu kasema, kapokea ujumbe unaompa shida sana, ujume wa simu kitu kama hicho…’akasema

‘Oh, labda ni huyo mshenzi, kamtumia ujumbe kuwa anarudi..’nikasema kwa hasira

‘Haiwezekani….’akasema docta rafiki.

‘Huyo mtu hana jema…ikibidi hata simu msiwe mnamruhusu atumie, lakinikwa hekima zaidi…’akasema docta.

‘Ni kazi, hataki kabisa kuchana na simu yake…’nikasema

‘Basi lakini kwa hatua aliyofikia, ni maendeleo mazuri tu…’akasema

Na baadae huyo docta akaaga kuondoka, na mimi nikaona niende kumuona mume wangu kama kalaa…niliingia na kumkuta anachat kweye simu.

‘Mume wangu hujalala..?’ nikamuuliza

‘Kuna kitu nakifuta kwenye simu yangu lakini hakitaki…’akasema

‘Kitu gani nikusaidie…’nikasema

‘Hapana…ni ujumbe, ..haina shida, umeshafutika…’akasema na sasa akazima simu yake, na kiukweli mimi sina muda na simu yake hata sijui anatumia neno gani la siri, lakini nikawa na hamasa sana ya kujua kaandikiwa ujumbe gani.

Nilipohakikisha mume wangu kalala, nikaichukua simu yake na kutoka nayo nje, nikampigia mtu wangu mmoja mtaalamu wa simu, anisaidie kuwasha simu iliyowekewa kifungo..ni mtaalamu sana, na akasema anakuja.

NB: Samahanini sana kwa kutokuwa hewani kwa kipindi cha siku tatu hivi, ni matatizo ya umeme na mtandano, na mitihani ya hapa na pale..WAZO LA LEO: Ndoa nyingi zina matatizo yake, na huenda yakawa ni matatizo madogo tu, lakini kwa wanandoa wakashindwa kuyatatua, kwa vile, hakuna anayekubali kushuka chini, kila mmoja anajiona anafahamu zaidi ya mwingine...au mmoja anaogopa kumuelezea mwenzake ukweli.....wewe kama rafikji tumia hekima kuwashauri, usitumie mwanya huo kuharibu badala ya kujenga. Hekima ya ushauri ni muhimu sana kwa watu kama hawo.
 

Abdallahking

JF-Expert Member
Mar 19, 2018
1,989
2,000
SEHEMU YA 55


‘Hakikisha umeharibu kila kitu…kila kitu, hasa mikataba, mengine nitayamaliza nikija…’Ni meseji pekee iliyokuwa imebakia kwenye simu, na imetumwa kutoka namba za nje...mume wangu alihakikisha kafuta kila kitu, hadi picha.

‘Hasa mikataba, mikataba gani hiyo ya kazi, na ni nani huyu kamwandikia mume wangu, …’ nikajikuta nikisema, nikirejesha simu ya mume wangu sehemu nilipoichukulia, mume wangu alikuwa kalala kwa amani kabisa.

Ujumbe huo ulinifanya niwazie kwenda ofisini, kuhakikisha kama kila kitu kipo sawa, na kuhakikisha mikataba ya kazi, na mingineyo ipo sawa sawa,…niliweza kuondoka, maana hali ya mume wangu ilikuwa sasa inaendelea vyema, na ningeliweza kumuagiza mfanyakazi wa ndani akaendelea na huduma nyingine bila shaka, muhimu ni mume wangu mwenyewe akubali,

‘Mume wangu naona hali inaimarika sasa namshukuru mungu kwa hilo…’nikasema

‘Kweli mke wangu nakushukuru sana…’akasema

‘Sasa nilikuwa na ombi moja, nataka kesho asubuhi na mapema nifike ofisini kwangu mara moja, unaweza kuniruhusu…?’ nikamuuliza

‘Ofisini eeh, …ooh, hivi kweli, samahani sana mke wangu,ina maana siku zote ulikuwa huendi kazini kwa ajili yangu, mimi nilijua upo likizo…’akasema

‘Nilichukua likizo kwa ajili yako…’nikasema

‘Nashkuru sana mke wangu, sasa…, wewe nenda tu, si umeona mwenyewe siku hizi najitahidi, yaani sijui kwanini wiki hii nimeingiwa na kitu kikanifanya mwili uwe na nguvu za ajabu, nikaweza kusimama, na sasa natembea japo kwa shida…mmh, nahisi hizi ni nguvu za ajabu…’akasema

‘Hongera, tumshukuru mungu…’nikasema

‘Haya wewe kesho nenda tu..

Basi kesho yake asubuhi nikafika ofisini.

*****

Kesho yake nilipofika ofisini, kwanza nilihangaika na maswala ya kikazi, ambayo yalinihitajia mimi kama mkurugenzi mkuu, na nilipomaliza, nikawa natatafakari kitu gani kingine nifanye kabla sijaondoka.

‘Lakini usichelewe…’ nilikumbuka kauli ya mume wangu.

Hata hivyo, muda ulikuwa bado, nikapiga simu nyumbani, na mfanyakazi akasema kila kitu kipo sawa, mume wangu anachukua mazoezi mwenyewe ya kutembea, ..

‘Sawa naona nitachelewa kidogo…mwambie nilimpigia sikumpata sawa..’nikasema

Siku hiyo nilijiona sina raha kabisa, na ilitakiwa niwe na raha, maana mume wangu hali yake inaimarika, keshaanza kutembea kidogo kidogo....nilishangaa kumuona akiwa furaha kuliko siku za nyuma, ni kama vile amesikia jambo kubwa ambalo limefurahisaha sana

Kiukweli niliombea iwe hivyo, ili apone haraka na maisha yaendelee, ila sikutaka kumdadisi sana, kujua kuna nini kimetokea, nilijitahidi kujizuia sana , kwa kutokumuongelesha au kumuuliza maswali ya kumpa mawazo, japokuwa sio kazi rahisi, kichwa changu kilikuwa na maswali mengi yasiyo na majibu na mwenye majibu ni yeye.

Wakati nipo mezani nikifanya hiki na kile akili bado ilikuwa inafanya kazi, inawaza, na sasa nikakumbuka kauli ya mume wangu:

Nakupenda sana mke wangu, niache nikuambie ukweli, nimekukosea sana, na ninachoogopa ni kuwa huenda kosa langu likaenda kuwaathiri wengine, sasa umemuingilia mdogo wangu, sijui kakukosea nini, haya…kesho atakuwa mwingine, unaona eehe, ni vyema tukayamaliza haya sisi wenyewe…kama ni dhambi zangu nibebe mimi mwenyewe… achana na mambo ya baba yako…au .

Inaonekana kuna kitu kwa mume wangu…sasa ni kitu gani hicho

‘Hakikisha umeharibu kila kitu…kila kitu, hasa mikataba, mengine nitayamaliza nikija…’

‘Hasa mikataba….’ Nikasema hilo neno na lulirejea mara nyingi, na sijui ni kwanini kuna kitu kikanikumbusha jambo…. nikakumbuka…

‘Mkataba wa ndoa…’

Nilipokumbuka hivyo, nikasimama,

‘Hivi kweli eeh, ule mkataba wetu wa ndoa,…ooh, afadhali, nimekumbuka, …sasa mambo yatakwisha kwa amani…sasa kama ni kweli, …mkataba ule utafanya kazi yake,...’nikasimama na kujinyosha,

‘Mkataba wa ndoa…’nikasema nikichezesha mikono kuonyesha kuwa nimekumbuka jambo la muhimu sana.

**********

Nilipokumbuka hili nikataka kujirizisha , nilitaka nikausome tena ule mkataba…najua mume wangu atakuwa keshalisahau hilo, lakini ulikuwa ni muhimu sana kwenye maisha yetu,…na ndio ulionifanya nimuamini sana mume wangu, kwani mkataba huo ulikuwa umetufunga tusifanye makosa..

‘Lakini kwa hili…wanalosema kuwa mume wangu kafanya,..ina maana kweli hakumbuki huo mkataba, hapana, watu wengelijua wasingelisema hilo, mume wangu aliuthamini sana huo mkataba, aliahidi na akawa wa kwanza kuutekeleza huo mkataba,…sasa iweje,..siamini,….’nikasema

`Yah,..hili sasa litakuwa ndilo suluhisho la hili tatizo, na sizani kama mume wangu kalisahau hilo, kama kasahau, basi kakusudia kweli, na kama kakusidia kweli, basi sheria itachukua mkondo wake, maana ahadi ni deni…’nikasema kwa sauti.

Hapo nikapata nguvu ya ajabu,….niliinuka kwa haraka kwenye kiti, nikasimama kwanza nikajinyosha tena na tena,…, sikuwa na haraka, sikuwa na jambo jingine muhimu kwa muda huo la kufanya, ...

‘Kwenye ule mkataba ushahidi ni muhimu sana, hasa likitokea kosa, hilo lilisisistizwa sana, …’nikawaza hapo nikakuna kichwa

‘Sasa mimi nina ushahidi gani, kuwa hayo waliyosema watu ni kweli, kuwa huenda , mume wangu kafanya kosa, na kosa lenyewe ni lipi, mmh…kazini, huko sina uhakika, lakini hili kosa kubwa la kuvunja masharti ya ndoa, je kweli kafanya hivyo, ushahidi upo wapi…?’ nikajiuliza

‘Ok, ngoja kwanza,…nikausome vyema ule mkataba, mambo ya ushahid ni mengine, je nitauweza kuutumia muda ukifika, je …haaa, sizani, mume wangu hawezi kufany ahivyo, ina maana kasahau, haaaah, mungu wangu....’nikasema.

Nikatembea hadi kwenye kabati langu maalumu, kabati hilo, huwa naweka kumbukumbu zangu muhimu, na hakuna mtu mwingine mwenye mamlaka ya kufungua hilo kabati, ….Kwanza nikafungua sehemu ya ukutani, kuna kabati maalumu za nyaraka za ofisini, lipo ndani ya ukuta, na humo kuna sehemu maalumu, ina ufunguo wake, na kuna sehemu imejificha sana hapo ndio niliweka ufungua wa kabati…

Nikafungua kabati, na ndani ya kabati kuna sehemu maalumu, humo nimeficha ufungua wa sehemu ambapo nimeweka hizo nyaraka, hakuna anayeweza kuuona huo ufunguo,… ni muda mrefu sijalifungua hilo kabati, maana vyote vilivyopo humo ndani, sio mambo ya kila siku ya kikazi. Na humo niliweka nakala zangu nyingine za mikataba ya kazi , jengo nk, pia kuna nakala za vyeti vya ndoa, na nakala za vyeti vya watoto…


********

Wakati nimeshauchukua huo ufunguo, ndio nikakumbuka jisi gani tulifikia hadi kuamua kuwa na mkataba wa ndoa,… ilikuwa kama masihara tu, ilikuwa kama fikira zilizokuwepo kabla ya kuolewa , na baada ya kuolewa nikasahau, sikuona umuhimu wake tena.

Nakumbuka ilikuwa kipindi nakaribia kujifungua, hilo wazo likanijia akilini, ikawa naliwazia sana, mpaka nikashindwa kuvumilia, ndio nikampigia simu wakili wa kazini, nikamuelezea hilo wazo.

‘Muheshimiwa, kuna kitu kinanisumbua sana akilini, ni wazo tu, lakini nimefikiria sana, nikaona lina umuhimu wake,..mimi napendelea kuwa na kitu kama mkataba wa ndoa kati yangu na mume wangu....’nikasema

‘ Wazo zuri sana,…basi kama mtakubaliana wewe na mume wako.., mimi nipo tayari, na nitawatengenezea mkataba mnzuri sana, na wenyewe mtaona jinsi gani utakavyowasaidia, ...ongea kwanza na mume wako mkubaliane, maana hilo ni swala la nyie wawili, kukubaliana kwanza...’akasema.

Nikahamasika,na jambo hilo , niliona uwe mkataba mkubwa zaidi, ambao utagusia kila kitu, mambo yote ya familia, kuanzia ya kifamilia hadi ya mali zetu, na hili nililifanya makusudi, ili hata nisipokuwepo mimi, au mume wangu basi kusije kukatokea mambo mengine ya kuja kuidhulumu watoto wetu.

Basi siku hiyo nilikaa nikiliwazia hilo, na jioni alipokuja mume wangu, nikaona nimwambie…ilikuwa siku ya kumbukumbu sana, na tarehe hiyo ilikuwa muhimu kwenye familia yetu.


‘Mume wangu kuna kitu nataka nikuambie...’nilimwambia, na yeye akanisogelea na kushika shika tumbo langu, huku akitabsamu , akasema;

‘Usiniambia siku zinakaribia, maana nina hamu sana ya kumuona mtoto wetu huyu’akasema huku akinishika shika tumbo langu..kiukweli siku za awali, hakuna mtu angeniambia kitu dhidi ya mume wangu nikakisikiliza, nilimpenda sana mume wangu na nilikuwa namuamini sana.

‘Usiwe na shaka mume wangu, siku yoyote kuanzia leo tunaweza tukaitwa baba au mama fulani, lakini sio hicho nilichotaka kukuambia.....’nikasema

‘Mhh, ok…kuna nini, niambie tu...mama watoto wangu …mama kijacho…’akasema huku akiendelea kushika shika tumbo langu.

‘Kuna kitu siku nyingi nilikiwaza..awali nilichukulia kama mambo ya kishule tu, lakini jana , juzi nikaliwazia hilo, nikaona kumbe lina umuhimu wake,..na nilipoona wazazi wetu wameanza kutkubali, nikaingiwa na hamasa, ila sitaki wazazi wangu walifahamu hilo ni mimi na wewe tu…’nikasema

‘Ehe, niambie…unazidi kunipa hamasa…’akasema

‘Lakini unielewe mume wangu, ...sina nia mbaya na wazazi wangu, au jamaa zangu, au jamaa zako, lakini haya hutokea sana katika dunia hii, na sisi kama wazazi inabidi tuwe makini kwa hili...’nikaanzia mbali.

‘Kwani kuna tatizo kutoka kwa wazazi wako tena?’ akauliza akionyesha mashaka

‘Hapana, hili ni kati yangu mimi na wewe, na familia yetu inayokuja, hatujui tutapata watoto wangapi, na hatujui watakuwa wakike au wakiume wangapi, ....hilo ni mimi na wewe lakini linalenga maisha ya mbeleni…’nikasema.

‘Hahaha mke wangu bwana, una wasiwasi,..’akasema akiwa bado hajafahamu nataka kuongea nini.

‘Mume wangu sipo huko kwenye kuzaa kwangu, nipo kwenye baada ya kuzaa, maisha yetu , mali zetu, na mipangilio yetu ya kila siku, maana hilo ndilo muhimu sana....’nikamwambia.

‘Mhhh, mhh, kwahiyo watakaje labda....’akasema huku akikaa vizuri na kuniangalia machoni.

‘Nataka tuwe na mkataba wa kifamilia...’nikasema na yeye akawa kama anashituka halafu akapepesa pepesa macho.

‘Mkataba wa kifamilia, wa nini tena,..si sis tuna ndoa yetu tayari ndoa ni mkataba tosha au sio,… unahitajia mkataba gani tena, huniamini au kuna nini umekigundua dhidi yangu, au familia yangu au yako?’ akaniuliza kwa mashaka.

‘Niliongea na wakili wetu wa kampuni,.....ambaye kama unavyojua, anashughulika kwenye kampuni zote mbili yangu na ya kwako pia, mimi sina lengo la kuingilia kampuni yako saana, lakini hili la mkataba ni kwa ajili ya mali zetu zote, zikiwemo kampuni zetu, ili kusije kukatokea sintofahamu baadaye....’nikasema.

‘Mhhh, okey, niambie maana mpaka sasa sijakupata vyema, na hata hivyo huyo wakili hajaongea na mimi... kwahiyo sijui unachotaka kusema ni nini hasa…’akasema.

‘Ni hivi, katika maswala yote ya mali, kama hakuna matatizo, hakuna shida, lakini kukija kutokea matatizo, watu , binadamu tulivyo, cha kwanza kukimbilia ni mali, hutaamini, watu mlikuwa mnapendana, mnasaidiana, ni marafiki, lakini kukitokea mfarakano kidogo tu, wote akili na macho yao ni kwenye mali...’nikasema

‘Ni kweli, lakini sio mimi….’akasema

‘Najua, sote tutasema hivyo…lakini sio kwetu tu, na wengine wa nje, umeona visa vingapi vinatokea, baba au mama, au baba na mama wakiondoka, kunatokea nini,, watu ambao hata wahajui mali imetokea wapi ndio wa kwanza kuja kuvamia mali za mayatima, wakitamani kila kitu..’nikasema

‘Ni kweli…’akasema

‘Sasa mimi nimesoma sheria kidogo, na nilitaka kile nilichokisomea angalau kije kufanya kazi kimatendo kwenye familia yetu, unaonaje hapo kwanza,…’nikasema.

‘Mke wangu mbona unanitia wasiwasi, ina maana unaogopa kuwa ukienda kujifungua ....unaweza usirudi, hapana bwana,…mke wangu kuzaa ni kawaida tu, hutapata lolote baya...hutakufa bwana, usinitishe…usinitie wasiwasi na majonzi, hakuna shida, huna matatizo yoyote, docta kasema huna tatizo lolote…utajifungua salama…’akasema.

‘Mimi siongei hili kwa vile nakwenda kujifungua, hapana, naliongelea hili kwa ujumla wake, ni jambo la maisha yetu,...na ukumbuke mume wangu, sisi kama wandamu, hatuna mamlaka na mungu, kuwa nitaishi muda gani au nitakufa lini,...’nikasema.

‘Ni kweli…’akasema bado akiniangalia kwa mashaka.

'Lakini hata hivyo ni vyema tukawa na utaratibu mzuri tu, tukajiandaa kwa lolote lile, hata kama tupo hai, bado mkataba unaweza kutusaidia katika maisha yetu, tukawa na utaratibu mnzuri tu kwa nia njema,...’nikasema

‘Ni sawa, nana kukuelewa…’akasema

‘Na hatuombei mabaya…, maana sisi ni wanadamu,kama kutatokea mfarakano wowote, makataba huo utakuja kutusaidia...hamna haja ya kushikana mashati, wakili yupo na mkataba upo..’nikamwambia.

‘Sawa, sawa kabisa....kwahiyo ulikuwa unataka kusema nini, ..tuwe na mkataba, kuhusu nini hasa mali, au…maana ndoa ina masharti yake, kidini kisheria, imebainishwa kila kity au..sijakuelewa zaidi, ?’ akauliza akishika kichwa, nahisi alikuwa akiwazia mbali, na mimi nikamwambia;

‘Eheeeh, sasa tulia nikuambia, mimi niliongea na wakili wangu, akanishauri kuwa sisi ni wanandoa na pia mungu katujalia tujaliwa kuwa na watoto, tuna kampuni, na bahati nzuri tuna kampuni mbili, yako ya ya kwangu..na baba yupo ana hisa kwetu japokuwa ni kidogo, nia ni kuhakikisha anatulinda, tulifanya hivyo kwa nia njema tu..sio kwamba kila mtu ana maisha yake, hapana, ni katika kujijenga zaidi….’nikasema.

‘Sawa kabisa, na huo ulikuwa ni ushauri wako, japokuwa mimi nilitaka tuwe na hisa nusu kwa nusu kwenye kampuni yangu, hata kama sio ya kwako, maana mtaji karibu wote unatoka kwako na kwa wazazi wako...’akasema.

‘Hapana hilo halikufanyika kwa nia mbaya...sote ni wazazi wetu, na uchungu wa familia ulio nao wewe ni sawa na nilio nao mimi, ndio maana hakuna aliyefikiria kuwa ukipata hisa zote hizo, utadhulumu, au utakimbia nazo, ..hilo halipo, na utambue kuwa mimi nakuamini moja kwa moja...amini hivyo...’nikamwambia.

‘Sawa kabisa hata mimi nakuamini sana,...’akasema.

‘Sasa ni hivi, niliongea na wakili wetu, nikamwambia atayarishie mkataba, mkataba ambao, utagusa kila kitu chetu, kuanzia, mali, watoto na hata ndoa yetu,...hii itasaidia sana, ili tuwe makini na si kwenye mali tu, bali pia na kwenye ndoa yetu, mkataba huo uainishe kuwa kama mmoja wetu atakiuka maswala ya ndoa, basi ...amevunja mkataba na mali na kila kitu chake, kinachukuliwa,..’nikasema

‘Mke wangu, unajifunga wewe mwenyewe…’akasema kwa kujiamini

‘Nikuulize wewe je upo tayari na kitu kama hicho , maana mimi sina shida....’hapo nikatulia.

‘Una maana mtu akikiuka hata kwenye maswala ya ndoa…kama, usaliti au sio..ok, inakwenda hadi kwenye mali, mtu anakuwa hana haki na mali tena, kuachia kuchana nak….ok, …mimi sina shida na hilo,..ni sawa kabisa, lakini wewe huoni kuwa wewe ndio utadhulumiwa…’akasema

‘Usijali…’nikasema

‘Unajua nina maana gani, mali ni zako, mtaji umetoka kwa wazazi wako, leo umevunja mkataba mali inakuja kwangu, je wazazi wako watakubali hivyo, hapana hapo kuna walakini...’akasema.

‘Ndio hivyo, kwani wewe unatarajia kukiuka masharti ya ndoa, mimi naliona kwangu ni kinga, sitaweza kukiuka, na sheria ni msimeno, nikikiuka sheria ipo una haki ya kudai haki yako..au sio..?’ nikamuuliza.

‘Kwangu mimi mke wangu sina shida, mimi nakupenda sana mke wangu, sizani kama kuna mtu anaweza kuja kunivuruga akili…, hakuna..kwahiyo mimi naunga mkono huo mkataba, tena bila wasiwasi....lakini ni wewe tu, kama ikatokea, haya utapoteza kila kitu, ila siwezi kukuacha....’akasema na mimi nikamkatisha na kusema;

‘Sawa mimi nilitaka nikuweke wazi kwa hilo,na nilimwambia wakili autayarishe, halafu tutakutana sote kwa pamoja tuusome, tuone kama kuna chochote cha kubadili, au kuongeza,..na ningelipendelea ikiwezekana iwe kama katiba yetu ya familia, na nina imani kuwa hakuna atayekiuka huo mkataba, mimi sina shaka kwangu...’nikasema na kumwangalia.

‘Hata mimi..mimi sina shaka na hilo, ..wewe niamini mia kwa mia...’akasema.

‘Mimi nina uzoefu , mimi naheshimu sana hayo mambo ya mkataba, kwani nimeona jinsi gani unavyosaidia maswala ya kikazi, ndio maana nikaona kwanini mkataba kama hiyo tusiitumie kwenye familia zetu, ili kukwepa makatizo mbeleni..kaa ufikiria kwanza…’nikasema.

‘Hakuna shida kabisa, mimi nipo pamoja na wewe, na nipo tayari kwa hilo...naliunga mkono kwa nguvu moja.’akasema.

‘Sawa kama umekubali basi, tuombe mungu, ...na ni vyema wewe ukakaa ni kuliwazia hilo kwanza, ili uone ni vitu gani muhimu vinahitajika kwenye mkataba huo, isiwe ni mawazo yangu tu, ....au isiwe ni mawazo ya wakili wetu tu,...mkataba huo uwe kama katiba yetu..unaonaje..?’ nikasema.

‘Ni sawa kabisa mke wangu

‘Basi ni vyema, basi kaa ufikirie zaidi….’nikasema nikipumua, sikutarajia kuwa mume wangu atakubaliana na hilo.

‘Mimi sina cha kufikiria zaidi, cha muhimu tukutane na huyo wakili tuone jinsi gani alivyoandaa, na kama kuna nyongeza mimi nitasema, na wewe pia utasema, ili mwisho wa siku tuwe na kitu kimoja cha watu wote, hilo naona lisichukue muda, hata leo, kama wakili keshaandaa, tunaweza kumuita...’akasema.

‘Sawa tutamuita wakili wetu kesho,kama yupo tayari, na kama keshaandaa, nilimuambia akasema ataandaa ,lakini kwanza mimi na wewe tukubaliane....’nikasema

‘Sawa mke wangu, mimi sina shida kabisa mke wangu nakuunga mkono kwa wazo hilo la hekima, nipo tayari kwa wakati wowote...’akasema.

Na baada ya siku mbili mkataba ukatayarishwa, baada ya kukutana na kupitia kila kipengele, na tukaongezea na mengine mengi, ilimradi uwe mkataba unaogusa kila kitu kwenye maisha yetu, na tukaupitisha , ukapelekwa mbele kisheria, na mwisho wa siku ukawa ndio katiba yetu.


Mwanzoni tulikuwa tukifuatilia sana, na ikawa kila mmoja ana hamasa na utaratibu wote, hadi tukawa tumeweza kushika kila jambo, na kila mmoja akawa na tahadhari , asije akavunja mkataba, na kila mara tunakumbusha,kama jambo limafanyika, sivyo ndivyo, utasikia `mkataba unasemaje...’

Siku zikaenda, mambo yakwa mengi, watu tukajisahau,ikafikia hatua hakuna aliyejali kangalia mkataba unasemaje,ila kuna yale mambo ya msingi, kama ya ndoa, masilahi, na uwajibikaji,...mengine madogo madogo yakawa yanakiukwa hapa na pale, hakuna aliyejali,...ilimrdi tunaaminiana...tukajisahau lakini maisha yakaenda mbele, maana kulikuwa hakuna matatizo.


`Ngoja nikausome tena ule mkataba wa familia...’ nikasema sasa nikifungua kabati, hiyo ni nakala niliificha sehemu maalumu, hakuna mtu anayeweza kuupata.

Ufunguo ulikuwepo pale pale,....nikauchukua, na kusogea kwenye kabati, nikahakikisha nimefunga mlango wa ofisini, kabla sijafungua hilo kabati, maana sikutaka mtu aingie na kuja kunisumbua. Nikasogea kwenye lile kabati, na kuchuchumaa, maana sehemu nilipoweka hizo nyaraka ni sehemu ya chini ya hilo kabati, ...

Nikafungua kidroo hicho, kilikuwa na namna ya kukifungua, sio kwa haraka, ni kama unafuatilia namba, nikafuatilia kwa makini mpaka mlango wake ukafunguka...., nakumbuka kabisa wapi niliuweka ile nakala ilikuwa pembeni,..sehemu yake maalumu, niliisimamisha maana ni mkataba mrefu, sikutaka ijikunje…

Nikavuta kidroo chake, kilikuwa kitupu hakuna kitu…

‘Haiwezekani…’nikasema

Nikavuta sehemu yote, kulikuwa na nyaraka nyingine tu ambazo kwa muda huo sikuwa na umuhimu nazo...

Hapo sasa, nikahisi moyo ukinienda mbio,....nikatulia kidogo, labda nimesahau, labda niliwahi kuuchukua huo mkataba, hapana, sijawahi, ni muda sijautumia, sasa upo wapi.

‘Haiwezekani, nakumbuka kabisa huo mkataba niliuweka hapo, kwenye sehemu yake maalumu…’nikawa naongea peke yangu sasa. Na mimi ni hodari sana wa kuweka vitu vyangu kwenye mpangilio wake, na nahakikisha kila nikitoka ofisini kwenda popote, kila kitu nakiweka katika mahali pake kwa mapangilio wake, hilo sikosei hata mara moja.

Nikatuliza kichwa na kutafakari, lakini hakuna dalili yoyote kichwani ya kuniambia kuwa labda niliwahi kuutoa hapo. Nikaingiza mkono ndani na kusogeza kwa ndani kabisa, kama umegandia kwa ndani, hakukuwa na kitu kama hicho, nikaanza kuhisi vibaya. Sasa nikatoa kila kitu, na kupanga upya, ili kuhakikisha, , lakini sikuona cha mkataba wala nini….

Mkataba haupo, ….

‘Ni nani huyu mwenye nia mbaya,kaweza kuugundua huo ufungua, na akautoa, na kufungua hili kabati, halafu akalifunga na kuhakikisha kuwa hajagusa kitu kingine chochote, ni nani huyu…’nikawaza

Kiukweli ufungua wa hapo ni huo huo, hakuna akiba...na hakuna anayefahamu kuwa ufunguo huo upo wapi zaidi ya mimi mwenyewe,….na ni nani anayefahamu kuhusu huo mkataba, zaidi ya mume wangu na wakili…,nikajaribu kuangalia tena kwa makini, lakini mkataba ulikuwa haupo....

Mkataba haukuwepo....!

‘Hakikisha umeharibu kila kitu…kila kitu, hasa mikataba, mengine nitayamaliza nikija…’


NB: Sehemu hii ni muhimu sana, ndio maana nimeandika kwa taraibu na msisitizo, msichoke kusoma sehemu hii, itatusaidia sana kwenye maisha yetu


WAZO LA LEO: Kama tutakuwa na taratibu za mikataba kwenye ndoa zetu, kwenye familia zetu, kwenye vikundi vyetu, kwenye maisha yetu,kwenye sehemu zetu za kazi, nk, tungeliepuka migongano na mfarakano, maana mambo mengi yangelitatuliwa kisheria. Familia nyingi zinajikuta kwenye matatizo,pale anapofariki mmojawapo, au pale kunapotokea tatizo, na kutokuelewana. Na mwisho wa mifarakano hiyo, au matatizo hayo, wahanga wa haya yote ni watoto na akina mama, ambao wanakuja kudhulumiwa haki zao. Je hatuoni kuwa ili kukwepa hayo yote, ni bora kukawa na mikataba katika maisha yetu? Tuliwazie hili na wanasheria watusaidie...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom