Mkuki Kwa Nguruwe (Kisa Cha Kweli)

Abdallahking

JF-Expert Member
Mar 19, 2018
3,983
10,804
Mkasa : MKUKI KWA NGURUWE
Mwandishi: MSUYA M MSUYA (EMUTHREE)
Imeletwa kwenu na
: BURE SERIES

SEHEMU YA 1



Ni kisa na mkasa, chenye mafunzo ndani yake, kinachotokana na ushauri wa kirafiki kati ya marafiki wawili. Ushauri uliokuja kuzaa mtafaruku hadi marafiki hawa wawili wakaja kuwa maadui makubwa wakutaka hata kuuana.

Ulikuwa ushauri wenye nia njema kwa mlengwa, lakini ….athari zake kwa wengine zinaumiza,…je hao wengine wakiwa ni wewe mshauri itakuwaje….

Hutapenda kuona rafiki yako akiteseka, utafanya kila hali ili aondokane na shida hiyo, njia mbadala zilishindikana, ikabakia wazo hilo...lililokujia akilini na kumshauri mwenzako, afanye tu, bila kuangalia upande mwingine wa athari zake….

Kisa hiki ni kumbukumbu za wale wanaoteseka, wenye shida mbali mbali, wenye mitihani ya maisha, wengine wakihitajia kuolewa lakini hawajapata wa kuoa au kuolewa, hawa wanahitajia ushauri, je tuwape ushauri gani…

Wapo wengine wakihitajia watoto, lakini mola hajawajalia,..au wapo wengine walitendwa na wenza wao, wakaachika, au kuachwa kwa namna moja au nyingine. Wapo waliovumilia..wapo walioshindwa kuvumilia,…, na wapo waliojikuta kwenye njia panda…je tuwapatia ushauri gani…

Kisa hiki hiki ni maalumu kwako wewe mtoa ushauri, na wewe mshauriwa…tuweni makini sana kwa dhamana hii ya ushauri! Ushauri sio kuongea tu kwa vile…sio wewe utayefanyiwa, sio wewe …hapana shauri ukijiweka kwenye hiyo nafasi , kama ingelikuwa ni wewe..ingelikuwaje…


Japokuwa unaweza ukatoa wazo hilo kwa nia njema kabisa, ukitaka kumsaidia mwenzako, lakini jiulize huyo atakayetendewa hataumia,…au kama ungelitendewa wewe ungakubali kutendewa, ….maana isije ikawa MKUKI NI KWA NGURUWE TU.

*************

Ilikuwa vigelegele vya shangwe, pale nilipofunga harusi yangu, kiukweli ilikuwa harusi kubwa, kutokana na hali zetu, na aliyesaidia kuhakikisha kila kitu kimekwenda sawa, alikuwa rafiki yangu kipenzi…

‘Rafiki yangu, mume wako ni bonge la handsome…hapo sitii kasoro, na nikuambie kitu, wewe usisumbuke kwa lolote lile, mwili wako na wangu kila kitu niachie mimi, muhimu ni gharama, nipatie fungu, na wewe kaa, tulia, kama ningelikuwa na pesa, nisingelipenda wewe utoe hata senti moja, lakini nitajitahidi…’akasema

‘Ujitahidi kwa vipi, usije kutoa hata senti yako moja, pesa ya harusi hii ilishaandaliwa kwa kila kitu, wewe isimamie tu, na kila kitu nitakukabidhi wewe, nashukuru sana rafiki yangu, wewe ni mimi na mimi ni wewe, …wewe ni rafiki yangu tunajuana, kwa kila hali, nisingelipenda wewe kujiingiza kwenye madeni,… unasikia, ukifanya hivyo utaniudhi…’nikasema

Basi yeye akasimamia kila kitu, nikaja nikafunga ndoa na mume wangu..na maisha na rafiki yangu yakawa ni pale pale, ila alichojitahidi kwa hivi sasa yeye akawa hafiki mara kwa mara nyumbani kwangu, kama ilivyokuwa awali, yeye alifika akiwa na uhakika mimi nipo nyumbani…nilimuelewa, na sio kwamba nilimshuku vibaya hapana ni yeye tu, aliona isje ikajenga fitina…’akaendelea kusimulia.

Masiku, miezi, miaka, ikaenda mimi nikajaliwa watoto, lakini rafiki yangu bado akawa hajaolewa , sio kwasababu kuwa hakupata wachumba, hapana, wachumba ni wengi waliotaka kumuoa, lakini yeye akawa hawakubali kutokana na sababu hii na ile, aliyoiona yeye. Na awali sikupenda kumuingilia sana kwa maamuzi yake hayo, maana ninamfahamu alivyo…ana msimamo wake.

Lakini siku zilivyozidi kwenda mbele ikabidi mimi niingilie kati, nakuumuliza yeye anataka mume wa namna gani, ..japokuwa nafahamu kwa jinsi tulivyokuwa tukiongea awali kabla ya kuolewa, kuwa yeye angelipenda mume wa namna hii na ile, na mimi nikawa namuelezea hivyo, lakini mimi nilipoolewa nikaja kugundua kuwa ndoto za akilini za kuwa utampata mume mwenye kila kitu unachokitaka ni ndoto tu, aghalabu kuwa kweli…

‘Nikuambie rafiki yangu ukweli, huyo mwanaume unayemtaka wewe hajazaliwa, huwezi kumpata mume wa kila kitu unachokitaka wewe, vingine vitakuja huko mbele kwa mbele, na vingine hutaweza kuvipata hadi kufa kwako, ndivyo maisha yalivyo…’nikamshauri siku za mwanzoni,…

‘Usijali rafiki yangu, ipo siku nitaolewa tu, na mume ninayemtaka mimi, hilo la kuwa hajazaliwa halipo,..wapo, ninajua wapo…nitasubiri, ipo siku nitampata , hata hivyo, kuolewa, ni kuolewa, …mimi mwenyewe bado nina malengo yangu..nisingelipnda kukimbilia kuolewa kwanza…’akasema

Maisha yakaenda hivyo, na umri ukakimbia, umri hausemi, …unashangaa sura inabadilika, na majina yababadilika, kijana inageuka mtu mnzima, dada, inageuka kuwa mdada, baadaye…, mama,…mama bila mtoto, baba bila mtoto, mawazo yanaanza kuingia akilini, mawazo..

***************


‘Rafiki yangu nilimpenda sana, tulianza urafiki tukiwa shuleni, na hata tulipoanza kazi, ninafahamu kuwa mimi nina uwezo kuliko yeye kihali, maisha ya familia yangu yalikuwa juu, mwenzangu alitokea familia ya chini, ninaweza kusema hivyo…’ akaendelea kusimulia

‘Mimi nilijitolea kwa kila niwezavyo, rafiki yangu awe kama mimi, kila nilipoweza, akiniambia au hata kama hajaniambia, nilijikuta namsaidia mwenzangu, ilifikia muda kila ninachonunua namnunulia na mwenzangu, kwahiyo tulikuwa kama mapacha..

‘Unajua ilikuwa sifanyi jambo mpaka nishauriane na yeye kabla sijafunga ndoa, na baada ya ndoa, ikaendelea hivyo, japokuwa mengine ya ndani ya ndoa ilibidi nisimuhusishe sana,….kama ujuavyo sheria za ndoa zilivyo.

‘Lakini hata nilipoolewa, sikuacha hiyo tabia, ya kusaidiana na yeye..ila ikafika muda natakiwa kuwa na familia yangu na mume wangu zaidi, hii hali iliniuma pale rafiki yangu anapokuja ananikuta mimi nipo na mume wangu, yeye hana…iliniuma sana, nilitamani huyo mume awe wetu sote, lakini mmh…hapo pagumu.


Baada ya ndoa mambo mengine yalijiweka yenyewe rafiki yangu, alianza kupanga muda wake, ni lini aje kwangu, au lini tukutane naye, hakupenda kuja nyumbani kwangu kama mimi sipo,…sio kwamba sikumiani kwa hilo…au hakupenda wakutane na mume wangu kupata chakula cha mchana bila ya mimi kuwepo, hadi mume wangu akaja kuniuliza ni kwanini;

‘Huyo rafiki yako, ni mwaminifu sana, unajua kuna siku nakutana naye, namuomba nimpeleke lunch, hataki, eti kisa hapendi ije kulete fitina , mkaja kukosana wewe na rafiki yako…, sasa mimi ni shemeji yake nitamfanya nini , eti hivi kweli inaweza mimi nikakusaliti wewe mke wangu, kwa rafiki yako kipenzi…’akasema.

‘Lakini nyie wanaume hamuaminiki,….mimi namuunga mkono kwa hilo,..hata hivyo mimi sina wasiwasi kamwe na rafiki yangu…’nikasema.

‘Ina maana mke wangu kwa kusema hivyo huniamini…?’ mke akamuuliza mke wake.

‘Sio swala la kuaminiana hapo, shetani ana mbinu nyingi, …na kwanini ujiweke kwenye rehani ya mitihani, kama unaweza kuikwepa ni bora kufanya hivyo, kuliko kujitwika mitihani hiyo,….’akasema mke

‘Ok, nimekuelewa sana mke wangu, lakini nikuulize kitu ni kwanini rafiki yako hakubali kuolewa, yeye ni mnzuri ana umbo la mvuto, anataka nini na umri unakwenda…?’ akaniuliza mume wangu.

‘Hata sijui, hajajaliwa bado, siku itafika, ataolewa, ni kweli umri umekwenda, na hata sijui nifanye nini ili ampate mume anayemtaka,…hata sijui…’nikasema.
 
SEHEMU YA 2


‘Japokuwa yeye ni mnzuri, lakini umri unakwenda mshauri sana rafiki yako, leo anapendeza hivyo, kila mwanaume anamtaka, lakini itafika sehemu hatavutia tena, hayo ndiyo maumbile yaliovyo, atakuja kujijutia muda umeshakwenda…’akasema.

‘Najitahidi sana,…hata sijui nimfanyeje tena…’nikasema.

Kiukweli rafiki yangu huyo sikuwa na shaka naye hata kama ningelimkuta yupo na mume wangu, ninamfahamu sana kwa msimamo wake…anaogopa sana waume za watu, ….huwa akiahidi kitu kaahidi, na kwangu nilimuona kama sehemu ya ndugu zangu, na hata watu walimfahamu hivyo kwa msimamo wake huo, wa kutokujihusisha na rafiki ambaye ni mume wa mtu. Wanaume wengi walimjaribu wakashindwa kwa msimamo wke huo.

***************

Kuna kipindi alimpata mwanaume mmoja wakawa wanakutana mara kwa mara nikajua huyo atamuoa, lakini baadaye nilipomuulizia, akanipa jibu la kukatisha tamaa.

‘Yule jamaa sitamkia tena,…hanifai, nilijua ni mtu mwenye msimamo, ..mtu wa matumizi, …lakini kumbe ni nguvu za soda, eti anakuja kunilalamikia kuwa anadaiwa hiki na kile, kwani nilimuambia akope….aah, nimeachana naye…’akasema

‘Hilo tu…?’ nikamuuliza

‘Wewe unaliona dogo hilo, achana naye, ..mengine sio lazima nikuambie,.hata kama wewe ni rafiki yangu, huyo nimeshambwaga…’akasema na sikutaka kumuingilia zaidi,..nafahamu msimamo wake ulivyo.

Kiukweli urafiki wetu ulikuwa ni dhati, na kila mmoja alijua msimamo wa mwingine na hilo ndilo litufanya tuwe hatuyumbi,…lakini ikatokea la kutokea, urafiki ukageuka kuwa shubiri, ukagubikwa na uadui wa kutaka hata kuuana….’akasema

‘Kwanini sasa, mimi nilijua marafiki kama nyie, mliojuana, hamtaweza kuachana…?’ nikauliza

‘Hapana, yule simtaki tena, hata kumuona simtaki hata aje nyumbani kwangu…,’ akasema wka hasira….kwa kauli hiyo nikawa na hamasa ya kutaka kujua kilichoajiri kati yao wawili,

Awali hakutaka kunisimulia undani wa maisha yao, hasa kilichosababisha hadi urafiki wako ukafa na kujenga chuki za kutaka kuuana, lakini baadae akaanza kunisimulia…kilichowafanya marafiki waliojulikana kuwa ni mrafiki wa kweli, marafiki ambao kila mtu alikuwa akitolea mfano kwao, lakini sasa ni maadui wakubwa….

***********

Miaka ikapita na mimi nikajaliwa kuwa na watoto wawili mapacha wa kike na rafiki yangu akawa akitoka kazini anakuja tunakuwa naye, ananisaidia kuwalea, kiasi kwamba watoto hawa walimuona kama mama yao. Na kwa ukaribu huo, watoto wangu walimpenda sana.

‘Nawapenda sana watoto wako, natamani niwe na watoto kama hawa, kwa sura, …natamani mume wangu anizalie kama watoto hawa…’akasema

‘Utawapata tu usijali…lakini muhimu uolewe, umri unakwenda, urembo wa msichana una kikono chake…’nikamwambia tukiwa tunaongea…

Kuna kitu ambacho anacho rafiki yangu, alipenda sana kuchagua wanaume…sio kwa wanaume tu, hata vitu vyake akitaka kununua, yeye anachukua muda mrefu sana kufikia maamuzi, atachagua wee, atatoa kasoro wee….mpaka aridhike, itachukukua muda sana..kilichoniumiza ni kuona rafiki yangu haolewi, na umri unakwenda, yeye hakulijali hilo mapema na siku zikazidi kusonga mbele.

‘Rafiki yangu ukumbuke umri na urembo wa mwanamke, una kikomo, jinsi unavyozidi kukua, na urembo nao unapungua, ..na ujue mwenyezimungu anakupatia neema zake uzitumie, ukizipuuza, itafika muda atakunyang’anya, na hapo utaaanza kulalamika…’nikamwambia.

‘Usijali…ipo sku nitakuambia kusudio langu ni nini…unajua rafiki yangu sipendi nije kuumia,…sipendi nije kujutia,..muda utafika na wewe hutaamini…’akasema

‘Hapo sikuelewi, ina maana kuna kitu unanificha…?’ nikamuuliza

‘Hapana…wewe niamini tu, siwezi kukuficha kitu , wewe ni mimi na mimi ni wewe,lakini siwezi kukuambia kitu ambacho hata mimi sina uhakika nacho , bado sijawa na uhakika wowote kwa hivi sasa, ni nani na nani wa kunioa, nimtakaye hajaonekana na kila ninayempenda, nakuta keshawahiwa, nashindwa kuelewa ni kwanini…’akasema

**************

Siku zikaenda watoto wangu wakawa wakubwa, na wanaanza shule, hebu fikiria, miaka mingapi, kama kumi hivi, bado rafiki yangu hajaolewa,…

Siku moja mwenzangu huyu alikuja nyumbani kwangu, akanikuta mimi nipo na watoto wangu, huwa nikiwa nyumbani kama nimemaliza kazi zangu , huwa napenda kucheza na watoto wangu, najishusha nakuwa kama mtoto mdogo, tunacheza ile michezo niliyokuwa nikicheza nikiwa mdogo, basi ni faraja kwa watoto wangu.

Rafiki yangu akaingia na akawa ananiangalia nikicheza na watoto, aliniangalia kwa makini sana,..nikahisi kama anataka kulia, siku zote huwa ana ujasiri fulani, akija kwa vile watoto wamemzoe kama mama yao, basi watamkimbilia, wataanza kucheza naye, na huku kucheza na watoto yeye ndio kanifundisha…

Lakini siku hiyo, haikuwa hivyo, alikuwa akiwa kanywea, hana raha kabisa, ule uso uliojaa ujasiri haupo tena,, watoto kama kawaida yao walipomuona wakamkimbilia, na akasalimiana nao, kiukweli watoto wangu walimpenda sana rafiki yangu huyu, hata yeye, na hakuchoka kuwasifia kuwa ni watoto wazuri, anapenda kuwa na watoto kama hao.

Siku hiyo hakuwa mchangamfu kabisa, nikajua kuna jambo, awali nilihisi labda anaumwa, lakini nilipomuuliza akasema haumwi,..nikaona kuna jambo jingine kubwa limemtokea, labda…, ikabidi niwatoe watoto ili nipate muda wa kuongea naye


‘Ok.. rafiki yangu vipi leo,…sio kawaida yako, hutaki hata kujiunga tukacheze na watoto kama kawaida yako.., unajua watoto wangu wakikuona wanahisi furaha sana, wanakuona wewe ni mama yao wa ukweli, kuliko hata mimi, vipi leo kulikoni…?’ nikamuuliza

‘Oh rafiki yangu jana sikulala, mawazo,….nahisi sio mimi tena,…sikuwa hivi kabla,….’ Nikaona machozi yakimlenga lenga.

‘Mhh, usilie bwana, niambie kuna tatizo gani…?’ nikamuuliza.

‘Unajua rafiki yangu mara nyingi huwa najipa matumaini, lakini kipindi hiki cha siku mbili tatu, nimekuwa nikiumia sana, nawaza kupitiliza, na hata kujiuliza, ni kwanini, unajua alipo…nitenda yule mwanaume, kunikasaliti wakati nilishapanga yeye ndiye wa kunioa, namkuta na mwanamke mwingine ndani, …imenivunja sana nguvu…’akasema

‘Lakini wapo wengine au sio..keshaoa, achana naye….’nikasema

‘Kwanini sasa inatokea hivyo, kile ninayempenda, tunakwenda vizuri, baadae hali inageuka, inatokea jambo tunakosana na huyo mwanaume ama awe msaliti, au awe na imani nyingine ya dini, na siwezi kuacha imani yangu ya dini, sasa nifanyeje jamani…yaani hata sielewi, inafikia muda siwaamini tena wanaume, kwanini nisimpate mwanaume kama huyo wako….’akasema

‘Utampata tu rafiki yangu, wewe subiria muda utafika…’nikasema

‘Yaani hata kwenye ndoto nimeota nakuona wewe upo na watoto wako na mume wako mnafurahi, mimi nipo peke yangu porini, mkiwa, ..oh, mara nikajiukuta nipo kati kati ya bahari nachukuliwa na maji, napiga ukelele, wa kuomba msaada, hakuna wakunisaidia, nikawa nawaita nyie, mje kuniokoa lakini mkawa hamnisikii, nikawa nazama, nikashtuka …’akatulia

‘Hiyo si ndoto tu, au…?’ nikamuuliza

‘Ni ndoto ndio..lakini nahisi imetokea kwa vile jana niliwaza sana,..mara nyingi najipa matumaini, nikirudi nafanya hiki na kile siwezi sana, lakini jana, sijui ilikuwaje, hawa watu wamenitibua kweli, ..ndio maana sitaki kuolewa…’akasema

‘Akina nani tena…?’ nikamuuliza

‘Si hawa wanaume..inafikia sasa wananiringia mimi, …kuna mmoja kanibwatukia mpaka hamu yake ikaisha, akafikia kusema, nitaishia kuzeeka bila mwanaume..sawa, labda ana ukweli wake, lakini haya ndio maisha yangu, kama anataka anioe, anioe basi, yeye anasema anataka kunipima kwanza, kunichezea, hapana hilo siwezi kabisa…’akasema

‘Kwahiyo, umeshakata tamaa au sio…?’ nikamuuliza

Hapo akakaa kimia akiwa kashika shavu ile ya kusononeka, kiukweli kama rafiki yake ilinuma sana, nikamsogelea na kumkumbatia, hapo akalia kweli, hadi alipotulia, nikamwambia akae , najua sasa ile hasira yake imekwisha

‘Unajua rafiki yangu, ndio maana nilikushauri awali uolewe na yule mwanaume wa kwanza aliyekuwa rafiki yako, ukamkataa, na hawa wengine ilikuwa sio bahati yako, ni wao walikusaliti, sio kusidio lako, tumuachie mungu tu…’nikasema

‘Mhh..ni kweli rafiki yangu sasa kweli naona nimechelewa, maana hata waume nao siwaoni kabisa wanaonifaa, wa umri ninaoutaka mimi hawapo tena, ninaokutana nao, ndio hao wanaotaka kuuchezea mwili wangu, kitu ambacho sikitaki,..natamani atokee mume wa kweli, alete posa, simuoni..wale niliowataka ndio hao wameshaoa…kiujumla kwa sasa sina raha tena…’akasema


‘Sasa unatakaje, maana hata mimi sipati usingizi nikikuwazia wewe. Tumejadiliana na mume wangu tuone jinsi gani ya kukusaidia, lakini wanaume tulio-waona wanakufaa, ndio hao wameshaoa, kama ulivyosema, lakini bado wapo wengine, na wewe huwataki, kwasababu zako…na tulijua yule mliyekuwa naye angekufaa, sasa unasema hamuelewani tena,…sasa, tukusaidieje..?’ nikamuuliza.

‘Kiukweli, nikikuona hivi, wewe upo na watoto wako, nawazia mbali kabisa, najua nilishakosea, na umri ndio huu umeshakwenda sana....naona jinsi gani ulivyo na raha na watoto wako,....nikiwaona watoto wako najisikia kukosa kitu muhimu sana katika maisha,…’akasema

‘Utawapata tu…’nikampa matumaini hayo, lakini moyoni najiuliza kwa vipi.

‘Nitawapataje sasa…?’ akauliza

‘Kwanini unasema hivyo rafiki yangu, kuwapata utawapata tu, ukiolewa au sio, kwanza muhimu ndio hilo,kuolewa, mkubali mmojawapo akuoe, sasa sio muda wa kuchagua tena…’nikasema hivyo na siku hiyo ikaishia hivyo, na masiku yakazidi , miezi, miaka, rafiki yangu hajapata mume wa kumuoa.

Na siku nyingine ambayo naikumbuka sana, akafika kwangu, akiwa hana raha, zaidi ya siku nyingine, nikajua ni yale yale…moyoni nikawa najiuliza nitamsaidiaje, nifanyeje, ningelikuwa na ndugu yangu wa kiume ningelimshinikiza amuoe, lakini sina,, ningekuwa sina wivu, ningemshauri aolewe na mume wangu, lakini nina wivu wa kufa mtu

Hata mume wangu hataki kuoa wake wawili alishaniambia,…kwani siku moja nilimtania tu, akaniambia niache kabisa mawazo hayo, yeye hana uwezo wa kuoa mke zaidi ya mmoja, huyo mmoja kwake, anaona ni kazi…ni mwanaume wangu namfahamu hivyo, kweli hawezi, na hataki..sina shaka na hilo

Sasa nitamsaidiaje rafiki yangu….na katika maongezi ndio likanijia wazo….wazo ambalo lilikuwa ni kisu cha kunichoma mimi mwenyewe…

Ni wazo gani hilo


WAZO LA LEO: Urafiki mwema ni ule wa kujaliana kwa shida na raha, na mkikutana mnashauriana mambo ya heri, mambo yenye tija, na hakikisha kuwa pale unapotoa ushauri kwa mwenzako unampatia ushauri ambao hata wewe ungeliweza kuufanya au kufanyiwa. Usije ukamshauri mwenzako kwenye jambo ambalo kama utakuja kufanyiwa wewe hutakuja kupendezewa nalo.
 
SEHEMU YA 3


Ilipita muda rafiki yangu akawa haonekani, hafiki kwangu na sio kawaida yake na baya zaidi hata kwenye simu yake nikipiga simpati, kwa hali kama hiyo sikuweza kuvumilia, nikafunga safari hadi nyumbani kwake…

Nilipofika nyumbani kwake, sikuweza kumpata, nikauliza majirani wake, wakasema, siku hizi anatoka asubuhi sana kwenda kazini na anarudi usiku sana,…bado sikurizika na hilo jibu, nikaona nipitia kazini kwake, lakini wakati nataka kufanya hivyo, nikapigiwa simu ya muhimu kwenye shughuli zangu za kibiashara, ikabidi nikatize safari hiyo, moyoni nikijipa matumaini kuwa,.., huenda ana sababu zake za msingi za kufanya hivyo.

Baadaye jioni, nikamuona huyu anakuja, alioneka kuwa mnyonge sana, kama mgonjwa, usoni hana raha, uso umesawajika, kachoka, mpaka nikaingiwa na mashaka, nikahisi kuna tatizo, ni lazima kuna tatizo…!

Kwa muda huo, watoto walikuwa kwenye meza wanajisomea, kipindi hicho walikuwa darasa la tano,…wakubwa, na watoto wakike hukua haraka!

Kama kawaida yao walipomuona mama yao kafika…, maana napenda kumuita hivyo, ‘mama yao’ kwa jinsi walivyomzoea, kwa haraka wakaacha kusoma na kusimama na kumsalimia kwa kumkumbatia, wamezoeana hivyo, ..na yeye kama kawaida yake japokuwa alikuwa haonyeshi furaha akajitahidi kuongea nao, akawafundisha fundisha hapo mezani, baadae akawaachia kazi za kufanya, halafu…, tukaenda chumba cha maongezi.

‘Haya niambie maana hata bila kukuuliza kila kitu kinaonekana dhahiri, kwanini tunafanyiana hivi, urafiki wetu umekwenda wapi…?’ nikaanza kulalamika.

‘Rafiki yangu sio kwamba nimefanya makusudi, hata mimi nilikuwa na wakatu mgumu, lakini …kila nikitaka kukupigia, nashindwa, nahisi nitaishia kulia kwenye simu, ..nikitaka nije, ooh…lakini leo sijambo, naona naanza kuizoea hiyo hali, maji yameshamwagika hayazoleki..’akasema

‘Mhh..bado, sijakuelewa…’nikasema

‘Jana niliwaza sana…baada hayo kutokea, baada ya kujipa muda wa kutafakari kwa kina,…, unajua ni kweli,…nilifanya makosa, na kiukweli …hata sijui nifanyeje, na…na…umri wa mwanamke una ukomo wa kuzaa, na mimi nahisi naendea huko, baada ya kwuaza hilo, niliogopa sana kuwa sasa nimeshazeeka bila ya kuwa na …na…hata kumbukumbu…’akasema

‘Mhh, wanasema kitaalamu ndio…lakini mbona watu wanazaa tena wazee tu, ni hivyo kiunjumla, lakini sio kwamba wote watakuwa kwenye hatari hiyo,…kuwa ukizee kw umru huo wa utu uzima ni hatari, hata hivyo…mb- mbona wewe bado tu mdogo, hujafikia kwenye hiyo hatari…, au sio…?’ nikamuuliza

‘Mhh…hapo sasa, urafiki wetu ule wa zamani wa kuambizana ukweli naona umepita, kwa vile mimi sasa nimekiri hilo, kuwa…nimeshaze-zeeka, au sio,…naona hutaki kunishauri mambo ya ukweli, kwa ajili tu ya kunipa matumaini, au sio,….’akasema

‘Mbona nilishakuambia sana hilo…, nikakushauri sana tu…, nikaona basi nijinyamazie tu, maana nakuelewa sana, wewe sio wa jana kwangu, ukiwa na maamuzi yako huingiliki, hata kama mimi ni rafiki yako, huwezi kubadilika mpaka mwenyewe upende…’nikasema

‘Yaani rafiki yangu hilo ndilo limekuwa nikijiuliza akilini mwangu, baada ya kutafakari sana nikaona nije nikuone,...nimegundua kuwa sasa hivi natakiwa nichukue hatua nyingine kabla sijachelewa zaidi…na kiukweli baada ya kutoka hayo, nahisi kipaumbele changu kwa hivi sasa sio mwanaume, ..sio kuolewa, …huu sio muda wa kuwazia kuolewa tena…na baada ya yote hayo, naona ili kuepusha shari zaidi, bora niishi peke yangu, ..kwa kifupi mimi sitaki tena kujiingiza kwenye mawazo ya kuolewa…, nimeshajizoelea kuishi kihivi hivi, kivyangu-vyangu, kuwa na uhuru wa kufanya nipendavyo…’akasema

‘Sizani kama hilo ni sahihi, …hayo sio maisha ya kibina-adamu, lazima kuolewa, ili uweze kupata familia yako, au hutaki watoto,…?’ nikamuuliza

‘Watoto…., watoto….mmh, ….yaani umeshanigusa, hilo….ooh, hata sijui nifanyeje…’akasema akiangalia mlangoni, nahis alitaka kuangali akitu ambacho hakioni.

‘Ndio, sisi ni wanadamu umri wetu una …mipaka na hatujui lini mtu anaondoka duniani, na ubora wa mtu, uzae utoe mbegu na mbegu zije kuotesha mti mwingine, kizazi kinakua,…au sio, usipozaa hutakumbukwa tena hapa duniani…’nikasema

‘Sawa kabisa, hilo ….ndilo lililoniumia jana,…lakini kwa vipi,…na mimi sipendi kuwa mtumwa wa kujipendekeza, eti nikajiangushe kwa mwanaume kuwa yamepita basi, nimekusamehe, hapana, na hata hivyo haiwezekani, siwezi kuingie kwenye mashindani ya kugombea mwanaume…’akasema

‘Kuna kitu unanificha au..?’ nikamuliza

‘Unajua rafiki yangu, nikuambie ukweli, ninachotamani kwa sasa ni kupata mrithi,…kuhakikisha na mimi nabakia ni kizazi cha huko mbeleni, hata kama…hilo,…ndilo naliwazia….’akasema

‘Ni kweli, ni lazima upate kizazi chako, ni lazima upate mtoto, na utapataje, bila kuingia kwenye ndoa,..hilo …labda ndilo la kuwazia,…’nikasema

‘Hapana siwazii, ndoa…mimi nawazia kupata mtoto, ninajua nikipata mtoto basi, maisha yangu yatakuwa na furaha sana…’akasema

‘Hahaha, sasa leo umekuja na jipya, unataka mtoto bila ndoa,…leo umeshabadilika au,sijakusikia vyema,…kuwa unataka uzae nje ya ndoa, au mimi sijakuelewa, au hebu niambie vyema....utapataje mtoto bila ya mwanaume au unataka mtoto wa kurithi, sijakuelewa hapo..?’ nikamuuliza

‘Ninataka mtoto wa kwangu wa kuzaa mimi mwenyewe, lakini nataka iwe halali, isiwe nafanya vibaya, …ndio maana nimekuja kwako tulijadili hilo, kama huko kuolewa hakupo, maana nimesubiri sana sijampata mume wa kunioa, wengi wanataka kuuchezea huu mwili wangu tu,…kwa vile hajatokea mume wa kunioa, basi, nipate angalau hata huyo mtoto, …’akasema.

‘Unataka kusema nini sasa…?’ nikamuuliza na alikuwa kama kaichokoza fikra fulani niliyokuwa nayo akilini, lakini sikupenda kabisa kumshauri rafiki yangu nilijua ni makosa, lakini sasa naona anaelekea huko-huko, ila sikutaka kuianzisha mimi, nikasubiria.

‘Natamani mtoto rafiki yangu, lakini kwa vipi, kama ulivyosema sijaolewa, na mtoto akizaliwa, najua hata kuwa na muonekano mnzuri kwa jamii, atapewa ‘majina mapya…’ akasema kama anaimba

‘Na mbaya zaidi,..hilo mimi silitaki,..eti aje kuitwa mtoto aliyepatikana kwa njia za haramu, mimi nitaonekana muhuni…ooh, kwanini mimi..unajua najishia vibaya sana…kwanini lakini…, silipendi, ndio maana nimejitahidi kujizuia sana nisije kwanza hapa, maana ningelifika kwa muda huo ningeliishia kulia,..sitaki huo unyonge,..’akasema

‘Sasa ina maana unatakaje sasa rafiki yangu..au kwani imekuwaje tena, maana sisi tulishajua sasa mambo yanaelekea kwema, au..?’ nikamuuliza

‘Hapo sasa, ndio maana nimewaza sana hilo…mpaka kichwa kinauma, nimekuja kwako tushauriane, nilikuwa nimejitenga kidogo kuja huku nikiwazia hili jambo kwa makini sana, nimeshindwa namna, nifanyeje…mimi nataka mtoto, natamani nipate na mimi mtoto wangu…., nilitamani ndoa, ndoa haijatokea, sasa hata mtoto jamani…’akasema kwa sauti ya huzuni.

‘Nikushauri rafiki yangu, ukianza mtindo huo, utazalishwa na waume tofauti tofauti, na kuwa na watoto wa kila mmoja na baba yake, huoni hiyo itakuja kukuletea mawazo mengine uzeeni kwako,…maana sawa, utakutana na mwanaume ilimradi mwanaume upate mtoto, utazaa wa kike, ..kesho utataka wa kiume, utaenda kutembea na bwana mwingine atakuzalisha,kumbe anakuja tena wa kike…kesho kutwa utataka mwingine…huoni itakuleta sifa mbaya…?’ nikamwambia

‘Aaah, hayo ya huko mbele anayajua mungu peke yake, tugange haya yaliyopo sasa,,, kwani wewe unajua kesho itakuwaje, nikifa hapa si ndio mtanisahau kabisa, sina hata kumbukumbu huku nyuma, au sio, hiyo ndio ajenda yetu, tuijadili …’akasema hivyo , na kwa vile namfahamu sana rafiki yangu sikutaka kumchukulia kwa haraka.

‘Unajua rafiki yangu nilikushauri sana awali, ukanipuuzia, sasa umri ndio huo umekwenda, na tabia yako haibadiliki, wanaume wameshakusoma wameshakugundua ulivyo,…kuwa wewe ni mtu wa matumizi tu,..dharau, msomi sana,… mtoto wa bei mbaya, mtu wa matumizi makubwa, wanaume hawapendi hayo maisha,…wanmeshakuogopa, na maisha yenyewe yalivyo,..oh, angalia sana…’nikasema

‘Sasa ndio imekuwa hivyo, mimi ndio nipo hivyo, sina mbadala, na hata nijitahidi vipi kwasasa ni nani ataniamini kuwa nimebadilika,..labda niende ulaya nikamtafute mnzungu mzee…hahaha, …nacheka utafikiri nina raha, naumia mwenzako,…ni nani atakayenipenda hivi sasa, hakuna…, lakini sitaki kuzalilika…, nataka maisha ya hapa hapa kwetu, nataka mtoto wa damu ya kiafrika, nataka mtoto kihalali, sasa kwa vipi….’akasema


‘Vipi yule shemeji , kawaje kwani, mbona naona anakupenda sana imekuwaje, sisi tulitaka tuonane na nyie wawili tunishinikize ndoa…kwanini yeye asikuoe, ili upate huyo mtoto, mimi nakushauri hivyo…’nikamshauri.

‘Mhh, ungelijua,..yule ..hahaha sitaki hata kumsikia tena, sitai simtaki, na hata hivyo ipo wazi, sio wangu tena…’akasema

‘Kwanini…niambie..’nikasema

‘Siku kadhaa , alisita kuja kwangu, sikujua ni kwanini, nikasubiria wee, niaona kwanini nisjiumize kwa mawazo, nikasema ngoja niende kwake…labda anaumwa, sikutaka kumpigia simu, maana tulishazoeana kihivyo…basi, nikaenda kwake,.., ile nafika eneo la nyumba yake,…nikahisi mwili unasisimuka ajabu…, nikahisi kuna tatizo…lakini nikajipa moyo, nikafika nikagonga geti…kumbe lipo wazi, nikafungua hadi kwenye mlango wa nyumba,…’ hapo akatulia kidogo.

‘Unajua kabla sijagonga mlango, ukafunguliwa,…, mara anatokea mdada half cast, si unajue waniga fulani,..kijamika jamaika fulani, alivyo sio….kavaa khanga moja, ile ya khanga moja hakuna kitu kingine ndani, mhh, kuashiria nini hapo, kuwa katokea wapi sio.. utajaza mwenyewe……’akatulia akikunja uso kwa hasira

‘Mhh, kwahiyo ina maana gani hapo…?’ nikamuuliza

‘Ndio hapo nakuambia, mimi nina gundu…nina mkosi gani sijui, na uelewe baada y aule ushauri wenu na shemeji, nilipanga niende nimwambie sasa tufunge ndoa, nimekukubali, na sitaki kupoteza muda tena, na hilo alikuwa akilisubiria, niliwahi kumwambia akasita, akawa haniamini, sasa nilitaka nimuhakikishie kuwa nipo tayari,… siku hiyo nilipanga iwe hivyo,..hebu jiweke kwenye nafasi yangu uone nilivyoumia,… sasa sijiu kwanini alinifanya hivyo, hata sijui muda wote huo, kwanini hakuaniambia ana mchumba wake anasoma huko marekani…leo hii, inatokea hivyo…’akasema

‘Ulimuuliza baada ya hapo…?’ nikamuuliza

‘Mimi tena, ..mimi, weeh, unanijua nilivyo, wee…mimi nikamuuliza,hahaha, sikuwa na muda huo,… hapana,…nilipojua kuwa huyo ni mchumba wake, nikaondoka zangu na hata aliponipigia simu sikutaka kabisa kupokea, na hali hiyo ilinitesa sana, sikutaka hata kuja kuongea na nyie, na ningelikutana na yeye, angelinijua mimi ni paka mwenye makucha makali…’akatulia

‘Sasa ulijuaje kuwa ni mchumba wake..sijakuelewa hapo?’ nikamuuliza

‘Nilimuuliza, ilibidi amuite kwani alikuwa ndani, na mara huyu, ti-ti-ti…katoka na taulo na likitambi-tambi lake, unajua kajiachia sana, na likitambi lake,.. sipendi hali hiyo, lakini nilishafikia sehemu nikaanza kumpenda tu, alivyo, kubembeleza, hakati tamaa..kumbe alikuwa na lengo lake…’akatulia

‘Nikamuuliza huyo kinyago ni nani…?’

‘Kinyago, hahaha huyu ni mchumba wangu….’akasema na huyo binti, akasimama pemebni yake na kumwekea mikono hivi, kimahaba, kuninyaa…nikihisi ile hali natamani irejee niwe na gun, niwashoot…lakini yamepita…’akatulia

‘Pole sana…’nikasema
 
SEHEMU YA 4


‘Kiukweli…niliumia sana, unajua kuumia, mtu nilishasema huyu sasa ndiye wangu, leo hii inatokea hivyo, ni mara ya ngapi yanatokea haya, hapana siwezi tena,siwezi kuyabeba haya tena…sitaki mwanaume tena,…’akageuka akizuia machozi.

‘Pole sana sikujua,…na kwanini hukunipigia angalau simu…?’ nikamuuliza

‘Hayo tuyaache, mimi nimekuja na wazo hilo unisaidie kwa ushauri nifanyeje sasa ili na mimi nimpate mtoto, maana …nimeshafika sehemu sitaki kupenda mwanaume tena…, nataka nimpate mtoto wa kuniliwaza tu..basi…’akasema


‘Kwahiyo upo thabiti na msimao huo, are sure about it ….umedhamiria kufanya hivyo, au unatakaje, maana mtoto sio wa kupata hivi hivi tu kama kuku, au sio..kuwa upite hivi jogoo akupande, au sio…?’ Nikamuuliza

‘Mimi kwa hivi sasa sitaki mwanaume, na kama yupo, yupi tena, hao wakunitesa, hakuna tena mwanaume mwanifu, hawapo..wote ni waongo , wahuni, wana hadaa, wema wazuri, waaminifu wameshaoa, nina imani hiyo, hakuna…sasa nifanyeje nife bila hata ya mtoto…’akasema

‘Sijakuelewa hapo ina maana unataka mtoto kwa vipi hapo,…?’ nikamuuliza kwa mshangao kidogo.

‘Vyovyote iwavyo,…kwani kama ingelikuwepo ndoa, angelikuwepo wa kunioa ningelihangaika hivi, kwanini nihangaike…ndoa siioni tena, siwaoni kabisa wa ndoa hapa, wengi wao nimeshawajua ni tamaa zao za mwili wangu tu,na hilo ndio sasa silitaki tena, nimechoka kuchezewa-chezewa, wakunioa simuoni tena, …’akasema


‘Hapo sasa pagumu, ..maana wewe ni rafiki yangu, siwezi kukushauri jambo ambalo hata mimi silipendi,…’nikasema

‘Rafiki yangu, wewe ndiye umenishinikiza na mawazo haya, sikuwa na mawazo kabisa ya kuolewa…unajua, nilijionea sawa tu…,sikuwa na mawazo ya maisha ya famalia, lakini wewe nikija hapa tukiongea unakuja na kauli zako hizo, olewa, olewa…mtoto , mtoto, na zidi nikikuona una watoto wako, na mimi navutika, naingiwa na hamasa hiyo….’akasema

‘Basi tafuta mume mwingine aku-oe, hata kama humpendi kihivyo, mtakuja kupendana mbele kwa mbele…’nikasema

‘Hahaha..mume , ilimradi mume, mimi….haya tuseme hilo sawa, haya yupo wapi huyo mwanaume…’akasema

‘Kwahiyo wewe kwa hivi sasa hufikirii kupata mwanaume wa kukupenda tena, mbona wewe ni mnzuri, wanume wanakutamani, mimi hilo siamini kuwa hakuna mwanaume anayekutaka tena..’nikasema

‘Wewe unasema tu, kwa vile unaye,..sio rahisi kihivyo,..na siwezi, kujiuza, kujizalilisha,…ila wazo langu ni hilo, nishauri, kama huna ushauri niondoke zangu…’akasema

‘Mhh kifupi nimekuelewa umefikia hapa kwa maamuzi hayo baada ya kutendwa,…chuki ikajitokeza dhidi ya wanaume au sio , achana na huyo piga moyo konde utapata mwingine au kwanini hadi ukate tamaaa kihivyo…?’ nikamuuliza.

‘Ingewezekana akapatikana wa kunioa, ambaye pia namkubali, ..na asije kunitenda hivyo tena, ningekuwa na uhakika huo, sawa, lakini huyo mwanaume wa ngapi, watano wote wananifanyia hivyo hivyo…mimi, nina mkosi gani,…sitaki tena nimesha kata tamaa …licha ya tabia yangu ya kuchagua-chagua, lakini ilishafikia muda nikasema haya, si kuna kuolewa, haya nioeni,..anatokea huyu tukifikia mahali pa kufanikisha linatokea la kutokea..

‘Ni bahati mbaya tu…’nikasema

‘Huyu wa mwisho ndio akanimaliza kabisa…hapana,…nimechoka, kwanini mimi, ina maana adhabu za kuwakataa waume nikiwa binti ndio zinaendelea mpaka sasa, ina maana mimi nina madhambi makubwa kiaisi hicho…’akageuka kuangalia pembeni akificha machozi.

‘Hapana sio sababu hizo, ila wanaume nao wana chaguzi zao, wana mitizamo yao, wengi wao akili zako ni moja, wao wanataka wenye tabia fulani, tabia nzuri, ..nk.. hata kama wao hawana tabia hizo,…hawajui kuwa na wewe ulikuwa na mtizamo wako…’nikwambia

‘Tusipoteze muda …mimi sasa nataka mtoto tu inatosha, lakini mtoto….aweje, …kwa vipi, nitampataje, nataka ushauri wako, nisaidie rafiki yangu…

‘Mhh, unaniweka pagumu,..unajua rafiki yangu, ukizaa mtoto bila ya mume, huyo- huyo mtoto atakuja kumuhitajia baba yake, utafanyeje huko mbele, …maana sawa, nitakushauri kapachikwe mimba sijui kama utakavyo, kwani kupata mimba ni ngumu, kama una kizazi…’nikasema

‘Kwahiyo…?’ akauliza akikuna kuna kichwa.

‘Au labda ukarithi, wapo watoto mayatima kwanini usiende kumchukua mmoja ukafuata taratibu za kurithi,…’nikamwambia hapo akaniangalia kwa jicho baya, halafu akasema kwa hasira.

‘Nimekuambia mimi nataka wa kumzaa mimi mwenyewe, aje kunyonya ziwa langu aje kupitia taratibu zote za mtoto wangu …na zaidi ya hapo awe mtoto atakayekidhi viwango vyangu, unajua, ...’akasema akiwaangalia watoto wangu, mbao walifika kuna kitu walihitajia, nikawasikilia halafu wakaondoka.

‘Kama ni hivyo mbona ni kazi rahisi sana....’nikasema hapo akaniangalia kwa hamasa, sijui alitaka niseme hivyo, nilivyosema au kwanini aliniangalia machoni kwa hamasa kubwa.

‘Ni kazi rahisi eeh, sasa niambie nifanyeje….maana wewe ni rafiki yangu, na kwenye dini wanasemaje, mpendelee rafiki yako, au sio..umpe kile unachokipenda, name natarajia utanifanyia hivyo..nishauri, nisiendelee kuteseka, maana baada ya hapo, unaweza ukasikia mengine, naweza hata kujiua,..sikutanii, nimeshafikia kubaya…’akasema

‘Oh, imekuwa hayo…’nikasema

‘Sitanii, niambie sasa, nifanyeje, …wewe ndiye rafiki yangu wa pekee nikishindwa hapa, basi, dunia, hainitaki tena, tumeshirikiana mengi tokea utotoni, hili nalo nahisi utanisaidia,...maana wewe ni mimi, japokuwa kwa hili huwezi kujua ninavyoumia kichwani,…unajua … nilipowaona watoto wako wakiingia hapa, nikahisi ni wangu..nawapenda sana watoto wako….’akasema

‘Basi kama umedhamiria hivyo,,…japokuwa sio sahihi, mimi nitakupa ushauri wangu ila..ninaona tena sana iwe siri, kati yako mimi na wewe….sawa….?...’mara mlango ukagongwa, mume wangu akafika….

NB: Msiseme ninazunguka, ..hii ni tamithlya, inajiongeza, ngoja huo ushauri sehem ijayo.

WAZO LA LEO: Udhaifi wetu kibinadamu unaweza kutufanya tufikie kufanya yale ambayo hata hatukukusudia, …uhimili wetu unafikia kikomo, hasa ukiwa huna imani thabiti ya kumjua mola muweza, kuwa yeye ndiye mpaji. Na imani hii haianzi ghafla tu, imani hii huanzia utotoni. Nawausia wenzangu na kujihusia mimi mwenyewe, tuwajenge watoto wetu mapema kwenye imani sahihi za dini. Ulimwengu hivi sasa unashuhudia mambo ya ajabu , yanayotokea hivi sasa, na zaidi ya yaliyoandikwa kwenye vitabu vya imani, yamepitiliza, …iliyobakia ni mungu mwenyewe anajua. Tumuombe mola wetu avilinde vizazi vyetu, kwenye mitihani hii , ambayo huko zama ilitokea gharika, ..watu wakaangamia, je hivi sasa itatokea nini…Ewe mola tunakuomba utusamehe, utuongoze kwenye njia sahihi tusije kuangamia kama hao, waliowahi kuangamia.
 
SEHEMU YA 5


Kama nilivyokwisha kusema awali, rafiki yangu tulishibana sana, na tulijaliana sana, na hakuna angelipenda kufanya jambo kwa mwenzake ila liwe la heri na lisiwe la kumkwanza mwingine, tulichunga sana hilo, tokea tulipokuwa na akili…kwa hali hiyo tulichunga mipaka yetu kuhakikisha hatukwazani.

Na kwa upande wa mume wangu alikuwa mpole sana, hakupenda makuu, hakuwa na tabia mbaya , hakuwa mlevi, kuvuta sigara, au tabia za uhuni-uhuni, na alinijali sana na kuijali ndoa yake. Sikuwa na wasiwasi kabisa na mume wangu, na usingeliweza kunidanganya kitu kuhusu mume wangu…na yeye hakupenda kufanya jambo linaloweza kunikera mimi au familia yake, alichunga sana hilo, ni mume wa pekee..ndio maana hata rafiki yangu alimuheshimu sana

‘Mume wako namuheshimu kama mkwe, nampenda sana kwa tabia yake, yaonyesha kabisa hana tamaa, au tabia mbaya, na wanaume wa namna hii ni wachache saa,..unajua nikimuona mahali natamani asinione, sipendi, hali ya kuwa naye faragha, japokuwa ananisalimia vyema tu…na kuna kipindi ananialika chakula cha mchana, namkatalia

‘Kwanini unafanya hivyo, huoni atakufikiria vibaya, huyo ni shemeji yako, si zani kama mnaweza kufanya lolote baya…?’ nikamuliza rafiki yangu siku moja kipindi hicho nina uja uzito.

‘Hapana sitaki watu waje kusema lolote dhidi yetu, najua watu wanaweza kujenga fitina na urafiki wetu ukaja kuleta madoa, nachunga sana hilo…sisi tumetoka mbali,..na kama tulivyowahi kuambizana, muhimu ni kuchunga yale yote yanayoweza kuvuruga urafiki wetu, sitakufanyia chochote kibaya, nikijua kitakuja kukuumiza, ni bora nikafanye kwa wengine na sio kwako…’akasema

‘Usijali, mimi na wewe..sina shaka kwa hilo….mimi nafahamu hata kama itatokea mkalala chumba kimoja na mume wangu bado nina imani kuwa hutawezi kunisaliti, hahaha.’nikasema tukacheka.

‘Ni kweli…hahaha eti tulale chumba kimoja ina maana vyumba vya wageni havipo, tusifikie huko ..pa kujaribiana…’akasema

Mimi na rafiki yangu ilikuwa hivyo…

Nayaweka haya bayana kwanza, ili uone tulivyokuwa tumeshibana na huyo rafiki yangu, kwahiyo kwa kutoa kwangu ushauri kama ule.., sikuwa nina mashaka yoyote na yeye, maana wengine watasema kwanini, ukamshauri mwenzako hivyo, wakati una mume, kwanini sikumshuku vibaya…na najua itakuwa hivyo…. aah, nilimshauri rafiki yangu nikijua atafanya kile ambacho hakiwezi kuniumiza na atafanikiwa na hatimaye na yeye atakuwa na furaha,…

‘Sasa nilimshauri nini, hebu sikia ushauri wangu….

Tuendelee na kisa chetu…

*************

‘Kama ni hivyo, mimi sioni kwamba kuna tatizo, kwanza wewe tayari ni mzoefu wa wanaume,…mimi sijawahi kuwa na mahusiano yoyote zaidi ya huyo mume wangu, kwahiyo kwako, sioni kama ni tatizo, au…?’ nikamuuliza, baada ya mume wangu kuondoka,…

Mume wangu alipofika tulikatisha mazungumzo, hakukaa sana, alisema alikuja mara moja, kuna sehemu anakwenda mara moja…


‘Ugumu unakujaje …nataka mtoto ambaye ana sura ninayoitamani mimi, ..yaani ninachowazia, sio ilimradi tu kupata mtoto, ukichagua nyama, chagua iliyonona, au sio, ….unajua sitaki kukufuru, ila kwa vile nimeamua hivyo, basi kiwe kile kitakachonisuuza moyo wangu….’akasema.


‘Wewe cha muhimu si ni kupata mtoto, hujali tena cha ndoa, au sio..hapo uwe na uhakika,..usije kusema aaha rafiki yangu, kanichuuza…kama ni hivyo, …, basi zaa kwanza na mwanaume yoyote…ningependa kukushauri hivyo…’nikasema na kumkagua usoni.


‘Hapana ….sio hivyo…’akasema.


‘Sio hivyo kwa vipi tena, kwani unataka akuoe,….au wewe watakaje…mimi nilionea hivyo, wewe uzae kwanza na yoyote yule… , huku ukiendelea kusubiria kama utapata mwanaume chagua lako ambaye ataweza kukuoa, lakini huku ushapata mtoto wako ili kutokuingia kwenye umri hatari hujazaa..…unaona hapo, hata akiolewa umeshafikia huo umri, huna haja ya kuzaa tena maana unaye mtoto tayari unaona hilo wazo langu lilivyokaa...’nikamwambia na yeye akaniangalia sasa kwa uso uliojaa hamasa.


‘Hapo sasa nimekuelewa, hivi kweli hilo inawezekana kirahisi hivyo…?’ akauliza


‘Kwanini isiwezekane, hahaha, wewe ni mjanja bwana, usitake kunifanya kwua mimi sikufahamu, …’nikasema.


‘Mhh, kunifahamu unanifahamu lakini sivyo kama nitakavyo mimi….’akasema

‘Unatakaje…?’ nikamuuliza

‘Kwanza niambie, kwa vipi hapo, maana nilitaka nizae ndani ya ndoa,..huo ndio ukweli wangu, sasa ndoa imegoma, hivi sasa tunashauriana kuwa ni zae tu hata nje ya ndoa…si hivyo…?’ akaniuliza

‘Hilo ni jibu lipigie mstari, au…?’ nikasema na kumuuliza

‘Mmhh, hapo kwangu bado pagumu kweli kweli,…isingelikuwa hoja hiyo ya kuchelewa kwa umri, nsingelijali sana, isingelikuwa ….aah, hapana mimi nataka mtoto, kwa vyovyote vile…lakini sipendi maana hapo nitakuwa nimekiuka kiapo changu,…nitakuwa msaliti wa ahadi yengu mwenyewe..unajua , niliapa mimi sitazaa nje ya ndoa, sasa nifanyeje mungu wangu,..?’ akaniuliza.

‘Hili si unalifanya kwasababu, hii tuichukue kama dharura, maana …. umri umekwenda, au sio, unaogopa utafikia kikomo kabla hujapata mtoto, hiyo si dharura, au sio…. basi wewe cha kufanya ni kutembea na mwanaume yoyote, …mimi hapo nasema ‘yo-yo-te’ sijui kwako wewe….maana mtoto ni mtoto au sio, kwa mzazi kama mimi…’nikasema

‘Ha-pa-na sio kwa yoyote, hilo hapo natofautiana na wewe kidogo, tuliweke sawa hilo, ..maana yoyote atanizalia mtoto yoyote, hapana, mimi nataka yule atakayenipatia nikitakacho, moyo unapenda, unaona hapo, tuliangalia kihivyo, mimi naona hapo turekebishe kidogo....’akasema.

‘Mpaka hapo tunakwenda sawa, siwezi kukukatilia hivyo uakavyo, ila wasiwasi ni kuwa ukianza kumtafuta umtakaye inaweza ikachukua muda tena,…na hujui ya kesho au sio….’nikasema

'Mhhh…hapo sasa, unaleta ugumu , mimi kama nimeamua kula haramu, basi acaha nile haramu haswaa…unielewe hapo, sitaki nile haramu halafu nisikie kichefu chefu, hapama, nataka mume anipatie mtoto ninayempenda….’akasema

‘Wewe ndio unaleta ugumu, unarudi kule pa kuchagua chagua..mwishowe siku zinakwenda, …’nikasema

‘Hapana si ndio tunawekana sawa, tukishakubaliana hilo, kuwa nataka mume atakaye nizalia mtoto ni nimpendaye,…hapo tutaingia kuangalia ni nani…unajua pamoja na yote mimi najali sana mtoto wangu aweje, naanza kuangalia sasa…nisije kujitia baadaye…mtoto awe na sura , tabia, maumbile…ninayoyatamani mimi, eeh, hapo hapo tufanyeje ..’akawa kama anaota au kujenga taswira fulani akilini

‘Aaah, unajua kwangu mimi kama mzazi mtoto ni mtoto tu…hayo ya sura, sijui nini, hayo ni wewe ambaye hujabahatika kuzaa, …mmh, na wewe kwa kuchagua, unachagua mpaka maumbile ya mwenyezimungu, usikufuru kihivyo,….’nikasema

‘We-we..unasema mtoto ni mtoto tu, ina maana mimi kuchukua dhima hiyo basi nijizalie tu,… hapana..ni lazima nifanye jambo nije kulifurahia mwenyewe, sitaki nije kujutia baadae,.. najua nimetenda dhambi, tena ya kudhamiria,…sasa nije kupata adhabu hivi hivi tu, mungu anisamehe tu, sipendi hili jamani,…sasa mimi nitakavyo nikipate nikitakacho,..nizae mtoto nikimuangalia hivi eeh , moyo unasuuzika na wala nisije kujijutia…’akasema

‘Oh, mungu wangu , hapo sio dharura tena,..ni dhamira mbaya,..hebu niambie kwahiyo wewe unatakaje…?’ nikamuuliza

‘Ninataka huyu mwanaume akinipa mimba, nizae mtoto mwenye sura nzuri, umbo nzuri, maana na mtoto anarithi tabia, basi awe na tabia nzuri kutoka kwa baba yake,…na hata mimi nikimuona huyo mtoto ninafurahi mwenyewe…’akasema akitabasamu sio kama alivyokuwa awali, sasa uso umeshaanza kunawiri na urembo wake ukawa bayana, kiukweli rafki yangu ni mrembo, sijui kwanini kapata bahati hiyo mbaya ya kutokuelewa.

‘Mhh, ….haya, kama utakavyo ni hivyo, basi twende hivyo hivyo, nikubaliane na wewe, na lile wazo langu la mwanaume yoyoete tuliondoe, sawa, twende sasa,…kwahiyo inabidi hapo uchague mwanaume sasa kama ni hivyo mbona ulikosa wa kukuoa, maana usione ni rahisi kumpata atakayekidhi viwango vyote, ndoa inajengwa na wawili na ndiyo inazaa chema..’nikasema

‘Ndio hapo unisaidie, wewe ushaingia kwenye ndoa, ..na najua vyovyote iwavyo, mtoto huwa anatokana na damu ya wazazi wake, hata tabia, uziri, umbile ndio basi tena…nisaidie kwa hapo…’akasema

‘Unajua wewe unanitwika mzigo ambao mimi sina tabia nao…mimi sijui kuchagua chagua kihivyo, najua chema ukimuomba mungu atakupatia, sio mpaka nianza kuchagua tu..kama nguo,..hapa hatuzungumizii nguo, tunazungumzia mtu, na mtu huletwa na utashi, wa muumbaji, ..sio kweli kuwa unaweza kumpata mume akakupatia hichoukitakacho…’nikasema

‘Rafiki yangu tuangalia uhalisia, hili ulilonishauri, la kuzaa eeh, hata nje ndoa, ni uhalisia, pia linaendana na maumbile, ..tusikwepe ukweli hapa…’akasema

‘Ok, sawa nimekuelewa…..’nikasema
 
SEHEMU YA 6


‘Sasa tuseme tumeshakubaliana huyo mwanaume aweje, ..eeh,awe nitakavyo mimi, kazi inakuja , nitamuanzaje, kuwa nataka unipe mimba, au nataka…inakuwa kama nauza mwili wangu..huoni hapo najizalilisha…’akasema


‘Hilo rafiki yangu utaanzaje, mimi siwezi kujua, najua wanaume wakiona ishara fulani wanajua huyo mwanamke anataka kitu..kapenda, tatizo ni huyo mwanaume uliyemchagua je…ana tabia hiyo,…’nikasema

‘Unajua kuna kitu nikuambia ukweli rafiki yangu, pamoja na ya kuwa hawataki kunioa,..lakini nimegundua kitu, wanaume wengi wananiangalia kwa matamanio,..wengine wananitongoza, tatizo ni hilo wengi wao, wanachotaka ni mwili wangu, na wengi wao sijawapenda…sasa hapo, nifanyeje….?' akasema.

‘Unajua pamoja nakushauri hivyo, bado mimi silipendi hilo wazo,…lakini pia nakuona kweli umri umekwenda, na wanaume ndio hao, …mikosi, sijui tuite hivyo, au ndio huko kuchagua kwako kumefikia…’nikasema

‘Tusirudi huko, tutashindwa kufikia muafaka,…najua mungu anakuadhibu, kwa kasumba yangu hiyo, sawa….’akasema

‘Hapana usifikirie hivyo….mimi bado nilikuwa na imani kuwa muda bado upo,…lakini mtoto kweli ana umuhimu wake, cha kufanya mtafaute huyo unayempenda, mengine utajua mwenyewe cha kufanya, usitake mimi nikutanue kila kitu...’ nikasema na hapo akanikazia macho kwa kushangaa.

‘Nimtafute yoyote ninaye mpenda, bila kujali,…aah ina maana unanishauri hivyo, yoyote ninayempenda, …mmh, hapo sasa ndio naanza kuogopa, maana,….sijui sijui..nifanyeje rafiki yangu…?’ akaniuliza

' Wewe wazo lako si kuzaa tu na mwanaume yeyote unayeona atakuwezesha kupata mtoto mwenye sura unayoipenda wewe, si ndio hivyo naona hata `wadhungu’ wanafanya hivyo, wanaingia kwenye mitandao, wanaandika wakitakacho kuna mawakala wanakutafutia, sasa huku hakuna, ila wewe unaweza kutafuta mwenyewe,....na kwako wewe sizani kama itakuwa ni ngumu kihivyo, wewe mwenyewe unajifanya u mzungu, unaishi kizungu-zungu, matawi ya juu, kwanini kitu kidogo kama hicho kikushinde, haikuwa na haja ya kuja kuniuliza hayo yote.., au sio, mtafute unayempenda uzae naye...kwa siri…unielewe hapo…'hatimaye nikamshauri hivyo rafiki yangu.

‘Sasa nikufuchulia ukweli,..sikuwa na wazo hilo kabisa, maana naogopa sana, ila uliponishauri hivyo wewe rafiki yangu kuwa naweza ..sas anikuambie ukweli, wengi ninaowapenda, kama mungu angenijalia, …wengi ninao ona wanaweza kunipatia mtoto nimtakaje ni waume za watu, ndio hapo naogopa sana.…’nikasema

‘Oh waume za watu ina maana hakuna mwanaume mwingine ambaye hajaoa, hapo uanishangaza, waume wapo wengi, wana umbile, sura nzuri, kwanini ushindwe kuwapata, mimi hapo sioni kuwa ni tatizo …’nikasema

‘Ni tatizo,..maana ni waume za watu, ndio sana nawapenda, ndio sana nikiangalia watoto wao nasema hata mimi nataka mtoto kama yule, nina ushahidi wa kizazi chao, hawa ambao hawajazaa, sina ushahidi nao, ndio maana naingiwa na mashaka nao, uone wazo langu lilivyo, hao, nawa-penda, sio kuwa….unielewe, sio kwamba nina nia mbaya nao, lakini ndio najua wataweza kunizalia kile nikitakacho na nina uhakika nacho..…’akasema

‘Mhh, rafiki yangu utavuruga ndoa za watu, ….’nikasema

‘Sasa mbona unaharibu, unanitisha, basi tuache….’akasema

‘Sio nakutisha, nawazia mbali unajua…’nikasema

‘Kiukweli mimi sipendi kuvuruga ndoa za watu…yaani sijui kwanini, sijawahi kumuona wa kumpenda ninayevutika naye, ambaye nahisi nikizaa naye nitapata mtoto mwenye sura na umbile nilipendalo ambaye hajaoa,…huo ndio ukweli..nakuambia ukweli kwa vile wewe ni rafiki yangu,… sijawahi kumuona, nimezunguka nimeangaza huku na kule hakuna,....ninao waona na kuwapenda wengi ni waume za watu...sijui kwanini inanitokea hivyo,…’akaniambia.

‘Sawa mimi nimekuelewa sana, mimi sioni tatizo, kwa vile hutarajii kuishi na huyo mwanaume, ..nikuuliza hapo, kwani wewe najali nini sasa maana sasa unataka nikufundishe kila kitu, kwanza ninataka unihakikishie kuwa lengo lako sio kuvunja ndoa ya watu, ni kuzaa tu, na kuzaa huko kuwe ni siri yako…usije kuniingiza kwenye lawama ya kuvunja ndoa za watu, mimi sipo….’ nikasema

‘Ndio hivyo….’akasema

‘Na pili wewe unataka mwanaume salama asiye kuwa na tatizo, nahisi nimekuelewa hivyo…na unahisi kuwa wao watakuwa na tabia nzuri, sasa kama anakubali kutembea nje ya ndoa, mimi naingiwa na walakini na tabia hiyo, lakini wewe utakua jinsi gani ya kumshawishi , maana wanaume hata aweje, ukimfikisha mahali sizani kama anaweza kurudi nyuma….’ nikamwambia.

‘Mhh, hapo kuna mawili, nimuambia lengo langu au nimfiche lengo langu, mimi sitaki iwe hivyo, unaona hapo, nataka iwe siri ili sije kuvuruga ndoa au sio, nionavyo mimi,…haaah…. unajua umenitia hamasa kwa wazo lako, nimelipenda, japokuwa sipendi kutembea na mume wa mtu,…kwani nitakuwa nimevunja ahadi yangu nyingine kubwa , tena kubwa sana…’akasema

‘Ahadi gani…?’ nikamuuliza

‘Ahadi ya kuwa sitatembea na mume wa mtu, vinginevyo aje kunioa…’akasema

‘Nimeshakuambia uichukulie hiyo kama dharura tu, ikipita basi isahau kabisa, msahau huyo mwanaume na usahau kile kitu, usije kunogewa ikawa ndio basi tena…’nikasema

‘Mhh, hapo nipagumu, kutembea na waume za watu na huenda awe ni mume wa rafiki yangu, hapana mimi nawaheshimu sana marafiki zangu....hilo mimi naliona tuliache tu, sio wazo zuri, na kumpata ...ambaye atanipatia mtoto nimtakaye inakuwa ngumu, ninaowapenda zaidi ni waume za marafiki zangu, mmh, mimi naona mungu kapanga iwe hivyo, tuliache …..’akasema.

‘Wewe usijali, ukimpata huyo mwanaume, hata kama ni mume wa mtu, tembea naye bila kumwambia kitu, hakikisha umelenga zile tarehe…., nia na lengo ni akupe uja uzito, mkishamalizana, unaachana naye kabisa…., na fanya hivyo ukiona kweli mimba imeingia,…maana yawezekana ukajaribu mara ya kwanza isiingie…’nikasema

‘Hapo sasa si ndio nitaanza kujenga mazoea…’akasema

‘Hapana, akili yako iswe kumchukua mume wa mtu,…mimi nina imani hiyo mara ya kwanza inaweza kuleta matunda,..ukishamalizana naye, achana naye, usiwe na mawasiliano naye tena, achana naye kabisa mpige marufuku kukufuata fuata tena….mimi naona iwe hivyo.,…’nikamsahauri hivyo.

‘Hiyo ni kazi kubwa, maana hapo natakiwa nitongoze mwanaume wa matu, wakati siku zote natongozwa mimi, nitamuanzaje huyo mwanaume, tena mwanaume wa mtu tena labda awe ni mume wa marafiki zangu,…’akaangalia juu akiwanza.

‘Mwanaume ukimuonyeshea ishara tu wao wanajua, na wewe bado mrembo unavutia, sizani kama hilo litakuwa tatizo kwako, mimi sioni kama ni tatizo, ndio inauma, na sijui, jitahidi umalizane na hilo usahau, mimi naona ufanye hivyo. Maana sasa unaniingiza kwenye kuchagua chagua……’nikasema

‘ Sio hivyo, ..hapa tunapanga kitu chenye uhakika,….maana hapo unazungumzia mume wa mtu ninayemfahamu ,maana ili niwe na uhakika inabidi awe ni mwanaume ninayemfahamu, si ndio hivyo,..ambaye natamani anizalie watoto kama ….unaona inakuwa ngumu, nitakuja kumuangaliaje huyo rafiki yangu, ndio maana nikasema hili wazo sio zuri, naona tuliache tu...’akatulia kidogo.

‘Wewe unajali nini kwani unaondoka na huyo bwana..hahaha, naona unanifanya na mimi niwazie mambo niliyokuwa sinayo kichwani mwangu, wewe kama lengo lako ni mtoto na ni kweli umri ndio huo,… fanya hivyo, na iwe siri yetu wawili tu..,usije kumuambia mtu kuwa mimi nilikushauri hivyo….sitaki..’nikasema huku nikicheka.

‘Mhh, unajua ni rahisi kusema, lakini kwenye kutenda ni kugumu, maana ni kweli watoto wa marafiki zangu nawapenda sana, na natamani niwapate kama hao hao....hapo ndipo naona ugumu, kuwasaliti marafiki zangu, wewe huoni hapo inaweza kuleta shida baadaye, wanaweza wakaja kugundua, urafiki utageuka kuwa ni uadui, sipendi kukosana na marafiki zangu....mmh, ngoja nifikirie huo ushauri wako…’akaniambia.

‘Sio swala la kufikiria sasa rafiki yangu, …hapo ni swala la kulifanyia kazi, sizani kama itakuwa ni ngumu kwako, wewe ni mrembo bwana, nashangaa kwanini hujaolewa, kila mtu anakushangaa mrembo kama wewe huna mume...’nikamwambia.

‘Kila mtu ananishangaa, basi anipatie mume wake,, waache wafikiria watakavyo, mimi hilo sijali kabisa..maisha yangu hayawahusu....kwangu mimi hilo la watu kiukweli ninachohofia kwasasa, nisije nikafikia umri ambao hautakiwi kuzaa tena, sijapata mtoto, yaani hilo ndilo tatizo kwangu si vinginevyo....’akaniambia.

‘Kama ni hivyo , basi fuata ushauri wangu, na wala usipoteze muda, kama waume za watu ndio unaowatamani, ndio watakao kupatia mtoto unayemtamani, basi hao wapo wengi, ila chunga sana, ....’nikamwambia

‘Nichunge nini tena, unanikatisha tamaa…?’ akauliza akiniangalia kwa mshangao.

‘Kuna waume wana wake zao ni wakorofi, wakija kugundua wanaweza kukuharibu hiyo sura yako, tafuta waume ambao wake zao ni wastaarabu, ...na iwe siri yako, usimwambia yoyote...haya,usipoteze muda tena kalifanyie kazii hilo…’nikamshauri.

‘Sawa rafiki yangu, maana umenipa wazo ambalo sikuwa nalo kichwani kabisa...kiukweli naogopa sana, waume za watu...bado naogopa....kutembea na mume wa mtu, na mbaya zaidi awe ni mume wa rafiki ninamyemuheshimu sana ..naogopa sana... hapana hiyo sio tabia yangu, itakuwa ni mara ya kwanza kutembea na mume wa mtu...’akasema.

Rafiki yangu alitulia kwa muda, nadhani alikuwa akiwaza jinsi gani atakavyotembea na huyo mume wa mtu, na wakishamaliza, jinsi gani atakavyojisikia vibaya, na kama kweli huyo mwanaume ni muungwana na yeye atabakia akiwa anajutia....nikamtoa kwenye mawazo hayo na kusema;

‘Shauri lako kama na hilo nalo ni mpaka uchague chague kama nazi endelea kufanya hivyo, hilo halina kuchagua tena hapo, maana mwenyewe umeshasema kuwa waume za watu wapo wengi unaowapenda, na umeshaona watoto wao au sio, sasa watakaje, nikuchagulie mimi au..?’ nikamuuliza

‘Hapana, umeshanipa njia inatosha…na kiukweli marafiki zangu wote nawafahamu watoto wao, nafahamu yupi ni yupi anafaa, nitachagua mmojawapo, au sio..?’ akaniuliza

‘Ndio hivyo, chagua yoyote atakayekukidhi matakwa yako, sizani kama hilo ni tatizo kwako, au…?’ nikamuuliza

‘Sijui kama ni tatizo, maana sio kawaida yangu, lakini nitajaribu, maana wengi, nawaoana wakinitizama kwa jicho la kunitamani, kwahiyo..sawa, natumai sitaharibu kitu, ngoja nione itakavyokuwa, nashukuru sana rafiki yangu, kwa kunijali,..wewe ndiye rafiki wa kweli, hilo wazo limekaa vyema japokuwa ..mmh…’akasema

‘Usijali,..sasa kazi ni kwako wewe ushawajua ni nani anakuvutia zaidi, mweka kwenye anga zako, tembea naye,hakuna atakayejua...wewe mjanja bwana, hilo lifanyie kazi, haraka iwezekanavyo, kabla mambo hayajabanika..’nikamwambia na yeye akataka kuondoka

‘Mbona huwaagi watoto , …naona wazo hilo limekuhamasisha sana…’nikasema
‘Oh, yaani we acha tu,….’akasema na kuwafuata watoto kule wanapojisomea, na kuwa-aga…wakamsindikiza hadi mlangoni… , na alipofika mbele kidogo, akageuka na kuwaangalia , akatabasamu na kuwapungia mkono na huyoo, akaondoka zake….

‘Mlikuwa mnajadili nini….?’ Ilikuwa sauti ya mume wangu ilinishtua kwakweli… sikujua bado yupo, maana aliaga kuwa anaondoka!


Nb, mkuki ukachongwa, tayari kwa kumchoma nguruwe......


WAZO LA LEO: Wengi twachukulia rahisi tu kuongea, kutamka neno, vyovyote akili zetu zitakavyotutuma, tukumbuke kuwa kila neno lina thamani yake inaweza kuwa mbaya au nzuri... Neno dogo tu laweza kuzua sintofahamu, likajenga chuki, likaumiza, na hata kubomoa kile ulichoanza kujenga…rafiki wa leo anaweza kuwa adui mkubwa wa kesho, sababu tu ya kauli.. , kauli zaweza hata kuua.
Wachamungu wa kweli wametuasa kuwa ni bora kufunga mdomo wako, ukauzuia ulimi wako, ili kujiepusha na mtihani wa ulimi.

Najiusia mimi mwenyewe na kuwausia wenzangu, tuweni makini sana na kauli zetu, tuchunge sana ndimi zetu.
 
SEHEMU YA 7

Baada ya kuutoa ushauri kwa rafiki yangu, kukapita kipindi cha pilika pilika nyingi, mambo yakawa mengi ya kupambana na maisha, kiasi kwamba hatukuwa na muda wa kukutana na rafiki yangu , hata tukikutana ni ile ya haraka haraka kila mtu anakimbilia kwenye shughuli zake, na mara rafiki yangu akanipa taarifa kuwa anahamishiwa Zanzibar kikazi,

‘Hamna shida kazi ni kasi, na popote uwapo tutazidi kuwasiliana…’nikamwambia aliponipigia simu na wakati ananipigia yupo tayari anaelekea kupanda express bot, kwani taarifa ilikuwa ya haraka, na alitakiwa haraka akawasili kwenye hicho kituo kipya, na huko atapata maelekezo zaidi…basi, tukawa tunawasiliana kwa simu tu, kuulizana hali na siku, na masiki yakapita.

Ikawa akija Dar, hakai sana, na mimi nikawa na mishughuliko mingi ya shughuli zangu, wakati mwingine anakuja mimi nipo mikoani, kazi ni kazi, hakuna kulala, ilimradi afya zipo,…na kipindi chote hicho, tunapigiana simu au tunakutana kwa haraka, hutaamini sikuwa na hata na akili ya kumuulizia lile zoezi letu lilikwendaje…

Miezi mingi ikapita, na siku moja akaja kunitembelea nyumbani kwangu, alifika mara moja kikazi, basi tukaanza kuongea hili na lile, alikuwa kavaa Madera yake mapana tu, mimi nilijuwa kwa vile kahamsihiwa huko Zanzibar, basi kajifunza asili za huko, za kujisitiri mwili mnzima,….ila nilihisi kuna mabadiliko, ukimuangalia usoni kazidi kuwa mweupe, na unene kidogo, sijui kwasababu ya hizo nguo alizovaa, japokuwa nilikuwa na haraka kama alivyo yeye, nikamuuliza.

‘Vipi mwenzangu, toka lini ukavaa nguo hivyo, maana wewe ulikuwa ni mdhungu, haahaha, naona sasa ushakumwa mnzaibari tena, na nahisi huko ushampata shemeji au sio, kwa hilo umbo na sura yako, sizani waname watakuacha upite hivi hivi tu, halafu hebu niambie, nahisi mmh,…na nakuona kama mambo tayari au, ..?’ nikaanza kumtania.

‘Acha utani wako bwana, nimpate wapi mume mie, umri ushaenda, ..naona wengi wameamua kunikimbia, lakini sijali, ..na wala hilo haliniumizi kichwa,… kabisa, kabisa,….mimi nimeamua kula, kuishi kivyangu, yaani sitaki tena usuhuba na hao watu, huwezi amini, nimeamua hivyo na imewezekana....’akasema.

Hapo ndio nikaumbuka kile nilichomshauri , ikabidi nimuulize

‘Vipi lile swala letu uliweza kulifanyia kazi?’ nikamuuliza.

‘Hahaha..unajua niliwazia sana hilo, nakumbuka tuliongea kuwa kama …unajua iwe siri, na..aah, …’akasita kuongea

‘Aaah, mbona unasita kuongea, au ulizarau…?’ nikamuuliza

‘Mhh, hapana sikuzarau, ..sio maana hiyo ya kuzarau,..unajua niliwaza sana huo ushauri,…, nikaona nisiende mbali…..lakini wewe ni rafiki yangu, na hili tulilijadili pamoja, niliogopa ule usemi wako kuwa niwe makini maana wanawake wengine ni vichaa….’akatulia , sikuwa nimemuelewa hadi hapo ana maana gani.

‘Kifupi ulifanya au hukufanikiwa…?’ nikamuuliza

‘Ndio maana nimekuja kwako hivi leo, sina muda, hapa unaona meseji zimeshaanza kuingia natafutwa huko ...’akasema akitabasamu,…usoni ulionyesha furaha ya kweli, japokuwa kuna kiwingu cha kuonyesha ana mawazo fulani.

‘Kwahiyo kifupi tuseme tayari…?’ nikamuuliza nikiwa na hamasa ya kutaka kujua

'Mhh,…rafiki yangu, wewe na mimi ni marafiki, usingeliweza kunishauri kitu nikipinge bure bure…. ushauri wako nimeufuata na sasa hivi unavyoniona hapa nina uja uzito…hapa nilipo sitamani hata kula…kichefu chefu..yaani taabu kweli kweli..hivi mimba ndivyo zilivyo hivyo…, hapana nikizaa huyu mmoja, sizai tena, sitaki tena kuzaa.....’akaniambia.

'Mambo si hayo, ....umefanya jambo la maana sana, ....ulikuwa unapoteza muda tu,.. na umri ndio huo, na kama ulivyosema waume wanakuona sasa umeshakuwa mtu mzima, huna ujana tena, ..na ukiachia mwili hivyo,…mmh,…’nikasema

‘Sijaachia mwili, nachoka tu, halafu …sijisiki vyema,…’akasema

‘Ni kawaida, hali kama hiyo ni kawaida, muhimu ni kufuata masharti ya dakitari, hakikisha huharibu ulichokitaka, sawa….usije kujipilikisha na kazi, mimba ikaja kuharibika…’nikasema.

‘Hutaamini, nafuatilia masharti yote, naingia kwenye mitandao…nauliza madocta, sitaki kufanya makosa, na mungu anisaidie…’akasema

‘Hongera sana…’nikasogea na kumkumbatia rafiki yangu huyo…lakini sijui kwanini kuna kitu nilihisi akilini mwangu,..hata siwezi kukielewa, hata hivyo furaha iliweza kukimeza hicho kitu, ni kama mashaka,…’

‘Mhh,…hongera wakati hata sijafikia ….unipe nikishajifungua, au sio…na kiukweli, nashukuru sana rafiki yangu, umenishauri, na najua utaendelea kuwa name, hata siwezi kuelezea ninavyojisikia, japokuwa moyoni, kuna muda nawaza sana…’akasema

‘Unawaza nini sasa, hayo yameshapita muhimu ganga hili lililope mbele yako, jinsi ya kupambana na ujauzito maana nao sio mchezo, mengine yasahau kabisa,…unanielewa, wala usifikirie kuwa umekosea, ..hayo muachie mungu atakusamehe..’nikasema

‘Mhh…kweli wewe ni rafiki wa kweli..tatizo ndio hilo,… hapa nilipo, najisikia vibaya, sitaki kuongea saaana, mate yanajaa mdomoni…’akasema akitoa leso yake na kuweka mdomoni

‘Pole ndio uuke huo…’nikasema

‘Mungu anisamehe tu, na mnisamehe kwakweli….’akasema

‘Hamna shida wewe tema mate yako tu…ilimradi uteme sakafuni…’nikasema

‘Unajua haya yote ni kutokana na ushauri wako, wakati mwingine najilaumu kwanini, niliamua kuvunja nadhiri yangu, lakini sawa, kwa vile ni wewe sina shaka....’akasema.

‘Usijali kabisa…..mimi nilikupatia ushauri huo nikiwa najua wewe ni rafiki yangu, nikupe ushauri wenye tija,…usiwe na shaka na hilo..na sioni tatizo lipo wapi, …muhimu kama ulifuata kama nilivyokuambia, sizani kama itakuwa na tatizo,…kwani huyo mwanaume, uliwahi kumwambia baada ya kuhisi kuwa una ujauzito unaotokana na yeye?’ nikamuuliza.

‘Mhh, …aah, …unajua wanaume walivyo, baada ya lile tendo,…nisikufiche, ili kuwa na uhakika zaidi,…nilikutana nae mara mbili, mara mbili tu….sasa ikawa ni taabu, unajua wanaume walivyo, na..na…nilipohamishiwa huko Zanzibar, nikashukuru sana, maana huko mpaka aje sio kazi rahisi…na, nilimkanya kabisa kuwa mimi, sitaki tena urafiki na yeye, ndio hivyo, na sitaki kuyaongelea hayo tena tuyaache tu, ila nilitaka ni…niwe muwazi kwako…’akasema

‘Safi kabisa, lakini je baada ya kujihisi una mimba uliwahi kumuambia…?’ nikamuuliza

‘Unajua.hapana sitaki tuliongelee zaidi…nataka kukuambia…hapana, naogopa…’akasema

‘Unaogopa nini sasa, nimekuuliza hivi umemwambia…?’ nikamuuliza

‘Kama nilivyokuambia, wanaume hawana dogo, na hata siku ile, ya kwanza nilimuambia nimfenya hivyo kwa vile nimeshindwa kuvumilia, ila naheshimu ndoa yake, kwahiyo iwe ni mwanzo na mwisho…’akasema

‘Safi kabisa, inatosha ulivyomuambia…’nikasema

‘Lakini bado akawa ananifuatilia, japokuwa nilijitahdii sana kumficha,...na nikajitahidi sana kuwa mbali naye, lakini sijui kwanini, imekuwa kama nimemuonjesha asali , ….yaani nipo kwenye wakati mgumu sana, ndio maana nakuambia nimekosea sana….sijui nifanye nini sasa…kwani hata nafsi inamtaka najizuia napata shida sana….’akasema.

‘Lakini nilikuambia kuwa kama ni mume wa mtu, ukishahakikisha kuwa keshakupachika mimba, achana naye kabisa, nilikushauri kuwa usimwambie hata huyo mwanaume kuwa una mimba yake, utasumbuliwa sana…, unajua waume wengine walivyo, hawatakubali damu yao ipotee hivi hivi, na hujui hatima yake itakuwa…na kumbuka kama ni mume wa mtu , ….utakuja hatarisha ndoa ya watu, kuwa makini sana kwa hilo…’nikasema

‘Hata sijiu nifanye nini, ndio maana nikaja kwako tena, nipata ushauri, au sijui niitoe maana najuta, na inanipa wakati mgumu, namtaka aje awe karibu nami, unaona ilivyo, hata sijui nifanye nini, ndio maana nafikia kujuta, najiona kama nimebeba dhambi mwilini mwangu…?’ akasema sasa akikwepa kabisa kuniangalia machoni
 
SEHEMU YA 8



‘Kwani , hebu niambie ukweli huyo shemeji ni nani, maana sasa unanivutia intake kumfahamu, inaonekana umempenda sana…., hebu niambie ni nani ili niweza kukupa njia nyingine ya kumfanya asikusumbue tena..?’ nikamuuliza, nikiwa na shauku kubwa sana.

'Na wewe bwana, ina maana hapana…. sasa, itakuwa wewe ni wa kwanza kuvunja ushauri wako, mwenyewe ulianiambia nikishatembea na huyo mwanaume, nisimwambia yoyote hata wewe mwenyewe, sasa wewe unataka niseme, unajua hilo limekuwa likiniumiza kichwa, nawaza nikuambie tu, au ..hapana mimi naona nifanye kama ulivyonishauri, au sio…maana hakuna siri ya watu wawili..’akaniambia.

‘Lakini mimi ndiye niliyekushauri,…sasa , anyway,….fanya ilivyo sahihi, ni kweli ni bora iwe siri yako, ..hata hivyo ukiona ni lazima kuniambia ni nani, usisite kuniambia, kwangu usiwe na shaka kabisa, maana hatufichanai au..’nikamwambia

‘Lakini pia wewe ndiye uliyenishauri kuwa nikishahakikisha nina mimba nisije kusema au kumtaja huyo mtu, kwa yoyote vile…, unakumbuka eeh, basi tufanye hivyo, najua utanisamehe…. tusubiri nizae kwanza, ....’akasema

‘Usijali kabisa, kunificha ni sawa,….hiyo inanipa uhakika kuwa hutasema lolotekwa yoyote, kama umeshindwa kuniambia mimi, nina uhakika hutaweza kusema lolote kwa mwinginewe, au sio…’nikasema

‘Ni kweli, basi,…haina haja kukuambia, ..na hapa nilipo najisikia vibaya,...ngoja niondoke, hapa nisije nikakutapikia bure, na na..nashindwa, natamani niku—ooh, najisikia vibaya sasa...’akasema na haraka akimbilia nje.

‘Kama mambo yenyewe ni hivyo , hicho kinaweza kikawa ni kidume, na ukija safari nyingine ni lazima uniambie huyo shemeji ni nani, ...au nitakuja nyumbani kwako, upo mpaka lini...’nikamwambia na yeye akawa ameshatoka nje, …nilipomfuata nilimkuta ameshaingia kwenye gari lake na kuondoka.

*********

Miezi mingi ikapita, ... kwasababu ya kikazi na mambo ya hapa na pale, na kwa vile sasa yeye yupo huko Zanzibar, hatukuweza kuonana na rafiki yangu huyo, na siku moja nikapokea simu, namba ilikuwa ngeni kwenye simu yangu, nikapokea nikijua yawezekana ni wateja wangu.

‘Habari nani mwenzangu..?’ nikauliza

Sauti ya kinyongea kama mtu mgonjwa ikasikika,..kwanza sikujua ni nani..hata kufikiri,…mambo mengi kichwani,…

‘Oh, …ni mimi, yaani …’akasema akitoa sauti ya kinyonge

‘Ni, ni …wewe ni nani maana namba hii ni ngeni kabisa…?’ nikauliza nikjaribu kuwaza ni mteja gani huyo. Na kwanini anaonekana mgonjwa akilini nikahisi inawezekana akawa mmoja wa wateja ninaye mdai.

‘Hii namba ni..simu ya rafiki yangu , ya kwangu imezima haina chaji,…’akasema

‘Ok,….pole..nani mwenzangu, nikusaidie nini…’nikasema

‘Nilikutumia ujumbe nilipofika juzi, lakini ukawa kimia,…..’akasema

‘Ujumbe…ujumbe gani, kwani wewe ni nani…?’ nikauliza kikazi zaidi.

‘Ni mimi…nilikutumia ujumbe nikitokea Zanzabar,….nikajua utakuwa wa kwanza kuja kuniona…nikaona kimia, nikakupigia , lakini kila nikipiga simu yako ipo inatumika, na bahati mbaya nilikuwa natumia namba nyingine, ambayo nilikuwa sijakupatia, ya Zantel…’akasema

‘Oh, ina maana ni wewe..mbona sauti ipo hivyo…?’ nikamuuliza baada ya kugundua kuwa ni huyo rafiki yangu.

‘Ni mimi …sipo vizuri ..aaah , maumivu…’akasema na kabla hajaongea zaidi ni kasema;

‘Ujumbe wako niliupata,nilipanga nije kwako nikiwa na uhakika kuwa umeshafika…, ulisema umechoka…punguza kazi, pata muda wa kupumzika, ikibidi chukua likiza usije kupata matatizo…’nikasema


‘Unajua nilitaka niende kijijini kwa wazazi…, ili kukwepa yale uliyonishauri, lakini nikaogopa, unajua tena kijijini, nitaulizwa maswali mengi, nikaona bora nipambane kivyangu….’akasema

‘Vizuri, usijali, mimi si nipo, kama utakuwa hapa Dar, usijali kabisa, ..hata ikibidi unaweza kuja kukaa hapa mpaka muda wa kujifungua…’nikasema,


‘Kujifungua…hahaha…. nimekupigia kukufahamisha kuwa mimi nipo hospitali…’akasema na kukawa na ukimia, na nikasikia kama sauti ya kichanga kinalia.

‘Umelazwa,….ina maana…?’ nikauliza

‘Ndio nimeshajifungua mtoto wa kiume...’akasema na nikajikuta nashikwa na mshituko, kama vile nimeambiwa jambo baya, badala ya kufurahi, sijui kwanini…nikajikuta nimetulia kidogo.

Mara simu ikawa inataka kuingia, …na nakumbuka kulikuwa na mteja muhimu nilitakiwa niongee naye, na hapa rafiki yangu kanipatia jambo muhimu sana…sijui ilikuwaje nikajikuta nimekata simu ya rafiki yangu na simu nyingine ikaingia…alikuwa ni mume wangu.

‘Oh, ni wewe…nilikuwa naongea na rafiki yangu, ….’nikasema na yeye akasema, alinipigia kuniarifu kuwa atachelewa, kuna sehemu atapitia…

‘Wapi huko, maana hata mimi nataka kutoka, ….’nikasema

‘Napitia hospitalini…..’akasema

‘Unaumwa…?’ nikamuuliza

‘Hapana kuna mtu nakwenda kumuona…’akasema

‘Basi hata mimi nakwenda hospitalini, kuna mtu nataka kumuona…’nikasema

‘Hospitali gani…..?’ akaniuliza…na hapo nikashindwa kumjibu maana nilikuwa sijamaliza kuongea na rafiki yangu, nikasema

‘Subiri kidogo nitakujibu, wewe unakwenda hospitalini gani…?’ nikamuuliza

NB: Haya mambo ndio hayo yameanza kujitokeza mkuki ulishafanya kazi yake, sasa tuone matokea yake


WAZO LA LEO: Kwa watu wengi, ulimi huwa ni mgumu sana kuuzia, mnaweza kupanga kuwa hilo utakaloambiwa liwe siri, lakini kwa wepesi wa ulimi ulivyo, au kutokana na tabia zetu zilivyo, hatuwezi kuhimili, twatamani kuongea sana, ukaja kuliongea hata lile la siri, …siri ikavuja, na siri sio ya watu wawili. Tujifunze sana kutunza kile tulichoahidiana na wenzetu, kama uliambiwa iwe siri, basi na iwe siri kweli,..tukikumbuka kuwa ahadi ni dhamana.
 
SEHEMU YA 9


Ikabidi nimpigie simu tena rafiki yangu ili kuhakikisha kuwa hajatoka, maana hospitali nyingine ukijifungua kama huna tatizo, unaruhusiwa mapema tu, na mazungumzo yetu yakawa hivi;

‘Samahani rafiki yangu, simu ilikatika, mzee aliingilia kati, unajua tena, mume ni mumw inabidi umpe kipaumbele au sio, nisamehe tu kwa hilo, …hebu niambie kwanza unaendeleaje?’ nikamuuliza

‘Kiukweli, ni maumivu tu…hapa yananitesa kweli, wamenipa dawa za maumivu lakini bado,…oh, ….ila sikupata taabu kujifungua, sio ile kama ninavyohadithiwa, namshukuru sana mungu….ooooh, , nimejifungua salama, iliyobakia ni jinsi…lakini nitajitahidi kama ulivyonishauri …’akasema

‘Yaani siamini ina maana miezi tisa tayari… hivi urafiki wetu umekuwaje, ndio ..lakini ndio maisha au sio…kweli, kweli siku zinakwenda na maisha yanabadilika, umesema ..upo hospitali gani vile maana mimi nimebahatisha tu?’ nikamuuliza.

‘Hilo swali gani tena rafiki yangu…, mimi siendi kwenye hospitali tofauti na ile hospitali yangu niliyozoea kutibiwa na ndipo nilipojifungulia, wewe kama upo bize, haina haja…utanikuta nyumbani,..nilikuwa nakufahamisha tu...’akasema rafiki yangu huyo na mimi huwa naifahamu hiyo hospitali yake anayopenda kwenda mara kwa mara akiumwa.., sikutaka kumuuliza zaidi, nikasema;

‘Eti kama nipo bize, hilo usithubutu kusema, mimi na wewe tena, ninakuja hivi sasa nipo njiani,…maana taarifa hiyo kwanza ilinishtua, na furaha ikawa kama mshtuko fulani, sijui kwanini…’nikasema

‘Oh, unakuja….mbona unasumbuka hivyo, kuna mtu ….’akasema akiwa kama anauma uma maneno

‘Ninakuja usiwe na shaka, kama ni kukuchukua nitakuchukua mimi,…oh, nimefurahi kweli, ....nakuja sasa hivi, nataka niwe wa kwanza baada ya manesi kumshika huyo mtoto na kumpa huduma stahiki, mimi ndiye wa kuendelea kutokea hapo, sijali kazi hilo ni muhimu kwangu kwa sasa...’nikasema na kukata simu.

Kiukweli nilikuwa na mambo muhimu sana lakini niliamua kuyasitisha kwa kuona umuhimu wa jambo hilo, nilimthamini sana rafiki yangu na, haraka nikaingia kwenye gari kuelekea huko hospitalini. Sikukumbuka kumpigia tena mume wangu kumuarifu mimi ninakwenda hospitali gani!

Tuendelee na kisa chetu

****************


'Rafiki yangu nimejifungua, mtoto wa kiume...bado nipo hospitalini...' nilijikuta maneno hayo yakijirudia rudia kichwani, hasa nikikazia hilo la ‘mtoto wa kiume…’

‘Mtoto wa kiume…mmh,….ana bahati kweli…’nikasema nikakumbuka mume wangu jana alivyokuwa akiongelea kuhusu watoto na alitamka neno kuwa hivi sasa anatamani kumpata mtoto wa kiume, akishampata huyo hasumbuki tena, nikamwambia

‘Kupata mtoto wa kiume ni majaliwa ya mungu, ..’nilisema hivyo, tukaishia kuongea maneno mengine.

Nikiwa kati kati ya bara bara ndio nikakumbuka kuwa mume wangu alitaka nimuambie naelekea hospitali gani, nikampigia simu , lakini kila nilipojaribu namba yake inasema inatumika, sikujali sana, nikijua mwenzangu katingwa na majukumu, yake ya kikazi.

Mimi nikaongeza mwendo, na kuelekea hospitalini hapo alipolazwa huyo rafiki yangu, na wakati naendesha nikaona nimpigie tena huyo rafiki yangu, nia ni kujua kinachoendelea kama nahitajika kumchukulia chochote cha kula. Lakini badala ya kuliongelea hilo kwanza tukajikuta tunaongea mambo mengine.

'Oh, hongera sana mambo si hayo, ..wewe ulikuwa unapoteza muda bure, uzee ndio huo. Ulikuwa unasubiri mtoto aje akuite bibi,..’nikaanza kwa utani na akawa anacheka, na kusema.

‘Usinitanie mbona sijazeeka kiasi hicho cha kuitwa bibi…ni kweli ukiangalia wenzangu wenye umri kama wangu, unaweza kuwasalamia lakini mimi bado naonekana kijana tu…sasa naogopa nisije kuelekea huko’akaniambia na mimi nikasema;

‘Ni kwasababu ulikwepa majukumu ya kuolewa na kuogopa kuzaa mapema, ndio maana bado unaonekana bado kijana, ngoja upate mtoto wa pili, na upate shemeji anayejua mfumo dume, kama hutabadilika sasa hivi na kuitwa bibi...’nikaendelea kumtania.

‘Nani azae tena, …mimi...subutu yake..na kwa vile sina mume, …hilo limepita.., hii kasheshe niliyoipata siwezi tena kubeba mimba, kwanza uone ilivyo, nimezaa nikiwa mzazi peke yangu, nawaza huko mbele, mtoto akikuwa, anaweza kuanza kudai baba yake ni nani….na ole wake akiniuliza , nitampa jibu hatakumbuka kuniuliza tena….’akasema.

‘Oh, kwanini useme hivyo mpendwa, siumesema huyo shemeji anajua una mimba, na kwahiyo nahisi utakuwa umeshamwambia kuwa umeshajifungua, japokuwa kiukweli hayo uliyoyafanya hayanihusu , umekwenda kinyume na makubaliano yetu, ni hatari, nahofia ndoa za watu, ….’nikasema.

‘Ukifika tutaongea bwana, ….pamoja na mengine niliwazia sana ushauri wako, kuwa nimtafute mwanaume ambaye sitakuja kupatishwa taabu na mkewe, na..laki ni stutakuja kuyaongea, nataka nije kuyaweka wazi mapema tu….’akasema

‘Kwahiyo unataka kusema nini, kuwa utamuhusisha na huyo mzazi mwenzako je mke wake itakuwaje…?’ nikamuuliza

‘Nitajitahidi sana …unajua, sizani kama ni tatizo, hata hivyo, ifike muda tuongee, tuone tutafanyaje, na huyo mwanaume …sihitajii sana kumueleza, japokuwa ananiganda sana, unajua awali kabla sijajifungua nilikuwa natamani sana awepo, kuna hali ilikuwa inanivuta awepo,..mpaka nakereka,…lakini sasa nimeshajifungua, sitaki hata kumuona, sijui kwanini ....’akasema

‘Haya tutakuja kuongea tu, na kuhakikisha kila kitu tunakiweka sawa, mtoto wako ni wangu, hilo halina shida, usijali kabisa....’nikasema huku nikimuwazia huyo rafiki yangu na mtoto wake, nikikumbuka ushauri nilio mpa, na kujisifia moyoni kuwa nimefanya jambo moja kubwa kwa rafiki yangu, nikasema.



‘Ninakuja na zawadi kibao kuonyesha jinsi gani nilivyofurahi, na shemeji nilimuambia kuwa ninakwenda hospitalini kumuona mzazi, unajua alichoniambia,….eti na yeye kuna hospitali anakwenda kumuona mzazi pia…’nikasema

‘Oh, ndivyo kasema hivyo, …..’akasema hivyo.

‘Nahisi ni mfanyakazi wao ….sijamuulizia sana, lakini anaweza akaja kukuona, ingelikuwa ni bora tungelifika sote,…wanaume hawajui zawadi gani kwa mtoto ningemshauri zawadi gani tuje nayo,…’nikasema

‘Ok….sawa, nimekuelewa, …ukija tutaongea….’akasema na mimi nikaendelea kuongea;

‘Unajua hizi kazi zetu tena, mimi na yeye siku hizi tumekuwa kila mtu bize-bize, yeye na shunguli zake, na kazi zake za kuajiriwa, na bado anahitajika kusimamia, kwenye ofisi yake aliyoifungua, kwahiyo kazi zinamuendesha mbio mbio, kama ilivyo mimi,…mimi tu, nina ofisi yangu mwenyewe bado nasumbuka hivyo, na wafanyakazi, je yeye mwenye majukumu mawili itakuwaje…kwenye ajira ya kuajiriwa na kwenye ofisi yake ya kujiajiri, sio mchezo. …’nikasema

‘Hongera zenu mlioweza kujiajiri na sasa mnaajiri wafanyakazi, hata mimi natamani niwe hivyo, natamani sana maisha yenu, yaani sijui kwanini, nataka niwe kama nyie…’akasema

‘Unajua …nilitaka nimwambieje shemeji yako, aje tukutane mahali ili tukakununulie kila kitu sitaki ugharimie chochote, cha mtoto hadi wewe mwenyewe…mimi ninataka kila kitu nitoe mimi, unasikia, wewe ni rafki yangu, hilo halina mjadala…’nikasema.

‘Mhh, rafiki yangu, utanifanya nilemae bure…hapana… mimi nataka niwajibike kama mzazi, kuanzia mwanzo hadi mwisho, nataka nifaidi kile nilichokikosa miaka yote hiyo, nataka niwe mzazi,… sio mlezi,….’akasema

‘Hili usiniambie, bado utaendelea kuwa mzazi,…najua tutanyaje….Hivi nikuulize maana tumeongea sana, vipi kuhusu chakula ….ngoja kwanza nikakununulie supu ya nguvu, napitia kwenye hoteli, .. nitakuja nayo hiyo supu sijapika mwenyewe, nitakuwa nakupikia …lakini kwa leo, kwa dharura, ngoja tununue hotelini…, sitaki mtu mwingine alete unasikia….najua ndio chakula chako kwa hivi sasa…’nikasema


‘Haya usichelewe maana huenda wakaturuhusu leo hii…, kwa hivi sasa docta hajapita bado, …..na mimi sipendi kuendelea kukaa hapa ndani, madawa na harufu za kihospitali sizipendi ....we acha tu..hata hiyo supu sizani kama nitaweza kuinywa,…mimi naona ususumbuke kuinunua,..labda kama utainywa wewe…’akasema

‘Ina bidi uanze kuzizoea hali za namna hiyo, maana kuna kiliniki ya mtoto, laaima ufike hospitalini, na huwezi jua, ...akiumwa unatakiwa kuja kumuona docta, tena docta wa watoto…’nikasema

‘Najua najua..hayo baadae…’akasema

‘Sio unajua sikiliza, hayo ni muhimu sana, mtoto mchanga akiumwa uhakikishe unampeleka kwa docta bingwa wa watoto,..sio unaitisha madocta mitaani, au nyumbani,..na usimpeleke mtoto kwa docta wa kawaida, unaweza ukamkomaza mtoto kwa madawa yasiyomsaidia.....’nikamwambia.

‘Haya bwana, wajifanya wewe ni mzoefu sana nakusikiliza, kwani upo wapi, maana nakusubiria, mshauri wangu, na…hebu kwanza,…ok, … nakata simu, maana naona kama docta anakuja....’akasema na mimi nikakata simu.

************
 
SEHEMU YA 10


Nilifika kwenye hiyo hospitali mapema, maana kulikuwa hakuna foleni kama nilivyotarajia, nikampigia simu katibu muhutasi wangu abadilishe ratiba zangu za siku, ofisi yangu ya kujiajiri ni kubwa, ina kila kitu kinachohitajika kama kampuni inayojitegemea.

Nilipofika hospitalini, nikapitia njia tofauti ya kuingilia, nilipitia njia wanayotumia wafanyakazi wa hapo maana wao wanasehemu yao, nikaenda kulisimamisha gari langu sehemu wanayosimamisha magari yao, kama mfanyakazi wa hapo, nikaongea na mlinzi alilalamika, lakini nikampa pesa ya soda, akanyamaza.

Nikaenda moja kwa moja kwenye wodi ya wazazi, nikamuona rafiki yangu, akiwa amekaa kwenye kitanda, huku akiwa na mkoba wake pembeni, nikashangaa, na kumuuliza.

‘Vipi tena, mbona umekaa mkao wakuondoka…?’ nikamuuliza nikimkagua akiwa kambeba kichanga chake na mimi nikasogea na kumpokea.

‘Yaani ulipomaliza kuongea na mimi kwenye simu , akaja docta, na akaniambia sina haja ya kuendelea kukaa zaidi hospitalini, nilishukuru kitu, alisema kwa vile mimi sina tatizo lolote, ninaweza kuondoka tu…, basi, nikaona nifungashe-fungashe vitu vyangu, nimempigia simu ndugu yangu aje kunichukua, japokuwa....’akatulia kidogo akimwangalia mtoto.

Wakati anaongea akili yangu ilishazama kwenye mtoto, nikawa namkagua,unajue tena sisi akina mama, macho yetu yameumbwa hivyo kudadisi, sura, umevaa nini upoje…kwahiyo kwa muda mfupi nilikuwa nimeshamkagua mtoto , usoni, ..na sikutaka kumuuliza kwanini kakatisha kuendelea kuongea, nikasema;

'Mhh, mtoto mnzuri kweli, halafu,ana kila ngapi, mnzito…….umegundua kitu, kwanini watoto wachanga wote huwa wanafanana, maana namuona mtoto wako anafanana sana na watoto wangu, walipokuwa wachanga...’nikasema na yeye akaniangalia kwa haraka, halafu akageuka kumwangalia mtoto wake, huku akitabasamu, hakusema kitu akawa anamweka vizuri.

‘Naona kweli ndoto yako imetimia, maana ule usemi wako wa kuwa unatamani mtoto wako afanane na watoto wangu, umekamilika…’nikasema

‘Mhh, nashukuru kwa hilo,ahsante sana rafiki yangu, bila wema wako sijui ingelikuwaje, .….’akasema akitabasamu.

‘Ni kweli, unajua rafiki yangu…ni kweli sasa kile tulichokitaka kimetimia, kweli mungu kasikia kilio chako…yaani nikimuangalia huyu mtoto wako, nakumbuka watoto wangu walivyokuwa wachanga,…’nikasema nikiendelea kumkagua mtoto.

‘Kwanza angalia vimdomo vyake, na…na, macho yake japokuwa kalala.....yaani kama ungelimuweka na watoto wangu enzi hizo wakiwa wachanga, ungelisema ni mapacha na watoto wangu….’nikasema huku nikiendelea kumchunguza yule kachanga.

'Kweli,...japokuwa nilitaka wasichana kama wa kwako, na wawe mapacha kama wakwako, …unajua nilitakamani kuzaa mapacha kama wewe…lakini mungu kanipa mvulana, na kweli eeh,…kumbe … wanafanana na watoto wako, oh…’akasema

‘Unajua watoto wangu wanafanana zaidi na baba yao kisura , na kirangi wanafanana na mimi, watu wengi wanasema hivyo, hata wewe uliwahi kuniambia hivyo…’nikasema

‘Hivi eeeh, ni kweli, …anafanana shemeji…unajua nilikuwa sijaligundua hilo…akili yote ni kwenye furaha kuwa nimempata mtoto…'akasema na akawa kama anaonyesha uso wa haya, hata kuniangalia machoni inakuwa ni ngumu mimi sikuwa na mwazo yoyote zaidi ya kujua ni kufanana tu;

‘Mhh, nina hamu sana ya kumuona huyo shemeji, maana sipati picha, kama umeamua kumuhusisha basi hata mimi nastahiki kumuona, au sio,..kwani nikuulize huyo shemeji yangu ni nani, nahisi kama anafanana sana na watoto wangu, je ameshafika kukuona?’ nikamuuliza

‘Bwanaeeh, hayo tuyaache kwanza, tutaongea vizuri tukifika nyumbani, najua una hamu kujua mambo mengi kwa wakati mmoja,…kila kitu nitakuambia,.. lakini kila kitu na wakati wake au sio, tukianza kuongea hapa, huoni watu watatusikia,a au….’akasema

‘Mhh, leo twaanza kufichana, haya bwana, lakini kama umeamua kumuhusisha huyo shemeji,…kiukweli sikupendezewa na hilo, halikuwa kwenye makubaliano yetu, mimi ni mwanamke…, nipo kwenye ndoa, nafahamu ndoa ilivyo…hili lilitakiwa liwe siri yako mimi na wewe, sasa umeshaanza kuharibu mapema, sijui una lengo gani, sijapendezewa na hilo, kwanini ukamwambia huyo mwanaume…’nikasema

‘Lakini …sikupenda iwe hivyo,…nilijitahidi sana rafiki yangu… hata hivyo…sizani kama itakuwa na matatizo, sizani..’akasema

‘Najua haitakuwa na matatizo,…nitajitahidi kukusaidia, na kukushauri inavyotakiwa, ila nakuonyesha hatari yake,…ndoa ni kitu kingine,…na kwa hili, mimi nataka nionane na huyo shemeji nimsomeshe mwenyewe, ili aelewe…, sitaki uje kupata matatizo, sitaki nikuone unakuja kuishi maisha ya kujihami, maana hujui wanawake wa ndoa walivyo…’nikasema

Nikamuuliza huku akilini nikimuwazia huyo shemeji, ambaye nahisi atakuwa akifanana na mume wangu, kwani kiukweli watoto wangu wanafanana na baba yao, na kiukweli, ukimuangalia huyu kichanga, anafanana sana na watoto wangu.
‘Mwambie kuanzia sasa hatakiwi kabisa…na wala asije hapa kukuona…’nikasema

‘Mbona keshafika, alikuwa wa kwanza kufika hapa, na ,na hukumuona huko nje, au aliniambia anasubiria nikiruhusiwa mapema, kama ndugu yangu hajafika atanichukua yeye,… yupo huko nje, ila mimi nimemkatalia kama ulivyonishauri,nimemuambia aondoke, sasa kama bado yupo huko nje shauri lake…’akasema

‘Ina maana alishafika…tatizo sikuingilia mlango wa kawaida, nimeingialia mlango wa mastafu…unajua rafiki yangu unafanya visivyo kabisa…’nikasema

‘Sikutaka kabisa yeye aje nilimuelezea yote hayo, kuwa kuanzia sasa sitaki anifuate fuate, lakini akasema na yeye atachukua tahadhari, hata hivyo hawezi kuniacha, …ndio maana alikuja mapema ili anichukue , halafu arudi nyumbani kwake…hata yeye hapendi…lakini unajua tena…hata hivyo nilimuambia huu ni ushauri wako …’akasema

‘Masikini…mmh, unajua naanza kuwazia mbali, huyo mke wa huyo mwanaume, unajua inauma sana....lakini tutaona la kufanya, ila nataka nionane naye huyo mwanaume kwanza ni muhimu nikutane naye nimsomeshe mimi mwenyewe.., kama ni lazima vitu vyote vipitie kwangu, na mimi nitajua jinsi gani ya kufanya…’nikasema

‘Usijali rafiki yangu, …mimi nataka hili jambo niliweke wazi kwako, ndio maana nataka tukaliongelee huko nyumbani, wewe ni rafiki yangu, najua hutanilamu kwa lolote lile, nilifuata ushauri wako tu…’akasema

‘Siwezi kukulaumu kabisa, kwanini nikulaumu..ushauri nimeutoa mimi mwenyewe, sasa itakuwa ni ajabu nianze kukulaumu, ila ni lazima tuchukua tahadhari, maana utu, ubinadamu,…kuna kuumia hapo, mwenye mume, akijua ni lazima ataumia, ndio hilo silitaki kabisa…’nikasema na rafiki yangu akawa kama ananywea fulani hivi.

‘Umefanya makosa sana…’nikasema

‘Usinilaumu rafiki yangu, maana nilifanya juhudi zote,….lakini ikashindikana…hata sijui alijuaje kuwa nimejifungua, sikutaka kabisa kumfahamisha hilo maana nilikuja kutoka Zanzibari kwa siri, na sikuwahi kumpigia simu, …’akasema

‘Sasa alijuaje…?’ nikauliza

‘Hata sijui, kaniambia … kumbe alikuwa akinifuatilia kila siku alipogundua kuwa nimefikia muda wa kujifungua, akawa anafuatulia nitakwenda hospitali gani, sijui kwanini …nashangaa nimejifungua, sina hili wala lile huyu hapa , akawa yeye ndiye wa kwanza kuja kunipa hongera, na alipogundua kuwa nimejifungua mtoto wa kiume, amefurahi kweli kweli, nikampa onyo, kuwa huyo sio mtoto wake...’akasema

‘Kwahiyo kumbe mlikuwa mnaelewana sana na huyo shemeji, mlikuwa karibu sana kihivyo usinidanganye rafiki yangu, umefanya makosa ambayo utakuja kujijutia, nakueleza ukweli ulivyo…, inatakiwa tuwe makini kuanzia hivi sasa, utakuja kupata lawama kubwa sana.

‘Kuelewana kwa vipi, si tuliliongea hili kuwa nimetafute yule ambaye namuelewa sana,….na unajua,… nikuambie kitu, shemeji alinibana sana...mwanzoni nilimficha, lakini wanaume bwana, akawa akinidadisi mara kwa mara hasa alipoona mabadiliko, najuta kwanini nilishindwa kumdanganya, ...na tatizo kama nilivyokuambia awali , nilikuwa natamani sana awepo karibu yangu mara kwa mara..na…kila mara nataka angalau nisikie sauti yake, angalau, …mimba ina matatizo jamani….’akasema

‘Nayafahamu sana, ukiwa na mimba unaweza ukampenda sana mume wako au ukamchukia sana, inatokea hivyo, lakini mimi naangalia kote kote, kwa vile mimi ni mzazi, mimi nipo kwenye ndoa, nayafahamu hayo zaidi, jinsi gani mtu unavyoumia ukiibiwa mume wako…’nikasema

‘Usitake kunitia kwenye lawama tena, ushauri wako ndio umeifanya hii kazi, na najua wewe hutaweza kunilaumu kwa hili…’akasema kidogo akionyesha hasira.

‘Sio kwamba nakualaumu, ..unasikia kwa vile ni mimi nimeutoa ushauri, nataka ushauri uende ilivyo, isje ukapata matatizo, tunahitajika kuchukua tahadhari zote, unielewe hapo…’nikasema

‘Sawa basi tuondoke, maana dawa ndio hizo hap anazileta nesi, kila kitu sasa kipo sawa sawa….’akasema

‘Kwahiyo mimi nashauri ni bora twende nyumbani kwangu ili niweze kukusaidia vizuri, sitaweza kujigawa, mimi nilikuja na wazo hilo japokuwa sijaongea na mume wangu, lakini hili sio lazima nimuambie anakufahamu wewe kama ndugu yangu…’nikasema.

NB: Ngoja tuishie hapa kwa leo


WAZO LA LEO: Urafiki wa kweli hujengwa na kuaminiana,..kama mtakuwa manafichana mambo yenu, ujue urafiki huo una walakini. Lakini pamoja na hayo, tusiwe tunafanya mambo kama kufurahishana tu, unamshauri rafiki yako, ili tu afurahi, bila kujali athari zake mbeleni.
 
SEHEMU YA 3


Ilipita muda rafiki yangu akawa haonekani, hafiki kwangu na sio kawaida yake na baya zaidi hata kwenye simu yake nikipiga simpati, kwa hali kama hiyo sikuweza kuvumilia, nikafunga safari hadi nyumbani kwake…

Nilipofika nyumbani kwake, sikuweza kumpata, nikauliza majirani wake, wakasema, siku hizi anatoka asubuhi sana kwenda kazini na anarudi usiku sana,…bado sikurizika na hilo jibu, nikaona nipitia kazini kwake, lakini wakati nataka kufanya hivyo, nikapigiwa simu ya muhimu kwenye shughuli zangu za kibiashara, ikabidi nikatize safari hiyo, moyoni nikijipa matumaini kuwa,.., huenda ana sababu zake za msingi za kufanya hivyo.

Baadaye jioni, nikamuona huyu anakuja, alioneka kuwa mnyonge sana, kama mgonjwa, usoni hana raha, uso umesawajika, kachoka, mpaka nikaingiwa na mashaka, nikahisi kuna tatizo, ni lazima kuna tatizo…!

Kwa muda huo, watoto walikuwa kwenye meza wanajisomea, kipindi hicho walikuwa darasa la tano,…wakubwa, na watoto wakike hukua haraka!

Kama kawaida yao walipomuona mama yao kafika…, maana napenda kumuita hivyo, ‘mama yao’ kwa jinsi walivyomzoea, kwa haraka wakaacha kusoma na kusimama na kumsalimia kwa kumkumbatia, wamezoeana hivyo, ..na yeye kama kawaida yake japokuwa alikuwa haonyeshi furaha akajitahidi kuongea nao, akawafundisha fundisha hapo mezani, baadae akawaachia kazi za kufanya, halafu…, tukaenda chumba cha maongezi.

‘Haya niambie maana hata bila kukuuliza kila kitu kinaonekana dhahiri, kwanini tunafanyiana hivi, urafiki wetu umekwenda wapi…?’ nikaanza kulalamika.

‘Rafiki yangu sio kwamba nimefanya makusudi, hata mimi nilikuwa na wakatu mgumu, lakini …kila nikitaka kukupigia, nashindwa, nahisi nitaishia kulia kwenye simu, ..nikitaka nije, ooh…lakini leo sijambo, naona naanza kuizoea hiyo hali, maji yameshamwagika hayazoleki..’akasema

‘Mhh..bado, sijakuelewa…’nikasema

‘Jana niliwaza sana…baada hayo kutokea, baada ya kujipa muda wa kutafakari kwa kina,…, unajua ni kweli,…nilifanya makosa, na kiukweli …hata sijui nifanyeje, na…na…umri wa mwanamke una ukomo wa kuzaa, na mimi nahisi naendea huko, baada ya kwuaza hilo, niliogopa sana kuwa sasa nimeshazeeka bila ya kuwa na …na…hata kumbukumbu…’akasema

‘Mhh, wanasema kitaalamu ndio…lakini mbona watu wanazaa tena wazee tu, ni hivyo kiunjumla, lakini sio kwamba wote watakuwa kwenye hatari hiyo,…kuwa ukizee kw umru huo wa utu uzima ni hatari, hata hivyo…mb- mbona wewe bado tu mdogo, hujafikia kwenye hiyo hatari…, au sio…?’ nikamuuliza

‘Mhh…hapo sasa, urafiki wetu ule wa zamani wa kuambizana ukweli naona umepita, kwa vile mimi sasa nimekiri hilo, kuwa…nimeshaze-zeeka, au sio,…naona hutaki kunishauri mambo ya ukweli, kwa ajili tu ya kunipa matumaini, au sio,….’akasema

‘Mbona nilishakuambia sana hilo…, nikakushauri sana tu…, nikaona basi nijinyamazie tu, maana nakuelewa sana, wewe sio wa jana kwangu, ukiwa na maamuzi yako huingiliki, hata kama mimi ni rafiki yako, huwezi kubadilika mpaka mwenyewe upende…’nikasema

‘Yaani rafiki yangu hilo ndilo limekuwa nikijiuliza akilini mwangu, baada ya kutafakari sana nikaona nije nikuone,...nimegundua kuwa sasa hivi natakiwa nichukue hatua nyingine kabla sijachelewa zaidi…na kiukweli baada ya kutoka hayo, nahisi kipaumbele changu kwa hivi sasa sio mwanaume, ..sio kuolewa, …huu sio muda wa kuwazia kuolewa tena…na baada ya yote hayo, naona ili kuepusha shari zaidi, bora niishi peke yangu, ..kwa kifupi mimi sitaki tena kujiingiza kwenye mawazo ya kuolewa…, nimeshajizoelea kuishi kihivi hivi, kivyangu-vyangu, kuwa na uhuru wa kufanya nipendavyo…’akasema

‘Sizani kama hilo ni sahihi, …hayo sio maisha ya kibina-adamu, lazima kuolewa, ili uweze kupata familia yako, au hutaki watoto,…?’ nikamuuliza

‘Watoto…., watoto….mmh, ….yaani umeshanigusa, hilo….ooh, hata sijui nifanyeje…’akasema akiangalia mlangoni, nahis alitaka kuangali akitu ambacho hakioni.

‘Ndio, sisi ni wanadamu umri wetu una …mipaka na hatujui lini mtu anaondoka duniani, na ubora wa mtu, uzae utoe mbegu na mbegu zije kuotesha mti mwingine, kizazi kinakua,…au sio, usipozaa hutakumbukwa tena hapa duniani…’nikasema

‘Sawa kabisa, hilo ….ndilo lililoniumia jana,…lakini kwa vipi,…na mimi sipendi kuwa mtumwa wa kujipendekeza, eti nikajiangushe kwa mwanaume kuwa yamepita basi, nimekusamehe, hapana, na hata hivyo haiwezekani, siwezi kuingie kwenye mashindani ya kugombea mwanaume…’akasema

‘Kuna kitu unanificha au..?’ nikamuliza

‘Unajua rafiki yangu, nikuambie ukweli, ninachotamani kwa sasa ni kupata mrithi,…kuhakikisha na mimi nabakia ni kizazi cha huko mbeleni, hata kama…hilo,…ndilo naliwazia….’akasema

‘Ni kweli, ni lazima upate kizazi chako, ni lazima upate mtoto, na utapataje, bila kuingia kwenye ndoa,..hilo …labda ndilo la kuwazia,…’nikasema

‘Hapana siwazii, ndoa…mimi nawazia kupata mtoto, ninajua nikipata mtoto basi, maisha yangu yatakuwa na furaha sana…’akasema

‘Hahaha, sasa leo umekuja na jipya, unataka mtoto bila ndoa,…leo umeshabadilika au,sijakusikia vyema,…kuwa unataka uzae nje ya ndoa, au mimi sijakuelewa, au hebu niambie vyema....utapataje mtoto bila ya mwanaume au unataka mtoto wa kurithi, sijakuelewa hapo..?’ nikamuuliza

‘Ninataka mtoto wa kwangu wa kuzaa mimi mwenyewe, lakini nataka iwe halali, isiwe nafanya vibaya, …ndio maana nimekuja kwako tulijadili hilo, kama huko kuolewa hakupo, maana nimesubiri sana sijampata mume wa kunioa, wengi wanataka kuuchezea huu mwili wangu tu,…kwa vile hajatokea mume wa kunioa, basi, nipate angalau hata huyo mtoto, …’akasema.

‘Unataka kusema nini sasa…?’ nikamuuliza na alikuwa kama kaichokoza fikra fulani niliyokuwa nayo akilini, lakini sikupenda kabisa kumshauri rafiki yangu nilijua ni makosa, lakini sasa naona anaelekea huko-huko, ila sikutaka kuianzisha mimi, nikasubiria.

‘Natamani mtoto rafiki yangu, lakini kwa vipi, kama ulivyosema sijaolewa, na mtoto akizaliwa, najua hata kuwa na muonekano mnzuri kwa jamii, atapewa ‘majina mapya…’ akasema kama anaimba

‘Na mbaya zaidi,..hilo mimi silitaki,..eti aje kuitwa mtoto aliyepatikana kwa njia za haramu, mimi nitaonekana muhuni…ooh, kwanini mimi..unajua najishia vibaya sana…kwanini lakini…, silipendi, ndio maana nimejitahidi kujizuia sana nisije kwanza hapa, maana ningelifika kwa muda huo ningeliishia kulia,..sitaki huo unyonge,..’akasema

‘Sasa ina maana unatakaje sasa rafiki yangu..au kwani imekuwaje tena, maana sisi tulishajua sasa mambo yanaelekea kwema, au..?’ nikamuuliza

‘Hapo sasa, ndio maana nimewaza sana hilo…mpaka kichwa kinauma, nimekuja kwako tushauriane, nilikuwa nimejitenga kidogo kuja huku nikiwazia hili jambo kwa makini sana, nimeshindwa namna, nifanyeje…mimi nataka mtoto, natamani nipate na mimi mtoto wangu…., nilitamani ndoa, ndoa haijatokea, sasa hata mtoto jamani…’akasema kwa sauti ya huzuni.

‘Nikushauri rafiki yangu, ukianza mtindo huo, utazalishwa na waume tofauti tofauti, na kuwa na watoto wa kila mmoja na baba yake, huoni hiyo itakuja kukuletea mawazo mengine uzeeni kwako,…maana sawa, utakutana na mwanaume ilimradi mwanaume upate mtoto, utazaa wa kike, ..kesho utataka wa kiume, utaenda kutembea na bwana mwingine atakuzalisha,kumbe anakuja tena wa kike…kesho kutwa utataka mwingine…huoni itakuleta sifa mbaya…?’ nikamwambia

‘Aaah, hayo ya huko mbele anayajua mungu peke yake, tugange haya yaliyopo sasa,,, kwani wewe unajua kesho itakuwaje, nikifa hapa si ndio mtanisahau kabisa, sina hata kumbukumbu huku nyuma, au sio, hiyo ndio ajenda yetu, tuijadili …’akasema hivyo , na kwa vile namfahamu sana rafiki yangu sikutaka kumchukulia kwa haraka.

‘Unajua rafiki yangu nilikushauri sana awali, ukanipuuzia, sasa umri ndio huo umekwenda, na tabia yako haibadiliki, wanaume wameshakusoma wameshakugundua ulivyo,…kuwa wewe ni mtu wa matumizi tu,..dharau, msomi sana,… mtoto wa bei mbaya, mtu wa matumizi makubwa, wanaume hawapendi hayo maisha,…wanmeshakuogopa, na maisha yenyewe yalivyo,..oh, angalia sana…’nikasema

‘Sasa ndio imekuwa hivyo, mimi ndio nipo hivyo, sina mbadala, na hata nijitahidi vipi kwasasa ni nani ataniamini kuwa nimebadilika,..labda niende ulaya nikamtafute mnzungu mzee…hahaha, …nacheka utafikiri nina raha, naumia mwenzako,…ni nani atakayenipenda hivi sasa, hakuna…, lakini sitaki kuzalilika…, nataka maisha ya hapa hapa kwetu, nataka mtoto wa damu ya kiafrika, nataka mtoto kihalali, sasa kwa vipi….’akasema


‘Vipi yule shemeji , kawaje kwani, mbona naona anakupenda sana imekuwaje, sisi tulitaka tuonane na nyie wawili tunishinikize ndoa…kwanini yeye asikuoe, ili upate huyo mtoto, mimi nakushauri hivyo…’nikamshauri.

‘Mhh, ungelijua,..yule ..hahaha sitaki hata kumsikia tena, sitai simtaki, na hata hivyo ipo wazi, sio wangu tena…’akasema

‘Kwanini…niambie..’nikasema

‘Siku kadhaa , alisita kuja kwangu, sikujua ni kwanini, nikasubiria wee, niaona kwanini nisjiumize kwa mawazo, nikasema ngoja niende kwake…labda anaumwa, sikutaka kumpigia simu, maana tulishazoeana kihivyo…basi, nikaenda kwake,.., ile nafika eneo la nyumba yake,…nikahisi mwili unasisimuka ajabu…, nikahisi kuna tatizo…lakini nikajipa moyo, nikafika nikagonga geti…kumbe lipo wazi, nikafungua hadi kwenye mlango wa nyumba,…’ hapo akatulia kidogo.

‘Unajua kabla sijagonga mlango, ukafunguliwa,…, mara anatokea mdada half cast, si unajue waniga fulani,..kijamika jamaika fulani, alivyo sio….kavaa khanga moja, ile ya khanga moja hakuna kitu kingine ndani, mhh, kuashiria nini hapo, kuwa katokea wapi sio.. utajaza mwenyewe……’akatulia akikunja uso kwa hasira

‘Mhh, kwahiyo ina maana gani hapo…?’ nikamuuliza

‘Ndio hapo nakuambia, mimi nina gundu…nina mkosi gani sijui, na uelewe baada y aule ushauri wenu na shemeji, nilipanga niende nimwambie sasa tufunge ndoa, nimekukubali, na sitaki kupoteza muda tena, na hilo alikuwa akilisubiria, niliwahi kumwambia akasita, akawa haniamini, sasa nilitaka nimuhakikishie kuwa nipo tayari,… siku hiyo nilipanga iwe hivyo,..hebu jiweke kwenye nafasi yangu uone nilivyoumia,… sasa sijiu kwanini alinifanya hivyo, hata sijui muda wote huo, kwanini hakuaniambia ana mchumba wake anasoma huko marekani…leo hii, inatokea hivyo…’akasema

‘Ulimuuliza baada ya hapo…?’ nikamuuliza

‘Mimi tena, ..mimi, weeh, unanijua nilivyo, wee…mimi nikamuuliza,hahaha, sikuwa na muda huo,… hapana,…nilipojua kuwa huyo ni mchumba wake, nikaondoka zangu na hata aliponipigia simu sikutaka kabisa kupokea, na hali hiyo ilinitesa sana, sikutaka hata kuja kuongea na nyie, na ningelikutana na yeye, angelinijua mimi ni paka mwenye makucha makali…’akatulia

‘Sasa ulijuaje kuwa ni mchumba wake..sijakuelewa hapo?’ nikamuuliza

‘Nilimuuliza, ilibidi amuite kwani alikuwa ndani, na mara huyu, ti-ti-ti…katoka na taulo na likitambi-tambi lake, unajua kajiachia sana, na likitambi lake,.. sipendi hali hiyo, lakini nilishafikia sehemu nikaanza kumpenda tu, alivyo, kubembeleza, hakati tamaa..kumbe alikuwa na lengo lake…’akatulia

‘Nikamuuliza huyo kinyago ni nani…?’

‘Kinyago, hahaha huyu ni mchumba wangu….’akasema na huyo binti, akasimama pemebni yake na kumwekea mikono hivi, kimahaba, kuninyaa…nikihisi ile hali natamani irejee niwe na gun, niwashoot…lakini yamepita…’akatulia

‘Pole sana…’nikasema
ntaendelea kesho ngoja nilale
 
SEHEMU YA 11


‘Kwahiyo mimi naona twende ukaishi kwangu…;’

‘Hapana, hilo sio wazo zuri kabisa, mimi sikubaliani nalo, huwa nafuata ushauri wako, lakini sio huo…..nataka nikaishi kwangu, sitaweza kuishi nyumba moja na shemeji, hahaha, unajua mimi nataka nikakae kwangu ili niweze kumlea mtoto wangu mwenyewe, nataka niipata ile shida ya mama…’akasema

‘Mhh,..sijakuelewa kwahiyo kinachokukataza kuja kuishi kwangu ni kumuogopa shemeji yako, hayo yameanzia wapi, …ya kuanza kumuogopa, si unamfahamu alivyo, hana muda na mtu kabisa, ni simba mwenda pole, ila namuamini sana mume wangu hana tatizo na mtu, hajawahi kunificha ficha mambo yake, labda kama yapo mengine siyajui…’nikasema.

‘Ni kweli simba mwendo pole, …hata hivyo, nimesema tu hivyo…’akasema

‘Au wewe una lako jambo,nahisi mumeshapanga na mwenzako kuwa uendelee kukaa kwako, ili aweze kukutembelea…bila kuwa na kikwazo, si ndio hivyo….’nikamwambia

‘Aaah, hapana..sio hivyo, sijaongea naye kuhusu hilo, ila sio vizuri,….na.., na kwanza hilo halimuhusu kabisa…ila mimi mwnyewe naona tu nikakae kwangu, tafadhali nielewe hivyo…, na hilo tusiishie kubishana nalo.., wewe kama huna muda, …na najua hutakuwa nao, kuna ndugu yangu kasema atakuja….’akasema

‘Nikuulize swali moja, je huyo mzazi mwenzako unampenda….?’ Nikamuuliza

‘Swali gani hilo jamani, nitampendaje mume wa mtu,…au umesahau tulichokijadili tokea awali, …yeye kazi yake imekwisha au sio….lakini nataka tukifika nyumbani tuongee vizuri, hili jambo tuliweke wazi, nataka nikuambia kila kitu au unasemaje, ili isije kuleta matatizo baadae unaonaje…?’ akaniuliza

‘Sawa, kwani kuna shida kwa hilo, mimi na wewe tena, au sio, hata mimi nina hamu ya kusikia ikiwezakana kila kitu, usinifiche mimi, sawa hilo litanipa faraja kuwa unaniamini …’nikasema

'Unajua baada ya hili,..sizani kama nitarudia tena ….maana hata yeye, amekuwa kwenye wakati mgumu, japokuwa unajua tena wanaume,, sikutaka wazo la kuwa marafiki wa siri, hilo nimelipinga, japokuwa aliniomba hivyo…unajua hata kama imetokea hivi, bado msimamo wangu upo pale pale, sitaki mume wa mtu, hili nimetokea kama dharura basi..kuanzia leo..sitaki tena mwanaume, hasa mume wa mtu, iliyotokea imetokea, hiyo mara moja na sitarudia tena hili....’akasema.

‘Hahaha, hata sisi tulisema hivyo, kuwa sitazaa tena, lakini kiukweli, watoto wanaraha zake, ukiona mwenzako ana watoto zaidi ya mmoja, wanakimbizana, utatamani sana na wewe uwe nao…, kama mimi sasa hivi natamani nipate mtoto, nipate mtoto wa kiume, kama anavyotamani shemeji yako, ...’nikasema.

‘Mhhh….kweli eeh, labda…’akasema na kutulia kimia kama anawaza jambo.


‘Unajua kama huyo mwanaume angelikuwa sio mume wa mtu, ningekushinikiza akuoe, maana naona umempenda kweli,…lakini sasa, kama ni mume wa mtu achana naye kabisa,…unasikia, ukitaka usalama, na ili hili lisivuje, achana na huyo mwanaume, ndio maana nilitaka nikutane naye, ili nimkanye, na mambo yaishie hapa hapa,kwani mlikubalianaje, kuwa atakuwa akikutembelea au,...?’ nikamuuliza.

‘Nitakubaliana vipi bwana…., na mtu mwenyewe sio mtu wa kunioa...kwanza sipendi kumuongelea tena ...naona hilo tuliache kwanza….’akasema na niliona kweli hakutaka kumuongelea huyo shemeji, nilifahamu ni kwanini, lakini moyoni nilikuwa na hamu sana ya kufahamu huyo mwanaume wake.

Kila mara nilipo-muangalia huyo kichanga, nakuwa kama nawatizama watoto wangu walipokuwa wadogo, na hamu ya kukutana na huyo jamaa ndio inazidi, kwani nahisi atakuwa anafanana sana na mume wangu. Wakati mwingine niliwazia huenda ni mmoja wandugu za mume wangu, lakini nani nisiyemfahamu.

Basi taratibu za hospitalini zilipokwisha nikamshauri kuwa mimi nitampeleka nyumbani, haina haja ya kusubiria gari lake,..kwani aliagiza mtu aje kumfuata, hakutaka kupelekwa na mtu mwingine,

‘Nimesema mimi ndio nitakufikisha nyumbani,…’nikasema, na hapo akawa hana ubishi kwa hilo, na muda huo, ….nikawa nataka kumpigia mume wangu simu, lakini nafasi ikawa hanipi kufanya hivyo, nilitaka nimuarifu kuwa tumeshaondoka hospitalini kama ananitafuta,..na huenda atakuwa na hamu ya kuja kumuona mzazi, lakini kama kawaida nilipojaribu kupiga simu yake ikawa inatumika.

‘Huyu shemeji yako bwana…’nikasema

‘Shemeji yangu..nani, mume wako, kwani vipi, kasemaje…?’ akaniuliza akiniangalia kwa hamasa

‘Kila mara simu yake ipo inatumika, yaani nikitaka niwasiliane naye labda nimtumie ujumbe wa maneno…, ndio baadae anakupigia, siwezi kumlaumu yupo na shughuli nyingi sana,..’nikasema

‘Hamna shida, usimsumbue tafadhali….’akasema

‘Sio kumsumbua, atakuja kunilaumu kuwa sijamfahamisha,…..’nikasema, na akaonekana hana raha, akawa kaangalia nje.


‘Mhh, usiseme sasa tunataka kufichana nakuona kama una mawazo sana badala ya kuwa na furaha, hiki ni kipindi chako cha kufurahi au sio, mimi ndiye rafiki yako, mshauri wako, na lako ni langu, kama kuna kitu unahisi kinakukwaza, niambie nijue ni jinsi gani ya kukusaidia, unanielewa hapo….au ni kuhusu huyo shemeji…?’nikamuuliza.

‘Shemeji!….mmh,…’akasema na akawa kama anawaza jambo halafu akasema;

‘ Ni kweli kama usingelikuwa wewe, nisingelikuwa na wazo hili, lakini mhh, kuna kitu bado sijakielewa, na sijui kwanini naogopa,…labda kwa hivi sasa nibadili mawazo….kwanini, nisifuate masharti yako kabisa, ili kuepusha shari,…’akasema

‘Kuepusha shari…! Ahari gani kwani,…mimi nakushangaa, n kwanini ulikwenda kinyume na maagizo yetu, ungelifuata nilivyokuambia usingelikuwa kwenye wakati mgumu wa mawazo ..sasa nakuona huna raha, sijui kwanini….’nikasema

‘Ni lazima iwe hivi, na hujui tu, nilijua ni rahisi kwa vile ni wewe, lakini mmh, unajua nilijitahidi sana, yaani mpaka nafikia hatua hiyo…niliwazia sana…kiukweli nimepitia wakati mgumu sana…sijui kwanini niliamua kwa haraka iwe hivyo, sikuwa na nia na yeye, lakini imeshatokea tena nitafanyaje, nakutegemea wewe tu…’akasema

‘Ina maana huyo shemeji, ..hukuwa na …sijakuelewa hapo, hebu nifafanulie kidogo, ni kama ulilazimishwa, au ilikuwaje…?’nikasema na kuumuliza

‘Unaonaje tukafunga huu mjadala wa huyo shemeji,..ili nifikirie zaidi, tukifika nyumbani nitakuwa na maamuzi kuwa tulijadili na mimi nikuambie kila kitu au la, ….najua wewe ni mshauri wangu, lakini…kwa hivi sasa naomba tusimjadili shemeji, unaonaje,…tusubirie hadi nifikie muafaka fulani kichwani…’akasema

‘Sawa ungeliwazia hilo tokea awali, lisingelileta mashaka, ingelikuwa ni siri yako tu, lakini sasa umeshaanza kuliweka wazi, na mimi huwezi kunificha tena, ni wewe umenihamasisha, na sio wewe tu hata mtoto ananifanya niwe na hamasa ya kumuona huyo baba yake, ni nani huyo shemeji yangu…’nikasema

‘Sio baba yake jamani…, tafadhali, hiyo kauli siitaki kusikia,,…’akasema

‘Naongea nikiwa mimi na wewe,…hata hivyo kwanini,…ndio nafahamu kwanini unasema hivyo,..lakini wewe mwenyewe umeshamshirikisha huyo mtu au sio, hata hivyo usijali, kwangu mimi najua kila kitu, ni siri yetu mimi na wewe au sio…’nikasema

‘Ukisema ni baba yake wakati ni mume wa mtu naumia sana...mimi sina mpango wa kuolewa na yeye na wala sina mpango wa mahusiano na yeye tena, ilikuwa ni kwa minajili ya hilo zoezi na sasa limekamilika basi….na kiukweli, sitaki hata kuyakumbukia hayo yaliyopita....’akasema na mimi nikaingiwa na hamu zaidi ya kujua ilikuwaje siku hizo walipokutana naye ilikuwaje , lakini sikutaka kushinikiza aniambie jinsi livyokuwa .

‘Ok sawa, lakin kama rafiki yako nahitajia kufahamu mengi ili nisiumie kichwa changu kuwazia hilo,…usiniweke njia panda tena,… na kama umeshampa tahadhari huyo mwanaume, ya kuwa iwe mwanzo na mwisho basi haina shida…’nikasema

‘Nimemwambia shemeji, hili jambo limetokea lakini nataka iwe siri, kwani hata hivyo tangu awali sikutaka alifahamu hili kuwa ndio yeye aliyemipa huo uja uzito, ila kwa kunifuata fuata kwake mara kwa mara ndio nikajikuta nikimwambia hivyo…najua nimefanya kosa kubwa, kinachoniumiza zaidi ni kumuona jinsi alivyokuwa na furaha alipomuona huyo mtoto, sijui kwanini…’akasema.

‘Eeeh,…alikuwa na furaha, ndivyo wanaume walivyo…na huenda na yeye alikuwa akihitajia mtoto, hana watoto nini…?’ nikamuuliza

‘Mbona anao,…’akasema

‘Basi huenda, alihitajia mtoto wa kiume, ..ndivyo ilivyo, ni kama mimi na mume wangu, mfano si kama huyu mume wangu, anahitajia sana mtoto wa kiume, ila nimemuambia asije akakufuru, akaenda kutembea nje, sisi tumtegemee mungu tu, na ipo siku atawapata, …tena mapacha wa kiume kama walivyokuwa mapacha wa kike…hahaha…’nikasema na kucheka.

‘Mapacha tena,!…Unanifanya nikumbuke kuwa hata mimi nilitaka nipate mapacha, ndio maana nilimuona shemeji ataweza kulifanya hilo, kumbe …sio kwa kila mwanamke inaweza kutokea, ni mipango ya mungu au sio…’akasema

‘Kwahiyo kumbe na yeye ana watoto mapacha, kama wangu ehe…wewe naye, kila kitu unataka sawa na mimi, hahaha…lakini ndio uafiki wetu ulivyo,..usingelikuwa wewe ni kama ndugu yangu, ningelisema…uolewe na mume wangu,…hahaha natania bwana, wewe, kuolewa uke wenza sio mchezo, ni heri yeye mwenyewe aamua,..hujui mimi nina wivu sana, naweza kuua, hata hivyo, mume wangu hataki,..na mimi pia sitaweza,….’nikasema na kucheka.

‘Hata mimi sitaki kuolewa uke wenza…..’akasema kwa sauti nzito

‘Mbona umezaa na mume wa mtu…’nikasema kiutani huku nikicheka.

‘Na wewe bwana unaanza kunigeuka, halafu....nimeshampa onyo, kuwa kazi yake imekwisha, sitaki tena mahusiano na yeye na nimemwambia hii iwe siri, kwani sijui kama litapokelewaje, maana kusema na kutenda ni vitu viwili tofauti…’akasema

‘Kupokelewa na nani, na huyo mke wake au sio, ni ngumu, halitaweza kupokelewa vyema, hilo ndivyo ilivyo, najichukulia mwenyewe mimi, ..nisikie mume wangu kafanya hivyo, mbona kutachimbia, sio rahisi kihivyo, ndio maana nilitaka hili lifanyike kisiri na iwe siri yako, wewe…’nikasema

‘Mimi nilijua kutokana na ushauri wako, wewe upo radhi..na nilijua hakutakuwa na matatizo, kwani ushauri wako ulikuwa wa kunitega mimi…’akasema

‘Sio wa kukutega bwana, wewe ndio umeharibu, ..hukufuata kama nilivyokuagiza,..’nikasema

‘Mhh, kwa kauli hiyo, mimi naanza kuhisi uwoga fulani hivi,..maana huwezi kujua msimamo wa mtu nafsini mwake,..na mimi ni jambo la mwisho nililotaka litokee maisha mwangu, mimi sikupenda na sitaki kabisa kuharibu ndoa za mtu. Nitaumia sana, itanifanya nihame huu mji…’akasema

‘Nio maana nilikutahadharisha kuwa hata hilo tendo, eeh, usije kumfahamisha kuwa lengo lako ni nini..na mbegu ikiota usije kumwambia huyoo mkulima…umenielewa hapo…’nikasema

‘Wewe ni rafiki yangu nakuamini sana, na siri hii unaifahamu wewe tu kwa vile wewe ndiye mshauri wangu,….na kama ulivyonishauri wewe kuwa iwe hivyo, ndivyo nilivyofanya, na kuanzia sasa itakwua hivyo, nimekosea huko nyuma, sitaki nikosee tena…,’akasema na kutulia kidogo.

‘Sawa lakini niachosema hapa, eeh, ni wewe hukufanya nilivyotaka mimi…’nikasema
 
SEHEMU YA 12

‘Nasema hivyo wewe ulinishauri kuwa hata kama ni mume wa mtu, nisijali kwa vile ni jambo la dharura, na nichague kwa marafiki zangu ambao naona hawataniletea matatizo,..naomba unisikilize hapo kwa makini…’akasema

‘Sawa basi tutaliongea huko mbele, au sio, au unataka tuliongelee humu kwenye gari nisimamishe kidogo, au sio…?’ nikamuuliza na kusimamisha gari.

‘Hapana nataka nikuweke wazi tu,…kuwa mimi hata kufikia kulifanya hilo haikuwa kazi rahisi kama unavyofikiria wewe..na nilijitahidi iwe hivyo,…kuwa ni dharura tu, lakini ikashindikana maana ilikuwa kama natishwa sasa, usipo..nitamuambia..vitu kama hivyo..unanielewa hapo…mimi sitaki nikuweke wazi kabisa,…maana nimeshaanza kuogopa,… ila naomba usinilaumu kwa hili kabisa, nilifanya juhudi zote ikashindikana…’akasema

‘Ndio maana nasema, kuanzia sasa usifanye jambo bila kuniuliza na huyo mtu kama ingeliwezekana nilitaka awe anapitia kwangu, maana kwa hali yako kwa sasa huhitajiki kukutana naye tena, unanielewa hapo, kuna kitu kinaitwa kubemenda mtoto, uliwahi kusikia kitu kama hicho…, wengi wanakizarau, lakini kina maana yake kubwa sana…’nikasema

‘Mimi wala sipo huko, huyo mtu ilitokea hivyo, na simtaki tena, hata kumuona, nikiwa na mimba ndio nilikuwa natamani …sasa hivi, sitaki kabisa, hata nikimuona naona aibu, nahisi dhambi,....na nitajitahidi kumfukuza akija…’akasema


‘Lakini, sio nakualamu, haya yote umeyataka wewe, nilikushauri vizuri tu,...sasa ni hivi, kwa vile keshajua, na amekuwa na kimbelembele chake, kama atazidi kukufuata fuata, eeh, nina wazo jingine…, usimwache hivi hivi, maana mtoto akikua anaweza kuanza kudai baba yake ni nani…’nikasema

‘Unataka kusema nini…?’ akaniuliza akinitolea macho.

‘Naongelea hili nikiwa na maana ya hali halisi, ..mtoto utamficha wewe kuwa baba yake ni nani, lakini jamii, itakuja kuligundua hilo, na mtoto atakuja kuambiwa, wakati huo wewe umeshaumia sana,..kulea nk…sasa kama anajilengesha kihivyo, basi, mbebeshe dhamana…. muwajibishe , sio kwamba hatuwezi kumtunza, hapana, lakini ili aone kuwa na yeye anathamani fulani, na ili asije kuharibu mpe bajeti yake..’nikasema.

‘Hapana, hapana,…hilo wazo siliafiki, kwa hilo tutakosana, mimi bado nipo kwenye makubaliano yetu ya awali,…, naomba tuyalinde kabisa,..ndio nimeshaharibu kidogo…lakini tusiendelee kuharibu zaidi, na …mimi naona hata kile nilichotaka tukijadili kiishe tu, tuondoke tu….’akasema


‘Usitake kuniudhi, si umeshamuambia yeye…sasa hapo kuna siri gani tena eeh, au mimi na yeye unayemthamini na kumuamini zaidi ni nani,…, mimi nataka tuwe sawa, inachotakiwa kwa vile umeshaharibu , basi na huyo muhusika naye awajibike kama baba, hutaweza kumtenganisha na huyo mtoto tena, huyo baba anaweza kujitahidi kuonana na huyo mtoto, unajua kitakuja kutokea nini,…unielewe hapo, …, hapo kwa hivi sasa hakuna siri, kama tulivyopanaga awali….’nikasema

‘Mhh, hapana,….mimi sitaki kumuhusisha huyo mwanaume na mtoto wangu, sitaki anisaidie kwa lolote lile, mimi mwenyewe nilishajiandaa kwa hilo, nitajua jinsi gani ya kufanya,…na sitaki mtu yoyote yule kubeba majukumu ya kumlea mwanangu, sitaki lawama na mtu…usije kunielewe vibaya wewe ni rafiki yangu…’akasema

‘Kwanini unasema hivyo…?’ nikamuuliza

‘Huyu ni mtoto wangu, na lengo lake tulishaliweka bayana tokea awali,…au sio… hata jina la baba yake nitaandika ukoo wetu, basi, mengine tuyaache kama yalivyo,.....’akasema

‘Ulitakiwa ulifahamu hilo kabla hujamuhusisha huyo mtu, wewe ndio umeharibu, nitarudia tena hilo mara nyingi ili uelewe,..na huenda hata sijui kwanini ulimchagua mtu kama huyo ambaye sasa anakuja kukusumbua, labda kumbe ungelinishirikisha na hilo, huenda hili lisingelitokea,…’nikasema

‘Ndio nakiri kuwa nimefanya makosa, lakini sitaki kuendelea kuyafanya makosa zaidi,..na kumchagua huyo, niliangalia mambo mengi tu..urafiki wetu nk…, na jingine kubwa ni usalama wangu na mtoto wangu,… lakini hata hivyo, yeye ni mume wa mtu, na kwangu mume wa mtu ni sumu, hili kosa nililolifanya sasa naanza kulijutia,na kamwe sitarudia tena, namuomba mungu anisamehe, na anisaidie…’akainama kama anajijutia.

‘Kwahiyo unataka kusemaje,…maana hapo ni kama unaniweka pembeni, kuwa nisijihusishe na mambo yako tena, au…?’ nikamuuliza

‘Hapana sina maana hiyo, najua wewe ni muhusika mkuu wa hili, na kwako nahitajia msaada mkubwa kwako… bila ya wewe bado nitakuwa kwenye wakati mgumu, ..nashukuru kwa hilo, kuwa wewe ndiye umeliwezesha hili, kwa upande huo napata faraja sana, kwani nimepata kile nilichokuwa nikikitaka, kabla sijafikia miaka ya hatari ya kuzaa, ila mengine eeh, tuyaache kama yalivyo, ..’akatulia huku akimwangalia mtoto.

‘Ok, japokuwa sijakuelewa….ngoja tufika nyumbani, na …najua hata shemeji yako akikuona atakuulizia baba yake ni nani…mimi siwezi kumuambia lolote hata kama ni mume wangu,..najua jinsi gani ya kumweka sawa…’nikasema

‘Nampenda sana mtoto wangu..kinachonisikitisha ni tendo lenyewe, ..sikupenda kutembea na mume wa mtu, sikupenda kabisa....ni mawazo yako yaliniteka akili yangu, na sio kwamba nakulaumu kwa hilo,…lakini je yataisha salama,…ninaanza kuingiwa na mashaka,… je hizo lawama hazitaendelea,, hapo ndio naogopa zaidi…’akasema

‘Mimi sioni kwamba kuna tatizo hapo, nakulaumu tu kwa vile hukutaka kufanya kama nilivyokuelekeza, na wasiwasi wangu ni kuwa huyo shemeji, huyo mwanaume anaweza kuwa ndiye tatizo, na lisije kufika hadi kwa mke wake, ndio hapo naogopa mimi…’nikasema

‘Oh, sijui…lakini kwanini….’akashika kichwa huku akimuangalia mtoto wake…

‘Kwanini vipi tena, yaishe tutatafuta njia ….tukishirikiana tutaliweka sawa,…na huenda ukampata mume ..ukimpata mume hili litajifunika kabisa…’nikasema

‘Kumpata mume, wakati nimeshazaa tayari…mmmh, sijui,.. kuna wakati mwingine nawazia mbali na kujiuliza, ni kwanini mimi, na ina maana mimi nilitakiwa iwe hivi, nizae tu bila kuolewa, na huenda nitaishia kuzalilika hivi…, na sasa naanza kuhisi uwoga ambao sikuwa nao…nilitarajia hili litakuja kuisha kwa salama tu, na kwa hili nimejifunza kitu, sitarudia tena makosa haya, huyu anatosha kabisa sitaki tena mwingine...’akasema.

‘Pole sana rafiki yangu, hiyo ndio ujue kwanini watu wanasema ni nani kama mama,…sisi akina mama wakati mwingine tunabeba mzigo mnzito wa siri…usione wakina mama wana watoto wengine wanawabebesha waume wao watoto sio wao, lakini inabakia kuwa siri ya hadi kifo…ni maisha tu…’nikasema

‘Ndio maana, nataka nimlee mtoto wangu peke yangu….’akasema


‘Hamna shida, lakini mimi nitakusaidia kadri ya uwezo wangu, nahili litapita tu.., na mambo yatakuwa sawa tu…, kama tutashirikiana na kuhakikisha huyo mwanaume hakusumbui na kujiweka kimbele mbele, kama ana mke wake, aendelee kuwa na mkewe, kosa limtendeka, basi liishie hapo hapo….’nikasema

‘Na hapo ndio najikuta kujuta kuwa nimetenda kosa, kwanini sikuchagua mtu mwingine zaidi ya huyo, nilijua huyo ndiye chagua sahihi, lakini mmh, lakini `anyway’ cha muhimu ni kuwa kile nilichokitaka nimekipata, na nashukuru sana kwa ushauri wako huo, wewe ni rafiki yangu mwema sana, nakushukuru sana, mengine kwa sasa eeh, niachie mimi mwenyewe, usitake kujua zaidi..’akaniambia.

Nikaangalia saa nikaona tumepoteza muda mwingi tukiongea, na muda huo tulikuwa tumesimamisha gari, nikasema;

`Haya twende….kwahiyo sasa umeamua kuwa twende kwako, umeanza kunikimbia rafiki yako kidogo kidogo, naanza kulihisi hivyo,…mimi nilipendelea huyu mtoto ikiwezekana akulie na kulelewa pale kwangu, ili uwe na nafasi ya kuhangaika na shughuli nyingine ujue wewe ni baba, na mama pia…’nikasema

‘Hapana….nataka nikakae kwangu…’akasema

‘Unajua niliposikia umejifungua, nikawaza huyo mtoto akiwa kwangu, na mabinti zangu waanavyopenda watoto, nikajua huyo atakuwa sehemu ya watoto wetu, sijawaambia na wakisikia, sijui itakuwaje, watafurahi sana, watataka wakae na kaka yao… , mdogo wao, anayefanana na wao, kwanini unapinga wazo langu...’ nikamuuliza .

‘Unajua hata huyo shemeji, alipofika hapa alisema hivyo hivyo…’akasema na akawa kama kasahau kitu akashika mdomo.

‘Alisemaje…?’ nikamuuliza, na akasita kidogo, baadaye akasema

‘Hamna shida …’akasema

‘Mimi sitaki hiyo tabia, ya kuongea jambo, halafu unaghairi, hujui unaniweka kwenye wakati mgumu wa kuwawa waza, usingelikuwa wewe ni rafiki yangu, ningelikufikiria vibaya…’nikasema

‘Alisema hivi, kaamua kuacha shughuli zake kwa ajili yangu, kwa ajili ya mtoto, kwahiyo nisikatae yeye kunichukua hadi nyumbani…..sipendi kufuatana naye tena, nimemkatalia, na ungelifika mapema mngelikutana naye hapa, sijui ingekuwaje, na mimi sikulitaka hilo,....nimemuonya kuwa sitaki anifuate fuate tena, lakini namuona kama kapagawa,hasa alipomuona mtoto utafikiri hana mke na watoto..’akaniambia..

‘Mhh, kwani yeye ana watoto wangapi…?’ nikamuuliza

‘Anaaaah, mh, ana watoto wawili wa kike…’akasema

‘Kama mimi, wewe una hatari kweli, kwanini ukachagua mwanaume sawa na mume wangu, hahaha, nimekugundua, wewe unataka kila kitu tuwe sawa, lakini umezaa wa kiume na sio mapacha, yote ni heri tu au sio….’nikasema

Akatabasamu….na kuangalia pembeni, halafu akasema;

‘Aaah mimi sijui, nilichotaka ni mtoto, sasa kama kuna mtu anapenda mtoto wa kike au mtoto wa kiume, mimi sina wazo hilo,…hilo kwangu halikuwa na sababu niliongea mengine wakati ule kuwa nataka awe hivi na vile lakini …ilikuwa ni kuonga tu, sasa hivi naona mtoto ni mtoto tu…hayo ya mtoto gani, wa kiume au wa kike, ni mawazo ya mtu binafsi, na sitaki hata kuyasikia, ...’akasema

Na tukaondoka kuelekea nyumbani kwake, maana alikataa kabisa niende naye kwangu, sikutaka kumlazimisha zaidi… na mara simu yangu ikalia, alikuwa na mume wangu, nikapokea,

‘Nimekuwa nikikupigia lakini ukawa hupatikani, simu yako muda wote inatumika, vipi ulikwenda kumuona mzazi uliyesema unakwenda kumuona..?’ nikamuuliza

Akasema ndio, ameshamuona tayari, ila anaweza akaenda huko nyumbani kwake, kuna mambo anataka kuyaweka sawa….

‘Kajifungua mtoto gani, mambo gani tena kwani ana udugu na familia yenu….?’ Nikamuuliza, akasema mtoto wa kiume, hakusema zaidi

‘Oh, nahisi umeona wivu sana kwa vile ni mtoto wa kiume na wewe unataka mtoto wa kiume nikuambie kitu hata huyu rafiki yangu kajifungua mtoto wa kiume…yaani we acha tu,..na sisi tukijaliwa tutampata tu, mtoto au watoto wa kiume hahaha, mume wangu, usiwe na wivu,.. …unasemaje…, sijakusikia vyema…’ nikasema kuna kitu aliongea lakini sikukisikia vyema

Baadae akaniuliza nikitoka huko nitakwenda wapi, au nitarudi nyumbani muda gani, nikasema;


‘Sijajua, ila nikimfikisha huyu mzazi kwake, naweza kurudi nyumbani mara moja kuhakikisha shughuli zangu zinakwenda vyema, baadae naweza nikurudi tena kuhakikisha kuwa mzazi yupo na mtu, au nikusubirie huko kwa mzazi, unasemaje, utakuja saa ngapi, ?’ nikamuuliza, na hakujibu mara moja nikazidi kumuambia

‘Ni vizuri uwe wa awali awali, njooo bwana kwani upo wapi, kazini…’nikamuuliza, akasema yupo njiani, barabarani,…

Mara akageuza mazungumzo na kuanza kuniuliza mambo mengine ya kikazi, na baadae nikamuuliza tena

‘Sasa utakuja huji, …mbona hujanijibu swali langu…’nikamuuliza na yeye cha ajabu akaniuliza kuja wapi....,

‘Hivi upo sawa wewe, tunajadili kuhusu rafiki yangu, huyu ni mtu muhimu sana kwangu, kama upo na shughuli zako sawa, lakini nilitaka uje unikute hapa, kuna mambo nilitaka tuyajadili pamoja …’nikasema akauliza mambo gani

‘Ukifika nitakuambia…kwahiyo unasemaje utakuja, ni muhimu sana kwangu…kuna kitu nimekigundua, na…ungelikuja …eeh, unasema, …mbona una mumunya maneno, sikuelewi, …nimefanya makosa gani, hebu uje….kwanini sasa…’nikasema na yeye akasema kwa hivi sasa hana nafsi, niwahi kurudi nyumbani kwani kuna jambo muhimu anahitajia tulijadili mimi na yeye, nikamuuliza jambo gani, hakujibu hapo hapo, ….baadae akasema;

‘Njoo haraka nyumbani nakusubiria…’

‘Ok nakuja…’nikasema

NB: Haya mambo yanaanza kujipika


WAZO LA LEO: Tunaweza kupanga mambo yetu, lakini yawe ya heri, tukipanga mambo yenye ‘shari’ ndani yake, shari hiyo hiyo inaweza ikawa ni sababu ya kuharibu hayo mambo. Hatutafanikia,na hata tukifanikiwa, shari bado itatusakama kwenye maisha yetu. Tusisahau kuwa tukiwa wawili, mwenyezimungu yupo nasi, ..kwahiyo hatuwezi kuficha mambo yetu. Ni bora tujitahidi sana kukwepa mambo mabaya, na kujadili mambo yenye heri, ambayo yatakuja kuleta baraka kwenye maisha yetu.
 
SEHEMU YA 13

Mume wangu aliponiambia yupo barabarani, nikakumbuka kitu, wakati tunatoka pale hospitalini, ..japokuwa sina uhakika sana, niliona kama gari la mume wangu likitoka,..unajua gari langu niliegesha sehemu ya nyuma ya jengo la hospitali…

Hapo nikawaza jambo, huenda mume wangu alikwenda kumuona mzazi hapo hapo hospitalini, ..sikuweza kukumbuka kumuuliza huyo mzazi alilazwa hospitalini gani, kama ningelijua kumbe ingelikuwa ni rahisi tu, ningelimuita aje tumuone rafiki yangu.

Lakini haikuwa na umuhimu kwa muda huo…

Tuendelee na kisa chetu…

**********

‘Mhh, aisee, mtoto wako anafanana sana na watoto wangu, sasa nimemwangalia kwa makini, mwanzoni nilijua ni kwa vile watoto wachanga huwa wanafanana sana wanapozaliwa…, lakini kwa huyu, nimehakikisha, anafanana sana na watoto wangu, isingelikuwa wewe ni rafiki yangu,… ndugu yengu, ningelifikiria vibaya, lakini sizani kama wewe unaweza kufanya hivyo hahaha, sina mawazo hayo mabaya, samahani…’nikasema

‘Kufanyaje…?’ akauliza akikwepa kuniangalia

‘Hebu tuyaache hayo, haya niambie ilikuwaje, ni nani huyo shemeji , maana umekuwa ukisema tu shemeji, shemeji, unajia nikuambie kitu, kila hatua navutika kufahamu ukweli, niambie nisibakie hewani, maana kiukweli umeweza…, hujafanya makosa, na umekipata kile ulichokitaka, mimi nakuaminia, sikufanya makosa kukushauri…’nikasema

‘Nikuambie nini tena rafiki yangu nimeshakuambia,… kosa la awali sitaki kulirudia tena, kuna kauli zako zimenitisha amani…, naona hata ushauri wako, haukuwa na usawa kivile…, ulinishauri tu, kwa kunifurahisha…’akasema akinikwepa kuniangalia machoni.

‘Mhh, sijakuelewa, hapo una maana gani, ina maana mimi nilifanya makosa kukushauri hivyo au….rafiki yangu hapo sasa wanifanya nitake uniambie ukweli,…sasa niambie ukweli, tusije kuudhiana bure…unanifahamu nilivyo, subira yangu ni kubwa lakini ikifikia mahali …inakuwa siwezi tena,.., unanifanya nianze kuvuta hisia ambazo hazipo na mimi sio mtu wa namna hiyo , hasa kwako..’nikasema

Rafiki yangu akabakia kimia, halafu akamuangalia mtoto wake, kwa muda huo nilikuwa naye mimi, ….akasogea na kumchukua, na mimi nikajiweka sawa, kusubiria maelezo,, namfahamu rafiki yangu huyo, akiamua jambo lake , kaamua, lakini pia ananifahamumimi nilivyo, nikisisitiza kitu ujue kweli ninakitaka, sio kawaida yangu kusisitiza kitu, kama hakina umuhimu,

Alitulia kidogo huku akimuangalia mtoto wake,…ilikuwa kama yupo kwenye wakatimgumu sana, nilitaka kumuambia basi, asiumize kichwa, lakini mimi nitakuwa sina amani, sio amani ya kutokumuamini, mimi namuamini sana rafiki yangu huyo,..ila hali ile ilinifanya intake nimfahamu tu huyo mwanaume aliyempa mimba sijui kwanini,

Baadae rafiki yangu akainua uso na kuniangalia,….uso ulikuwa kwenye hisia, ni kama mtu anayehisi maumivu, na kiukweli sikutaka mjadala huo uendelee, naona namtesa, lakini yeye baadae akasema;

‘Kwanini unataka niendelee kuharibu, si wewe ulishaanza kunilaumu kuwa nimeharibu, sasa kwanini tuendelee kufany ahivyo tena…?’ akaniuliza

‘Hapana…hata mimi sikulitaka hilo, ila hizo kauli zako, kauli zako zenyewe zinakusuta, zinavuta hisia nyingine kabisa,....nahisi kuna jambo unanificha, … isije ukawa kweli umetembea na mdogo wa mume wangu, hapana kama ulifnaya hivyo, sio vizuri, sijui lakini...!'nikasema na yeye hapo akacheka kidogo, na kilikuwa sio kicheko kile cha furaha ni kama kulazimisha hivi, yeye baadaye akasema;

'Hapana sijatembea naye, na kwanini…hahaha, hapana…bwana, na wewe mawazo yako ….katika wote, …huyo sikuwa na mpango naye kabisa, unajua aliwahi kunitongoza kipindi fulani, unakumbuka nilikuambia…na tulivyokosana naye pale, ikawa basi tena tatizo lake…, hajui kubembeleza, analazimisha, alihisi mimi ni muhuni, tokea kipindi kile sijawahi kuwa na uhusiano naye wa karibu, nikusalimiana tu kama tukikutana,…kiukweli, siwezi kuficha, awali nilitamani sana awe rafiki yangu, sasa alipokuja kuoa ndio ikawa basi, nikamtoa kabisa akilini mwangu...’akasema sasa kwa kujiamini.

‘Ulimtoa sasa ukamtafuta …hahaha, wewe bwana, nakufahamu ulivyo, ukitaka jambo lako hushindwi…au uniambie ukweli, ulimpata wapi mwanaume anayefanana na mume wangu,…na ni nani huyo, hapo ….sikuachii,… kama sio huyo basi ni nani mwingine,…niambie ukweli rafiki yangu..usiniache njia panda…’nikasema


‘Unajua …hadi hapa nakuona kama huna amani na mimi, na ndio maana najiuliza ule ushauri wako ulikuwa wa nini hasa, kweli ulitoka moyoni,….sasa nafikia kuogopa,..ni kweli, wewe ni rafiki yangu mkubwa sana, na mara nyingi tumekuwa tukishauriana mambo mengi, na mara nyingi wazo lako huwa nalichukulia kwa uzito mkubwa sana, …sikutaka nikufiche kwa hili, kabisa, nilipanga nikuambie kila kitu, lakini naona bora tuyaache tu, kwa usawa wa urafiki wetu..’akaniambia na mimi hapo nikasimama.

‘Hapana wewe niambie tu, ….usiponiambia moyo wangu utakuwa hauna amani….kiukweli ndio hivyo, sio kwamba nakudhania vibaya, katu wewe siwezi kukuweka huko huwezi na hutaweza, ila nataka kumfahamu huyo mtu tu..basi, ili niweze kukusaidia….’nikasema

‘Unakumbuka, niliwahi kukuambia kuwa nawapenda sana watoto wako, na ningelifurahia kupata watoto kama wako…hilo lilitoka ndani ya nafsi yangu, ni kweli nawapenda sana watoto wako, na mimi nilitamani nipate watoto wanaofanana na watoto wako…’akamuangalia mtoto wake.

‘Na…, na uliponishauri hivyo, ..mimi nikaona nifanye juhudi za kumpata mtu atakayenizalia mtoto kama wako, na muda huo nilikuwa natamani nipate mapacha, kama wa kwako, ....’akasema na mimi nikamuitikia kwa kichwa na yeye akaendelea kuongea kwa kusema;

‘Nililiwazia sana hilo,…sasa nifanyeje,…ndio nikaanza kuwachuja watu ninao watamani, maana sio kupenda…siwezi kusema nilimtafuta nimpendaye, …hivi utampandaje mume wa mtu,nikaona nisicheze mbali,…kiukweli, sisi ni marafiki wa kweli na tunaweza kufichiana siri...au sio rafiki yangu…?’ akaniuliza na mimi nikatikisa kichwa, .

‘Wewe na mimi ni kama pete na kidole….au sio…na umkuwa ukinipa kila ulicho nacho, na mimi halikadhalika, ilimradi tuchangiane kwa …urafiki wetu, hilo lipo wazi, wapo waliowahi kusema urafiki wa namna hiyo hawautaki…eti haufai, lakini mimi sioni kama kuna ubaya, au sio …?'akasema huku akisimama na kumlaza huyo mtoto kwenye kitanda chake chenye chandarua,

Unajua kiukweli, wengi watashangaa kwa hili, lakini kwangu mimi akili ilifungwa kabisa kumdhania vibaya rafiki yangu..kabisa kabisa, rafiki yangu nilimchukulia kama mdogo wangu, kwahiyo nisingeliweza kumfikiria chochote kile,…, hata alipotoa kauli hiyo sikuwa na mawazo yoyote mabaya, mimi akili yangu ilifikiria kwingine kabisa,…nikasema

‘Sasa kwanini inanificha, unanificha hata mimi rafiki yako, nilijua tu..’nikasema hivyo, na yeye akanitupia jicho kidogo, na kusema;

‘Unajua sikutaka kukuambia moja kwa moja, kutokana na kauli yako uliyoitoa awali, nikaona bora nisiseme ukweli, hata hivyo….’akasema hivyo na kukatisha, huko kukatisha katisha maneno kwake, ndio kulikuwa kunanipa hamasa ambayo haikuwepo kichwani kwangu kabisa. Hata hivyo sio hamsa ya kumdhania ubaya, hivi ndugi yako anaweza kutembea na mume wako,..kiuhalisia…hasa awe ni ndugu unayemuamini….huwezi kufikiria hilo kabisa.

‘Lakini yule ni mdogo wa mume wangu huoni italeta picha mbaya…’nikasema , na yeye akanitupia jicho kwa sura ya kushangaa, akasema;

‘Hahaha… rafiki yangu, mbona hivi…mimi siwezi kukuficha, na …hebu tuyaache hayo jamani,…’akasema akionyesha ile ishara ya mikono ya kuupia jambo.
 
SEHEMU YA 14


'Ni kweli kabisa sisi ni marafiki wa kweli...na hatuwezi kuangushana, lako ni langu na langu ni lako..nakubaliana na wewe, na wala usiwe na shaka na mimi, …mimi naona ajabu wewe kuogopa kuniambia ukweli, ….sasa nimeshaujua, hata kama, japokuwa bado nahitajia uhakiki wako,…mimi kama mimi nakuahidi kabisa, hilo litaishia moyoni, na hakuna mwingine anayeweza kufalifahamu hilo zaidi yako na mimi,..na huyu uliyemuambia ukaharibu, hilo nakuthibitishia...'nikasema huku nikiweka kidole mdomo kama ishara ya kuahidi

‘Hahaha kweli rafiki yangu, mmh, mbona nitashukuru, ila sio huyo jamani, unayemfikiria wewe, haaah, mimi hapo siwezi kuelewa, nilijua una..umeshafahamu, maana ..aah, sasa hata sijui nisemeji,…kwanini huelewi….’akasema

‘Nimeshaelewa, nakushangaa leo ulimi wako unakuwa mnzito tu…imeshapita hiyo na maji yakimwagika hayazoleki labda yamwagike kwenye udogo wa mfinyazi uliokauka…hahaha…uliposema tu kuwa hukutaka kucheza mbali, basi hapo imejieleza kila kitu, usiwe shaka kabisa, mimi nimelipokea kwa moyo mmoja..., na wewe bwana kwa kupenda stori ndefu, kwanini usiningeliniambia tu moja kwa moja kwa shemeji ndiye kayafanya hayo, basi, limekwisha, au….’nikasema

‘Tafadhali mimi nakuomba, tuyaache….’akasema

‘Tuyaache mbona unasema hivyo tena, au, …?’ nikauliza kwa kushangaa maana mpaka hapo nilishaamini kuwa ni mdogo wa mume wangu, ..yeye akabakia kimia, akiwa kainamisha kichwa chini.

‘Ina maana sio yeye, au…unaogopa nini kuniambia…?’ nikamuuliza

‘Tuyaache jamani…’akasema akitikisa kichwa.

‘Mimi nauliza tu, kama sio mdogo wa mume wangu ni nani mwingine anayefanana na mume wangu…, maana sasa unaanza kuniweka roho juu, kama tumechangia kuna ubaya gani, limetokea limetokea, eeh,....kwanini unaogopa kusema huo ukweli kuwa tumechangia, siwezi kukulaumu zaidi, ..najua wewe ni rafiki yangu, kuchangia, tunachangia sana, au sio,…sasa itakuwa …, mimi mkubwa na wewe mdogo mtu au…?’ nikasema na kuuliza.

‘Kama wewe ni rafiki wa kweli sizani kama hili jambo litakukwaza, ndivyo nilivyokuwa nimefikiria hivyo,…na…na…, na kama kweli ulikuwa na nia njema na wazo lako natumai hutaniona kuwa mimi ni mtu mbaya, kwani yote niliyafanya kwa kufuata ushauri wako…. Zaidi ya hayo kuna kukosea, nimekubali nimekosea kuliweka hili bayana mapema…na kiukweli , hata mimi sikupenda iwe hivyo kwa hali hiyo, ila ningefanyaje basi, mmh, …’akasema

‘Sijasema, au kukulaumu kwa hili kuwa umekosea kumchagua huyo…sawa lakini picha kwa jamii, ndio maana nilisisitiza sana usiri..jamii itatuelewaje au sio…, ninachojiuliza ni kwanini unifiche kitu kama hiki ambacho watu baadae watakuja kujiuliza na wengine watapa mwanya wa kusema la kusema…sasa ni vyema ningelijua mapema ili tuweze kuweka, kinga…’nikasema

‘Mimi nilikuamini sana rafiki yangu kwa ushauri wako, nikaona ngoja nifanye kama ulivyonishauri...sizani kama nimekosea jambo, ni ushauri wako ndio umefanikisha hili, na...na nitafurahia sana na wewe ukilipokea hili kwa moyo mkunjufu...ndio maana sitaki nikufiche kitu...’akasema

‘Kiukweli umefanya jambo la maana sana, kwani hivi ndivyo nilivyotaka,…. Uzae uapate mtoto na wewe…, maana mtoto ana raha zake, wewe mwenyewe utaona, utakuja kuniambia…sitawezi kukulaumu kwa vyovoye vile, maana ndivyo nilivyotaka mimi iwe hivyo, na kwanini nikwazike kwa hili ilihali wewe ni rafiki yangu kipenzi na pia hilo wazo nilikupa mimi. Nikuambie ukweli wazo hilo nililiwazia sana kabla sijakushauri,na lilitoka ndani ya moyo wangu, nipo tayari kukusaidia kwa vyovyote vile….’nikasema kwa kujiamini.

‘Basi kwa vile umenihakikishia hilo na wewe ni rafiki yangu mpenzi, nitakuambia kila kitu bila kukificha, ila nakuomba uwe mkweli wa kauli yako hiyo,..kuwa utalipokea kwa moyo mkunjufua…na nanomba iendelee kuwa ni siri kati yangu mimi na wewe, ama kuhusu shemeji, basi, tutaona jinsi ya kufanya au sio …’akasema

‘Hapo sasa umenena, na …unajua yule haivani sana na kaka yake, kwahiyo sina mazoea naye sana, usiwe na shaka na hilo, na tutajua jinsi gani ya kumbana kiasi kwamba hatafunua mdomo wake, anamuogopa sana mke wake yule, unasikia…’nikasema

‘Tatizo, ….moyo unaniuma, na naingiwa na uwoga, sipendi kabisa urafiki wetu uje kuharibika kwa hili, nakuomba sana, maana sijui nitauweka wapi uso wangu kama wewe ukiamua kunisaliti, ukanitangaza vibaya kwa watu, nitavunjika moyo wangu sana tena san,… kama …oh, kama…wewe utafanya hivyo, lakini zaidi ya hayo nitaumia sana kama hili litakukwaza na kukuumiza…nakuomba sana, tena sana….for the sake of this baby…uwe mkweli kwa akuli yako hiyo’akasema akimwangalia mtoto wake.

‘Kwanini unasema hivyo rafiki yangu kama vile huniamini au mimi siakuelewa hapo,..kwa hili nakuhakikishia kuwa tupo pamoja…hili nimekushauri mimi na nitakuwa mtu wa ajabu kama nitakulamu kwa lolote lile…wewe niambie tu,na nimeshajua ila ni uhakika wako…mimi nakuhakikishia kuwa tutakuwa pamoja kwa lolote lile, si ndio hivyo…mmh, sasa moyo umetulia...’nikatulia kidogo

Yeye akatulia na mara alipoinu akichwa na kuniangalia nikaona machozi yanamtoka,…hapo nikashikwa na mshangao kidogo, sio rahisi kwa rafiki yangu kutoa machozi, akitoa machozi ujue limemfika kweli, kama mwanamke inatokea…hapo mimi kwa huruma nikamsogelea, na kumshika, tukawa kama tumekumbatiaana kiupande upande…alitulia kwa muda, halafu akasema;

‘Rafiki yangu,.oooh, naumia, ….mimi ...nakuomba tuliache hili tu, nakuomba tena na tena, tuliache kama lilivyo, …sitaki,..na … nitaumia sana ikija kutokea kinyume na …..ulivyosema, ulivyoahidi, naogopa sana, kumbuka rafiki yangu ahadi ni deni, ulinishauri wewe, kumbuka hilo….’akasema

‘Hili ninakuthibitishia kutoka moyoni mwangu…, sizani kama huyo mke wa shemeji atalijua hili..zipo namna nyingi ya kulificha…tutashauriana muda ukifika…huyo hatajua kabisa …maana akijua vumbi lake naye sio mchezo…’nikasema

‘Hapo ndio waanza kuniogopesha…’akasema

‘Hatajua bwana…usiogope kabisa..nani atamuambia…mimi nakuahidi kama rafiki yako , mimi nipo tayari kupitisha rupia,… ikibidi…japokuwa ni mkali, lakini namfahamu madhaifu yake,…yule mwanamke anapenda sana pesa,...usiogope kabisa...mimi na wewe hakitaharibiki kitu,..na kwanini ulie, hebu nikuulize, niambie ukweli ni nani mwingine analijua hili….ni mimi na wewe tu au sio, usije kuwaambia hata wazazi wako unasikia, ukiharibu tena huko shauri lako..’nikasema.

‘Oh, basi …mimi naona unipe muda,… niliwazie hili zaidi, nitakuambia kila kitu, usijali, sasa hivi akili yangu haipo sawa....nashukuru sana rafiki yangu…ningeomba nikapumzika, au…sio nakufukuza..jamani…ila kumbuka tu ahadi ni deni..’akasema

‘Mimi nimeshakuambia hakuna kitu kitaharibika niamini mimi rafiki yako, kwanini nikuahidi kitu halafu nije kukusaliti, haitatokea kabisa, nakupenda sana..wewe ni sawa na mdogo wangu kabisa….hata mume wangu namuambiaga hivyo, na kila nikitaja majina ya wadogo zangu na wewe nakutaja, uone ninavyokuthamini, najua wewe huwezi kufanya jambo la kuniumiza mimi au mimi kufanya jambo la kukuumiza wewe….’nikasema

‘Mhh…hapo sasa….’akasema

‘Ndio hivyo…kwahiyo mimi siwezi kuja kukasirika eti kwa vile umefanya hivyo kwa shemeji…, hapana na kama wazo nilitoa mimi eeh, kwanini nije kuumia,…hapana nikifanya hivyo, itakuwa ni ujinga, …siwezi na sitaweza kukusaliti, unasikia, sawa…kama wahitajia kupumzika basi wewe pumzika, sijui nikufanyie nini kwa hivi sasa…’nikasema

Na mara simu yake ikaingia ujumbe, akaichukua na kuusoma, halafu akanitupia jicho, na mimi nikajifanya kama sikumuona, akawa anaandika kitu kwenye simu yake, nahisi alikuwa akijibu huo ujumbe wa simu, halafu akasema;

‘Mimi naona wewe uende tu, usiwe na shaka na mimi, ndugu yangu anakuja, na nikikuhitajia nitakuambia, usiache shughuli zako, mimi nafahamu sana shughuli zako zilivyo, kazi kwanza au sio, hata mimi sizani kama nitajilaza tu kwa vile nimejifngua, mwili wangu ni kuhangaika sio wa kulala lala…’akasema

‘Sawa mimi naondoka naona hata mume wangu ananisisitiza kwa ujumbe wa maneno kuwa niwahi nyumbani …na nikichelewa sitamkuta, sijui ana jambo gani muhimu kihivyo..ngoja niondoke ..haya ..ooh, baby kalala, hivi jina bado eeh, ..’nikasema

‘Adamu….’akasema

‘Safi kabisa, …ooh,babu Adam…bakia kwa amani eeh, …’nikasema nikipitisha mkono na kumshika kwa mbali kichwani, na taswira ile ile ya watoto wangu wakiwa wachanga ikanijia, ..sijui kwanini….na simu ya rafiki yangu ikawa inaita, ..aliangalia mpigaji, halafu akaniangalia,

Mimi nikasema

‘Haya mimi naondoka, wewe endelea, nitarudi…’nikasema na akawa kama anataka kunizuia, nisiondoke, nilijua anataka kuniaga huku anataka kuongea na simu, nikasema

‘Wewe endelea usijali na wala usinisindikize…, nikatoka kwa haraka, nikiwahi kwenye gari langu, na..kuanza kutoka, na wakati natoka, gari kama la mume wangu likawa linakuja, …ikanifanya nisimame, nihakikishe kuwa ndio lenyewe, na linakwenda wapi…




WAZO LA LEO: Ni rahisi sana kutamka neno, hasa la kuahidi, na hata kuapa kuwa nitaweza kutimiza malengo au kutimiza jambo fulani vyovyote iwavyo. Ni vyema, tukawa na uhakika na kauli zetu hizo, na kama hujalifahamu jambo sio vyema kuahidi kuwa ni lazima ufanya hivyo, `lazima’ sio kauli nzuri. Tukumbuke kuwa Ahadi ni deni, na ukiahidi jambo ujue unahitajika kulitekeleza, na ukikiuka ujue umehini ahadi yako, ni hiyo ni tabia ya mnafiki.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom