Mkuki Kwa Nguruwe (Kisa Cha Kweli)

TUKUTANE SIKU YA ALHAMISI TAREHE 2
Siku ya kesho nitaimalizia nikiwa barabarani.
 
SEHEMU YA 66


Ni wakati nafika mlangoni ili nigonge mlinzi anifungulie mara kitu kikanigonga kwa nyumba kichwani, na giza likatanda,.....nikadondoka, na

kupoteza fahamu….

Tuendelee na kisa chetu…

**********

Nilizindukana na kujikuta nipo hospitalini, akili ilipotulia nikagundua kuna mtu kakaa pembeni ya kitanda, …ndio nikamgundua kuwa alikuwa

ni mume wangu, wakati huo alikuwa kajiinamia, nikajaribu kujiinua, lakini nikahisi maumivu ya kichwa, nikashikilia kichwa, na mara ndio

mume wangu akagundua kuwa nimezindukana, kwa akanisogelea na kujaribu kunisaidia, nikainuka na kukaa vizuri,

‘Pole sana mke wangu unajisikiaje...’akasema kwa unyenyekevu.

‘Kwani kumetokea nini…mbona….oh, kuna kitu kilinigonga kichwani, ni nani kafanya hivyo…?’ nikauliza

‘Inaonekana kuna watu walitaka kukuumiza huko jela...’akasema

‘Kuniumiza kwasababu gani,…ni akina nani hao?’ nikawa nauliza maswali kwa mfululizo.

‘Hayo maswali kwasasa hayana msingi, cha muhimu ni kuwa upo salama, na hilo limesaidia kupatikana kwa dhamana yako haraka, kwani

kuna watu walishaiwekea pingamizi, wakidai kuwa upo mahali salama, ungeliachiwa ungekuwa kwenye hatari zaidi...’akasema.

‘Oh, kumbe....’nikasema huku nikishika kichwa, sehemu ambayo nilifungwa bandejii na mume wangu akaniangalia kwa mashaka na kuuliza

‘Kwani unajisikiaje?’ akaniuliza huku akiweka mkono sehemu ile iliyowekwa bandeji na mimi nikawa najihami asije akanitonesha, na

akaondoa mkono wake, na kuniangalia machoni. Alionekana huruma machoni…

‘Maumivu ya kichwa kwa mbali, lakini sio sana, haya niambie na wewe unaendeleaje, maana mgonjwa anamuuguza mgonjwa, nani zaidi

sasa...?’ nikamuuliza

‘Mimi kwasasa sijambo, sina wasiwasi kabisa, nipo tayari kupambana na yaliyopo mbele yangu, japokuwa nachechemea, lakini sio kivile…na

muhimu kwa sasa ni mazoezi tu...’akasema huku akijiweka vyema, kama vile anajiandaa kuongea.

‘Unajiandaa kupambana na yaliyopo mbele yako, yapi hayo mume wangu, unavyoongea ni kama umemlanga mtu au ni maswala ya kazi na

maendeleo...?’ nikamuuliza

‘Dunia hii ilivyo, maisha yetu wanadamu yalivyo, kila siku ni mapambano, au sio, huwezi kulala tu, ukafanikiwa, ni lazima upambane, na mimi

nimejifunza jambo hapo, ili ufanikiwe hakuna kulala..’akatulia kidogo.

Nilimuangalia kwa makini, na hayo maongezi yake nikahisi kama hayupo sawa, kwahiyo nikaogopa kuendelea kumuuliza maswali ya

kumkwanza, nisije nikaharibu nikataka kubadili muelekeo wa maongezi kwa kusema;

‘Hivi huyu wakili wangu yupo wapi...maana nataka kujua mambo yanaendeleaje...aniambie kulitokea nini..nakumbuka nilikuwa mimi nay eye

tu mle ndani, sasa…hapana, lakini sawa…labda…’ nikawa kama nauliza huku nikitafuta simu yangu, sikujua ipo wapi.

‘Wameondoka muda mfupi uliopita, watarudi, kuna mambo wanafuatulia, walisema zoezi limekamilika, sikuwaelewa,…kwani ....unatafuta simu

yako, nahisi ipo kwenye mkoba wako, nikuletee?’akaniuliza.

‘Mkoba wenyewe upo wapi, hata sijui…maana akili haipo..’nikasema

‘Mkoba wako huu hapa, walikuchukulia kila kitu chako, haina haja ya kurejea huko jela, kumbe ni uzembe wa watu tu, hukutakiwa

kupelekwa huko…’akasema

‘Nilijua tu, walitaka kunikomoa, kuijengea kashfa, lakini hawatafanikiwa ukweli utabakia kuwa silaha ya mkweli,…’nikasema

Wakati huo mume wangu aliinuka kuchukua mkoba wangu uliokuwa umewekwa kwenye meza, alionekana akiinuka kwa shida, yaonyesha

bado hajapona vyema ila anajikakamua tu. Akanipa simu yangu, nikaiwasha kwani ilikuwa imezimika, nikawa nimeishikilia mkononi.

‘Oh, hamna shida, ..hivi leo tarehe ngapi, ...’nikasema huku nikiangalia simu, akaniambia tarehe na saa, nikasema;

‘Ahsante sana mume wangu,..nikamtaja kwa jina lake, na yeye akatabasau na kusema

‘Ahsante mke wangu,…’ na kunitaja jina langu, siku nyingi sijasikia ukinitaja jina langu na mimi nikatabasamu, halafu nikasema;

‘Kama dhamana imepatikana basi iliyobakia ni kuangalia kesi hiyo itakwenda vipi, na huyo muuaji ajulikane ni nani, ili niwe huru

kabisa....’nikasema.

‘Mke wangu, kuuwawa kwa Makabrasha kumenishitua sana, sikutegemea kabisa, ni kama bado namuona vile , yaani jana tu mtu mlikuwa

naye, leo hayupo, keshatoweka duniani, hatutamuona tena,..na zaidi kafaje mpaka afikie adhabu hiyo.., hapo ndio inatisha zaidi…’akasema

‘Ni kweli pole sana, najua alikuwa wakili wako tegemezi na rafiki yako mpenzi, lakini yote ni mapenzi ya mungu..’nikasema

‘Mhh ndio hivyo,…kazi ni kazi ukiwa hai, hayupo tena, natakiwa kupambana mwenyewe…unajua nawaza sana baada ya hilo tukio kuwa sisi

wanadamu si chochote...na wengine wanajiona wana nguvu, kwa vile tu wana mali….’akasema.

‘Mhh…mali,…. ni kweli mali ni mtihani, na usipokuwa na mali ni mtihani pia, au sio...’nikasema kama namuuliza.

‘Ni kweli,..hilo nimeliona ni mtihani kweli ukiwa huna kitu, na …ukaoa mke mwenye uwezo, unajikuta mwanaume huna kauli, …sikuongelei

vibaya mke wangu, ila nimekuwa nikiliwazia sana hilo…nafahamu wewe huna shida, mke wangu wewe ni mtu tofauti na wanawake wengine,

lakini wewe utafanyanini, kama wazazi wanataka uwe watakavyo, eeh...’akasema

‘Kwanini unaongea hivyo, kwani kuna kitu gani kibaya umekiona dhidi yangu, au wazazi wangu, tulishaongea hayo sana tukayamaliza, au…

kuna nini cha zaidi?’ nikamuuliza huku nikimwangalia usoni.

‘Haya yanayoanza kujitokeza, yananipa shida kweli kweli, ndio maana hata nilipokuwa hospitalini, nilikuwa nikihangaika kujua jinsi gani ya

kuyaweka sawa, na nikawa natafuta njia ya kuyasawazisha, lakini mwili ulikuwa haukubali,..nilikuwa kwenye mtihani mkubwa sana...lakini

sasa naona kila kitu kitakuwa sawa , ni swala tu la kukubaliana...’akasema.

‘Kukubaliana?? Ukiwa na maana gani hapo, kwani hatukuwa tumekubaliwana awali, mambo yalikuwa shwari au sio, au kuna tatizo, mume

wangu nakuomba uniambie ukweli, kuna nini kinachoendelea…?’ nikauliza bila kujali lolote.

‘Kukubalina ni muhimu hasa kwa wote wanaohusika, ili mambo yaishe tu, kwani tunataka nini zaidi, alikuwepo Makabrasha aliyejiaminisha,

msomi, tena wa nje, mjanja kweli kweli, ..anajua sheria, anajua mbinu za maisha, mbona kashindwa kujilinda, leo yupo wapi,…mmh,hapo

ndio mimi naogopa sana..’akasema

‘Umeliona hilo eeeh, vyovyote utakavyofanya, ukatumia ujanja ujanja wa maisha, mwisho wake ..sote itakuwa hivyo, hakuna mjanja mbele

ya mungu, sasa kama ulidhulumu , kama ulifany madhambi itakuwaje, inatakiwa mimi na wewe tuliwazie hilo, au sio mume

wangu…’nikaongea , kuuma na kupilizia.

‘Ni kweli mke wangu, sasa tufanyeje ili mambo yawe sawa, ili tuwe kama zamani, unakumbuka tulivyokuwa tunaishi, …eeh, japokuwa

kiundani, nilikuwa najihisi mnyonge…unanielewa hapo, mume nakuwa hivo hivyo…’akasema

‘Mume wangu tatizo nahisi kuna mtu kakuharibu akili yako, kwani mimi nilikunyanyapaa, kila kitu tulifanya kwa makubaliano au sio…na

nilikubali kuwa pamoja na yote wewe ndiye mume wangu mwenye mamlaka ya mwanaume, haijalishi kitu, na kukufanya uwe na nguvu zaidi

tukafungua kampuni yako mwenyewe, ili usiwe mnyonge…’nikasema

‘Ni kweli lakini bado ilikuwa sio kama yangu…nilikuwa sijalifahamu hilo..lakini nilipogundua kuwa ni mimi tu, nilikuwa sifuatilii mambo, …unajua

hapo ndio namshukuru sana Makabrasha, kanionyesha mambo ambayo sikuwa nayafahamu, mola ampe makazi mema peponi…’akasema.

‘Mume wangu pamoja na yote hayo, kwanza nakuomba kama upo tayari, uniambie ukweli, sawa uliniomba msamaha, lakini kwa kosa gani,

hujaniambia hilo, lakini pia haya yanayotokea, …mpaka wewe kutafuta wakili yana ishara gani, ni kwanini ukafanya hivyo..kama upo tayari

nakuomba uniambie…’nikasema

‘Nipo tayari sana mke wangu na ndilo nililojiandaa nalo, sitaki tena kupoteza muda…’akasema

‘Sawa..msamaha mnzuri ni ule unakiri kosa ulilolifanya au sio…kiukweli na mungu ni shahidi au sio..sasa mume wangu nataka uniambie

ukweli umefanya kosa gani, mpaka ukafikia kupatwa na ajali, ilikuwa ni tatizo gani…?’ nikamuuliza


‘Mke wangu kweli unataka kuambiwa ukweli..utavumilia huo kweli, hutanichukia, huta… lakini hata hivyo, mbona ukweli wote upo wazi tu,…

mimi nakumbuka nilishakuambia na kukuomba msamaha au sio…lakini anyway, hilo halina shida, ila ukweli mara nyingi unauma, naogopa

kukuumiza mke wangu ...’akasema

‘Mhh, kwanini ukweli uume, ..labda kama una mashaka, ...lakini kama una nia thabiti,ya kujua na kukubali kwa nia njema sizani kama

utaumiza,...tatizo ni kuwa watu wengi hawataki kusema ukweli, wakichelea yatakayotokea baada ya ukweli…’nikasema tukichezeana akili

hapo, kwanza nikitaka kumweka sawa nisije kumuathiri.

‘Hapo ndio kwenye mtihani,lakini kwetu sisi sizani kama kutakuwa na matatizo au sio mke wangu, sasa hivi hata nikiongea ukweli, najiamini,

hakuna shida mke wangu kwahiyo leo ni siku ya ukweli, ukweli wote kutoka kwangu…’akasema

‘Kwanini sasa ujiamini, kwani zamani kulikuwa na kikwazo gani..?’ nikamuuliza

‘Nilikuwa sijafahamu haki zangu, lakini nashukuru kwa ushauri wako, na ushauri wa wakili wetu…unajua mke wangu una akili sana, wewe

unaona mambo vyema kabisa, na ushauri wako unakuwa wenye manufaa sana, ingelifaa wewe uwe mshauri wa watu…’akasema

‘Una maana gani..?’ nikauliza

‘Hata rafiki yako anakusifia sana, …unajua kushauri mambo, bila kujali ..maana ukimshauri mtu eeh, akifanya inamsaidia na unajua tena …na

mengi uliyomshauri yamemsaidia, na hata ukiangalia mengi uliyoyashauri kwenye familia yetu, tukayafuata imekuwa ni faraja sana…wewe

unaangalia mambo kwa usawa, ukiwajali wenzako, marafiki zako, familia yako, unaonaeeh, na zaidi hasa ushahur huo ukiwa kwenye

maandishi, ya kudumu ..yaani mimi sikuwa na mawazo hayo kabisa hata marehemu alisema wewe ni jembe…’akasema

‘Kwahiyo sasa umepona upo tayari kwa haya,…?’ nikamuuliza kwa mashaka

‘Ndio mke wangu, wala usiogope, kama huamini mpigie simu docta wangu, nimepona wewe tuongee , maana hili ni la muhimu sana, ili

tuyamalize haya tuwe huru, nina imani baada ya haya, hakutakuwa na tatizo tena, ..kabisa niamini mke wangu…’akasema

‘ Mume wangu…mimi japokuwa bado nina mashaka na afya yako, lakini kiukweli nilikuwa nasubiria hatua hii, nilikuwa natamani sana, upone

ili tuyamalize haya matatizo, japokuwa sasa yamezuka haya mambo mengine, ni shida kwakweli..sijui yataishaje, lakini tukimpata huyo

muuaji, basi nina imani mambo tayakwisha, nina imani..nikitoka hapa tutalimaliza hili...’nikasema nikimwangalia, na yeye akawa akiangalia

pembeni, nikamuuliza

‘Yah, hilo tutalifanyia kazi, kama mume , nina wajibu wa hilo…mke wangu niamini hilo tutalimaliza,…’akasema akitikisa kichwa.

‘Vipi hali yako kwa ujumla, kweli umepona vyema, maana tusije kanza kuongea hapa likazuka jingine,..?’ nikamuuliza tena….

‘Hahaha , mke wangu huamini, mimi nimepona, nilifuata masharti yao,kama walivyotaka, japokuwa ilikuwa kazi nzito, maana nilikuwa kama

mfungwa, lakini kiukweli ilinisaidia sana, na waliponipima kwa mara ya mwisho waliniambia nimepona kabisa, walisema kila kitu kipo safi,

hakuna matatizo tena, usiwe na wasiwasi na mimi mke wangu....’akasema.

‘Kwahiyo upo tayari kusema yote yaliyotokea, kuanzia yaliyotokea, ukaja kupata ajali, baadae nakumbuka ukaja hata kuniomba masamaha,

nimekuwa nikijiuliza huo msamaha ulikuwa wa kosa gani, sasa je upo tayari kwa hilo , ....?’nikamuuliza.

‘Hilo ndilo nataka tuliongelee leo kama na wewe upo sawa,..maana wewe unaumwa, au tusubiri kwanza hayo mengine ila kuna hili la

muhimu kidogo, mimi kama mume ninawajibu wa kuomba ushauri kwako, au sio, ni la haraka, halihitajii kusubiria, kama upo tayari, tuyajadili

mimi na wewe...’akasema

‘Sawa itakuwa vyema…’nikasema nikiwa sijui anataka tujadili nini, zaidi nilitaka yeye aniambie ukweli

‘Mke wangu kuna mengi yametokea, na muda umepita, na shughuli nyingi zimesimama, kiasi kwamba mtu unashindwa uanzie wapi…lakini

kuna haya yetu wenyewe, haya ndio msingi, na nazidi kushukuru kwa mawazo yak o ya kuona mbali,..sasa ni hivi,…’akatulia kidogo, na mimi

nikasubiria.

‘Mimi nataka tuyamalize ikibidi leo, …ila nitakuwa mtomvu wa shukurani kama nitamsahau Marehemu, na ndio maana naona umuhimu wa

kikao chetu, ili mengina yaishe , Marehemu alikuwa msaada wangu mkubwa, kiushauri, ....kanifungua macho, hasa kwenye maswala ya

maandishi,....’akatulia kidogo.

‘Una maana gani maana naona unatumia maneno hayo ya maandishi, maandishi…?’ nikamuuliza

‘Hapo namaanisha mikataba...’akasema

‘Mikataba…mmh, tuna mkataba mmoja wangu mimi na wewe, au mingine ni ya kikazi au?’ nikauliza na kabla hajajibu nikaendelea kuongea

‘Au wewe una maanisha mkataba huo wa hiari ..?’ nikauliza

‘Huo huo, ..yah, hiyo mikataba ya hiari, …’akasema

‘Lakini,..unajua nilishindwa kukuuliza kwa vile ulikuwa unaumwa, nimeoana ajabu kubwa sana, mbona mkataba ule wa hiari, haupo tena, na

sasa upo mkataba ambao sio ule wa awali…?’ nikauliza

‘Mke wangu, unasema nini…hapana, mkataba ni huo huo, au…?’ akauliza

‘Hahaha, nilijua tu, ni janja yako wewe na Makabrasha, au sio…ule mkataba wa hiari wa awali, umetoweka, na sasa upo mkataba wa

kugushi, sasa niambie maandishi au mkataba unaozungumzia wewe ni upi, wa kugushi au ule wa awali…?’ nikauliza.

‘Mkataba wa kugushi!? Mke wangu hakuna mkataba wa kugushi, hilo neno kugushi limetokea wapi tena …na unasema umetoweka kwa vipi ,

ni kitu hakiingii akilini mke wangu, una…aah,..una- taka kusema nini hapo…’ akaniuliza na maneno ya mwisho akaigiza lafudhi ya kizungu

sijui alikuwa na maana gani.

‘Kwahiyo unajifanya hujui kuwa wewe na Makabrsaha ndio mliofanya hayo!’nikamwambia huku nikimwangalia nikiwa na mashaka nisije

nikazua balaa, lakini sikuona mabadiliko,, yeye kwanza akainamisha kichwa chini, na baadaye akasema;

‘Mke wangu nakupenda sana, .sitaki kukudanganya, kama nilivyosema huu ni muda wa kuambizana ukweli, na…kiukweli kuanzia sasa sitaki

nikufiche kitu.,..nitakuambia kila kitu kilichofanyika, na nina imani utanielewa.’akasema

‘Sawa ukifanya hivyo, mbona tutaelewana tu, mimi sina shida, mwenye shida ni wewe tu ambaye ulihangaika na hadi kubadili mikataba, na

ajali ikaja kukuta, nahisi ni katika kuhangaika huko, sijui ulikuwa unaogopa nini..’nikasema

‘Najua,…hilo sio siri, sasa ni hivi, kiukweli ilibidi nifanye jambo, maana nisingelikubali mimi na wewe tuje kuachana, kisa mkataba, hapana

mimi nakupenda sana mke wangu,..bila kujali hayo…unasikia, mkataba na nini, ni katika kujihami tu, au sio… na mimi naahisi kuwa, nitailinda

ndoa yangu kwa kila hali, hilo nakuahidi, mke wangu, ..’akasema

‘Sawa, nimekusikia..’nikasema

‘Na ndoa hapa nina maana ya kila kitu, familia, mali, na..maisha yetu ya kila siku, kufungwa kwako ilikuwa moja ya pigo kwangu, ..sikuwepo

nyumbani, nilikuwa naumwa, nilitakiwa kama ni kufungwa nifungwe mimi…’akasema

‘Kwani wewe ndio uliua..?’ nikamuuliza

‘Hapana, wewe wanakushuku tu, kama wanakushuku, na mimi nipo, ningeliwaambia wanifunge mimi,…hadi hapo ukweli utakapopatikana,

lakini nilikuwa sijiwezi, naumwa, nipo hospitalini,ningelifanya nini..ni mtihani..lakini sasa nipo ngangari, tutapambana na hao watu…’akasema

‘Kwahiyo kwa kifupi ni kweli kuwa uliubadili mkataba wetu kutoka ule wa asili na kutengeneza mwingine wa kitapeli..’nikasema

nikimuangalia, maana hapo nilitumia lugha ya kumkwanza, lakini hakubadilika, alikuwa vile vile wa kujiamini.

‘Mke wangu, usitumie lugha hiyo, ‘kubadili’ …maana kiukweli hakuna kitu kama hicho, kwa lugha yako hiyo ya kubadili, au kugushi hakuna

kitu kama hicho eeh,....mimi kama mume wako niliona ni heri nifanye jambo, kuilinda ndoa yetu, na nilichofanya ni sahihi kabisa, kwa mujibu

wa mkataba unavyosema.. ‘akasema

‘Kwahiyo ulibadili mkataba kwa kutaka hayo unayoyataka wewe, na kujiwekea hayo mamlaka ya kufanya utakavyo.., nataka jibu tu hapo,

kweli au si kweli, je wewe na mkabrasha mlibadili kitu kwenye mkataba, niambie ukweli tu hapo..?’ nikauliza

‘Mke wangu…’akataka kujitetea

‘Hilo ni muhimu kwangu, kauli yako ni muhimu sana, ni kweli au si kweli, ukijibu hilo itakuwa ni faraja kwangu, niambie ukweli,..mlibadili huo

mkataba au sio, ni kwanini mlifanya hivyo, nataka jibu la ukweli, kwasababu umesema leo utaniambia ukweli..sio ndio hivyo..?’ nikamuuliza

‘Ndio..leo nitakuambia kila kiu ..muda ukiruhusu, ni wewe tu..’akasema

‘Haya jibu swali langu…’nikamwambia..

NB: Muda umekwisha, sehemu hii itaendelea…kuna tukio muhimu sana hapa hutaamini..ngoja niliweke sawa, lakin ngoja nitangulize kipande

hiki.

WAZO LA LEO: Mkataba ni kitu cha makubaliano, na mkataba ulio sahihi ni ule pande mbili zinahusika, na kukubaliana,..mikataba mingi

hasa ya ajira, inakuwa ya pande moja, na muajiriwa anakuwa hana hiyari, ni kukubali tu, huu sio mkataba sahihi.


Kuna mikataba ya mauziano ya bidhaa, kusiwe na ujanja ujanja wa kutapeliana, hii ni dhuluma, hata kama ukishinda kumshawishi

mwenzako ukamdhulumu hili ni deni kwako. Lakini pia kuna mikataba ya hiari kati ya pande mbili, ni lazima kila pande irizike na kila

kipengele. Tukumbuke mkiwa wawili mwenyezimungu yupo kati yanu, au hata mkiwa wengi mwenyezimungu yupo analithibitisha hilo, hadi

kwenye nafsi zetu, kudanganyana ni kujidanganya wenyewe. Tusipende kudhulumu kwa njia hii dhuluma ni dhuluma na madhara yake ni

makubwa .
 
SEHEMU YA 67


‘Sikiliza nikuambie sasa, eeh,..mimi sikufahamu au kuukariri mkataba kabla, kwahiyo sikuwa makini kwa kipengele kwa kipengele…mengi

nilikuwa nafanya kuhakikisha nakufurahisha, eeh kwasababu nakupenda mke wangu.…’akasema
‘Watu wakawa wana..fikia hatua sasa hata ya kuniuliza, umeoa au umeolewa, unaona eeh vitu kama hivyo, mimi sikujali,..sasa matatizo

yakaanza, kuna mambo mengine, nitakuja kukuelezea baadae, ..’akatulia

‘Marehemu nikakutana naye ndiye akanifungua macho, aliniuliza tatizo ni nini, awali sikumuambia, baadae kutokana na hayo matatizo …

unajua, ikabidi nimuambie, kuwa kuna mkataba, na mkataba umekuwa ni mnyororo kwangu,..’ hapo akakaa kidogo, baadae akasema

‘Akaomba aupitie,nikampa, samahani kwa hilo…akausoma , akasema, mbona kila kitu kipo sawa, ni wewe tu hutimizi wajibu wako, unaogopa

nini, hiki kipengele hapa kimekupa mamlaka, ..ilikuwa kama ndio naanza kukiona,…unaonaeeh..’akasema

‘Sasa kama ningelikaa kimia, huo mkataba ukafika kwa wazazi wako, hicho kipengele sikuwa nimekiona eeh cha mamlaka ya mume, na

vingine vingine,lakinikwa leo ni hiki cha mamlaka… mimi nina uhakika wazazi wako wangelikimbilia kuniwajibisha, na hapo ndoa ingelivunjika

tu,..’akasema

Nilimuangalia tu, na aliponitupia jicho na kuiona hiyo hali niliyokuwa nayo usoni, haraka akajibaragua na kama anatabasamu hivi, halafu

akasema;

‘Kwahiyo mke wangu, sasa mambo yote yapo shwari, usiwe na wasiwasi kabisa, sasa nitajitahidi kutimiza wajibu wangu, ..nimeshajielewa,

na makosa yaliyopita ..si ndwele, tugange yajayo, na nachukua fursa hii kukushukuru sana wewe mke wangu, uliona mbali sana…hata

Marehem alikusifia kwa hilo…’akasema

‘Hahaha, mume wangu usinifanye mimi ni mjinga kiasi hicho, kuwa mumeweza kubadili mkataba, na mumetengeza mkataba mwingine

ambao ndio huo unakufanya ujiamini saana..’nikasema

‘Kwanini unasema hivyo mke wangu..?’ akauliza

‘Hebu nijibu swali langu , ni kwanini mlibadili huo mkataba…najua mliubadili na marehemu kwa masilahi fulani…, sasa nataka kauli yako

wewe, ni kwanini ukafanya hivyo, maana unaongea kama vile..hata sikuelewi…’nikasema sasa kwa ukali.

‘Ninachosema mke wangu ni hivi, kama wazazi wako eeh...wangeliuchukua ule mkataba, kabla ya mimi sijaupitia vyema, wangeliweza kutoa

maamuzi na mimi nikakubalia tu, maana sikuwa na uelewa …maana wangeliangalia kosa, na adhabu ya kosa, lakini je vipengele vingine, vya

kutulinda, mimi na wewe , je kipengele cha mamlaka yangu...’akasema.

‘Kwahiyo wewe ulikwenda kwa marehemu ukamwambia umefanya kosa, na mkataba unasema ukifanya kosa adhabu yake ni hivi, sasa

ufanyeje, si ndio hivyo, ukampa mkataba, yeye akafany alichofanya, akakurejeshea na kusema sasa kila kitu kipo sawa, ..mume wangu

wewe hujui hilo ni kosa mnagushi mkataba halali..haya ulipofanya hivyo mlikubaliana malipo gani sasa, maana pesa huna, ulimlipa nini..?’

nikamuuliza

‘Mke wangu sio hivyo, hebu kwanza rejesha akili yako nyuma…’akatulia kidogo, na mimi nikatulia sikusema kitu.

‘Hili la kupata ushauri kutoka kwa marehemu, ililikuwa ni kama hitimisho la mambo mengi yaliyokuwa yamejificha, huenda hata mimi sikuwa

na mawazo hayo kabla, na sikuwa na uelewi wa kisheria kivile, unanielewa hapo, na sitakosea nikisema, matatizo yameanzia kwetu…

sikulaumu,…wakati mwingine..inatokea, na hatuwezi kumkufuru mungu,.. labda nijilaumu mimi mwenyewe kwa kutokujua majukumu

yangu...’akasema

‘Unasema….’nikasema hivyo tu

‘Kiukweli mke wangu Marehemu alikuwa rafiki yangu mkubwa sana, na mengi alikuwa akinishauri yeye, hata kabla ya hilo, na sikuwa na

mtilia maanani kipindi ch aawali, niliona kama ananionea wivu,..lakini sasa yalipotokea matatizo…, ikabidi nimkumbuke…’akasema

‘Matatizo gani sasa, niambie..?’ nikamuuliza

‘Matatizo,….yah, ndio nikafikia kukuomba msamaha, lakini hayo nitakuja kukuambia kwa wakati muafaka, usiwe na wasiwasi mke wangu,

kwanza ni kwanza, hili lililipo mbele yetu....’akasema

‘Kwahiyo sasa hivi unataka tuongelee nini hasa, hiyo kwanza ni kwanza ni nini..?’ nikamuuliza ilibidi nijishushe tu twende sawa na atakavyo

yeye

‘Kuna mambo kidogo, tunahitajika kukubaliana hapa leo hii, ni muhimu sana, nataka tuyaongee, ni kuhusu mikataba tu, tukakubaliana basi

kinachofuata ni utekelezaji tu...’akasema, na mimi kwa vile sikujua anataka kuongelea jambo gani, nikasema;

‘Mhh, haya mambo gani hayo, mimi nakusikiliza wewe sasa...lakini mimi nitafurahi sana nikiusikia ukweli wote…’nikasema

‘Ukweli,…! Mke wangu usijali,..mimi nipo tayari, nitakuambia kila kitu hatu akwa hatua, sitaki nikuchanganye, lakini hili kwanza la muhimu,

ambalo ni msingi wa mengine yote, na sio kubwa kihivyo, ni kukubaliana tu, na ni wajibu wangu kufanya hivyo, na wewe kunishauri, kwa vile

wewe ni mke wangu..’akasema

‘Haya ongea ,..’nikasema

‘Kuna mambo kwenye mkataba yalikuwa yamekaa kimtego-tego kwangu,…’akasema

‘Mambo gani sasa…?’ nikauliza kwa sauti mpaka akashtuka na kuniangalia machoni, halafu akasema

‘Yapo kwenye mkataba tutakuja kuyaona,lakini haina shida saana,…’akasema

‘Unaelewa ni nini maana ya mkataba, mkataba ni makubaliano ya watu wawili au zaidi au sio…sasa iweje mmoja achukue hatua ya

kurekebisha mkataba uliokubalika bila ya idhini ya mwingine kwa masilahi yake…’nikauliza

‘Sio hivyo mke wangu, naona kama hujanielewa, hakuna kitu kilichobadilika, mke wangu…’akasema

‘Una uhakika hakuna kitu mumebadilisha, …usiseme uwongo mume wangu maana nitakuja kulithibitisha hilo,na nikifikia huko sheria

itachukua mkondo wake,…’nikasema

‘Sheria itasimamia kwenye makubaliano yetu..au sio, haiwezi kuvuruga yale tuliokubaliana, na yapo wazi kwenye huo mkataba au sio..na

mimi sijasema kuwa nitafanya kinyume cha makubaliano yetu, na kama ilitokea tutarudi kwenye kipengele cha msamaha, nilishalifanya hilo,

na wewe ukanisamehe au sio, tena mbele ya mashahidi…’akasema

‘Kuna kipengele gani kilisema kuwa wewe kama mume unaweza kubadili mkataba bila ya mimi kuwepo, au cha kukupa mamlaka ufanye

wewe uonavyo ni sahihi, bila ya mimi kuwepo, eeeh hata kama inanigusa na mimi..?’ nikauliza

‘Mke wangu kuna mambo yakitokea mimi kama mume ni lazima niwajibike…na hilo sio kwa mujibu wangu, mkataba unasema hivyo, mimi

nina wajibu wa kuhakikisha familia yangu ipo salama, hebu ona mpaka watu wanafikia kuua,.. ujue watu hao hawana nia njema, sasa kama

nisiposimama kiume itakuwaje…ilibidi mambo yawekwe sawa…’akasema.

‘Unaposema hivyo, mambo yawekwe sawa una maana gani hapo,?’ nikamuuliza

‘Nina maana gani eeh…ina maana mke wangu hulioni hilo, hebu jiulize ni kwanini Makabrasha akauwawa,…alichofanya yeye ni ushauri tu, na

hatukuwa tumefikia mahali pa …undani zaidi, kabla hatujamalizana, kauwawa, masikini wa mungu…’akasema kiuonyonge.

‘Mume wangu upo sawa kweli wewe, mbona nakuuliza hivi unapindisha hivi upo sawa au ulikunywa kidogo leo , ulishaambiwa usinywe

pombe …?’ nikamuuliza maana nilimuona anaongea sasa kama kalewa, lakini hana harufu ya pombe

‘Nipo sawa kabisa mke wangu, nafanya hivi ili unielewe, ili nikitoka hapa , mimi naenda kufanya kazi, usije kusema aah, nimekiuka mkataba,

hapana…mkataba sasa ufanye kazi yake, mimi najiuliza hapo ni kwanini wakamuua Makabrasha…?’akasema


‘Kwanini unauliza hivyo, hata mimi sijui…’nikasema

‘Unaona eeh, wewe ni mke wangu , mambo kama hayo mimi ndiye nilitakiwa niwajibike, …lakini kwa pupa na tamaa za watu, ndio ikafikia

hapa,…kuna mambo yanahitajia umakini, sio jaziba, …’akasema

‘Una maana gani hapo kuwa unanishuku mimi,… eeh mimi nimejikuta katikati ya mambo haya, na hata kushutumiwa kuwa mimi ndiye

niliyemuua, wakati sijui kabisa ni nini kinachoendelea, lakini ukweli utajulikana tu…’nikasema

‘Umeonaeeh, sasa hiyo ni hatari..ina maanisha watu hao wapo tayari hata kuua, kisa ni nini, ..kwa vile kagusa kwenyewe, kwenye mali, au…

labda walihis kuwa tumeingilia mambo yao hapana hatukuwa na lengo hilo, basi kama ni hivyo watakumaliza sote, next ni mimi…’akasema

‘Kwahiyo kumbe wewe kuna watu unawashuku tayari je umeshawaambia polisi..?’ nikauliza

‘Aaah,..hiyo ni kazi yao bwana, sijaongea lolote na polisi, usiwe na wasiwasi kabisa na hilo…lakini kiuhalisia si inajionyesha, ni kwanini

wamuue huyo wakili, ni kwanini…ina maana kuna sababu, na jiulize ni kwanini itokee kipindi hiki ambacho anahangaika kuyaweka mambo

yetu sawa..’akasema

‘Mambo gani yetu..?’ nikamuuliza

‘Kama huo mkataba..’akasema

‘Ehee..mkataba una nini labda ambacho yeye alitaka kuweka sawa..?’ nikamuuliza

‘Yeye alishajitolea kuusimamia, kwa masilahi ya familia…unaona, hata kama ni kusimama mahalamani, ilimradi tu masilahi ya familia yetu

yalindwe, na mimi nilikubali kushirikiana naye, na ndio tulikuwa kwenye mipango ya kukufafanulia hayo hatua kwa hatua, nina imani

ingelimuelewa tu…sasa wamemuua..’akasema sauti kama ya kutaka kulia.

‘Kwahiyo unataka kusema kuwa kauliwa kwa vile alikuwa akihangaika kuyaweka mambo yenu sawa, kutengeza mkataba wenu wa kugushi,

kwahiyo waliomuua ni hao ambao hawakubaliani na huo mkataba wenu wa kugushi, au sio..?’ nikamuuliza

‘Usiseme mkataba wenu wa kugushi, rekebisha kauli yako, huo ni mkataba wetu na wewe ndiye uliyebuni hayo, au sio, na kiukweli sio

mkataba wa kugushi kabisa, niule ule mkataba, au umeshakuwa mkuki kwa nani…eeh, hapana usiwe na wasiwasi mke wangu, …na kiukweli

hao wanaoupinga ni kwa mashaka yao tu, na na..ulikuwa hauwahusu au sio,…’akasema

‘Na ni nani hao…ambao mnawashuku kuwa hawatakubaliana na mkataba wenu wa kugushi,..ukisema hivyo moja kwa moja unamnyoshea

mtu kidole, maana mkataba ule wa asili ulikuwa kati yangu mimi na wewe…

‘Sio swala la kushuku,..uhalisia unaonyesha..’akasema

‘Sasa ni nani, maana ukiacha wewe , mwingine kwenye mkataba huo ni wakili wetu, na mimi…kwahiyo unataka kusema nini hapo, kuwa ni

mimi nimemuua Makabrasha si ndio hivyo..?’ nikamuuliza

‘Hapana, sio wewe mke wangu, wewe hauwezi kufanya hivyo, wewe ndio mimi, wewe ni familia yangu, mimi nawashuku wale wasiotaka mimi

na wewe tuishi kwa furaha na amani….maadui wa ndoa yetu…’akasema

‘Akina nani hao sasa..ni, wazazi wangu au..?’ nikauliza

‘Sijawataja wao, na mimi siwezi kuwashuku wakwe zangu kihivyo, acha polisi wafanye kazi yao…na ..ni hivi mke wangu, shaka shaka ni

lazima ziwepo au sio, inawezekana kabisa wakawa watu wengine tu, wakitumia mgongo wa watu tunaowafahamu, na hilo ni lazima tulifanyie

kazi, tuwatafute ni akina nani hao, sisi kwa upande wetu tutakuwa tumenawa mikono au sio…’akasema

‘Sasa niambie ukweli, unataka nini sasa….maana kama hutaki kuniambia ni kwanini ukachukua maamuzi ya kubadili huo mkataba..sizani

kama tutaelewana, kwa hali kama hiyo sitaweza kukuamini kamwe..?’ nikamuuliza.

*********

‘Hata mimi mume wako huniamini, hahaha, utaniamini tu, wewe ni mke wangu, huwezi kwenda kinyume na mimi, au sio, na ukweli upi basi,

ndio huu ninaokuambia, tulianzia kwenye hii fitina ya mkataba, hii haikuja hivi hivi tu…lakini marehemu akaigundua, na kunionya kwa hilo,

ahsante marehemu…’akasema.

‘Mume wangu utaniambia ukweli au uondoke zako..?’ nikamuuliza.

‘Mimi ni mume wako, nitakuambia ukweli wote usijali, si ndio nimeanzia hapo kwenye mkataba, kuwa hauna shaka, mimi nilikuwa sifahamu

yaliyomo, sasa nimeyafahamu na ndio maana nimeanza kuufanyia kazi au..?’ akasema na kuuliza.

‘Sikiliza mume wangu, usije ukajidanganya na huo mkataba wa kugushi, ukajiona kuwa upo salama, huo mkataba ni wa kugushi, ni

ukiukwaji wa sheria, na hilo tunaweza kulithibitisha kisheria, kuwa huo mkataba wa sasa ni wa kugushi...hata kama kila mbinu zimetumika,…

kuubadili na kusambaza nakala kila mahali husika,.. haisaidii kitu , kwani wakili aliyesimamia hiyo hayupo, ..’nikasema.

‘Hakuna kosa kwenye huo mkataba mke wangu, kila kitu kipo sawa-sawa, na sijui kwanini unauita mkataba wa kugushi, wakati ni wewe

mwenyewe ulikuja na wazo hilo,iweje leo maneno yako uyapinge, au una ogopa nini, usiogope mke wangu mimi nipo ...’akasema.

‘Huo mkataba mpya mimi siutambui, maana sikushirikishwa,..kwanza ni mkataba wa nani na nani, ...nasema hivi ukinielewa nina maana

gani, na usinione mimi ni mjinga kihivyo….sasa ni hivi ili tuelewane mimi na wewe, nauhitajia ule mkataba wa mwanzo kwanza…’nikasema

‘Mkataba wa mwanzo upi tena mke wangu…?’ akauliza

‘Mume wangu usitake tubishane hapa, nikuuliza tu, kama uliona kuwa kuna marekebisho, ilikuwa ni haja gani kuhangaika hivyo,

ungelianiambia tu, kuwa kuna sehemu hupendezwi nazo, basi mimi na wewe tungelikaa tuone tufanye nini au, huo ndio uungwana

...’nikasema.

‘Na mimi narudia tena kukuambia mke wangu, mimi sijui kama kuna mkataba uliogushiwa, upi huo uliogushiwa, kwani kuna mikataba

mingapi, mkataba niujuao ni huo huo, na kama kuna kitu basi tutakaa tutaongea , hilo halina shaka, ila kwa leo eeh...!’akasema na

kunifanya sasa nianza kukasirika, nilishaona mume wangu kadhamiria.

‘Mume wangu acha hayo maneno...kwa kauli yako ya kuzunguka zunguka, kuna muda ulisema kama wazazi wetu waneguchukua kama

ulivyo, ndoa yetu ingelivunjika, je hivyo vipengele vya awali vya kuuvunja ndoa, ni vipi na hivyo vya sasa vya kufanya isivunjike ni vipi,

mume wangu nakuona kuwa mkweli tuyamalize haya mambo kwa amani,....’nikasema.

‘Mke wangu, mimi sijui mambo ya kugushi mkataba,...mimi sio mwanasheria, nitagushi vipi mkataba, na mkataba huandikwa na wanasheria,

baada ya mimi na wewe kukubaliana, tulikubaliana au sio…na mwanasheria akafanya kazi yake, na ndio mkataba ninao ufahamu

mimi,...’akasema.

‘Una uhakika na hayo unayoyasema…mume wangu usitake tupelekane kubaya, mimi sipo hivyo, kawaida yangu ni haki na ukweli, kwanini

tusiwe hivyo mume wangu unataka nini lakini, niambie…?’ nikamuuliza na yeye kwanza akaniangalia, halafu akaangalia chini na kusema;

‘Mke wangu, mimi nina uhakika na hilo ninalolisema, nimeshakuambia kuwa mimi nakupenda sana kweli si kweli,…, na hayo yaliyofanyika,

yalifanyika kwa nia njema tu, ya kuilinda ndoa yetu, na nakuhakikishia kuwa mkataba wetu upo vile vile na mambo yake mazuri tu…, na mimi

nitakuwa mume mwenye mamlaka kama mwanaume, sio mwanaume jina tu...’akasema

‘Una maana gani kusema hivyo?’ nikamuuliza.

‘Mkataba ndivyo unavyosema hivyo...kuwa mimi kama mume nitakuwa na mamlaka ya uongozi wa familia, nitaweza kupitisha maamuzi,

kama nionavyo ni sahihi kwa masilahi ya familia, hilo halihitajii mjadala, au sio…hata bila kuwa na mkataba hilo lipo wazi, kwanini

hunielewi…?’ Akaniuliza

‘Huo mkataba wa kugushi ndio unasema hivyo, hicho kipengele ni kigeni kwangu ..’nikasema

‘Na...wewe utakuwa msaidizi wangu, na hiyo ndio kawaida ya mume na mke, mambo mengine ni ya kuiga tu, ..hayana maana kwetu, ndio

hata Marehemu aliyaona, lakini sio kitu kikubwa sana, maana mimi ndio nilitakiwa nilione hilo, na mimi ndio natakiwa kusema..au sio,

…’akauliza na mimi nikaa kimia

‘Mke wangu, kikawaida eeh, mimi ndio natakiwa kuwa kiongozi wa familia,na ikibidi kurekebisha jambo kwa masilahi ya familia, sihitaji kibali

au sio…ili kuikoa familia, na kila kitu, huo ndio ukweli, zaidi ya hayo, mimi natakiwa kuilinda familia yangu, ukisaidiwa na wewe mke wako,

kwani hapo kuna makosa, ni maneno yale yale...’akasema.

‘Haya unayoyaongea wewe yapo kwenye huo mkataba wa kugushi au sio sio kwenye mkataba sahihi tuliainisha wazi kuwa, ili kuondoa

utata, kila jambo litafanyika kwa makubaliano,….na hili uliliongeza wewe siku ile ya majadiliano,…na tulikubaliana kabisa kuwa asilimia

kubwa ya mambo yetu yapo kwenye mkataba, kwahiyo kama kuna kasoro, au jambo lolote limejitokeza lenye sintofahamu basi, tukae

tujadiliane..’nikasema

‘Sawa kabisa,…’akasema

‘Na hii ina maana gani, mkataba hauwezi kubadilika mpaka kuwe na kikao cha kukubaliana, akiwemo wakili wetu, sasa hayo ya mume

kujiamulia mwenyewe akiona kuna sababu, yanatoka wapi,, na kwanini kuwe na mabadiliko, kuna nini kilitokea,…?’ nikamuuliza

‘Mkataba ni ule ule mke wangu, hakuna kilichobadilika, hata ukiuangalia, eeh, ni mambo yale yale, na yote…tulikubaliana mimi na wewe ..na

wakili wetu…wewe ni wasiwasi wako tu’akasema.

‘Tatizo lako, Makabrasha alikuingiza kwenye anga zake za ulaghai, na umesahau kuwa wewe sio mwanasheria, huyo mtetezi wako sasa

hivi hayupo tena duniani, kuna mambo ya kisheria huyafahamu,...na hayo yatakupeleka pabaya,...mkataba uliokubalika kisheria ni ule

tuliokaa mimi na wewe tukakubalina sio huo uliokaa wewe na mwanasheria wako, ....’nikasema.

‘Ndio huo huo mke wangu, wewe una nakala yako, na mimi nakala yangu, nenda unapoziweka ukazichukue,…lakini mimi nina nyingine hapa,

na nisisahau nakala nyingine ipo huko kwenye vyombo vya sheria… hakuna mkataba mwingine...kila kitu kipo vile vile, hakuna

kilichobadilika, na wewe na mimi tuliweka sahihi zetu na ya mwanasheria wetu, ndio hivyo...’akasema.

‘Mwanasheria gani?’ nikamuuliza.

‘Mwanasheria wetu wa familia, ..ngoja nikuonyeshe mkataba wetu, ninao nakala yetu hapa..hakuna kitu kilichobadilika, ni mambo madogo

madogo tu ulikuwa huyajui labda, ndio yanakuchanganya, eeh, usijali kabisa, hata kama wamemuua Makabrasha kuwa labda, nitakosa

mtetezi, mimi mwenyewe nitajitetea,..na haya yote mke angu ni kwa ajili ya masilahi yetu sote...’akasema huku akiutoa huo mkataba

Na wakati anafanya hivyo macho yangu yakahisi kama kuna mtu kasimama kwa nje, nahisi alikuwa akisikiliza tunachoongea, akasogea

kidogo, …sikuweza kumtambua ni nani,...nikataka kumpa ishara mume wangu, lakini hakuwa makini na yeye akawa ananionyesha sehemu

zile za sahihi akasema;

‘Huu ndio mkataba wetu,..unaona hii hapa ni sahihi yangu, hii ni ya kwako, hii ni sahihi ya mwanasheria wetu wa familia, mkataba ni ule ule,

utabadilishwaje na nani afanye hivyo...hakuna kilichobadilika kabisa , ...unaonaeeh...’akasema huku akifungua fungua huo mkataba, na

mimi nikawa namuangalia tu

‘Mume wangu usitake tufikishane huko..huko unapokwenda ni kubaya, usikubali hayo mambo aliyokudanganya Makabrasha, ..huyo jamaa

anajulikana sana kwa hadaa na ulaghai, hata watu wa usalama wanalitambua hilo..sasa na wewe usiwe mshirika wake, tunachotakiwa

kwasasa ni kusahihisha yale makosa yaliyotokea, ili tuanze pale tulipoishia, ..’nikasema

‘Ndio hivyo mke wangu ndio maana hata kama unataka basi hata huu mkataba tuachane nao au sio, na mimi niwe na mamlaka yangu kama

mume wako au sio, mbona wengine wanaishi tu bila hata ya mikataba unaona eeh, ni kwanini sisi, sababu ya mali au...’akasema

‘Sikiliza mume wangu,….tusilazimishe migogoro isiyo na msingi, na tusitake kulazimisha chuki na uhasama, wakati kuna njia nzuri ya haki,

yenye kuleta mariziano na maafikiano,...hebu nikuulize hivi wewe unachotaka hasa ni kitu gani, niambie ukweli ?’ nikamuuliza mwishoni.

‘Nakupenda sana mke wangu , sitaki mimi na wewe tuachane, mimi nataka ndoa yetu idumu na tuishi kwa amani na upendo...’akasema

‘Ni nani kasema hatupendana na hiyo hoja ya kuachana inatoka wapi, eeh, kuna nini kimeileta hiyo hoja ya kuachana?’ nikamuuliza.

‘Mkataba…eeh, …je ikiingia fitina, na wewe ukaridhia nayo, wakaja wazazi wako ukasema mkataba huu unasema hivyo, itakuwaje, fitina ni

mbaya mke wangu, kuna watu walishajenga majungu, na hata rafiki yako analifahamu hilo, nina uhakika hadi anaondoka bado mlikuwa

hamjawa sawa, kweli si kweli, na wewe ndiye ulikuwa mshauri wake mkuu, kila jambo anafanya kutokana na ushauri wako,…lakini hayo

yamepita kila kitu kipo sawa sasa, au sio,...’akasema

‘Ndivyo alivyokuambia kuwa kila alichokifanya kinatokana na ushauri wangu..?’ nikamuuliza

‘Rejea hoja yetu , kuhusu mkataba ni nani alitoa pendekezo hilo, lengo lake hasa ilikuwa ni nini, sema ukweli wako wote, na je sio kweli

kuwa wewe na rafiki yako, mlikuwa mnashauriana mambo mbali mbali, tatizo lako wewe mke wngu unasahau, unashauri baadae ikigeuka

unakana, usiwe hivyo, mkuki usiwe kwa nguruwe tu…’akasema

‘Sawa, tuwe wa kweli sote, je kuna vipengele kwenye mkataba mlivirekebisha wewe na Makabrasha tumalizane na hilo…?’ nikauliza

‘Hapana, hakuna kilichobadilika, …zaidi ni kuhakikisha kuwa mume ana mamlaka yake, mimi hizo sehemu nilikuwa sijazisomi, nilipozisoma

na kuziona nikajua kumbe nilikuwa siwajibiki..’akasma

‘Haya sawa, sasa nikuulize ni nini lengo la hayo yote , ni ndoa au ni mali…?’ nikamuuliza na hapo akashituka na kuniangalia machoni.

‘Mke wangu nimesema kuwa nakupenda sana....sipiganii mali hapa.., ninachopigania ni ndoa yetu,ndoa ni kila kitu humo..ni kwanini

niipiganie mali wakati ipo , mali tunayo au sio, tuna vitega uchumi vingi, ni swala tu la kuviendeleza....huwezi kupigania kitu chako, eti mke

wangu, mbona sikuelewi...’akasema.

‘Kwa hatua mliyofikia, hakuna jinsi, ni lazima ule mkataba wa asili uwepo, na huo wenu uwepo, tuangalia je ni kweli hakuna kitu

kilichobadilishwa, najua kuna madhambi umeyafanya, na kulikuwa na vipengele vya kukuwajibisha, ukaogoa, ndio maana ukakimbilia huko

kwa Makabrasha.’nikasema

‘Usimsingizie marehemu uwongo, yeye sio kazi yake kuondoa kitu kwenye mkataba, maana sio yeye aliyeutunga,..kazi yake kubwa ilikuwa

ni kunifafanua na kunishauri, yeye ni kweli, alipitia mkataba wetu, akausoma, na kuniambia upo safi kabisa, akanionyesha hivyo vipengele

muhimu ambayo mimi nilikuwa sivitilii manani, vya mamlaka yangu...’akasema.

‘Kwahiyo ndio ukafanya ulivyoona kuwa ni sahihi,..hata kama mimi sijarizia, ?’ nikamuuliza

‘Nimefuata mkataba unavyosema, au sio mke wangu, na .., kama ilitokea kukosea huko nyuma, ni kwa bahati mbaya, ndio maana

nilikuomba msamaha kipindi kile, unakumbuka,… sisi kama wana ndoa wakati mwingine tunakosea kama wanadamu, na kama mkataba

unavyosema mtu ukikosea unatakiwa kutubu, na kuomba msamaha, nilitimiza hayo au sio ...’akasema

‘Mume wangu sitaki kusikia hayo tena, tafadhali, nakuomba uondoke, nataka kupumzika, naona unazidi kunichanganya tu, hayo ni mambo

yenu na marehemu, naomba usiongelee tena kuhusu huo mkataba wenu wa kugushi....’nikasema

‘Lakini mke wangu kuna jambo jingine muhimu kabla sijaondoka, ...kuna mtu anasubiri, maamuzi yangu mimi na wewe’akasema

‘Nani anasubiri hayo maamuzi yangu mimi na wewe, na hapa tulikuwa tunaongea tu, na wewe mwenyewe ulisema kuwa haya ni mimi na

wewe,huyo mtu mwingine inamuhusu nini hapa …na nikuambie kitu,hakuna maamuzi yoyote yamepita hapa, ..hatujakubaliana lolote

hapa.mimi siutambui huko mkataba wenu, nitakubaliana na mkataba wetu ule wa awali zaidi ya hapo mimi sipo.’nikasema.

‘Kuna mtu muhimu sana, alikuwa anasubiria haya maamuzi yetu, ni haki yake lakini, na mimi nilikuja kutimiza wajibu wangu, kuomba ushauri

wako…’akasema

‘Mtu gani huyo, na ana haki gani hiyo…?’ nikauliza

‘Ni mtoto wa marehemu, anahitajia maamuzi yetu, ...’akasema, na hapo nikahisi moyo ukiniruka, ni kama mtu kakushtua ukiwa hujui

‘Nimeshakuambia hakuna maamuzi yoyote yaliyopitishwa hapa, kama una lako jambo endelea kivyako, na kama umedhamiria hayo

uliyokusudia, basi tutapambana mbele ya sheria, wewe si mjanja, sawa endelea na mpango wako huo, kila la heri ..’nikasema

‘Mke wangu usifike huko…’akasema

‘Usipoleta mkataba ule wa awali tutafika huko, maana nakuona hutaki kunielewa, na hutaki kusema ukweli, usihadaike na tamaa za watu

wengine, kumbuka tulipotoka, na kila mara nilikuwa nakuasa, acha tamaa, tushikamane, tuwe kitu kimoja, sasa haya yote yanatoka wapi,

unataka nini husemi…, au kuna kitu gani kimetokea, hutaki kuniambia ukweli,…kwa hali hii bora uondoke, hapa sijisikii vyema nataka

kupumzika,…’nikasema

‘Sawa kama umechoka hujisikii vyema mimi nitafuata mkataba unavyosema, au sio, mkataba umenipa mamlaka ya kufanya yale yaliyosahihi

kwa masilahi ya familia, na na nilichokuja kuonana na wewe ni kupata ushauri, …wewe pumzika, mambo mengine niachie mimi, au sio mke

wangu…’akasema.

‘Au sio kuhusu nini…mimi sijakushauri kitu hapa..’nikasema kwa hasira

‘Mke wangu si umesema niondoke,unataka kupumzika, au?’ akaniuliza huku akigeuka kuniangalia.

‘Sina cha kuongea na wewe hadi hapo utakapoleta ule mkataba wa zamani, na kuniambia ukweli wote, vinginevyo

hatutaelewana...’nikasema.

‘Hamna shida mke wangu, ..tutaongea tu, wewe pumzika, mimi ni mume wako wa halali, hakuna kibaya kitakachotokea, yote niachie mimi,

mimi nitatimiza kila kitu kama tulivyoainisha kwenye mkataba wetu..’akasema kwa kujiamini.

Na mara mlango ukafunguliwa,kwa nje, lakin hao watu hawakuingia, ulionekana mkono tu,..nahisi ni zaidi ya mmoja maana nilisikia

wakiongea, walikuwa wakibishana jambo …mara mlango ukafunguliwa wote sasa, nikaweza kuwaona wapo watu wawili, kwa upeo wangu.

Huyu mmoja alikuwa karibu sana na mlango, nilipomchunguza kwa makini nikaona kama anafanana sana na marehemu nahisi atakuwa

ndio huyo mtoto wa marehemu, kwa muda huo alikuwa akitaka kuingia ndani, na mume wangu akawa kamuwahi na akamzuia,akisema;

‘Mke wangu kachoka, naona mambo yote nitayamaliza mimi mwenyewe, tunaweza kuongea huko mbele ya safari, au ulikuwa unasemaje…?’

akauliza sasa wakiwa wamesimama mlangoni kwa nje.

‘Huyu ndiye yule wakili wangu niliyekuambia, atachukua nafasi ya baba yangu..’sauti yule ambaye nahisi ndio mtoto wa marehemu ikasema.

Na hapo hapo nikachukua simu yangu kwa siri, nikawaweka sawa kwenye kiyoo cha simu na kuwapiga picha, huku nikimchunguza huyo

mtu mwingine ambaye ni wakili kwa kauli ya huyo mtoto wa marehemu, kwa hisia zangu nilimuona ni kama aina za Marehemu, kwa hisia

zangu tu.

‘Habari yako muheshimiwa, …’ mume wangu akasalimia, na wakati anasalimia ndio akagundua kuwa mlango bado upo wazi, akasogea na

kushika mlango na kuufunga. Hata hivyo nilikuwa tayari nimeshawapiga picha.

Na mimi nilipohakikisha mlango umefungwa, kwa haraka nikampigia simu wakili wangu.

‘Sikiliza kama ulivyonishauri haya ni mazungumzo yangu mimi na mume wangu nimeyarekodi, na picha zao nakutumia sasa hivi, yasikilize

na wewe utajua ni nini cha kufanya , wahi kabla hawajafanya lolote, sawa...’

NB: Doa la tamaa limeshagusa mtima, ibilisi hachezi mbali hapo,...je itakuwaje, Kwa leo inatosha.



WAZO LA LEO: Imani ya kweli ya ucha mungu ni pale upomjali mwenzako, na ukawa tayari kutoa hata kile unachokipenda kumsaidia

mwenzako, na ukajali jirani zako, lakini hayo yote kwa ajili ya mwenyezimungu sio kwa ria. Je ni wangapi wapo tayari kuona mwenzake

anapata kabla yake, au zaidi yake, ni wangapi wanayajali matatizi ya wengine, ni wangapi wanaona mali ni kitu tu cha kupita, awe tayari

kusaidia wengine, hapa ni mtihani!
 
SEHEMU YA 68


Kiukweli ndoa yangu ilianza kuwa na wakati mgumu, na ikafikia mahali nikaona nianze kufanya yale ambayo sikutaka kabisa kuyafanya

katika maisha yangu, na katika ndoa yangu, na hata ikafika mahali sasa nianza kuamini kuwa mume wangu hakuwa mwaminifu kwangu,

kifupi kasaliti ndoa yetu, lakini bado nilitaka nisikia kauli yake mwenyewe akikiri ..

‘Nimetoka hospitalini, lakini sina amani..’nikasema

‘Kwanini mke wangu, …upo huru, hiyo kesi isikutia mashaka, haina nguvu, mimi nitaifuatilia na kuhakikisha imekwisha…’akasema

‘Sio kuhusu kesi,…ni kuhusu hayo yaliyosababisha hadi tufike hapa tulipo, sijafahamu ukweli wake bado..’nikasema

‘Kama yapi..eeh, niambie mke wangu nitakuambia kila kitu..’akasema

‘Kwa hili ilivyo yaonyesha wazi, kuwa wewe umenisaliti,..umeenda kinyume cha makubalianio yetu, na nilikuambia tokea mwanzo, kuwa

tunaoona, lakini tuchunge milaka ya ndoa yetu, nikakuuliza je kweli unanioa kwa mapenzi au kwa mali, unakumbuka ulisemaje…?’

nikamuuliza
‘Kwa mapenzi…nilikahidi na ni kweli…’akasema
‘Sivyo ilivyo, kidogo kidogo inaanza kudhihiri..naanza kuhisi kuwa huenda nilifanya makosa, naanza kuuona ukweli wa wazazi

wangu…’nikasema

‘Lakini sasa mke wangu ulitaka mimi nifanye nini, tuangalia ukweli na uhalisia, mimi sio mume wako…eeh, hebu angalia maisha tuliyokuwa

tukiishi je kweli mimi nilionekana kama mume wa familia, swali ni kwanini mpaka ikafikai kubuni hiyo mikataba, wangapi wana hiyo mikataba

kaam mume na mke eeh…’akasema

‘Jibu na swali lakini ni kuwa nilitaka kuwe na kitu cha kuhakikisha kauli yako, maana wazazi wangu walisema mengi, kukuhusu wewe, na sio

kukusema tu lakini rejea maisa yako ya nyuma yalivyokuwa na zaidi nilitaka kuhakiki kauli yako, na sasa je umetimiza ahadi yako…?’

nikamuuliza

‘Mke wangu ulitaka nifanye nini zaidi ili uonye kuwa mimi nimetimiza ahadi yangu, nimekuwa mwanaume mtiifu kwako, kila utakacho mimi

nakifanya, lini nilikukaidi eeh, na wewe je..umetimiza kila nilichokitaka..sema ukweli wako…’akasema

‘Kitu gani ulitaka kutoka kwangu mimi nikakukatalia,…?’ nikamuuliza

‘Mke wangu karibuni hapa, nimekuomba ukubaliane na mikataba , tukianzia na huo ulioubuni wewe mwenyewe, umekataa…huo ni mfano tu,

haya maisha ya ndani ya familia, nilikuomba tujitahidi tupata motto mwingine,…mungu angejalai tupate sasa wa kiume, uli…ulileta

vipingamizi..sasa ulitaka mimi….’hapo akatulia.

‘Kuhusu mkataba, hilo sitaweza kukubaliana na lo, huo mkataba wa kugushi mimi siutambui,, unasikia,…na hilo ni muhimu katika mustakabali

wa maisha yetu, usiporejesha huo mkataba wa zamani, basi ….’nikatulia

‘Mkataba mkataba…unaona mke wangu, huo ndio unaona ni muhimu kuliko ndoa yetu au sio..’akasema

‘Mkataba huo ulikuwa wa hiari, tulikubaliana sote, ukakubali mbele ya wakili, kwanini ulikubali, na kwanini sasa uupinge, na kwanini ugushi

..ina maana kuna jambo umelifanya lipo kinyume na mkataba …na huenda kinyume na ndoa yetu..’nikasema

‘Mkataba ulitusaidia sana tokea awali, maana ndani ya huo mkataba tuliweka yote ambayo yatamlinda kila mtu, na kulinda mali zetu kwa ajili

yetu na familia zetu, na hili nilitaka kuwaonyesha wazazi wangu kuwa wewe kweli umebadilika, nilitaka kujithibitishia hilo mimi mwenyewe …

ili niishi kwa amani…’nikasema

‘Hebu mke wangu tusilumbane zaidi, mimi nakuuliza hivi kwani kuna tatizo gani.

‘Tatizo ni kuwa wewe hutaki kuniambia ukweli, …’nikasema

‘Ukweli upi mke wangu..?’ akauliza

‘Najua hutaweza kuusema wote, nafahamu kuwa hapo ulipo unajiaminisha kuwa vyovyote itakavyokuwa mkataba wa kugushi utalikulinda,

lakini hebu fikiria, je ulichofanya ni sahihi, je sio kweli kuwa umeisaliti ndoa yako, na bado, hukutaka kutubu, ulichofanya wewe ni kutafuta

mbinu za kunufaisha matamanio yako,…’nikasema

‘Mke wangu kumbuka, kule hospitalini,nilifanya nini..sikukuomba msamaha mie.. ukasema umenisamehe…’akasema

‘Kwa kosa gani sasa…?’ nikauliza

‘Makosa yote ya kibinadamu, mimi sio malaika, mimi ..ni mwanadamu tu, nateleza, sasa siwezi kusema kila kosa nililolofanya, ..unajua mke

wangu, eeh mimi ni mtu mnzima, kuna makosa mengine nilifanya kwasababu maalumu,..japokuwa huenda wewe unaweza kuona sio sahihi,

lakini nilikuwa na sababu ya msingi sana…’akasema

‘Makosa kama yap hayo ya msingi kwako,…?’ nikamuuliza

‘Hilo ni moja ya mambo ambayo nahitajia kukaa na wewe , najua utanielewa, vuta subira, lakini nakuhakikishia sio kwa nia mbaya kabisa, ni

katika kuhakikisha ndoa na mali zetu zinabakia mikononi mwetu, wewe hulijui hilo kwa vile umefunikwa na …wazazi wako…’akasema

‘Je ni kweli kuwa umenisaliti…?’ nikauliza

‘Kwanini unasema hivyo mke wangu, hapana sijakusaliti kwa maana hiyo unayoitaka wewe, najua kwako wewe utaona ni makosa, lakini

mke wangu nilifanya hayo nikiwa na sababu za msingi, sikufanya hayo kwa kupenda kwangu, ..najua labda hutaweza kunielewa, ndio

maana nikakuomba msamaha..’akasema.

‘Nikuulize tena je ni kweli kuwa una mtoto nje ndoa..?’ nikaona nimuulize hivyo

‘Mtoto nje ya ndoa una maana gani mke wangu, …unajua nilishakuambia kuna mambo mengine nisingelipeda kuyaongea kwa sasa, kwa

sababu yanaweza kuleta picha mbaya, kutokana na ushauri wa wakili wetu, alinishauri marehemu na sasa huyu wakili mwingine hayo

yanahitajia , tukae tuyajadili mbele yake, ili kila kitu kiwekwe sawa…’akasema

‘Sizani kama tutakuja kuelewana…mimi nasema hivi, nataka ule mkataba wa awali kama kweli una nia njema, ..na ukiwepo, nitakaa na huyo

wakili wako, …vinginevyo, kuanzia sasa sitaki maongezi na wewe…’nikasema na kuondoka kuendelea na shughuli zangu.

***********
Pamoja na hayo aliyoyafanya mume wangu kugushi mkataba, lakini kuna kitu walishindwa..na hapo ikabidi kila mara aje kwangu kuniomba

na kila akija kwangu tunaishia kwenye malumbano tu…

Siku moja akaja na kuniomba tukae tuongee, mimi sikuwa na shida, kuongea tu, ..

‘Mke wangu kuna mambo yanakwama, hatuwezi kufanya mambo ya maendeleo..’akasema

‘Mambo gani…?’ nikamuuliza

‘Ya kibenki…’akasema

‘Kwani kwenye huo mkataba wenu wa kugushi, hamuwezi kufanya na hilo…?’ nikamuuliza

‘Mke wangu…’akataka kusema

‘Kama unataka tuelewane, rejesha ule mkataba wa awali, hapo tutakaa meza moja kama mke na mume, lakini kama utaendelea na mkataba

wenu huo wa kugushi, basi, nitakuacha uendelee na maisha yako na mimi nitaendelea na maisha yangu...’nikasema.

‘Hapana, siwezi kukubali hilo, mimi ni mume wako na mimi ndiye kiongozi wa familia, na natakiwa kuhakikisha familia yangu ipo pamoja,

...nataka watoto wetu watuone tuna upendo na mshikamano,..’akasema.

‘Wewe ndiye uliyesababisha haya yote, kashifa imeingia kwenye familia , tumeanza kwenye ulevi, ndoa isiyo na masikilizano, ..kuzaa nje,

imekwenda hasi kushutumiwa kuua, kugushi, ulaghai, hivi hayo ni maisha geni unayoyataka wewe, mimi sijakulia kwenye maisha ya namna

hiyo, familia yangu ni safi....’nikasema

‘Ina maana unaninyanyapaa kuwa familia yangu ni chafu, ndio maana haya yote yanatokea?’ akauliza

‘Usiongelee kuhusu familia yako ongea kuhusu wewe mwenyewe,...kwasababu wewe una uwezo wa kujibadili na kuwa mtu mwema,

mwaminifu, mkweli ....unaweza kabisa, lakini kama unataka kuishi kwa ujanja ujanja...hutafika mbali...’nikasema.

‘Mke wangu mimi kama mume wako, naomba kauli hiyo, ya kuiniona mimi mchafu, tapeli mlaghai,..iishie,tafadhali, maana sasa unataka na

mimi niwe mkali eeh, ..’akasema huku akinitolea macho, na mimi nikatabasamu na kusema;

‘Itaisha pale utakapoleta mkataba wetu wa awali, tuliokubalina kwa ridhaa moja,....’nikasema.

‘Mkataba ni mmoja tu, hakuna mkataba mwingine, mkataba ni ule ule,...ila wewe unataka kunipanda kichwani, ili nisiwe na sauti kama

mume..hili mimi siliafiki,...na nakuomba mke wangu, jaribu kuniangalia na mimi, unielewe na mimi...kwani nimefanya nini kibaya’akasema

kwa sauti ya upole.

‘Wewe sio mkweli, ...’nikasema

‘Kwa vipi, mbona nimekuambia ukweli, kuhusu mkataba wetu, ...sijaukiuka, ..kuna jingine mke wangu, hakuna, nimejaribu kuwa mume

mwema, silewi tena, hilo huliungi mkono, unataka nianze kuelewa tena, unafahamu madhara ya kulewa, eeh, unataka nikafanya nini

sasa...’akasema.

‘Usibadili mada, mkataba wetu wa zamani upo wapi,..pili huyo mtoto uliyezaa nje ni nani, na umezaa nani, nijibu hayo maswali, na hayo

ukiyaweka wazi, tutakubaliana, ...’nikasema.

‘Mkataba hauna shida, mkataba ndio huo, mimi sijui mkataba mwingine, na ni nani huyo mtoto niliyezaa nje eeh nionyeshe..’akasema

‘Una uhakika na hilo, maana likija kutokea kuwa haya ninayoongea ni kweli, sitarudi nyuma tena...’nikasema.

‘Mke wangu matendo yako ndiyo yaliyonisukuma hadi nikafika huko, sikuwa na raha kama mume, wewe muda wote upo na kazi zako,

sikuwa na raha kama mume, sikuwa na sauti kama mume, nilikuwa nipo nipo tu,....nikawa natafuta njia ya kijiliwaza,...nikaona pombe

atakuwa mpenzi wangu, kumbe pombe ina mitihani yake..je sasa watana nianze tena hayo maisha.’akasema huku natamani kumzaba kibao,

nilimuona kama mtoto mdogo vile.

‘Hivi wewe hujitambui hayo unayoyaongea, unaongea kama mtoto mdogo, ..ulewe kwasababu ya kujiliwaza, ....sikuelewi, ulienda kulewa

kwasababu ya starehe zako, mimi muda wote nilikuwa hapa ndani, kwanini hukuniambia unachokitaka wewe...?’ nikamuuliza.

‘Mke wangu mke wangu, ya kale yamekwisha, nakuomba mke wangu tuishi kama mke na mume, tupendane kama zamani, tugange

yajayo....’akasema.

‘Hujanijibu huyo mtoto uliyezaa nje, ni nani na ulizaa na nani?’ nikamuliza.

‘Hilo nitakuambia pale utakapokubaliana na mkataba wetu, maana kila kitu kipo wazi, na kama unachosema ni kweli basi

tutaambizana....’akasema.

‘Unanichefua,...nashindwa hata kukuelewa, sikiliza, mimi ninakupa wiki moja, nataka mkataba wa zamani uje, kama hautapatikana basi,

...tutaita mawakili wetu, tutaangalia haki ilipo, na ikibidi tutafikishana mbali,...nisingelipenda kuwashirikisha wazazi wangu kwa sasa...ila

baada ya wiki moja hiyo kwisha, kama utaendelea na ujinga wako huo....hutaamini kuwa ni mimi...’nikasema.

‘Mke wangu, kwanini unakasirika,...kwanini yote hayo, mbona mimi nakupenda, na nafanya haya yote kwa mapenzi ya dhati...jaribu

kunielewa na mimi....mbona hutaki angalau kuusoma huo mkataba hakuna kichobadiliak kabisa, na ukweli ni kuwa eeh, mke wangu, mimi

nailinda ndoa yangu, mimi sitakubali kamwe ndoa yetu ivunjike, ....nakuhakikishia hilo....’akasema.

‘Kama umekiuka mkataba, ambao tulikubaliana mbele ya wakili, na kauli yako na yangu ilitoka kuwa likifanyika hili au lile ndoa haipo, basi

haipo, kaulize mawakili kaulize hata watu wa dini, hukulazimishwa, tulikubaliana…kwa maandishi…’nikasema

‘Ni sawa, si kila kitu kipo kwenye mkataba au sio, mbona unaogopa wewe…’akasema

Mimi sikutaka kuongea naye siku hiyo, nikaondoka kuendelea na shughuli zangu nyingine

***********

Siku zikawa zinakwenda, na mimi nikaendelea na msimamo wangu wa kutokuutambua mkataba huo waliotayarisha wao, sikutaka kulifuatilia

kisheria zaidi, hata wakili wangu aliyetaka kulifuatilia kisheria, nilimwambia anipe muda kwanza nijaribu kivyangu, ikishindikana, itabidi

tuingie kisheria.

Ikafika mahali mimi na mume wangu hatuongeai, sikutaka hata kuonana naye, mimi niliweka agizo langu kuwa nitakaa meza moja na yeye

pale tu huo mkataba wa zamani utakapopatikana. Nikaanza kumwekea shinikizo, kwanza nikakata mawasiliano ya kuongea naye, na

kutokushirikiana naye kwenye shughuli zozote alizozifanya kimkataba.

Ikafikia hatua hata hundi za benki ambazo nilihitajia mimi kupitsha nikazizua, kwahiyo akawa hana uwezo wa kipesa zaidi ya kiasi kile

alichoruhusiwa kukutoa kwenye kampuni yake, kwani kiasi kikzidi sana ilitakiwa sahihi yangu na yake, kutokana na kumbukumbu za

kibenki.

Hali ilivyozid kuwa mbaya, akaona amtumie rafiki yake, ili aonge na mimi na siku hiyo akaja docta rafiki yake…akasema ana maongezi na

mimi, akaanzia mbali na baadae akaja kwenye jambo aliloniitia, akasema.

‘Shemeji pamoja na mengine, lakini kuna mambo ya kikazi, ukiwa na msimamo wako huo kazi zitasimama, na kampuni ya mumeo itakufa

kabisa...’akasema huyo rafiki wa mume wangu.

‘Kama analiona hilo ni wajibu wake, kuleta huo mkataba wa awali, na kama anajiona kuwa anauwezo wa kufanya anavyotaka basi aendelee,

na siku nitakapo kamilisha uchunguzi wangu na kuwa na ushahidi wa kutosha kuwa kweli kavunaj mkataba wa hiari, kuwa yeye alishirikiana

na marehemu kufanya hayo yaliyotokea, nitampeleka mahakamani....’nikasema.

‘Lakini mambo ya kampuni msiyaingize kwenye mambo yenu ya kifamilia’akashauri.

‘Sisi tulikuwa na utaratibu wetu mzuri tu, yote hayo ya kikampuni , ya kifamilia, tulikuwa tumekubaliana, ili kulinda mali za familia, ...kama

tusingelifanya hivyo, kampuni hizo zisingelikuwepo, angalia sasa anavyofanya yeye, nasikia kuwa ana mtoto nje, na kama ana mtoto nje,

ina maana ana kimada nje, ni nini kitaendelea hapo, kama sio kuanza kugawa mali halali za ndani ya ndoa kwa watu wasio na haki

hiyo…’nikasema.

‘Sitaki nikukumbushe ..lakini inabidi nikuambie, hayo umeyataka wewe mwenyewe...nilikuambia mwanzoni jaribu kuwa karibu na mume

wako, jaribu kuangalia ana shida gani anataka nini, ujue kuwa binadamu wote sio sawa, kuna utofauti wa kuwaza, unavyowaza wewe, sio

sawa na anavyowaza mwingine na uvumilivu wako sio sawa na uvumilivu wa matamanio kwa mwingine.’akasema.

‘Nakufahamu sana, huenda hayo mliyapanga pamoja, ili kujionyesha kuwa nyie ni wanaume, mnaweza kufanya mpendavyo, au sio...mlewe ,

mtembee ovyo na wanawake , mzae ovyo, si ndio,...?’ nikamuuliza.

‘Sina maana hiyo..ila maisha ya ndoa,msipovumiliana, mkaweza kukaa pamoja, mkajaribu kuziangalia zile tofauti zenu za kifikira,

mkazitafutia suluhu, siku mambo yakiharibika inaweza ikaleta shida sana kujirudi, kwasababu muda huo kila mmoja atajiona yupo

sahihi...kama mngelikaa na kujuana, na kuangalia mwenzangu anataka nini, mgeliweza kulizuia hilo....’akasema.

‘Mwambie rafiki yako, suluhisho la haya ni mkataba wetu wa awali, kwasababu siwezi kukubali huo mkataba wa kugushi, wamekaa na

mwenzake, marehemu, wakatunga mambo yao, mimi sikuwepo, na humo wameweka mambo ambayo mume wangu atajifanyia apendavyo,

bila hata kibali changu....huoni kuwa ni hatari, kutokana na hilo, nasikia kuna mkataba mwingine, ambao, yeye kama mume, kutokana na

mkataba huu, ana hiari ya kuuza hisa kwa mtu mwingine...’nikasema.

‘Mhh, una uhakika na hilo?’ akaniuliza.

‘Ndio maana sitakubali huu mkataba wao, ..kamwe, kwani nikikubali tu, kampuni yake, hatakuwa na hiari nayo, kwani hata marehemu

kauziwa hisa, ...ni nani alipitisha hilo, ....hebu niambie, mimi nikubali tu, ‘nikasema

‘Hilo sio kweli…’akasema

‘Wewe si unanichunguza, wewe si ulitumwa kunichunguza mbona hilo hujaligundua,,,,sasa hiyo ni kazi yako, chunguza na utakuja

kuniambia..’nikasema

‘Mhh..kama imefikia huko,…unajua mimi nilishaachana na mambo yenu, tuliacha ili mjenge suluhu, lakni kwa hali hiyo, kama ni kweli, mmh,

‘akasema

‘Sasa niambie mimi nifanya nini...ina maana gani kuhangaika, kutokulala, usiku na mchana tulihangaika, leo matunda yamepatikana,

yachukuliwe na watu wengine kirahis rahisi tu....na japokuwa hajakubali moja kwa moja, yeye ana mtoto nje, na kwenye huo mkataba wao

wa kugushi, motto huyo na mama yake, wana haki, na watachukua sehemu ya mali...’nikasema.

‘Huyo mtoto ni nani na mama yake ni nani…?’ akauliza

‘Hiyo kazi nakuachia wewe..’nikasema

‘Unajua siwezi kulifanya hilo kwa sasa, wewe mwenyewe ulinipiga marufuku kufuatilia mambo ya ndoa yako, nilishakuambia kama

unanihitajia ni kusaidie,nipo tayari,ukasema hutaki mim niingilie ndoa yako, kwani lengo langu ni kuvunja ndoa yako, ilinikera kwakweli, je

bado una msimamo huo, je bado hutaki nikusaidie…?’ akaniuliza.

‘Kama nilivyokuambia toka awali, wewe endelea na familia yako,mimi hili nitalimazia mimi mwenyewe, yupo wakili wangu, nikishindwa

nitamkabidhi, na hapo itakuwa ndio mwisho wa haya yote maana kila kitu kilikuwa wazi kwenye mkataba...’nikasema

‘Upo tayari kuvunja ndoa yako kwasababu ya hilo?’ akaniuliza

‘Wewe unaliona hili ni dogo eeh, ikifikia hapo, hutaamini, kwanza huo mkataba wa zamani ukipatikana tu,...kama tulivyoahidiana, hatua kwa

hatua, tutatekeleza, na kuna ahdi yangu kwa huyo mwanamke wake waliyezaa naye, mimi nitamuonyesha kuwa mimi ni nani...huwa nikiahidi

kitu sirudi nyuma,....’nikasema.

‘Ndio maana mume wako anaogopa kuuleta huo mkataba wenu wa zamani, anakufahamu ulivyo...’akasema.

‘Huo ni uwoga,...yeye kama ni mwanaume, anatakiwa aingie uwanjani, apambane kiume, na asipofanya hivyo, akaegemea mawazo ya

wenzake, atakosa yote....hajui mimi ninawaza nini, hajui nina mipango gani kichwani, ..hajui...kwani nimetoka naye wapi,...hakumbuki

hilo,...’nikasema.

‘Haya mimi sitaki tena kuingilia mambo yenu, nitakuja tu pale mtakaponihitajia, kama ulivyowaambia wazazi wako, kuwa wasiingilie mambo

yenu, sisi tunawaangalia lakini kama mkikwama, sisi tupo tayari kuwasaidia..’akasema na kuondoka.


Siku moja wakati nipo nyumbani nimepumzika, nikaambiwa kuna mgeni anataka kuongea na mimi, nilikuwa sitaki kuongea na mtu, lakini

nikaona ni vyema kumsikiliza huyo mgeni, kibusara, nikauliza;

‘Ni mgeni gani huyo?’ nikauliza.

‘Ni mtoto wa marehemu Makabrasha..’akasema msaidizi wangu wa ndani.

‘Huyo tena, nilishasema sitaki kuonana na yeye, kama anataka kuongea akaongee na huyo huyo mwenzao, sio mimi…’nikasema

‘Kasema hawezi kuondoka, bila ya kuonana na wewe, kwasababu huenda akasafiri, na hawezi kuondoka bila ya kuhakikisha ameyamaliza

mambo yote aliyotakiwa kuyafanya,…kwahiyo yupo nje anasubiria kukaribishwa…’akasema bint msadizi wangu wa nyumbani.

Nikawa kimia nikitafakari,…je dawa ni kukimbia jambo au kukabiliana nalo…nikikataa kuongea naye ina maana nimekimbia..nimeogopa,

nikiongea naye je…huenda kuna mitego, kuna jambo wamepanga,na huenda ikawa ni sababu ya kuniumiza zaidi kimawazo.

Nikachukua simu yangu na kumpigia wakili wangu wangu..nikamuelezea, wakili wangu wangu akasema

‘Fanya kama nilivyokuambia…

NB: Jamani hapa nimeazima laptop ya mtu, kuonyesha jinsi gani nawajali


WAZO LA LEO: Siri ya mafanikio, ni kujibidisha kwenye shughuli unayoifanya, na siri ya kushinda vita sio kukimbia, ni kukabiliana na adui

yako, na siri ya matatizo sio kulalamika tu, bali ni kujitoa muhanga na kukabiliana na matatizo hayo. Mitihani mingi ipo kwa minajili ya sisi

kufunguka akili zetu na kutafuta njia bora zaidi ya kukabiliana na matatizo hayo. Tuifanye mitihani hiyo kama sehemu ya daraja la kuvuka na

kusonga mbele..lakinii tujitahidi kupambana na mitihani hiyo kwa njia za heri, huku tukimuomba mola wetu.
 
SEHEMU YA 69

‘Ni mtoto wa marehemu Makabrasha anataka kuongea na mimi…’ nikamwambia wakili wangu naye akasema

‘Ongea naye ila fanya kama nilivyokuelekeza…’akasema wakili.

Nikachukua simu yangu maalumu na kuhakikisha ina chaji ya kutosha.

******

‘Mkaribisheni kule bustanini, nakuja kuongea naye…’nikamwambia binti wangu wa kazi, sikutaka kuongea naye ndani, kwani sikuwa na

amani naye kabisa, nilihisi kivuli cha baba yake kipo pembeni yake. Huenda mtoto kama baba, hulka hazitengamani

Walimkaribisha bustanini, na mimi nilipohakikisha kila kitu kipo sawa, nikamfuata huko bustanini, nikafika na kusalimiana naye, sikutaka

kumuonyesha jinsi gani nilivyochukia, maana moyoni niliona kuwa wao, kutokana na baba yao, watakuwa wamepanga jambo la kuifisidi

familia yangu, na nilitakiwa niwe makini kwenye kauli zangu kama alivyonishauri wakili.

'Karibu mgeni....'nikasema na alisimama na kusalimia kwa adabu tu, baadae sote tukaa kwenye viti, mimi ndio ni nikaanza kuongea;

‘Haya niambie una shida gani na mimi?’ nikamuuliza huku nikimwangalia moja kwa moja usoni, maana tulikaa tukiwa tunaangaliana na kati

kati yetu kulikuwa na meza. Nilitaka nimuone usoni, kwani mtu unaweza kumpima ukweli wake, au ujasiri wake, kwa kumwangalia usoni.

‘Samahani sana kwa usumbufu wangu, wa kutaka kuongea na wewe...maana nimejaribu mara nyingi bila mafanikio, na leo nilipanga, kama

ikishindikana basi sitaondoka,maana...siku zangu za likizo zimeisha, natakiwa kurudi kazini...Ulaya...’akasema.

‘Sawa pole sana,na pole sana kwa msiba, kwani sijapata hata muda wa kukupa pole yangu..ila salamu za rambi rambi nilizifikisha kwa

kupitia mume wangu , natumai ulizipata’nikasema

‘Hamna shida, nashukuru sana nilizipata, sina cha kuwalipa ila mola atawalipa zaidi, ….’akasema

‘Kiukweli imebidi iwe hivyo kutokana na hulka zenu,..kiukweli japokuwa marehemu haongelewi vibaya, alichokifanya baba yako kimenivunja

nguvu, ..namafahamu sana kutokana na tabia yake, lakini sikutarajia atakwenda kwa kiasi hicho,..sasa kauwawa, sijui ni nani wamefanya

hivyo….imezidi kunivunja nguvu, haya niambie ulikuwa unanitafutia nini, maana kila mara napaat ujumbe kuwa unataka kuongea na mimi..?’

nikauliza.

‘Mimi sina nia mbaya kama unavyofikiria wewe,..huenda ungelisikiliza toka awali tungelishamalizana mapema tu, na kila mtu akashika

hamsini zake. Hapa nilipo nakwama kuondoka maana mambo mengi bado hayajakaa sawa, na mimi nimeachiwa majukumu mengi na

marehemu baba, na familia yote inanitegemea mimi, kiukweli sikulipenda hili, lakini nitafanyaje....’akasema.

‘Hayo majukumu uliyoachiwa, yananihusu nini mimi, hayo si mambo yenu ya kifamilia au sio…?’ nikauliza na yeye bila kujali swali langu

akaendelea kuongea.

‘Mhh..ni hivi, mimi nilipofika hapa Dar kutoka nje kutokana na kifo cha baba...nilitarajia mengi, maana mimi namfahamu sana baba, yeye na

mimi hatukuwa sambamba kutokana na mitizamo yetu, hata hivyo yeye alinijali kama mtoto wake wa kwanza, na mamambo yake mengi

aliyaweka wazi kuwa mimi ndite nitakuwa msimamizi wa kila kitu..’akatulia kidogo.

‘Kifo chake kimenishtua sana, maana kuna mambo mengi tulikuwa hatujawekana sana…sikuwa tayari kwa haya majukumu kabisa....lakini

ndio hivyo, mapenzi ya mungu hayapingiki…’akashika leso yake na kufuta machoni, lakini sikuona dalili ya machozi

‘Nilipofika kiukweli kwanza kabisa nilitaka kujua ukweli wa kifo cha baba, na nilipewa taarifa yote kutokana na uchunguzi wa polisi. Na kwa

matizamo wangu wa haraka kutoka na taarifa za watu hata kabla ya taarifa ya polisi,..nilihisi nyie mnaweza mkahusika, ...na kiukweli kama

mngelikuwa nyie mnahusika, ningesimama kidete kuhakikisha haki inapatikana, bila kujali maagizo ya baba..’akashika kichwa, kama vile

kinauma.

‘Sasa uchunguzi wa polisi unaonyesha tofauti, imeonekana hauhusiki, na kwa kujirizisha, nikafanya uchunguzi wangu binafsi, na kuhakiki

taarifa niliyopewa, nikagundua kuwa mambo ni yale yale, hauhusiki..

'Sawa hausiki kwa moja kwa moja, lakni bado nikawa na dukuduku, ni kwanini,…baada ya baada ya baba kuwa wazi kwenu, ndio kifo chake

kitokee, hapo ulipa maulizo mengi, na sikupendelea sana kuunganisha haya na mambo ya kisiasa japokuwa hilo limebeba uzito wake ,

lakini kwa vile ushahidi waonyesha kuwa upende wenu haupo, sasa nihangaike nini tena na nyie...bado swali mpaka sasa ni kwanini…

tuliache hilo hapo....’akasema.

‘Ngoja nije kwenye hoja...mimi ninamfahamu sana marehemu baba yangu, nafahamu sana mbinu zake za kupata mali, baba ni mjanja na

alichukua kazi hiyo ya uwakili akijua kuwa itakuwa ni kinga ya ujanja wake…ni sawa kasoma, na kiukweli kaiva, lakini kwanini asifanye

kitaaluma yake zaidi, hilo mimi sijui, na hata tukikutana naye huwa tunaishia kulumabana juu ya hilo.....’akasema.

‘Kutokana na tabia hizo, niliposikia kuwa baba kafariki cha kwanza nilichouliza kafa kwa kifo cha kawaida au kauwawa, nikaambiwa kapigwa

risasi, nikajua tu ni yale yale, na nikauliza ni nani kashukiwa, nikaambiwa ni wewe..nikatamani sana kwanza nije niongee na wewe niujua

ukweli.

'Unajua kazi za namna hiyo, tabia ya namna hiyo,..ni lazima ujue kuwa kifo chako kipo pembeni, mimi naishi nje, na nimeona watu wa aina

hiyo wanavyouwawa, bila kufa, watu uliowatendea hivyo hawawezi kuwa na amani, amani yao ni kufa kwako...’akasema

‘Blackmail,ni kazi ya hatari sana, sio mchezo, kumghilibu mtu, na kupata kile alichokihangaikia kwa jasho lake kwa shida, wewe uje

ukichukue kilaini,sio rahisi kihivyo, sikuwa na ushahidi wa moja kwa moja wa hilo, ila nishaambiwa na watu naa hata na polisi kuwa alikuwa

akishukiwa hivyo…’akatulia

Nilitaka nimkatize lakini alikuwa akiongea kwa haraka sana, na nikaona nimuache tu aendelee..

‘Mimi nilikuwa sielewani na baba tangu niwe na fahamu naye, japokuwa sikuwahi kuishi naye kikaribu hivi, maisha yangu, nililelewa na

babu na bibi, maana mama alikuwa akiishi huko ,....na hata nilipokuwa nasoma hapa nchini, nilikuwa kwa babu, baadae wakati nipo elimu ya

juu, ndio nikapata muda kidogo wa kuishi na baba, hatukuwa tunaelewana, damu zetu hazikuendana kabisa....

‘Baba akataka nisomee uwakili, lakini mimi siupendi uwakili mambo yangu sayansi, mitandao, komputa, ni hivyo,..ndio ndoto zangu, yeye

aliona ni mambo ya tamaa yasiyo na umbele zaidi

'Mimi nikamwambia moja kwa moja baba, mimi sitaki kuja kutegemeamali zake nataka kuja kuishi maisha yanayotokana na juhudi zangu na

dua zangu zikakubaliwa, nikafaulu mitihani yangu, nikaomba kwenda kusomea nje ya nchi, na bahati nikapata nafasi hiyo ..’akatulia

akiangalia saa

‘Na nikuambie ukweli, kwenda kwangu kusoma nje, hakukuwa na mkono wake, nilihangaika kivyangu, nikafanikiwa kivyangu, na huko

nikasoma kwa shida sana, na aliposikia nasoma kwa shida, ndio akanitumia pesa...nilizikataahizo pesa zake kabisa...nikamrudishia,

hakuamini hilo, na akaniuliza kwanini, nikamwamba iweje sasa ndio ananijali, ..kwanini alinitelekeza utotoni mwangu, hayo yana storia

yake…’akasema

Hapo nikamuuliza;

‘Kwanini ulifanya hivyo?’ nikamuuliza nikimwangalia machoni, huyu mtu huwezi kumhisia vyovyote, hajionyeshi tabia yake usoni,..ni watu

wachache wenye tabia hii.

‘Kikubwa ni kuwa nilishamfahamu baba, nilijua pesa zake ni chafu na mimi sitaki pesa chafu, ndio maisha yangu nilivyoamua yawe hivyo,

wewe hujiulizi kwanini baba alikuwa hakai na mama, mama ni mtu wa dini, na alifahamu tabia ya baba, akaona akae mbali na yeye, na mimi

kiukweli nimerithi tabia ya mama, japokuwa sijasomea mambo ya dini...ila mimi nataka niishi kwa jasho langu, sio kama alivyokuwa akiishi

baba...’akasema.

'Kwahiyo kwa kauli yako mwenyewe unakiri kuwa baba yako hakuwa mwaminifu au sio..?' nikauliza

'Ni kweli, mola amsamehe madhambi yake tu...hilo siwezi kukukatalia...'akasema

'Sawa endelea maana mpaka sasa sijakuelewa mimi nahusikanaje hapo ...'nikasema

‘Kifo cha baba, kikatufanya tukutane kama familia, nashukuru sana kuwa wanafamilia wote walikuwa wakimfahamu sana baba, hakuna

aliyetaka kuingilia mambo yake, kila mmoja aliona kuwa akigusa huko huenda damu za watu, dhuluma za watu zitawaandama. Mimi

nikapewa jukumu la kusafisha jina la baba, maana keshafariki sasa tutafanyaje na maisha lazima yaendelee, ..je tutaendelea kukumbatia

hiyo hali, au tutaishije.. ni lazima jambo lifanyika..’akatulia.

'Niliongea na mama, na mama akasema tusaidie japokuwa ...ili roho ya baba iwe na amani, na hilo..likawa jukumu langu la

kwanza,...kuisafisha familia yetu na kuhakikisha kuwa hatueleweki vibaya, .....'akasema

'Kwa vipi sasa..?' nikajiukuta nimeuliza hivyo

‘Kazi yangu kubwa, ilikuwa kufuatilia kwa kila aliyeumia kutokana na baba...wapo wanaojulikana, na tulitangaza kama kuna mtu kwa namna

moja au nyingine alipata athari, kutokana na utendaji wa baba ajitokeze,..watu waliona kama ni utani,..mimi nikafanya kazi ya zaida ya

kuwafuatilia kwa kila niyekuja kuambiwa, au kuona kwenye kumbukumbu za baba...na ili hayo yafanikiwe, tulimtafuta mwanasheria ambaye

alisaidia kisheria....’akasema.

‘Sasa pamoja na yote...ikabakia wewe, kwa maana ya kisheria, sijui kama kuna baya aliwafanyia, sijui, ...ila kuna mambo ya kisheria,

ambayo ni muhimu sana nikae na wewe tuone tutafanyaje, nielewe sana nimechukua muda mrefu wa maelezo ili uelewe dhamira yatu….’

Hapo sasa akaniangalia usoni moja kwa moja.

'Mambo gani hayo ya kisheria..?' nikauliza

‘Kwanza nianze kwa kuingilia ndoa yako, niligundua kuwa …wewe na mume wako hampo sawa, hilo sihitaji wewe kukubali, ila nilipoongea na

baba ...mume wako hata bila kuniambia nikaligundua..lakini kuna mikataba imeachwa, inakuhusu wewe na mume wako, inahusu mali

nk...unajua mimi sikutaka hata kuingilia undani wake, nikawa nimeongea na mume wako kuwa kama kuna lolote baya ndani yake aniambie

tuachane na mikataba hiyo kabisa…’akatulia

‘Mume wako akasema kila kitu kipo sawa, na,yeye atasimamia kama ilivyo..,..sasa pamoja na huo mkataba, eeh,..unajua nikuambie ukweli

mimi namfahamu sana mume wako mimi namtambua kama baba yangu mdogo, kwa jinsi familia yao na yetu zilivyokuwa karibu, na baba

yangu na mume wako walikuwa marafiki sana japokuwa baba yangu alikuwa mkubwa kwa mume wako.

‘Kwahiyo nilitarajia msaada mkubwa kutoka kwake, na kiukweli sikutaka mimi nifanye lolote kwa jinsi mkataba unavyosema bila ya ushauri

wake..na sio ushauri wake tu, ila kiukweli mimi sikutaka kabisa..nilimuambia uwanja huo mume wako, afanye anavyoona ni sahihi…’akatulia

‘Kiukweli kwa jinsi mkataba unavyosema kama sisi tungelikuwa ni watu wa tamaa, basi tungelifaidika sana na vitega uchumi mlivyo navyo

nyie..., maana sisi ni warithi halali wa baba na mkataba unasema wazi warithi wa mali yake ni nani,…kuna kumiliki hisa zake ndani ya

kampuni ya mume wako, na mume wako anadaiwa pesa nyingi na mkataba unasema hivyo, na ulibaisniha kuwa malipo ya deni hilo ni

kupewa hisa zaidi kwenye kampuni ya mume wako, na zaidi pia kuna mkataab mwingine kuwa marehemu anatakiwa kupewa hisia kwenye

kampuni yako, kwa kupitia kwa mume wako,....’akasema

‘Matapeli wakubwa nyie....Huo mkataba upo wapi?’ nikamuuliza hapo na nikagundua kuwa nimekiuka ushauri wa wakili, lakini hasira tena

‘Huna haja ya kukasirika, nikuambie tena, sisi hatuna nia mbaya na nyie,..na huo mkataba ninao, kila kitu kipo wazi....’akasema

‘Nautaka huo mkataba niuone kwanza...’nikamwambia.

‘Bado anao mwanasheria wetu, ....’akasema

‘Anao kwa ajili gani sasa?’ nikamuuliza

‘Kuna mambo bado hayajakaa sawa, na hili linatokana na mume wako, kama mume wako angelikubaliana na sisi, basi tungelishamalizana,

na kuhakikisha kuwa tatizo hili limekwisha kabisa,...’akasema

‘Mambo gani hayo mume wangu hajakubaliana na nyie?’ nikamuuliza

‘Kuna vipengele vingi vipo humo, vikionyesha kuwa mume wako ndiye anamiliki kampuni yake na yako kwa asilimia fulani za hisa, lakini

katika mkataba aliouacha baba , kuna kipengele walishindwa kukubaliana, kwa idadi ya hisa, kwa maana kuwa wewe kama mshirika,

hujaridhika...’akasema

‘Kipengele gani hicho?’ nikauliza

‘Kutokana na deni lilivyo, baba alitaka kumiliki zaidi ya aslimia hamsini ya hiza za kampuni ya mume wako, na pia kwa vile baba atakuwa

anamiliki zaidi ya asilimia hamsini yeye alitaka hata jina la kampuni libadilike....na hapo kukatokea sintofahamu, nahisi hata kifo cha baba

kilitokea siku walipokuwa wakibishana kuhusiana na hilo, japokuwa walikuja kukubaliana kuwa jina libakie hilo hilo...’akasema

‘Wewe umejuaje hayo, na wakati hukuwepo....?’ nikamuuliza

‘Baba alikuwa na kawaida ya kuhifadhi kumbukumbu za matukio yote, ..tulichokuja kuona ni ajabu ni kuwa mle ndani kwenye hicho chumba

ofisini kwa baba kulikuwa na kifaa cha kunasia matukio, lakini sehemu kubwa imefutwa, kwahiyo haikuweza kuonyesha tukio la kupigwa

risasi kwa baba, sehemu hiyo haipo, ina maana huyo muuaji, alirudi na kufuta sehemu hiyo, na ina maana kuwa huyo mtu anafahamu siri

nyingi za baba.

'Mimi ni mtaalamu sana wa komputa, nikafanya mambo yangu, nikagundua sehemu ndogo iliyofutwa, inayoonyesha jinsi ya kifo cha baba

kilivyokuwa, lakini kwa bahati mbaya sikuweza kuipata sura ya huyo muuaji, au umbile lake kwa ujumla zaidi ya kichwa kilichojitokeza na

mkono uliokuwa umshika bastola, ndio nikagundua kuwa aliuwawa na watu wake waliokuwa hawaelewani naye...’akasema

‘Ni watu gani hao?’ nikauliza

‘Imeshindikana kuwagundua ni akina nani, naomba iendelee kuwa hivyo, na kwa vile huyo muuaji hakuonekana sura, ...na alitokeza kidogo

tu, kiasi cha kuweza kulenga shabaha..na, kwa vile alikuwa kavaa kitu usoni, na kuacha macho tu,hata polisi hawajafahamu sehemu hiyo,

…’akasema

‘Ina maana polisi hawakupata hiyo video…?’ nikauliza

‘Polisi walipata sehemu hiyo ambayo haionyeshi lolote, ila mimi kwa vile ni mtaalamu , ndio nikagundua hiyo sehemu iliyokuwa imefutwa,…

lakini pia kuna kumbukumbu za baba nilizokuja kuzigundua zilikielezea watu mbali mbali, lakini hazielezei uhasimu wowote, ila kuna vitisho

vya hapa na pale,..ikiwemo wewe na wengineo, sasa nani ni nani..sikutaka kuendelea zaidi, hilo niliwaachia polisi.

‘Sasa ulipofanya utundu wako na kuligundua hilo, uliwafahamisha polisi?’ nikamuuliza

‘Hapana, na nina sababu za kutokufanya hivyo…’akasema, na kunifanya nishangae kidogo,

'Oh, kwanini...?' nikamuuliza

‘Kwasababu kuna sehemu inamuonyesha mume wako...'akasema na kunifanya nishtuke

'Mume wangu, kwa vipi...?' nikauliza

'Ndio mume wako yupo kwenye hiyo kumbukumbu ya video ya matukio, yaliyotokea siku ile,..., na polisi wangeliona hiyo sehemu mume

wako angelikuwa kwenye hatia, mtu mwenyewe mbovu, halafu ashikwe na kuwekwa ndani itakuwaje...niliona ni heri tu ibakie hivyo hivyo,

kwa vile sio yeye aliyefanya hayo mauaji…’akasema

‘Mimi sikuelewi hapo mume wangu… hapo kuna makosa, unajua kipindi hicho mume wangu alikuwa kalazwa hospitalini, anaumwa,

ataonekanaje kwenye hiyo video ya matukio, uliyoiona humo ndani, usije ukatumia ujanja wa kimtandao, na kumweka mume wangu…?’

nikauliza kwa mshangao

‘Siku huyo mume wako alikwenda kumuona baba, marehemu baba, ndivyo inavyoonyesha, sasa alifikaje na kwanini, hilo kwangu sio

muhimu, ila kwenye hiyo video ya matukio, mume wako alionekana akibishana na baba, ipo wazi kabisa, na walikuwa wakibishana kuhusu

mkataba…’akasema

‘Mkataba gani huo…?’ nikauliza.

‘Kuna mkataba wa hisa za kibiashara, nina Imani umeshalipata hilo kuwa baba ana hisa kwenye kampuni ya mume wako, na huo mkataba

ulikuwa unaelezea hayo…’akasema

‘Hebu samahani kidogo, kwanini baba yako awe na hisa kwenye kampuni ya mume wangu, na unafahamu wazi kuwa kampuni ya mume

wangu inatokana na wazazi wangu ndio wao walimpatia mume wangu mtaji…?’ nikauliza

‘Hiyo ni historia ndefu kidogo, ila hapo kwenye matukio, ilisikika marehemu akimuambia mume wako kuwa anadaiwa pesa nyingi tu na baba,

…’akasema

‘Pesa nyingi kiasi gani cha kupewa hisa nyingi hivyo, ni hayo malipo ya uwakili wake, kwani hayo malipo yalikuwa kiasi gani..?’ nikamuuliza.

‘Kama nilivyokuambia awali hiyo ni historia ndefu kidogo nahisi kuna zaidi ya hilo, na mume wako analijua zaidi,..ila mimi naongea kutokana

na ilivyosikika kwenye video, kuna maongezi kuwa mambo mengi kuhusu kampuni ya mume wako yalitokana na juhudi za marehemu baba,

na tangia awali baba aliwekeza kiasi cha hisa ndani ya kampuni hiyo kwa siri, sasa alitaka iwe bayana kwenye huo mkataba, sasa mpaka

kufikia kiasi hicho kikubwa cha hisa..hilo utamuuliza mume wako....’akasema.

‘Hapo sizani kama ninaweza kuelewa,..ni udanganyifu mkubwa tu huo, kampuni hiyo ilianzishwa kwa mkopo kutoka kwa wazazi wangu,na

mpaka leo huo mkopo haujalipwa sasa iweje marehemu ajiingizie huko,…lakini… anyway, endelea....’nikasema.

‘Siku ile mume wako, alifika kwa baba, alionekana ana haraka, na mashaka, na alionekana mwenye maumivi nahisi ni kutokana na

kujilazimisha kupanda ngazi au kitu kama hicho, sijui labda kuna mtu alimpatia msaada,... ila yaonyesha keshaingia amekaa kwenye kiti

wanatoleana mikataba..’akasema

‘Je mumeshaongea na mume wangu kuhusu hayo uliyoyagundua, kuwa wewe unayafahamu hayo yote..?’ nikauliza

‘Anafahamu kama ilivyo kwenye mikataba, lakini hafahamu kuwa mimi nimegundua kilichotokea siku ile baba alipouwawa..hilo

sijamuambia,… ...haya hayafahamu mume wako na mpaka leo nikimuuliza kuwa aliwahi kuonana na baba siku ile ya tukio,

ananikatalia,...kwahiyo yeye hayajui kama walivyo polisi, nimeona nisimuambie…’akasema

‘Kwanini…?’ nikauliza

‘Mume wako hana tofauti na baba kwa tabia zao, za tamaa ya mali, bila kujali uhalisia wake, iwe dhuluma au halali kwao ni sawa,

nawafahamu sana kwa hilo, na sisi hatutaki kuwa miongoni mwa hilo, na nina amani kama tungelimuambia angetukataza kabisa kuliongelea

hilo kwako, sis hatutaki uhasama, sisi tunataka kulimaliza hili kwa njia ya heri…’akasema na sikumuelewa hapo lakini nikaona nisubiria

kwanza, nikasema

‘Ehe ilikuwaje sasa maana hapa unaongea wewe, siwezi nikakuamini mpaka nione huo ushahidi…’nikasema

‘Nitakuonyesha kila kitu madam, ila mpaka huo muda ukifika…’akasema

‘Muda gani…ukifika..?’ nikauliza sasa kwa mashaka

‘Ngoja kwanza nikuelezee ilivyokuwa, au hutakii kujua zaidi…’akasema

‘Haya elezea…’nikasema

‘Basi mume wako alipofika wakaanza kuongea, na nahisi siku hiyo walipanga iwe ni kuhitimisha makubaliano yao, nahisi kuna mambo

yalikuwa hayajawa sawa kwani kuna sehemu marehemu alimuulizia je mke wako kakubali, na mume wako akasema haina shida, yeye tu

anatosha, kwa vile mkataba upo wazi, na kukawa na kubishana kwa hilo na baadae marehemu akasema…’a hapo akautulia kidogo

‘Pamoja na hili kuna mambo ya kibenki, hayo hatuna ujanja nayo je una uhakika utaweza kumshawishi mke wako..na mume wako akasema,

muda utasema kwanza wamalizane na hilo la mikataba,....’ hiyo ilikuwa ni kauli ya marehemu na mume wako, ipo wazi...

‘Sasa kuna mambo mengi walijadiliana hapo, hayo utakuja kumuulizia mume wako, lakini nakuomba kwa hili nililokuambia usimuambie

kwanza mume wako, utakuja kuharibu kila kitu…muhimu kwako kufahamu ni kuwa mume wako baadae waliwekeana sahihi rasmi kuwa hisa

za marehemu zitakuwa kiasi gani, na za mume wako kiasi gani, ni unu kwa marehemu na iliyobakia sehemu ni yako na ya mume wako,

kama minajili jhiyo baba anakuwa ana hisa kubwa zaidi na anakuwa maamuzi zaidi, hapo sijui ni kwanini..’akasema

‘Mhh,hayo yote yanaonekana kwenye hiyo video…?’ nikauliza

‘Ndio…kila kitu kipo wazi, lakini hayo hayaonekani kwenye ushahidi walio nao polisi..sijui kama wana utaalamu kama niliufanya mimi hadi

kuligundua hilo na kama wangelikuwa nao basi mume wange angelishakamatwa, au sio…’akasema

‘Hiyo video sio ya kugushi kweli…?’ nikauliza

‘Kuna vitu vya kugushi,…madam,.. lakini sio vitu kama hivyo, unaweza kwenda kwa wataalamu wakakuthibitishia hilo, lakini naomba hili

liendelee kuwa siri kati yangu mimi na wewe…’akasema

‘Sawa endelea…’nikasema

‘Basi, walipomaliza, na wakati wanapeana mikono ya kuagana, ndio hapo tukio la mauaji likajitokeza…’hapo akatulia kidogo

‘Mara mlango ulifunguliwa kwa ghafla…lakini mtu hakujitokeza, marehemu akawa anauliza wewe ni nani… na mtu aliyekuwa kajifunika

sehemu zote za usoni,akajitokeza kichwa tu usingeliweza kuiona sura yake, na hapo hapo akampiga baba risasi, kifuani kwenye moyo, na

baba akaguna na kuwea kichwa mezani, nahisi alifariki hapo hapo..’akatulia kidogo.

‘Kwanini sasa usiwape polisi huo ushahidi ni muhimu sana kwangu, maana mpaka sasa sijasafisha jina langu kuwa mimi sihusiki na mauaji

hayo…’nikasema

‘Watu hao walitaka kumuua na mume wako…lakini wakati huyo muuaji anataka kufanya hivyo, ikasikika sauti ya mtu akiita kwa nje, kuwa

waondoke wapo kwenye hatari ya kukamatwa, ndio hapo mlango ukafungika, lakini kidogo hapo, kabla ya kuondoka, huyo muuaji alirusha

hiyo bastola kwa ndani....’akasema

‘Ikawaje maana mume wangu alikuwa humo ndani …?’ nikauliza

‘Ukiangalia hiyo sehemu utaona vyema jinsi gani mume wako alivyochanganyikiwa, kuonyesha kuwa hakuwa anafahamu hilo tendo, labda

kama alihusika,...maana ungelisema labda ni mtu wake, aliyempanga kuja kufanya hivyo, lakini utajiuliza kwanini..ili iweje,…na ukiangalia

ilivyo, utaona kabisa mume wako hakuhusika, alicvhanganyikiwa, akawa anahangaika huku na kule..na kama ni yeye, basi angeliondoka na

hiyo mikataba, lakini hakukumbuka kuichukua wakati anatoka kukimbia…’akasema.

‘Bado hapo …’nikasema

‘Ni hivi huyo jamaa alitokeza kichwa, na mara ikasikika tufu tufu…risisi zikimpiga marehemu, yeye akainama na kuweka mikono usoni

hivi..yaani kichwa kakilanza mezani huku kaweka mikono kuzuia machoni,…, kama vile mtu anavyoogopa kupigwa na yeye,

Alikaa hivyo kwa muda hadi hao watu walipoondoka..baadae ndio mume wako akainua kichwa taratibu, halafu akageuka kuangalia

mlangoni, akajihakikishia kuwa yupo salama, sasa ndio akamtizama marehemu akagundua kuwa marehemu keshafariki..

‘Utaona jinsi gani alivyochanganyikiwa, akawa anahangaika, akishindwa afanye nini...baadaye, sijui alijiwa na wazo gani, akafungua

mlango, na kutoka nje, hapo alikuwa akitembea kwa shida sana, ni kama alitojitonesha au hali..inaonekana hivyo,...huwezi kuona kitu nje ya

chumba, sasa sijui alivyoweza kutembea hadi kutoka eneo hilo…’akasema.

‘Kwahiyo wewe unasema sura ya huyo muuaji haikuonekana, na huyo mtu alitaka kumuua pia mume wangu, inaonyesha hivyo, na

inaonyesha kweli kuwa mume wangu hahusiki au sio…na huyo mtu hajulikani kuwa ni mwanamke au ni mwanaume?’ nikauliza

‘Haonekani, huwezi kufahamu...'akasema

‘Bado mimi najiuliza ni kwanini usiwaonyeshe polisi, maana ingewasaidia kujua zaidi?’ nikamuuliza.

‘Tunafuata maagizo ya marehemu baba, licha ya kuwa sikuwa na mahusiano mema na yeye, lakini nakumbuka jinsi alivyokuwa akiniambia

kuwa kwa vyovyote itakavyo kuwa awe hai au mzima, mume wako nimuheshimu kama baba yangu mdogo, kwani amewahi kumsaidia sana

katika maisha yake na sisi tumlinde na kumsaidia..’akasema

‘Ok…’nikasema hivyo

‘Na ..hata mimi alinisaidia sana mume wako nikiwa mdogo..na alimsaidia sana mama, kipindi mama alikuwa anaumwa sana, hana pesa,

yeye alijitolea kuuza mbuzi wake, aliyekuwa naye, mmoja, kwa ajili ya kumtibia mama,...mimi nilimwahidi baba kuwa mume wako atakuwa

baba yangu mdogo, na sitaweza kumvunjia heshima. Hili niliahdi na ndio maana nayafanya haya…’akasema

‘Sijakuelewa hapo, ina maana hata kama itaonekana kuwa yeye ni mhalfu, utamtetea tu, na huenda akahusika na kifo cha baba yako?’

nikamuuliza.

‘Mume wako hahusiki na kifo cha baba yangu, hilo nina uhakika nalo...usuhuba wao ni wahali ya juu, kifo cha baba kimemuumiza sana

mume wako, ..wewe hujui tu, marehemu baba alikuwa ndiye kichwa cha mume wako, kila uliloliona mume wako akilitenda lenye tija…, mara

nyingi, alikuwa akifuata ushauri wa baba...’akasema.

‘Hata kuzaa nje ya ndoa?’ nikamuuliza

‘Kuzaa nje ya ndoa…haaah, nani kasema?!’ akauliza kwa mshangao kidogo

‘Unajifanya hulijui hilo…kama kweli yote aliyokuwa akiyafanya baba yako kuwa anaweka kumbukumbu nina Imani hata hilo lipo, au sio…?’

nikauliza

‘Kuna mambo mengi nimeyagundua ya baba, lakini hilo,...mmh...lakini nikuambie kitu, nataka haya tuje kuyamaliza...kuna mambo mengine

siwezi kukuelezea kwa sasa mpaka hapo tutakapokuja kukubaliana, ndio maana nimekuja na maombi yangu kwako...’akasema

‘Maombi gani?’ nikamuuliza

‘Kwanza na lenye muhimu nakuonmba umsikilize mume wako...mkubaliane naye..mkisha kubaliana naye , mkawa kitu kimoja,basi sisi

tutajitoa kabisa kwenye huo mkataba ulioandaliwa kuwa baba alikuwa na hisa, hatutaki hizo hisa, lakini huwezi kuziondoa kihivi hivi, ni

mambo ya kisheria au sio, ...’akasema

‘Hahaha..nilijua tu…’nikasema

‘Ninasema hivyo kwa moyo safi , nielewe madam..., sina shida na mali zenu kabisa, hatuna shida na mali za dhuluma…ila mimi nina deni

kwenu, maana kama kuna pesa zilitoka kwenu, zikanisaidia mimi, natakiwa nifanye lolote kulipa fadhila au sio..sasa furaha yangu ni kuona

wewe na mume wako mnaishi vyema.

'Hilo halikuhusu au..kwanini unataka kuingilia ndoa yanu...?' nikamuuliza

‘Kwa kifupi madam, sisi hatutaki kujihusisha na ndoa yako au mali zenu, hatutaki kupata mali isiyo halali,...lakini tunahitajika kumsaidia

mume wako, kwani ...wema wake kwetu ni mkubwa sana, ndio mume wako ana tabia kama hizo..., lakini ni mwepesi kujirudi, nampenda

sana kwa hilo, sio kama baba, baba alikuwa haambiliki, sasa tunakuomba umsaidie mume wako, nina Imani atajirudi na mambo yenu

yatakuwa sawa,...hata ukiongea na mama atakuambia hilo…’akasema.

'Mama yako sio...yupo...?' nikauliza

'Yupo ndio, kaja kwa ajili ya huo msiba, wapo wanafamilia karibu wote...'akasema

Mimi hapo kwanza nikatabasamu moyoni nilihisi kupata jambo la kunipa faraja, japokuwa bado nilikuwa sijawa na uhakika, maana hayo ni

maongezi tu, ushahidi upo wapi,..nikajaribu kumuangalia huyo jamaa usoni kwa makini sana, kama nilivyokuambia sio rahisi kumtambua

huyu mtu hisia zake kupitia usoni je ni mkweli au ni muongo, na baadae nikasema;

‘Naweza kuonana na mama yako.....nataka niongee naye ?’

‘Kuonana na mama yangu sio tatizo na mkiongea naye atakuuliza kama umekubaliana na mimi, na mimi ndiye muamuzi..sasa nataka kauli

yako kuhusu ombi langu, je upo tayari kushirikiana nasi ili tulimalize hili jambo, ni muhimu sana kwangu?’ akauliza.

‘Kwanza nataka niongee na mama yako…..’nikasema, na mara gari la mume wangu likafika, nilimuona yupo na mtu ndani ya gari,

nikagundua kuwa ni wakili wake.


NB: Inatosha kwa leo



WAZO LA LEO: Urafiki ni mzuri, unajenga mahusiano mema, lakini tujaribu kuangalia aina gani ya marafiki zetu,kuna marafiki wengine

wanaweza wakawa ni sumu ya maisha yatu, kutokana na tabia na matendo yao..utawafahamu kutokana na hulka na matendo yao, hao sio

marafiki, hata kama mumeshibana vipi,…ikiwezekana ni bora utengane nao kabisa, kwani ukiungana nao, hata kama hutafanya

wanachokifanya wao, lakini ubaya wao unaweza kukuleta matatizo kwani ukikaa na muuza uturi, utanukia uturi....au sio?
 
SEHEMU YA 70



Mtoto wa marehemu alionekana mtu mwema kwangu…, na alikuwa tayari kuniambia mengi ambayo huenda yangelifanikisha malengo yangu,

ya kutaka kujua ni kitu gani kinachoendelea, kitu gani kilichoweza kumbadilisha mume kiasi hicho..na je ni kweli ana mtoto nje ya ndoa..huo

kwangu ungelikuwa ni ushahidi mkubwa sana...tatizo huyu mtoto wa marehemu akatoa sharti ambalo lilinipa wakati mgumu kulikubali,

Sio kwamba simpendi mume wangu, sio kwamba…simuamini, lakini kama ni kweli kayaafanya hayo ninayoyasikia, na kavunja mkataba, je

haiwezi ikawa ndio njia, na sababu ya kutenda mengine makubwa zaidi ya hayo.....na je nikikubaliana naye si ndio sababu ya kupoteza mali

na juhudi zangu zote, je wazazi watanielewa kweli….

‘Nataka umsikilize mume wako..mkubaliane naye..mkisha kubaliana naye , mkawa kitu kimoja,basi sisi tutajitoa kabisa kwenye huo mkataba

ulioandaliwa, mkataba huo ulionyesha kuwa baba ana hisa kwenye kampuni zako, ...’

‘Naweza kuonana na mama yako.....?’ nilimuomba hivyo..akili ikiwa imechanganywa na sharti hilo....

Endelea na kisa chetu.......

Mara mume wangu akaja na gari lake, na ndani ya hilo gari alikuwepo mtu mwingine alikuwa ni wakili wake, walifika na hawakutaka hata

kutusalimia, wakaingia ndani,..na mimi sikutaka kuwafuata, japokuwa ni adabu mgeni alifika umkaribishe, lakini kwa hali ilivyokuwa, ..sikujali

tena….

‘Mume wako anaonekana hayupo vizuri…’akasema

‘Ni kawaida ..nahisi ni majukumu ya kazini kwake, ila sijui kwanini kamleta huyo wakili hapa nyumbani, ..kama watanihitajia

wataniita..’nikasema

‘Yah….basi…kama haupo tayari, mama anaweza kuja wakati mwingine..’akasema

‘Kwanini, …nipo tayari,..hao wana mazungumzo yao, hayawezi kuzuia hili, kama wangenihitajia wangeniambia..si umeona..hawakutaka hata

kusalimia, ina maana wana mazungumzo yao binafsi…’nikasema

‘Sawa…kiukweli mama, atashukuru sana kuongea na wewe, kwani hata yeye alikuwa na hamu sana ya kuonana na wewe, lakini kweney

haya, yeye hana zaidi ya kuamua, zaidi ya yote ananitegemea mimi, yeye ni muwekezaji tu wa huko kijijini ...’akasema.

‘Kwanini alitaka kuonana na mimi, ni kuhusu mambo hayo hayo…?’ nikamuuliza

‘Pamoja na hayo yaliyotokea, yeye alishasikia sifa zako, za uchapa kazi wako, na kwa vile yeye ni mjasiriamali, alikuwa na hamu sana ya

kuonana na mtu kama wewe, ajifunze mengi kutoka kwako, na ni muongeaji, atakusimulia mengi ambayo hata hukuyaka kuyafahamu, uwe

mvumilivu tu...’akasema.

‘Kwani mama yako huko kijijini anafanya kazi gani hasa?’ nikamuuliza

‘Amejiajiri, ana miradi yake, ni mmoja wa viongozi wa akina mama, na hamu yake kubwa ni kuja kuwekeza hapa Dar kama itawezekana,

lakini sio rahisi kama ujuavyo, gharama, masomo …, lakini hiyo ni mipango ya baadaye...’akasema.

‘Nahisi kwa mtizamo wangu, mumepanga kufanya hivyo kwa urithi wa baba yako, au sio..na baba yako ana vitega uchumi vingi, nasikia ana

nyumba zaidi ya tano, .....?’nikauliza.

‘Nyumba zote tumepiga mnada, kwa ajili ya kulipa watu, waliopata madhara kutokana na mambo yake, ...sisi kama sisi, hatutaki chochote

kutoka kwake,mali zake na miradi yake, kwetu sio muhimu, muhimu ni kulisafisha jina lake ili mungu amsamehe makosa yake,..’akasema.

‘Mnaonekana hamtaki ubaya wa baba yenu uwangilie na nyie au ni mbinu tu za kuataka kunihadaa, kiukweli mimi siwaamini, nikuambie

ukweli kutoka moyoni mwangu, yaliyonikuta…yamenipa fundisho?’ nikauliza

‘Ndivyo tunavyotaka, lakini watu wengine wanaonekana kutokutuamini, sioni ajabu na wewe ukisema hivyo, lakini dhamira yetu ipo pale

pale, hata kama hamtatuamini sisi tutafanya yale tunayoona ni sahihi, tukimaliza hayo, basi wale wenye nia njema na sisi watatuamini

tu...’akasema

‘Mimi sina ubaya na nyie, kama kweli mna nia hiyo njema, ila sitaki mtu kuniingilia kwenye mambo yangu, ....baba yenu alianza hivyo,

akajitahidi, na nilimkanya sana, bado hakuchoka, akatafuta mbinu mpaka akaweza kuingia kwenye mambo yangu hata bila ya mimi

kufahamu..kama kweli mna nia njema mumeliona hilo, lakini nina iamni kuwa sio yeye, kuna mtu anamtumia…’nikamwambia.

‘Hayo mimi siyaamini sana, kuwa kuna mwanasiasa anamtumia, hapana,..mimi namfahamu baba, ni hulka yake, sawa anaweza kuwa

anatumiwa, lakini yeye si ana akili….sijui lakini, maana huko mimi sija..paangalia sana..’akasema

‘Sawa pamoja na sharti lako hilo, ambalo mimi kwangu ni gumu, na mimi nina sharti langu, kama tutakubaliana, basi nitajua na nyie mpo na

nia njema,…’nikasema

‘Sharti gani,…niambie tu , maana nia yetu ni kujenga…’akasema

‘Ili kweli niwaone kuwa hampo nyuma yake, na hamna nia njema, nawataka kwanza, nipate mkataba wangu, upo mkataba wangu wa asili

kati yangu na mume wangu, baba yako aliuchukua, akaugushi na kutengeneza mkataba huo ambao mnao sasa…yeye aliyeubadili, na najua

kabisa anao, ule wa asili, sasa nipeni huo, ....’nikasema na yeye akanikatiza kwa kusema;

‘Sisi hatujui lolote kuhusu mkataba wenu wa asili, na hatuna haja nao, sisi mkataba tulioupata ambao hata wakili wetu anaufanyia kazo ndio

huo, unaoonyesha kuwepo kwa hisa za baba kwenye kampuni zenu, na ndio maana kwanza tulitaka kulithibitisha hilo, …’akasema

‘Mtathibitishaje, kwasababu kulithibitisha hilo ni kuwaona wahusika, je mumelifanya hilo…?’ nikamuuliza

‘Ndio…tumeongea na mume wako, amelithibitisha hilo...ila alisema kuwa hiyo ya umiliki wa hisa zaidi ya nusu, ya hisa, haikuwa ni hiari yake,

..kulikuwa na shinikizo fulani kwake, juu ya uwezo wake,, ila yeye alikubali tu ili mambo yaishe..na tukamuuliza ni shinikizo gani..’akasema.

‘Je yeye aliweza kuwaambia ni kutokana na shinikizo gani?’ nikamuuliza

‘Hakutaka kusema ni shinikizo gani, lakini kwa vile tunamfahamu baba, kuwa akiwa anatafuta kitu, hasa mali, hajali aliyepo mbele yake,

hatukutegemea kuwa watafikia hatua ya kushinikizana kiasi hicho, kwani haiingii akilini, mume wako akubali kumpa nusu ya hisa baba, kwa

sababu ya deni, na ni kweli madeni yapo..kuna hati hizo,..lakini kwanini kuwe na shinikio..madeni ni madeni au sio…sasa ni nini, sisi

hatukutaka kumlazimisha mume wake atuambie...’akasema.

‘Wewe hukugundua ni kitu gani, si ulisema ulifanya uchunguzi wako au sio…?’ nikamuuliza.

‘Hapana, sisi hatukutaka kuingilia huko kwa undani zaidi, ili iweje, kwani tunataak nini, …mmh, mimi naona yale niliyotaka kukuambia kwa

sasa yanatosha, na kwa vile unataka kuongea na mama, ngoja nikamuite, muongee naye, nitamsubiria kwenye gari...na mume wako naona

anaongea na wakili wake, sijui watanihitajia au la..nisingelipenda kuongea naye kwa leo…’akasema

‘Ina maana mumekuja na mama yako kumbe mbona hukuingia naye..yupo wapi…!?’ nikamuuliza kwa mshangao.

‘Tulikuwa naye, alikuwa na mambo yake, nikamwambia napitia kwako kwanza kujaribu kama utakubali kuongea na mimi, na yeye akawa

anawasiliana na wateja wake kwenye simu, nikamuacha nje kwenye gari, yeye muda wote ni kuongea an simu, si unajua ujasiriamali

ulivyo...’akasema

‘Sawa nitafurahi nikiongea naye, na samahani sana, kama sitaweza kukubaliana na ombi lenu, nalisema hili mapema, uelewe msimamo

wangu, muhimu ni mkataba wangu wa awali, huo ndio utakuwa ufunguo wa makubaliano mengine bila huo, sizani kama tutaweza kukaa

meza moja na mume wangu...’nikasema.

‘Hamna shada, ..nimefurahi sana kuongea na wewe nahii iwe ni mwanzo tu wa mazunguzmo yetu, na nina imani tutashirikiana kulimaliza hili

jambo…na kama upo huo mkataba mwingine, kwanini usitolewe..usijali tutalimaliza hilo…haya ngoja mimi nikamuite mama aje muongee

naye..’akasema na kusimama, tukashikana mkono, na akaondoka na kuniacha nikiwa nimesimama nikimwangalia anavyoondoka.

**********

Mke wa marehemu alikuwa wale akina mama wahangaikaji, wake wa shoka, hata jinsi alivyokuwa akitembea kuja pale nilipokaa alionekana

,mama mchapakazi kweli,...mwendo wake sio ule wa kike kike wa kutembea kimikogo, anatembea kama mwanajeshi

Alipofika pale nilipokaa mimi nikasimama kwa adabu na kwanza , akasimama hatua chache kutoka pale niliposimama, kwanza akaniangalia

kama ananikagua, halafu akanisogelea tukakumbatiana, na kusalimiana.

‘Siamini kama ni wewe..’akasema

‘Kwa vipi dada...?’ nikamuuliza

‘Unafahamu, nimeziona picha zako kwenye magazeti tu, kwenye majirida mbali mbali yakitangaza biashara zako, ..lakini unavyoonekana

kwenye picha, sio sawa na nilivyokuona leo, leo upo kihalisia zaidi...’akasema

‘Kwani leo nipo vipi na huko kwenye magazeti naonekana vipi?’ nikamuuliza kwa mshangao kidogo

‘Tuyaache hayo, maana sisi akina mama tukikutana mengi tutakayoanza kuzungumzia,ni mavazi, muonekano , sura, hata tutasahau jambo

muhimu, na majukumu ya kila siku, mimi siku hizi sitaki kupoteza muda tena, na tangu nije hapa Dar, naona napoteza muda wangu bure tu

na mambo yasiyonisaidia kitu...’akasema huku akikaa kwenye kiti.

Akaletewa kinywaji, na matunda…akapiga mafundo mawili, halafu akainua uso na kuniangalia, akasema;

‘Haya niambie kulikoni, hivi Samahani kidogo, hivi wewe na mume wako mna matatizo gani?’ akakimbilia kuniuliza hilo swali. Na kunifanya

niingiwe ni tahayari kidogo

‘Mhh, kwanini…oh, kwanza nikupe pole za msiba wa mumeo,maana hatujaweza kukutana kwa sababu ya haya mambo yanayoendelea kwa

sasa, pili sio kweli kama watu wanavyodai kuwa eti mimi ndiye nimemuua mume wako…, kwanini mimi nimuue mume wako..’nikasema.

‘Ni kweli kibinadamu, hisia hizo zipo, japokuwa mimi na mume wangu tulikuwa mbali sana, huwezi amini hilo, nimeishi kama sina mume,

lakini ki ndoa yeye ni mume wangu eeh…,siwezi kumkataa hadi kesho, japokuwa sasa ni marehemu..ila hutaamini yeye, kwa kauli yake,

alishanifanya mimi sio mke wake....inasikitisha…’hapo akatulia kidogo.

‘Kwahiyo mlishatalikiana au..?’ nikamuuliza

‘Hamna talaka,..mimi sikukubaliana na hilo, …, kwahiyo bado alikuwa ni mume wangu, ndio maana sasa nimepewa cheo cha mjane, na hata

kwenye mirathi yake sikuamini,kuona na mimi nipo kwenye orodha ya warithi,…ni ajabu kabisa, alikumbuka kuniweka nahisi hili kalifanya

baade sana, sijui ni nani kamshawishi kufanya hivyo..hata hivyo kinafsi yangu, sikutaka chochote kutoka kwake,…mengine tuseme yote ni

mapenzi ya mungu..’akasema akionyesha huzuni.

‘Je wewe ulikuwa ukimpenda mume wako?’ nikajikuta nikimuuliza hivyo.

‘Sana tu...huwezi amini, mimi nilikuwa nampenda sana mume wangu, na nikuambie ukweli,..hili watu hawalifahamu na hata mume wangu

akitoa kauli zake hizo za kuwa hanitambui kama mke wake..alikuwa akisema hivyo akiwa kalewa tu…kuwa mimi ndiye niliyemtaka yeye…awe

mume wangu...’akasema na kunifanya niingiwe na hamu ya kuyafahamu maisha yao.

‘Hebu niambie ina maana wewe ndiye uliyemtongoza mume wako…au kwanini alikuwa akisema hivyo…, nisamehe kwa kuuliza haya, maana

imenipa hamasa tu ya kufahamu…?’nikamuuliza

‘Hahaha, ndio hivyo, siwezi kulipinga hivyo..lakini sio kwamba alikuwa hanipendi, kihivyo, hapana, kipindi hicho tulikuwa kwenye ushindani

wa kumpata yeye, unajua tena kijijini, na sisi tulijiona wasomi fulani..hivi, tukiwa darasa la sita, mwili na sura vilitudanganya…’akatabasamu.

‘Kulikuwa na kundi la mabint warembo wa hapo shuleni na kijini, nikiwemo mimi..unasikia…sasa, unajua tena, naongea haya..aah....tulikuwa

mabinti watatu, warembo…kila mmoja anataka yeye ndiye ampate huyo mwanaume, kipindi hicho yeye ni kijana mtanashari eeh, na ana

majigambo fulani, kiingereza mdomoni hakimtoki, ..’akatulia.

‘Mrembo..?’ nikauliza na yeye akacheka, halafu akasema

‘Kijijini bwana,..mwanaume akionekana msomi, kiingereza kingi…si unajua tena, huyu jamaa alikuwa msomo, kiukweli…na …ndio hivyo..basi

bwana, sisi ni mabinti wadogo warembo wa hapo kijijini...ilikuwa hapatoshi, kushindana ni nani atachukuliwa na huyo msomo,..hahaha,

..lakini ndio hivyo, mwisho wa siku nikasimama mimi kidedea, ..tukawa wapenzi, japokuwa ni upenzi wa kijijini...’akasema.

‘Hongera, ...’nikasema

‘Unafahamu, mimi tangu nikiwa mtoto, nililelewa kwa shida, sikuwahi kupata raha, ...wazazi wangu hawakunidekeza, hawakuwa na kitu,

kwahiyo ilikuwa ni maisha ya suluba, ..kula na kulala kwa shida, ..unajua maisha tena ya kijijini..basi ikatokea nikamfahamu huyo

mwanaume…, kiajabu ajabu tu..’akasema huku akitabasamu.

‘Yeye nakumbuka tangu nimfahamu, alikuwa ni mtu wa kusoma vitabu tu...hata alipokuja huku mjini, na baaadaye akawa anafika fika,

alikuwa muda mwingi ukimuona kashikilia kitabu, hivi vitabu vya hadithi, alikuwa anapenda sana kusoma vitabu vya kizungu, nakumbuka

kuna vitabu vyake, aliwahi kunionyesha, hata mimi baadaye nilipojiendeleza nimekuwa nikivisoma, hivi vinaitwa, eeh, Jemsi Hadley Chase,

na Peri Masoni, nahisi ndio maana akajikita kwenye uanasheria...’akasema.

‘Siku ya kwanza kukutana kwetu, ilikuwa kama vile wanavyoonyesha kwenye sinema, maana ilikuwa ni kwenye shughuli, mimi nilikuwa

kasichana, na bahati mbaya mwili wangu ulikuwa haraka, ni baadhi ya wasichana kijijini kwetu tuliokuwa kimwili haraka, ...ilikuwa siku hiyo

nafanya usafi kuwaandalia wageni, mara wakati nawapelekea watu maji ya kunywa, nikagongana naye, ..akadondosha kitabu chake,

kikalowana maji...maana kulikuwa na maji maji sakafuni, mimi nikakiokota na kukifuta kwa kitambaa changu cha mtandio. Picha ndio ilianzia

hapo…

Nilipomaliza nikamkabidhi kitabu chake, kumbe mwenzangu wakati wote huo nahangaika kukifuta kile kitabu, alikuwa akinitizama, na hata

namkabidhi hicho kitabu, bado alikuwa akinitizama tu machoni....hapo mimi bado mbichi nasoma, vititi saa sita..’akasema.

Nilishamuona kabla, na tulikuwa tukimuongelea shuleni, wasichana na tama zetu…lakini hilo la kukutana kihivyo, ilikuwa siku hiyo, na ndio

nikaweza kujuana naye, na kuanza kujenga urafiki, na urafiki ukatibua nyongo…’akatulia

‘Kwa vipi…?’ nikauliza

‘Alinibebesha mimba..na kunifanya nifukuzwe nyumbani kwa wazazi wangu..’akasema

‘Mungu wangu…’nikasema hivyo

‘Nilikwenda kuishi kwa bibi, mpaka nikajifungua...hebu fikiria, darasa la sita enzi hizo, unabebeshwa mimba,hata darasa la saba sikumaliza,

ingawaje baadaye nikijisomesha, kujiendeleza,…usinione hivi , nilijisomesha hadi sekondari, kiaina aina.

‘Basi aliponipa mimba, wazazi wangu wakafahamu, palikuwa hapatoshi jamaa huyo akakimbilia mjini, sio kweli kuwa alikuja huku mjini kwa

ajili ya masomo, hapana,..ni lugha ya kudanganya , kuficha ukweli, yeye alikimbia kuogopa balaa la wazazi wangu....’akasema

‘Lakini umesema yeye anasema ni wewe ndiye uliyemtongoza, naona hapo inaonyesha yeye alikupenda pendo la awali,...au sio, lile pendo

watu mnaonana hapo hapo, kunajengeka hisia za kupendana au sio...’nikasema.

‘Baada ya pale,…kwenye shughuli… siunajau tena mambo ya shule, nikawahadithia wenzangu, basi, marafiki zangu kila mmoja akataka

ampate yeye, na kila mmoja akawa anajibaragua kwake, kijinsi ajuavyo yeye, mimi ikaniuma sana, wivu tena… ina maana kuwaelezea

wenzangu ndio imekuwa nongwa..basi nikaona nisilaze damu, ...’akasema.

‘Nilipoona wenzangu wanambana sana huyo kijana, kila mara wapo naye, nikaamua kumwambia ukweli, ilikuwa ni kazi nzito kujielezea si

unajua tena wasichana…, lakini mwisho wa siku alikubali kuwa hata yeye ananipenda sana tangu siku ile kwenye shughuli, ya kudondosha

kitabu,...mambo yakakolea sasa kuanzia hapo, ikawa mimi na yeye, nikawa nachapwa nyumbani kwa ajili yake, sikusikia,...haniambii

mtu...na asiyesikia la mkuu huvunjika mguu...ikatokea kama mchezo tu, mimba hiyo...’akatulia.

‘Kiukweli mimba ilikuwa ni bahati mbaya, maana pamoja na urafiki wetu huo, hatukuwa na mambo ya kisasa, haya ya kimjini mjini,

hapana...ilikuwa ni kukaa pamoja kuongea, kutaniana, kukimbizana,...ila siku hiyo sikumbuki ni kitu gani kilitokea, na tukajikuta tumefanya

jambo ambalo ndilo lilimleta huyu mtoto wangu duniani, mliyetoka kuongea naye....’akatulia kidogo.

‘Nilitenda hilo mara moja, na ikawa ndio tiketi ya shida, ...shida kweli...na nikuambie ukweli, mtoto huyo alinitesa kweli kweli…ilikuwa ni

mimba ya fundisho, na sikutaka kuzaa tena..licha ya mimba yake, na hata malezi yake…, nilimlea kwa shida sana, huwezi amini. Siwezi hata

kukusimulia, ....hata hivyo.. mungu hakunitupa mja wake, mateso hayo yalinijenga..nikawa mke-dume, aliyejengeka kijasiri, unaniona nilivyo

hata kutembea kwangu..na nilitaka mtoto wangu awe hivyo hivyo, sikupenda awe mtoto wa ovyo ovyo, nilijitahidi kumlea kihali niliyoona ni

njema kwake..’akasema.

‘Ina maana ulipomzaa huyo mtoto, hukupata msaada kutoka kwa mume wako?’ nikamuuliza.

‘Msaada gani, angelipata wapi pesa za kunisaidia wakati huo, wakati huo wa awali, yeye mwenyewe alikuwa kula kulala..hana mbele wala

nyuma, na aliponipa mimba akakimbilia mjini kujificha, hakuonekana, hadi nilipojifungua na alifika kwa mara ya kwanza mtoto

anatembea,hamjui ,.....na sikutaka hata kuongea naye..’akasema.

‘Ikawaje sasa mpaka mkafunga ndoa?’ nikamuuliza

‘Wazazi wangu waliweka shinikizo..kuwa ni lazima anioe...huoni , hata nikiwa naye naonekana mimi ni mkubwa kuliko yeye, lakini ni

kwasababu ya maisha, na mwanamke mara nyingi anaonekana mkubwa, kama mkiwa umri karibu sawa..sisi wanawake tunakuwa haraka

haraka, na ukizaa ndio basi tena...’akasema.

‘Basi ikabidi kweli anioe, kuepusha shari, japokuwa hakutaka, alishaniona sifai tena..japokuwa mimi nilikuwa nampenda kweli kweli,...hata

tulipoona hatukuweza kuishi kwa upendo, ilionekana kama ndoa ya lazima, akawa ananinyanyasa, ...yaani sikuwa na raha na yeye, na

hakutaka hata kutembea na mimi, yaani kutembee mitaani kama mke na mume, haikuwahi kutokea....aliniona simfai, mwanamke wa kijijini,

mshamba, asiyejua kujiremba...na yeye keshakulia mjini, anawafahamu warembo wa mjini, eeh..’akasema akibenua mdomo kwa dharau.

‘Basi bwana, ..mimi nikawa mama wa kijijini, sikujali, bado nilimtambua yeye kama mume wangu, yeye akawa anishi mjini , mimi kijijini,

sikujali, nikawa napigika kijijini, maisha ya shida, anakuja mara moja au mbili kwa mwaka, ..hanitumii pesa, akibahatisha ni mara moja kwa

miezi mitatu, ni pesa yenyewe pesa basi, nikawa nahangaika kivyangu kumlea mwanangu, sikujali na wala sikukata tamaa...’akasema.

‘Nikawa naletewa taarifa za ajabu ajabu kutoka huko mjini, kuwa mume wangu ana wanawake, sio mwanamke, ana wanawake, anawabadili

kama nguo...ikafika mahali nikamuuliza, na kumshitaki kwa wazee, nilivyosikia, hutaamini kibao kiligeukia kwangu, kuwa mimi nasikiliza

majungu, ni wapi nilimuona na hawo wanawake,...iliniuma sana, kwani mmoja wa wanawake zake, namfahamu, alikuja kuniambia yeye

mwenyewe, kuwa mimi nitabakia huko kijijini yeye atakuwa akistarehe na huyo mume wangu, eti sababu mimi nilimuibia yeye...’akasema.

‘Mwanzoni nilipata shida sana, na ikafikia hatua nikaamua kumwendea huko mjini, ili nikapate huo ushahidi wanaoutaka wazee, najuta

kwanini nilifanya hivyo, maana nilizalilika,....sitasahau, kwani siku hiyo nikiwa nimevalia zile nguo zetu, kwetu kijijini niliziona za maana ,

gauni refu...mikono mirefu, kitambaa kichwani,...nikaingia dar, ilikuwa ni mara ya tatu, nilishawahi kufika kabla.

‘Nilikuwa nafahamu wapi mume wangu huyo anaishi, nikafika bila hata ya yeye kufahamu, ilikuwa saa kumi kumi hivi, nikafika nyumbani

kwake, ...kulikuwa na mvua mvua inaanza kunyesha, nikafike eneo alikopanga chumba, alikuwa na chumba kimoja, maisha muda huo

hayajamnyookea,…anasoma na kufanya kazi, nikagonga mlango , mara akatokea mwanamke na khanga moja kiunoni, akafungua mlango,

huku akisema kwa nyodo.

‘Hivi nani hawa wanaharibuu starehe za wenzao, ni Malaya gani wewe...’akasema huku akinifungulia mlango, na kuniona mimi, akashikwa

na butwaa, maana ananifahamu, ndio huyo aliyeniambia, kuwa mimi ndiye nilimuibia mchumba wake..kiukweli, yeye alionekana mrembo kwa

maisha aliyokuwa akiishi ya mjini, mimi nimeshachakaa na maisha magumu ya kijijini, na kuzaa .

‘Ni wewe....?’ akauliza kwanza kwa aibu lakini baadaye akabadilika na kugeuka kuangalia ndani, na kusema kwa sauti iliyojaa dharau;

‘Haya wewe bwana, kuna mgeni wako nje..’akasema na kuingia ndani, na mimi nikaingia na kumkuta mume wangu akiwa na taulo kiunoni,

kakaa kwenye sofa, akageuka na kuniona, hakuonyesha ile dalili ya kushituka akasema;

‘Wewe mwanamke ni nani kakuambia uje bila taarifa, bila ya kibali changu, nataka nikiinuka hapa haupo ..rudi huko, huko

ulipotoka..’akasema huku haniangalii usoni...’

‘Mume wangu niende wapi, ..wakati nimekuja kwako, ..nitapata wapi basi muda kama huu?’ nikamuuliza kwa adabu zile za kijijini, huku

moyo unaniuma kweli.

‘Utajua mwenyewe....kwani ni nani alikuambia uje, nilishakuambia kuwa mimi sikutaki...unang’ang’ania tu kuwa wewe ni mke wangu, hebu

jiangalie wewe ulivyo, una hadhi gani, na shepu gani ya kuwa mke wangu, ...huoni aibu, eti kusema `mume wangu’, sikiliza rudi huko huko

ulipotoka,unasikia...’akasema na kusimama,

Mimi sikusogea nikasimama pale pale, na yeye bila kujali kuwa kavaa taulo, akaanza kunisukumia nje huku yule mwanamke wake,

akiniangalia kwa nyodo kashikilia kiuno...sikuona taabu, awali nikapambana naye , lakini mwanaume ni mwanaume,…akanitoa nje..nilikaa

pale nje, kibarazani hadi walipomaliza mambo yao, ...’akasema huku akitabasamu tu.

‘Ina maana hawakujali, na bado walikuwa wakiendelea na starehe zao?’ nikamuuliza.

‘Yaani tena kwa karaha, maana walijua nipo hapo nje, na mvua inanyesha..lakini kila kilichokuwa kikifanyika huko ndani, nilikuwa nakisikia,

kwa dharau..ili kunionyesha kuwa mimi sina maana..’nililowana, maana kibaraza kilikuwa hakina sehemu nzuri ya kujificha, na walipomaliza

starehe zako, wakatoka wakaenda bafuni kuoga, wakavalia, wakaondoka, sijui walipokwenda, nikabakia hapo hapo..nje,sijui niende wapi…

nalia…nifanyeje sasa, na kuja mjini nilipanga nije kupambana na hao wanawake wanaoniibia.

‘Bahati nzuri jirani yao, akanikaribisha ndani, akanipa nguo nikabadili, akanipikia tukala, japokuwa chakula hakikushuka vyema, na huyo

huyo jirani yake ndiye aliyenisaidia nauli, kesho yake asubuhi nikaondoka nikarudi nilikotoka,...hebu ona huo unyama, hata nauli

hakunipa...nimesaidiwa na majirani ambao waliniambia mume wangu kila siku anakuja ni mke mwingine...na sijui kwa vipi hakupata

ukimwi...’akasema huku akikunja uso.

‘Niliporudi kijijini, nikamsimulia mama yangu hayo nailiyoyaona, akasema, hayo ndio yo niliyoyataka, waliniambia sikusikia, ni kweli ,

walinisema sana, kipindi hicho, nilipoanza mahusiano na marehemu, wazazi wangu walichapa sana, lakini sikuwasikia, na hayo yaliyokuja

kutokea nilikiri kuwa ilikuwa ni dhambi zangu ndizo ziliandama ngoja nipatilizwe, ...nilitubu sana, nililia sana, lakini itasaidia nini…’akasema.

‘Niliishi kijijini kwa shida, hadi nilipokutana na huyo mume wako....’akasema

‘Na mume wangu..!! ?’ nikauliza nikianza kuwa na hamasa zaidi kwani huko ndipo nilipataka kufahamu ukweli zaidi wa mume wangu.

‘Ndio na …mume wako,…’akasema

‘Mkawa….eeh..’nikasema hivyo

‘Hahaha…mume wako kwangu namuona kama mdogo wangu, lakini alinionea huruma sana, kwani alikuwa akiniona ninavyoteseka, yeye

alikuwa akihangaika na shughuli zake anapita kwetu ananiachia chochote,, huwa alikuwa akiniita shemeji....basi ndivyo tulivyozoeana.

Hakuwahi kupita hapo bila kuniacha kitu.

‘Kuna kipindi niliumwa sana...karibu ya kufa, hatukuwa na hata senti nyumbani, sina pesa ya kununua dawa, kwani nikwenda hospitalini na

kuandikiwa dawa za kununua, ...hatuna pesa, na tatizo hilo lilikuwa kubwa, hadi nikaambiwa nikafanyiwe upasuaji, ..nipelekwe mjini, sina

pesa, wazazi hawana pesa , na mume wangu alipoambiwa hakujali..alitaka nife tu...’akatulia.

‘Namshukuru sana mume wako, nafahamu kipindi hicho, alikuwa hajaku-oa...kama sikosei, akauza mbuzi wake, akapata pesa, na kuzileta

nyumbani, hatukuamini, akasema amekuja kunisaidia ili nikatibiwe...na kweli nikapelekwa mjini nikafanyiwa upasuaji, nikatibiwa

nikapona..sitamsahau mume wako...’akasema.

‘Je alifanya hivyo kwa sababu gani hasa?’ nikamuuliza

‘Yeye, alisema alifanya hivyo, kwa vile mume wangu ni rafiki yake ,mume wangu alikuwa akimfundisha fundisha ufundi wa magari,

..udereva,..unafahamu mambo ya kijijini, basi wakaivana, sijui zaidi ya hapo ilitokeaje wakaivana kiasi hicho, kwahiyo yeye alinitambua

kama shemeji , mke wa rafiki yake, akanijali kihivyo.....na ujirani mwema tu...’akasema.

‘Kwahiyo kwetu sisi , kama familia, tunamthamini sana mume wako, ni mtu mwema sana, mume wako ana roho nzuri , uliza huko kijijini,

alipenda kuwasaidia sana watu,..sio mimi tu, ..yeye alikuwa na tabia yake ya kupenda kusaidia watu, .. japokuwa familia yao ina tabia

ambayo wengi wanaiona sio nzuri, baba yale ni mlevi kupindukia, na mama yake akawa hivyo hivyo....basi ni familia ya shida, lakini yeye

akawa anajibidisha na maisha yake, kuhangaika kivyake..hadi hapo mlipokutana naye...’akasema.

‘Mhh, kweli umenifungua masikio, hayo yaliyokukuta ni makubwa, mimi niliona nipo kwenye mitihani, lakini kumbe wapo wengine

wanakutana na mitihani zaidi ya unavyowazia, wewe ya kwako ilikuwa zaidi, sasa ikawaje, maana muda umekwenda, kuna mambo ulitaka

kuongea na mimi na mimi nataka kujua…eeh..?’ nikamuuliza. Na sote tukageuka kuangalia kule mlango mwa nyumba yangu, kulikuwa na

jambo…

‘Sasa ikawaje…oh, namuona mume wako anatoka, nilionana naye hapo nje wakati anaingia, tukaongea kidogo…ana haraka zake…?’

akasema,na ni wakati huo mume wangu alikuwa akitoka na wakili wake, na aligeuka akatuona ni kama vile ndio anatuona kwa mara ya

kwanza, ikabidi sasa aje pale tulipokaa…..

....NB: Nimejitolea leo kuleta sehemu hii…Ni kisa mkasa, lakini kwa huyu mama kuna mengi ya kujifunza, tutakuja kuona ilikuwaje kati ya

mama huyu na mume wake, na kwanini alifika huku mjini, je inaweza ikawa njia ya kumfanya mdada abadili nia yake na kumsamehe mume

wake..tuzidi kuwemo..?


WAZO LA LEO: Maisha yana mitihani yake, ukiona kwako ni kugumu, ujue kuwa kuna wenzako kwao ni kugumu mara mbili zaidi yako,

ukipatwa na mitihani, ujue kuna wengine mitihani hiyo ni mazoezi tu ya nyumbani(homework), kwahiyo ili uone uhalisia waangalie hawa

waliopo chini yako, ambao wanataabika zaidi yako.

.
.
.
.
.

ITAENDELEA ALHAMISI
 
SEHEMU YA 71


Na ili uvuke huo mtihani waangalia walipo juu yako, jifunze kutoka kwao,uwe na wivu wa maendeleo...usikate tamaa, pambana, lakini kwenye njia iliyo sahihi, ukijua kuwa wewe sio wa kwanza kupata mitihani kama hiyo, wapo waliopata mitihani hiyo na wakaishinda, kwanini wewe usiweze...kumbuka jambo moja, kila kitu kila jambo lina ugumu wake, lakini baada ya dhiki, mara nyingi huwa ni faraja, hasa kwa wale wenye kuvumilia na kujibidisha kwenye shughuli zao.., huku wakimtegemea mola wao.


Mhh, kweli umenifungua masikio, hayo yaliyokukuta ni makubwa, mimi niliona nipo kwenye mitihani, lakini wewe ilikuwa zaidi, sasa ikawaje?’ nikamuuliza.nikitaka kufahamu mengi kuhusu maisha ya huyo mama, ambaye nilimuita dada...

Aliendelea kunisimulia maisha yake na mume wake ambaye sasa ni marehemu...

*******

`Mimi sikukata tamaa na mume wangu, niliendelea kumsubiria, nilimuomba mungu, kuwa ipo siku,atajirudi, na kunikumbuka , lakini haikiutokea, mimi nikaendele kuishi kijijini, nikijitegemea, na hata ikafikia wazee wao wenyewe wakaamua kuliingilia kati. Ikabidi mume wangu aitwe kwenye kikao cha wazee, na yeye mbele yako akaja kukubalia kuwa kakosea, na akakubali kuwa mimi ni mke wake wa halali, na yeye anawajibika kwa hilo.

‘Sasa kwanini unamfanyia hivyo mwenzako?’ akaulizwa

‘Nilipitiwa tu na mihangaiko ya kutafuta riziki’akasema.

‘Hizo riziki unamtafutia nani sasa?’ akaulizwa

‘Mimi na familia yangu..’akasema

‘Mbona hukimbuki familia yako, au familia yako ni akina nani?’akaulizwa

‘Ni mke na watoto wangu, lakini pesa haitoshi...mambo ni mengi sana huko mjini, kuna kodi za nyumba kuna gharaam nyingi tu, lakini najitahidi au sio ...’akajitetea

‘Sasa unasemaje, ?’ wakamuuliza

‘Wazee wangu, mimi najitahidi na kiukweli nimeanza kujiweka sawa, kwani nina ndoto ya kusoma sana, na kuwa wakili…kwahiyo mambo yatakuwa sawa na nina uhakika familia yangu nitaihudumia vyema…’akasema

Kiukweli hata mimi kwenye kikao hicho niliona kama mume wangu kabadilika, sikusikia kauli zake zile..sijui kwa vile ni wazee, au ..lakini moyoni nikaamini kuwa huenda kweli mume wangu kabadilika

Ikafikia muda akaniomba msamaha mbele ya wazazi kuwa kakosa na hatarudia tena, uone wanaume walivyo…, lakini aliporudi mjini hali ikawa ile ile...hata wazee hawakuamini kuwa ndio Yule mtu aliyekiri na kuomba msamaha..basi ikabidi tukachoka, tukaamua kumuacha aendelee na maisha yake, na mimi nikajibadili sasa ..maana mitihani ni shule…ndio mwanzo wa kuanza kujiajiri...

Bahati nzuri, walikuja wawekezaji wanasaidi wanawake waliokatiza masomo kwa uja uzito na mimi nikajiandikisha, ufadhili ukanisaidia nikaanza kusoma, masomo ya watu wazima sasa, japokuwa mimi bado nilikuwa sio mkubwa kihivyo,.. nikafanya mtihani wa darasa la saba nikafaulu kwenda

Nikaanza elimu ya sekondari ya miaka miwili…nilikuwa na akili darasani kwahiyo niliweza kufaulu vyema…hadi nikafika elimu ya juu,...hutaamini, nilifaulu kwa njia hiyo nikasomea…diploma, nikaishia hapo...nikaanza mapambano ya kujiajiri…nilikuwa nasoma huku nafanya vibiashara…nalea..hivyo hivyo..

‘Ukiniona hivi huwezi amini, lakini nia na lengo langu ilikuwa kufika chuo kikuu, watu hawajui, hata huyo mume wangu alikuwa hajui..hamna aliyemwambia,maana haulizi hana habari na mimi, ..ni kama hana mke, ..mimi niliamua na nikafanikiwa, lakini sikuwahi kumkataa kuwa yeye sio mume wangu.

‘Alishangaa siku moja nipo Dar, nahutubia akina mama mpango wa kuwezeshana akina mama, waliokatisha masomo kwa ajili ya uja uzito, sijui ilitokeaje na yeye siku hiyo alikuwepo kwenye huo mkutano, nilipomaliza kuhutubia akanifuata na kuniuliza

‘Wewe mwanamke, umewezaje kufikia hatua hiyo, na kwanini unasimulia maisha yangu mimi na wewe…, ina maana mimi nilikutesa kiasi hicho…kwani nilikulazimisha, unakumbuka, nilikuambia sikutaka kukuoa, ni wazazi wako walinilazimisha, unakumbuka, sasa unakuja kunilaumu mbele ya vikao kama hivi, ujinga mtupu…akanilaumu sana…?’ akaniuliza na mimi nikamjibu

‘Ni kutokana na hayo uliyonitendea, hata hivyo mimi nashukuru sana...’nikamwambia, na ghafla huyo …akaniomba msamaha, mimi nikamwambia mimi sina kinyongo na yeye na bado mimi ni mke wake, lakini siwezi kwenda kwake, maana bado nipo kwenye hiyo adhabu aliyonipa...

Kuna kipindi aliniambia amenipa adhabu, ya yeye kulazimisha kunio mimi wakati alikuwa hanipendi, ...na ndio maana nikamwambia hivyo, kuwa mimi bado nipo kwenye adhabu yake...nikaondoka kesho yake, kiukweli mimi sikufika nyumbani kwake, japokuwa aliniomba nifanye hivyo,.. nilimwambia naogopa yasije yakanikuta yale yaliyonikuta kipindi cha nyuma.

Basi kuanzia siku hiyo, sasa ikawa yeye anakuja huko nyumbani kijijini, na akafika kwa wazee wangu, akawaomba msamaha,…na mimi pia, na mimi niliendelea kumwambia kuwa mimi ni mke wake, asiwe na wasiwasi, sina kinyongo na yeye, lakini bado nipo kwenye adhabu yake...

‘Ina maana alipokuwa akifika, alikuwa anakuja kwako, au kwao…kwani wewe ulikuwa unaishi wapi hadi muda huo , ?’ nikamuuliza

‘Alikuwa anakuja kwao, mimi nilikuwa naishi na babu na bibi, ...kwa wazazi wake, au nyumbani kwao, sikuweza kuishi nao, kulikuwa na manyanyaso, ikabidi niwe naishi na wazee wangu hao, na walikuwa wakinihitajia sana…ilikubalika iwe hivyuo, sio kwa kulazimisha…’akasema

‘Sasa alipokuwa kija kama hivyo, mimi sikumkubalia kuja kulala kwangu, nikimwanbia bado nipo kwenye adhabu aliyonipa...hali hiyo ilimtesa sana,...akahangaika, sijui kwanini aliamua kufanya hivyo...kiukweli mimi sikugeuka nyuma,...’akasema.

‘Vipi mtoto…alikuwa akiishi wapi..?’ nikamuuliza

‘Mtoto naye akawa anakuwa akawa an juhudi sana darasani…akafaulu hadi sekondari, na hatukutaka msaada wa baba yake sio kwamba tulimkataza hivyo, hapana ni yeye mwenyewe tu....ila aliendelea kumtambua kama baba yake, nilimwambia huyo ni baba yako,asije hata siku moja kumkana, au kumsema lolote baya, na alinitii, ila hatukutaka msaada wake, akiwa na shida ni mimi nawajibika.

Sasa baada ya kuniona huko Dar, akawa sasa anatuma pesa za matumizi, tulipokea na kiukweli sikupendelea kuzitumia, hata hivyo, kwa vile ni wajibu wake, ikabidi tuwe tunazitumia tu, ila sikuwa na ile hali ya kumtegemea yeye kabisa.....’

‘Ikatokea wazazi wakaingilia kati, hadi tukasuluhishwa...nikaona haina haja, na kwa vile mimi nampenda mume wangu, nikakubali yaishe, tukaanza maisha mapya,..lakini kwa masharti kuwa mimi nitaendelea kuishi huko huko kijijini, yeye aendelee kuishi mjini na wanawake zake, siku akijiskia anakuja huko kijijini namkaribisha kama mume wangu, anakaa siku mbili anaondoka zake, nimezoea, sina shida naye, mpaka umauti ulipomkuta.

‘Oh…kweli wewe.., una moyo kweli…’nikasema

‘Nilikuja kuajiriwa na kampuni isiyo ya kiserikali kwa ajili ya kusaidia akina mama waliokatiza masomo kwa ajili ya uja uzito, kwahiyo sikuwa na shida, ya kumtegemea mume tena,...sikuwa namfuatilia maisha yake, na mengi nilikuwa naambiwa na watu tu...mtoto wangu ndiye aliyejitahidi kumfuatilia na kujaribu kumkanya, lakini hakumsikiliza mtu, alidai kuwa hayo ndio maisha yake, mtu asimuingilie.

‘Sasa kwanini nije kuchukua urithi wake, .kwanini nije, kuchukua mambo yake, ambayo hatujui yametoka wapi...sisi tuliamua kila kitu chake tukiuze, tulipe watu, na kama hakuna watu tutatoa sadaka…’akasema

‘Mhh…lakini..’nikataka kusema neno lakini hakunipa nafasi akaendelea kuongea.

‘Na katika huu msiba ndio tukaja kugundua kuwa kumbe ana watoto wengi wa nje, ana madeni mengi ya watu,...na hawo waliofanyiwa ubaya, ni wengi, japokuwa awali hawakutaka kujitokeza…ndio tukajaribu kuwalipa lipa na kuwaomba msamaha, na hili zoezi ndilo tunaendelea nalo mpaka sasa nia ni kumsaidia marehemu,....’akasema.

‘Kwahiyo ndio maana mlikuwa mnanitafuta mimi, lakini mimi simdai, ila nasikia anamdai mume wangu, mimi sijui..?’ nikamuuliza

‘Ni pamoja na hayo, ila cha muhimu kwa hivi sasa ni huo mkataba, madeni hayana nguvu sana…sasa sisi tunachotaka kwako ni kujua ukweli, na kama tulivyohisi, tumegundua kuwa ni yale yale ...kwahiyo, tunaomba, mtuambie tufanye nini, kwani sisi hatutaki kitu chochote kutoka kwake, ila tunachotaka ni kuyaweka mambo yawe sawa, kusiwe na kudaiana , na tunafanya haya kwa vile mtoto wangu ndiye kapewa hilo jukumu....’akasema

‘Je unafahamu lolote kuwa mkataba huo mlio nao…umetokana na kugushi mkataba mwingine uliokuwa halali?’ nikamuuliza

‘Nimesikia hilo kwa wakili wetu, na yeye alisikia kutoka kwa wakili wako,sasa ukweli upo wapi, ndio tukaona kuna umuhimu wa kuonana na wewe ...’akasema.

‘Je mna amini hilo, kuwa mume wenu alikuwa na hisa kwetu?’ nikamuuliza

‘Sisi hatuna haja ya kupekenyua ukweli, ukweli mnaufahamu nyie..sisi hatuna haja na hizo hisa, hata kama kulikuwa na ukweli, hatuna haja nao....tulishaanza maisha yetu, hatukuwa tunamtegemea yeye, kwanini sasa kafariki tuanze kugombea mali yake, kama walivyokuja watoto wake wa nje kuja kugombea mali yake....sisi tuliwaambia kuwa kama wanahitaji mali ya marehemu, basi wakubali na madeni yake, na alipopigwa mahesabu ikaonekana madeni na mengi, kuliko, wenyewe wakakimbia.

‘Hayo ni ya mume wako, sasa tuongee kuhusu mume wangu,...kwanini mnamtetea yeye mnajuaje kuwa yeye sio mkosaji kama alivyokuwa mume wako ?’ nikamuuliza

‘Sisi hatumtetei, ila tunatimiza wajibu wetu, yeye kama wengine, ni miongoni mwa watu walioathirika kutokana na tabia ya mume wangu....anahitajia kupata haki yake,...alihadaiwa, na akajikuta anatoa hisa kwa mume wangu, tunahisi hivyo, …japokuwa bado hatujaupata ukweli, ukipataikana ukweli tutafanya inavyostahiki...’akasema

‘Kwa vipi mtaweza kuupata huo ukweli?’ nikamuuliza

‘Kutokana na mikataba,.wakili wetu katushauri hivyo..hatuna jinsi nyingine, sisi , na mtoto wangu,..tunajitoa kwenye huo mkataba, na nio bora uvunjwe kabisa, lakini kama miktaba hilo ilitengezwa kisheria, basi sheria ifanye kazi yake kuivunja, au sio, ndio utaratibu muafaka, tusaidiane kwa hilo…’akasema

‘Ndio lakini huo mkataba mliona nao, sio sahihi, ni wa kugushi…’nikasema

‘Ndio maana mwanasheria wetu anaufanyia kazi, ila tunahitajia msaada wenu, ..mume wako kasema wewe unaweza ukawa ni kikwazo, ndio maana tokea awali tumekuwa tuklitaka kuonana na wewe..hukushangaa nilivyokuuliza awali, je mna matatizo gani wewe na mume wako…nashukuru kuwa tumekuona na iliyobakia ni wewe kushirikiana na sisi, tulimalize hili jambo..’akasema.

‘Nakushukuru sana kwa kuwa mkweli kwangu na kunielezea sehemu ya maisha yako, na mimi sina kinyongo na nyie tena, ...ama kuhusu maswala ya mume wangu, hayo hayawahusu, nawaombeni msijaribu kuyaingilia,...kama mnataka kumsaidia kwa hilo, nyie mshaurini yeye aulete ule mkataba wetu wa awali, ambao tuliandikishana mimi na yeye,kuhusu mambo yote,yeye akaghilibiwa na mume wako akakubali ubadilishwe, ...hilo tu, ...’nikasema.

‘Sisi hatuujui kama kuna mkataba mwingine tumaliskia hili hivi karibuni kutoka kwa hao mawakili, .sasa..hata sijui huo mktaba mwingine upo wapi..na je uhalali wa hiyo mikataba itakuwaje…’akasema huyo mama

‘Hata mimi siujui huo mkataba wenu mnao-uongelea, na wala siutambui, maana ulitengenezwa kimbinu kutokana na kuvunja mkataba watu wa awali bila mimi kujua, umegishiwa na sahihi na kila kitu, sijui walifanyaje...kwahiyo huo mkataba mlio nao ni batili,..’nikasema.

‘Kwahiyo nyie au wewe unataka sisi tufanye nini?’ akaniuliza.

‘Kwa hivi sasa niseme tu, kuwa nyie mumeshatimiza wajibu wenu, ..nawashukuru sana kwa hilo, sisi au mimi sina kinyongo na nyie na kwa vile mume wako, ...hayupo tena hapa duniani, huwezi kumuhukumu maiti au sio…, anayehukumiwa kwa hivi sasa ni swahiba wake..naye ni ni mume wangu...nafikiri umenielewa hapo….’nikasema.

‘Mdogo wangu, mimi nataka kukupa ushauri tu, ni ushauri wa bure, kama utauona una maana haya, kama ndio wa kupitwa na wakati haya, ukitaka kuufuata ufuate kama hutaki basi, ni hivi, hakuna mkataba wa ndoa zaidi ya ndoa yenyewe, mkataba wa ndoa ni kiapo chenu cha ndoa, pale mliposimama wewe na mume wako, ukakubali kuolewa na yeye na yeye kukubali kukuoa,..au sio’akatulia kidogo huku akionyeshea kwa mikono.

‘Hilo ni sawa, lakini matendo ya wanandoa yanaweza kuuvunja huo mkataba…amini hilo, …kuna matendo yanaharibu kabisa ndoa…lakini watu hatufuatilii..je ni nani wa kulaumiwa hapo…’nikasema

‘Ni sawa, lakini kusameheana kupo, au sio…nakubali hilo..lakini ninachotaka kusema kuhusu ndoa,…msije kuvunja ndoa kwa sababu ya vitu vingine kama mali..na watoto..’akasema

‘Watoto kwa vipi…?’ nikamuuliza

‘Ndugu yangu tusiongee sana, huo ndio ushauri wangu, unajua kwenye hii kazi nimejifunza mengi, nakubali ukweli, kuwa wanandoa, tupo kwenye mitihani mikubwa sana, hasa mmoja wapo anapokuwa sio mkweli,.....’akasema

‘Sasa hapo utafanya nini..hebu niambie kama mmoja wapo anavunja mkataba, na hakuna kitu mlichoandikiana naye….’nikasema

‘Nikuambie ukweli, sisi wanadamu , nikiwa na maana sisi wanandoa, hata kama tutajaribu kuwekeana mikataba mingine, tunayoona sisi ni kisheria zaidi, tukajenga ukuta wa kulindana, tukaweka na walinzi wa kutulinda, ndani na nje, ...tukafanya kila iwezekanavyo, ili mmoja asivunje miiko ya ndoa, …hatatuweza..’akasema

‘Kwanini..?’ nikamuuliza

‘Mikataba halisi ya ndoa ipo kwetu sisi wenyewe…kama mioyo yetu, kama sisi wenyewe hatukujibidisha hivyo, tukakubali mioyoni mwetu kuwa ndoa ni kati ya muma na mke, kuwa ina masharti yake, ambayo kila mmoja anatakiwa kuyatimiza kidhahiri na kificho,...kama hatutajua hayo sisi wenyewe, tukayakubali sisi wenyewe ndani ya nafsi zetu, haiwezi kusadia kitu,...kamwe, hatutaweza kufanikiwa....’akasema.

‘Kwahiyo unataka mimi nifanye nini…?’ nikamuuliza

‘Mimi nakushauri kama mkubwa kwako, maana kiukweli wewe ni mdogo wangu mbali tu, nimkuzidi kiumri, na huenda hata kiuzoefu, mimi nimepitia kwenye mitihani mingi migumu, niliyokusimulia hapa ni cha mtoto, nikushauri jambo, hakuna haja ya kuhangaika sana kwa hili…, cha muhimu kwa sasa ni kumsameheana tu…’akasema

‘Kusamehe sio tatizo tatizo unasamehe nini sasa…’nikasema

‘Sio lazima kila la kusamehe liwe wazi kwako mengine ni bira uyasamehe bila kuyafahamu maana ukiyafahamu huenda ukashindwa kuyasamehe, yaache yabakia na muhusika mwenyewe atajuana na mola wake, nina uhakika mumeo kakukosea, hata kama hajakutamkia, maana madume, wanaweza kujifanya hawajakosea, lakini kiukweli kwenye nafsi zao, wanajua kabisa wamekosea...na wengi hujijutia..’akatulia kidogo.

‘Ni rahisi kumsema mwenzako au sio…’nikasema

‘Unajua nikuambie jambo sisi wanawake, kwa waume zetu ni kama mama zao, tunabeba yote kama mzazi anavyobeba makosa ya mtoto wake, ..mtoto, anaweza kukosea sana, lakini mwisho wake kama mzazi, unamsamehe, unaona mtoto ni mtoto tu…’akasema

‘Lakini mume sio mtoto, ana akili zake na pia kapewa wadhiaf wa kiongozi wa familia, au sio…’nikasema

‘Ndio…lakini kuna mambo sisi tumetukuzwa nayo,…uvumilivu, malezi, kunyenyekea,…mapenzi haya ni tunu kwetu, tusiyabeze, wapo waliojaliwa ni heri kwao, lakini..nasema tena lakini wapo,...wengine wanaweza kuleweshwa na tama ndogo tu, ya kiwiliwili cha mwanamke, akaghilibika, na akajikuta kafanya lisifanyika, kama walivyo watoto...ukimuuliza anajifanya hajui, au hata kukataa, anakataa…, sasa sisi tujitahidi tu kuwasamehe....’akasema na mimi nikawa natikisa kichwa kutokukubaliana na maneno yake.

‘Nikuambie tena,....wengine wanaweza hata kukubali makosa yao, lakini anakubali mdomoni tu, mwingine anaweza asikubali, lakini moyoni kakubali makosa, ila anaogopa kuonekana kakosea,sasa mimi namfahamu sana mume wako,... kama kakubali kujirudi, kama yupo tayari kuishi na wewe, na kuwa hatafanya tena hayo makosa yaliyotokea,...basi msamehe tu,….mengine muachie mola wako…’akasema

‘Hapana, mimi nataka mkaaba ufanye kazi yake ili watu wajifunze…tusiendekeze mambo…’nikasema

‘Mkataba,..mkataba…mama nanihii…kwani huo mkataba ndio ndoa,..huo mkataba hauna maana yoyote kama hutaweza kuishinda nafsi yako.. ..unaweza ukawepo na bado kwa siri watu wakawa wanauvunja tu, utajuaje…, sasa inasaidia nini hapo..mkataba mnzuri upo ndani ya mioyo yenu....’akasema.

‘Mhh..mimi naona nyie mnamtetea sana jamaa yenu, kwa vile lakini kama mngelitendewa kama mimi najua mngelichukua hatua……’nikasema

‘Sio kumtetea, nakushauri tu, …mangapi yametokea kwangu, nimekuhadithia ili ujifunze kidogo kutoka kwangu, nakushauri tena, achana na kuhangaika na huo mkataba, ...wao wanajua wenyewe kwanini waliubadilisha, wewe shikilia mkataba wao ambao mungu anautambua, kiapo cha ndoa, na timiza wajibu wako kwenye hilo, sasa kwa ushauri wangu, kaeni tena pamoja, jadilianeni, muone chanzo cha kosa ni nini, huenda chanzo ni wewe mwenyewe lakini hujatambua hilo,…’akasema

‘Kama chanzo ni mimi, kwanini hajaniambia, nikajijua na kujirekebisha, yeye si mume wa familia, ilitakiwa yeye aniambie, ..kama alikaa kimia, mimi nilijionea ni sawa tu,…sasa mimi natimiza wajibu wangu siwezi kukaa kimia, …tuje kuangalia sote…’nikasema

‘Jingine si nyie mna watoto, sasa mnataka watoto wenu waje kujifunza nini kutoka kwenu,...wakiona baba na mama wapo kitu kimoja, wanakaa wanashauriana kila mara wanafikia muafaka, na wao wanajiwekea nadhiri mioyoni mwao kuwa nikiwa mkubwa, nikaoa, nitaishi kama walivyokuwa wakiishi baba na mama...’akasema na mimi hapo nikakaa kimia.

‘Sasa kama nyie wawili, kila mara mazozano, au mumanuniana,..au kila mtu na hamsini zake…na baadae mnaishia kutengana,..kuachana,..wao watamfuata nani, au wao watajifunza nini, wataona kumbe kuishi kila mtu maisha yake, inawezekana, ndio mtindo wa maisha, lifikirieni hilo kwa ajili ya kizazi chenu, na huo ndio mzigo tunaoubeba sisi wanawake...’akasema.

‘Nakushukuru sana kwa ushauri wako dada yangu, lakini nilikuwa na swali moja nataka nikuulize, ili nione kama kweli wewe unatetea pande zote mbili, ili kuona suluhu ya kweli, .. je mume wangu aliwahi kukuambia kuwa ana mtoto nje ya ndoa?’ nikamuuliza. Alikunja uso kidogo, halafu akatabasamu, na kusema…

‘Mhh, kwa jibu la moja kwa moja, kiukweli kwangu hajawahi kunitamkia hivyo, huwa naongea naye, kama mtu na dada yake, kama shemeji yake, tunataniana hapa na pale, lakini kwa hilo hajawahi kuniambia, siwezi kukuficha…’akasema na akawa kama anawaza jambo, halau akasema

‘Unajua watoto wa nje..kwangu wapo..na siwezi kuona ajabu kwako pia…lakini hayo sio kosa lako, au sio..na sio kosa la hao watoto au sio….na wao wana haki yao,..sio kwamba natetea hilo, hapana, lakini kama limetokea ..ufanyeje sasa…ndio iwe kigezo cha kuvunja ndoa…’akasema

‘Sio kigezo kwa mimi, ni kigezo cha yeye, kuwa kavunja ndoa,…je hilo ni sahihi kwenye ndoa..kwenye ndoa, ilisemwa kuwa anaweza kuzaa nje bila ndoa..niambie ukweli hapo…je kuzini sio dhambi, ni nini adhabu ya mzinifu ndani ya ndoa..tusije kutetea dhambi tukaja kupata dhambi…’nikasema

‘Hahahaha…ukisema hivyo, nahisi wengi watavunaj ndoa zao, na wengi watapigwa mawe mpaka kufa…sasa sijui…lakini msamaha ni bora zaidi au sio..ukimsamehe abada ya kukiri kosa basi,…tufanyeje sasa…’akasema

‘Unaona..udhaifu wetu huo..wewe awali umesema sisi wanawake ni wazazi ni walezi, na kila mmoja ni mchungi kwa mwenzake, je tutachungana hivyo kwa kuyakubali makosa, yafanyike tu..tusamehe tu..wengine wataona ni mchezo, acha adhabu ifanye kazi yake uone watu kama hawataogopa….’nikasema

‘Ni sawa, lakini wewe hujafanya makosa yanayofanana na hilo…usiangalie upande mmoja tu…unaweza ukawa umezini kwa namna nyingine..samahani usiona natetea hayo, maana hata mimi yananiuma sana..lakini tuangalia jinsi gani ya kuokoa, kuliko kubomoa…nakubali kama kafanya hivyo kakosea, lakini tufanyeje..naangalia upande wa watoto…’akasema

‘Watoto, watakua watajifunza, ukweli utakuwa bayana, …mimi bado nipo pale pale…ukweli, na ukweli wetu ulisimamiwa na mkataba, ni kwanini wakaja kuuharibu mkataba , kama kweli alitaka haki, …kama kweli alikosea, basi angelikuja akaniambia, ndio ningeumia..lakini ningelijua kuwa kweli mwenzangu kateleza, lakini kwa hatua waliyofikia, hapana..’nikasema

‘Unajau kiukweli mimi sina uhakika na hilo, ila…, ninachokumbuka, ni kuwa, kuna siku nimemuuliza, hivi yeye kwa sasa ana watoto wangapi, aliniambia kuwa tu ana watoto wengi, lakini.., hakusema idadi,....’akasema.

‘Hakukuambia kuwa ana watoto wangapi..na hujui kuwa mimi nina watoto wangapi?’ nikamuuliza…’ nikasema.

‘Hakusema idadi kiukweli, ila nakumbuka kauli yake aliyotoa ni kuwa, yeye atahakikisha watoto wake, wote, bila kujali ni mke au ni mume, atawaandikishia haki zao, na ni vyema kufanya hivyo kimaandishi....’akasema

‘Ehee…kama ni wakike au wa kiume…unakumbuka ni lini..?’ nikauliza

‘Sio muda mrefu,…na alisema, kitu kama hicho kuwa hataki watoto wake waje kubaguana, awe wa kiume au wa kike….nakumbuka kitu kama hicho, na kwa kauli hiyo, nilifahamu kuwa nyie mna watoto wa kike na wa kiume’ akasema.

‘Hapo kuna kitu, …lakini kwa kauli yako tu, sasa naanza kuhisi kuna yawezekana kweli kuwa akawa na mtoto nje, huyo mtoto wa kiume katoka wapi...?.’nikamuuliza huku nikionyesha kushangaa, na yeye akaonyesha kushangaa jinsi nilivyomuuliza, akaniuliza swali;

‘Kwani nyie mna watoto wangapi?’ akauliza huku akiangali huku na kule, kama anawatafuta watoto.

‘Mhh, usijali dada yangu, naona tuishia hapo, au kuna jingine ulitaka kuniuliza maana nyie mumesema mlikuwa mkinitafuta sana…maana haya mambo mengine ni mambo yangu na mume wangu, tutaelewana tu...’nikasema.

‘Aaah, uliniuliza swali, nikakujibu, na wewe naomba unijibu swali langu...ili kama nina cha kukushauri, nitakushauri, sina nia ya umbea,au nimekosea jamani...’akasema.

‘Kiukweli, sisi tuna watoto wawili tu, tena wakike wote...’nikasema.

‘Basi labda mimi nilisikia vibaya, lakini nina uhakika, kutokana na kauli yake, ni kama vile mna watoto wa kike an wa kiume...hata kwenye huo mkataba niliouona, mimi sikuusoma sana,..maana sikuona umuhimu wake, kuna kitu kama hicho,...sikumbuki vizuri, na kwahiyo hapo siwezi kusema kitu,...nisije nikawa mbeya,, ila lisemwalo lipo, kama halipo laja....’akaniangalia kwa macho ya udadisi.

‘Nitaligundua tu, nina uhakika kabla ya wiki nitakuwa nimeshagundua ukweli...na hapo ..sijui, maana huo ni ushahidi wangu wa kutosha, na kuanzia hapo nitajua nichukua maamuzi gani..na ka hatua hii,.....’nikasema.

‘Kwahiyo huenda hilo ndilo linafanya msielewane nyie wawili au sio, ....na hilo huenda ni moja ya jambo ambalo wewe unaliona linalovunja mkataba wenu au sio..ni sawa kwa hilo hata mimi silipingi, unapotoka nje ya ndoa umeshavunja mkataba wa ndoa..lakini kusameheana ni bora zaidi, au sio…’akasema

‘Sio rahisi kihivyo….mimi ni mvumilivu sana, na wengi mpaka huniona ni mjinga, sielewi, sikubali ukweli…lakini nina subira ya namna hiyo, ila sasa ikizidi kama hivi, basi moyo wangu ukikengeuka, siwezi tena…’nikasema

‘Yeye si kakubali kuwa kakosa au sio, na wewe ukubali kumsamehe....kama kuna mtoto nje, ambaye humjui, basi jadilianeni muone jinsi gani mtamtambua huyo mtoto...wewe waonaje kwa hilo…?’ akasema na kuuliza.

‘Mkataba wetu ulikataa hilo, na hadi hii leo yeye hajakubali hilo, sasa wewe unanishaurije hivyo,kwanza kazini, kuzini si kuvunja mkataba, halafu kama ana mtoto, sio ndio ushahidi wenyewe…tatu anavinja mkataba, anaugushi..kwanini afanye hivyo,…anamdanganya nani hapo.., aah, mimi hilo sitavumilia kabisa…’nikasema

‘Kama nilivyokushauri, labda mimi ni tofauti na wengine, unielewe vizuri hapo, maana kiukweli mimi sijui...kama limeshafanyika, na mtoto yupo, na yeye anawajibika kwake, na sijui labda huenda anawajibika na kwa mama wa mtoto pia, na kama bado mtoto ni mchanga,kiukweli ni lazima awajibike, hana ujanja hapo, na ni vyema, akuambie ukweli....muulize, kwa wakati muafaka, atakuambia...’akatulia.

‘Nimeshamuuliza sana, lakini hataki kuwa mkweli…’nikasema

‘Kwahiyo kumbe mna mabinti wawili, hamjajaliwa kupata mvulana....ndio maana niliwahi kusikia zamani kidogo, kuwa akizaa mtoto wakiume atakuwa katimiza ndoto yake...lakini ni zamani kidogo,...’akasema

‘Zamani ya vipi…?’ nikauliza

‘Aaah, zamani, sikumbuki, ila muhimu kaeni mliongelee kama wanandoa,....ili mambo yaishe, mgange yajayo..msisubiri mpaka kutokea msiba, mmoja wenu hayupo duniani ndio hawo watoto wa nje, wanaanza kujitokeza, na kuleta mfarakano, kama ilivyotokea kwetu, japokuwa tumeshayamaliza kiaina, ..’akasema.

‘Nimekuelewa dada yangu, nakushukuru kwa ushauri wako,...lakini hayo ya mume wangu, yaacheni kama yalivyo, ninafahamu jinsi gani ya kufanya, nilitaka kuwa na uhakika tu,…’nikasema.

‘Sasa nikuulize kitu, je akija kwa hivi sasa akakuambia ukweli, utamsamehe?’ akaniuliza. Na kabla sijamjibu macho yetu yakaona jambo….

Kule mlangoni nikawaona mume wangu na Yule wakili wake wakitoka, wakawa wanashikana mikono kama kuagana, na mume wangu akageuka na kutuona ..akamshika bega wakili akaongea naye jambo, na wote wawili wakawa wanakuja kuelekea pale tulipo…

NB: Ni nini kitaajiri hapo


WAZO LA LEO: ushauri mnzuri ni ule unaoangalia usawa, kuwa ninachomshauri mwenzangu hata mimi ningalifurahia kufanyiwa hivyo. Mshauri mwenzako kwa wema, mshauri kwenye mambo ambayo yatamjenga,..na hata yeye akifanya au wewe ukifanyiwa hatupata madhara yoyote.
 
SEHEMU YA 72



‘Nimekuelewa sana dada yangu, nakushukuru kwa ushauri wako,...lakini. eeh…’nikasita maana niliona kama gari linaingia getini, halafu nikasema

‘Hayo ya mume wangu,..najua mnampenda na kumthamini sana, lakini nawaombeni hayo mniachie mimi mwenyewe…’nikasema na sasa geti likawa linafunguliwa, lilikuwa gari la mume wangu.

‘Oh wamerudi na kunikuta tena hapa, mimi naondoka…’akasema

‘Kwanini haraka hivyo…hatujamalizana …’nikasema

Na kabla hajajibu mume wangu akateremka kwenye gari, na wakili wake,…na walipoteremka, badala ya kuelekea ndani, wakawa wanakuja pale tulipokuwa tumekaa, na ikabidi tukatizie mazungumzo yetu.

Tuendelee na kisa chetu.....

‘Aheri bado mpo..nahisi hili litatufurahisha sote,…maana shemeji yangu upo, na…na mke wangu ..unajua leo kutwa nzima tumekuwa tukilihangaikia hili,…kutafuta haki, ..na haki haiji hivi hivi wakati mwingine au sio..’akasema mume wangu na kumuangalia wakili wake ambaye alitikisa kichwa kukubaliana na yeye.

‘Sasa hivi tumetokea polisi, kumuona Yule mpelelezi anyeshughulikia hii kesi yako ..mke wangu mambo sasa yanakwenda vizuri tu..imebakia maswala machache,..si unajua tena nchi yeu ilivyo…’akasema na kumuangalia wakili wake.

‘Kwanini…maana haya yapo mikononi mwao, na tulikubaliana kuwa hakuna haja ya kuwafuatilia, tuwaachie wao wafanye kazi yao…’nikasema

‘Ndio hivyo mke wangu, lakini ni wajibu wangu, eeh, na wakili hapa kulifuatilia hilo, kuhakikisha kuwa, mke wangu upo na amani, haiwezekani watu wakushuku tu, haiwezekani mtu auwawe tu, na sisi tubakie kimia, ni kwanini …eeh, Yule alikuwa ni rafiki yangu mkubwa..hapana mimi sitakubali kukaa kimia mpaka haki ipatikane…’akasema

‘Ok, kwahiyo…?’ nikauliza, na sasa wakili ndiye akaanza kuongea.

‘Kifupi ni kuwa polisi wanasema bado wanalifanyia kazi, lakini kwa kuhusu wewe kama mshukiwa muhimu, halipo tena,…’akasema

‘Kabisa…kazi nzuri ya wakili wetu…’akasema mume wangu.

‘Lakini hata hivyo kabrasha la kesi halijafungwa, si unajua tena mambo ya kisheria, kuna taratibu zinatakiwa kufutwa, ..na hilo ndilo tulikuwa tunalifuatilia, ili kuhakikisha kuwa gabrasha hilo limefungwa..na wewe utakuwa huru kabisa…’akasema

‘Lakini mimi nina wakili wangu analifanyia kazi hilo…’nikasema

‘Haina shida, yeye afanye kivyake na sisi kivyetu,..lengo letu ni moja, na mwisho wa siku tutakaa pamoja…na kuona kila mmoja kafikia wapi, muhimu ni kuhakikisha kuwa kesi hii haipo tena, ..lakini wkati huo huo, haki imetendeka, na muuaji kapatikana…maana aliyefariki ni jamaa yetu..’akasema wakili.

‘Sawa nashukuru …’nikasema

‘Sasa tatizo mke wangu, kila kitu ni gharama au sio..na unajua hali niliyo nayo, nakwama kabisa, nilikuwa naomba…tukaongee ndani, unipitishie hundi yangu..’akasema

‘Hundi ya malipo gani…?’ nikauliza

‘Ya wakili, na kufuatilia..na mambo mengine ya kikazi..ni pesa nyingi kidogo, na sitaweza kupitisha hundi hiyo kwa sahihi yangu tu..’akasema

‘Naomba hilo tutaliongea baadae..’nikasema

‘Ni muhimu na haraka kuna mambo mengine nayafuatilia,…’akasema

‘Mume wangu tulishaliongea hilo, mimi siwezi kuweka sahihi yangu …kwa kazi yoyote ya ushirika, hasa za makampuni, mpaja swala langu litatuliwe, hilo lipo wazi, kwahiyo kama ni hundi ya namna hayo, samahani sana…’nikasema

‘Mke wangu hili ni la muhimu sana, tunataka tumalizane na kesi yako,..na haki ya marehemu ipatikane,..ina maana wewe huna uchungu na hilo..na hata kama huna uchungu na hilo,na je wewe hutaki uwe huru…?’ akauliza

‘Nitaongea na wakili wangu…’nikasema sasa nikisimama kutaka kupiga simu kwa wakili wangu.

‘Wakili wao wa nini sasa haya ni yetu, hayamuhusu…’akasema

‘Wakili wangu ndiye anasimamia kesi ya mkataba..kila jambo kama ni muhimu yeye ndiye anatakiwa atoe maamuzi ya kisheria, siwezi kulikwepa hilo…’nikasema na wakili wangu akawa hewani.

‘Vipi umefanya kama nilivyokuambia…?’ akatangulia kuniuliza

‘Kabisa…lakini kuna tatizo hapa, mume wangu kaleta hundi ya ushirika anasema anataka niweke sahihi yangu..nishauri…’nikasema na kumsikiliza kwa makini halafu nilipomaliza kuongea naye, nikasema;

‘Kama nilivyosema kila kitu kinachohusu mkataba wangu wa zamani kitapitia kwa wakili wangu,kwahiyo kama ni ya haraka usubiria anakuja…’nikasema na hapo mume wangu akamgeuikia mwenzake na kusema

‘Twende zetu…’akamshika mkono na wakaanza kuondoka.

‘Vipi tena…?’ nikauliza lakini hawakunijibu kitu haoo, wakaingia kwenye gari na kuondoka zao.

*********

Yule mama akawa kimia, nahisi alijifunza jambo hapo, akasimama sasa akitaka kuondoka.

‘Mimi naondoka maana kijana wangu ana mambo mengi ya kufuatilia…’akasema

‘Umeona mwenyewe mambo yalivyo..’nikasema

‘Lakini yatakwisha tu, ila nahisi mume wako ana jambo…ila anaogopa kukuambia, hebu nikuulize ni nini kikubwa kwenye huo mkataba wenu ..ambacho unahisi kakivunja,…?’ akaniuliza

‘Siwezi kusema lolote kwa hivi sasa, ..’nikasema na hapo akakaa tena kwenye kiti na kwa sauti ya chini akaniliza

‘Nilikuuliza kitu, je mume wako akiamua kukuambia ukweli, utamsamehe?’ akauliza sasa akiangalia saa yake ya mkononi.

‘Hapo mimi sijui, ..kiukweli kachelewa sana kuwa mkweli na zaidi anazidi kuharibu, na kwahiyo kama ataamua kufany ahivyo, najua kabisa itakuwa ni kutokana na kushawishiwa, au kwa vile kaona kakwama…’nikasema

‘Nimekuelewa sana dada, ila nauliza hivyo maana ndoa ni mashikamano ya mume na mke, na kila mmoja anawajibika kuitii ndoa yake, lakini ni lazima mfike sehemu myamalize au sio…’akasema.

‘Ni kweli yataisha tu, lakini kuisha kwake ni baada y akuupata huo mkataba wa zamani, tukae tuona unaemaje, na yeye akiri makosa yake, ..mengine yatafuta baada ya hapo…

‘Nakuelewa sana mdogo wangu,...unajua kuna makosa madogo madogo tunayoyafanya sisi wanandoa hasa wa kike, tunaona ni sahihi au ni madogo tu, kwa namna yetu, kumbe kwa wenzetu ni tatizo kwao, na wao kwa uwezo wao wanaweza kufanya jambo, na matokea yake kuna leta matatizo, na ushukuru wewe una uwezo wako…’akasimama sasa akitaka kuondoka

‘Nafahamu hilo,najua hata mimi nina makosa yangu, lakini sio ya kuvunja mkataba ..maana ni mambo ya kuelezana, kama nilikosea, angeniambia,..usitetee hilo…sawa tulikuwa tunahangaika na majukumu ya kazi, na mambo mengine yakawa kama hayana msingi, lakini je hayo ndio yafanye mtu aka…hapana…’nikasema. ‘Ndio awali nikakuambia kuwa sisi wanawake tuna dhima ya kuwalea wanaume wakati mwingine kama watoto wetu,…sina nia mbaya hapa…’akatulia kama anawaza jambo.

‘Mfano nikuulize hivi ukiwa unamlisha mtoto wako vyema, akanisha vyema anaweza kwenda kuomba chakula kwa jirani…?’ akaniuliza

‘Una maana gani…?’ nikamuuliza

‘Nijibu tu…’akasema

‘Hawezi…’nikasema

‘Basi ndio hivyo, wakati mwingine tunaweza kuwanyima watoto wetu, eeh, unanielewa hapo, chakula,..haki yake, ikafikia akazidiwa, sasa akienda kuom,ba chakula kwa jirani, utamlaumu nani…hahaha…’akasema na kucheka.

‘Sijawahi kufanya hivyo…labda …hapana, unajua hayo ni maswala ya kuambiana, kwani mimi si mke wake, kwanini aogope kuniambia…ana njaa…’nikasema

‘Haahaha..tuyaache hayo..ila yakitokea haya ndio tunapata fundisho, mimi nitashukuru sana mkilimaliza hili kwa amani, na sitafurahi kama mtaishia kubaya, haya juhudi yetu itakuwa haina maana…’akasema

'Msimamo wangu upo wazi, …sifanyi kwa nia mbaya, lakini ikifikia huko, nitafanyaje, je kama ndio imeanza hivyo, huko mbele itakuwaje, sasa hivi kaanza kuandikisha watoto wa nje, je mama wa hao watoto ana dhamira gani,…ni lazima niwe makini hapo…’nikasema

‘Ninachoweza kusema kwa msameheane, wewe ulivyo,....hutapoteza kitu hapo au sio, bado una nafasi ya kuendelea na ..na kampuni yako,…nasema hivyo sio kwavile na mtetea shemeji yangu, hapana…’akasema

‘Mhh…unajishuku dada…’nikasema

‘Pamoja na hayo, mimi namfahamu sehemu nyingina ya tabia yake…kila mtu ana hulka lakini kuna hulka hujificha,..yeye ni mwanaume mwema sana, akimpta mtu wa kumjua alivyo, ana huruma sana kwa watu, japokuwa katokea kizazi cha tabia hizo zisizopendeza watu, na mengine ni shida tu..watu hawajapenda wawe hivyo.....’akasema.

‘Nimekuelewa….ngoja tuone ..’nikasema

‘Sasa mimi naondoka tuonane lini sasa…nafahamu kuna maswala hayo ya mawakili, wanafanya kazi zao, naona wanakipizana huku na kule,.. hata hivyo ni lazima maisha yaendelee, naopmba tuje tukae tuongee tuone maisha yanakwendaje, …haya yanayotokea sasa yasitufanye kusimamisha mambo mengine, naomba nije tusaidiane mawazo ya maendeleo…’akasema

‘Sawa kwa hilo tu, hamna shida kabisa, tupo pamoja…’nikasema

‘Na kwa hili je…?’ akauliza sasa akinyosha mkono wa kuagana.

‘Hahaha, dada hujanielewa mpaka hapo…niakuambie kitu, baada ya wiki mimi nitawapatia jibu langu,…kuhusu hili…kwa hivi sasa niacheni nipambane na mume wangu.....’nikasema na kikunja uso wangu kuashiria dhamira ya kweli.

‘Mhh, baada ya wiki sio sawa, basi ngoja waupitie huko mkataba waone wafanyeje, hayo ni mambo ya kisheria, au sio…?’ akauliza

‘Huo mkataba wa kugushi, ..au?’ nikasema kama nauliza

‘Mhh..mimi sijui sasa…naona kwa hili litaleta utata…na hapo ndio tunazidi kuchelewa,…namuonea huruma sana kijana wangu…kwani na yeye anachelewa kuondoka, lakini hawezi kuondoka kabla hili tatizo halijaisha, ya mungu mengi...’akasema.

‘Ninachoweza kukuambia dada, huo mkataba kwangu ni batili, na kama mtaendelea kuutumia basi msije kunilaumu, itabidi mimi niende mbele ya sheria, ili haki itendeke…sasa kwa ushauri wangu wa haraka, msubirie baada ya wiki, au hata kabla ya hapo, kama mume wangu atakuwa tayari kutimiza masharti yangu, nitawaambia, ni nini cha kufanya..’nikasema

‘Sawa nimekuelewa, nashukuru sana,..’sasa akataka kuondoka na ghafla akasimama.

‘Mungu wangu sijui kama mliongea na kijana wangu..kuna jambo limezuka…’akasema sasa akarudi kukaa..

‘Samahani kidogo, ni muhimu kwa kweli…’akasema

‘Jambo gani tena…?’ nikauliza

‘Unajua huku kuzaa ovyo ovyo nje ..mitihani yake ndio hiyo,,..juzi,..kuna msaidizi wa kijana wangu. Msaidizi katika mambo hayo ya mirathi,… Unajua marehemu kila kitu alikiacha kwenye maandishi, utafikiri alijua atakufa…ndio hivyo, usomi nao unasaidia, au sio…si ndio hivyo hata nyie mnakuwa na mikataba ya ndoa nk..kusoma huko…’akasema

‘Mhh..kuna tatizi gani ..?’ nikauliza

‘Huyo msaidizi wake sasa..ni mtoto wa marehemu mwingine, alizaa na mwanamke mwingine..na katika maelezo yake kwenye hayo maandishi aliyoacha,..alitaka huyo kijana atambulikane na awe msaidizi wa kijana wangu, kila kitu kwenye maandishi tena ya kisheria..unaona hapo..’akasema.

‘Sasa huyu msaidizi wake,…ni tatizo, yeye ni mtoto kama baba, unanielewa hapo…’akaniangalia

‘Bado sijakuelewa…’nikasema

‘Ni hivi huyo kijana kamlanda baba yake sio kimatendo tu, bali pia na yeye aliamua kusomea sheria..na ni wakili pia…’akasema

‘Mhh..kwahiyo…’nikasema

‘Na hata tabia za kazi ni kama alivyo baba yake, utafikiri alimfunza hiyo tabia, si unamuelewa marehemu alivyokuwa, basi mtoto ndio zaidi, na kiumri hajapitana sana na kijana wangu…’akasema

‘Sawa kwani kuna tatizo gani hapo, sioni tatizo maana sina jambo na yeye, hayo ni yenu ya kifamilia au sio, au unataka kusema nini hapo…’nikasema

‘Mengi yaliyopitishwa kwenye kikao cha kifamilia yeye alikuwa mpingaji sana, yeye alitaka kila kitu alichosema marehemu kitekelezwe hasa kikiwa kwenye maandishi, mkataba…, unajua nilimuambia kijana wangu mapema awe tayari kwa hili, kwahiyo mambo mengine asiyaweke wazi…’akasema

‘Kwanini sasa na ni haki ya kila mtu au sio, haikuwa na haja y akuficha jambo…’nikasema

‘Wewe ni mungu tu alituongoza, maana huo mkataba wa kuelezea kuwa kuna ..hizo kwenye makampuni yenu, haukuwahi kwenye hicho kikao, kijana wangu alikuja kupewa baadae na kwahiyo hilo halikuzungumzwa siku hiyo..siku hiyo ilikuwa ni madeni, na watoto hao wa nje waliposikia madeni ni mengi kuliko mali za kurithi, wakaondoka mmoja mmoja, maana kijana wangu aliwaambia kila mtu akubali kushika sehemu yake ya deni,…nani akubali hapo, hata huyo msaidizi wake akaondoka akidai ana kesi anafuatilia...’akasema

‘Kwahiyo…unataka kusema kuwa huo mkataba wa kugushi bado haujafika kwa warithi, kama huyo ..na wengineo ..ni vizuri, lakini mimi siutambui…’nikasema

‘Sasa huo mkataba halali upo wapi mdogo wangu…’akawa kama anauliza

‘Utapatikana tu dada….mume wangu atakuwa anafahamu upo wapi…’nikasema

‘Tatizo ni muda..mana sijui kajuaje …huyo mtoto, katupigia simu akidao kuwa tumemficha ukweli…sasa ni hivi kutokana na muda, kama kijana wangu akiondoka, kurudi ulaya kabla hatujamalizana na hilo, mtakuja kupambana na huyo mtoto, ni mkorofi kweli kweli, nina uhakika …hamtaelewana naye, ndio maana tunataka mambo haya yaishe haraka, iwezekanavyo, wewe kaa na mume wako myamalize haya mambo kwa haraka jamani, …’akasema

‘Kuisha haraka ni mume wangu…nimeshakuambia hilo, yeye ndiye anachelewesha haya mambo, kama nyie mnaweza kumshauri fanyeni hivyo, alete mkataba wa zamani, umenielewa hapo dada…’nikasema

‘Nilivyosikia, huu mkataba uliopo sasa nakala zipo kila mahali panahusika, sasa sio rahisi mtu kukubaliana na kauli yako, sijui unanielewa hapo…’akasema

‘Usijali, hilo litafanyiwa kazi..hamna shida …’nikasema

‘Mimi sitaki kubishana kwa hilo, ila ninachotaka kukisema hapa ni hivi…unajua huyo kijana ni mtata kwa sheria,…anapenda sana kesi, nina uhakika atawasumbua sana kwa hilo, na kama siku ile huo mkataba ungelifika mikono mwake, sijui uingekuwaje...’akatulia

‘Dada…’nikataka kusema na yeye akanikatisha, akisema;

‘Sisi kuwa kusaidia hilo, tumesema hatujui, hatuna uhakika, tutalifuatilia tukiupata basi tutamjulisha, lakini hakukubali, kasema huo mkataba tunaufahamu tumemficha…...ndio maana tunataka tulimalize hili haraka…’akasema

‘Kwahiyo mlitaka mimi nifanye nini..?’ nikauliza

‘Sisi lengo letu ni kuhakikisha kuwa huo mkataba unafanyiwa kazi, na kuondolewa kabisa,..mimi kwa ushauri wangu, kubali tu huo mkataba uliopo halafu tunaongea na wakili sisi kama familia tunajitoa, nyie sasa mtajua mnafanyaje na mume wako,..ni ushauri wangu huo…’akasema.

‘Msiwe na shaka na mimi, mimi simuogopi yoyote, ilimradi nipo kwenye haki yangu, wanachotaka kupata sio haki yao, au sio.....kama kweli huyo wakili na anaifahamu sheria, tutaangalia ukweli upo wapi na haki itatendeka, lakini kama ndio hawo wenye tamaa..basi tutapambana hadi mahakamani, hilo usijali kabisa…’nikasema.

‘Lakini muda sasa, na gharama…kijana wangu anaondoka hivyo, lifikirie hilo kwa makini..’akasema.

‘Sawa nimekuelewa...’nikasema na mara simu yangu ikalia, nilipoangalia nikaona ni namba ngeni kwenye simu yangu,, ...sikutaka kuongea na mtu nisiyemfahamu kwa muda huo...tukaagana na mgeni wangu huo, huku simu inaendelea kulia, baada ikakatika, ..baadae kidogo ikaita tena…, nikapokea na kuuliza

‘Nani mwenzangu...?’ nikauliza

‘Mimi ni mtoto wa marehemu Makabrasha....’akasema

‘Yupo huyo..na unasemaje?’ nikuliza

‘Nimesikia tetesi kuwa kuna mkataba unaoonyesha kuwa marehem alikuwa na hisa kwenye kampuni zako, ni kweli si kweli…?’ akauliza

‘Mimi sijui hilo, ni nani kakuambia..?’ nikauliza

‘Wewe si mmoja wa wakurugenzi, kwanini hujui, na ni haki yetu kaam warithi kulifahamu, je ni kweli au si kweli…?’ akauliza

‘Nimeshakuambia mimi sijui…je ndio taratibu za mirathi zipo hivyo, wewe kuuliza hivyo tu kwenye simu,..unajua sheria wewe..?’ nikauliza

‘Naifahamu sana, mimi ni wakili, nimekuuliza hivyo, kwasababu kuna hali inayoendelea kwa kiongozi wetu wa familia, analifahamu hilo na alilificha, sasa natafuta ukweli, ili sheria ichukue mkondo wake…’akasema

‘Kwa kifupi, fuata sheria, ongea na kiongozi wenu, na ikibidi ongeeni na wakili wetu, unanielewa,…’nikasema

‘Nasema hivi kama marehemu alikuwa na hisa kwenye kampuni zako, inatakiwa utuambie, utupe memorandum, na vielelezo vyote vinavyostahiki, ili tuweze kuorodhesha kwenye madai yetu, ndio maana nikakuuliza ili kuupata huo ukweli..’akasema

‘Na mimi ndio nimekupatia hilo jibu…’nikasema

‘Sawa mimi nitafuatilia kuupata huo ukweli, na kama kuna njama zozote za kuuficha ukweli, basi, sitasita kwenda mbele ya sheria…’akasema

‘Na samahani nikuulize tu, ni nani kakuambia mambo hayo?’ nikamuuliza

‘Nimesikia tetesi, hata kwenye kikao walisema kuna mikataba mingine haijapatikana, wanaifuatilia…., niliwaambia mimi ni wakili wanipe mimi nifanye ufuatiliaji wakachelea kunipatia, sema siku ile nilikuwa na kesi nyingine ya haraka siweza kusubiria.., lakini sasa nipo na nafasi, nataka kuuona huo mkataba...’akasema

‘Unasema ulisikia tetesi,..na unadai wewe ni wakili, unajua mambo hayo ya kisheria yanafuatiliwaje au sio..au wewe tetesi tu kwako ni sababu, je ukisikia tetesi kuwa wewe sio mtoto halali wa marehemu utasemaje…?’ nikamuuliza.

‘Unasema nini?’ akauliza kwa hamaki

‘Kuna tetesi kuwa wewe sio mtoto halali wa marehemu, wewe ni mtoto wa kusingiziwa, je unazikubali hizo tetesi?’ nikamuuliza.

‘Sikiliza mimi nakuuliza mambo ya muhimu wewe unaleta mzaha, sikiliza mimi nafahamu sana sheria, kama ni kweli, huo mkataba una haki zetu, nakuhakikishia mimi nitafika hadi mahakamani…sasa kwa vile umejibu ki-huni, nakupatia wiki moja tu, hilo liwe wazi, na ...hizo tetesi zako, hawo waliokuambia waambie, hawana akili kwanini hawakusema hivyo wakati marehemu yupo hai...’akasema.

‘Nilikuwa nataka kukuonyesha kuwa tetesi sio ukweli wa mambo, kama ulisikia tetesi kuwa kuna mkataba kama huo wa halali wa hivyo unavyosema, ilibidi ufuatilie kwanza sehemu husika..na ni vyema ukamuona wakili wenu, kwani si mna wakili anayefuatilia mambo yenu ya kifamilia..’nikamwambia.

‘Mimi mwenyewe ni wakili, ndiye nimeteuliwa katima mambo ya kisheria, lakini siku ile walinificha hilo jambo, sasa nimeanza kulifuatilia mpaka nione mwisho wake...’akasema

‘Sawa, kama unaona ni haki yako fuatilia, ...ila ni vyema ukawa na uhakika na hicho unachokidai,..sawa muheshimiwa..’nikamwambia.

‘Sawa …ila nitegemee kukuona, siku yoyote naweza kuja kuongea na wewe kaika kulifuatilia hilo, nataka nionane na wewe uso kwa uso,….jiandae kwa hilo….’akasema na kukata simu.

NB: Tuhitimishe? sehemu hii ilihitajia marekebisho mengi..lkn hatukupata muda,....


WAZO LEO:Kunapotokea mzazi mmoja kufariki hasa wa kiume, kuna watu wanajitokeza kudai, mali wakisema na wao wana haki ya urithi, watu hawa wakati wa uhai wa merehemu, walikuwa hawaonekani, na zaidi inawezekana kabisa marehemu alikuwa akiumwa kwa muda mrefu, lakini hawakuwahi kufika, angalau hata kusaidia kidogo, hata angalau kutoa pole, mpaka mzazi huyo nafariki.

Watu kama hao huja kujitokeza baadae wakati wa mirathi. Je huo urithi, umetokea wapi, ukumbuke hiyo mali ilitafutwa na watu, na ni hawo hao waliohangaika na marehemu, wenye uchungu naye…, wewe unakuja baadaye unadai, mali, hiyo mali kwako itakuwa sio halali ...ni vyema tukajua kuwa, kila penya faida kuna gharama zake pia.

Ilikuwa siku maalumu ya kupokea taarifa kutoka kwa watu wangu, kuna vijana huwa nawapa kazi zangu, kwa kuwaamini, hasa zinazohusu mambo yangu binafsi, hata ya kikazi pia…nilifika ofisini na kumwamboa katibu muhutasi kuwa hao vijana wangu waitwe mmoja mmoja…na wakati nipo tayari, mara mlango ukagongwa...

‘Unaweza kuingia..’nikasema

Akaingia jamaa mmoja…yeye ni mtu wa masoko, lakini pamoja na kazi hiyoo yeye nimatumia kwa mambo ya uchunguzi ikibidi..ana utaalamu huo, na nilishampeleka shule kusomea upelelezi kidogo, inasaidia kwa kazi zangu…Nilimwambia kuwa nataka asomee upelelezi kidogo, kwa nia ya mashindano ya kibiashara, lakini pia nataka anisaidie kwenye kazi zangu.Tunaelewana sana.

‘Kutokana na uchunguzi wangu, mtu aliyechukua huo mkataba atakuwa ni mtu wa humo humo ndani, alitumiwa,…maana hakuna mtu wa nje aliyweza uingia kwenye ofisi yako, akaonekana…’akasema

‘Huyo mtu wa nje ni nani, uliweza kumtambua …?’ nikauliza

‘Imekuwa ngumu kidogo…’akasema

‘Je ni nani aliwahi kuifika kati ya watu niliokuambia uwachunguze, ?’ nikamuuliza

‘Mtu ambaye aliweza kufika mara kwa mara ni docta Yule unayemuita Rafiki wa mume wako,…’akasema

‘Ehe…je uliweza kufahamu, kama aliweza kuingia ofisini kwangu au kuongea labda na mfanyakazi wangu wa usafi…?’ nikamuuliza.?’ nikamuuliza

‘Yeye hata wakati ukiwepo alikuwa akifika kama alivyofika kipindi hiki…yeye hufika kwa minajili ya kikazi, akifuatilia malipo yake ya matibabu ya wagonjwa, ya wafanyakazi wako, na mara zote alizofika alikuwa akiishia mapokezi....’akasema.

‘Una uhakika na hilo…?’ nikamuuliza

‘Kwa uchunguzi wangu naweza kusema hivyo, sizani kama aliweza kuingia ofisini mwako,…’akasema

‘Mwingine ni nani…?’ nikamuuliza akilini mwangu nikianza kujiuliza kama docta anaweza kufanya kitu kama hicho, haiwezekani, kwasababu hana faida yoyote na huo mkataba…labda kumsaidia rafiki yake…hapana haiwezekani.

‘Na mwingine aliyeonekana, ni bosi, nina maana ....rafiki yako, kuna kupindi alifika kabla hajaondoka kusoma na pia aliporejea,..’akasema

‘Aliporejea..!?...alifuata nini…?’ nikamuuliza

‘Alikuja akikuulizia, lakini hakuweza kuingia ndani ya ofisi yako, naye aliishia mapokezi, na hakukaa sana, kwani aliambiwa haupo....’akasema

‘Na kabla…?’ nikauliza

‘Kabla ni kipindi ukiwepo, au…kama haupo, anaishia mapokezi tu…..’akasema

‘Kwahiyo hakuna mtu yoyoye mwingine ambaye tunayemshuku, aliyeonakana akiongoea na mfanyakazi wangu wa usafi, ambaye ndiye anayetunza ufunguo za ofisi yangu?’ nikamuuliza

‘Tatizo ni kuwa huyo mfanyakazi wako wa usafi, anaongea na watu wengi sana, sasa sio rahisi kuhisi yupi ni yupi, hata nilipotumia mbinu za ziadi kupata taarifa kwake, ilionekana kama tunamshutumu mtu ambaye hajafanya jambo kama hilo, nina uhakika kama ni mtu aliingia, yeye atakuwa hajui kabisa..’akasema.

‘Sasa alipaje ufunguo….?’ Nikauliza

‘Hapo hatukuweza kupata ukweli,….’akasema

‘Ina maana kwa uchunguzi wako,…maana nimekupa kazi hiyo ili nimpate huyo mtu, wewe umegundua nini, angalau kidogo cha kusaidia…au umeshindwa kumpata…?’ nikamuuliza

‘Mwanzoni nilimuhisi katibu wako muhutasi, kwasababu yeye ana haki ya kuingia na kutoka ofisi kwako, lakini nilipofuatilia nyendo zake, niliona hahusiki, maana alikuwa likizo kipindi chote hicho ambapo wewe hukuwepo ofisini.’akasema

‘Kwa kifupi bado hujamgundua ni nani alifanya hivyo..?’ nikauliza

‘Kiukweli bado bosi, tatizo wewe hutaki tufanye tuonavyo sisi, wewe umeteka tufanye utakavyo wewe sasa inakuwa ni ngumu kidogo, ukitaka tumgundue kwa njia zetu, tupe hiyo nafasi, tutampata tu,…’akasema

‘Hapana msifanye hivyo, nilitaka kufahamu mambo machache kutoka kwenu sitaki kuleta utata kwa hili, unanielewa, basi tusipoteze muda, wewe endelea na kazi zako…’nikasema

‘Sawa bosi….’akasema hivyo na kuondoka.

Wa pili alikuwa mtu ambaye nilimpa kazi ya kuchunguza nyendo za mume wangu kipindi hicho, kabla hajapata ajali..akasema;

‘Siku mume wako alipopata ajali, alionekana akiwa katokea maeneo ya rafiki yako,kwahiyo huenda alipita hapo,au alitokea hapo kwa rafiki yako ...’akasema

‘Huna uhakika kuwa alitokea kwa rafiki yangu…?’ nikauliza

‘Uhakika wa moja kwa moja haupo…kwasababu hakuonekana akiingia au kutokea kwenye nyumba ya rafiki yako,…’akasema

‘Kwahiyo ni kweli kuwa alipita tu…?’ nikauliza

‘Mara nyingi yeye anasafisha gari lake kwa muosha magari karibu na anapoishi rafiki yako,…cha ajabu muosha magari, japokuwa hayupo, lakini nilimfuatilia mpaka huko kijijini kwao, nikaweza kuongea naye, hakuataka kabisa kuongea na mimi, ila baada ya kumpatia chochote, ndio akaongea

‘Anasemaje..na kwanini kaondoka hapa Dar..?’ nikamuuliza

‘Anasema maisha yamemshinda tu, kaona akafanyie shughuli zake kijijini…’akasema

‘Ehe,siku hiyo ilikuwaje…akiwa kazini kwake,..hakuwahi kuosha gari la mume wangu..?’ nikamuuliza

‘Anadai hakuwahi kuosha gari la mume wako, hakumbuki kabisa..anasema yeye anaosha magari ya watu wengi, na sio kazi yake kukariri..lakini ana uhakika hakuwahi kuosha gari la mume wako, …’akasema

‘Ni kweli au anaogopa tu kusema ukweli..?’ nikauliza

‘Nimetumia kila mbinu hajakubali hilo, nahisi hakuwahi kuosha, au hakumbuki kweli, sizani kama angetuficha...’akasema

‘Kwahiyo ni kweli kuwa mume wangu alipita tu maeneo hayo na hakuwahi kufika kwa rafiki yangu..?’ nikauliza

‘Itakuwa hivyo, ila waliomuona akiendesha gari, wanasema alikuwa katokea maeneo ya huko, na alikuwa akiendesha kwa mwendo kazi sana, nikama vile alikuwa akiwahi jambo, na.....hakuwa amelewa kabisa, kwani ofisini kulikuwa na kikao, na alipotoka kwenye kikao hakupitia kwenye ulevi..’akasema

‘Hakupita kwenye ulevi, aliyekuambia hivyo, amejuaje, …ina maana alifahamu anapoelekea …alipokwenda mume wangu..?’ nikauliza

‘Wanafahamu wapi anapokunywa mara kwa mara..na hao walimuona akitoka ofisini, na kuendesha gari…kuelekea upande mwingine, hawakufuatilia,…na tulijaribu kutafuta mtu mwingine …hakuna aliyemuona akielekea kwa rafiki yako…’akasema

‘Hilo naweza kuamini kuwa hakuwa huko kwa rafiki yangu maana mimi mwenyewe nilikuwa huko, kama angelifika mimi ningelimuona.’nikasema

‘Sasa ajali yake ilitokea kwa vile alikuwa kwenye mwendo kazi, na alipokuwa akata kona..ndio akakumbana na hilo gari jingine..akafunga breki lakini zilikataa, ndio ikapatikana na hiyo ajali...., alikuwa mwepesi kuruka nje..,na wakati anatoka alionekana, akiwa na mkoba, .....’akasema

‘Aliruka kabla…mmh, hapo, unataka kusema nini, na huo mkoba wa…komputa au…?’ akauliza

‘Ni mikoba hii ya kawaida, na kwa vile aliumia sana, aliyekuja kumsaidia, anasema mume wako hakutaka kabisa kuachana na huo mkoba, na kuna mmoja alitaka kumsaidia, lakini akakataa,...’akasema.

‘Na alipofika mlangoni mwa nyumba yenu, alionekana kupiga simu,..ndio akaja jirani yenu mmoja…ndiye aliyemsadia hadi kwa nyumbani kwa docta..na huyo docta ndiye aliyemsaidia kwa huduma ya kwanza...’akasema.

‘Mlipochunguza nyendo zake za huku nyuma , mligundua nini?’ nikamuuliza.

‘Mara nyingi alikuwa akienda kunywa na rafiki yake, yule docta, na wakati mwingine akiwa peke yake, alionekana mpweke, na hakupenda kukaa na watu asiowafahamu…’akasema

‘Na zaidi ya huyo docta ni nani wengine alipenda kunywa nao…nikimaanisha wanawake labda?’ nikauliza

‘Kiukweli hao hawakosekani, wakiwa kwenye makundi, …lakini haikuonyesha wazi kuwa ana rafiki wa kike wa kupitisha naye muda…’akasema

‘Hakuna mwanamke ambaye alikuwa naye karibu sana..hakuna hata mmoja..?’ nikauliza

‘Mwanamke ambaye mara nyingi anakuwa naye karibu ni rafiki yako, huyo anayesoma huko nje, yeye mara kwa mara walikuwa wakionekana naye, najua hata wewe mwenyewe unalifahamu hilo, ni hata mkiwa wote yeye anakuwepo, au sio, huwezi kumshuku vibaya..na wengine ni wafanyakazi wake, au wa ofisi anayoifanyia kazi...’akasema.

‘Je mume wangu hakuwahi kumsindikiza rafiki yangu huyo hadi kwake,, na hata kuingia kwake, na hata kukaa kwa muda mrefu wa kutilia mashaka, au japokuwa kwa muda mfupi?’ akaulizwa.

‘Ndio, mara nyingi tu, huwa wanamfikisha kwake, na kuondoka, kuna muda wanafika na kukaa humo kwa kipindi kirefu tu, kwa vile ni rafiki yako, hatujaona kama kuna lolote baya, sizani kama wanaweza kuvuka mipaka, ulisema wewe unamuamini kwahiyo hata sisi tumechukulia hivyo....’akasema

‘Kwa uchunguzi wako, hakuna dalili zozote za mahusiano ya kimapenzi kati ya rafiki yangu, na mume wangu,..?’ nikauliza

‘Hatukiliona hilo…hawajawahi kulionyesha hilo hadharani…, maana hata wakiwa kwenye starehe, walionekana wakijali, kuheshimiana, na mume wako sio mtu wa kufanya mambo ya aibu anajichunga sana, kama alivyo rafiki yako, hatukuweza kulibaini hilo…’akasema.

‘Na huyo rafiki yangu hakuwa na mahusiano na mdogo wa mume wangu..?’ nikauliza

‘Kwa uchunguzi wetu, yaonekana rafiki yako hayupo karibu sana na huyo shemeji yako, na yaonekana kama hawaelewani kina namna fulani, kwahiyo haiwezekani wakawa wapenzi....’akasema

‘Haiwezekani, ina maana mume wangu hakuwa na rafiki mwingine wa kike.....sasa huyo mtoto ninayesikia anaye ni kutoka kwa mwanamke gani?’ nikauliza

‘Mtoto…mmh, hapana, ..kwa uchunguzi wetu, ....hilo halikuweza kuonekana, kwani kama ulivyotaka, ni kuwa tuchunguze bila kuweka tetesi, tuwe na uhakika na hicho tulichokifanya, na sisi hatukuona au kugundua mwanamke mwenye mahusiano na mume wako…’akasema

‘Na ni kweli mumegundua kuwa hana mtoto nje…?’ nikauliza

‘Hilo hatujaligundua, hatuwezi kusema kitu ambacho hatuna uhakika nacho kama ulivyotaka..kama unataka tulifanyie kazi hilo, kuwa kama ana mtoto nje, tunaweza kulifanyia uchunguzi, lakini kwa mipaka uliyotuwekea sisi hatujagundua chochote kuhusu mtoto wa nje…’akasema

‘Sawa, ndivyo nilitaka,…sikutaka hayo myafanyie kazi, kama kesi, hakuna kesi hapa ni kutaka kujirizisha tu,..ila kuna kitu nataka unifanyie, nenda huko alipojifungulia huyo rafiki yangu uone kama utagundua baba wa huyo mtoto wake, je alizaa na nani, unaweza kulifanyia kazi hilo…?’ nikamuuliza

‘Naweza bosi…’akasema

‘Unajua …awali sikutaka ulifanye hilo, sasa kalifanyie kazi, na pili, utafute kama kweli mume wangu ana mtoto nje, mmh, yah, lakini usifanye kuonyesha mimi nataka kulifahamu hilo, chukua muda, unanielewa…’nikasema

‘Sawa nakuelewa bosi, ila kuna kitu, nilitaka kukuambia,....ila wewe ulisema tusihangaike sana na rafiki yako na ..na…’akasita kidogo

‘Niambie ni kitu gani…?’ nikauliza

‘Ulisema haina haja ya kumchunguza rafiki yako, na ulisema kuna mwanaume aliwahi kufika hospitalini,..wa kwanza, kuna kitu kama hicho, ila ulisema haina haja ya kulichunguza hilo, lakini kwa uchunguizi wetu mwanaume wa kwanza kumtembea pale hospilaini alikuwa ni mume wako, hakuna mwingine …..’akasema.

‘Unasema kweli,…haiwezekani, mbona rafiki yangu alinificha hilo.., na hata mume wangu, mmh..hapa kuna kitu,..una uhakika na hilo..!?’ nikauliza kwa mshangao

‘Ndio…nina uhakika na hilo…’akasema na alitaka kuongea jambo, lakini mimi nikamtiza kwa swali jingine

‘Je vyanzo vyenu viliwahi kumuona mtoto wa rafiki yangu, kisura,..anafananaje?’ akaulizwa

‘Ni kitu ambacho wengi wetu waliona ni ajabu, kwani mtoto huyo amekuwa akifichwa sana, hajawahi kuonekana sura yake na mtu yoyote....’akasema

‘Haiwezekani, ina maana na ujanja wenu wote hamkuweza kuiona sura ya huyo mtoto wake, hajawahi kupiga picha, ?’ nikawauliza

‘Unamfahamu sana rafiki yako huyo, kazi za uchunguzi, ulinzi na usalama anazifahamu sana, na akiamua kufanya jambo, analifanya kwa makini sana, nahisi hakupenda kabisa mtu kuiona sura ya mtoto wake…’akasema

‘Mhh..haiwezekani, kwahiyo nyie hamjafahamu yupo je…?’ nikamuuliza

‘Wengine wanasema ana sura ya kihindi, wengine ana sura ya kizungu,…sasa hatujui kwakweli, nahisi basi atakuwa akimvalisha vitu ambavyo huwezi kabisa kugundua sura ya mtoto ya asili, nahisi alikuwa akimvalisha nywela za bandia hata sura za bandia....’akasema.

‘Sura ya kihindi, hahaha..hapana mimi nimemuona ni mwafrika kabisa…’nikasema

‘Ndivyo watu waliobahatika kumuona wanadai hivyo…’akasema

‘Unahisi ni kwanini amefanya hivyo....?.’nikawauliza

‘Huenda hataki baba wa mtoto huyo ajulikane, au huyo baba amfahamu huyo mtoto kuwa ni wake...’akasema

‘Kwanini?’ nikamuuliza

‘Huenda ni kuogopa kashifa... Au yeye mwenyewe rafiki yako hataki baba wa mtoto huyo afahamu kuwa ni mtoto wake....’akasema.

`Nashukuru, huenda nikakuhitajia tena, endelea na uchunguzi....’

*******

Baadaye alikuja mtu ambaye nilimpa kazi ya kuchunguza kifo cha Makabrasha, yeye aliwahi kufanyia kazi za upelelezi, lakini kwasababu za kiafya akaacha kazi, ..na hata alipopona hakutaka tena kuirudia hiyo kazi, akawa anafanya kazi hiyo binafsi, na yeye akatoa taarifa yake.

‘Kifo cha Makabrasha, kimefunikwa kiaina, nahisi hata polisi walishachoka na tabia ya huyo mtu, na waliona kufa kwake ni bora tu, japokuwa walifanya juhudi ya kumtafuta muuaji, lakini hawakufika popote, wakahitimisha walivyoona wao....’akasema

‘Kwanini unasema hivyo?’

‘Kwasababu ya matendo ya marehemu, kwani alifikia hatua ya kuwawekea hata hao polisi mitego, akiwanasa kwenye mambo yanayoenda kinyume na maadili ya kazi zao, anawarekodi, na huja kutumia kumbukumbu hizo kuwatishia, kuwa wakifanya lolote na yeye atawalipua, kwahiyo hata wao, wakawa hawana jinsi, ila kufuata anavyotaka yeye....unaona eeh..’akasema

‘Kwahiyo unataka kusema nini?’ nikamuuliza

‘Ninachotaka kukuambia ni kuwa ukweli wa kifo cha Makabrasha hautaweza kugundulikana kiraisi unaweza ukaweka shaka shaka kuwa huenda hata hao watu wa usalama wanajua kitu fulani,lakini hawataki..kiukweli, haipo wazi, na hata wao hawajachukulia kifo chake kwenye uzito wake...’akasema

‘Haiwezekani, ina maana watu wa usalama wanaweza kuhusika..hiyo dhana unaiwekaje hapo…?’ nikauliza

‘Sijasema wanaweza kuhusika, ila wanaweza kujua jambo..unielewe hapo..’akasema

‘Sasa ni nani anaweza kuhusika kwa uchunguzi wako, sizani kama muuaji anaweza kupotea hivi hivi..?’ nikauliza

‘Huyo muuaji aliyefanya hayo mauaji, ni mtu ambaye alijua ni nini anakifanya, na inaokena sio mauaji ya kukurupuka, ni mtu alijiandaa kwa muda mrefu, huenda alikuwa kwenye hilo jengo, siku mbili kabla akimvizia..’akasema

‘Kwa vipi…?’ nikauliza

‘Ni lazima huyo mtu awe anafahamu taratibu zote za marehemu, ratiba yake, na..anafahamu mfumo mnzima wa mawasiliani, na mfumo wa jengo na ofisi ya Makabrasha...’akasema.

‘Mapka kufahamu mfumo, ina maana basi anaweza kuwa alihusika na ujenzi wa hilop jengo au..?’ nikamuuliza

‘Anaweza asiwe ni mjenzi, badi ni mtu aliyelisoma hilo jengo…maana ukisema ni mjenzi wa hlo jengo, huyo jamaa tunamfahamu, na kwa muda sasa wapo mikoni kuna ujenzi wanafanya huko, lakini wanaweza kuuza siri za mjengo huo,..huyo mtu aliyefanya hayo mauaji sio wa kawaida, ni mtaalamu kweli kweli.....kwani kwa jinsi alivyoingia, na kwajinsi alivyoweza kusoma mfumo wa mawasiliano, na mtandao uliokuwa umewekwa humo ndani,, ...sio mtu wa kawaida....’akasema

‘Haya niambie kutokana na uchunguzi wenu Makabrasha aliuwawa kivipi, na kwanini?’ nikamuuliza

‘Huyo mtu inawezekana alikuwepo humo ndani kwa siku mbili kabla, kama nilivyosema, na silaha aliyoitumia, itakuwa ililetwa usiku wake, na ikaingizwa kwa kupitia nyuma ya ukuta....’akasema

‘Kwanini unasema hivyo..?’ nikauliza

‘Kwasababu kama ingelipitia kwenye njia ya kawaida, kupitia mlangoni, ...kungelitokea milio ya kuashiria hivyo.....kuna mfumo mle ndani, wa kugundua kuwa mtu kabeba kitu cha hatari, kuna mfumo wa kuchukua kumbukumbu za matukio, ina maana kila anayeingia ataonekana,..lakini cha ajabu siku hiyo ya tukio, hayo yote hayakuonekana kwenye mtandao uliowekwa humo ndani...’akasema.

‘Ili uingie kwenye jengo hilo kuna njia moja tu, na ukishaingia kwenye jengo, ili upande juu, kuna njia moja tu, na huko kote waliweka vinasa matukio na sauti,..hebu fikiri, kote huko hakukuonekana hilo tukio, kumefutwa kabisa..ina maana huyo mtu hakutaka kabisa kuonekana chochote siku hiyo..

‘Na ina maana basi hata kama huyo mtu aliingia na silaha, ...labda akamuhonga mlinzi, lakini angelipita wapi na hiyo silaha, kwasababu mawasiliano ya kudhibiti hiyo hali ipo sehemu ya siri, huko juu, ...inawezekana basi walinzi wawe wamekula njama,...’akasema

‘Si ndio hapo hata mimi nashindwa kuelewa na kwanini polis wasimkamate hata Yule mlinzi, wangembana nahisi angeweza kuwafahamisha jambo..’nikasema

‘Alikamatwa, lakini hawakuweza kupata chochote kutoka kwake…’akasema

‘Pale mlangoni huwezi kuingia na silaha, pamoja na kukaguliwa na mlindi lakini pia kuna mtambo,...mtu akipita silaha, kuna kelele za kuashiria hatari, na hizo kelele, zingelijulikana kwa watu wote, pale huwezi kuingia na silaha mle ndani kabisa,....’akasema.

‘Sasa hiyo silaha iliingiaje humo ndani…?’ nikauliza

‘Hiyo silaha itakuwa ilipitishwa nyuma ya jengo, na walichofanya ni kutengeneza kamba ndefu, iliyoshuka hadi chini, na mtu aliyekuwa chini, akaifunga ile silaha kwenye hiyo kamba, na huyo aliyekuwa juu, akavuta hadi juu, na kuhakikisha, haipiti sehemu zenye kuhisi au kugundua kitu cha hatari..na huenda kwa muda huo, huyo mtu alikuwa keshazima viwambo vya hatari vya ndani....’akasema.

‘Mtu huyo asingeliweza kuzima viwambo hivyo kwa jengo zima, walinzi wa chini wangeliona hilo, na wangeliweka kwenye taarifa zao, hakuna taarifa kama hiyo, na hata tulipojaribu kufanya uchunguzi kwa watu hao, haukukuwa na dalili zozote kama hizo siku hiyo...’akasema

‘Kwahiyo muuaji, atakuwa alikuwa ndani, na muda ulipofika, akafanya kazi yake kirahisi, akaondoka..na cha ajabu basi hata tukio lenyewe,hilo la mauaji halipo...polisi wanadai kuwa walioona baadhi ya sehemu ya tukio hilo, lakini sio kweli..hakuna kitu kama hicho,...kuna mtu aliyekuja kuondoa kila kitu...cha siku hiyo, na huyo mtu alifahamu ni nini anakifanya , ...’akasema.

‘Kwahiyo hamkuweza kugundua lolote, kwa njia zenu, kuwa huenda mtu fulani anaweza kuhusika?’ nikamuuliza.

‘Huyo aliyefanya hivyo ni mtaalamu, kweli..hatukuweza, na kwa vile polisi wenyewe wamesalimu amri na kuona kuwa ni kifo cha kulipiza kisasi, mimi naona haina haja ya kuhangaika sana..ila kuna kitu ninachoshangaaa,...’akasema

‘Kitu gani....?’ nikauliza

‘Siku ile ya tukio, kuna watu wanasema kuna mtu, japokuwa alijibadili, lakini anafanana na mume wako kimaumbile’akasema

‘Unataka kusema nini hapo?’ nikamuuliza

‘Mume wako alikuwepo kwenye hilo jengo, wakati tukio hilo linafanyika, na polisi hawakuligundua hilo, ..kama wangeligundua hilo, nina imani kuwa mume wako angelikuwa hatarini, wangemshika....mimi nilijaribu kufanya uchunguzi wangu, na hata kuongea na mume wako, lakini hakutaka kutoa ushirikiano...je kuna njia yoyote naweza kuongea naye,...?’ akaniuliza.

‘Hapana, haina haja, inatosha....’nikasema.

‘Lakini nina uhakika sio yeye aliyefanya hayo mauaji, ila nahisi atakuwa anamfahamu huyo muuaji....’akasema

‘Kwanini unasema hivyo?’ nikamuuliza

‘Mume wako sio mtaalamu sana wa kutumia silaha, huyo muuaji, anafahamu kutumia silaha, na alifahamu wapi pa kulenga, ...ni mtaalamu kweli kweli, na alijua akilenga wapi mtu haponi....na kwahiyo huyo mtu atakuwa kapitia jeshi au kitu kama hicho, sio raia wa kaiwada tu..ni mtu anayefahamu ni nini anakifanya.’akasema

‘Nashukuru kwa taarifa yako....’ nilisema hivyo, na sikutaka kujua zaidi,…na hasa niliposikia kuwa mume wangu keshagundulikana kuwa alikuwepo humo kwenye jengo, na ina maana hata polisi watakuwa wameshagundua, sasa ni kwanini hajamkamata…

Nilihitajia muda wa kuliwazia hilo, na huyo jamaa akawa anataka kuondoka, halafu akasema;

‘Yule mdada, rafiki yako…unamuamini sana…?’ akauliza

‘Kwanini…?’ nikauliza

‘Nakuuliz tu…kuna kitu nimekigundua, nitakuja kukuambia, lakini kwa hivi sasa bado sijamuelewa, ndio ni mtu wako wa karibu, lakini…kuna kitu simuelewi..mbona walikuwa karibu sana na marehemu…’akasema

‘Kwa vipi…?’ nikamuuliza

‘Kuna matukio mbali mbali wameonakana wakiwa pamoja, wanaongea, na mara nyingi, rafiki yako anakuwa hayupo wazi kuonekana, ina maana wanaongea kwa siri, na hataki watu wafahamu kuwa anawasiliana na huyo marehemu…’akasema

‘Kwani siku hiyo ya tukio walionekana na marehemu…?’ nikauliza

‘Ndio..lakini kwa njia hiyo hiyo…’akasema

‘Unahisi yeye anaweza kuwa muuaji…?’ nikauliza

‘Sijasema hivyo, na wala haijagundulikana hivyo,…na hawezi kufanya kosa hilo.. lakini ngoja nilifanyie kazi, nipe muda,…’akasema

‘Nauliza hivi, kwa hisia zako mpaka hapo anaweza akawa ndiye muuaji..?’ nikauliza na huyo jamaa akaanza kuondoka, baada ya kutikisa kichwa tu,.. hakusema neno.


WAZO LA LEO: Dhana mbaya, au tetesi zisizo kuwa na uhakika, zaweza kukushinikiza kufanya jambo lisilo faa, tuweni makini sana na dhana, au mambo ya kusikia, hasa atika dunia hii ya utandawazi, ukisikia jambo, au kusoma jambo, lihakiki kwanza ukweli wake, kabla hujasema neno, au kabla hujaamini ukweli wake, fanya uchunguzi kwanza, ili kujiaminisha, usikimbilie kushutumu au kutoa kauli zenye kuumiza, kulaani au kuhukumu watu wengine.
 
SEHEMU YA 73

Tukumbukeni ulimi na kalamu(mitandao) inaweza kuwa ni chanzo cha fitina mbaya kwa jamii, tuweni makini sana kwa hili, siku ya hukumu kila kitu tutaulizwa, na kwanini tuwe sababu ya kuumiza wengine,..maandishi tu yaweza kuua, yanaweza kutesa nafasi ya mtu na huwezi kujua ni namna gani mtu huyo ataumia, mauimvu thamani yake ni kubwa sana, utawezaje kuilipa hiyo.

Tumuombe mola wetu atusamehe na atupe hekima ya kuandika membo yenye maana kwa jamii..!




Baada ya kuongea na watu wangu, nakuona hakuna kingine cha maana, nia ilikuwa kama nitapata kitu kingine cha ziada, lakini sikufanikiwa, zaidi ya yale ninayoyafahamu mwenyewe,…baadae, nikaona nitoke ofisini, nia ilikuwa kurudi nyumbani, nikapitia kwa fundi wa gari langu, nikamuachia ili lifanyiewe service, nikachukua bajaji, hadi kukaribia nyumbani kwangu.

‘Kabla sijapita kwangu nikachungulia ndani kwa docta, nikaona gari lake lipo, sijui kwanini leo yupo nyumbani, nikaona kama jirani mwema ngoja nimsalimie tu.

‘Bajaji nisimamishe hapa..chukua pesa yako, inatosha..’nikampa pesa yake na kwaharaka nikatoka kwenye bajaji na kuingia kwa docta, geti lilikuwa wazi, sikuona mtu nje, nahisi hata mfanyakazi wao hayupo…na wakati huo nikakumbuka maneno ya mtu wangu alipokuwa akitoa taaarifa….

Yeye hata wakati ukiwepo alikuwa akifika kama alivyofika kipindi hiki…yeye hufika kwa minajili ya kikazi, akifuatilia malipo yake ya matibabu ya wagonjwa, ya wafanyakazi wako, na mara zote alizofika alikuwa akiishia mapokezi…’

‘Ngoja niongee naye tu, lakini nina imani hana zaidi cha kunisaidia…’nikasema wakati huo nimeshafika kwenye mlango, nikagonga..

‘Fungua mlango upo wazi…’ilikuwa sauti ya docta

Ninajua kuwa mke wake hayupo, kwahiyo sikuwa na mashaka ya kuwasumbua, maana muda kaam huo wanakimama wengi wapo na pilika pilika za kuwajibina na familia zao kwa maandalizi ya usiku, ..

Nikaingia ndani, …alikuwa kalala kwenye sofa, akionyesha katingwa na mawazo, na nahisi alikuwa kachoka kutokana na kazi zake za kuwatibu wagonjwa,..alikuwa akiangalia…aliponiona kuwa ni mimi, akashikwa na mshangao, akasimama, tabasamu kwa mbali mdomoni..

‘Niambie hamna tatizo..maana nimechoka kweli..kuna tatizo..?’ akaniuliza akionyesha mashaka na kweli hata kusimama ilikuwa yaonyesha kachoka.

‘Nimekuja kwako mara moja, kuna maswali machache tu nataka unisaidie kunijibia, kama hutojali...’nikasema

‘Ok, afadhali…uliza tu zilipendwa wangu…, lakini ukumbuke tulishakubaliana, kuwa mimi sihitajiki tena kwenye mambo yenu wewe na mume wako au sio, hata mume wako alinijia juu sana, akanisema kuwa mimi nachangia kuivunja ndoa yenu, kwahiyo nimeona bora niwe mbali nanyi kidogo…’akasema akijihami

‘Ninachotaka kusikia kwako ni ukweli, ukiniambia ukweli, aah, mimi sina shida na wewe,...tatizo wewe huwa unanificha mambo ukijidai kuwa unanijali, kunijali gani huko, wakati unaona naharibikiwa katika maisha yangu…’nikasema

‘Ukweli gani unautaka kutoka kwangu shemeji, kuwa mkweli na wewe kwangu, nimejaribu kila niwezevyo, mlitaka mimi nifanye nini, eeh, niambieni..?’ akaniuliza.

‘Nataka kufahamu kuwa je ni kweli kuwa mume wangu ana mtoto mwingine nje..nina uhakika unalo jibu lake…niambie ukweli, ili nikuache upumzike,...?’ nikamuuliza

‘Unarudi kule kule...nakuomba utoke tu, kiukweli hapa nimechoka, kulikuwana kazi kubwa sana,..na akili yangu yahitajia, kitu cha kuniliwaza sio kunitesa…’akasema

‘mpigie simu mkeo aje…kwanini unamuacha anakaa kipindi kirefu huko, utaibiwa…’nikasema

‘Hahaha…nitaibiwa, akitaka siwezi kumzuia,..ndoa ni mwanandoa mwenyewe, hakuna mtu wa kumchunga mwanandoa zaidi ya yeye mwenyewe…’akasema

‘Ni kweli ndio maana nimekuja kwako, kwani unaweza ukawa na nadharia hiyo kichwani lakini mwenzako akakuchezea shere…je ni kweli mume wangu ana mtoto mwingine nje…ya ndoa..?’ nikauliza

‘Shemeji, haya ni matokea ya maisha yenu,…na sina jibu la swali lako, ila nina maelezo ya kukumbusha tu, kuwa hayo unayowaza, hiyo hali inayokusumbua ni matokea ya maisha yenu wenyewe…’akasema

‘Unajichelewesha mwenyewe, hutaki kupumzika…’nikasema

‘Ni lazima nikuambie hili, kuwa..nilishakuambia kuwa mume wako, alifikia kubadilika kutokana na jinsi mlivyokuwa mkiishi..sasa mimi sijui, huenda labda alikuwa na mahusiano na mwanamke mwingine, ila mimi simfahamu…’akasema akinyosha mikono ya kujitoa hivi.

‘Nasubiria jibu…’nikasema
‘Unajua ni hivi, mwanzoni nilihisi huenda mume wako kabadilika na kuanza kujiingiza kwenye mahusiano ya nje,lakini baadaye, nilipochunguza sana, nikaona kama hakuna ukweli ndani yake, huenda, kama waliwahi kufanya hivyo, basi ilikuwa ni bahati mbaya tu...’akasema

‘Ilikuwa bahati mbaya, kwa nani, hiyo kauli inaonyesha kuwa unamfahamu mtu aliyekuwa karibu na mume wangu,…kwahiyo nastahiki kuupata ukweli kutoka kwako, je ni kweli kuwa mume wangu ana mtoto nje ya ndoa, ni nani huyo, ?’ nikamuuliza

‘Nimekuambia kama iliwahi kutokea hivyo, mimi sikuwahi kuona, na kama ilitokea, basi ni siku mimi sikuwepo, kwasababu mimi nisingelikubali hilo litokee, unajua jinsi gani ninavyokujali…’akasema

‘Kwahiyo zile tetesi zako za awali, sio za kweli,…?’ nikamuuliza

‘Tetezi zipi hizo…?’ akauliza

‘Kuwa huenda mume wangu ana mahusiano nje…’akasema

‘Niliwahi kukuambia hivyo!! ? …hapana ulinichukulia vibaya, mimi nakumbuka kuwa nilikuonya tu , kuwa kwa mienendo yenu, kwa tabia zenu, za kuwa hata mkirudi nyumbani mnajifanya mpo bize, hamjali hata ndoa zenu ipo siku mume wako atakwenda kutembea nje ya ndoa, wewe si hujali, unajifanya huna hisia, sasa wanaume wengu kuvumilia ni shida, nilikuambia hivyo, au….’akasema

‘Na kwanini kila ukiwepo,…hasa kule hospitalini, kila nikitaka kumuuliza mume wangu aniambie ukweli, ulikuwa unamzuia, ni kama unafahamu jambo, lakini hukutaka mume wangu aniambie ukweli, ni kitu gani hicho, niambie ukweli, kwani baada ya hapa, naweza tusiwe na urafiki tena mimi na wewe…?’ nikamuuliza

‘Kwa kipindi kama kile, mimi kama dakitari, pia mimi kama rafiki yenu mkubwa, nilijitahidi kuzuia madhara, kwa mumeo na kwako, nakufahmu kama nilivyomfahamu mume wako, haikuwa na haja ya kuongea mambo yanayoweza kuamusha hisia na matokea yake yangelikuwa mabaya, ..’akasema

‘Hahaha..hata sikuamini, …kwanini lakini…’nikasema

‘Na ningekuzuiaje usiongee na mume wako wakati mpo naye siku zote…’akasema

‘Na kwanini ulimshuku rafiki yangu kuna anaweza akawa na mahusiano na mume wangu..bado nahisi wewe una ukweli hutaki kuaniambia,…niambie kama kweli wewe unanijali..?’ nikamuuliza

‘Awali nilikuwa na shaka hiyo...lakini nimekuja kufanya uchunguzi nikaona hilo halipo, na kama lipo,…mimi sijui, labda lilifanyika kwa siri kubwa sana, nimeongea na rafiki yangu, nikamuomba aniambia ukweli...hajataka kuniambia ukwelina tukaishia kukwaruzana, mpaka ananipiga marufuku ya kufika kwako, uelewe hali ilipofikia hapo…’akasema

‘Kwa kukukataa kwa mume wangu kukuambia ukweli ndio umerizika kuwa ni kweli hakuwa na mashusiano ya yeye, au unaogopa kusema kwa vile mumekwaruzana na mume wangu…?’ nikamuuliza

‘Pamoja na hilo, lakini kwa juhudi zangu nyingine nimeona hakuna kitu kama hicho, na mtoto wa rafiki yako, wengine wanasema ana sura ya kizungu, wengine mwarabu, sasa mume wako ni mwarabu, …kwakweli, baada ya yote hayo, nimeona niachane na nyie, mpaka hapo mtakaponihitajia…’akasema

‘Swali langu ni hili, Je ni kweli mume wangu ana mtoto nje..nijibu tu kwa kifupi, ili niondoke zangu?’ nikamuuliza

‘Mimi sijui, kwasababu hajawahi kuniambia hivyo...’akasema

‘Una uhakika na hilo…?’ nikamuuliza

‘Siwezi nikasema nina uhakika na hilo, je kama anaye, na mimi sijui, ukaja kugundua uaminifu kwangu kwako utakuwaje, nakushauri tu, hujachelewa, kwanini usimuulize kwa staha akuambie ukweli yeye mwenyewe…’akasema.

‘Mara nyingi unamkinga rafiki yako,…sasa unasikia, kama nikija kugundua kuwa ana mtoto nje utasemaje, ..maana kama anaye nina uhakika wewe unalifahamu hilo, ina unamficha siri rafiki yako, lakini kwanini hujiulizi na mimi je..itaniathiri vipi, je inaathiri vipi familia yangu, umejiuliza hilo…’nikasema

‘Kwa hali ile mliyokuwa mkienda nayo, na kwa tabia yake ile ya kulewa, kupitiliza, hilo siwezi kuona ni ajabu....kama nilivyokuambia awali, kwahiyo kama nikujilaumu jilaumu wewe mwenyewe,…....’akasema

‘Kwahiyo wewe huwezi kuona ajabu kuwa yeye ana mtoto nje, ndivyo mlivyo wanaume, je ni sahihi kufanya hivyo, je mimi ningelikuwa hivyo, mgelikubaliana na hilo…?’ nikauliza

‘Kwanini unaniuliza maswali hayo, kuna nini kimetokea shemeji hebu niambie ukweli…?’ akaniuliza

‘Mimi ninachotaka ni ukweli tu…’nikasema

‘Ukweli mimi sina..na zote hizo ni shaka shaka tu, na shaka shaka, zimekujaje kwako, wakati hupendelei tabia hiyo, usiige tabia hiyo utajitwika mzigo kabla haujatua kichwani mwako, utajiumiza mapema, kaeni wawili muongelee matatizo yenu yaishe…’akasema

‘Yataishaje wakati kuna matatizo mengi ambayo, nahitajia maelezo yake, yatakiwshaje wakati kama huu ambapo kuna mambo ya kuharibu kila kitu,.., kuna njama za kuhakikisha kuwa mali za familia zinachukuliwa na watu wengine, mimi sijui, na ni nani kaidhinisha hilo…’nikasema

‘Mhh..kwahiyo tatizo ni wasiwasi wa mali, au sio…?’ akauliza

‘Kutokana na mkataba wa kugushiwa, mali itagawiwa kwa watoto wa nje, kwa wtoto wa marehemu pia, na huyo mtoto wa nje ana haki sawa na watoto wetu…hayo kayaidhinisha nani,…mkataba wa kugishiwa unasema hivyo,…haya sawa, je ni kweli yupo huyo mtoto wa nje, mbona siambiwi ukweli, je kweli sina haki ya kulifahamu hilo….sio kwamba natetea mali, nataka kulifahamu je hiyo sio haki yangu….’nikasema

‘Hapo mimi siwezi kukusaidia kabisa, mkataba mliweka wewe na mume wako na wakili wako, au sio…hao ndio wa kupambana nao, na wala usiwarushie watazamaji mpira ukategemea kuwa watakusaiaid kufunga magali,..huo ni mchezo wako, cheza na mumeo au nimekosea hapo…?’ akauliza

‘Najua sasa utajiweka pembeni, ufurahia ndoa ikisambaratika, si ndio ulichokuwa wewe unakitaka, sawa, nitaucheza huo mpira mwenyewe, ..tatizo ni mkataba wangu upo wapi…’nikasema

‘Kwani ulikuwa haukusajiliwa..?’ akaniuliza

‘Ulisajiliwa na kwa taratibu zote kabisa..lakini sijui kilichotokea, ukaja kubadilisha, kila sehemu husika,..hata nakala yangu ya halali, ikapotea na kuwekewa nakala ya bandia,..’nikasema

‘Hata huko kwa mdhamina …haiwezekani…’akasema

‘Ndio hivyo…’nikasema

‘Kiukweli kutokana na majukumu yangu kuwa mengi, niliacha kabisa kufuatilia mambo yako, na hata wazazi wako wamesema tuachane na familia yako,kwa vile nawe umezidi kiburi, wanakuangalia tu, wameshasema utaweza mwenyewe na uskishindwa utawatafuta…’akasema

‘Sijashindwa bado…ila kuna hayo yaliyozuka kuwa mume wangu ana mtoto nje…hilo linanifanya niwe na wakati mgumu, na hataki kuniambia ukweli,..na kila hatua anazidisha matatizo, je nitaishi na matatizo haya mpaka lini, je nitaweza kuyavumilia…’nikasema

‘Nikuulize tu swali, Je kama ni kweli..unielewe hapo, mimi sijui, ila nauliza tu je kama huyo mtoto yupo utafanyaje…?’ akaniuliza

‘Kwanza nikufahamu ukweli,..hiyo ni haki yangu ya msingi,..kwasababu kama ni kurithi mali, hiyo mali, tumechuma wote..na mali hiyo imetokana na wazazi wangu, je ni haki kuitoa kwa watu baki, bila maelezo…sasa mimi nitafanyaje, hilo tulishawahi kuongea mimi na mume wangu,kutokana na hali ilivyo, ndio tukakubaliana kuwe na mikataba..kwahiyo kwangu haina shida, sheria itafuta mkondo wake…’nikasema

‘Na huo mkataba mpya unasemaje kuhusu hilo…?’ akaniuliza

‘Siutambui,..najua wameweka vipengele vya kujilinda, haina haja ya mimi kuupekenyua sana, haunihusu …’nikasema

‘Lakini mimi bado nina mashaka, maana hilo la mtoto wa nje, mara nyingi halina siri, watu hawawezi kulivumilia hilo, kama kweli angelikuwepo, hiyo taarifa iingeshavuma, ni kwanini iwe siri kihivyo...’akasema.

‘Ndio maana nilitaka kuufahamu ukweli kutoka kwako, maana mpaka inatokea hisia hizo, ina maana kuwa mume wangu alikuwa na mahusiano na mwanamke fulani, sasa kazaa naye au sio yeye, bado haijasaidia kuuficha ukweli kuwa mume wangu alikuwa akitembea nje ya ndoa, au sio...?’ nikamuuliza.

‘Kutokana na ulevi wake, yote yawezekana, ila nasema ukweli kutoka moyoni, kama ilitokea hivyo, basi siku hiyo mimi sikuwepo, kwa ushauri wangu shemeji, kuliko kujiumiza kihivyo, naona hilo achana nalo, litakupotezea muda, na mawazo mengi bure, kama yupo yupo tu....’akasema

‘Sasa hapo unataka kusema nini, kama yupo yupo tu, ina maana mimi nikubali tu hivyo kirahisi..na nikikubali unafahamu madhara yake, leo hii watu baki wameshaanza kugombea mali..wanayodhania ni ya baba yao..unahisi sababu ni nini, ni kwa vile watu mnakumbatia haramu…sasa ngoja niupate huo mataba wangu uone nitakachokifanya...’nikasema.

‘Mimi sijakumbatia haramu , mimi sijaunga mkono hayo, najua ni makosa, lakini ni nini chanzo cha hayo makosa, usije ukawa wewe ndio chanzo…’akasema akiangalia saa yake

‘Nikuulize swali hili, halafu niondoke zangu, awali ulisema kuwa utafany auchunguzi kugundua baba wa mtoto wa rafiki yangu, je uliwahi kuufanya…umegundua baba wa huyo mtoto ni nani..?’ nikamuuliza.

‘Hiyo imekuwa ni siri ya hali ya juu, na hata nilipokwenda kumuuliza dakitari aliyehusika naye siku ile sikuweza kupata lolote, hilo limekuwa siri kubwa sana,..na ni ajabu kutokea hivyo…lakini sikutaka kulifuatilia sana, kutokana na kauli yako wewe mwenyewe, nikajua huenda umeridhika na hilo, huenda wewe unahusika, nikuulize swali wewe si uliwahi kumuona huyo mtoto, je sura yake ipoje,....?’ akaniuliza.

‘Sura yake ipoje,!!!..haiwezi kunipatia uhakika wa swali langu maana sura yake inaweza kufanana nay a watoto wangu, ya watoto wa shemeji, ya….kwahiyo hilo bado halileti jibu sahihi…’nikasema

‘Kama ni hivyo, kwanini uumize kichwa chako, kumbe jibu unalo tayari, muhimu kwa sasa ni kumbana mumeo, au sio….tafuta njia ya kumfanya mumeo aongee, nina imani huwezi kushindwa hilo, au ..unahitajia msaada wangu…?’akasema na kuuliza

‘Kirahisi hivyo, unajua kilichotayarishwa na mume wangu,…tatizo sio hilo tu, ni baada ya kukubali hilo,…na hayo makubaliano ya kuwa haki ziende huko, kwanini mume wangu hakunishirikisha,…huo mkataba mpya ni wa nini…na kwanini hadi familia za marehemu zihusike, huoni kuwa kukubali kwangu kutaharibu mengi…’nikasema

‘Mhh…hapo kuna kazi..lakini..kama ni kweli, utafanyaje sasa, utavunja ndoa yako…?’ akauliza

‘Hayo sio muhimu kwangu kwa hivi sasa… , muhimu kwangu ni kuufahamu ukweli kwanza…na pili muhimu kwangu ni kuwa na huo mkataba wetu wa asili, basi, baada ya hapo kila kitu kitajimaliza chenyewe, na matatizo yataisha..swali ni kwanini ukweli unafichwa, kuna nini kimetayarishwa, mume wangu anaogopa nini…’nikasema

‘Jibu ni tahisi tu…anaogopa huo mkataba wenu wa awali…’akasema

‘Ok…nimekuelewa…’nikasema

‘Mimi nakushauri hivi, kwa vile mume wako kajirudi, ..achana na mambo hayo, ya kumchunguza chunguza sana…kwasababu hilo limeshamuweka kubaya, sasa hivi anatapa tapa..na huwezi kujua zaidi ya hapo ana malengo gani…’akasema

‘Kwahiyo..?’ nikauliza

‘Yavutie subira, kubali kwanza kwa nia ya kuupata ukweli, baada ya hapo, utajua mwenyewe la kufanya…’akasema

‘Huo ni mtego…mimi siwezi kujiingiza kwenye mtego wa tembo..sina uwezo huo…muhimu nitasimamia kwenye ukweli na haki…’nikasema

‘Ni sawa, lakini nilikuambia, je kama hayo yote ni matokea ya wewe mwenyewe utasemaje…?’ akanuliza

‘Hivi, ..mume wangu ni mtoto mdogo, au hao alioshirikiana nao ni watoto wadogo, hawafahamu njia sahihi…unataka kusema mtu akikuambia ule mavi utakula, kwa vile umeshauriwa na rafiki yako mpenzi…hilo sio swali la kuniambia hivyo, kuwa huenda inatokana na mimi..’nikasema

‘Una maana gani..ina maana kuwa kuna mambo yamtokea hapo kutokana na ushauri wako, au…niambie ukweli…’akasema

‘Unanipotezea muda wangu swali jingine kabla sijaondoka je wewe uliwahi kuongea na wazazi wangu hivi karibuni?’ nikamuulzia

‘Jana tu, nilikuwa na wazazi wako…tulikuwa na kikao kirefu tu mimi na wao…’akasema

‘Wanasema nini juu ya hili tukio...?’ nikamuuliza

‘Wao wameamua kukuachia mambo yako, ila wanachoogopa ni kuwa mume wako anaweza kukuingiza kwenye kashifa kubwa, wanahisi hiyo iliyotokea ni ndogo tu…wanaweza kuihimili…, lakini baadaye kunaweza kukazuka mambo ambayo hata wao hawatataka kuyasikia..si unamfahamu baba yako alivyo....’akasema

‘Kwahiyo wao wanashauri nini?’ nikamuuliza

‘Unafahamu msimamo wa wazazi wako toka awali, msimamo wao ni ule ule, hawana imani na mume wako, hilo, sio wao tu, hata wale waliopo karibu na baba yako wanamuonya dhidi ya mume wako,..sasa sijui, ..’akasema na kutikisa kichwa.

‘Mhh..najua tu, hayo ni mambo ya kisiasa, na likitokea wanavyotaka wao, bado italetwa ajenda nyingine, …’nikasema

‘Unajua kuwa wazazi wako wamegundua kuwa mume wako sio mkweli, na ana tamaa, na anaweza akaharibu maisha yako ya baadaye, kuna kipindi waliniomba niingilie kati, ikibidi, ....ooh, sipendi huo ushauri wao’akasema

‘Ikibidi nini..?’ nikauliza

‘Wao, wanazidi kusema kuwa ndoa yako na mume wako haifai,…itakuja kukuumiza sana, na huenda, usiwezi kufaidi matunda ya jasho lenu,..mumeo, ana watu wanaomzunguka, na kumtumia yeye kama daraja, …yeye bila kulifahamu hilo anakubali tu,..mwisho wa siku watamtekeleza, kifupi wao, wanaona ni bora, ndop hiyo ivunjwe, kwa masilahi ya kizazi cha baadae,...’akasema.

‘Hivi nyie mnaona kuwa hilo jambo rahisi sana...?’ nikauliza

‘Ni ushauri wao,..ni ushauri wa marafiki za wazazi wako, ni ushauri wa ….kila mtu mwenye nia njema na nyie… ila hawajataka kukushinikiza kwa vile baba yako yupo kwenye ushindani wa kisiasa…hataki kujiingiza sana kwenye ndoa yako,…’akasema

‘Mimi siwezi kulisikiliza hilo kwa vile yule ni baba wa watoto wangu, ...hamuoni kuwa nikifanya hivyo, nitawaumiza watoto wangu, kwanini hamliangalii hilo pia, sio kwangu tu, je kwa watoto wangu, watoto wangu wanampenda sana baba yao..’nikasma sasa nikitamani hata kulia.

‘Usijiweke mnyonge kihivyo, sitaki ulie kwa hilo, wewe ni shupavu, pambana, mimi nina imani kuwa utashinda…’akasema

‘Hapana inaniumiza sana..nikiona mtu, ambaye niligangaika naye, ili tu atokane na ile hali, nilimpenda nikijua atabadilika, leo hii..hapana..hata hivyo, mimi sitaki watoto wangu waje kuumia, ni kweli hata mimi imefikia hatua natamani nifanye hivyo..lakini kila nikiwaangalia watoto wangu, nakosa amani...nashindwa kuchukua huo uamuzi...’akasema

‘Hata mimi, nimeliona hilo,..ndio maana nimekuwa nikipingana na ushauri wa wazazi wako, kama ningelikuwa sijaoa, ningelifanya juhudi ya ziada , na ningafanya hivyo,...hata hivyo, mwisho wa yote ni wewe mwenyewe, kama kosa limetokea, na una uhakika halitajirudia tena basi msamehe mume wako, sio lazima mtu awe kama watu wanavyohisi, yeye kama binadamu anaweza kujirudi na akabadilika....’akasema.

‘Tatizo mume wangu hajakubali kuwa mkweli, na ili kuficha uwongo wake, yeye anazidi kuzua mambo mengine makubwa, na makubwa zaidi, ambayo sitaweza kuyavumilia, na nahisi kutokana na hayo mambo makubwa, yatazuka mengine makubwa, na amani kwenye familia itakuwa haipo tena, je nikae tu nivumilie, nivumilia mpaka lini..’nikasema.

‘Hayo mambo mengine makubwa ni nini,…ni huo mkataba mpya au…?’ akauliza

‘Kuhusu huo mkataba, kuhusu watoto wa marehemu, kuhusu huyo mtoto wake wa nje…asiyejulikana…hayo yanazidi kuongezeka, bado sijamfahamu mama wa huyo mtoto, je atakuja na ajenda gani..bado watoto wa marehemu hawanipi amani…kwanini hivyo….’nikasema.

‘Hata wazazi wako wanahisi hivyo hivyo’akasema

‘Ina maana wazazi wangu wanafahamu kuwa mume wangu ana mtoto nje?’ nikamuuliza.

‘Huwezi kuwaficha wazazi wako kitu, wazazi wako wana macho ya kuona mbali, wana masikio yakusikia kila kinachotokea kwenye ardhi, kukuhusu wewe, japokuwa hawataki kuthibitisha hilo, lakini nahisi wameshaliona hilo, na hilo ndilo linalowafanya wasimwamini mume wako, ...’akasema

‘Waliwahi kukuambia au kukuulizia hilo…?’ nikauliza

‘Hapana,…hawajasema moja kwa moja, na wao wanakwepa kuliongelea hivyo, najua wana maana yao…ila hilo la watoto wa marehemu kuja kudai hisa,…wamasema wanalisubiria kwa hamu....’akasema.

‘Je wao wanataka mimi nifanye nini?’ nikauliza

‘Wanasema waliwahi kugundua kuwa wewe una mkataba ambao ukiutumia utaweza kumaliza kila kitu, lakini cha ajabu mkataba waliokuja kuuona wao, hauna manufaa kwako, na ndio baadae wakasikia kuwa mkataba huo sio halali, ulikuwepo mwingine. Na ndio maana hawajui ukweli upo wapi…’akasema

‘Ni nani aliwaambia kuhusu kugushiwa kwa huo mkataba je ni wakili wangu nini?’ nikauliza

‘Hapana, ni wakili wao....’akasema

‘Kwahiyo wakili wao anafahamu mengi kuhusu hiyo mikataba?’ nikauliza

‘Sina uhakika na hilo, kwani yule ni mtu wa wazazi wako hawezi kuongea zaidi, yeye anaongea yale wazazi wako wanayotaka aongee, hasa inapofikia maswala ya kifamilia...’akasema.

‘Je nitawezaje kuupata mkataba huo wa awali....?’ nikawa kama namuuliza yeye

‘Je ukiupata huo mkataba wa awali, unaweza kufanya nini?’ akaniuliza akiniangalia kwa macho ya kunijaribu

‘Mkataba wenyewe utaongea, na kiukweli, sijui…sizani,…nasema hivi, safari hii sirudi nyuma, mkataba wenyewe utasema ni nini cha kufanya, kwakeli nimechoka, ....naona sasa basi....na kama ni kweli kuna mtoto nje, ..nitahakikisha nafanya lile lilipo kwenye huo mkataba, sitavunja ahadi yangu kamwe...’nikasema

‘Uwe makini lakini.., usije ukafanya jambo ukaja kujilaumu baadae...’akasema.

‘Huwezi kubeba mtu asiyebebeka, ...wema wangu usiniponze, ...siwezi kutengeneza maadui kutoka ndani kwa marafiki zangu wenyewe, ni lazima,nijue ukweli, na kama ukweli ndio huo, basi, ni bora nibakie bila marafiki kuliko kuwa na marafiki wanafiki, ambao wananichekea tukiangaliana wakigeuka, wananing’ong’a....’nikasema na kusimama kutaka kuondoka.

‘Una uhakika na hilo…?’ akauliza

‘Lipi sasa..?’ nikauliza

‘Kuwa ukipata mkataba wako wa zamani, hutarudi nyuma, utaacha sheria ichukue mkondo wake..?’ akaniuliza

‘Umenisikia au sio, kama ungelikuwa wewe ungelifanya nini hapo…, baada ya haya yote, jiulize tu…nimevumilia mangapi, wangapi wamenicheka kuwa naona lakini najifanya sioni..sasa imetosha,…lakini muhimu ni ukweli, na ushahidi…sitaki mambo ya kuhisi tu..’nikasema nikianza kuondoka, huku machozi yakinitoka natamani kulia...

‘Sawa ngoja tuone…ili jikaze usiwe dhaifi kihihivyo, hiyo sio damu ya baba yako..thibitisha hilo kwa vitendo…’akasema na mimi nikawa nipo nje, naondoka zangu, sikusubiria anisindikize kama kawaida yake.

********

Nilipofika nyumbani, niliona gari la mume wangu, siku hizi anatumia gari jingine, la kampuni yake, nikajua yupo ndani, nikatembea kwa haraka kwenda ndani, akilini nikitaka kuongea naye niufahamu ukweli wote, hilo la mtoto wan je liliniumiza sana kichwa.

‘Leo ataniambia ukweli wote…’nikasema nikiingia ndani

Nilitaka leo tukae naye kikao, ..sikutaka tena kuzungushana, kama hataki itabidi nichukuea hatua kubwa zaidi, ikibidi niende mahakamani kwa kugushi mkataba, kwa kuvunja kiapo cha ndoa, kwani kwasasa nina ushahidi wa kutosha, na nina mashahidi..

Nikaingia ndani, hadi chumbani, sikumuona nikajua yupo maktaba, nikafungua mlango wa makitaba, hakufunga kwa ndani kwani mara nyingi, kama hutaki kusumbuliwa, huwa unajifungia kwa ndani, nikafungua mlango taratibu na kuingia ndani.

Mume wangu alikuwa kachuchumaa kwenye kabati langu, ...!

Hilo ni kabato langu, na mara nyingi nalitumia mwenyewe, na akitaka kitu huwa nakwenda kukichukua mimi mwenyewe, kwani hana ufunguo wake… na hapo ndipo niliweka ule mkataba

Na nilipotupa macho kwenye kabati ninapoweka bastola, niliona kabati lipo kama limefunguliwa, moyo ukanilipuka, huyu mtu kapatia wapi ufungua, alikuwa hajanigundua kuwa nimeingia, alikuwa kainama akiwa anapekuapekua , ..katoa vitu vingi nje, kuna kitu anatafuta, ...nikavuta subira.

‘Mbo-mbo-na haipo ooh….’akasema akijiuliza na sasa akataka kugeuka, kabla hajageuka nikamuuliza

‘Unatafuta nini kwenye kabati langu, na ufunguo umaupatia wapi...’nikamshitua, oh...alivyoshituka, nikajua nimeua, nimefanya kisichotakiwa kutokana na afya yake!

NB: Mambo yanaanza kujitokeza, wewe unahisi nini hapo…hii ndio ya wikiendi, tujadilikidogo kuhusu hili..je mtoto wa nje ana haki sawa na watoto wa ndani..kama baba akiamua hivyo, je mama hastahiki kufahamu kila kitu, na je akifahamu hatua gani achukue…TUJADILI?


WAZO LA HEKIMA: Mnapo-oana,na mkafikia kwenye msigishano ambao unaweza kuleta madhara ya ndoa, mjaribu kuangalia hatima ya watoto wenu, je tatizo hilo ni kubwa sana la hata kuvunjika kwa ndoa yenu, inawezekana ikafikia hapo,na hakuna njia nyingine, kama ni hivyo basi ni bora mkapata ushauri wa kitaalamu ni jinsi gani mnawezaje kuwasaidia watoto wenu, ili wasije kuathirika kisaikolojia....
 
SEHEMU YA 74

msiwajengee watoto wenu chuki, kwa mama au baba kwa kuwapandikiza uhasama watoto ili tu eti wamchukie baba au mama, hilo ni kosa kubwa sana kwani wao hawahusiki kwenye matatizo yenu na kuwapandikizia chuki hizo mnawajengea tabia mbaye kwenye maisha yao ya baadae


Labda nielezee vizuri,... jinsi chumba chetu maalumu, tulichokiita ,maktaba kilivyokuwa,…
Kwa vile kila mmoja alikuwa na kampuni yake, na mara nyingi kulikuwa na kazi nyingine ilibidi tuzifanyie nyumbani,kila mtu kwa wakati wake, au siku nyingine tunakutana na kuwemo humo, …

Kutokana na hali hiyo, tukapanga kuwa maktaba hiyo ibororeshwe zaidi iwe kama ofisi ndogo ya nyumbani..na kwa vile kila mmoja ana ofisi yake, tukakubaliana kugawanywe sehemu mbili, lakini sio kuwa kuweka uzio kabisa, ni kwa mtindo wa makabati na meza, kutenga huku na kule,..kiukweli tulipatengeneza vizuri sana.


Hakuna aliyekuwa akihangaika na sehemu ya mwenzake, labda uamue tu kumtuma mwenzako, kuwa nisaidie kunichukulia kitu fulani kwenye sehemu ya vitu vyangu..sasa kila mmoja akawa anapaboresha sehemu yake kwa jinsi aonavyo yeye.

Kwangu nikaongeza kabati moja imara, ukiliona utasema ni meza au kabato la vipodozi na vitu vya kike lakini kwa ndani, nikaongeza sehemu maalumu ya kuweka vitu vyangu vya siri,..ambavyo sitaki mtu aviguse..hata mume wangu sehemu hiyo alikuwa haijui..Anaweza akawa anaifahamu, maana sikuwa namficha sana, lakini hakuwa na habari kabisa na vitu vya kabati hilo.

‘Hilo kabati lako la kike kike, sitaki hata kulisogelea,…’kuna siku aliwahi kuniambia hivyo

Sasa humo ndio niliweka nakala ya mkataba wangu, kwangu mkataba huo ulikua ni moja ya vitu muhimu sana ..nikimaliza kusoma kama kuna kitu nataka kukifuatilia, naurudisha hapo…

Kulikuwa na kabati la vitu vya kuchangiana, lakini pia ni maalumu kwa kumbukumbu zetu za nyumbani, hapo kila mtu angeliweza kuweka au kuchukua vitu,lakini mara nyingi,nimekuwa nikilitumia mimi mwenyewe tu na mume wngu hana habari nalo.

Lenyewe lina sehemu ya nje na ya ndani, unaweza ukachukua vitu vya nje, bila kujua kuwa kuna sehemu nyingine ya ndani,..sasa sehemu hiyo ya ndani, ndio kuna vikabati maalumu,..humo kuna nyaraka za nyumbani za kuchangia…na kuna sehemu maalumu, ndio kuna sehemu tunaifadhia silaha….

Kupotea kwa mkataba wangu, kwenye kabati langu, na mimi mwenyewe ndiye mwenye ufungua, kuliniweka kwenye njia panda, sikutaka hata siku moja kumshuku mume wangu kwa baya lolote lile, yeye ni mimi, na mimi ni yeye, nilimuamini sana kutoka moyoni mwangu, ....sasa mkataba wangu umepotea, na mtu ambaye anayeweza kuuchukua ni mume wangu, swali lilikuja kwa kutumia ufungua gani, na mimi ufungua za kabati langu ninao mimi mwenyewe, na hakuna nakala ya akiba ambayo niliwahi kuiweka sehemu, na ufunguo zangu mara nyingi natembea nazo.

Leo hii ninafika nyumbani ninamkuta mume wangu akiwa kwenye kabati langu,..na kabati limefunguliwa, na ufungua zipo zimening’inia kwenye sehemu yake..na kulihakikisha hilo nilisogea taratibu hadi pale alipochuchumaa

Kwa muda huo hakuwa na habari kabisa kuwa nimeingia, na alionekana kuna kitu muhimu anakitafuta hasa pale aliposema

‘Mbo-mbo-na haipo ooh….’

Na kilichoniuzi zaidi ni kuona nyaraka muhimu za ofisi nyaraka ambazo kwangu ni muhimu sana, alikuwa kazisambaza chini, bila mpangilio maalumu, mimi napenda vitu vyangu viwe kwenye mpangilio maalmu,..hapo subira, ilinishinda ndio nikasema...

‘Unafanya nini kwenye kabati langu...’nikamshitua...

Tuendelee na kisa chetu..............

Mume wangu aliposikia sauti yangu, alishituka, hadi ile karatasi aliyokuwa kaishikilia mkononi kwa muda huo, ili ilimdondoka,… kwanza alitulia, kama anatafakari jambo, na baadaye akajifanya kama hajali..na kwa haraka, akaikota ile karatasi, halafu . akageuza kichwa kidogo na kuniangalia usoni, halafu akasema;

‘Afadhali mke wangu umekuja, maana hapa akili yote imevurugika,..kauli zako za hivi karibuni zimenifanya nichanganyikiwe kabisa…’akasema na sasa akawa anaendeela kama kutafuta kitu.

‘Unajua, ..sijui ndio huku kuumwa,..hii ajali imenifanya niwe mtu wa ajabu kabisa,..uliposema kuhusu mkataba mwingine wa zamani,…nimekuwa nikihangaika kujiuliza ni upi huo…lakini kuna kitu,,…unasikia..’ sasa akaacha kutafuta na kukaa vyema sakafuni.

‘Nakumbuka hata wewe ulikuwa nayo, nakala yako au sio..na mimi ya kwangu, hii niliyo nayo mimi, ni ambayo niliitoa nakala , kutoka kwenye ila nakala ya mwanzo, nahisi ndio hiyo unayoiita nakala ya mkataba wa zamani, kweli si kweli..’akatulia

‘Sasa akili ikanijia,…kama wewe ulikuwa na nakala yako, kwanini usema kuwa imebadilishwa,…sasa nikawa natafuta ukweli..tatizo ni hili nakala yangu, ya zamani…eeh, siioni, nia nione kama kweli ipo tofauti na hii ambayo nilikwenda kuitoa nakala..unielewe hapo, nakala ni ile ile,, ila nilikwenda kuitoa nakala nyingine kwa ajili ya wakili..ni ile ile..

‘Cha ajabu, kwenye kabati langu haipo…ni ile ya zamani, unanielewa hapo, ambayo niliichukua na kuitoa nakala,…hapo kabisa..ipo hii ambayo ni nakala kutoka kwenye nakala hiyo…hii ya sasa unaiona imefifia kidogo,…kama imefutika futika vile lakin ikila kitu ni kile kile...sasa nikawa nahangaika weeeh, mwishowe nikasema, aah..’akasema na mimi nikamkatisha kwa kuuliza

‘Kwahiyo unatafuta nini hapa kwenye kabati langu, ndio mkataba au..?’ nikauliza

‘Kiukweli, nikuombe samahani kwa hilo..lakini sio kosa,..si ndio…niambie mke wangu hapo nimekosea nini…sawa, kiutu , ilitakiwa nifanye hivyo,..lakini nikuulize kwani..kuna kosa mtu akitafuta kitu kwenye sehemu za mke wake..mhh, kosa labda ni kwa vile sikukufahamisha mapema kwa vile…kuna vitu vyako vya kiofisi, lakini ofisi zi zetu wote au…ama kwa hilo, basi nikuombe samaha mke wangu…’akasema.

Aliinua macho na kunitizama..nilishikwa na kitu kama mshangao…hayo macho…sio yale ya mume wang ninayemfahamu…lakini sikujali hilo

‘Mume wangu, toka lini tukawa tunachangiana makabati, kila mmoja ana kabati lake na kila mmoja ana vitu vyake na humu naweka vitu vyagu vya kikazi, angalia jinsi gani ulivyoviweka ovyo vitu vyangu sakafuni, …kwanini jamani…’nikawa naviangalia vile vitu, sakafuni.

Hapo akatikisa kichwa, ni kama vile haamini, na akaehema kwa nguvu, halafu akaendelea na shughuli yake kama hajali, na mimi nikasema kwa hasira.

‘Mume wangu unafanya nini…unajua utaratibu wangu wa kikazi ulivyo,..kwa jinsi ulivyovuruga hivi…hata ule utaratibu wangu wa kumbukumbu za kwenye kabrsaha umeuharibu, itachukua muda tena kuutengeza vizuri,...huoni kuwa unataka kuniweka mimi mahala pabaya..vikiharibika hivi au vikipotea..unaniweka mimi kubaya....’nikasema.

‘Usijali kabisa mke wangu hakitaharibika kitu hapa, niamini mimi, mimi ni mume wako, nitahakikisha hakiharbiki kitu hapa, hata hivyo…kama nilivyokuambia, siku hizi akili yangu imekuwa ya ajabu kabisa, inanasa kila kitu ninachokifanya, yaani siku hizi mke wangu naona nipo mtu wa ajabu sana, nina akili mbili tofauti, hii ya ajabu, inakuja na kuondoka, ..wewe mwenyewe utaona, nitakirudisha kila kitu kwa mahali pake, bila hata kukosea wewe mwenyewe utaona...’akasema.

‘Kwahiyo umesema ulikuwa unatafuta nini humu,… mkataba wako kwenye kabati langu, kwanza ni mkataba upi huo, unajifanya nini hapa..?’ nikamuuliza kwa hasira.

‘Nakala ya zamani, ya mkataba...mwenyewe ulisema unahitaji ile nakala yangu ya zamani, si ndio hivyo…umesema bila hiyo huwezi kukaa kiti kimoja na mimi na wakili au sio..’akasema

‘Kwahiyo ipo kwenye kabati langu, uliiweka wewe..?’ nikamuuliza

‘Ni hivi… pale nilipokuwa nimeiweka nakala yangu, kule kwenye kabati langu, siioni, siku hizi akili yangu inanituma mambo mengi, na nikiweka kitu sisahau pale nilipokiweka, sasa ni ajabu kabisa kuwa siuoni, imekuwaje tena, hapana lazima kuna tatizo...’akatulia sasa akianza kupanga karatasi zangu zilizokuwa sakafuni.

‘Mume wangu…tafadhali…’nikasema kabla sijamaliza akasema

‘’Najua utanifikiria vibaya, lakini sivyo hivyo…mimi nilijua labda wewe umeamua kuichukua il nakala yangu ya zamani,…na kwa bahati mbaya ukaja kuiweka hapa kwako, kiusalama zaidi, hapa kwako kuna usalama sana au sio…’ akasema, huku akiendelea kupekua kwenye mafaili yangu.

‘Sikiliza mume wangu, ..sijapendezewa kabisa na hiki kitendo ulichokifanya, ..na sio tabia yako, imekuwaje siku hizi, mume wangu, ...kuna nini unanitafuta wewe mume, kuna tatizo gani limekutokea ili niweze kukusaidia..kwanini unahangaika hivi mpaka unaniletea matatizo makubwa kwenye maisha yangu..?’ nikamuuliza huku nikiendelea kumwangalia.

‘Hujapendezewa na mimi, kwanini…..hapana mke wangu usinifikirie vibaya kabisa,…na mke wangu, nikuulize, wewe si mke wangu, nimekuoa kwa taratibu zote za ndoa, au sio…je nikifanya hivi kuna kosa gani…?’ akauliza

‘Kuja kupekua kwenye kabati langu, tena kuna mambo ya kofisi, je mimi nikifike kwenye kabati lako nikafany ahivyo utafurahia,…kila siku unazidi kunichefua, kuna kitu gani kinakusumbua hivyo…’nikasema na kumuuliza

‘Hakuna kitu kinanisumbua, ila kwanza nijibu swali langu halafu nitakuambia tatizo ni nini….swali langu ni hivi…, wewe si mke wangu..?’ akauliza na mimi nilikaa kimia, akauliza tena

‘Mke wangu nauliza tena, samahani nijibu tu, wewe si mke wangu…?’ akauliza na mimi nikaona isiwe shida nikajibu

‘Ndio..’nikasema hivyo tu.

‘Sasa kama ni hivyo, nina makosa gani kumkagua mke wangu…’akasema

‘Mume wangu acha maneno yako ya mitaani, kunikagua kwa vipi..?’ nikauliza

‘Kama mimi ni mume wako, kila chako ni change au sio…na pia changu ni chako au sio..tuseme kiukweli kutoka haki za kindoa, achilia mbali mambo ya mikataba, achilia mbali sheria za kidunia,...na hata ukirudi kwenye mkataba kama umeusome vyema inasema hivyo hivyo,… na wewe mwenyewe ni mmoja wa waanzilishi wa huo mkataba wetu na sahihi yako ipo, usikate ukweli mke wangu, ach ubinafsi…’akasema

‘Mimi siutambui huo mkataba wenu wa kugushi..’nikasema kwa hasira,…mume wangu kwanza akatabsamu, halafu taratibu akanigeukia, na kuniangalia…

Kama kuna mtu kampanga mume wangu, basi huyu kafanya kazi kubwa sana, anavyofanya sio kuigiza, utafikiri ni kweli kabisa, yaani utafirikia naongea na mto tofuati sio kama yule mume ninayemfahamu ukimuambia kitu hewala, hewala..tu.

‘Hapana…sio wa kugushi mke wangu, kwanini unasema hivyo,…ni ule ule tulioutengeza pamoja…,tuwe wakweli hata mkataba wa halali wa ndoa, unasemaje, mimi ni mume wako, na wewe ni mke wangu, kwanini sasa isiwe halali kwangu kufanya ya halali…hili ni halali kwangu au sio…nakagua vitu vya mke wangu, ambaye ni mke wangu, au sio,…?’ akauliza.

‘Usipoteze lengo…tafadhali…’nikasema

***************

‘Mke wangu nikuulize tu, kwanini huniamini,..eeh, na …na ..kimkataba…, mimi kama mume wako nina haki ya kuangalia chochote kwenye mali zetu, ...au nimekosea..kasome mkataba vyema…?’ akaniuliza na safari hii alianza kurudisha vitu kwenye kabati, nikawa namwangalia tu.

Hutaamini baada ya dakika moja, alikuwa karudisha kila kitu kama kilivyokuwa awali, halafu akaniangalia, kama vile anataka mimi nikague kama kila kitu kipo sawa, baadae akainama na kufunga, ufunguo ulikuwa umening’inia pale pale…alipogakikisha kafunga, akauchomoa ufungu…, nikagundua kuwa ufunguo ule ni kuchongesha, aaaah, kumbe, ...

‘Huo ufungua uliupatia wapi?’ nikamuuliza, sasa nikijaribu kuukagua huo ufungua, na yeye kwa haraka akauweka mfukoni mwake.

‘Mbona ninao siku nyingi mke wangu...niliamua kuwa na nakala ya ufungua zote, maana sisi sote ni binadamu tu, tunaweza kupoteza ufunguo, kwahiyo kuna haja ya kila mmoja awe na nakala za mwenzake, ni vibaya kufanya hivyo, au…’akasema kama ananiuliza

‘Hilo ulilifanya lini bila ya mimi kufahamu..?’ nikamuuliza

‘Hilo la kuchongesha ufunguo…?!! Mmh, mke wangu umesahau jambo kuwa mimi ni mume wako, natakiwa kuwa mbele kwa ajili ya familia yetu,..ni lazima niwe makini kwa kila kitu, na usalama wetu, na mali zetu pia, kwahiyo hilo sio la kuniuliza, nilifanya muda tu,..na hivi sasa nina uhakika kila kitu kipo salama au kufanya hivyo,..ni-ni..nimekosea mke wangu…’akasema

Alisema hivyo sasa akiwa kamaliza kupanga kila kitu, akawa kama akumbuka kitu, kwa haraka sana akageuza kichwa kule kwenye kabati la pamoja, lipo wazi…kwa haraka ya ajabu, akaliendea, akahakiki kama kila kitu kipo sawa, huyoo, akalifunga.

‘Umeona eeh…kila kitu kipo sawa..kama kilivyokuwa..umeonaeeh,…’akapitisha macho huku na kule, baada y akurizika akaniangalia mimi.

‘Twende…’akasema

‘Mume wangu usijifanye mjanja sana, unajua mimi nafahamu kila kitu, hizo zote ni mbinu zenu, kwanza mumefanya njama za kubadili mkataba, ili kutengeneza mkataba utakaokidhi matakwa yako, na mkafanya mbinu ya kuhakikisha nakala zote za mkataba huo wa kugushi zipo kile idara, lakini mumesahau kitu kimoja…’nikasema

‘Kitu gani mke wangu…’hapo akasema kama kashtuka, halafu akajifanya yupo sawa.

‘Nina uhakika, mliamua kuchongesha hizo ufunguo, ili wewe uje kuiba mkataba wangu, ili mkabadili na kuhakikisha nakala za awali, mumeziharibu, na pia ukaja ukachukua bastola yangu, nakumbuka wewe ulikuwa hutaki hata kuishika hiyo bastola,....imekuwaje sasa…?’ nikamuuliza

‘Bastola!!!…mke wangu, toka lini nikagusa silaha yako, mimi naogopa sana siliha hiyo, aah, hapo umezidi, bastola, mimi na bastola wapi na wapi…’akasema

‘Na kwa taarifa yako, silaha iliyotumika kwenye hayo mauaji ya wakili wako,..ni hiyo bastola, na wewe ndiye mwingine mwenye nakala ya kabati hilo, mimi wamegundua kuwa sihusiki, sasa wao wanamtafuta huyo mtu mwingine mwenye nakala ya hilo kabati, kumbe ni wewe, ole wako polisi wakifahamu hilo...’nikasema

‘Unasema nini mke wangu, sijakuelewa hapo bado, kwanini mimi nilichongesha ili nije kuiba, hahaha, hapo mke wangu unakosea sana,.... kwa nini niibe, kuna mtu anaiba kitu chake, mbona mke wangu unaniangusha,...usisahau kuwa mimi ni mume wako, sio mtu mwingine yoyote,...’akasema,

Moyoni, akilini, nilikwua nimejawa na hasira, lakini nilikumbuka jinsi alivyokuwa akinishauri docta, kuwa nisije kulogwa na kusema mume wangu kapona, kwani hapo alipo ikitokea tena,… mshtuko,… akapatwa na kiharusi (stroke) basi, sitaweza kumponya tena!

Hapo mimi.., nikabakia kukunja uso, na aliponiangalia usoni jinsi nilivyobadilika, aligeuka kwa haraka akatoka nje ya hiyo makitaba…alikuwa anatembea kwa mwendo wa haraka …kama haumwi, kikawaida yeye anatembea kwa shida, kwa kuchechemea..!

**********

Nilichukua mkoba wangu na kuutafuta ufunguo wangu, ulikuwepo kwenye moja ya fungua zangu ninazotembea nazo, nikafungua lile kabati na kila kitu kilikuwa kwenye nafasi yake, na ule mkataba wa kugushi upo hapo hapo..

Sikutaka hata kuukagua kama ni ule ule wa kugushi au ni ule wa awali nikafunga lile kabati vyema, na akilini mwangu nikapanga nikitoka hapo nabadili ufunguo zote na naweka taratibu mpya za kufungua hilo kabati kwa namba za siri.

Nilitoka mle makitaba na kuingia kwenye chumba chetu cha kulala, kuna mlango wa kuingilia huko,..nilitarajia nitamkuta mume wangu kalala huko,..lakini hakuwepo, mimi kwa haraka, nikabadili nguo, na kuelekea sebuleni, chumba cha maongezi.

Chumba cha maongezi, nilimkuta mume wangu akiwa kakaa huku kashikilia mkataba, ..mwanzoni nilifikiria ni ule mkataba wa zamani, lakini ulikuwa ule ule waliougushi wao, niliugundua kwa jinsi ulivyo juu, ..jalada lake limefifia kidogo.

Nilimsogelea na kumwangalia, alikuwa katulia, hana wasiwasi, na alionekana alikuwa akisoma sehemu fulani kwenye huo mkataba, kwa makini, na alipohisi nimesimama karibu yake, akauweka pembeni huo mkataba, na kuinua uso kuniangalia, akatabasamu na kabla hajasema neno, nikasema;

‘Haya hebu niambie ukweli, ni kitu gani kinachoendelea hapa kwenye nyumba yetu?’ nikamuuliza..yeye akasogea kidogo, kama kunipa nafasi nikae karibu yake, sikufanya hivyo.

‘Mke wangu hebu kwanza kaa, njoo ukae karibu yangu,…mimi ni mume wako wala usiniogope, kuwa labda kwa vile naumwa, ninaweza kukudhuru, hapana, hilo halitaweza kutokea abadani, ninakupenda sana mke wangu…’akasema

Na mimi nikakaa, lakini sio karibu yake kihivyo, akasema

‘Mhh, mke wangu, kwani kuna nini kibaya umeiona kimetokea ambacho kinakufanya useme hivyo,…, mimi sioni kama kuna kitu kibaya kimetokea, hiyo ajali isiwe ni sababu ya kuharibu maisha yetu, ajali ni ajali tu, na ajali haina kinga, na mengine yanatokea ni…maisha tu…’akasema na mimi hapo nikabakia kimia kwanza.

‘Mke wangu haya yanaweza kumtokea yoyote, hasa sisi tunaotumia vifaa vya moto..kilichotokea kwangu sio uzembe, sio…au kama watu wanavyosema,..ilitokea tu..na hali ninayokwenda nayo itakwisha tu, nisaidie nipone kabisa…’akasema

Hapo nilitaka kumuambia kumbe kweli hajapona, maana wakati mwingine ukimuuliza anasema kapona lakini hapo anajifanya hajapona kabisa.

‘Ni haki yako kunisaidia..nikikosea,…nikifanya kinyuma na kawaida, ujue ni madhara hayo ya ajali..na hapa nilipo, sio kwamba nakumbuka kila kitu kihivyo, inatokea …nika-ka-sahau,..yawezekana, wakati mwingine nahis kama nipo kwenye njozi, lakini kiukweli nimepona, au sio…’akasema, na mimi sikumjibu kitu.

‘Au mke wangu niambie …, labda mimi sijui, maana muda mrefu nimekuwa hopsitalini, je kuna tatizo lolote…nipo tofauti, nimechanganyikiwa labda..niambie ukweli au…? ‘akauliza

‘Mume wangu, leo ni siku ya mwisho, sitakaa tuongee hivi tena, labda kuwe na kuelawana, na kuelewana kwetu, nimeshakuambia,kutakuja pale tu, wewe utakapokubali kuniambia ukweli, wote na pili ule mkataba wa asili uweppo mezani…’nikasema

‘Eheee,…wewe unautaka ukweli, lakini,…ukweli upi.. hamna shida, mimi nitakuambia kila kitu, ila sasa nikuulize unataka mimi nikuambia ukweli gani labda, nisaidie hapo mke wangu…’akasema

‘Leo ni siku ambayo…kama hutaniambia ukweli, sijui…maana tukimaliza hapa ni utekelezaji,…hata kama utauficha huo mkataba,…na vinginevyo,..tutafikishana mahakamani, au….’hapo nikatulia, alipogeuka kuniangalia

‘Mahakamani, kuna nini cha kwenda huko, hapana mahakamani hapafai, yetu tutayamaliza hapa hapa nyumbani au sio....?’ akauliza

‘Vitendo vyako vimenichosha, kwanza umekiuka makubaliano yetu, umevunja mkataba wa ndoa, na hata sikuelewi,…. na hutaki kuniambia ukweli, ...ni kwanini lakini, kwanini unanitesa hivyo, una lengo gani na mimi…?’ nikamuuliza na yeye akanitupia jicho, halafu akafungua ule mkataba wake, akawa kama anasoma jambo, mimi sikutaka hata kumsogelea na kuangalia anasoma kitu gani.

‘Kwanini unasema ….eeeh,maana tukimaliza hapa na utekelezaji, ama twende mahakamani,…hapana usiseme hivyo, tupo wote, na kila siku tutaongea tu huo ndio utaratibu wa mke na mume au sio..hata bila mikataba, hilo la kuongea ni jambo la kawaida kwa mke na mume, sasa niambie nimekufanya nini kibaya, mpaka useme hivyo…?’ akasema na kuuliza, na aliponiona nipo kimiya akasema;

‘Kwani mke wangu situlishaelewana, na ndio maana nilikuwa nataka niutafute ile nakala yangu ya zamani,…ili tukae tulianganishe kama kuna maneno yameongezeka au kupungua,…sijaiona kabisa..na ya kwako ipo pale pale au sio…kwanini tuandikie mate,..nenda kaulete, ..tulinganishe tuone kama kuna utofauti wowote, utakuta kitu ni kile kile neno kwa neno....’akasema.

‘Mume wangu…’nikataka kusema, yeye akanisogelea akiwa kafungua mkataba wake na kusema…

‘Hebu angalia, mwenyewe, ....maneno ni yale yale..hebu soma uone…’akasema huku akinipa ule mkataba, na mimi sikuugusa na wala sikuinua mkono wangu, nikawa namwangalai usoni nikasema.

‘Mume wangu kwanini upo hivyo, upo sawa kweli wewe, ni kwanini hutaki ku-usema ukweli, ni kwanini mlichukua hatua ya kuubadili huo mkataba bila makaubaliano na mimi…niambie tu ukweli, ili twende sawa….?’ nikamuuliza

‘Mke wangu, mimi nakumbuka , hilo swali nilishakujibu, hakuna aliyebadili huo mkataba,mbona huniamini mke wangu, mimi nipo sawa kabisa, kifahamu, au..?, tuache kuhusu mimi, eeh,...hebu niambie ni wapi huo mkataba umebadilishwa, na kama ulibadilishwa kwanini sahihi yako iendelee kuwepo hapo, huoni unakosea kabisa kisheria….eeh, niambie sahihi zote za wahusika sizipo, angalia hapa, hii sio sahihi yako…hata ukienda mahakamani watahakiki hilo…’akasema.

‘Kwahiyo kumbe bado upo na msimamo wako ule ule,....hutaki kusema ukweli, hutaki kuniambia ni nini kinachoendelea, na ni ni kusudio lako,au kusudio lenu, na washirika wako....eeh, na sasa watoto wanadai wanachohisi ni haki yao , si ndio unataka hivyo…’nikasema huku nimemkazia macho, yeye akaniangalia mara moja halafu akatabsamu, na kusema;

‘Haki ni haki tu…tusiibeze haki, au sio, na…hayo niachie mimi, na nikuulize tena mke wangu, labda kuna kitu wewe unakihis hakipo sawa, ni kitu gani, niambie ukweli, kama ni mkataba upo vile vile..na kwanini mtu afanye ufoji huo, agushi, kwanini,...hebu niambie wewe…?’ akaniuliza

Mimi hapo nikakaa kimia.

‘Mke wangu , tusaidiane, huenda mimi nipo dunia nyingine, huenda kuna kitu umekigundua kwangu na unaogopa kuniambia, au nimebadilika, baada ya kuumwa, nimekuwa tofauti, ...’akasema

Hapo nikasimama,..nilitaka kuondoka kabisa kwa hasira…, lakini nikajiuliza nitakuwa nimefanya nini sasa, leo ni lazima nimbane mpaka asema ukweli wote hawezi kujifanya mjanja hivyo hapo ndio..nikageuka kumuangalia,

Yeye akawa anausoma ule mkataba, hajali kabisa, hana wasiwasi….

Nilimuangalia mume wangu, kiukweli nilimuona kama sio Yule mume ninayemfahamu kabisa,…maana mume niliyemzoea alikuwa nikimuuliza jambo, tunakubaliana, tunaongea yanakwisha, lakini huyu wa sasa, wala hanijali, na pili amekuwa kama yupo mbali, kama alivyosema, ni kama yupo dunia nyingine tofauti ya ukweli….

‘Mume wangu , pengine, hujanifahamu , pengine unafikiria kuwa nakutania, pengine, nahitajika kuchukua hatua nyingine ndio utanielewa,....’nikasema na kutulia kidogo.

‘Nakusikiliza endelea…’akasema hivyo akiendelea kuusoma huo mkataba.

‘Hivi unajidanganya nini, hivi wewe hufahamu kuwa hilo unalolifanya linaweza likakufunga, na hata kukuvunjia ndoa yako, unayoringia nayo wakati wewe mwenyewe umeshaivunja…ukweli ndio huo, umeshaivunja ndoa yako,..hebu niambie imebakia nini…sasa...’nikamwambia na yeye hapo akashituka, na kuinua uso kuniangalia...

‘Unasema nini..kuvunja ndoa yetu, hapana mke wangu, hilo halipo, na hali-hali-tatokea abadani, labda mimi niwe nimekufa....kwanza kwanini unasema hivyo?’ akaniuliza na safari hii akawa ananiangalia moja kwa moja usoni,akionyesha wasiwasi. Kikweli kuna kitu kwenye macho yake nakiona sio cha kawaida….lhata hivyo, hali ya kujali haikuwepo tena.

'Kutokana na makubaliano yetu ya awali, hata kama mumeugushi huo mkataba halali, na kupandikiza huo wa kwenu, na kuweka mambo yenu ya kujihami…lakini ukumbuke, kugushi ni dhambi, kugushi nyaraka za kiheria ni kosa kubwa sana…sasa jiulize unataka kufanya hivyo kwa ajili ya nani…’nikasema

‘Hapo jiulize wewe mwenyewe…’akasema kwa kujiamini kabisa

‘Sawa nikuambie kitu.., hata kama unajifanya mjanja sana,lakini ukumbuke kuwa makubaliano yetu ya awali yapo pale pale, na moja ya makubaliano yetu ni kuwa mmoja akivunja miiko ya ndoa..unaifahamu hiyo miiko, ile mikubwa…’nikasema

‘Kama upi huo…?’ akauliza

‘Kuzini…kutembea nje ya ndoa…’nikasema

‘Nini, …wewe mke wangu ni nani anaweza kufanya dhambi hiyo, hapana…mimi nakubali hilo ni kosa, ..na kwenye mkataba wetu inasemaje..hebu kidogo…’akasma na sasa akifungua mkataba wake, na akawa kama ansoma

‘Yah, hapa kupo wazi…ni kosa, ila sasa unajua kiubinadamu, eeh..si semi hivyo kwa vile, labda..hapana mimi sijafanya, ikitokea wewe ukafanya hivyo, kwanza kuwepo na ushahidi…wa bayana, lakini pia…sisi ni wanandoa, tumzee, tuna watoto…mmoja akaghafilika, kutokana na sababu…maana huwezi kufanya dhambi kama hiyo bila sababu…’akasema

‘Sababu gani,…hakuna sababu hapo, kuzini ni kuzini tu…’nikasema kwa hasira.

‘Je kama imetokana na wewe..’akasema

‘Kwa vipi..?’ nikauliza

‘Tuache hayo, ila hapa kwenye mkataba inasema hivi, kama …itatokea hivyo, kwasababu za kujitetea, kuna sababu japo kidogo, ya kujitetea, inayoingia akilini, japokuwa..ushahidi upo, na mmoja akaomba msamaha, ukakubalika, basi,..ni kusameheana ya kale yaishe watu wagenge yajayo,…hiki ni kipengere cha nyongeza..’akasema

‘Hivi wewe mume wangu kweli hilo lilikuwepo…?’ nikamuuliza.

‘Si ndio nimesoma hapa…hebu soma wewe mwenyewe…lakini pia kuna vipengele vingine hakuna haja ya kivisoma,…kama vile mume wakiona kuna haja, ya kufanya jambo lenye tija kwa familia,..yeye kama kiongozi wa familia anaweza…ni vipengele vye kujitetea,..vinasaidia kisheria,..lakini muhimu ni kusameheana …’akasema

‘Kwahiyo uliongeza hivyo, ulipobaini kuwa umezini….?’ Nikamuuliza

‘Nani kazini,…mimi,…mke wangu unanifahamu nilivyo, mimi….hapana sijaweza kufanya hivyo, kwanza ni nini kuzini….mmh…hivi kuna kipengele hapa…’akawa anafunua kutafuta.

‘Hapana achana na huo mkataba wa kugushi, nijibu swali langu,…’nikasema kwa ukali,

‘Kabla sijakujibu swali, twende pole pole, kwani huo mkataba unaojua wewe ulisemaje…?’ akauliza

‘Unajifanya hujui..ni hivyo…kama umezini, ina maana umetembea nje ya ndoa,… kukawa na ushahidi wa kutosha, basi ndoa haipo..na huna haki tena kwenye mali zilizochumwa kwenye ndoa…’nikasema

‘Wauuuh…hiyo mpya kwangu…’akasema

‘Na kwenye kile kikao, wewe mwenyewe ulilisitiza sana hilo kwa kujiamini,..na ukasema ushahidi ni lazima uwepo, nikakuuliza ushahidi gani na watu wanafanya kwa siri, ulisema wewe mwenyewe, mtu kama huyo ataumbuka, anaweza akapata mtoto , huo ni ushaidi tosha,..ikipimwa ikahakikiwa kwa DNA, basi huo ni ushahidi wa kisheria, unabisha…’nikasema

‘Kikao gani hicho..?’ akauliza akionyesha mshangao

‘Utabisha lakini mbele ya sheria, utanaswa tu…na kwa vile hutaki kukiri kosa, ukasema ukweli, basi mimi kuanzia leo, najiandaa kwenda mahakamani…’nikasema

‘Mke wangu unakwenda mahakamani kwa kosa gani, mimi nimefanya kosa gani…?’ akaniuliza

‘La kuvunja mkataba wa ndoa, na kugushi mkataba halali wa ndoa…’nikasema

‘Nimevunja mkataba wa ndoa…!! ?’ akauliza kwa mshangao

‘Ndio umezini…’nikasema

‘Kuzini….’akasema hivyo, sasa akawa anatoa macho kama kuogopa

‘Mimi,…hapana, sijawahi kufanya hivyo, hata kama ulitoa kibali hicho, lakini mimi sijafanya…’akasema hivyo akiongea kwa haraka haraka kiasi kwamba sikumsikia vyema.

Akatulia kama anasubiria mimi niongee, kiukweli, ukimuangalia mume alivyo, ni kama mtu aliyechanganyikiwa, hajui kabisa anachokisema, lakini hakuweza kunishawishi kwa hali hiyo, kangu mimi , nilimuona kama anaigiza tu.

‘Ndio wewe umezini, usijitete hapa, kubali tuyamalize, hapa hapa…maana tukifika huko mbele mimi ninao ushahidi…’nikasema na nilitaka aulize ushahidi gani lakini hakuuliza hivyo, yeye akasema

‘Mke wangu unasema nini,....sijawahi kufanya hivyo,.....ni nani kakuambia nimezini, ....na na...mbona sikuelewi..nimezini na nani , umedanganywa mke wangu, temea mate chini, sijawahi, ..kamwe…’akawa sasa kama anahangaika hivi.

‘Usijifanye mjanja,..leo imefika mwisho wako, ..leteni mkataba ule wa zamani tuyamalize kwa amani, mimi nitakusamehe, lakini kama haupo huo mkataba wa zamani, basi kitakachofuatia hapo ni mimi kwenda mahakamani..’nikasema

‘Mke wangu…’akasema hivyo na mimi nikaa kimia, na akarudia tena... , ‘mke wangu kwanini unalirudia hilo, mimi nakupenda sana mke wangu, kweli kabisa....hilo la mkataba wa zamani, silijui mimi, sikumbuki kama kuna mkataba mwingine zaidi wa huu, kama ungelikuwepo,ningeuleta, tuyamalize mimi na wewe mbona tumekuwa wa kuridhiana mambo,ulishawahi kuniambia jambo nikakataa..eeh…sasa huo mkataba ..upo wapi huo…’akasema

‘Sikiliza,… usijifanye kuigiza mambo hapa,..najua yote hayo, mumepanga uigize hivyo..ujifanye umechanganyikiwa, ujifanye hukumbuki kitu….na ujanja wako umeshafika mwisho,..sasa ni muda wa wewe kuniambia ukweli ili tuyamalize kwa amani,..kwani unataka nini, niambie…sasa nakuulize tena kwa amani, ..je sio kweli kuwa wewe una mtoto nje ya ndoa?’ nikamuuliza

Kwanza ilikuwa kama kapatwa na kitu kimemfinya hivi, akashtuka, na alitulia kidogo, halafu akainua uso, na kuniangalia…kiukweli hayo macho yake sijayaona kabla…akaniangalia, ..mpaka mimi sasa niangalia pembeni..

‘Mtoto nje wa ndoa…!!!’akasema hivyo halafu akatulia, …hakusema neno, mpaka nilipouliza tena..

‘Nimekuuliza hivi, sio kweli kuwa wewe una mtoto nje wa ndoa, ambaye hata kwenye mkataba wenu mwingine wewe umemuandikishia urithi, na kwenye huu mkataba wangu mimi na wewe wa kugushi, kuna maneno mumeyaongezea kuwepo kwake, ili na yeye atambulikane na apewe haki sawa na wengine, sio kweli ..na hapo hapo nakuuliza ni kwanini kipengele hicho mkakiongezea maneno kama hayo, kama sio kweli….?’ Nikamuuliza

‘Mkataba unasema hivyo au sio..huu mkataba, niliona sio, mkataba wetu mimi na wewe au sio…sasa ngoja nikuonyeshe hapo…unaona hapa, na huu ndio mkataba wetu au sio…, umeukubali mwenyewe..kwahiyo hiyo sehemu inasemaje, nikumbushe kidogo mke wangu, mimi nashahau sahau wakati mwingine…’akasema

‘Hapo hukumbuki vyema, lakini kwenye kurudisha vitu kwenye kabati, hukusahau kitu..hapa kwa hivi sasa huna akili za ajabu,..huoni kuwa unajifunga wewe mwenyewe…’nikasema


‘Hahaha, hapana mke wangu, sijifungi bwana…ila wewe wanipambikia mambo, huyo mtoto eeh,....mke wangu kiukweli mimi sikumbuki hilo, ila kuna kitu nataka nikuambie ukweli, ..hebu kaa kwanza, nitakuambia kila kitu…’akasema na mimi sikukaa, akainaimisha kichwa chini kwanza kama anawaza jambo…

‘Mke wangu nimekuwa nikiota ndoto ya ajabu sana, kuwa kweli mimi nina mtoto, tena mtoto huyo ni wa kiume….’akasema

‘Hahaha, umeshaanza kukubali, …haya sema ukweli wote mimi sasa nitakusikiliza…’nikasema sasa nikikaa.

‘Sasa tulia basi nikuambie..hiyo ni ndoto jamani…’akasema

‘Haya wewe singizia vyovyote vile, ..una mtoto wa kiume au sio, na huyo ndiye kakufanya ubadili hadi huo mkataba…’nikasema

‘Sikiliza kwanza, nikuhadithis hiyo ndoto, sio kweli, ni ndoto,..ndoto,..kuota usiku, na kwa bahati mbaya,…nimekuwa nikiota hiyo ndoto sana baada ya ajali,…wakati nilipoanza kupata kumbukumbu zangu…kuwa nina mtoto wa kiume,’ akasema

‘Una mtoto wa kiume au sio, sasa swali ulizaa na nani huyo mtoto…?’ nikauliza

‘Kwanza nikuulize wewe huyo mtoto yupo au hayupo…?’ akaniuliza mimi sasa.

‘Unaniuliza mimi tena…’nikasema

‘Mke wangu nisaidie kujibu hilo swali, maana nateseka sana, kumuwaza, kama yupo, ni heri sana kwangu na kwetu kama familia…’akasema

‘Mume wangu…nimechoka, na maneno yako,…nakuuliza tena hili swali, kama ni ndoto au ni kweli, je una mtoto nje ya ndoa, kauli yako ndiyo itathibitisha hili, kama hayupo, basi hatakuwepo,…ilo uweke akilini, kimkataba na kila hali, sasa kama yupo, ni vyema hilo uliweke wazi,…’nikasema

‘Kama hayupo..hatakuwepo, au sio…’akasema sasa akitabasamu.

‘Ndio hivyo, ukitoa kauli yako sasa hivi, kuwa hakuna mtoto wa nje..ndio hatakuwepo hivyo…, akitokea…huyo shetani, au sio….’nikasema, nikijua kama yupo hawezi kumkana.

‘Usiseme hivyo, damu ni nzito kuliko maji…’akasema

‘Hahaha, umeona eeh, hebu rudia tena…?’ nikauliza kama sikusikia

‘Nasema hivi, usiite watoto wa nje mashetani, kwani wao wana kosa gani,…’ akauliza

‘Kwahiyo wewe unaye, ili tusimuite ni shetani, sema ukweli wako usimkane mtoto wako…?’ nikamuuliza

‘Mimi sijui….’hapo akasema hivyo

‘Haya niambie uliota nini…?’ nikamuuliza

‘Ehee hapo sasa tuendelee na ndoto yangu, na tusaidiane kwa hili, ninaota mara nyingi tu, kuwa tuna mtoto wakiume, tatizo sasa ni huyo mama yake,..hataki ..’akasema

‘Hataki nini..?’ nikauliza

‘Hataki huyo mtoto atambulikane kwa jamii…’akasema

‘Kwanini, ni kashfa au..?’ nikamuuliza

‘Sijui,…ni ndoto, inanitesa sana, sasa nataka wewe unisaidie kwa hilo, akili yangu inawaza sana hilo, na zaidi ni kauli ya madocta,..hawajaniambia wazi wazi, lakini nayo ilikuwa kama ndoto…’akasema

‘Wamesemaje…hao madocta..?’ nikamuuliza

‘Mimi sitaweza kuzaa tena…’akasema kwa sauti ya unyonge..

‘Hayo ni ya kwako, nikuulize tena, ni nani mama wa huyo mtoto..?’ nikamuuliza

‘Huyo mwanamke…cha ajabu kabisa, alikimbia na huyo mtoto na ghafla, sasa wakati nahangaika, eeh…puuh, ajali..na ghafla, nikashtuka kutoka usingizi…’akasema

‘Mume wangu acha ujanja…’nikasema

‘Sasa nikuambie kingine mke wangu, huyo mtoto wetu anafanana kabisa na watoto wetu utafikiri mapacha..sasa najiuliza ni kwanini huyo mwanamke akimbie na mtoto wetu,…’akawa kama anataka kulia.

‘Nakuuliza hivi,…huyo mama aliyekimbia na huyo mtoto si unamfahamu…?’ nikamuuliza

‘Ndio namfahamu, kwanini nisimfahamu…’akasema

‘Ni nani sasa…?’ nikamuuliza na hapo akainua uso, akanitizama na sasa niliona dalili za machoni machoni kwake…anataka kama kulia, moyoni sikuwa na huruma naye tena, kila kitu cha huruma kilikuwa kimefungwa, nikamkazia macho yaliyojaa hasira nikisubiria jibu lake.

NB: MBONA NDEFU HIVI


WAZO LA LEO: Huwezi ukahalalisha dhambi kwa kutengeneza dhambi nyingine juu yake…, usifanye dhambi ili kuficha dhambi uliyowahi kuifanya, dawa ya dhambi ni kutubu, na kutubu kupo kwa namna nyingi, …moja wapo ni kukiri kosa, kwa Yule uliyemtendea ukamuomba msamaha, akikubali kutoka moyoni kuwa kakusamehe, basi hapo huna shaka…lakini kutumia ujanja wa kuhadaa ili kosa lisionekane kosa na ili Yule uliyemkosea aseme tu kakusamehe,…bila ya ridhaa yake kutoka moyoni, bado utakuwa kwenye deni ya dhambi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom