Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa CHADEMA Zanzibar Said Issa Mohammed amemtaka Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche @hechejohn kumheshimu na kutokutoa lugha zisizo sahihi dhidi yake ikiwemo ya kuwa ‘akazie swaum kwa kula nguruwe'. Akieleza kuwa yeye ni muislam na ulaji wa nguruwe kwa misingi ya dini yake hauruhusiwi(haramu)
Said ameyasema hayo leo Machi 05, 2026 akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kueleza kuwa kauli hizo za Heche zinalenga kupotosha ukweli ambao amekuwa akiusema juu ya kutokuwa na uwiano kwenye mgawanyo wa mali za CHADEMA.
Pia Soma: Said Mohamed: Hatujaenda mahakamani kuiua CHADEMA, bali kuiimarisha ifanikiwe
“tuheshimiane tu kwenye dini, Heche ni Mwenyekiti wangu wa vijana kwa hiyo tuheshimiane tu kwenye dini Waislam kula nguruwe ni haramu sasa yeye anavyosema nikale nguruwe kukazia sjui swaum kwa sababu nazungumza uongo”