Mkomeshe Mwanaume anayehitaji Namba yako ya simu

Mkomeshe Mwanaume anayehitaji Namba yako ya simu

Wana mmu hamjambo? Heri ya mwaka mpya 2018!
Leo nataka nizungumze na wadada wenzangu juu ya upuuzi wa wanaume wa kuomba namba (za simu)
Uombaji wa namba ni kitu nakichukia sana kwa sababu kama mtu anataka kuzungumza nami azungumze tukionana uso kwa uso sio kuomba namba. Kwa uzoefu wangu wanaomba namba ni madomo zege.
Sasa wewe fanya hivi:Kwa kuwa mara zote hawataji neno simu ila husema naomba namba zako, basi wewe mpe namba za saizi ya kiuno, viatu nk.(kama hutaki mahusiano ya simu)Akishangaashangaa mweleze wazi kwamba hiyo ndio namba yako ya (kiuno au viatu) kisha nyamaza, utamwona huyooo anaishia zake ameinamisha kichwa. Hakuna haja ya kutoa maneno makali kama hutaki kutoa namba yako ya simu!
Nawatakieni mwaka mpya wa mafanikio.
Ni mimi Miss Nai
[emoji121]
MKUU,

HAPO MTAANI KWENU KUNA WANAPOUZA BANGI YA MALAWI?

SAMAHANI LAKINI.
[emoji121] [emoji121] [emoji121]
 
Nimekosa cha kujibu,
Lakini kaa ukijua wanawake wanakabiliwa na changamoto nyingi zaidi kuliko wanaume.
 
Wanaume wenzangu wanawake wa aina hii, usidhubutu wala kuhangaika nao
 
Nashuhudia mchuano wa Timu Toa Namba na Timu Usitoe Namba ....

Naendelea kupata Soda na Popcorn huku naserereka na kutiririka na comments zenu mwanzo hata mwisho.

Mleta thread, kwa hii utaelewa tabia za watu haswaaa....
 
Back
Top Bottom