Mkomeshe Mwanaume anayehitaji Namba yako ya simu

Mkomeshe Mwanaume anayehitaji Namba yako ya simu

Wanawake msisikilize ushauri wa mtoa maada..
Anawadanganya..
La sivyo mtaishia kuwa ma single mother...
Maana hao madomozege mnaowazingua sasa hivi ndo wanaume watulivu..
Hao wepesi wa kutongoza ndo wanawatumia na kuwa dump...

Akili za kuambiwa changanya na zako...

Kwanza mtoma maada njoo pm tuyajenge
Kwa nini uombe namba
Mwanaume jasiri anatema sumu face to face
 
Siku hizi wanaume hatuombi namba bali tunaombwa.
Nitumie namba ya nini ili nipate nini hasa. Ukiomba namba kwangu na ukapewa wewe unakuwa unajielewa. Hatupendi ujinga siku hizi.
 
Wana mmu hamjambo? Heri ya mwaka mpya 2018!
Leo nataka nizungumze na wadada wenzangu juu ya upuuzi wa wanaume wa kuomba namba (za simu)
Uombaji wa namba ni kitu nakichukia sana kwa sababu kama mtu anataka kuzungumza nami azungumze tukionana uso kwa uso sio kuomba namba. Kwa uzoefu wangu wanaomba namba ni madomo zege.
Sasa wewe fanya hivi:Kwa kuwa mara zote hawataji neno simu ila husema naomba namba zako, basi wewe mpe namba za saizi ya kiuno, viatu nk.(kama hutaki mahusiano ya simu)Akishangaashangaa mweleze wazi kwamba hiyo ndio namba yako ya (kiuno au viatu) kisha nyamaza, utamwona huyooo anaishia zake ameinamisha kichwa. Hakuna haja ya kutoa maneno makali kama hutaki kutoa namba yako ya simu!
Nawatakieni mwaka mpya wa mafanikio.
Ni mimi Miss Nai
Una sifa zote za NUNAYEMBE.

Mnataka kuolewa ila bado mchakato wa kutongozwa mnawaita watongozaji WAPUUZI. Au una sura mbaya sasa umekata tamaa?
 
Kwa nini uombe namba
Mwanaume jasiri anatema sumu face to face
Watu wako busy mkuu.
Yam umekutana na binti kwenye daladala ukavutiwa nae uanze kumtongoza hapo hapo bila hata kufahamiana..

Au umekutana na mtu njiani hujui anaenda wapi au anaenda kufanya nini ww unaanza kuntongoza hapo hapo..
Haya mambo yana taratibu zake na taratibu zenyewe ni kama kuchukua mawasiliano ili siku mkiwa free muelezane hisia zenu...
 
Simu ndio kila kitu. Hata kama atakutongoza ana kwa ana, mkakubaliana, lazima mtapeana namba ili muweze kwenda kula tunda sehemu fulani. Hukwepi kutoa namba
 
Back
Top Bottom