Mkoa wa Lindi: Historia na Taarifa Muhimu

Mkoa wa Lindi: Historia na Taarifa Muhimu

lindi kwa ujumla iko na makabila mangapi, na ina wilaya ngapi.
 
mkuu. madukwappa ila hospital jana ambayo imeonyeshwa itv membe aliitembelea ambayo haina jokofu za maiti ina hadhi gani.ki mkoa?
_na je,kwanini huo mkoa ni masikini na bado wanangangana na ccm?
 
Last edited by a moderator:
Barabara haisumbui??

Kipo kipande kama cha km. 15 kinasumbua cha nyamwage ambacho hakina lami kikikamikika mambo yatakuwa mazuri zaidi... Nadhani hata daladala zinaweza kuanza safari kwenda lindi mjini kutokea dar.. Tatizo bado lipo kutoka makao makuu ya mkoa kwenda wilaya zingine kama ruangwa liwale na mchingwea
 
madukwappa, Salma anatoka kijiji gani hapo lindi
Kwanini lindi wananchi ni maskini sana
Makabila gani yanapatikana mkoa wa lindi
Hadi enzi hizi mabinti wa lindi bado wanachezwa unyago?
 
Last edited by a moderator:
Niko Ruangwa hapa ni Radio za CCM tu ndo zinakamata; TBC, UHURU na Newala, na clouds FM kwa mbaliiiiiii.
Na Hapo tumefunga antenna juu kama ya TV.

MTU ALIYE NYIKANI upo Ruangwa mjini,nanganga,matambarale au nandagala????i was there before eid,vumbi jekunduuu,msalimie tenten kama unamjua
 
Last edited by a moderator:
Mamlaka ya mawasiliano inabid iwasaidie kuwashawish wamiliki wa vyombo vya habar waje huko.Mzee Meng wasaidie hawa watu kupata habari.

kwa nini wewe usione fursa ukaanzishe kituo cha radio, siyo msaada huo ni biashara!
 
madukwappa, Salma anatoka kijiji gani hapo lindi
Kwanini lindi wananchi ni maskini sana
Makabila gani yanapatikana mkoa wa lindi
Hadi enzi hizi mabinti wa lindi bado wanachezwa unyago?

ram binafs sijui mama salmer anatoka kijij gan.ila Lindi makabila yapo mengi,maarufu ni wamakua na wayao,na wasichana bado wanachezwa kama kawaida,umaskin bado upo tena mkubwa tu,ila ubovu wa miundombinu pia tatizo,maana kaz wanafanya(wanalima sana) wananyonywa
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: ram
Hospitali ya nyangao ni moja kati ya hospitali mashuhuri kanda ya kusini tangu enzi za ukolon ilikuwa inatumiwa ktk utoaji wa huduma za afya.. Kiukweli ni hospitali muhimu kwa wakazi ya mikoa ya kusini.....
Kwa sasa inaendeshwa kwa ubia wa kanisa na serikali... Lakini inaonekana serikali haijawa na commitment ya kutosha ktk kuhakiksha huduma bora za afya zinapatkana ktk hospitali hii kongwe

kwa upande wa umaskin nadhan nilijibu jana tafadhali refer post za nyuma

kuhusu kwanini kusini wanang'ang'ania CCM mimi naamini wananch wa kusin hasa Lindi hawafurahii umaskini au vitendo vinavyofanywa na wawakilishi..

TATIZO NI KWAMBA HIVYO VYAMA VINGONE VYA UPINZANI ikiwemo CHADEMA NCCR MAGEUZI na CUF havitoi kipaumbele ktl harakati za kisiasa mkkoa ya kusini. Angalau kidogo CUF wameoneaha jitihada na ndyo maana walishnda jimbo la LINDI MJINI... Syo vyama vya siasa tu.. Hata makampuni binafsi. Vyombo vya habari kwa kiasi kikubwa imeitenga kanda ya kusini ktk nyanja zote ktl hali kama hyo suala la mabadiliko linakuwa ngumu kidogo

hospital ya ruangwa ina zaid ya miaka 20 haina xray as huduma,na wahudumu ni voda fasta wa std seven,wanapewa induction course-Mbunge wao ni Kassim Majaliwa
 
Mkuu MADUKWAPPA unfahamu chochote kuhusu NGENDE na UGANGA wake? Ngende ipo au propaganda? Ipo wapi wapi Liwale /Lindi au Mahenge / Morogoro. Je kuna waganga wa kibinadamu tu au kweli ni mizimu? Vipi kuhusu utajiri wa NGENDE?
 
Ni nini kinasababisha:-
1) matukio ya kutoa talaka kushamiri sana pande hizo za kusini Lindi inclusive. (unakuta kijana ana miaka 25 ameshaoa na kuacha mara nne, ama binti kwa umri wa miaka 25 ana watoto watatu kila mtoto na baba yake)

2) mabinti kushika ujauzito (kwa asilimia kubwa) wakiwa na umri mdogo sana.

3) Inakuwa vigumu mno kumkuta binti mwenye umri wa miaka 20 hajazalishwa na mara nyingi katelekezwa na mzazi mwenzie hivyo kujikuta mtoto analelewa ujombani.

4) umedai mikoa ya kusini (lindi inclusive) imechangia kutoa viongozi wengi wa kitafa, sasa basi kwa "ubinafsi uliodai" unaweza kukubaliana nami kuwa mchango huo pia umechangia kulididimiza taifa letu in ubinafsi perspective towards intenational platforms.

USIJIBU KWA UMAJUMUI TAFADHALI.
 
Ni kweli usemalo.. Umwinyi bado upo... Nadhani jambo la msingi ni kuwaelimisha vijana wa sasa kubadilika na kuachana na huo mtizamo wa kimwinyi. Wasome kwa bidii wafanye kazi kwa kushirikiana na kwa lengo moja la kukabiliana na umaskini na kuibadilisha mkoa wa lindi.. Nafikiri ni jambo linalowezekana kwa kutumia informal na formal education.. Badala ya kushindwa kwenye vijiwe vya kahawa na kupiga story.. Vijana wajitume katk kaz za kiuchumi

Well said kaka
 
kama unavyojua Nchi yetu hii kila raia anaruhusiwa kuishi popote na kufanya shughuli zake ili mradi afuate sheria na taratibu
yapo makabila mengi ila makabila ya asili ya mkoa wa Lindi ni
WAMWERA WAMAKUA WAMAGINGO WAMAKONDE WAMATUMBI WANGINDO WAYAO n.k

kwa upande wa wilaya mkoa wa lindi unaundwa na wilaya 6 ambazo ni NACHINGWEA. RUANGWA. LIWALE. KILWA. LINDI VIJIJINI. LINDI MANISPAA
Fanya marekebisho kidogo; kwa mamlaka ya serikali za mitaa uko sahihi ila kihalisia wilaya ni 5 yaani Hapo ni wilaya ya Lindi na zingine zinabaki kama zilivyo.
 
Back
Top Bottom