Mkoa wa Lindi: Historia na Taarifa Muhimu

Mkoa wa Lindi: Historia na Taarifa Muhimu

Nadhani nimejibu hili swali.. Kiufupi wanaliwa kwa baadhi ya makabila hasa wamakua wamakonde na wamwera.. Ila syo wote.. Binafsi sili panya.. Ila panya wanaoliwa syo hawa wa majumbani.. Ni wale panya wa porini wenye rangi tofauti na hawa wa ndani.. Ni sawa na wale waliohimizwa na wataalamu wa SUA.. waliwe..NDEZI.. KARIBU SANA

Aidha ulaji wa panya huendana na imani za dini..mfano waamini wa dini ya kiislamu panya kwao ni haramu..hivyo ili kuepusha machukizo kwa wengine huwezi kukuta panya wanauzwa kiholela sokoni bali huzwa kwa wale tu wanaokula.
 
Lindi na Mtwara wakati wa mkoloni na hata baada ya uhuru zilikuwa mkoa mmoja. Ni sababu zipi zilizopelekea mkoa huo kugawanywa na Mtwara ikapewa eneo dogo la utawala wakati Lindi ikapewa eneo kubwa la utawala?
 
sababu kuu ya kuugawa mkoa kuwa mikoa kuwa miwili naamini ni kitokana na eneo kuwa kubwa...... Pia serikali hugaww mkoa ili kurahisisha ktk utoaji huduma za jamii kwa wananchi... Ni kweli lindi ilipewa eneo kubwa mno na ndyo maana serikali ina mpango wa kuugawa mkoa wa lindi tena ili kufikisha huduma kwa wnanchi kwa urahisi.. Inasemekana mkoa mwingine makao makuu yatakuwa ktk wilaya ya nachingwea...
Suala la kwanini lindi ilipewa eneo kubwa siwezi jua kwa kweli
mazungumzo yanayoendelea sasa kati ya viongozi wa wilaya za Masasi,Nanyumbu(Mtwara) Nachingwea na Tunduru ni ya kuunganisha wilaya hizo ili kuanzishwe mkoa wa Kusini.lengo kuu likiwa ni kuwafikishia huduma za jamii kwa ukaribu wananchi.
 
Kama nimekupata vizuri unasema ufuta huuzwa kwa vyama vya ushirika na wakulima, je wanatumia mfumo wa stakabadhi ghalani? Je watu binafsi hawaruhusiwi kununua ufuta toka kwa wakulima?

Je mbaazi hazilipi kama ufuta au korosho? inaeleweka nazo zalimwa kwa wingi huko. Je nazo zauzwa kwa vyama vya ushirika tu? na ni mfumo wa stakabadhi ghalani?
 
Zao pekee linalouzwa kwa mfumo wa stakabadhi ghalani ni korosho ..vyama vya ushirika vinatumika pia kama vituo vya kununulia mazao mchanganyiko kwa sababu ya urahisi wa maeneo ya kuhifadhia baada ya kununua..ufuta unalipa kuliko mbaazi na korosho.
 
Kwa nini hospitali ya Nyangao anakotoka mbunge na waziri Membe anayetarajia kugombea urais 2015 haina jokofu la kuhifadhia maiti na leo kaaibika kwa kujionea mwenyewe?

mbunge Membe anatokea Rondo isipokuwa pale nyangao ana ndugu wa damu kule bwawani kwa marehemu mzee donato.
 
Kwanza tukumbuke kuwa hospitali ya nyangao mwanzo ilikuwa inamilikiwa na wamisionari ambapo ilikuwa inaendeshwa na wazungu baaye ikawa chini ya kanisa.. Huduma zake zilikuwa nzuri kama ilivyo ktk hospitali zingine za.mishen kama vile Mnero~nachingwea. Ndanda~masasi
.. Hata hivyo serikali miaka ya karibuni imeamua kujimilikisha hospitali ya nyangao hapo ndipo hiluduma zilivyoanza kuwa mbovu kutokana mipango mibovu ya serikali...

Mkuu Hospitali ya Nyangao bado iko chini ya Kanisa kupitia Jimbo Kuu chini ya baba Ngonyani lina haki kwa asilimia kubwa pale,serikali imeingia kwa asilimia ndogo sana.
 
Mpk sasa kwa upande wa shule binafsi lindi haiko vizuri.... kwa manispaa Shule zinazotegemewa ni za serikali.. Hasa LINDI SEKONDARI AMBAYO NI YA SERIKALI PIA.... Kuna shule ya private maarufu inaitwa Ruo.. Hata hivyo sikushauri umpeleke maana haina rekodi nzuri

Kwa Lindi Manispaa kuna shule za secondari kama 8 hivi, na Lindi (v) kuna takribani shule 25......!! Hiyo Ruo ipo Lindi (v)
 
Ungepewa nafasi ya kupanga mipango ya maendeleo na kuwezeshwa kwa namna moja au nyingine vipaumbele vyako vya maendeleo vingejikita kwenye maeneo yapi na kwa nini katika mkoa wenu wa Lindi?
 
Mpk sasa kwa upande wa shule binafsi lindi haiko vizuri.... kwa manispaa Shule zinazotegemewa ni za serikali.. Hasa LINDI SEKONDARI AMBAYO NI YA SERIKALI PIA.... Kuna shule ya private maarufu inaitwa Ruo.. Hata hivyo sikushauri umpeleke maana haina rekodi nzuri

Ipo pia shule binafsi ya Khailat kule likotwa.
 
Ungepewa nafasi ya kupanga mipango ya maendeleo na kuwezeshwa kwa namna moja au nyingine vipaumbele vyako vya maendeleo vingejikita kwenye maeneo yapi na kwa nini katika mkoa wenu wa Lindi?

Jambo kuu na la msingi ni kuimarisha na kuboresha elimu hususan masomo ya sayansi kwa kuhakikisha kunakuwepo na maabara kwenye sekondari,maabara sio kwa maana ya majengo tu bali vifaa na walimu wa masomo husika. Mkazo kwa masomo ya sayansi ni muhimu ili kuwajengea uwezo vijana wa Lindi na Mtwara kunufaika na kuwa na uwezo wa kutumika kwenye viwanda vinavyotarajiwa kujengwa kutokana na uwepo wa gesi asilia. Aidha suala lingine la msingi ni kuufungua mkoa wa Lindi kwa kuimarisha miundombinu ya barabara na mikoa ya Dar es salam na Ruvuma,kuimarisha uwanja wa ndege wa Lindi na kuifufua bandari.
 
vip ushirikina na wazee wa kamati za ufundi,maana nasikia mko fiti,tuone n namna gani ya kuileta taifa stars maana nahs tumelogwa.
 
Back
Top Bottom