Mkoa wa Lindi: Historia na Taarifa Muhimu

Mkoa wa Lindi: Historia na Taarifa Muhimu

vip ushirikina na wazee wa kamati za ufundi,maana nasikia mko fiti,tuone n namna gani ya kuileta taifa stars maana nahs tumelogwa.

Hili suala lipo kila sehemu au kabila katika Tanzania..ukiwa Lindi unawaona Wasumbawanga washirikina sana..wasumbawanga anawasifia Watanga nk..ni sehemu tu ya maisha ya Binadamu na hakuna aliye maarufu kuliko mwingine kwenye hili.
 
Nikiangalia kwa haraka haraka tatizo la miuondo mbinu ni kama linakaribia kumalizika kwa upande wa barabara hasa ambapo sasa zimebakia KM15 kama ulivyosema, na kwa upande wa bandari pamoja na bandari ya Lindi kujaa michanga , mpo jirani na Bandari kubwa ya asili yenye kina kirefu ya Mtwara, kwani mna tatizo la kutosafirisha mazao sababu ya miundo mbinu kama mikoa ya Katavi na Rukwa? sioni kwa namna gani hili linaweza kuwa kipaumbele muhimu kwa nyakati zijazo labda ni za kutoka vijijini na wilayani?

Umeeleza suala la kuanzisha shule za sayansi kwa wingi ili kutoa ajira nyingi kwenye gesi asilia, sina uhakika kama una takwimu za wanafunzi wanaomaliza shule kwa mwaka iwe msingi, sekondari za chini na juu, maana mkoa wa Lindi ni miongoni mwa mikoa yenye watu wachache pamoja na ukubwa wa eneo lake, hivyo hali kadhalika inaweza kuwa hata na wanafunzi wanaomaliza kwa mwaka. Vile vile mkae mkikumbuka sekta hii ya gesi ni ya kimataifa zaidi hivyo ushindani wake kwenye soko la ajira ni mpana na mrefu. Ni kweli elimu hii ya gesi ndiyo iwe ya kipaumbele kwa hapo kaibuni? au kwenye maeneo mengine?

Lakini nina wasiwasi na uwezo wenu wa kuzalisha mazao ya chakula, maana baa la njaa hugonga hodi kila mara, vile vile hata na uzalishaji wa mazao ya ufuta, korosho, ambayo inaweza kuwa inatokana na kilimo duni na wa kimaskini.
 
Ahsante Mkuu MPUNGA .kuna haja ya kuwa na bandari za ziada kwani uwepo wa makampuni ya gesi umeifanya bandari ya Mtwara kutumiwa na makampuni yanayojishughulisha na gesi kwa Tanzania na maeneo ya kaskazini ya Msumbiji(upanuzi wa bandari unaendelea) hivyo bado kuna haja ya kuifufua bandari kwa minajili ya kusafirishia mazao. Kuhusu suala la elimu ya sayansi kweli sina takwimu sahihi lakini kama nilivyosema pamoja na masuala ya gesi kuwa ya kimataifa zaidi lakini kuna kazi ambazo bado zinahitaji wazawa wenye ujuzi wa awali.Malalamiko ni mengi kwa vijana kwamba ajira zinatolewa kwa wageni lakini hoja inabaki kuwa vijana wenyeji hawana ujuzi wa awali ambao msingi wake ni masomo ya sayansi. Suala la 'njaa' au tuseme upungufu wa chakula ni kwa baadhi ya maeneo ambayo husababishwa na wadudu na wanyama waharibifu na kwa kiasi fulani mvua zisizotosheleza.Lakini kuna ziada ya chakula cha muhogo kutoka maeneo ya Newala lakini pale inapotokea kuna wananchi wameathirika na wanahitaji chakula cha msaada hawakubali muhogo bali mahindi kutoka Serikali Kuu.
 
Last edited by a moderator:
hv kuna uhusiano ganI kati ya jina st warburger na hospital ya nyangao
 
hv kuna uhusiano ganI kati ya jina st warburger na hospital ya nyangao

St warburger ni wamisionari wa Benedictini walioko huko Ulaya kwenye monestari ya st warburger(makao makuu yao). Inawezekana wao ndio waliojenga na kuindesha hospitali ya Nyangao.( mwenye maelezo ya kina anaweza kunirekebisha nilipokosea)
 
Vipi suala la Maji? wananchi wanapata maji ya chumvi? au maji safi? vipi kuhusu wauza maji kwa mkokoteni dumu la lita 20 kiasi gani mnanunua?
 
Nimekatiza sehemu mbalimbali nikitumia usafiri wa bodaboda katika maeneo ya mjini nachingwea na pembezoni mwake. Nimekumbana na wajasiria mali walio amua kujiajiri kwa kuuza mafuta ya petrol kwa njia ya kujaza kwenye chupa za maji ya uhai. Vipi hili suala mnalionaje, ni kua watu wanalala na petroli kwenye majumba yao.
 
Naomba nimjibie hili kwakuwa na mimi huwa napita sometimes hapo nikielekea Mtwara.

Basi linalotoka saa 12 alfajiri Ubungo hufika Lindi mjini saa sita na nusu mchana mpaka saa saba. Umbali wa Dar to Lindi ni around 440 km hivi na kidogo

Yeah. Na mimi niweke inputs kidogo. Umbali wa Dar- Lindi kwa mujibu wa Tanroads ni kilometa 460 net. Na umbali wa Lindi- Mtwara ni kilometa105, Lindi - Mnazi mmoja kilometa 20, Lindi-Masasi kilometa121, Masasi- Nachingwea( ambayo ni wilaya iliyochangamka sana mkoani Lindi ) ni kilometa 80. Hivyo Lindi hadi Nachingwea ni kilometa:121+80=201, na hivyo kufanya umbali kutoka Dar-Nachingwea kuwa kilometa 680 hivi, umbali karibu sawa na Dar- Makambako. Bahati mbaya Masasi- Nachingwea hamna lami.
 
Kaka Madukwapa. Miji ya Lindi na Mtwara yote iko pwani tena pwani hasa kwa maana imezungukwa na bahari. Lakini kuna hili la umwinyi. Mji wa Lindi unalalamikiwa kuwa na ubwenyenye sana na ndiyo maana unadumaa, tofauti na Mtwara ambao pamoja na kuwa eneo la pwani wako tofauti kidogo na wenzao, je kwa tathmini yako, madai haya ni ya kweli?
Kama ni ya kweli unashauri nini kifanyike? Kwa upande wa Mtwara, kitongoji cha Mikindani na Kiyanga( Chuno) vina tabia sawa na mji wa Lindi yaani Umwinyi sawa na Bagamoyo na Ujiji, na kwa haraka maeneo hayo yanakuwa nyuma, kwa mtazamo wako, nini kinaweza kufanyika kubadili mindset za watu wa maeneo tajwa? (Nikideclare interest mimi ni mwenyeji wa kusini pale mjini Mtwara japo niko nje ya kusini kikazi na kutafuta rizki)
 
sababu kuu ya kuugawa mkoa kuwa mikoa kuwa miwili naamini ni kitokana na eneo kuwa kubwa...... Pia serikali hugaww mkoa ili kurahisisha ktk utoaji huduma za jamii kwa wananchi... Ni kweli lindi ilipewa eneo kubwa mno na ndyo maana serikali ina mpango wa kuugawa mkoa wa lindi tena ili kufikisha huduma kwa wnanchi kwa urahisi.. Inasemekana mkoa mwingine makao makuu yatakuwa ktk wilaya ya nachingwea...
Suala la kwanini lindi ilipewa eneo kubwa siwezi jua kwa kweli

Cha ajabu ni kuwa mkoa wa Lindi una eneo mara tatu ya Mtwara lakini watu wake ni wachache sana kuliko Mtwara. Eneo kubwa la mkoa wa Lindi ni misitu.
 
Radio za fm zinazosikika Lindi vituo vyake viko Mtwara mjini kama vile Pride fm,Safari radio na info radio..aidha kuna radio zingine za fm zinazosikika kutoka Dar .

Niko Ruangwa hapa ni Radio za CCM tu ndo zinakamata; TBC, UHURU na Newala, na clouds FM kwa mbaliiiiiii.
Na Hapo tumefunga antenna juu kama ya TV.
 
mimi nimezaliwa na kukaa mda mrefu wilaya ya nachingwea.. Ila sijawahi ona tatizo la ukosefu wa nafasi za kulala guest.. Mkuu kuwa mkweli kama umeulizia guest za jiran na stend bas ni kawaida kujaa maana jiulize wagen mpo wangapi.. Kuna msimu kunakuwa na wageni wengi sana hasa wafanyabiashara wa madini viongozi wa serikali na watumishi wapya.. Nakushauri tafuta mwenyeji akupeleke guest zingine mbali kidogo na stendi...Kuhusu uasherati ni hulka ya mtu... Ktk mikoa yote wapo watu wanaopenda uasherati.. La msingi ni ww kuepuka uasherati vinginnevyo utavuna UKIMWI
Angeenda usafiri guest house pale.
 
Nilifika eneo moja la mpigamiti lile eneo linalima sana mahindi na mambo yetu yale ya ngende ila barabara yakufika kule kutoka Liwale mjini ni mbovu kabisa,.Je,serikali yenu ya mkoa wa Lindi ina mpango gani wa kuunganisha barabara ya lami kutoka Nachingwea mpaka Liwale na kuunganisha barabara ya changarawe kutoka Liwale mjini mpaka Mpigamiti.Kwa utafiti wangu niliofanya kidogo nimeona wilaya ya Liwale inalima sana mazao ya chakula.
 
Kwa sasa kg ya ufuta ni sh 2200 hadi 2500 msimu wa kuvuna ufuta ni mwezi june.. Na huuzwa ktk vyama vya ushirika... Maandalizi yake huanza mapema mwezi february.. Na humwagwa shambani mwezi march na kuvunwa.mwezi june... Kuhusu hekta moja kutoa gunia ngapi inategemea na mkulima.. jimsi anavyolijali shamba lake na kufuata kanun za kilimo

On average inakuwa ngapi??
 
Naomba nimjibie hili kwakuwa na mimi huwa napita sometimes hapo nikielekea Mtwara.

Basi linalotoka saa 12 alfajiri Ubungo hufika Lindi mjini saa sita na nusu mchana mpaka saa saba. Umbali wa Dar to Lindi ni around 440 km hivi na kidogo

Barabara haisumbui??
 
Kutoka.dar kwenda lindi ni wastani wa.mwendo wa kawaida wa masaa 6 kwa sababu kipo kipande cha zaidi ya km 15 hakina lami.. Tunaamin kikikamilika tutumia hata masaa 5. Kwa sasa uktoka dar saa 1 unaweza fika lindi saa 7 mchana.. Usafiri si shida sana tena naamini ishindani itaongezeka kipamde cha barabara kilichobaki kikimilka na hvyo itashusha zaidi nauli.. Kwa sasa yapo mabasi yanayoanza.safari saa 12 asubuh. Saa 2 asubuh na saa 6 mchana...
Hata hivyo kwa wilaya Ya kilwa ambyo ipo karibu zaidi na dar kuna daladala myingi zinafanya safari zake mara kwa mara.. Kwa upande wa mchingwea ni mwendo wa masaa 9 hadi kumi kutoka dar.. Yapo mabasi yanatoka saa 2 na saa 12 asubuhi.. Kwa upande wa wilaya ya liwale ni mwendo wa masaa hadi 12 kwa sababu ni wilaya iliyo mbali sana kutoka makao makuu ya mkoa.. Kwa uoande wa ruangwa ni mwendo wa masaa 9 hadi 10

Umejibu vyema mkuu, Thanks

Hiko kipande kinajengwa au wamesimama tu?
 
Back
Top Bottom