KERO Kero ya Maji katika manispaa ya Lindi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kumekuwa na changamoto ya maji kutotoka katika manispaa ya mji wa Lindi katika maeneo mengi haswa Lindi Mjini, Ng'apa, Mchinga, Mitwero. Na ni zaidi ya wiki moja sasa bila maeneo haya kupata maji. Maeneo haya ni maeneo muhimu kama sehemu za mjini kati, lakini pia yana sehemu muhimu kama Hospitali ya Rufaa ya mkoa, Chuo Cha Sayansi za Afya Lindi, Shule za Sekondari na msingi, Zahanati n.k

Sababu inayotolewa na mamlaka imekuwa ni "changamoto ya umeme katika chanzo cha maji cha Ng'apa." Lakini mamlaka haielezei wazi ni changamoto gani na ni hatua zipi zimechukuliwa ili kuitatua. Na pia ni jitihada zipi zinafanyika kwa kushirikiana na Tanesco ili kutatua changamoto hiyo na wananchi waendelee kupata huduma hii ya msingi.

Soma Pia: LUWASA yaagizwa kuchunguza changamoto ya miundombinu ya maji Lindi

Viongozi wa mkoa na manispaa, mbunge wa jimbo la Lindi na Mchinga, waichukulie kero hii kuwa ukubwa wake na wawasaidie wananchi wa Lindi kuondokana na kero hiyo maana inawaweka katika kipindi kigumu sana.
 
Miaka sitini ya uhuru bado maji ni tatizo.....
 
Back
Top Bottom