Mkoa gani mzuri wa kuanzia life hapa bongo?

Naskia Hungumalwa bado mnajua nyerere ndo mkuu wa nchi. Nina shangazi yangu huko ame re-seat mtihani wa la saba mara 16 mpaka amepita kwa huruma ya baraza.

Dah hii kubwa kuliko, la saba re-seat mara 16 fom foo itakuaje?


 
Nenda ukaishi katika mikoa inayoyotwa Big Four, Morogoro, Iringa, Mbeya na Ruvuma watu wanalima sana na vitu bei cheee hasa ukiwa wilayani.

mkuu! Kama jamaa yupo serious ni bonge la ushauri,kwani akiwa wilayani, atajishughulisha na kilimo pia, kama njia ya kuongezea kipato. Mi namshauri aende moro, wilaya kama k'mbero, ulanga, hata kilosa panamfaa!
 
uzuri wa Mwanza:
1. Bei za chakula na makazi ni fair/chini.
2. Usalama upo.
3. Ukiwa mlokole makanisa kibao, yamechangamka.
4. Ukiwa mtu wa burudani (za ndani na nje) viwanja kibao.
5. Miundombinu ya uhakika. Roads, airport, port.

mwanza hoyee!
 
Senetor,naomba uanze kuhesabu kura bila kuchakachua. haya 1 2 3 - 21 duh mza imepata kura nying. karb mza mkuu!
 
kaka njo kwe2 2nduma kwana usafiri kwenda mikoa mingine ni nafu we njo na mabox 5 ya kondom 2
 
Senetor stay in dar, don't go anywhere, dar es salaam is one of the fastest growing city in africa, a lot of opportunities are there, head office karibu zote ziko huku, raha zipo huku, pesa zinatafutwa huku, in dar es salaam everyday is a new day with a new challenge, traffic jam ya kufa mtu lakini tunanua magari daily, please senetor stay to face challenges of the big city, as challenges makes us grow, hao wanaokushauri uende mikoa wanakupoteza, dar is easy kupata pesa than mikoan, unaweza ukashangaa mshahara wako usiuguse hata mwaka unaishi kwa deals tu, please senetor stay
 
Dar,Mwanza,Arusha na Mbeya ndo miji itayokufanya ubongo ucheze,kwingine utaishia kubweteka ujione umefika kumbe ndo kwanza hata hujaanza!
 
Wadau wa MMU,naomba kuuliza,ivi hapa tanzania ni mkoa gani mzuri ambao atleast life liko cheap,ambapo mtu anae anza maisha let say na salary ya kuanzia 400k-600k anaweza kusurvive?

Nakushauri uende MWANZA
 
Dar,Mwanza,Arusha na Mbeya ndo miji itayokufanya ubongo ucheze,kwingine utaishia kubweteka ujione umefika kumbe ndo kwanza hata hujaanza!
 
Siwez comment unless umeweka hadharani vitu ambavyo unataka viwepo uko unakotaka uende kuishi!
Is it cost of living,cost of living,good infrastructures,starehe kwa wingi etc
 
Dar, hasa maeneo ya Mbez beach,Masaki na Msasani...maisha ni marahisi sana maana kipato ni maradufu ya matumizi yako. iwe halali au haramu. upo apo....kazi ni kwako.
 
Serikali yetu inahakikisha hakuna anayekufa kwa njaa hivyo usihofu...ok, sehemu yo yote katika JMT inafaa inategemea unafanya kazi katika taasisi gani, ukiwa polisi trafik inalipa sana, au kama TRA, Baadhi ya benki nk. kinachatakiwa ni kuchangamkia dili, mshahara kwa kawaida hautoshi na hautatosha kwa mtumishi wa kawaida hasa wewe unaeanza kazi, infact siku za mwanzo utapigika mpaka uingizwe kwenye channel baada ya kuaminika kwamba hutatoa siri au ww sio Speke (mpelelezi).
 
maisha ni popote na maisha yako yatategemea na jinsi wewe mwenyewe utakavyotaka yawe.unaweza kuishi popote pale kulingana na wewe utakavyotaka uishi.mikoa yote inakaliwa na watu na hakuna mkoa hata mmoja ambao watu wake wameuhama kwa kisingizio kuwa eti maisha ya mkoa huo yamekuwa ya juu sana kuliko sehemu nyingine.kwa hiyo nduguyangu itategemea na mtizamo wako ulivyo.kwa hapa TZ mikoa yote iko poa tu.hata pemba life ni poa tu.
 
Kwanza nawaomba wana MMU kujibu swali kama lilivyo...mtu anauliza mkoa unamtajia sumbawanga,songea,loliondo n.k.
Pili nimebahatika kutembelea mikoa yote bara na visiwani kasoro mikoa mipya.
Kama vipi Chagua kwa kufuata rank hii
1:Morogoro
2:Mwanza
3:Iringa
4:Mbeya
5:Njombe (mkoa mpya)
6:pwani
 
Dogo unachagua mkoa au unachagua kazi? Inabidi ufahamu kuwa hata hiyo mikoa unayoiona ina nafuu ya maisha haina maana kuwa unafuu unajileta wenyewe. Watu wanachakarika, wanajituma na kuwa wabunifu, yote hayo ni katika kukabili na kuyatawala mazingira yawazungukayo.
Acha kujidekeza, Ukitaka kuishi maisha ya peponi kwa kutegemea mshahara utakufa si tu masikini bali fukara wa kutpwa.
Kijana usipende sana maisha raisi na uraisi wake bila kuweka akili na kupindisha mgongo. Inakuwaje wataka cha uvungu ila mvivu kupinda mgongo!

USIONE VYAELEA VIMEUNDWA!
 
nenda chuo cha maisha,namaanisha TABORA mkuu,pale vitu bei cheap lakini upatikanaji wa pesa ndio issue.

Kweli kabisa mkuu,mkoa wetu tunauweza wanyamwezi wenyewe tu!!Ha ha haaa!!Ukiweza kuishi Tabora huwezi shindwa kuishi popote duniani!
 
Back
Top Bottom