Vladmir Putini
JF-Expert Member
- Mar 22, 2022
- 777
- 1,442
Wakuu habarini za muda huu,
poleni kwa majukumu. Maisha yana changamoto espicially kwa vijana ila tusikate tamaa tuendelee kupambana.
Wakuu kama mada inavyojieleza, nilikuwa naomba ushauri wenu mnijuze ni mkoa/mji gani hapa Tanzania nikienda kuishi gharama zake za maisha walau zina afadhali/ziko chini tofauti na mikoa mingine?!
Nimekuja humu kwa sababu naamini kuna watu kutoka sehemu mbali mbali za Tanzania hii na wengine wameishi sehemu mbalimbali pia wana experience hiyo tayari.
Binafsi sijaishi sehemu nyingi sana Tanzania, nimeishi mikoa ya Singida (nilikozaliwa na kukulia), Arusha, Mwanza, na Zanzibar(Unguja) nilipo kwa sasa.
Sasa kwa hizi sehemu chache nilizo bahatika kuishi kuna baadhi ya sehemu hasa Arusha na Unguja gharama za maisha ziko juu mno, kuanzia room za kulipa kodi ili uishi, bidhaa za vyakula, mavazi yani ziko juu mno.
Mfano, room za kuishi kwa zanzibar chumba kawaida tu chenye umeme ni elfu mpaka 50 per month alafu ni cha kawaida sana na kidogo tu, chumba cha master (self contained room) ni mpaka elf 70+ mpaka laki moja per month.
Sasa kwa uchumi wangu kwa kweli haya maisha kwa huku naona kama magumu sana.
Sasa kama nilivyosema kwa sasa nipo Zanzibar(Unguja) ila nataka nikimbie nitoke huku kabisa, nna mtaji kama wa million 3 hivi nilikuwa naomba wadau mnishauri ni mkoa gani hapa Tanzania naweza ishi ambapo gharama za maisha zitakuwa za chini kidogo ambapo naweza kuanza maisha kwa hizo million 3.
Sehemu ambayo naweza fanya bishara ndogo ndogo, hata kama ni kilimo cha msingi maisha yaende tu.
NB: Nna 28 years, sijaoa kwa hiyo kuhama kwangu toka sehemu moja kwenda nyingine ni rahisi sana.