Mkoa gani mzuri wa kuanzia life hapa bongo?

Wakuu kuna watu wanajaribu sana kuisema Arusha kuwa maisha ya hapa yako juu
Ni kweli kuwa maisha ya hapa yako juu ila sio kihivyo sana
Ni namna ya kwako ya kuishi na kujipanga
Kweli maisha yako juu ila ukijipanga mambo yanaenda tuu

mkuu,arusha tuna investments zetu huko so mara nying napatembeleaga..napajua vzr,vitu viko ghali sana,huwezi pata rum ya maana chini ya buku 80.
 
dah!!atleast morogoro.vp kuhusu dodoma na mwanza?

mwanza maisha yapo cheap sana, karibu. ce wenyeji tulianza kwa box 3 bt tumeishi. maji yapo ya kumwaga,vyakula ndo usiseme hakunaga uhaba wa vyakula. coni shda kbsa hapa mwanza. may b wanajf wengne walio rock city wafunguke zaidi. karibu masato na masangara mkuu!
 
twara kaka,kule maisha ni ya chini sana,hata kwa kilo 2.5 unaisha maisha fresh tuu
 
Naskia Hungumalwa bado mnajua nyerere ndo mkuu wa nchi. Nina shangazi yangu huko ame re-seat mtihani wa la saba mara 16 mpaka amepita kwa huruma ya baraza.


Huyo ana mambo yake bana
Huku tumeendelea bana na tuna kila kitu kilimo ndio usiseme mashamba makubwa yenye rutuba bana
Kwa sasa kana unataka nunua mpunga njoo huku

mkuu,arusha tuna investments zetu huko so mara nying napatembeleaga..napajua vzr,vitu viko ghali sana,huwezi pata rum ya maana chini ya buku 80.


Mkuu ni kweli ila inategemea na maeneo unayotaka kuishi
kama ni sakina au njiro au moshono au nguleklo ni lazima rum ziwe ghali ila kuna maeneo rum bado ziko bei cheap
Kuna nyumba nilikaa mimi sakina tena nyumba nzima ya rum nne nilikuwa nalipa laki na nusu kwa mwaka na ilikuw ana huduma zote
So mkuu ni uchaguzi wa maeneo na aina ya maisha unayotaka
Ukitaka maisha ya juu na kila siku uko kwenye stuli ndefu lazima upigike kaka
 
Mh ungekuwa muazi kidogo kuna kazi ambazo si kila mahali zipo chali na hali ya hewa inatofautiana ndugu joto baridi vumbi jiachie tukusaidie zaidi
 
Mkuu Simiyu tena
Duh huuko hapana aise
Msimu wa ukame unakuwa ukame kweli
Na maji ni km 10 tena kw apunda tena ya kisima
Sema anawez apata pata samaki wa pale Magu mitaaya Lamadi hivi

maji ya kisima ni safi, salama, natural, na yanaleta long life, wanaotumia maji ya kisima wanapata umri mkubwa mpaka wanadhaniwa wachawi.
 
Mi nadhani kila mahala panategemea style yako ya maisha...kwa sababu kwenye hiyo miji kuna watu wana kipiatomkwa mwezi chini ya hizo unazopata na wanasurvive.....so inategemea na priorities zako umewekeza vipi...?
 
Nenda ukaishi katika mikoa inayoyotwa Big Four, Morogoro, Iringa, Mbeya na Ruvuma watu wanalima sana na vitu bei cheee hasa ukiwa wilayani.

Iringa noma, si panaongoza kwa kale kamdudu hatari?. Mie namshauri aje hapa Morogoro - Kirombero. Kuna bwabwa la kutosha.
 
uzuri wa Mwanza:
1. Bei za chakula na makazi ni fair/chini.
2. Usalama upo.
3. Ukiwa mlokole makanisa kibao, yamechangamka.
4. Ukiwa mtu wa burudani (za ndani na nje) viwanja kibao.
5. Miundombinu ya uhakika. Roads, airport, port.
 
Back
Top Bottom