Mkeo/mpenzio afanyeje ukubali.....

Another dimension..asante japo its too general.Sitaku kuamini kuwa kwenye DECI walikuwa wanawake tu.
Sitaki kuamini kuwa waliokufa kule kwa Kibwetere walikuwa wanawake tu.Nasita kuamini kuwa waliokuwa kwenye cults deaths kule Jonestown - Guyana walikuwa wanawake tu! I could go on and on - hadi kwa akina Kakobe, na wengineo
Sio kwamba ni wanawake peke yao, ukiangalia ratio hata bila kuhesabu utaona wanawake ndio wengi. Kama ukibahatika kuwauliza wanaume waliopo utagundua nao hawapo jumla jumla ila wanapima joto kiaina.
 
Dada WOS, Kwa mtiririko wa hizi post nimepata jibu moja tu kwa swali la kwanza;WANAUME WANAOGOPA KUFA.
Swali la pili bado jibu sijaliona,sijui washawishiwe vipi!
Charity DC amekuwa akipreach bedroom diplomacy natamani kweli atuonyeshe ndo ikoje maana angesaidia sana hapa.

DC please baba nakuomba niko chini ya miguu yako (najua umevaa sarawili) tupe japo kiduchu huko kwingine tutaweka vetu itakaa tu!!
 
Hata mimi huwa wananishangaza sana.Nimegundua kwamba wanaume ni waoga kulijko wanawake.

Dada WOS, Kwa mtiririko wa hizi post nimepata jibu moja tu kwa swali la kwanza;WANAUME WANAOGOPA KUFA.
Swali la pili bado jibu sijaliona,sijui washawishiwe vipi!

Kukataa kupima tu ndo wanaonekana waoga? Mbona usiku kitu kikigonga nje mama anakimbilia uvunguni wakati mzee anaende mlango kupambana. Hamjawajulia tu ndo maana mnawasha mto bila sababu wakati maji ya kuuzima yamekatika.

Hilo limejibiwa sana (red). Hebu jaribu kusoma tena. Hujakutana na kitu kinaitwa bedroom diplomacy?
 
On A SERIOUS NOTE....
Chris na Fidel...
hivi mnaogopa nini hasa?
kama mu waoga hivyo kwanini bado kamchezo hamuachi?
Woga huu ungeelekezwa katika ku abstain hamuoni tungepunguza kiwango cha maambukizi na Tanzania bila UKIMWI ingewezekana?

Ni katamu kweli kweliiiii.......
Kimsingi gonjwa hili limekaa mahali pabaya:mad:
 
bht,

Sifichi kichwa, tatizo langu ni majibu ya kumwambia mtu ataishi kwa matumaini! Frankly speaking sielewi maana ya neno "kuishi kwa matumaini" - To me that sounds like "a death row"!
ACCORDING TO ME!...mtu ataishi kwa matumaini AKISHAJUA HANA VIRUSI VYA UKIMWI!

hainiingii kichwani kwamba UNA VVU,THEN UNAISHI KWA MATUMAINI!I CAN'T CONNECT THEM DOTS,lol
 
ACCORDING TO ME!...mtu ataishi kwa matumaini AKISHAJUA HANA VIRUSI VYA UKIMWI!

hainiingii kichwani kwamba UNA VVU,THEN UNAISHI KWA MATUMAINI!I CAN'T CONNECT THEM DOTS,lol

G wewe ni kichwa!

Ni mwendo wa kupeana false hopes!

Labda niseme kuwa, wengi wetu tunawaongelea watu wengine. Hautajawahi kupima au kama tumepima hatukukutwa na hivyo VVU. Kwa hiyo hakuna mtu hapa anayeishi na VVU. Kama kuna mtu alishapima akakuta anavyo ndo aje atueleze (bila kuahidiwa posho au mchango wa kuanzisha NGO) ili tuwe practical. Hizi theory zitatumaliza!
 
Kukataa kupima tu ndo wanaonekana waoga? Mbona usiku kitu kikigonga nje mama anakimbilia uvunguni wakati mzee anaende mlango kupambana. Hamjawajulia tu ndo maana mnawasha mto bila sababu wakati maji ya kuuzima yamekatika.

Hilo limejibiwa sana (red). Hebu jaribu kusoma tena. Hujakutana na kitu kinaitwa bedroom diplomacy?[/QUOTE]

Charity DC amekuwa akipreach bedroom diplomacy natamani kweli atuonyeshe ndo ikoje maana angesaidia sana hapa.

DC please baba nakuomba niko chini ya miguu yako (najua umevaa sarawili) tupe japo kiduchu huko kwingine tutaweka vetu itakaa tu!!

Plzzz DC naomba tufunde kidogo hii kitu BD.
 
Mimi nikapime? Labda mnibebe kwa greda la Konoike nikiwa nimefungwa pingu za Jerry Muro Miguuni na mikononi!
Hahaha kazi kweli kweli,juzi nimepima damu hahaha nimepewa majibu kesho yake ile napewa majibu kitu cha kwanza ilikuwa ni kuangalia kwenye HIV antibodies du naona Sijui Elisa test na kipimo kingine nimekisahau jina jibu NEGATIVE.baada ya kutoka hapo ndo sasa nikaanza kuangalia haemoglobin,sijui sedimentation rate na mengineyo.
Inahitaji MOYO,Mmme wangu na yeye huwa anapima bila matatizo,ila wanaume wengine wako kama wewe.Tatizo huwa ni pale mna mgonjwa anahitaji damu hahaha nakumbuka kaka zangu huwa wanakimbia.
 
Charity DC amekuwa akipreach bedroom diplomacy natamani kweli atuonyeshe ndo ikoje maana angesaidia sana hapa.

DC please baba nakuomba niko chini ya miguu yako (najua umevaa sarawili) tupe japo kiduchu huko kwingine tutaweka vetu itakaa tu!!

Hapana dada, leo nimevaa sketi kama za wale jamaa wa Scotland!

Lakini mbona nimeshasema sana! Ngoja nikatafute kitu cha kuongeza glucose nisije kudondoka mkasema naogopa ANGAZA!
 
Sifichi kichwa, tatizo langu ni majibu ya kumwambia mtu ataishi kwa matumaini! Frankly speaking sielewi maana ya neno "kuishi kwa matumaini" - To me that sounds like "a death row"!

Hahahaha ndo hivyo unaishi kwa matumaini kwa kudra za mwenyezi Mungu baada ya kupima.
Yaani ukipita barabarani unayaona masanduku unajisemea moyoni any time nitawekwa mle.
Alafu baba_Enock vp Billionare clup siku hizi hupiti piti? Juzi kati nilikuwepo pale kula beer za 2000 samahani kwa offtopic.
 
ACCORDING TO ME!...mtu ataishi kwa matumaini AKISHAJUA HANA VIRUSI VYA UKIMWI!

hainiingii kichwani kwamba UNA VVU,THEN UNAISHI KWA MATUMAINI!I CAN'T CONNECT THEM DOTS,lol

True bro,

Ukipima na kukuta upo +ve - naamini kila siku utakuwa unaota makaburi na majeneza and all sorts of nightmares! Wengi nadhani wa-turn into nusu-mfu nusu-mzima - hauwezi kuishi kwa matumaini wakati you are truly sure (ceteris paribas) kwamba in the next 3-5 years watu watakulia "mchele" na kukunywea bia!

Also, wengi wakikutwa +ve wanaaza KUKESHA na KUSALI - the likes of Waumini wa Kakobe e.t.c - Kwa njia hii mwili unakuwa drained nguvu yote (hapati chakula, hapati mapumziko ya kutosha, hapati basic needs)na kifo kinamnyemelea within no time.
 
leteni MICHANGO ZAIDI...naona mada inanoga....
woga wa kufa.....
kuishi kwa matumaini hakueleweki maana yake nini...
tatizo kupokea majibu...
wanaume wanapima risks za kupima..against faida....
eheeee......
 
biashara ya kupima MIMI SITAKI KUISIKIA!niliwahi KUDANGANYIKA nikapima lakini kabla ya kupima dokta aliniuliza UNAPIMA ILI IWEJE?...UMEFANYA NINI KIBAYA/AU UMEKANYAGA WAPI AMBAPO HUJIAMINI?......akanipa muda ''KIJANA,NENDA HOME KAFIKIRIE MARA MBILI,UAMUZI UNAOTAKA KUUCHUKUA NI MGUMU MNO..''

NIKACHAPA RABA,MPAKA KESHO
Geoff kabla ya ndoa yako hamkupima?kupima ni muhimu ili kujua afya zenu,mimi huwa nasema hata walio SeroPositive kwa sasa na wao kuna siku hapo nyuma walikuwa seroNegative.Ni muhimu kujua immunity.Ila kusema ukweli unatakiwa uwe tayari kupokea majibu.
 
True bro,

Ukipima na kukuta upo +ve - naamini kila siku utakuwa unaota makaburi na majeneza and all sorts of nightmare! Wengi nadhani wa-turn into nusu-mfu nusu-mzima - hauwezi kuishi kwa matumaini wakati you are truly sure (ceteris paribas) kwamba in the next 3-5 years watu watakulia mchele na kukunywea bia!

the red part..... siyo kweli ndugu yangu...labda kama unaenda kupima wakati uko stage ya UKIMWI....
Ukipima stage ya virusi tu with no symptoms..utadunda hadi hata wale wasiokuwa + ve wanakata roho wewe upo tu ...ndio faida ya kujua mapema
 
True bro,

Ukipima na kukuta upo +ve - naamini kila siku utakuwa unaota makaburi na majeneza and all sorts of nightmare! Wengi nadhani wa-turn into nusu-mfu nusu-mzima - hauwezi kuishi kwa matumaini wakati you are truly sure (ceteris paribas) kwamba in the next 3-5 years watu watakulia mchele na kukunywea bia!
halafu kibaya zaidi....!
1-WATAKUZIKA UCHI
2-WATAKUKANYAGIA MKEO
3-MALI ZAKO NDUGU ZAKO NA WANAO WATAZITUMIA KUFANYA UASHERATI

nikiwaza hilo,ANGAZA NAPAONA KAMA KUZIMU!lol
 
Hahahaha ndo hivyo unaishi kwa matumaini kwa kudra za mwenyezi Mungu baada ya kupima.
Yaani ukipita barabarani unayaona masanduku unajisemea moyoni any time nitawekwa mle.
Alafu baba_Enock vp Billionare clup siku hizi hupiti piti? Juzi kati nilikuwepo pale kula beer za 2000 samahani kwa offtopic.

Hilo linasikitisha sana na kufanya watu wapoteze hata hamu ya kuishi. Ila nimejikuta nacheka hadi machozi yananitoka. Nisameheni jamani, hili suala ni zito!
 
Hahaha kazi kweli kweli,juzi nimepima damu hahaha nimepewa majibu kesho yake ile napewa majibu kitu cha kwanza ilikuwa ni kuangalia kwenye HIV antibodies du naona Sijui Elisa test na kipimo kingine nimekisahau jina jibu NEGATIVE.baada ya kutoka hapo ndo sasa nikaanza kuangalia haemoglobin,sijui sedimentation rate na mengineyo.
Inahitaji MOYO,Mmme wangu na yeye huwa anapima bila matatizo,ila wanaume wengine wako kama wewe.Tatizo huwa ni pale mna mgonjwa anahitaji damu hahaha nakumbuka kaka zangu huwa wanakimbia.
Mama 5J,
Hiyo red, Kama mnaishi kwa uaminifu kwenye ndoa yenu una wasi wasi gani? Kama huna mashaka umeguswa na damu chafu au umepita nje ya bedroom mliyohalalishiwa kwa nini kupimapima???
 
Back
Top Bottom