Mkeo/mpenzio afanyeje ukubali..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkeo/mpenzio afanyeje ukubali.....

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by WomanOfSubstance, Mar 4, 2010.

 1. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #1
  Mar 4, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 0
  Katika suala zima la kupambana na UKIMWI, kitu ambacho kimeendelea kuleta utata na mtafaruku mkubwa katika familia, ndoa na mahusiano mengi ni suala la kupima na kujua hali ya mhusika kama amepata maambukizi ama lah!
  Tatizo linalowapata wanawake wengi ni kuwashawishi wanaume kupima virusi. Wanawake wajawazito hujikuta "wakilazimika" kupima ili kuwakinga watoto walio matumboni mwao na virusi wakati wa kujifungua au wakati wa kunyonyesha. Wapo pia wale wenye kutaka kujua hali zao ili waishi kwa matumaini ikiwa ni pamoja na kujikinga na maambukizi mapya. Tatizo linakuja: mwanamke akipima akagundulika ana virusi, basi kumetokea vurugu na fujo za kila aina na lawama kwamba kwanini kaenda kupima.Ina maana kuishi maisha ya kubabaisha na kuficha kichwa mchangani kama mbuni ndio njia iliyo bora zaidi?
  je,
  1. Kwanini wanaume wengi hawataki kupima na kujua afya zao ( majority wanajua kabisa kuwa wanaishi maisha hatarishi ( risky life styles)
  2.Mbinu gani zitumike kuwashawishi wanaume wasiotaka kujua afya zao kupima kwa hiari?
   
 2. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #2
  Mar 4, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,476
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Hii mada dada mh ngoja waje wenyewe.
  Mimi ningependa kujua mbinu za kuwashawishi kwenda kucheck afya zao.
   
 3. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #3
  Mar 4, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,834
  Likes Received: 249
  Trophy Points: 180
  Tatizo la msingi ni UDUNI wa huduma za afya.

  Swali kubwa linakuwa: je nikipimaVVU na nikaonekana +ve what is the way forward?

  Majibu tunayopewa na washauri nasaha hayatoshelezi kujibu swali hilo!
   
 4. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #4
  Mar 4, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 0
  Na hili ndilo linawatatiza wengi na kuwatia hofu ya bure.
  Kwanza watu wanapaswa kujua kuwa kuwa na VVU haimaanishi una UKIMWI. Kugundua mapema kunakuwezesha kuvisimamisha virusi visiingie kwenye stage ya kukupa UKIMWI.Unapojidanganya na kubaki na ujinga wa kutokujua, ujue sooner rather than later utaingia kwenye UKIMWI na utateseka hadi kufa mapema, kumbe ungeweza kujiongezea afya,siha na maisha yenye ubora.Chagua unataka kipi kati ya hayo.
  Kumbuka kutokujua hali yako, hakukufanyi wewe ukawa salama!
   
 5. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #5
  Mar 4, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 0
  MJ1 na mimi nawataka hasa wao waje watuambie........
   
 6. bht

  bht JF-Expert Member

  #6
  Mar 4, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  sasa baba E mbona kamchezo ka mbuni haka?? waficha kichwa tu.....
   
 7. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #7
  Mar 4, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,973
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 145
  haya mambo wengine hatuyapendi kabisaaaaaaaaaa ukisha pima ukijua itakusaidia nn?
   
 8. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #8
  Mar 4, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,174
  Likes Received: 3,218
  Trophy Points: 280
  utaishi kwa matumaini
   
 9. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #9
  Mar 4, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 54,221
  Likes Received: 31,338
  Trophy Points: 280
  Mimi nikapime? Labda mnibebe kwa greda la Konoike nikiwa nimefungwa pingu za Jerry Muro Miguuni na mikononi!
   
 10. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #10
  Mar 4, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 0
  On A SERIOUS NOTE....
  Chris na Fidel...
  hivi mnaogopa nini hasa?
  kama mu waoga hivyo kwanini bado kamchezo hamuachi?
  Woga huu ungeelekezwa katika ku abstain hamuoni tungepunguza kiwango cha maambukizi na Tanzania bila UKIMWI ingewezekana?
   
 11. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #11
  Mar 4, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,174
  Likes Received: 3,218
  Trophy Points: 280
  heeeeeee!!
   
 12. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #12
  Mar 4, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,936
  Likes Received: 384
  Trophy Points: 180
  Hofu ya Kupima mara nyingi hutokana na kazi za nje (vimada) ambao wanaume huwa nao. Na kwa kujua kwamba wanajilipua tu huko( kumega bila kinga) hofu huwajaa kwamba hujui status ya yule kimada na wewe ulikula pekupeku, sasa na wewe unakua hujui status yako ikoje na unahisi ushamuunganisha mkeo na gridi ya taifa(HIV). Hapo ukiambiwa baba fulani twende tukapime basi ni kama Volcano ime erupt, huo ukali unaotoka hapo si mchezo. Mimi nilimuahidi mwenzi wangu kwamba pindi tutakapohitaji mtoto wa pili lazima tukapime kwanza, nadhani hii ni mbinu vile vile ya kumweka mwenzio kwenye mstari akishapima akajikuta yupo fresh anaweza akaacha kazi za nje.
   
 13. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #13
  Mar 4, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 54,221
  Likes Received: 31,338
  Trophy Points: 280
  Mi kwakweli kama waifu ana mashaka akapime yeye.
  Kamchezo hako tunakacheza salama mama, ila huwezi jua manake kuna njia nyingi za kuupata huu ugonjwa! Sasa dah! no comment!
   
 14. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #14
  Mar 4, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,476
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Hawakukosea kusema Wanaume kiini cha mabadiliko lakini dawa yenu inachemka. Tatizo wapenzi wenu wakiwawekea tinted mnakwenda nje- ngoja tuhamasishe wanawake wote kuvaa miwani za mbao : No kupima no that thing tuone mtaishije lol
   
 15. Lily Flower

  Lily Flower JF-Expert Member

  #15
  Mar 4, 2010
  Joined: Oct 16, 2009
  Messages: 2,555
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Dah!!! braza hii ni kali tena uwoga wa nini wote huo?
   
 16. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #16
  Mar 4, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  dada wos, kupima ni biashara ya wazungu. waafrika tangu zamanimpaka leo tunaishi na ukimwi mwilini mwetu na hatuna shida, ukiacha ukimwi wa HIV, ukimwi wa utapiamlo na uchafu wa mazingira ni hatari zaidi. hivyo mi naunga mkono kupima kama ni sehemu ya tiba, aimeen kama itathibitika beyond reasonable doubt kuwa bila kupima hali itakuwa mbaya sana kisaikolijia.

  on top of that, kuishi na nyoka ndani bila kujua kuwa yuko ndani, ni bpora mara elfu kuliko kujua kuwa yuko ndani lakini ukashindwa kumfukuza/kumuua, nadhani hata kusinzia huwezi. now you know why we don like hayo mambo ya angaza.
   
 17. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #17
  Mar 4, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 0
  Chris..leo ni mimi na wewe tu hadi kieleweke!
  Bado narudi tena palepale - imagine kuna vyombo viwili vyenye maji... kimoja maji yake yametiwa sumu ukinywa utakuja kufa baada ya muda mfupi na cha pili maji yake ni salama unaweza kunywa. Unachotakiwa ni wewe kuomba tu wayapime ujue yapi ni salama.

  Je, ukiambiwa hivyo utasema ngoja nibahatishe ninywe nione kama nitakufa, au utaomba yapimwe ujue yapi ni salama uyanywe?
   
 18. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #18
  Mar 4, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,973
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 145
  Nitaishije kwa matumaini wkt naendelea kuishi navyo jua mm.

  Hahahaha mm siwezi kwenda kupima hata kwa pingu sioni kabisa umuhimu wa kupima .

  Mi naogopa kufa kwa kiholo tu maana ukijua ndo unajipunguzia siku hata kama mzima.
   
 19. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #19
  Mar 4, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 0
  Ama kweli akilini kichwani! Nimeamini.
  The blue part nimebaki hoi!...ngoja tuone michango zaidi
   
 20. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #20
  Mar 4, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 0
  unahitaji counselling y a nguvu tu..... utaenda mwenyewe bila hata kulazimishwa.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...