Mkeo/mpenzio afanyeje ukubali.....

title inahusu kupima.... ila kuna mchangiaji kasema wanawake wanapenda kufuata mkumbo kwenye mambo ya jumla jumla....wakati wanaume wanapenda kwanza kufanya risk assessment... i think s/he was refering to my eg kuhusu kupima kanisani baada ya uhamashishaji....

WOS,

Kama ni suala la title basi tulitakiwa kujadili mbinu ambazo mtu anaweza kutumia kumshawishi mwenzi wake wakapime.

Kama ni hivyo basi mimi nashauri akina mama waende tena shule ili wajue lini na wapi wanaweza kuwambia waume zao hayo mambo ya ANGAZA. Kwa ujumla wanaume hawapendi kuelezwa mambo ya kupima VVU (umeona mwenyewe maoni ya wengi). Kwa hiyo hili suala labda mkalijadili kwenye KP ili mje na suluhu.

Hata MJ1 aliyesema kuwa itumike nguvu (no test no food) ni bure kwani haitasaidia. Wengine wataishia kulambwa makofi na kutoa bila kufikia malengo yao. Labda wanawake waanze kufundishwa sexual diplomacy (au tuiite diplomasia ya chumbani). Kwa sasa hiyo kitu imepotea kabisa. Baadhi ya akina mama wanadiriki kuwa wababe sana bila kukua kuwa wanaanzisha vita ya mayai na mawe.
 
biashara ya kupima MIMI SITAKI KUISIKIA!niliwahi KUDANGANYIKA nikapima lakini kabla ya kupima dokta aliniuliza UNAPIMA ILI IWEJE?...UMEFANYA NINI KIBAYA/AU UMEKANYAGA WAPI AMBAPO HUJIAMINI?......akanipa muda ''KIJANA,NENDA HOME KAFIKIRIE MARA MBILI,UAMUZI UNAOTAKA KUUCHUKUA NI MGUMU MNO..''

NIKACHAPA RABA,MPAKA KESHO
 
Wewe bwana leo utakula SENKSI zangu mpaka kabox kaishe.
Tuendelee kiongozi!
 
Hahahaha alafu wadau wa kijiweni wanasema JK hakupewa majibu alikataa hahahahahaha dah hii imekaaje?
hahaha! siyo JK na mimi peke yetu tunaokimbia hiyo kitu. Hebu msome huyu hapa chini!

biashara ya kupima MIMI SITAKI KUISIKIA!niliwahi KUDANGANYIKA nikapima lakini kabla ya kupima dokta aliniuliza UNAPIMA ILI IWEJE?...UMEFANYA NINI KIBAYA/AU UMEKANYAGA WAPI AMBAPO HUJIAMINI?......akanipa muda ''KIJANA,NENDA HOME KAFIKIRIE MARA MBILI,UAMUZI UNAOTAKA KUUCHUKUA NI MGUMU MNO..''

NIKACHAPA RABA,MPAKA KESHO
 
hahahah..hajashikwa mtu pabaya...
utasubiri symptoms ndio upime? faida yake itakuwa nini kama virusi vimesha graduate to AIDS?..UNAKUMBUKA METHALI YA USIPOZIBA UFA UTAJENGA UKUTA?

Kwa VVU/Ukimwi hakuna cha kuziba ukutua. Ukikutwa unavyo ni kuwa hiyo nyumba imeshaporomoka kama imechapwa na mabomu ya Mbagala. Tungejadili jinsi ya kuficha hayo mabomu lakini wahanga waachwe tu wauguze majeraha pole pole badala ya kuanza kuchezea chezea vidonda vyao.

I mean kupima bila lengo wala mpango wa ku-deal na matokeo ni kitu kisichoeleweka (kwa upande wangu). Kwa hiyo nitapima tu kama kuna sababu ya msingi. Na kama mwenzagu anaiona hiyo sababu basi atafute nafasi nzuri sana tuongee. Akija vibaya tunaweza kumalizana kabla ya VVU.
 
hahaha! siyo JK na mimi peke yetu tunaokimbia hiyo kitu. Hebu msome huyu hapa chini!
ile kitu wacha maneno bana!lol
PREZIDAA MWENYEWE NDO KAMA HIVI hataki kusikia!madaktari wenyewe hawataki kusikia....!

mi ni nani bwana!......HAPIMI MTU HAPA!
 
hahaha! siyo JK na mimi peke yetu tunaokimbia hiyo kitu. Hebu msome huyu hapa chini!

Jamani mwisho wa siku lazima tukubali kuwa kupima ni hiari na si kushurutishwa.
Mtu unaamua wewe mwenyewe baada ya kujua faida na hasara za kupima basi unaenda kwenye VTC unapimwa na kuondoka na majibu kama haupo tayari usilazimishe nafsi.
 
WOS,

Kama ni suala la title basi tulitakiwa kujadili mbinu ambazo mtu anaweza kutumia kumshawishi mwenzi wake wakapime.

Kama ni hivyo basi mimi nashauri akina mama waende tena shule ili wajue lini na wapi wanaweza kuwambia waume zao hayo mambo ya ANGAZA. Kwa ujumla wanaume hawapendi kuelezwa mambo ya kupima VVU (umeona mwenyewe maoni ya wengi). Kwa hiyo hili suala labda mkalijadili kwenye KP ili mje na suluhu.

Hata MJ1 aliyesema kuwa itumike nguvu (no test no food) ni bure kwani haitasaidia. Wengine wataishia kulambwa makofi na kutoa bila kufikia malengo yao. Labda wanawake waanze kufundishwa sexual diplomacy (au tuiite diplomasia ya chumbani). Kwa sasa hiyo kitu imepotea kabisa. Baadhi ya akina mama wanadiriki kuwa wababe sana bila kukua kuwa wanaanzisha vita ya mayai na mawe.
Nashukuru sana DC kwa mawazo mazuri..nawashukuru pia wanaume wengine wooote wanaochangia mawazo yao.Kimsingi tuko pamoja sana... kila idea ni valid kabisa na nawahakikishia itafika kunakohusika -
ila DC naomba wewe. Tall na wengineo mlio raise issue ya dialogue na bedroom diplomacy hebu tufafanulieni zaidi..... mna maana gani mnaposema wanaume hawapendi kuambia vitu na wanawake - does this apply katika mazingira yote? je wataalamu wa kike wanapowapeni ushauri pia hamtaki?
 
Kwa VVU/Ukimwi hakuna cha kuziba ukutua. Ukikutwa unavyo ni kuwa hiyo nyumba imeshaporomoka kama imechapwa na mabomu ya Mbagala. Tungejadili jinsi ya kuficha hayo mabomu lakini wahanga waachwe tu wauguze majeraha pole pole badala ya kuanza kuchezea chezea vidonda vyao.

I mean kupima bila lengo wala mpango wa ku-deal na matokeo ni kitu kisichoeleweka (kwa upande wangu). Kwa hiyo nitapima tu kama kuna sababu ya msingi. Na kama mwenzagu anaiona hiyo sababu basi atafute nafasi nzuri sana tuongee. Akija vibaya tunaweza kumalizana kabla ya VVU.
Twende kazi kiongozi. Mi kazi yangu ni kukugongea senksi tu. Kwamba nakuunga mkono!
 
Nashukuru sana DC kwa mawazo mazuri..nawashukuru pia wanaume wengine wooote wanaochangia mawazo yao.Kimsingi tuko pamoja sana... kila idea ni valid kabisa na nawahakikishia itafika kunakohusika -
ila DC naomba wewe. Tall na wengineo mlio raise issue ya dialogue na bedroom diplomacy hebu tufafanulieni zaidi..... mna maana gani mnaposema wanaume hawapendi kuambia vitu na wanawake - does this apply katika mazingira yote? je wataalamu wa kike wanapowapeni ushauri pia hamtaki?

Afadhali sasa tunaongea lugha moja. Na haki yako ya SENKSI nimekupa kwakweli.
 
Nikisema kuna watu both wamaume kwa wanawake ambao wako selfsh naomba msinitafune- wajua mtu unapokuwa unajifikiria wewe tu peke yako ndipo unapoona ugumu wa kupima but hebu fikiria wanao wadogo na familia yako uipendayo- ukiwafikiria hao tu badala ya kuanza kufikiria nikukutwa, nitakufa, nitapata aibu, nitaishi kwa shida n.k ndipo unaona ugumu wa kupima na kuishia kuamua bora hivi hivi tu nikishaugua ndo nitajua cha kufanya unasahau kuwa by the time unajua basi ushaambukiza hata wife/husband ambaye pengine angebakia mzima angelea wanao wasipate shida.

Mnanishangaza kuwa waoga kihivyo na bado mila mwazidumisha !!
 
Nashukuru sana DC kwa mawazo mazuri..nawashukuru pia wanaume wengine wooote wanaochangia mawazo yao.Kimsingi tuko pamoja sana... kila idea ni valid kabisa na nawahakikishia itafika kunakohusika -
ila DC naomba wewe. Tall na wengineo mlio raise issue ya dialogue na bedroom diplomacy hebu tufafanulieni zaidi..... mna maana gani mnaposema wanaume hawapendi kuambia vitu na wanawake - does this apply katika mazingira yote? je wataalamu wa kike wanapowapeni ushauri pia hamtaki?

Hapana. Wanapenda sana kuambiwa ila siyo kuguswa guswa sehemu mbaya. I mean hakuna mtu anapenda kuelezwa hadithi mbaya saa ya kula. Subiri tumalize kula halafu tupumzike ndo uanze kunieleza. Mimi nimekuja na njaa zangu halafu mtu analeta porojo sijui VVU, sijui nini... inakera sana na unaweza kumtoa mtu nundu!

Bahati mbaya siyo suala la nani anatoa ushauri. Mimi naongelea bedroom diplomacy. Wanawake wakakate shule ili wajue jinsi ya ku-present issue ngumu. Haya ni mambo mazito kwa hiyo yanahitaju kupewa uzito mkubwa. Tunawapenda sana na kuwajali ila hatupendi kero. Ndo maana nyumba ndogo zinatumia hiyo psychology ya kumpunguzia kero mwanamume ili afugwe milele!
 
je,
1. Kwanini wanaume wengi hawataki kupima na kujua afya zao ( majority wanajua kabisa kuwa wanaishi maisha hatarishi ( risky life styles)
2.Mbinu gani zitumike kuwashawishi wanaume wasiotaka kujua afya zao kupima kwa hiari?

Dada WOS, Kwa mtiririko wa hizi post nimepata jibu moja tu kwa swali la kwanza;WANAUME WANAOGOPA KUFA.
Swali la pili bado jibu sijaliona,sijui washawishiwe vipi!
 
Nikisema kuna watu both wamaume kwa wanawake ambao wako selfsh naomba msinitafune- wajua mtu unapokuwa unajifikiria wewe tu peke yako ndipo unapoona ugumu wa kupima but hebu fikiria wanao wadogo na familia yako uipendayo- ukiwafikiria hao tu badala ya kuanza kufikiria nikukutwa, nitakufa, nitapata aibu, nitaishi kwa shida n.k ndipo unaona ugumu wa kupima na kuishia kuamua bora hivi hivi tu nikishaugua ndo nitajua cha kufanya unasahau kuwa by the time unajua basi ushaambukiza hata wife/husband ambaye pengine angebakia mzima angelea wanao wasipate shida.

Mnanishangaza kuwa waoga kihivyo na bado mila mwazidumisha !!

MJ katika suala la kifo unaongelea nafsi moja tu. Asikudanganye mtu. Ikifikia saa ya kutoa roho kwa mwenyewe (Israel) basi kila nafsi itasimama peke yake. Mke, watoto n.k tunawaongelea wakati tuko poa, saa ikifika kila mtu na lwake! Na katika VVU/Ukimwi mtu nafikiria hiyo saa.
 
sasa baba E mbona kamchezo ka mbuni haka?? waficha kichwa tu.....

bht,

Sifichi kichwa, tatizo langu ni majibu ya kumwambia mtu ataishi kwa matumaini! Frankly speaking sielewi maana ya neno "kuishi kwa matumaini" - To me that sounds like "a death row"!
 
Back
Top Bottom