Nadhani kijana ameomba radhi na naamini mmemsamehe na kama ni hivyo nawashukuru. Mimi hiyo thread sikuiona lakini naungana na wote mliochukizwa na maneno yake.
Sasa tuache yaliyopita tumsaidie suala lake.
Mwanamke akiwa na mimba kunakuwa na hormones fulani ambazo zinaongezeka katika mzungumo wa damu. Hormones hizo zinatekekeza majukumu yanayohusiana na mimba aliyo nayo. Mfano progesterone hormone inailinda mimba isitoke kwa sababu mimba si sehemu ya miwili wa mwanamke, ni kitu kinachopaswa kuwemo mwilini kwa muda tu na ili iendelee kuwa mwilini kwa miezi 9 lazima kuwe na biological mehanism ya kihakikisha mwili hauikatai hiyo mimba. Kukitokea tatizo lolote mwiini likashusha sana kiwango cha progesterone lazima mimba itoke! Progesterone huwa inashuka pale muda wa kujifungua unapowadia.
Sasa, hormone hii na zingine zinapoongezeka kwenye damu kwa sababu ya mimba huwa zinavuruga ubongo wa mwanamke na kumfanya aanze tabia zisizo za kawaida kama kukataa vyakula fulani na kupenda kula vitu ambavyo wala hakuvizoea(lakini pia kula vitu kama udongo yaweza kuwa ni kwa sababu ya kupungukiwa na madini fulani). Pia kisaikolojia anaathirika na kuanza kuchukia vitu na hata watu wakati mwingine hata mumewe.
Kwa hiyo kijana, mke kumchukia mume wake sio kwa sababu mimba sio yake. Hiyo ni moja ya imani potofu sawa na wale wanaokeketa wanawake eti wasiwe wahuni wawe waaminifu kwa waume zao. Kipimo cha DNA ndio pekee kinachoweza kukupa uhakika kama mtoto ni wako au la. Maana hata kama mkeo akikupenda wakati wa ujauzito bado mimba inaweza isiwe ya kwako. Jenga utamaduni wa kuwauliza wataalam badala ya kushikilia mapokeo ya kimila.