Mke wangu wa ndoa ame-hack simu yangu

Mke wangu wa ndoa ame-hack simu yangu

Napata shida sana watu wengine wanapochangia ki-gender gender. Title peke yake inasema hv: "Mke wangu wa ndoa ame-hack simu yangu", usisome uzi kwa makengeza ili mradi tu jicho moja litazame gender! Kwa mujibu wa ile sheria ya Makosa ya Mtandao hii ni police case!
Mbona hata wewe una like zile wanaume wanakusifu kuwa wewe ndio kichwa?! Hakuna raha ya ndoa Kama hakuna uwaminifu.
 
Kuna mtu kwenye mitandao ya simu ndo anampa info zako. haja-hack wala nini.
 
OK Ukimshtaki na akafungwa, then what? Utaoa mke mwngine akuzaidie kulea watoto? Wewe ndio una matatizo na si mkeo. Alichofanya ni kupata habari za ziada kuhusu wewe ili aweze kufanya "informed decision" na asikurupuke. Kubali makosa au justify ulichotenda.
"Kwa kuzingatia usumbufu uliojitokeza kwa kuingilia mawasiliano yangu ya siri hasa kupitia mis-perception ya taarifa alizokutana nazo, nimepata wazo la kumshtaki kwa mujibu wa ile SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAO, 2015 ila nikaona kabla sijafanya hivyo nililete suala hili hapa ili nipate michango yenu ya mawazo hasa juu ya nini cha kufanya".
Nimekurudishia hiki kipengele cha uzi wangu ili nikukumbushe lengo kuu la kuleta uzi huu hapa, acheni kukurupuka na matokeo yake mnajikuta kuchangia nje ya mada kwa kuongozwa na mihemko isiyojulikana, huwezi kujibu swali ambalo hujalielewa, that's why people fail exams!
 
Mbona hata wewe una like zile wanaume wanakusifu kuwa wewe ndio kichwa?! Hakuna raha ya ndoa Kama hakuna uwaminifu.
Ahaa, kumbe hapa tunajadili tukiwa tayari tumesha-side upande unaotuhusu ki-gender? Ok, hii haitatusaidia sana, ukifanya research hutakiwi kuwa biased kwani taarifa ya utafiti huo inatakiwa isaidie JAMII yote in regardless of gender, amkeni jamani!
By the way: Sikujua kuwa Nyani Ngabu, Cipro~, et al ni wa ile gender nyingine! Kumbe hapa tunajifunza mengi.
 
Issue siyo cmu, ni kosa la jinai alilofanya chini ya mwavuli wa ndoa, unaniambia nikimpeleka mahakamani wata-drop case kwa kuwa ni cmu tu? Soma angalau title peke yake ndio uchangie, sielewi pale mtu anapokimbilia kuchangia wakati hata kichwa cha habari hajakielewa!
Pole sana mkuu, Ila furaha na huzuni katika ndoa ni kawaida sana, huyo mama analala nawewe unapokoloma, mkijamba usiku, mkiamka asubuhi midomo inanuka wewe na yeye mpo pamoja. Kaaeni myazungumze
 
Pole sana mkuu, Ila furaha na huzuni katika ndoa ni kawaida sana, huyo mama analala nawewe unapokoloma, mkijamba usiku, mkiamka asubuhi midomo inanuka wewe na yeye mpo pamoja. Kaaeni myazungumze
Wewe hata kuolewa kwako nadhani itakuwa shida, hakuna mwanaume atakayemvumilia mwanamke mropokaji kama wewe, aaaargh!
 
Tatizo siku hiz wavulana wengi wanaoa kabla hawahawa wanaume, ishu ya ndani kwenu unaileta hadharan hivi ijadiliwe na watu ili iweje? Kua kiakili wewe
 
Wewe hata kuolewa kwako nadhani itakuwa shida, hakuna mwanaume atakayemvumilia mwanamke mropokaji kama wewe, aaaargh!
Shindwa na ulegee Nipo kwenye ndoa Mwaka wa7 huu. Case za sms na sim kwangu hazipo.
 
Watu mnaingiaga kwenye ndoa huku mkiwa hata hamjielewi.

Inavyoonekana mnaingiaga tu ili kukidhi matakwa potofu ya jamii.

Sasa wewe unalalamika eti mkeo anazifahami taarifa zako za siri.

Siri gani hizo ilhali mko kwenye ndoa?

Au mliwekeana makubaliano ya mipaka kwenye ndoa yenu kabla hamjaifunga?
aisee mpendwa umemaliza
 
Ubarikiwe sana, kuna wakati nilitaka kuhoji hilo ila kwa vile mimi ni victim hapa nikasita, ndio maana mara kadhaa nimekuwa nikiwakumbusha kuwa kabla mtu hajachangia angalau asome title ya hii post na maelezo ya mwishoni mwa uzi huu, you made my day!
I'm telling you, none of them are great thinkers. they're not direct to helping someone as requested...sasa huu kama sio utapeli ni nini
 
Habari wanajamvi,

Katika hali isiyo ya kawaida nimegundua kuwa mke wangu wa ndoa ame-hack simu yangu na kuweza ku-access mawasiliano yangu yote hasa ya sms tokea mwezi wa 10 mwaka jana 2015 na kuzihifadhi kwenye simu yake.

Sina uhakika kama aliweza kupata mawasiliano mengine tofauti na sms.

Ninasema ku-hack kwa sababu tunaishi mikoa tofauti na hivyo hakuwa na namna yoyote ya ku-access simu yangu physically toka wakati huo, pia simu yangu ambayo ni smart phone ina security (password) in case angetumia mtu aliye karibu yangu.

Nimegundua hii hacking baada ya kuwa na hali ya kutoelewana kati yetu kwa muda sasa ambapo pamoja na mambo mengine niligundua kuna taarifa zangu za siri anazozifahamu ndipo nilipoanza uchunguzi na kugundua kuwa ana hizo sms.

Miongoni mwa sms anazoshikia bango ni zile zinazohusiana na miamala ya Mpesa ambapo nimewatumia pesa ndg, jamaa na marafiki ambao sikuona umuhimu wa kumtaaifu hivyo akazijengea hoja mbali mbali ikiwemo ya uhusiano wa kimapenzi wakati si kweli!

Nimejaribu kumbana aseme amewezaje ku-access "private communications" zangu ila amegoma kabisa kuweka wazi.

Cha kushangaza zaidi ni kuwa hana utaalam wowote wa masuala ya mawasiliano!

Kwa kuzingatia usumbufu uliojitokeza kwa kuingilia mawasiliano yangu ya siri hasa kupitia mis-perception ya taarifa alizokutana nazo, nimepata wazo la kumshtaki kwa mujibu wa ile SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAO, 2015 ila nikaona kabla sijafanya hivyo nililete suala hili hapa ili nipate michango yenu ya mawazo hasa juu ya nini cha kufanya.

Suala hili limenichanganya sana hasa ukizingatia kuwa tumekuwa kwenye ndoa takribani miaka 8 sasa na tuna watoto 2.

Naombeni michango yenu ya mawazo.

Ahsante!

Dogo amka.unachapiwa na Fundi simu.
 
Huyu jamaa akiendelea kulialia hapa yataibuka na mengine afate ushauri nlo mpa kwanza. Ndipo mambo ya suluhu yafate
Ushauri gani mkuu, sijaona ushauri zaidi ya kufafanua mipaka ya ndoa na kuwa kuna privacy baina ya wanandoa.
 
Sina cha kukushauri, ila napenda kukupa pole tu kwa kuhackiwa simu yako na michepuko yako kuwa out
 
Mkuu kumbuka huyo ni MKE wako na sio Demu tu wa mtaani. Hajafanya vizuri kwasababu amekuwa akikuinspect kwa siri ILA usimfungulie mashtaka kwani Hakimu wa ndoa/familia yako ni wewe mwenyewe.

Kama upo naye mbali basi wasiliana naye tu kawaida kwnz ila ukifika home ukae naye umwambie hujafurahia alichokifanya na aishie hapo,na akuambie ni nani aliyemfunza hiyo technic...akibisha na kuleta kiburi basi PIGA CHINI mtafute mwanamke mstaarabu.
 
Back
Top Bottom