Mke wangu wa ndoa ame-hack simu yangu

Mke wangu wa ndoa ame-hack simu yangu

kama ni uwazi na yeye angekupa uwezo wa kuingilia mawasiliano yake inaonekana ana mambo sio mazuri ndio maana hakuamini
inawezekana hajahak ila amewatumia wafanyakazi wa mitandao ya simu
 
Habari wanajamvi,

Katika hali isiyo ya kawaida nimegundua kuwa mke wangu wa ndoa ame-hack simu yangu na kuweza ku-access mawasiliano yangu yote hasa ya sms tokea mwezi wa 10 mwaka jana 2015 na kuzihifadhi kwenye simu yake.

Sina uhakika kama aliweza kupata mawasiliano mengine tofauti na sms.

Ninasema ku-hack kwa sababu tunaishi mikoa tofauti na hivyo hakuwa na namna yoyote ya ku-access simu yangu physically toka wakati huo, pia simu yangu ambayo ni smart phone ina security (password) in case angetumia mtu aliye karibu yangu.

Nimegundua hii hacking baada ya kuwa na hali ya kutoelewana kati yetu kwa muda sasa ambapo pamoja na mambo mengine niligundua kuna taarifa zangu za siri anazozifahamu ndipo nilipoanza uchunguzi na kugundua kuwa ana hizo sms.

Miongoni mwa sms anazoshikia bango ni zile zinazohusiana na miamala ya Mpesa ambapo nimewatumia pesa ndg, jamaa na marafiki ambao sikuona umuhimu wa kumtaaifu hivyo akazijengea hoja mbali mbali ikiwemo ya uhusiano wa kimapenzi wakati si kweli!

Nimejaribu kumbana aseme amewezaje ku-access "private communications" zangu ila amegoma kabisa kuweka wazi.

Cha kushangaza zaidi ni kuwa hana utaalam wowote wa masuala ya mawasiliano!

Kwa kuzingatia usumbufu uliojitokeza kwa kuingilia mawasiliano yangu ya siri hasa kupitia mis-perception ya taarifa alizokutana nazo, nimepata wazo la kumshtaki kwa mujibu wa ile SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAO, 2015 ila nikaona kabla sijafanya hivyo nililete suala hili hapa ili nipate michango yenu ya mawazo hasa juu ya nini cha kufanya.

Suala hili limenichanganya sana hasa ukizingatia kuwa tumekuwa kwenye ndoa takribani miaka 8 sasa na tuna watoto 2.

Naombeni michango yenu ya mawazo.

Ahsante!
Huyo mkeo kiboko
 
Dunia ina mambo sana kwahiyo kilichokuuma sana nikuingilia mawasiano tu ama kuna jambo jingine hadi ufikirie kumfungulia mashitaka mama watoto heeee!!!!!umekiri mwenyewe kumbe ulishawahi kuwa na mchepuko so pengine anahisi akiwa mbali uko mchepuko unaendelea nao ndo maana akahack.
 
Mbona hizo sms sio za siri, angalia sehemu zako za siri ndo utajua kuwa mawasiliano hayo sio ya siri
 
We unawapa tu ela unaoona inafaa kuwapa, ndoa ni kitu kingine mbona. Ndoa sio biashara eti itakufa ukisaidia ndugu na jamaa zako...!!!!!

Uyo ni mkeo sawa...!! Linapokuja suala la yeye kupekecha na kutaka kukujua undani wengi husema ni halali yao kwa ville ni wake...!!!
Hii sio sawa....
Anapokuwa anafukuafukua simu ni lazma atakuwa anatafuta mabaya yako tu na sio mazuri and this is never right nijuavyo mimi.....!!

Simu ni kama roho tu ya mwenzio
Ivi ukikuta mambo ambayo huyaekewi uko na wanavojua kuliwasha in case they find wat they want, ndoa si inakuwa shakani...!!?

Best way ni kupiga stop tabia izi za kupekuana cm.

Kuhack iz possible tangu muda mrefu , mi najua iyo kitu.

Lipo duka fulani lilikuwa linauuza iyo kifaa kwa shilingi 50 ela ivi. One takes ure line and imbeds into this kind of moderm alafu kuna kijimuamala pale kinaungAnisha sm yako na yake.. Bas .. You ar done
 
Watu mnaingiaga kwenye ndoa huku mkiwa hata hamjielewi.

Inavyoonekana mnaingiaga tu ili kukidhi matakwa potofu ya jamii.

Sasa wewe unalalamika eti mkeo anazifahami taarifa zako za siri.

Siri gani hizo ilhali mko kwenye ndoa?

Au mliwekeana makubaliano ya mipaka kwenye ndoa yenu kabla hamjaifunga?
 
Yaan ana makosa anajijua halafu anataka msaada. Hizo siri; sir gan ambazo mkeo hatakiw kuzijua? Ngoja ndoa yake izamee
 
Inasikitisha kuona kuwa huu uzi umegeuka na kuwa tatizo la kijinsia badala ya watu kujadili wakiwa huru na kutolea maoni yatakayonisaidia kufanya maamuzi sahihi, kina dada wote wananiponda while wanaume wenzangu wanaonekana kuunga mkono kuwa mke wangu amefanya makosa, tutafika kweli kwa mtindo huu? Sitaki kuwa biased kama hao kina dada ila ukweli ni kuwa wamejikuta wanajadili historia ya ndoa yetu ambayo pia hawaijui na kuweka pembeni topic iliyo hapo juu inayozungumzia Mke wa ndoa kuingilia mawasiliano yangu bila idhini yangu ambalo ni kosa kisheria!
 
Halafu ukishamshitaki ataendelea kua mke wako bado au?
Ninyi wote bado mnasumbuliwa na ubinafsi, imewapasa wana ndoa kuishi pamoja haya mambo ya wote mko Tanzania hii hii halafu mwingine yuko mkoa mwingine kwa makazi ya kudumu hua siyaelewi sana na nafikiri matatizo mengi huanzia hapo.
 
Yaan ana makosa anajijua halafu anataka msaada. Hizo siri; sir gan ambazo mkeo hatakiw kuzijua? Ngoja ndoa yake izamee
Hivi ndoa ikizama huwa inakulaga pande ipi vile? Ndio maana mnakuwa very defensive!
 
Halafu ukishamshitaki ataendelea kua mke wako bado au?
Ninyi wote bado mnasumbuliwa na ubinafsi, imewapasa wana ndoa kuishi pamoja haya mambo ya wote mko Tanzania hii hii halafu mwingine yuko mkoa mwingine kwa makazi ya kudumu hua siyaelewi sana na nafikiri matatizo mengi huanzia hapo.
Mhalifu ataendeleaje kuwa mke wangu?
 
Hivi ndoa ikizama huwa inakulaga pande ipi vile? Ndio maana mnakuwa very defensive!
Hata kwako itakula tuu baba. Hiyo sheria ya mtandao weka kando kwanza bt huyo mmama anafight na haki yake ya kuwa mke kwako lazima ajue usalama wake. Siku hiz magonjwa meengi
 
Back
Top Bottom