Mke wangu wa ndoa ame-hack simu yangu

Mke wangu wa ndoa ame-hack simu yangu

Mkuu umejaribu kwenda mtandao husika kulalamikia suala hilo? Isijekawa kuna mtu ndani ya mtandao anampa kila unalofanya
 
Nashukuru, kweli wewe ni Kubwa Lao. In fact alianza tabia ya kunichunguza kwa kutumia watu tulio kuwa nao karibu kama vile majirani zangu na wafanyakazi wenzangu na baadaye akagundua kuwa hao hao wanamgeuka kwa kuja kuniambia hivyo akabadili style. Tatizo kubwa lililopelekea yeye kuanza tabia hiyo ni baada ya yeye kugundua kuwa nina kamchepuko ingawa hili tulishalijadili kama wanandoa na kulimaliza yapata miaka 3 sasa.
Nadhani mpk hapo ndugu yangu MpiganiaUhuru kesi imeisha, kumbe ana haki ya kufanya hivyo hasa kwa kua umesema mnaishi mbalimbali lkn pia mlishawahi kusuluhisha tatizo la mchepuko

Mana sio kitu cha ajabu kwa ñyani kurudi kwenye msitu wake!!

Labda nikushauri tu!! Kaa na mwenZio ongea nae kuhusu tabia hiyo lkn pia aijue haki yako ya faragha pia ni muhimu sana.
 
kwa mm binafsi si amin kama amehack maana iyo michezo niladhima izo apps aweke sim zote mbil yake na yako maana naijua sana apo atakua anacheza na baadhi ya watumishi wa makampuni ya sim ambao si waaminifu wanampa taalifa zako wala si kuhack
 
Pole sana mdau...
Ndoa ni changamoto, tena haiendweshwi kwa akili za darasani.

Mke wako wa ndoa tena unakiapo nae. Naomba nikuulize swali mdau, kwenye hizo texts alizo nazo hakuna texr za kumkwaza yeye?( michepuko yako).....kabla ujafikiria kwenda kumshitaki. Jiangalie njoa zako mwenyewe kwanza, HAPO ULIMPA SABABU za yeye kufanya hayo yote. Kwann hakufanya January to September??

Wake up mdau...badilisha njia zako be good n faith to ur wife.
 
Habari wanajamvi,

Katika hali isiyo ya kawaida nimegundua kuwa mke wangu wa ndoa ame-hack simu yangu na kuweza ku-access mawasiliano yangu yote hasa ya sms tokea mwezi wa 10 mwaka jana 2015 na kuzihifadhi kwenye simu yake. Sina uhakika kama aliweza kupata mawasiliano mengine tofauti na sms. Ninasema ku-hack kwa sababu tunaishi mikoa tofauti na hivyo hakuwa na namna yoyote ya ku-access simu yangu physically toka wakati huo, pia cmu yangu ambayo ni smart phone ina security (password) in case angetumia mtu aliye karibu yangu. Nimegundua hii hacking baada ya kuwa na hali ya kutoelewana kati yetu kwa muda sasa ambapo pamoja na mambo mengine niligundua kuna taarifa zangu za siri anazozifahamu ndipo nilipoanza uchunguzi na kugundua kuwa ana hizo sms. Miongoni mwa sms anazoshikia bango ni zile zinazohusiana na miamala ya Mpesa ambapo nimewatumia pesa ndg, jamaa na marafiki ambao ckuona umuhimu wa kumtaatifu hivyo akazijengea hoja mbali mbali ikiwemo ya uhusiano wa kimapenzi wakati si kweli! Nimejaribu kumbana aseme amewezaje ku-access "private communications" zangu ila amegoma kabisa kuweka wazi. Cha kushangaza zaidi ni kuwa hana utaalam wowote wa masuala ya mawasiliano!
Kwa kuzingatia usumbufu uliojitokeza kwa kuingilia mawasiliano yangu ya siri hasa kupitia mis-perception ya taarifa alizokutana nazo, nimepata wazo la kumshtaki kwa mujibu wa ile SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAO, 2015 ila nikaona kabla cjafanya hivyo nililete suala hili hapa ili nipate michango yenu ya mawazo hasa juu ya nini cha kufanya. Suala hili limenichanganya sana hasa ukizingatia kuwa tumekuwa kwenye ndoa takribani miaka 8 sasa na tuna watoto 2. Naombeni michango yenu ya mawazo.

Ahsante!
Ni mkeo wa ndoa, na tena mna watoto wawili tayari halafu unataka kumfungulia kesi ili afungwe kisa kaingilia mawasiliano yako, aisee Wewe ni mpumbavu sana mkuu, hujui kuwa mkeo ndo Wewe mwenyewe? ninyi ni mwili mmoja kwa hiyo ana haki ya kujua privacy zako zote Na Wewe ndo una makosa huwezi kutuma pesa popote bila mkeo kujua, ni lazima umshirikishe kwa kila jambo ndo maana ya mke, huyo si hawara yako ni mkeo sasa unakuwaje na akili ya kivuta bangi eti umshtaki mkeo?
Tatizo watu hamjui thamani ya ndoa na maana ya mke, hapo unajiona Wewe uko sawa sana kwa utumbo uliofanya wa kumficha mkeo, hivi angekuwa yeye anatuma pesa anakuficha ungemwelewa? au kwa kuwa yeye ni mwanamke basi hana haki, Nakushauri usijaribu kabisa kumshtaki labda kama umeamua kuvunja ndoa na halafu akifungwa utawaambia nini hao watoto? kwamba mama yao ulimfunga!
Nakushauri tena usijaribu kabisa huo upuuzi, cha kufanya uonane na mkeo haraka myamalize matatizo yenu, ugomvi ktk ndoa ni jambo la kawaida pote duniani ila siyo tena kumfunga mwenzako, mkishindwana mwachane salama msije kutesa watoto wasio na hatia kwa upumbavu wenu.
 
Sehem za siri zenu mnaonyeshana hadi kuzaa watoto wawili, Ila sim inakufanya umshtaki!
Hivi ndugu zangu watanzania kwa nini tunakosa kuaminiana ktk ndoa zetu? wewe una familia yako na watoto bado unalalamika unataka kumshitaki mkeo kisa kaingilia privacy yako... sasa nini maana yakuoa unaoa ili iweje? unajua maana na umuhimu wa ndo kweli wewe nakushauri kabla hujamshitaki mkeo nenda aidha kwa mchungaji wako aliyefungisha ndoa yenu ama uende msikitini kama ndoa yako ilifungishwa na Sheikh.. utapata solusheni sahihi ndg yangu usitake kuharibu ndoa yako kwa jambo lenye kushaurika.
 
huwezii ukaenda kumshtaki mkuu huo ni wehu, japokua kweli amekosea kwenda ku hack simu yako , naona wote mngekaa chini wewe ukawa muwazi kwake ni watu gani uliokua unawatumia hela, na kwa nini ulikua unaona haina haja ya kumwambia, ikibidi omba hata msamaha wa kinafiki ili mambo yaendelee.
then inakuja zamu yake sasa kukwambia ilikuaje hadi aka hack simu yako, akuweke wazi kabisa na yeye.
asipokua muelewa kwa hapa endelea kuishi naye kibishi
hali ikizidi kua mbaya na kiburi chake pia kikizidi chukua maamuzi magumu
talaka ihusike na ikibidi mfungulie hayo mashtaka kwa ajili ya usalama wako maana anaweza kukufanyia chochote kutokana na chuki na hasira za talaka
 
Na hao wanao kushauri ukafungue kesi ni wehu kama wewe......vaa viatu vyake kwanza kwenye hilo uone unge fanya nini??
Bado nakusisitizia wewe ulimpa sababu ya yeye kufanya hayo yote....tena ukamwombe msamaha haraka sana. Ana kila sababu kufanya hayo yote.
 
  • Thanks
Reactions: nao
Ni mkeo wa ndoa, na tena mna watoto wawili tayari halafu unataka kumfungulia kesi ili afungwe kisa kaingilia mawasiliano yako, aisee Wewe ni mpumbavu sana mkuu, hujui kuwa mkeo ndo Wewe mwenyewe? ninyi ni mwili mmoja kwa hiyo ana haki ya kujua privacy zako zote Na Wewe ndo una makosa huwezi kutuma pesa popote bila mkeo kujua, ni lazima umshirikishe kwa kila jambo ndo maana ya mke, huyo si hawara yako ni mkeo sasa unakuwaje na akili ya kivuta bangi eti umshtaki mkeo?
Tatizo watu hamjui thamani ya ndoa na maana ya mke, hapo unajiona Wewe uko sawa sana kwa utumbo uliofanya wa kumficha mkeo, hivi angekuwa yeye anatuma pesa anakuficha ungemwelewa? au kwa kuwa yeye ni mwanamke basi hana haki, Nakushauri usijaribu kabisa kumshtaki labda kama umeamua kuvunja ndoa na halafu akifungwa utawaambia nini hao watoto? kwamba mama yao ulimfunga!
Nakushauri tena usijaribu kabisa huo upuuzi, cha kufanya uonane na mkeo haraka myamalize matatizo yenu, ugomvi ktk ndoa ni jambo la kawaida pote duniani ila siyo tena kumfunga mwenzako, mkishindwana mwachane salama msije kutesa watoto wasio na hatia kwa upumbavu wenu.
Kweli wewe ni Cipro~, povu jiingi! Sababu kuu ya kuleta huu uzi hapa ni kupata ushauri na ndio maana ckukimbilia mahakamani kwanza kutokana na side effects zake, hiyo mitusi vipi? Mtu maakini akishasoma uzi huu atajua kuwa tayari ndoa yetu ina mgogoro, usijidai huoni!
 
Ningependa zaidi kupata michango toka kwa wazoefu wa ndoa kuliko wale wenye ndoa za "kufikirika" vichwani.
Nipo kwenye ndoa kwa miaka 6 sasa Wewe una makosa huwezi kumficha mkeo, ndoa ni zaidi ya unavyofikiri Wewe, ndo maana wengi ndoa zimewashinda, Wewe unataka kuishi kwa chenga kivipi? mkiendelea hivyo hiyo ndoa itakufa.
 
  • Thanks
Reactions: nao
Nipo kwenye ndoa kwa miaka 6 sasa Wewe una makosa huwezi kumficha mkeo, ndoa ni zaidi ya unavyofikiri Wewe, ndo maana wengi ndoa zimewashinda, Wewe unataka kuishi kwa chenga kivipi? mkiendelea hivyo hiyo ndoa itakufa.
Kwa hiyo kwa upande wako kosa hapa ni kumficha mke wangu baadhi ya taarifa ambazo infact sio tangible na sio ujasusi aliofanya?
 
Watu mnaingiaga kwenye ndoa huku mkiwa hata hamjielewi.

Inavyoonekana mnaingiaga tu ili kukidhi matakwa potofu ya jamii.

Sasa wewe unalalamika eti mkeo anazifahami taarifa zako za siri.

Siri gani hizo ilhali mko kwenye ndoa?

Au mliwekeana makubaliano ya mipaka kwenye ndoa yenu kabla hamjaifunga?

Unamaana gani hapo mkuu. ?
 
Kuhack simu bila kupata simu yako ningumu sana,labda mkeo nae kama anakabuzi kampuni moja ya simu ambako ndio kanampa taarifa zote,ivyo nimoja ya kutafuta njia ya kuachana na wewe sasa kajamaa kanajitahid kumpa hiyo miamala na text ili ajue pa kuanzia
Iwapo hiyo simu unayoitumia ulipewa zawadi na mkeo, basi bila shaka alijiandaa kupata taarifa zako kwa njia ya siri. Kama ni mkeo wa ndoa haina haja kumshitaki mahakamani kwani yote hayo yamejengeka juu ya kuwa na wivu nawe. Na wivu ndio mapenzi.
 
Sehem za siri zenu mnaonyeshana hadi kuzaa watoto wawili, Ila sim inakufanya umshtaki!
Afadhali umenisaidia kumweleza ukweli,maana anajiona yeye pekee ndo mwenye ndoa humu, anataka kuweka limit ya ndoa wakati kuvuliana nguo na kufanya mapenzi ndo mwisho wa yote, eti ku hack mawasiliano yake ndo amshtaki mwanamke, mbona hakumshtaki alipo hack dushelele lake hadi wakazaa watoto wawili, Tatizo la kudandia ndoa bila kujua uzito wake ndo hili sasa .
 
Naomba nikuulize swali mdau, kwenye hizo texts alizo nazo hakuna text za kumkwaza yeye?( michepuko yako).....kabla ujafikiria kwenda kumshitaki
Hakuna, vinginevyo nisingepata ujasiri wa kusema kuwa nafikiria kumshtaki na yeye kuishia kuomba msamaha!
 
Back
Top Bottom