Mke wangu wa ndoa ame-hack simu yangu

MpiganiaUhuru

JF-Expert Member
Mar 31, 2012
777
912
Habari wanajamvi,

Katika hali isiyo ya kawaida nimegundua kuwa mke wangu wa ndoa ame-hack simu yangu na kuweza ku-access mawasiliano yangu yote hasa ya sms tokea mwezi wa 10 mwaka jana 2015 na kuzihifadhi kwenye simu yake.

Sina uhakika kama aliweza kupata mawasiliano mengine tofauti na sms.

Ninasema ku-hack kwa sababu tunaishi mikoa tofauti na hivyo hakuwa na namna yoyote ya ku-access simu yangu physically toka wakati huo, pia simu yangu ambayo ni smart phone ina security (password) in case angetumia mtu aliye karibu yangu.

Nimegundua hii hacking baada ya kuwa na hali ya kutoelewana kati yetu kwa muda sasa ambapo pamoja na mambo mengine niligundua kuna taarifa zangu za siri anazozifahamu ndipo nilipoanza uchunguzi na kugundua kuwa ana hizo sms.

Miongoni mwa sms anazoshikia bango ni zile zinazohusiana na miamala ya Mpesa ambapo nimewatumia pesa ndg, jamaa na marafiki ambao sikuona umuhimu wa kumtaaifu hivyo akazijengea hoja mbali mbali ikiwemo ya uhusiano wa kimapenzi wakati si kweli!

Nimejaribu kumbana aseme amewezaje ku-access "private communications" zangu ila amegoma kabisa kuweka wazi.

Cha kushangaza zaidi ni kuwa hana utaalam wowote wa masuala ya mawasiliano!

Kwa kuzingatia usumbufu uliojitokeza kwa kuingilia mawasiliano yangu ya siri hasa kupitia mis-perception ya taarifa alizokutana nazo, nimepata wazo la kumshtaki kwa mujibu wa ile SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAO, 2015 ila nikaona kabla sijafanya hivyo nililete suala hili hapa ili nipate michango yenu ya mawazo hasa juu ya nini cha kufanya.

Suala hili limenichanganya sana hasa ukizingatia kuwa tumekuwa kwenye ndoa takribani miaka 8 sasa na tuna watoto 2.

Naombeni michango yenu ya mawazo.

Ahsante!
 
Watu mnaingiaga kwenye ndoa huku mkiwa hata hamjielewi.

Inavyoonekana mnaingiaga tu ili kukidhi matakwa potofu ya jamii.

Sasa wewe unalalamika eti mkeo anazifahamu taarifa zako za siri.

Siri gani hizo ilhali mko kwenye ndoa?

Au mliwekeana makubaliano ya mipaka kwenye ndoa yenu kabla hamjaifunga?
 
Habari wanajamvi,

Katika hali isiyo ya kawaida nimegundua kuwa mke wangu wa ndoa ame-hack simu yangu na kuweza ku-access mawasiliano yangu yote hasa ya sms tokea mwezi wa 10 mwaka jana 2015 na kuzihifadhi kwenye simu yake. Sina uhakika kama aliweza kupata mawasiliano mengine tofauti na sms. Ninasema ku-hack kwa sababu tunaishi mikoa tofauti na hivyo hakuwa na namna yoyote ya ku-access simu yangu physically toka wakati huo, pia cmu yangu ambayo ni smart phone ina security (password) in case angetumia mtu aliye karibu yangu. Nimegundua hii hacking baada ya kuwa na hali ya kutoelewana kati yetu kwa muda sasa ambapo pamoja na mambo mengine niligundua kuna taarifa zangu za siri anazozifahamu ndipo nilipoanza uchunguzi na kugundua kuwa ana hizo sms. Miongoni mwa sms anazoshikia bango ni zile zinazohusiana na miamala ya Mpesa ambapo nimewatumia pesa ndg, jamaa na marafiki ambao ckuona umuhimu wa kumtaatifu hivyo akazijengea hoja mbali mbali ikiwemo ya uhusiano wa kimapenzi wakati si kweli! Nimejaribu kumbana aseme amewezaje ku-access "private communications" zangu ila amegoma kabisa kuweka wazi. Cha kushangaza zaidi ni kuwa hana utaalam wowote wa masuala ya mawasiliano!
Kwa kuzingatia usumbufu uliojitokeza kwa kuingilia mawasiliano yangu ya siri hasa kupitia mis-perception ya taarifa alizokutana nazo, nimepata wazo la kumshtaki kwa mujibu wa ile SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAO, 2015 ila nikaona kabla cjafanya hivyo nililete suala hili hapa ili nipate michango yenu ya mawazo hasa juu ya nini cha kufanya. Suala hili limenichanganya sana hasa ukizingatia kuwa tumekuwa kwenye ndoa takribani miaka 8 sasa na tuna watoto 2. Naombeni michango yenu ya mawazo.

Ahsante!

Mke wako wa ndoa na unampenda! hamna sababu ya kupaniki umekosea kutokuwa muwazi kwake. Wazo langu kaa naye chini mweleze ukweli wa mambo, usimfiche fiche vitu ni mkeo wa ndoa huyo. Naamini utakuwa ok.
 
Wewe Nyani Ngabu uko kwenye ndoa? Mawazo uliyotoa ni kama yale niliyokuwa nayo kabla cjaoa, kwamba ndoa ni mwili mmoja, la hasha! Ndio maana wenzetu wa Magharibi walianzisha ndoa za mikataba, hamuwezi ku-share kila kitu! Lakini pia huwezi kuniambia kuwa ukishaoa /olewa unapoteza nafsi yako, kwanza kumbuka mlikutana mkiwa wote ni watu wazima tena wenye background tofauti. I doubt if u r married!
 
Nina tajiriba ya kutosha kuweza kuhoji utayari wako/ wenu wa ndoa.
 
Mke wako wa ndoa na unampenda! hamna sababu ya kupaniki umekosea kutokuwa muwazi kwake. Wazo langu kaa naye chini mweleze ukweli wa mambo, usimfiche fiche vitu ni mkeo wa ndoa huyo. Naamini utakuwa ok.
Kuwa muwazi una maanisha kama hv: Shangazi amenipigia cmu anaomba nimsaidie elf, ninamtumia sawa! Yule mtoto wa jirani yangu pale ameniomba nimchangie elf 10 ili aongezee alipe ada, nimtumie? Huu ndio uwazi unaonaanisha kuwa niwe nao kwa wife? Ila pia ukubaliane na mimi kuwa ndoa ni tamu na imenyooka pale mwanzo, baada ya muda mtagundua kuwa kila mmoja wenu ana mapungufu yaliyokuwa yamejificha na hapo ndo sehemu ya kuanza kufanya adjustment za hapa na pale ili ndoa iendelee bila misuguano ya mara kwa mara. Yako ina umri gani? Tupeane mauzoefu!
 
Sioni sababu gani unapata ugumu kumshirikisha mwenzio maombi ya kugawia watu (hata kama ni ndugu zako) rasilimali za familia. Fedha hata kama ni zako, hizo ni za kwenu ndani ya familia hivyo mke ana uhalali wa kuhoji zinatumika vipi. Hapa naona shida unayo wewe na bado hujatambua kuwa unachokifanya ni tatizo. Bahati mbaya maelezo yako yanaonesha wote na mkeo mmekuwa ni watu wa kufichana mambo. Yeye ana siri zake nawe una zake. Kwa style hii ndoa haiwezi kuwa na afya. Inakuwepo tu ndoa jina.
 
Nimekupata, naomba unisaidie na hili: Ikiwa tayari nimeshakosea aidha kwa bahati mbaya au kwa kutojua ktk kumshirikisha kitu fulani, je ni halali yeye kwenda kukiiba?
 
Nimekupata, naomba unisaidie na hili: Ikiwa tayari nimeshakosea aidha kwa bahati mbaya au kwa kutojua ktk kumshirikisha kitu fulani, je ni halali yeye kwenda kukiiba?
Sio halali. Kimsingi hakuna mtu aliye perfect, hivyo kama umekosea au yeye kakosea njia sahihi ya kusuluhisha ni mazungumzo na kufahamishana wapi mmoja kakosea. Hii inasaidia hata kuliepuka hilo kosa siku za mbeleni. Uwazi na kuongea lugha moja ni nguzo muhimu kwenye ndoa.
 
Mi si wa ndoa ila issue ni simple...... flash simu yako au nunua Nyingine weka Lain yako na kuwa safe zaidi renew Lain yako baada ya kuhakikisha una back up contact zako zote
Hii itasaidia nini mkuu?
 
hakuna hacking hapo ..... huyo uliyemtumia pesa kwa Mpesa ndiye aliyemwambia mkeo ....

be careful and don't think you are smart
 
hakuna hacking hapo ..... huyo uliyemtumia pesa kwa Mpesa ndiye aliyemwambia mkeo ....

be careful and don't think you are smart
Kama umesoma vizuri post yangu ni kuwa mambo ya Mpesa nilitoa kama mfano, otherwise nilisema ana sms zangu zote kwenye cmu yake!
 
Back
Top Bottom