Mke wangu wa ndoa ame-hack simu yangu

Mke wangu wa ndoa ame-hack simu yangu

Pole mshtaki halafu mnafungaje ndoa huku meingine akiwa mashariki mwingine kusini hapo kwanza Amna ndoa pili ndoa nikuwa mwili mmoja unaweka siri ya nin?
 
Mke wako wa ndoa na unampenda! hamna sababu ya kupaniki umekosea kutokuwa muwazi kwake. Wazo langu kaa naye chini mweleze ukweli wa mambo, usimfiche fiche vitu ni mkeo wa ndoa huyo. Naamini utakuwa ok.
Acha zako mkuu

Kuna ndoa na kuna self privacy yani ndugu yangu ana shida mpaka nimpigie simu mke eti ooh mke wangu unajua kule kijiji ndugu yangu yule nanii anashida na laki moja hivyo naomba ruhusa yako nimtumie
Come on meen.

Kwanza huyo mke kazidi mipaka wanawake wao wakifanyiwa hivi utayasikia mpaka kwenye redio kama mume ni wake wivu na kumpekenyua ya nini

Sie waislamu tumekatazwa kupekenyuana kabisa ni makosa kwan yaweza leta ugomvi.

Halafu kwenye simu si swala la mpesa tu kuna masuala mengine ya sms za kawaida kumuoa mtu haimaanishi haki yako ya self privacy imeondoka.

Mke ana makosa totally
 
Sio halali. Kimsingi hakuna mtu aliye perfect, hivyo kama umekosea au yeye kakosea njia sahihi ya kusuluhisha ni mazungumzo na kufahamishana wapi mmoja kakosea. Hii inasaidia hata kuliepuka hilo kosa siku za mbeleni. Uwazi na kuongea lugha moja ni nguzo muhimu kwenye ndoa.
Huyu jamaa akiendelea kulialia hapa yataibuka na mengine afate ushauri nlo mpa kwanza. Ndipo mambo ya suluhu yafate
 
Hili nalo! Eti nimshtaki? Ili iweje akifungwa? Huyo mke ulimpenda mwenyewe au? Na inaelekea alikuwa na wasiwasi na mienendo yako ndio maana akafanya hivyo. Halafu hujatupa picha yote atakuwa kakukamata na kale kamchepuko Kako!
 
Ningependa zaidi kupata michango toka kwa wazoefu wa ndoa kuliko wale wenye ndoa za "kufikirika" vichwani.
Whats your intention mkuu kwahyo unafurahia kuingiliwa kwenye mawasiliano yako??

Mi nna declare kua sjaoa ila hayo mambo ya usuluhishi nimesoma. Na kuya practice pia hyo ndoa nimeisoma vizuri mpaka sasa nimesha andaa hukumu ya ndoa 3 moja nliivunja

Kinachokutokea mi nshakifanya skuona faida mbali na magomvi yasokwisha

Kama ww ni mkirsto soma Tito 3:9 holy bible inakwambia jiepushe na ujinga na nasaba za magomvi we umesema kila sku ni kelele we nnachokiona kwako utataka mkae chini kitu ambacho si kibaya ila kwanza ondoa tatizo una haki zako binafsi mbali ya kuwa umeoa. Una haki zako.

Ondoa tatizo kwanza liletalo magomvi
 
Mtoa mada ameoa kwa ajili ya tendo la ndoa tu. Eti anamshtaki mkewe amesoma sms zake zote.
Nimeishia kumshangaa inaonekana kunakitu nyuma ya pazia haiwezekani mkeo ku hack simu yako bila sababu
Hii ndoa ina tatizo na mapenzi yameanza kupungua kwa wana ndoa hawa inawezekana hata miaka 10 haina.
Niko pembeni nasubiria kifuatacho ITV
 
Yani wote wewe na mkeo hamjielewi kabsa MNA umri gani kwanza?!

Mwanaume ni kichwa cha familia achana kushindana na mkeo.....
 
Yani wote wewe na mkeo hamjielewi kabsa MNA umri gani kwanza?!

Mwanaume ni kichwa cha familia achana kushindana na mkeo.....
Yes mwanaume ndo kicha cha family kuna vitu unatakiwa kusimama kama mwanaume na kuna vitu vya kushirikiana kma familia mwanaume aondoe kwanza tatizo.
 
Yes mwanaume ndo kicha cha family kuna vitu unatakiwa kusimama kama mwanaume na kuna vitu vya kushirikiana kma familia mwanaume aondoe kwanza tatizo.

Yan kumbe kuna haja ya kupewa semina ya nn maana ya kuwa kichwa cha familia yan na akili zako zooooote unaumiza kichwa kwjl ya SMS alizonasa mkeo?!
Tujifunze kwa viumbe wengne bas kama tumeshindwa kujiongeza jins gani ya kuhandle wife with luv mpk vitu vngne vnakufa automatic
 
Mtoa mada ameoa kwa ajili ya tendo la ndoa tu. Eti anamshtaki mkewe amesoma sms zake zote.
Napata shida sana watu wengine wanapochangia ki-gender gender. Title peke yake inasema hv: "Mke wangu wa ndoa ame-hack simu yangu", usisome uzi kwa makengeza ili mradi tu jicho moja litazame gender! Kwa mujibu wa ile sheria ya Makosa ya Mtandao hii ni police case!
 
Pole mshtaki halafu mnafungaje ndoa huku meingine akiwa mashariki mwingine kusini hapo kwanza Amna ndoa pili ndoa nikuwa mwili mmoja unaweka siri ya nin?
Kwa watumishi wa uma wanandoa kukaa huku na kule ni jambo very common au tuache kazi kisa ndoa?
 
Sema inaelekea wewe ni mstaarabu sana ameHack kuanzia mwaka jana ad leo ajakuacha. Ingekua wengne hapa sio kuachwa na kesi juu
 
Unaweza kumuuliza mke wako ka hack vipi na mimi nihack Ya baba watoto wangu? Tuletee humu
 
Mkuu @MpiganiaUhuri, kabla hatujachangia tafadhali weka hapa "contract" ya ndoa yenu tupitie yaliyomo!!!!!
 
Mkuu nadhani mkeo alikuwa anajaribu kuilinda ndoa yake..Uenda kuna vitu alivihisi ndo ikapelekea yy kufanya hivyo...Nwei Sasa unataka kumshtaki mkeo zen nini kinafwata baada ya hapo?
 
  • Thanks
Reactions: nao
Sehem za siri zenu mnaonyeshana hadi kuzaa watoto wawili, Ila sim inakufanya umshtaki!
Issue siyo cmu, ni kosa la jinai alilofanya chini ya mwavuli wa ndoa, unaniambia nikimpeleka mahakamani wata-drop case kwa kuwa ni cmu tu? Soma angalau title peke yake ndio uchangie, sielewi pale mtu anapokimbilia kuchangia wakati hata kichwa cha habari hajakielewa!
 
Regardless ..... .... hakuna siri chini ya jua ..... hizo sms anazipata kwa hao unaowatumia .... because hao wanaojifanya wanafanya siri na wewe they are bluffing you
Nimethibitisha kuwa hz sms amezipatia kwangu kwani zile za Mpesa zinaonesha amount iliyotumwa hadi salio la mtumaji, haiwezekani aliyetumiwa pesa atumiwe na salio lako!
 
Dont try to outsmart yourself by giving us irrelevant excuses. Be a man then act accordingly.
 
Lkn pia mpk mkeo kufikia hatua hiyo ni wazi kabisa wewe ni straiker mwenye vichepuko so kaingia hofu na wewe!!

Hebu weka sababu basi zilizopelekea mkeo kufanya hilo, weka dhambi zako ili tujue pumba na mchele ni upi sio tu tunakushauri wakati huenda we ndie mwenye shida
Nashukuru, kweli wewe ni Kubwa Lao. In fact alianza tabia ya kunichunguza kwa kutumia watu tulio kuwa nao karibu kama vile majirani zangu na wafanyakazi wenzangu na baadaye akagundua kuwa hao hao wanamgeuka kwa kuja kuniambia hivyo akabadili style. Tatizo kubwa lililopelekea yeye kuanza tabia hiyo ni baada ya yeye kugundua kuwa nina kamchepuko ingawa hili tulishalijadili kama wanandoa na kulimaliza yapata miaka 3 sasa.
 
Back
Top Bottom