Mke wangu ni mgumu sana kujishusha

Mke wangu ni mgumu sana kujishusha

Na ndio maana unapata tabu kwenye ndoa. Bro hizi ndoa bila micheps utachanganyikiwa. Kidume uwe na wanawake watatu maishani mwako. Mke na micheps wawili mbona dunia utaona tamu

Nalichukua hili wazo kwa ajiri ya tafakuri zaidi.
 
Sio kweli mke wangu niliyetengana nae nimeishi nae for 5 yrs, ninamzidi umri,elimu na kipata but hakuwahi kusema neno samahani hata akosee vipi.Nadhani culture ya MTU inachangia maana ni Mhehe.

Ulifanya maamuzi sahihi kumpiga chini. Mimi pia naelekea kufanya maamuzi hayohayo
 
KUNA MWANAUME MWENZAKO ANAMFIKISHA MKEO MAHAL AMBAPO WEWE HUWEZI KUMFIKISHA... NDIO MAANA MKEO HAJISHUSHI KWAKO...
By the way kwani mkeo ni mama yako kwamba huwez kumuacha kumfukuza...? Tafuta mwanamke mwingine uinjoi maisha
 
Nilihisi kitu kama hiki,Wanawake wengi waajiriwa hata akiwa hana hela kumzidi mume wake hawapo submissive kwa wame wao.
Ungekuwa na wewe mtimishi kama yeye halafu umzidi cheo lazima angekuheshimu.

Hivi Sababu inakuaga nini?
 
Kwani toka mwanzo hukuona red flag?Uliona na hukumwacha,Why?Unapenda ndoa punguza Ego,nyenyekea,na kama huitaki endeleeni na Hiyo tabia mwaka ni mrefu lazima ife.

Ndoa naitaka sana, ila siwezi kuwa namnyenyekea yeye kila siku
 
Muelekeze tatizo lako afu mwambie ulivyo choka kama hataki kubadilika mwambie muachane yeye ndo aamue maana kuna watu wanaonaga wao ni bora sana kuliko wengine

Nishamuelekeza sana. Atatulia kwa miezi kadhaa halafu anarudia tena
 
Niliwahi kupitia changamoto kama hii, mwanamke alikua jeuri na hajui kujishusha, yaani ukipandisha sauti na yeye anapandisha

Nikawaza sana yaani huyu mwanamke nimemzidi kila kitu kuanzia elimu mpaka kipato, maisha yake yote ananitegemea mimi maana yeye ni mama tu wa nyumbani sasa hii jeuri anaitoa wapi.

Sometimes kwenye malumbano ananitishia tukiachana tunagawana kila kitu.

Nilikuja kumpa surprise ya maisha baada ya kusikia nimeoa mke mwingine, aliongea kila lugha lkn sikusikia. Hofu ya kugawana mali na mwanamke mwingine endapo angezaa ikamjia maana tuna nyumba mbili na two plots.

Kwa bahati mbaya uchaguzi wangu wa mke wa pili haukua mzuri maana nilifanya kwa hasira hivyo ndoa haikudumu. Lkn mke wangu sasa amejirekebisha sana, anaogopa nisije nikaoa tena.

Kila siku ananiambia kama nitaoa tena basi nioe kwa tamaa zangu lkn yeye hanipi tena sababu za kuoa maana ameshajifunza.
 
  • Thanks
Reactions: _ly
Ndoa ni ya watu wawili mkuu. Shida nini hapo?
Kwenye Kiswahili hakuna kuoana. Mwanamme anaoa, mwanamke anaolewa.

Kitendo cha kuoa kinafanywa na mwanamme, mwanamke anafanyiwa kitendo hicho.

Wewe katika saikolojia yako tu unajiona hujaoa, unaona mmeoana.

Mpaka hapo, katika utamaduni wa Kiswahili, umeanza mechi kwa goli la kujifunga mwenyewe.

Katika Kiswahili hakuna kuoana. Mwanamme anaoa, mwanamke anaolewa.

Sema nilioa, usiseme tulioana.

Unaweza kuona hiki ni kitu kidogo, lakini, hii ni saikolojia kubwa sana inayoonesha huelewi who wears the pants in your marriage.
 
Wakuu nawasalimu kwa jina la muungano.

Niende moja kwa moja kwenye mada kuu, nimekua kwenye ndoa na huyu mke wangu yapata miaka nane sasa, tulioana wote tukiwa vijana na ni binti ambae tulisoma nae kuanzia primary tukaja kukutana chuo, kwahiyo namfahamu vizuri tu. Nikiri tu kwenye mambo mengine ya kifamilia yupo vizuri sana, ila tatizo linaanza ni kujishusha na kuomba msamaha pale tunapotibuana.

Hii hali inanikwaza sana sababu bila kujishusha mimi tunaeza kukaa hadi mwezi hatuongei eti ameninunia. Mara nyingi huwa inanilazimu mimi kujishusha baada ya kubanwa na upwiru sana. Kwa ninavofahamu kupishana kauli kwenye ndoa kupo na ni jukumu la wanandoa wote kuipambania ndoa kwa kujishusha na kuyaongea, ila mwanamke ndio anatakiwa awe mstari wa mbele kujishusha ili mambo yaende, ila kwa huyu mke wangu imekua tofauti.

Kwa sasa tuna watoto watatu ila hii hali inanifanya nihisi kama nalazimisha mapenzi hivi hadi nimeanza kupata mawazo ya kuivunja hii ndoa. Nakwazika sana.

Naombeni ushauri wenu wakuu.
Ongeza mwingine
 
Pesa namzidi sana tu, ila sina mchep

Jitahidi uwe nao bro, unawezaje kuangalia channel moja kila siku?!
Ndiomana anakuona bwege sababu anajua huna pa kwenda, au una shida ya kimaumbile [emoji2088][emoji2088][emoji2088]
 
Usioneshe msimamo ili tu arudi kwenye njia ila ONESHA MSIMAMO WA KWELI KWENYE MAMBO YA MSINGI kama hanyooki basi huyo sio wako
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom