Mke wangu ni mgumu sana kujishusha

Mke wangu ni mgumu sana kujishusha

Watu wa hivyo usigombane nao, kama amekosea kaa kimya...atajishtukia mwenyewe...kama umemkosea na akaanza kukuuliza au kugomba kaa kimya. Dawa yao ni kukaa kimya tu.
 
1. Chukulia kwamba huo ni ugonjwa wake.

2. Kama hauna mazara sana na ni kiburi cha uanaume, we shula tu.

3. Mwenye akili ndo anaitunza ndoa, kwa hiyo itunze.

Angalizo:

Kama kweli kuna jambo la muhimu sana kakosea, halafu hataki kukubali, Nakushauri kaza mpaka mwisho, atashuka tu.

Kuna kitu kinaitwa break point, yakwako ipo karibu, iongeze tu izidi yake, ikishazidi atashuka tu, akikuwoma hiyo tabia atakutesa sana.
Nimekusoma saana ila moja ya kitu muhimu kwenye maisha ya ndoa kwa mwanaume ni kua don't care... yaan kujitoa ufahamu ama kumpuuzia mwanamke kwenye mambo madogomadogo, i mean kumtreat ka mtoto na si kushindana nae
 
Wakuu nawasalimu kwa jina la muungano.

Niende moja kwa moja kwenye mada kuu, nimekua kwenye ndoa na huyu mke wangu yapata miaka nane sasa, tulioana wote tukiwa vijana na ni binti ambae tulisoma nae kuanzia primary tukaja kukutana chuo, kwahiyo namfahamu vizuri tu. Nikiri tu kwenye mambo mengine ya kifamilia yupo vizuri sana, ila tatizo linaanza ni kujishusha na kuomba msamaha pale tunapotibuana.

Hii hali inanikwaza sana sababu bila kujishusha mimi tunaeza kukaa hadi mwezi hatuongei eti ameninunia. Mara nyingi huwa inanilazimu mimi kujishusha baada ya kubanwa na upwiru sana. Kwa ninavofahamu kupishana kauli kwenye ndoa kupo na ni jukumu la wanandoa wote kuipambania ndoa kwa kujishusha na kuyaongea, ila mwanamke ndio anatakiwa awe mstari wa mbele kujishusha ili mambo yaende, ila kwa huyu mke wangu imekua tofauti.

Kwa sasa tuna watoto watatu ila hii hali inanifanya nihisi kama nalazimisha mapenzi hivi hadi nimeanza kupata mawazo ya kuivunja hii ndoa. Nakwazika sana.

Naombeni ushauri wenu wakuu.
Jibu ni moja tu anakudharau.

Ulimpenda sababu ya pesa/ elimu yake.
Sasa vumilia.

Vijana mnasema Bora shape tabia mtavumiliana
 
Wakuu nawasalimu kwa jina la muungano.

Niende moja kwa moja kwenye mada kuu, nimekua kwenye ndoa na huyu mke wangu yapata miaka nane sasa, tulioana wote tukiwa vijana na ni binti ambae tulisoma nae kuanzia primary tukaja kukutana chuo, kwahiyo namfahamu vizuri tu. Nikiri tu kwenye mambo mengine ya kifamilia yupo vizuri sana, ila tatizo linaanza ni kujishusha na kuomba msamaha pale tunapotibuana.

Hii hali inanikwaza sana sababu bila kujishusha mimi tunaeza kukaa hadi mwezi hatuongei eti ameninunia. Mara nyingi huwa inanilazimu mimi kujishusha baada ya kubanwa na upwiru sana. Kwa ninavofahamu kupishana kauli kwenye ndoa kupo na ni jukumu la wanandoa wote kuipambania ndoa kwa kujishusha na kuyaongea, ila mwanamke ndio anatakiwa awe mstari wa mbele kujishusha ili mambo yaende, ila kwa huyu mke wangu imekua tofauti.

Kwa sasa tuna watoto watatu ila hii hali inanifanya nihisi kama nalazimisha mapenzi hivi hadi nimeanza kupata mawazo ya kuivunja hii ndoa. Nakwazika sana.

Naombeni ushauri wenu wakuu.
Kataa Utumwa

Kataa Unyonyaji

Kataa Ujambazi

Tokomeza Ndoa

Pinga Ndoa

Kataa Ndoa
 
Wakati mpo katika mapenzi na uchumba alikuwa anajishusha kukiwa na mzozo? Au umemfikisha kwenye ndoa ndiyo ukinyonga wake ukamuisha? Au uliziona alama za tahadhari ukakaza fuvu kutokana na utamu wa mbususu uliyokuwa unapewa kwa kuibia ibia? 😁😁😁
Hii ni kweli huyo demu hajaanza leo
 
Unakuta baba ni mzee,amekaa kwenye ndoa hadi ana wajukuu,chakushangaza eti naye ananuna! Si mkae muongee muwekane sawa mambo yaishe? Eti mtu ni boss huko ofisini kwake anatoka nyumbani eti kamnunia mkewe.
Haifai kwa kweli suluhisho ni kuyajenga maisha ya ndoa yaendelee
 
Niliwahi kupitia changamoto kama hii, mwanamke alikua jeuri na hajui kujishusha, yaani ukipandisha sauti na yeye anapandisha

Nikawaza sana yaani huyu mwanamke nimemzidi kila kitu kuanzia elimu mpaka kipato, maisha yake yote ananitegemea mimi maana yeye ni mama tu wa nyumbani sasa hii jeuri anaitoa wapi.

Sometimes kwenye malumbano ananitishia tukiachana tunagawana kila kitu.

Nilikuja kumpa surprise ya maisha baada ya kusikia nimeoa mke mwingine, aliongea kila lugha lkn sikusikia. Hofu ya kugawana mali na mwanamke mwingine endapo angezaa ikamjia maana tuna nyumba mbili na two plots.

Kwa bahati mbaya uchaguzi wangu wa mke wa pili haukua mzuri maana nilifanya kwa hasira hivyo ndoa haikudumu. Lkn mke wangu sasa amejirekebisha sana, anaogopa nisije nikaoa tena.

Kila siku ananiambia kama nitaoa tena basi nioe kwa tamaa zangu lkn yeye hanipi tena sababu za kuoa maana ameshajifunza.

Hii inaonekana ni njia nzuri zaidi.

Kwaiyo huyo wa pili ukamkuta na shida kubwa zaidi ya hii hadi ukaamua kumuacha?
 
Kwenye Kiswahili hakuna kuoana. Mwanamme anaoa, mwanamke anaolewa.

Kitendo cha kuoa kinafanywa na mwanamme, mwanamke anafanyiwa kitendo hicho.

Wewe katika saikolojia yako tu unajiona hujaoa, unaona mmeoana.

Mpaka hapo, katika utamaduni wa Kiswahili, umeanza mechi kwa goli la kujifunga mwenyewe.

Katika Kiswahili hakuna kuoana. Mwanamme anaoa, mwanamke anaolewa.

Sema nilioa, usiseme tulioana.

Unaweza kuona hiki ni kitu kidogo, lakini, hii ni saikolojia kubwa sana inayoonesha huelewi who wears the pants in your marriage.

Nimekuelewa mkuu
 
Jitahidi uwe nao bro, unawezaje kuangalia channel moja kila siku?!
Ndiomana anakuona bwege sababu anajua huna pa kwenda, au una shida ya kimaumbile [emoji2088][emoji2088][emoji2088]

Sipendi kufanya hivo, sababu me mwenyewe sitaki kufanyiwa hivo. Ila nayachukua maoni yako.
 
Nimekusoma saana ila moja ya kitu muhimu kwenye maisha ya ndoa kwa mwanaume ni kua don't care... yaan kujitoa ufahamu ama kumpuuzia mwanamke kwenye mambo madogomadogo, i mean kumtreat ka mtoto na si kushindana nae

Nitaijaribu na hii. Ingawa ninavomfaham nikifanya hivo kelele zitakua mara dufu sababu atahisi nimepata mchepuko
 
Kwa ninavofahamu kupishana kauli kwenye ndoa kupo na ni jukumu la wanandoa wote kuipambania ndoa kwa kujishusha na kuyaongea, ila mwanamke ndio anatakiwa awe mstari wa mbele kujishusha ili mambo yaende,
Kwa nini wewe ndo usiwe mstari wa mbele kupambania ndoa..
Mke amekuzalia watoto 3 bado unahisi anajilazimisha kwako?? Upo serious kabisa??
 
Kipindi cha kumchumbia mwanamke ni muhimu sana kumjua.

Ni muhimu sana kujua tabia zake kwa undani.

Ili usije kuchelewa kumjua, ukamjua wakati mna watoto watatu, halafu ikawa shida kubwa sana.
 
Hiki ndio kinachoniuma zaidi. Kwaio nimpige chini tu mkuu?
Mkuu ni maamuzi yako,mwenyewe nimeishi na wife kwa 6 yrs na tuna watoto 2 ana tabia fulani ambazo nimekuja kukugundua hawezi kabisa kubadilika maana ndivyo alivyolelewa na nitabia alizonazo Mama yake.

Hiyo tabia yake ya inasababisha tunagombana karibu kila siku,anakuwa anachukia sana kugombezwa nami hiyo tabia yake inaniudhi kupita kipimo lazima nimweleze timekuwa tukiishi hivyo.

Mwaka Jana nilipanga nioe mwanamke mwingine but badaye nikafikiria swala LA uchumi na magonjwa nikahairisha na kubadili mipango.Mwaka huu nikachukua maamuzi magumu ya Ku divorce-maana haikuwa ndoa tena bali karaha.
 
Kipindi cha kumchumbia mwanamke ni muhimu sana kumjua.

Ni muhimu sana kujua tabia zake kwa undani.

Ili usije kuchelewa kumjua, ukamjua wakati mna watoto watatu, halafu ikawa shida kubwa sana.

A see kwa kweli kwenye uchumba ndio sehemu sahihi ukibugi tu hapo utajita maisha yako yote.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom