Mke wangu mchoyo anapika chakula kidogo sishibi kabisa

Mke wangu mchoyo anapika chakula kidogo sishibi kabisa

Nimeoa nina miezi 5 sasa ila tatizo kubwa ni kwamba mke wangu anapika chakula kidogo mno yani sishibi kabisa na namuachia hela ya matumizi ya kutosha ila sielewi nini kinamsumbua

Mpaka inafika kipindi kabla sijarudi nyumbani nipitie hotelini nile kwanza halafu ndio niende kwangu nimeongea nae sana lakini anaacha siku kadhaa halafu anarudia tena tabia yake ushauri wenu wakuu nimuache au nimfanye nini?
Hili ni swali la kuleta jukwaani kweli?
Haya ndio matatizo ya ndoa za utotoni.
 
Ngoja niwaite hawa wapendwa watoe mawazo yao kwenye huu uzi
Shunie Beef Lasagna witnessj Hajar Sky Eclat mahondaw Miss Natafuta na wanajf wengine bila kumsahau Mama Sabrina
Hahahaaaa. Nimecheka Dada.

Tuseme tu huyo mwanaume hajitambui Dada, sababu suala kama hilo linatakiwa alimalize na mkewe huko kwa kumuuliza sababu ya kufanya hivyo na kama sababu haina uzito basi anamwambia tu rekebisha hiyo na uwe unapika chakula cha kutosha.

Sasa kuanza kulalamika huku ili mke wake aonekane ni kiumbe cha ajabu tunashindwa kumshangaa.

Akae chini azungumze na mkewe na si kupoteza pesa kila kukicha kwa chakula cha kununua wakati nyumbani kipo.
 
Nimeoa nina miezi 5 sasa ila tatizo kubwa ni kwamba mke wangu anapika chakula kidogo mno yani sishibi kabisa na namuachia hela ya matumizi ya kutosha ila sielewi nini kinamsumbua

Mpaka inafika kipindi kabla sijarudi nyumbani nipitie hotelini nile kwanza halafu ndio niende kwangu nimeongea nae sana lakini anaacha siku kadhaa halafu anarudia tena tabia yake ushauri wenu wakuu nimuache au nimfanye nini?
Kama hataki kubadilika msusie kabisa chakula chae usile. Ili azidi kufurahi.
 
Hahahaaaa. Nimecheka Dada.

Tuseme tu huyo mwanaume hajitambui, sababu suala kama hilo linatakiwa alimalize na mkewe huko kwa kumuuliza sababu ya kufanya hivyo na kama sababu haina uzito basi anamwambia tu rekebisha hiyo na uwe unapika chakula cha kutosha.

Sasa kuanza kulalamika huku ili mke wake aonekane ni kiumbe cha ajabu tunashindwa kumshangaa.

Akae chini azungumze na mkewe na si kupoteza pesa kila kukicha kwa chakula cha kununua wakati nyumbani kipo.
Ila tuseme ukweli, kuna wanawake wachoyo aisee[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Tatizo sasa hivi wanawake mambo mengi yaan fedha ya chakula mwenzako anaweka vikoba mwisho mmoja aliondoka na mtaji wa milioni moja mpaka leo na amehama Arusha.Yaan hatutafika kwa style hii sijui mrejesho wanawake acheni pia michezo ya ajabu
 
Hapana wala usimwache ispokua sasa usimwachie pesa Bali nunua mwenye mahitaji yote
Nakubaliana nawe, wanawake wengine ni wajanjajanja ukimpa mfano hela ya kununulia mchele kilo moja yy atanunua nusu au robo tatu hela nyingine anaweka na atatumia huohuo kwa kubania hadi bajeti nyingine ipitishwe...
Hapo mko wenyewe je mkiwa na familia au kupata ugeni si ndio mtashindia maji?
 
Matumizi niache halafu nije nipike tena kweli na yeye yupo nyumbani tu
Usiwe unamwachia tena hela ya matumizi, fanya manunuzi mwenyewe au muende pamoja kama ni bajeti ya wiki au mwezi, huyo ni mjanja atakua anabana matumizi...
 
Hii si uchumi ni tabia mbaya hivi anashindwaje kumpikia mumewe chakula chakutosha ashibe, au anataka mumewe ashindwe kazi.

Chakula muhimu sasa mume akila si ndo furaha huyo mchoyo hafu wanaume na sisi ulaji huwa tofauti na sisi kah. Mwanamke mwenzetu anatia aibu na kumtesa baby wake
Yaani ww ni moja ya wanawake wanaojielewa, umesema vyema...
 
Lakini hili nimeliona sana haswa Dar watu wengi hununua vitu nusu nusu jibane ukipata ela nunua mchele,unga,sukari,mafuta afu uone inakuaje
 
Hii story inanikumbusha mfanyakazi mwenzangu mmoja, alioa mke akawa anapika chakula kidogo jamaa hashibi. Siku moja jamaa akamwambia kuwa, kesho tuna wageni watatu hivyo pika chakula cha kutosha watakula mchana hapa nyumbani. Bi dada akapika chakula kama alivyoambiwa na mmewe.

Baada ya chakula kuiva akamuuliza mme mbona wageni hawafiki na chakula tayari. Jamaa akamwambia tuendelee kula wako njiani.

Jamaa akaanza kupiga msosi hotpot la kwanza likaisha, akamwambia mkewe lete na kile kingine wakija utapika kingine.

Baada ya kumaliza kula. Akamwambia hiki ndiyo kipimo cha chakula kila siku hakuna mgeni yeyote.

Hivyo nawe unaweza tumia njia hiyo.
Hahaaaaaa huyo nae alitia fora, yani kapiga hotpot zima then kaomba some more...
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Back
Top Bottom