Mke wangu mchoyo anapika chakula kidogo sishibi kabisa

Mke wangu mchoyo anapika chakula kidogo sishibi kabisa

Nimeoa nina miezi 5 sasa ila tatizo kubwa ni kwamba mke wangu anapika chakula kidogo mno yani sishibi kabisa na namuachia hela ya matumizi ya kutosha ila sielewi nini kinamsumbua

Mpaka inafika kipindi kabla sijarudi nyumbani nipitie hotelini nile kwanza halafu ndio niende kwangu nimeongea nae sana lakini anaacha siku kadhaa halafu anarudia tena tabia yake ushauri wenu wakuu nimuache au nimfanye nini?

Dawa ya mke mkorofi ni kuoa mke wa pili

c.c @MoneyPenny Mzigua90
 
Nimeoa nina miezi 5 sasa ila tatizo kubwa ni kwamba mke wangu anapika chakula kidogo mno yani sishibi kabisa na namuachia hela ya matumizi ya kutosha ila sielewi nini kinamsumbua

Mpaka inafika kipindi kabla sijarudi nyumbani nipitie hotelini nile kwanza halafu ndio niende kwangu nimeongea nae sana lakini anaacha siku kadhaa halafu anarudia tena tabia yake ushauri wenu wakuu nimuache au nimfanye nini?
Sasa hiyo pia unataka ushauri daah shida tupu
Hiyo kuoa nahic ulilazimishwa pia
 
Nakushauri kama ndo tabia yake badi kila ukirud ukikuta msos mdog upakue subir
Muite bek tatu mwambie aandae kingine mkiwa wote mmekaa na kupeana michapo ya siku akimaliza bek tatu changanya na chake kula...
Hapo hapo akiwa bek tatu muelekeze mbele yake mwambie dada huu ndo msos naotaka kuukuta mezani...
Mwachie jukumu bek tatu full stop
Uone kama hatojirekebisha
Mambo ya ku ignore msikwaruzane na mwenzio mbona yanawezekana
 
Hahahaaaa. Nimecheka Dada.

Tuseme tu huyo mwanaume hajitambui Dada, sababu suala kama hilo linatakiwa alimalize na mkewe huko kwa kumuuliza sababu ya kufanya hivyo na kama sababu haina uzito basi anamwambia tu rekebisha hiyo na uwe unapika chakula cha kutosha.

Sasa kuanza kulalamika huku ili mke wake aonekane ni kiumbe cha ajabu tunashindwa kumshangaa.

Akae chini azungumze na mkewe na si kupoteza pesa kila kukicha kwa chakula cha kununua wakati nyumbani kipo.
Nakwambia ndoa hiziiiiiii!!!!!
 
Usijisifu una mbio, msifu na anayekukimbiza.

Tatizo linaweza kuwa;

1. Mpishi - Muulize vizuri usikie ya upande wake
2. Mlaji - Jiulize, ulaji wako ni wa kawaida? Usijekuta ukila jioni mpaka jioni na mpishi hajui.
 
Mambo ya kuacha hela ya matumizi ndio shida. Nenda kafanye shopping ya kutosha mchele,unga , mafuta, nyama,nyanya,maharage,ndizi Kazi yake iwe ni kupika . Mambo ya kudunduriza ndio effect.kila siku kilo moja ya mchele ndio effect
 
Watanzania wengi hatuna nidhamu kwenye kula,

Kuna watu, km mimi nishajijengea utaratibu tangu huko nyuma kuwa usiku nakula vitu vyepesi.

Naweza kunywa yoghurt au Juice na andazi moja na matunda nikalala.

Sasa kwa utamaduni huu nilionao, ukija kwangu waweza sema mimi mchoyo au nakunyanyasaa.

Inaweza kuwa mkewe si mtu wa kula na anazingatia sana suala la lishe.

Sasa mleta mada yeye kashazoea kushiba usiku utafikiri anakwenda kupasua mawee.

Jinsi mwili unavyouzoesha ndivyo unavyokuendeshaa.

Tatizo naliona kwake, SIO LAZIMA KUSHIBA.
Mimi nishazoea hivyo usiku nile kitu kizito ndio nilale kama ilivyo kawaida yetu wa Tanzania
 
Ijumaa ukitoka kazini akikupa msosi kidogo kula maliza afu ilambe sahani mbele yake,ondoka home rudi nyumbani jumamosi usiku, akikuuliza ulikuwa wapi mwambie nilikuwa nimeenda kula.
Hahaha da ushauri wako mkuu hatari
 
Mkuu pesa utafute wewe, then chakula usishibe, bajeti ya msosi umeacha home.. hapo wife ana shida mahali

Au ndio wale pesa yote wanapeleka vikoba?? otherwise ni UCHOYO kiwango cha stigilaz Goji
Nahisi mambo ya wanawake pengine anacheza michezo yao hiyo ngoja nifuatilie
 
Usijisifu una mbio, msifu na anayekukimbiza.

Tatizo linaweza kuwa;

1. Mpishi - Muulize vizuri usikie ya upande wake
2. Mlaji - Jiulize, ulaji wako ni wa kawaida? Usijekuta ukila jioni mpaka jioni na mpishi hajui.
Ulaji wa kawaida tu mkuu
 
Back
Top Bottom