Wala hawajali, nilishawahi kuwa na mtu yani message ikiingia tu simu inarukiwa kama mpira wa basketi! Alikuwa anakagua messages zote picha zote, platforms zote! Kama mleta mada tu, ila ss huyu wangu alikuwa kiboko! Alikuwa akiona tu na marafiki wamechangamka changamka anakaa chini anablock marafiki zangu ana unfollow, atafuta namba zao, namba za kiume zote haijalishi nani zitafutwa zote! Calls zinakagauliwa moja moja mpaka dk tulizoongea, yani tunaongea nini! Hataki hata uzoee jirani, sijui ukie da dukani au gengeni hakuna hta kucheka na muuza genge, nunua rudi ndani! Yani ni miaka zaidi ya mitano tulishaachana lakini kila mwaka ndio nagundua fulani kablockiwa mwaka huu! Nilipoteza marafiki wengi connection yani kiufupi nilijikuta naanza upya! Ila ni tabia za narcists hizi!